Search This Blog

Saturday, January 14, 2012

YANGA YAITANDIKA SOFAPAKA - MNYAMA ZAMU YAKE KESHO DHIDI YA TUSKER


Mabingwa wa Tanzania Bara na Afrika Mashariki na Kati, Yanga wameendeleza ushindi katika michezo ya kirafiki, baada ya kuwafunga Sofapaka ya Kenya leo hii katika uwanja wa Taifa.

Katika mchezo wa leo uliochezwa katika uwanja wa Taifa, Yanga wamewachapa Sofapaka toka Kenya goli 2-1 katika mchezo wa kujipima ubavu, ambapo Yanga waliutumia mchezo kwa ajili ya maandalizi wa ligi kuu ya Vodacom na michuano ya klabu bingwa Afrika.

Yanga walianza kuandika goli la kwanza kupitia kwa mchezaji bora wa Uganda kwa mwaka 2011, Hamis Kiiza katika dakika ya 29 kabla ya kurejea tena nyavuni katika dakika ya 60.

Goli la Sofapaka lilifungwa na Thomas Wanyama katika dakika ya 88.


Kesho katika uwanja wa Taifa Mnyama Simba atacheza na mabingwa wa Kenya Tusker saa kumi jioni.

ALEX NJIANI KUELEKEA QPR.


QPR na Chelsea wamekubaliana ada ya uhamisho ya mchezaji Alex.

Rangers walikataliwa na Chelsea kwa ofa waliyotoa mwanzoni mwa wiki hii, lakini sasa wamefikia makubaliano rasmi juu ya kumsaini mbrazili huyo.

Kikwazo pekee kilichobakia sasa ni mchezaji kukubaliana mahitaji binafsi ya matajiri wapya wa London.

Chelsea wamekubali ofa ya QPR kwa Alex masaa 24 baada ya kumsaini Gary Cahil aliyetokea Bolton.

GARY CAHILI KUTAMBULISHWA LEO STAMFORD BRIDGEChelsea wamekamilisha usajili wa beki Gary Cahil lakini hatoweza kucheza leo dhidi ya Sunderland in premier league clash katika uwanja wa Stamford Bridge.


Cahil jana alikubaliana na mahitaji binafsi ya kupata mshahara wa £80,000 kwa wiki kwa mkataba wa miaka 5 na anatarajiwa kusafiri kwenda London kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya leo jumamosi.


The Blues walikuwa na matumaini ya kukamilisha uhamisho wa Cahil mapema jana mchana ili aweze kucheza mechi ya leo dhidi ya Black Cats, lakini haikuwezekana hivyo leo baada ya kufanyiwa vipimo, Gary Cahil atatambulishwa rasmi kwa mashabiki kabla ya mchezo huo.


Ni zaidi ya wiki mbili sasa tangu Bolton wakubali ada ya uhamisho ya £7million kutoka kwa Chelsea kwa ajili ya Cahil, ambaye alikuwa katika miezi 6 ya mwisho ya mkataba wake.


Mazungumzo kati ya Chelsea na mchezaji ndio yalikwamisha uhamisho huo kukamilika mapema, huku Andre-Villas Boas akisema mahitaji makubwa ya mshahara ndio kikwazo.


Inaaminika Cahil alikuwa akitaka alipwe kiasi cha £100,000 per week, £30000 zaidi ya kiasi ambacho Chelsea walikuwa wapo tayari kulipa, wakiwa katika program ya kupunguza matumizi makubwa yatokanayo na mishahara ya wachezaji .


KIIZA AWAFUNIKA AKINA OKWI NA OCHAN UGANDA - ABEBA TUZO


Straika wa kimataifa wa Yanga, Hamis Kiiza alichaguliwa kuwa Mwanasoka Bora wa Mwaka wa nchini kwao Uganda na kuwapiku nyota wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya na pia Emmanuel Okwi wa klabu ya Simba yenye uhasama wa jadi na timu yake, ‘Wekundu wa Msimbazi’, Simba.

Kiiza alishinda tuzo hiyo inayoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Uganda (USPA) baada ya kupigiwa kura nyingi kutokana na kiwango cha juu alichoonyesha katika msimu wa 2010/2011.

Mbali na Okwi ambaye hakukaribia hata 3-bora, wengine waliofunikwa na Kiiza katika kuwania tuzo hiyo ni Dennis Onyango anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini, Andy Mwesigwa anayeichezea klabu ya Ordabasy ya nchini Kazakhastan na David Obua anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Heart ya nchini Scotland.

Akizungumzia tuzo hiyo, Afisa Habari wa klabu ya Yanga, Luis Sendeu, alisema kuwa wao wamefurahia tuzo aliyotwaa Kiiza na wanaamini kuwa mafanikio yake yametokana na juhudi anazoonyesha uwanjani wakati akiitumikia timu ya taifa lao, ‘The Cranes’ na pia mchango anaoutoa wakati akicheza katika ngazi ya klabu.

"Mashabiki wa Yanga wamefarijika na tuzo hii ya Kiiza. Tunaungana naye kusherehekea tuzo hiyo ambayo ina heshima kubwa kwani amewashinda nyota wengi wa soka nchini kwao," alisema Sendeu.

Kiiza alifanya vizuri akiwa na timu ya URA katika msimu wa 2010/2011 ambapo aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Uganda baada ya kufunga mabao 14.

Pia aliibuka kuwa mchezaji bora katika mashindano ya Bell yanayofanyika kila mwaka nchini mwao.

Baada ya mafanikio hayo akiwa URA, Kiiza alijiunga na Yanga na kuisaidia kutwaa taji la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati ‘Kombe la Kagame’ na pia aliisaidia 'The Cranes' kutwaa ubingwa wa Kombe la Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Chalenji) lililoshindaniwa Desemba jijini Dar es Salaam.

WADHAMINI WARUDISHA CECAFA KAGAME CUP


UDHAMINI mnono unaopatikana Tanzania umelifanya Baraza la vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kuamua kurudisha Kombe la Kagame jijini Dar es Salaam tena mwaka huu.

