Search This Blog

Saturday, November 17, 2012

MCHEZAJI WA UJERUMANI AAMKA KUTOKA KWENYE COMA BAADA YA MWEZI 1

Klabu ya Bundesliga Hoffenheim imesema kiungo wake Boris Vukcevic ameamka kutoka kwenye coma, mwezi mmoja baada ya kujeruhiwa na ajali ya gari.

Vukcevic aliwekwa kwenye coma baada ya kufanyiwa upasuaji kufuatia ajali ya gari aliyopata tarehe 28 mwezi wa September, gari yake ilipongana na gari lingine kubwa.

Hoffenheim inasema kwamba kiungo huyo mwenye miaka 22, raia wa Ujerumani alipata fahamu masaa yaliyopita na kuweza kuzungumza na ndugu zake, lakini klabu hiy imesema kwa muonekano wa jeraha lake kichwani alilopata kwenye ajali ni vigumu kutoa utabii wowote juu ya upataji nafuu yake na kupona kabisa.

KILIMANJARO MARATHONI 2013 YAZINDULIWA

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Bi. Kushilla Thomas akishirikiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Bi. Juliana Yassoda kukata utepe kuzindua rasmi mbio za Kilimanjaro Marathon 2013 zinazotarajiwa kufanyika Moshi mwezi Machi mwaka 2013. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. (Picha: Executive Solutions)

Wash United kuungana na Taifa Stars kuweka mazingira na Usafi ‘salama’Mpira wa miguu unaweza kufanya nini kuhusu mazingira na usafi?
Zaidi ya watu bilioni 2.6 duniani wanaishi bila ya kuwa na vyoo. Barani Afrika, magonjwa ya kuhara yanayosabishwa na ukosefu wa vyoo na usafi ni hatari zaidi na ndio yanayosababisha vifo kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano, hii ni zaidi ya magonjwa kama Ukimwi, Malaria na surua ikifuatia. Takwimu kutoka mashirika ya UNICEF na WHO zinaonyesha kuwa nchini Tanzania zaidi ya asilimia 90 ya watanzania wanaishi katika mazingira machafu, na asilimia 12 hawana vyoo wala maji. Matokeo yake zaidi ya watoto 24,000 nchini Tanzania hufariki dunia kila mwaka. Tabia ya kunawa mikono kwa kutumia sabuni ni njia rahisi na haina gharama kubwa katika kuzuia magonjwa ya kuhara ambayo haitumiki sana hapa nchini hasa kwa watoto. Tatizo kubwa ni kwamba usafi wa mazingira na afya haupewi kipaumbele katika mawazo ya watu wengi katika vyombo vya habari na jamii kwa ujumla.
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Wash United inafanya kazi kuweka sawa mambo ya mazingira na usafi katika ngazi zote mahala popote na kuhamasisha watu kunawa mikono kwa sabuni kila mara. Wash United ni mpango mpya wa kwanza kutumia nguvu ya mpira wa miguu na mastaa wake katika kuhamasisha unywaji wa maji safi, mazingira safi na usafi kwa wote barani Afrika na duniani kote. Katika kukamilisha mpango wake huu Wash United imeungana na wadau mbalimbali duniani, kwa hapa Tanzania shughuli zinaendeshwa kwa msaada wa shirika la maendeleo la Ujerumani (GIZ).
Kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF)
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania limekubali kushirikiana na mpango wa Wash United katika kuhamasusha tabia ya kutunza mazingira na usafi kwenye timu za vijana kupitia mradi timu za vijana wa shirikisho hilo. Katibu mkuu wa TFF Ndugu Angetile Osiah, leo amesaini mkataba wa makubaliano kati ya TFF na Wash United. “Ushirikiano kati ya Taasisi ya Wash United na Shirikisho la mpira wa Miguu ni mpya na wa kujitolea katika sekta ya mpira wa miguu Tanzania. Akiongea kuhusu Wash United, mratibu wa Wash United nchini Tanzania Ndugu Femin Mabachi alisema “Kupitia mpira wa miguu na kwa kushirikiana na TFF, tunaweza kutunza mazingira na usafi ‘salama’ na kuongeza uwiano katika kushughulikia mambo haya katika jamii yetu.
Taifa Stars Kuongoza mpango wa Wash United
Kwa kuungana na Wash United, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litakuwa limejiunga na zaidi ya mastaa 100 wa mpira wa miguu kama Didier Drogba, Michael Ballack, Arjen Robben, Bayern Munich, Taasisi za Real Madrid na ile ya Barcelona na pia zaidi ya wananchama 30,000 wa Wash United duniani kote. Nahodha wa Taifa Stars Juma Kaseja atawaongoza wachezaji wenzake kuwa washiriki kwenye mpango huu wa Wash United na kushiriki katika kampeni nchini Tanzania na duniani kote. Zaidi ya yote wachezaji wa timu ya Taifa watashiriki katika shughuli za mchezo wa mpira wa miguu mashuleni zitakazofanyika hapa nchini zitazokuwa zikiendeshwa na taasisi hizi.

