Search This Blog

Friday, January 13, 2012

CLOUDS MEDIA GROUP YAITANDIKA MAXMALIPO MABAO 5-0

Timu ya watoa burudani Clouds Media Group The Dream Team leo iliendeleza rekodi yake ya kutofungwa tangu mwaka 2012 uanze baada ya kuwafunga bila huruma Max Malipo kwa mabao 5-0 . Mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Tanganyika Packers ulianza majira ya saa kumi na nusu ambapo kikosi cha Clouds kiliwakilishwa na Golikipa Frank , beki wa kulia ambaye pia ni nahodha wa timu Geoffrey Lea,Shaffih Dauda,Ibrahim Massoud Maestro,Ali Siso,Abdul Mohamed , Antonio Nugaz,James Andrea Tupa Tupa,Peter Ngassa,Anatoly Kabezi ,Salim Mhando na Athumani Kikucha. Katika Mchezo huo mabao ya Clouds Media Group Yalifungwa na Salim Mhando aliyefunga mabao mawili,Athuman Kikucha ambaye naye alifunga mawili na Antonio Nugaz hata hivyo kiungo muhimu wa timu hii Shaffih Dauda aliumia mwanzoni kwenye dakika ya 25 ya mchezo na hivyo alilazimika kutoka na bado haijajulikana atakaa nje kwa muda gani. Kwa wale ambao hawakupata nafasi ya kuushuhudia mchezo huu wasikose kutazama kipindi cha Sports Bar siku ya jumatatu .
Huu ni mchezo wa pili kwa Clouds Media Group Fc The Dream Team kushinda tangu mwaka huu uanze baada ya kuwafunga Infinity Communications Ijumaa iliyopita kwa matokeo ya 4-2. Kama kawaida Chama Linawakaribisha watu wote wanaotaka kucheza mechi kutuma maombi ambayo yatajibiwa kutokana na vigezo mbalimbali ambavyo timu ya Clouds huhitaji kufikiwa na wale wote wanaotaka kucheza na timu hii kila siku za ijumaa.

2 comments:

  1. shaffih umeniacha hoi eti hujui utakaa nje kwa muda gani!

    ReplyDelete
  2. Ebana Shaffih vipi mshikaji wetu Mbwiga??nimetafuuuuta jina la kijana machachali Mbwiga mbwaguke .....nimelikosa ,,au yeye ni kibendera?au alishastaafuuuuu
    Mdau from S.Korea

    ReplyDelete