Michuano hiyo ya Kagame iliyofanyika mwaka jana na kushuhudia Yanga ikitwaa ubingwa baada ya kuifunga Simba katika fainali huku umeme ukikatika Uwanja wa Taifa, mwaka huu yalipangwa kufanyika Rwanda.
Akizungumza na gazeti la The New Times la Rwanda, Katibu mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye, alisema wameamua kurudisha mashindano hayo Tanzania kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana mwaka jana.

Pamoja na mafanikio ya mashindano hayo, Cecafa pia kuna jambo moja la muhimu la kupatikana kwa wadhamini Tanzania ambao wameshapata siku moja iliyopita.

Taarifa hiyo inalifanya jiji la Dar es Salaam kuwa mwenyeji kwa mara ya pili mfululizo kwa Kombe la Kagame kama ilivyokuwa kwa Kombe la Chalenji lililofanyika mwaka jana na kushudia Uganda 'Cranes' wakitwaa ubingwa huo kwa kuichapa Rwanda.

Zanzibar na Sudan pia walikuwa wakipewa nafasi ya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mikubwa kwa klabu Afrika Mashariki na Kati, lakini tatizo la fedha limewakosesha nafasi hiyo.

Fainali ya mwaka jana ya Kombe la Kagame, ilizikutanisha timu zote za Tanzania, Simba na Yanga na kushuhudia kocha Sam Timbe akipata taji lake la nne la Kombe la Kagame baada ya kufanya hivyo akiwa na SC Villa (2005), Polisi (2006), Atraco (2009) na Yanga (2011).

Friday, January 13, 2012

CLOUDS MEDIA GROUP YAITANDIKA MAXMALIPO MABAO 5-0

Timu ya watoa burudani Clouds Media Group The Dream Team leo iliendeleza rekodi yake ya kutofungwa tangu mwaka 2012 uanze baada ya kuwafunga bila huruma Max Malipo kwa mabao 5-0 . Mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Tanganyika Packers ulianza majira ya saa kumi na nusu ambapo kikosi cha Clouds kiliwakilishwa na Golikipa Frank , beki wa kulia ambaye pia ni nahodha wa timu Geoffrey Lea,Shaffih Dauda,Ibrahim Massoud Maestro,Ali Siso,Abdul Mohamed , Antonio Nugaz,James Andrea Tupa Tupa,Peter Ngassa,Anatoly Kabezi ,Salim Mhando na Athumani Kikucha. Katika Mchezo huo mabao ya Clouds Media Group Yalifungwa na Salim Mhando aliyefunga mabao mawili,Athuman Kikucha ambaye naye alifunga mawili na Antonio Nugaz hata hivyo kiungo muhimu wa timu hii Shaffih Dauda aliumia mwanzoni kwenye dakika ya 25 ya mchezo na hivyo alilazimika kutoka na bado haijajulikana atakaa nje kwa muda gani. Kwa wale ambao hawakupata nafasi ya kuushuhudia mchezo huu wasikose kutazama kipindi cha Sports Bar siku ya jumatatu .
Huu ni mchezo wa pili kwa Clouds Media Group Fc The Dream Team kushinda tangu mwaka huu uanze baada ya kuwafunga Infinity Communications Ijumaa iliyopita kwa matokeo ya 4-2. Kama kawaida Chama Linawakaribisha watu wote wanaotaka kucheza mechi kutuma maombi ambayo yatajibiwa kutokana na vigezo mbalimbali ambavyo timu ya Clouds huhitaji kufikiwa na wale wote wanaotaka kucheza na timu hii kila siku za ijumaa.

INTER YAMRUDIA CARLOS TEVEZ

Inter Milan wapo tayari kufungua upya mazungumzo na Manchester City juu ya Carlos Tevez baada ya mahasimu wao AC Milan kujitoa katika mazungumzo kwa ajili ya kumsajili muargentina huyo.

Mapema wiki hii Raisi wa Inter Milan Massimo Morati alisema wameshindwa kupambana na Milan katika harakati za kumsaini Tevez, lakini hiyo ilikuwa kabla ya makamu wa raisi wa Milan Adriano Galliani kujitoa katika mazungumzo na City baada ya Alexandre Pato kukataa kujiunga na PSG.

Huku mustakabali wa Tevez ukiwa bado haupo sawa, Morrati yupo tayari kurudi katika meza ya mazungumzo na City.

Mbele ya mchezo wa derby wiki hii Morrati aliwaambia waandishi wa habari, “Sisi na City wote tunajua yote kuhusu hali ya Tevez lakini tumeamua kuhairisha mazungumzo hadi wiki ijayo, kwa kuwa sasa attention yote ipo katika mchezo wa Jumapili.”

TFF YATOA ITC KWA SAMATA, OCHAN

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa wachezaji Mbwana Samata na Patrick Ochan waliojiunga na timu ya TP Mazembe wakitokea Simba. TFF ilipokea maombi ya uhamisho huo wa kimataifa Januari 10 mwaka huu kutoka Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (FECOFA) kwa niaba ya TP Mazembe. Kwa kupata ITC maana yake ni kuwa Samata na Ochan sasa wanaweza kuichezea TP Mazembe kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo mechi zake za mchujo zinaanza mwezi ujao. Pia TP Mazembe inatakiwa kulipa asilimia 5 ya mauzo ya Samata ikiwa ni mchango maalumu (Solidarity Contribution) kwa timu alizopitia mchezaji huyo kwani hajafikisha umri wa miaka 23. Timu zitakazopata mgao wa asilimia hiyo 5 ni Kimbangulile FC na Mbagala Market ambayo siku hizi inaitwa African Lyon. Kwa mujibu wa kanuni za uhamisho wa wachezaji za Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA) fedha hizo zinatakiwa kulipwa ndani ya siku 30 tangu ITC ilipotolewa kwa mchezaji husika.

USAJILI WA YANGA, SIMBA WAPITA CAF

Wachezaji wote wa klabu za Yanga na Simba walioombewa usajili Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho umepita. Klabu hizo ziliombea wachezaji 28 kila moja. Hata hivyo Simba ambayo itacheza Kombe la Shirikisho awali iliombea usajili wachezaji 26 kabla ya baadaye kuwaongeza Ulimboka Mwakingwe na Derreck Walulya. Katika michuano hiyo Yanga imepangiwa Zamalek ya Misri ambapo itaanzia nyumbani wakati Simba itaanzia ugenini jijini Kigali, Rwanda kwa kuikabili Kiyovu Sport ya huko.

DARRON GIBSON ASAJILIWA EVERTON.Kiungo wa Manchester United Darron Gibson amejiunga na Everton kwa deal la mkataba wa miaka 4 na nusu.


The 24-year old Gibson amaehamia upande wa Merseyside kwa ada ya uhamisho ambayo haikutajwa, akiwa mchezaji wa pili kusajiliwa mwezi January na Everton baada ya London Donavan kutoka LA Galaxy.


Kiungo huyo ambaye ni zao la timu ya vijana ya United, alifunga mabao 10 katika michezo 60 tangu alipoingia katika kikosi cha kwanza cha United mwaka 2005.

TWIGA STARS UWANJANI KESHO

Timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) kesho (Januari 14 mwaka huu) inacheza na wenyeji Namibia katika mechi ya kwanza kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) itakayofanyika Uwanja wa Sam Nujoma jijini Windhoek kuanza saa 12 jioni kwa saa za Afrika Mashariki. Twiga Stars iliwasili salama jijini Windhoek jana (Januari 12 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwa ndege ya Air Namibia ikitokea Johannesburg ambapo imefikia Safari Hotel. Baada ya mapumziko jana jioni ilifanya mazoezi.Leo jioni (Januari 13 mwaka huu) imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Sam Nujoma ambapo ndipo mechi itachezwa kesho. Hali ya hewa ya Windhoek ni baridi kidogo kulinganisha na Dar es Salaam.

VILLAS BOAS: LAMPARD AUZWI, BADO NAMUHITAJI.


Frank Lampard ameambiwa kwamba anabakia kuwa mchezaji muhimu katika mipango ya Chelsea hata kama kwa sasa sio mchezaji anayeanza kila siku.

Future ya Lamapard imekuwa ikizua gumzo tangu Andre Villas Boas alipoanza kumueka benchi.

Sportmail liliripoti wiki iliyopita kwamba Manchester United walikuwa wakijipanga kutake advantage ya hali hiyo katika kocha na kiungo huyo ili wapeleke ofa ya kumsajili.

Lakini Villas-Boas amesema Lampard, 33, anakubaliana na majukumu anayopewa ndani ya klabu hiyo.

Mreno huyo alisema: “Kwa hakika, Lampard hauzwi. Kila mchezaji anataka kupata nafasi ya kucheza.

“Ni kawaida kila mchezaji anataka kuhusika katika upangwaji kikosini. Frank, na jinsi alivyo na historia anayoiwakilisha, anataka kucheza muda wote, lakini kila mchezaji anashindania nafasi.

“Nimeshasema msimu hivi msimu mzima, hata kama Frank atakuwa akipata uda wa kucheza kuliko wengine, na ukiangalia kwa umakini Frank ni mchezaji wa tano au sita katika wale wanaongoza kutumika at Chelsea.”

Wakati huo huo, Chelsea wamekataa ofa ya £3million kutoka Queens Park Rangers kwa ajili ya mlinzi Alex.

Villas Boas ana matumaini ya kumsaini rasmi Gary Cahil kutoka Bolton mapema kabla ya mchezo dhidi ya Sunderland.

SILVA ATOA ONYO: MECHI ZOTE ZIJAZO TUTACHEZA KAMA FAINALI


David Silva jana usiku alitoa onyo kwa wapinzani wao na kuwaambia wachezaji wenzake wa Manchester City : Tuchezeni mechi zote zilizobakia kama fainali.”

Mhispania huyo ambaye kwasasa anajiuguuza na maumivu ya kifundo cha mguu alikuwa jukwaani akiangalia namna timu yake ikipoteza mechi yake ya pili katika uwanja wao dhidi ya Liverpool ndani ya kipindi cha masaa 72.

Silva sasa anajipanga kucheza dhidi ya Wigan Jumatatu, huku City wakiwa wanajipanga kuongeza wigo wa pointi katika uongozi wao wa premier league, na kuwaacha Spurs na United wakigombea nafasi ya pili.

“Kutolewa katika FA Cup na United ilikuwa uchungu sana – tulikuwa tunataka sana kurudisha ubingwa ule.

Lakini iliniuma zaidi kuona timu yangu ikifungwa katika Carling nikiwa naangalia jukwaani. Yalikuwa matokeo mabaya na naamini tutaibuka katika mchezo wa pili @Anfield. Bado tuna nafasi nzuri ya kufika fainali.” Alimaliza Silva.

KARAMA NYILAWILA: SITISHWI NA KUNYANG'ANYWA MKANDA


Bondia Karama Nyilawila ameibuka na kudai kitendo cha kunyang'anywa mkanda wake wa ubingwa wa Dunia wa WBF, na waandaaji wa mashindano hayo hakimsumbui kwani yeye anachoangalia ni maslahi yake.

WBF jana ilitangaza kumnyang'anya ubingwa huo kupitia kwa wasimamizi wa pambano hilo hapa nchini Rais wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST), Emmanuel Mlundwa baada ya kutangaza kucheza pambano lisilo la ubingwa na Francis Cheka, kitu ambacho hakikutakiwa na WBF.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Nyilawila alisema, hawezi kucheza pambano kwa kutafuta sifa bila kuwa na fedha ya kujikimu kimaisha kwani yeye anachoangalia zaidi ni maslahi.

"Kunyang'anywa ubingwa hakunitishi kama historia ya kuwa bingwa wa Dunia wa WBF mwaka juzi itabaki kuwa pale pale ingawa wameninyang'anya mkanda bila kupigwa, mimi natafuta pesa sifa hazina nafasi kwangu kwani ubingwa wa Dunia naweza kuwania hata katika mikanda mingine kwa kuwa vyama vya mchezo wa ngumi vipo vingi Duniani," alisema Nyilawila.

Alisema amekaa kipindi kirefu bila kuwa na pesa na hata kupanda ulingoni sasa amepata sehemu ya kujikwamua hawezi kuipoteza kwani hata pesa ambazo angezipata huko ni ndogo kuliko anazozipata katika pambano lake hilo na Cheka.

Alisema kwa sasa ameishapandisha uzito hadi kg 75 ambao amesaini kucheza na Cheka sasa ingemuwia vigumu kushusha haraka uzito huo hadi kufikia kg 72 ambao alisaini katika ubingwa huo wa Dunia.

Aliongeza kuwa pambano lake na Cheka liko palepale na kwa sasa anaendelea kujifua na ana imani kumchapa hata wakifika raundi ya mwisho.

Naye kwa upande wake Promota wa pambano hilo, Philemon Kyando alisema, maandalizi yanaendelea ambapo mabondia wote wapo katika ari ya kushindana, pambano hilo litasimamiwa na TPBC.

Aliwataja mabondia watakaosindikiza pambano hilo kuwa ni Maneno Osward 'Mtambo wa gongo' akicheza na Nasib Ismail, Chaurembo Palasa na Seba Temba, Venance Mponji na Ibrahim Elask na Antony Mathias akiwa na Juma Afande.

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Pacquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kibao ‘DVD’ hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila ‘Super ‘D’.

“Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Nyilawila ili kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi,” alisema Super ‘D’.

Wayne rooney alipoifungia Liverpool bao...

AZAM YATWAA KOMBE LA KWANZA.


Timu ya Azam FC imetwaa ubingwa wake wa kwanza mkubwa baada ya kulitwaa kombe la Mapinduzi 2012 kwa kuwachabanga Jamhuri 3-1 katika mchezo wa fainali ya kombe hilo uliochezwa uwanja wa Amaan.

Azam FC wamefuta ndoto za Jamhuri za kutwaa kombe hilo na kukabidhiwa kiasi cha shilingi milioni tano na medali za dhahabu kwa kushusha kipigo hicho kilichiowaacha mashabiki wa timu hiyo kuondoka vichwa chini.

Safari ya Azam FC visiwani hapa imekuwa ya mafanikio kwa kupata kombe hilo linalofungua njia kwa makombe mengine.

Katika mchezo huo Azam FC walicheza kandanda safi kama waliloonyesha katika mechi zilizopita wakati Jamhuri waliingia uwanjani muda wote walikuwa wanalinda lango lao lakini hawakuepuka kipigo hicho.

Jamhuri walikuwa wa kwanza kupata goli katika dakika ya 17 lilofungwa na Ally Othman Mmanga baada ya mabeki wa Azam na kipa mwadini kufanya uzembe na kushindwa kuokoa mpira huo.

Dakika ya 40 John Bocco alisawazisha goli hilo kwa shuti kali lililomshinda kipa wa Jamhuri Jafari Talib na kupeleka timu hizo mapumziko zikiwa sare ya 1-1.

Kipindi cha pili Azam FC walikuwa makini zaidi kutafuta ushindi huo kwa kucheza mpira wa hali ya juu, Azam FC walipata nafasi ya kutawala mchezo nyakati zote kutokana na Jamhuri kucheza upande mmoja wa kuzuia.

Kiungo wa Azam Salum Aboubakari ‘Sure Boy’ aliwasumbua viungo wa Jamhuri akishirikiana na viungo wengine, Abdulhalim Humud, Abdi Kassim na Michael Kipre waliweza kutumia nafasi zao kutengeneza mashambulizi mengi.

Dakika ya 87 beki wa Jamhuri Mrisho Ahmed alijifunga akiwa katika jitihada za kuokoa mpira wa kona uliopigwa na Mrisho Ngassa.

Ngassa aliyeingia kuchukua nafasi ya Abdi Kassim ‘Babi’ aliandika goli la tatu kwa Azam baada ya kumalizia kazi nzuri iliyotengenezwa na Kipre Tchetche ikamkuta Gaudence Mwaikimba na kutua miguu kwa Ngassa.

Ushindi huo wa 3-1 umeacha simanzi kwa Jamhuri na wazanzibari wengi umepeleka kombe hilo la kwanza kwa Azam FC tangu ilipoingia ligi kuu misimu minne iliyopita.

Golikipa Mwadini Ally amechaguliwa kuwa golikipa bora wa michuano hiyo kwa kufungwa magoli matatu tangu kuanza kwa michuano na mshambuliaji John Bocco ameibuka mfungaji bora kwa kuwa na magoli manne sawa na Ally Mmanga wa Jamhuri wote wamekabidhiwa zawadi na kiasi cha shilingi laki moja.

source: www.azamfc.co.tz

Thursday, January 12, 2012

AZAM KUENDELEZA UBABE WAKE LEO DHIDI YA JAMHURI? MAPINDUZI CUP FINAL.


Michuano ya Kombe la Mapinduzi inafikia tamati leo kwa timu ya soka ya Azam ya Dar es Salaam kumenyana na Jamhuri ya Pemba.

Mechi hiyo inatarajiwa kuwa na msisimko na ushindani wa hali ya juu kutokana na timu zote hizo kuonyesha soka safi tangu mwanzoni mwa michuano hiyo.


Azam ilifika hatua ya fainali baada ya kuwachapa mabingwa watetezi, Simba, mabao 2-0

katika mechi ya nusu fainali huku Jamhuri ikiifunga Mafunzo ya Unguja mabao 2-1 katika mechi nyingine ya nusu fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Amaan juzi usiku.


Fainali hiyo ambayo itachezwa saa 2:00 usiku wa leo, inatarajiwa kushuhudiwa pia na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, ambaye ndiye mgeni rasmi katika siku muhimu ya kuadhimisha siku ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Katika mchezo huo wa juzi, Jamhuri ilicheza mchezo safi na wa kufundishwa kitu ambacho

kimeweza kumpa jeuri kocha wao, Renatus Mayunga ambaye ameahidi kuwa atatumia

uzoefu wake ili aweze kutwaa ubingwa huo.


Akizungumza baada ya kumalizika kwa pambano hilo kocha huyo alisema kwamba

anaamini kuwa kikosi chake kitaweza kujirekebisha makosa na kucheza mchezo mzuri

utakaowapatia ubingwa.


Hata hivyo, alisema pamoja na kuwa Azam imeonesha kiwango kizuri lakini ana imani vijana wataweza kutoa ushindani na kuweza kushinda mchezo huo.


“Mchezo utakuwa mgumu kwa vile Azam imeonesha kiwango kizuri katika mechi zake zote lakini napendelea zaidi kombe libaki nyumbani,” alisema.


Naye kocha wa timu Azam, Stewart Hall ameahidi kuendeleza ushindi katika mchezo huo na kuweza kutwaa ubingwa.


Jumla ya timu nane zilikuwa zikishiriki michuano hiyo ambazo ni Yanga, Simba, Azam FC, Jamhuri, Mafunzo, Miembeni United, KMKM na Kikwajuni.

CAPTAIN FANTASTIC GERRARD AZIDI KUZAMISHA JAHAZI LA MACHESTER CITY

Wednesday, January 11, 2012

HENRY: NATAKA KUWAKOMESHA SPURS KABLA SIJAONDOKA EMIRATES


Thierry Henry anataka kuwaadabisha Tottenham Spurs kabla hajaondoka Arsenal na kurudi Marekani.

The French striker, 34, currently anacheza kwa mkopo @Emirates mpaka mwezi wa pili tarehe 16, akiwa na uhuru kuongeza siku za kukaa mpaka siku nyingine 10.

Kitu ambacho kitampa nafasi ya kucheza North London derby dhidi ya Tottenham tarehe 26 mwezi ujao.

Henry alisema: “ Itakuwa ndoto kucheza mechi hiyo dhidi ya Spurs. Yote inategemea jinsi kocha atakavyoamua ni kwa muda gani nitakuwepo hapa.

“Msisahau kuwa mimi bado mchezaji wa New York na kuwa nahodha pia kunaniongezea majukumu mengine ambayo napaswa kuyaheshimu.

“Kwa hakika nitakuwa bado nipo hapa kwa mchezo dhidi ya Manchester United na pia ningependa kucheza mechi ya Champions league dhidi ya AC Milan, ingawa sifikirii kama nitakuwepo hapa katika mchezo dhidi ya Tottenham kwasababu nitakiwa nirudi New York kujiandaa na msimu mpya."

SHWEINSTEIGER: XAVI NA INIESTA NI BORA DUNIANI


Siku moja baada ya Lionel Messi kutangazwa kuwa mchezaji bora wa dunia, kiungo wa Bayern Munich Bastian Schweinsteiger amesema anaamini kuwa viungo wa Barcelona Xavi na Andres Iniesta ndio wachezaji bora wa dunia kwa mujibu wake.

Nahodha huyo msaidizi wa Ujerumani kwa siku za hivi karibuni amekuwa akifananishwa na majembe hayo mawili ya Barcelona na Spain akiongea na mtandao wa Goal com, alisema Xavi na Iniesta wana uwezo mkubwa na amedhamiria kujituma mpaka kufikia uwezo wao.

“Xavi na Iniesta ni wachezaji wa mfano wa kuigwa. Wanacheza katika timu bora ya dunia. Na tutajaribu kuweza kupambana kufikia uwezo wao na kuwashinda. Endapo tutawafunga Barcelona basi hapo ndipo baadhi ya wachezaji wa Bayern wanaweza kuonekana kama wachezaji bora.”

SOMA ALICHOSEMA OKOCHA KUHUSU MICHUANO IJAYO YA MATAIFA YA AFRIKA


The Cup of African Nations is almost upon us and I am sure everyone is looking forward to seeing who will be crowned the Champions of Africa.

Congratulations to all the teams who have qualified. It is no easy task to make it through qualification and all of those who have done so are there because they deserve to be. I would like to take this opportunity to congratulate my Guinness Football Challenge colleague Kalusha Bwalya on Zambia's success in reaching the finals and wish them the best of luck.

In the absence of some of the so-called "big guns" I think it is fair to say that both Ghana and Ivory Coast are the favourites to win. But some of the shock results in the qualifiers have shown that no team can take anything for granted this year.

For me it is a great shame that Nigeria will not be participating. Along with Cameroon and Egypt, we are probably the surprise absentees. However a look through the teams that will be present reveals that African football is changing, as there will also be countries present who have never before reached this level, such as Niger and Botswana. This is a wake-up call for the more established footballing countries in Africa and shows that teams such as Nigeria need to rise to these new challenges in order to return to the top table of African football. But I am confident that with the right levels of commitment and planning, along with a new focus, Nigeria will bounce back.

What Nigeria is currently experiencing is not new in football. Generally speaking, teams that have a so-called golden era tend to have a dip in fortunes when that generation moves aside and the plans for a new generation are laid. However, I believe that Nigeria needs to let go of the past in order to really move forward, and that means focusing on the development of young talent and looking for fresh blood rather than relying on older players, some of who are past their best. Nigeria is blessed with football talent, but that talent needs to be nurtured and developed if we are to get the benefits of it and take our game to the next level.

Following our disappointing displays in the 2010 World Cup and our failure to qualify for CAN 2012, it is the perfect time to go back to the drawing board and try something new.

I was present at the African Player of the Year Awards in Accra, Ghana last month and was very privileged to receive the Legends Award alongside Mustapha Hadji. It was great to see Yaya Toure crowned as the 2011 African Player of the Year as he has been in outstanding form for both his club, Manchester City, as well as for Ivory Coast.

In second and third place came Ghanaian midfielder Andre Ayew and Malian Seydou Keita, while the African-based Player of the Year award went to Tunisian midfielder Oussama Darragi. All of these players are worthy of such accolades. But the fact that no Nigerian player has been in the top three for the African Footballer of the Year award since it was won last by Nwankwo Kanu in 2000 tells it's own story.

This, and the Super Eagles absence from CAN 2012, should act as a huge incentive to the next generation of Nigerian players to rise up and prove the critics and doubters wrong in the years to come. As we have seen in the Guinness Football Challenge, only outstanding players win awards and I believe that Nigerians can start to do that again, both as individuals and as a team, with a new injection of commitment, passion, ambition and, of course, hard work. But the over-riding priority is to start putting the focus on young talent. Just like in the Guinness Football Challenge, the beautiful game is all about reaching maximum potential, and with the right approach, I believe we will see the Super Eagles flying high once more.

Please remember to drink responsibly 18+/21+.

Jay Jay Okocha is a Guinness® Football Challenge™ ambassador and will be appearing on a special episode of the show later in the year.

SERIKALI: TWIGA TUTOENI KIMASOMASO WINDHOEKNaibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu ameitaka timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) kuhakikisha inabuka na ushindi kwenye mechi yake dhidi ya Namibia.

Mechi hiyo ya kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) itachezwa Januari 14 mwaka huu jijini Windhoek, Nambia na timu hizo zitarudiana Januari 29 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Waziri ametoa mwito huo leo mchana (Januari 11 mwaka huu) katika hafla fupi ya kuiaga timu hiyo na kuikabidhi Bendera ya Taifa iliyofanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Timu hiyo yenye msafara wa watu 25 inaondoka leo saa 2 usiku (Januari 11 mwaka huu) kwa ndege ya PrecisionAir kupitia Johannesburg, Afrika Kusini ambapo kesho alfajiri (Januari 12 mwaka huu) itaunganisha safari hiyo kwa ndege ya Air Namibia hadi Windhoek.

Wachezaji walioko kwenye kikosi hicho ni Asha Rashid, Aziza Mwadini, Ettoe Mlenzi, Fadhila Hamad, Fatuma Bushiri, Fatuma Khatib, Fatuma Mustapha, Fatuma Omari, Maimuna Said, Mwajuma Abdallah, Mwanahamisi Omari, Mwanaidi Hamisi, Mwapewa Mtumwa, Pulkaria Charaji, Rukia Hamisi, Siajabu Hassan, Semeni Abeid, Sophia Mwasikili za Zena Khamisi.

Benchi la Ufundi lina Kocha Mkuu Charles Boniface, Kocha Msaidizi Nasra Mohamed, daktari wa timu Dk. Christina Luambano na Meneja wa timu Furaha Francis.

Kiongozi wa msafara ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Lina Mhando na Naibu kiongozi wa msafara ni mjumbe wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Layla Abdallah.

Timu hiyo itarejea alfajiri ya Januari 16 mwaka huu kwa ndege ya PrecisionAir.

WADAU MNAUKUMBUKA HUU MTANANGE ?

PAMBA VS USHIRIKA

AISEE ANAYEUKUMBUKA HUU MPAMBANO ULIPIGWA KWENYE DIMBA LA CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA ATUKUMBUSHENADAHANI NIMEPENDEZA AU WEWE UNAONAJE ?MILOVAN: NIMERIDHISHWA NA UCHEZAJI WA TIMU YANGU


Head coach wa Simba, Milovan Cirkovic amesema ameridhishwa na kiwango kilichooneshwa na timu yake licha ya kufungwa mabao 2-0 na Azam FC, kwenye mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi juzi.

Wekundu hao wa Msimbazi walifungwa mabao hayo na washambuliaji, John Bocco na Gaudence Mwaikimba, lakini Mserbia huyo ameoneshwa kuridhishwa na kiwango cha timu
yake.

Bocco alifunga bao hilo kwa kumpiga chenga golikipa, Juma Kaseja ikiwa ni dakika ya tisa baada ya kuanza kwa mchezo huo.

Akitokea benchi, Mwaikimba aliongeza bao la pili kwa Azam ambalo ndilo liliwazima kabisa Simba.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga, ambaye aliingia dimbani kuchukua nafasi ya kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast, Kipre Balou, aliwatoka mabeki wa Simba kabla ya kumfunga Kaseja kwa shuti.

“Kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Azam siyo matokeo mabaya kwa timu yangu na nina imani kubwa na vijana wa timu yangu. Kiukweli tulitawala mchezo, lakini tulishindwa kutumia nafasi tulizopata. Wapinzani wetu walitumia nafasi zote walizozipata,” alisema.

“Ilikuwa mechi nzuri kwa upande wangu, kwasababu ulikuwa mchezo mzuri dhidi ya timu bora kwa sasa hapa nchini. Nafikiri tulicheza vizuri zaidi usiku ule (Jumatatu), lakini
tulicheza na timu nzuri zaidi,” alisema.

Milovan alibainisha kwamba wachezaji wake wanazidi kuimarika jinsi siku zinavyosonga mbele, na kuahidi kwamba watafanya vizuri zaidi wakati wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu inayoanza wiki mbili zijazo, pamoja na michuano ya Kombe la Shirikisho la CAF dhidi ya Kiyovu ya Rwanda mwezi ujao.

Naye kocha wa Azam FC, Stewart Hall raia wa Uingereza alisema kwamba timu yake ilifanya kazi kubwa na kuweza kupata ushindi huo.

Alisema licha ya wao kushinda, lakini Simba ilikuwa na safu nzuri zaidi ya ushambuliaji, ingawa ilishindwa kutumia nafasi nyingi ilizozipata.

Azam sasa itacheza na mshindi wa mchezo kati ya Mafunzo na Jamuhuri kwenye fainali ya Mapinduzi kesho kwenye Uwanja wa Amaan.

Mshindi wa mashindano hayo atajinyakulia zawadi ya Sh milioni 5 na mshindi wa pili Sh milioni 3.

TFF: WAOMBA MECHI YA YANGA NA ZAMALEK ISOGEZWE MBELE


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeomba mechi ya marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Dar es Salaam na Zamalek ya Misri iliyopangwa kufanyika jijini Cairo, Misri
Machi 1,2 au 3 isogezwe mbele kwa wiki moja.

Pia TFF imeomba mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba ya Dar es Salaam na Kiyovu ya Rwanda iliyokuwa ifanyike Dar es Salaam mwanzoni mwa Machi kama mechi ya Yanga nayo isogezwe mbele kwa wiki moja.

Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema Dar es Salaam jana kuwa wameandika barua Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuomba mabadiliko hayo kutokana na mechi hizo kukaribiana na ile ya timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Alisema Taifa Stars itacheza mechi na Ivory Coast kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia Februari 29, hivyo wachezaji kuweza kucheza mechi nyingine Machi mwanzoni itakuwa ni kutowapa nafasi ya kupumzika.

Alisema wachezaji wengi wanaounda Taifa Stars pia wapo kwenye timu za Simba na Yanga,
hivyo mazingira ya tarehe hizo yatawabana kuweza kutumikia majukumu ya pande zote mbili.

Yanga itacheza na Zamalek mchezo wa kwanza katika raundi ya awali jijini Dar es Salaam Februari 18 mwakani, kabla ya mchezo wa marudiano wiki mbili baadaye jijini Cairo nchini Misri.

Mshindi wa mechi hizo atakutana na kati ya Missile ya Gabon na Africa Sport ya Ivory Coast, katika raundi ya kwanza, itakayoanza Machi mwakani.

Wakati huohuo, Osiah alisema TFF haiwezi kushughulikia tuhuma zilizotolewa na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Miembeni United ya Zanzibar Salum Bausi kwamba alishinikizwa timu yake ifungwe na Simba katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi hatua ya makundi wiki iliyopita.

Akizungumza jana, Osiah alisema madai ya Bausi yanatakiwa yashughulikiwe na Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) ama mamlaka zinazopambana na rushwa Zanzibar.

Tuesday, January 10, 2012

MESSI ALIMCHAGUA XAVI KUWA MWANASOKA BORA WA DUNIA 2011..Captain -Argentina Lionel Messi 1. Xavi 2.Iniesta Andrés 3.Agüero Sergio
Captain -Cameroon Samuel Eto'o Messi 1. Lionel 2. Xavi 3. Iniesta Andrés
Captain- England John Terry 1. Xavi 2. Messi Lionel 3. Rooney Wayne
Captain-Italy Gianluigi Buffon 1. Messi Lionel 2. Rooney Wayne 3. Iniesta Andrés
Captain -Tanzania Henri Joseph 1. Messi Lionel 2. Cristiano Ronaldo 3. Xavi

Coach - Germany Joachim Loew 1. Xavi 2. Messi Lionel 3. Iniesta Andrés
Coach - Tanzania Jan Poulsen 1.Messi Lionel 2. Xavi 3. Cristiano Ronaldo
Media - Tanzania Boniface Wambura 1. Messi Lionel 2. Agüero Sergio 3. Villa David

Hili ndo bao bora la mwaka 2011 toka kwa Neymar

TAARIFA KUTOKA TFF.

AHADI YA WAZIRI MKUU KWA STARS
Waziri Mkuu Mizengo Pinda tayari amekabidhi sh. milioni 10 kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ikiwa ni ahadi yake aliyotoa kwa Taifa Stars ikiwa ni motisha kwa wachezaji wa timu hiyo kabla ya mechi yao na Chad iliyochezwa Novemba Mosi mwaka jana jijini N’Djamena.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa Meneja wa Taifa Stars, Leopold Tasso linaanda orodha ya wachezaji wanaostahili kunufaika na ahadi hiyo, na baadaye kuiwasilisha BMT kwa ajili ya mgawo kwa wahusika.

Tunamshukuru Waziri Mkuu Pinda kwa ahadi hiyo, kwani Taifa Stars ilifanikiwa kushinda mechi hiyo ya ugenini mabao 2-1, ushindi ambao bila shaka ulichagizwa na ahadi hiyo.

KUUZWA KWA TIMU YA SMALL KIDS
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana Desemba 30 mwaka jana ilijadili masuala mbalimbali yaliyofikishwa mbele yake ikiwemo malalamiko juu ya kuuzwa kwa timu ya Small Kids ya Rukwa.

Usikilizaji wa suala hilo uliahirishwa na Kamati kuagiza kwanza ipatiwe vitu vifuatavyo; Katiba iliyosajiliwa ya Small Kids, muhtasari (minutes) na uamuzi wa kikao chochote kilichofanyika kuzungumzia mauzo ya timu hiyo ambayo iko daraja la kwanza.

Pia Kamati inataka ipatiwe mawasiliano (correspondences) yote yaliyofanyika kuhusiana na ununuzi/mauzo ya timu hiyo. Hivyo suala hilo litasikilishwa katika kikao kingine cha kamati baada ya kuwasilishwa nyaraka hizo.

MGOGORO WA UONGOZI TAREFA
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji itatuma wajumbe wake wawili Tabora kukutana na Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora (TAREFA).
Wajumbe hao katika kikao chao na Kamati ya Utendaji ya TAREFA watasikiliza kuhusu kiini cha mgogoro uliopo na baadaye watawasilisha taarifa kwa Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji. Kamati itafanyia kazi ripoti hiyo kabla ya kufanya uamuzi.

MAREKEBISHO YA KATIBA ZA WANACHAMA
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji pia ilifanyia kazi suala la marekebisho ya katiba za wanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Katiba hizo zimegawanywa katika makundi matatu; katiba za wanachama wapya, katiba ambazo tayari zimerekebishwa na katiba ambazo hazijarekebishwa.

Maelekezo ya Kamati ni kuwa itatoa mwelekeo (roadmap) utakaoonesha muda wa mwisho (deadline) wa kufanya marekebisho kwa makundi yote hayo matatu ambapo kwa wanachama watakaoshindwa hawataruhusiwa kuingia kwenye Mkutano Mkuu wa TFF.

Maeneo ya msingi ya marekebisho ni sifa za uongozi. Katiba zote za wanachama wa TFF kwa upande wa sifa za uongozi ni lazima ziwe sawa. Maeneo mengine ni kuainishwa wazi kwa majukumu ya Kamati ya Utendaji, Mkutano Mkuu na namna ya kutatua migogoro ya wanachama ili kuepuka watu kwenda mahakamani.


Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

AZAM YAENDELEZA UBABE KWA VIGOGO: YAITANDIKA SIMBA 2-0 NA KUIVUA UBINGWA


Timu ya Azam FC imekuwa zaidi ya shule kwa timu za Simba na Yanga katika michuano ya Mapinduzi Cup, kufuatia kuifundisha Yanga kucheza mpira na kisha kuwapa somo Simba kutumia nafasi wanazopata.

Washambuliaji wawili wasio kubalika nchini Gaudence Mwaikimba na John Raphael Bocco ndio waliopeleka kilio kwa Simba hii leo, ambapo Simba walitengeneza nafasi za kutosha na kushindwa kuzitumia.

Mchezo ulitulia kati huku viungo wa Simba wakitawala eneo hilo katika kipindi cha kwanza na kutengeneza nafasi lukuki ambazo ziliishia kupotea huku Azam FC wakitumia vyema nafasi ya dakika 10 kujipatia goli la kuongoza lililo fungwa na John Raphael Bocco.

Simba ambao walionekana kuwa nadhamira ya kusawazisha goli hilo bila mafanikio, walipigiwa msumari wa pili na mtokea bench Gaudence Mwaikimba aliyechukua nafasi ya Kipre Tchetche katika dakika ya 85 na katika dakika ya 90 alitupia goli la pili.

Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Amani Zanzibar ulishuhudiwa na mashabiki lukuki, huku mchezo ukiwa ni wakasi na ushindani Mkubwa.

Kwa matokeo hayo ya goli 2-0 walio upata Azam FC, una wavua ubingwa Simba na hivyo Azam kutinga fainali ambayo itachezwa january 12 katika uwanja wa Amani, wakati mpinzani wake akitarajiwa kujulikana Kesho pale Mafunzo watakapo chuana na Jamhuri ya Pemba katika nusu fainali ya pili.

ABOODMSUNI

THE RETURN OF THE KING CHOGO: DAKIKA 10 ZAMTOSHA THIERRY HENRY KUWAFUNDISHA AKINA CHAMAKH NAMNA YA KUFUNGA.

MESSI, GUARDIOLA, FERGUSON WALAMBA TUZO ZA FIFA - HUKU BARCA, MADRID NA MAN UNITED WAKIUNDA KIKOSI CHA DUNIA CHA MWAKA 2011.


Top prize: Argentina's Lionel Messi won the Ballon D'Or for the third year in a rowLionel Messi alitunukiwa tuzo ya FIFA Ballon d’O kwa mara ya tatu mfululizo.

Barcelona;s 24-year old Argentina striker aliwashinda mchezaji mwenzie wa Barcelona Xavi na mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo katika tuzo hiyo ya mchezaji bora wa mwaka.

Happy boy: Messi poses with his award and Colombian singer Shakira Shemejiiiiiiiii Shakira akimpongeza Lionel Messi.

Messi, man of the match katika champions league final mwaka 2011, pia alishinda kombe la La Liga, Spanish Supercopa, UEFA Super Cup na Kombe la klabu bingwa ya dunia mwaka uliopita.

Manager wa Manchester United Sir Alex Ferguson na Xavi wote walitoa maneno ya heshima kwa Messi.

Ferguson alisema Messi anaweza kuwekwa katika mizani ya magwiji wa soka duniani katika miaka mingi ijayo, hata kama bado ana miaka 24.

‘Maneno yamekuwa yakisemwa kila kuhusu kwamba wachezaji kama Pele kutoka katika zama za miaka ya 50 wangeweza kucheza katika kipindi hiki, jibu ni kwamba wachezaji wakubwa wanaweza kucheza katika kizazi chochote. Lionel Messi angeweza kucheza katika miaka ya 1950s na sasa pia, kama ilivyo kwa Di Stefano, Pele, Maradona, Cruyff kwa sababu wote ni wachezaji magwiji.” –Fergie


Past and present: Messi is congratulated by former winners Michel Platini and RonaldoMessi akipongezwa na washindi wa zamani wa tuzo hiyo Micheal Platini na Ronaldo De Lima,


Xavi nae alimuunga mkono Ferguson kwa kusema:” Lionel bado mdogo, ana miaka 24 tu na nafikiri atavunja rekodi zote zilizopo katika huu mchezo. Atakuja kuwa moja ya wachezaji wakubwa waliowahi kutokea katika mchezo huu wa mpira wa miguu.”

Mapema jioni ya jana Ferguson na Pep Guardiola walizawadia tuzo katika shrehe hizo.


Sir Alex and Sepp Blatter

Ferguson alizawadiwa FIFA Presidential award for services to football, na alikabidhiwa tuzo hiyo na raisi wa FIFA Sepp Blatter.


Top man: Barcelona's Pep Guardiola wins the FIFA World Coach of the Year award

Pep Guardiola alitajwa kama kocha bora wa Dunia in 2011 baaada ya kuiongoza Barcelona kushinda makombe matano


Boy from Brazil: Neymar picks up the FIFA Puskas award for best goal (below)

Neymar alishinda tuzo ya Puskas kwa kufunga bao bora la mwaka.

Pia jana kilitangazwa kikosi bora cha mwaka kwa mujibu wa FIFA huku kikosi hicho kikitaliwa na wachezaji wa Barcelona, Manchester United na Real Madrid pekee.


The good and the great: Wayne Rooney receives the FIFA/FIFPro World XI award from Brazilian legend PeleWAYNE ROONEY AKIKABIDHIWA TUZO YA KUWA MOJA YA WACHEZAJI WALIOUNDA KIKOSI CHA MWAKA


KIKOSI CHA FIFA CHA MWAKA

Iker Casillas (Real Madrid), Dani Alves (Barcelona), Gerard Pique (Barcelona), Sergio Ramos (Real Madrid), Nemanja Vidic (Man Utd), Andres Iniesta (Barcelona), Xabi Alonso (Real Madrid), Xavi (Barcelona), Lionel Messi (Barcelona), Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Wayne Rooney (Man Utd).