Friday, November 16, 2012

WACHEZAJI 20 WALIOITEKA ULAYA KWA KUZISAIDIA TIMU ZAO
Kabla ya kuwataja wachezaji bora 20 ambao wameiteka Ulaya, napenda kuthamini mchango wa wachezaji hawa katika timu zao Yaya Toure, Xavi, Mario Gotze, Wayne Rooney, na Hazard. Hawa wamekuwa kwenye viwango bora kabisa msimu huu huku wakiziwezesha timu zao katika kupata matokeo bora.

Frank Ribery (20)

Mfaransa huyu amekuwa akijitolea kila kitu kwa ajili ya klabu yake ya Bayern Munchen. Licha ya matatizo yake ya kugombana na winger mwenzake wa Bayern, Arjen Robben mara kwa mara, Ribbery amekuwa bora mara zote anapoingia ndani ya uwanja. Hivi karibuni Ribbery alikaririwa akisema kwamba anaipenda Bayern kuliko timu ya taifa ya nchi yake, Ufaransa. Ribbery anashika nafasi ya 20 katika viwango hivi.

Edin Dzeko (19)

Amekuwa akitokea pale anapohitajika. Edin Dzeko amekuwa bora zaidi msimu huu hasa pale anapotokea benchi, watu kama Edin huitwa Super Sub. Yeye ndiye mtu ambaye amekuwa akiipa matokeo mazuri Manchester City mara kwa mara pale inapoonekana kushindwa. Huku akiwa na kiatu cha ufungaji bora cha ligi kuu ya Ujerumani pia mchezaji bora wa wachezaji wa ligi kuu ya Ujerumani, Dzeko ameendelea kumuonesha Roberto Mancini yeye ni mchezaji wa aina gani. Dzeko amekuwa wa 19.

Demba Ba (18)

Huu ndio ulikuwa usajili bora wa msimu wa 2011/2012 kulingana na makocha wa timu za ligi kuu ya Uingereza. Baada ya Papiss Cisse kusajiliwa January, 2012, Ba alifunga goli moja tu, tangu msimu huu kuanza imekuwa kinyume chake, Cisse hafungi na Ba amerudi kuwa roho ya timu. Kama akiendelea na kiwango hiki Ba anaweza kuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Uingereza. Ba anashika nafasi ya 18.

Marco Reus (17)

Moja ya vipaji kutoka Ujerumani vinavyokuja kwa kasi ni huyu Marco Reus. Akisajiliwa kutoka Borussia Monchengladbach kuja kuziba pengo la Shinji Kagawa, Marco ameweza kushirikiana vyema na Mjerumani mwenzake, Mario Gotze pia mshambuliaji Lewamdowski katika kuiboresha timu ya Borussia Dortmund. Marco Reus ndiye mchezaji bora wa Ujerumani kwa mwaka huu, 2012. Reus anashika nafasi ya 17.

Thomas Muller (16)

Mchezaji bora kijana wa kombe la dunia, 2010. Baada ya kuwa akitokea benchi msimu uliopita wakati Mario Gomez alipokuwa katika kiwango cha juu. Thomas Muller amekuwa akitengeneza chemistry nzuri na mshambuliaji mwingine wa Bayern Munich, Claudio Pizzaro. Mara nyingi Muller amekuwa hatajwi sana midomoni mwa wapenda kabumbu lakini yeye amaandelea kutunza kiwango chake vyema na sasa yupo kwenye kiwango cha hatari. Amekuwa wa 16.

Klaas-Jan Huntelaar (15)

Wenyewe humwita Hunter, amekuwa akifananishwa na Ruud van Nistelrooy na Marco van Basten kutokana na jinsi anavyouchezea mpira. Kocha wa zamani wa Barcelona Louis van Gaal aliwahi kusema kwamba huyu ndiye mchezaji bora katika dimba la penalti. Tangu ajiunge na Schalke 04 akitokea Milan, Huntelaar amekuwa kwenye kiwango bora na ndiyo mhimili wa Schalke. Hivi sasa ana ushirika mzuri kabisa na Mholanzi mwenzake aitwaye, Ibrahim Affelay. Amekuwa wa 15.

Oscar (14)

Kipaji cha ajabu kutoka Brazil. Uwezo wa kumiliki mpira, nguvu, pasi na jinsi anavyojitoa uwanjani haipingiki kwamba Oscar atakuja kuwa moja ya wachezaji hatari sana katika timu ya taifa ya Brazil. Oscar ndiye mchezaji wa Chelsea anayeng’ara zaidi katika ligi ya mabingwa Ulaya msimu huu kuliko mchezaji yeyote mwingine ndani ya klabu. Goli la pili aliloifunga Juventus katika mechi yake ya kwanza ya ligi ya mabingwa Ulaya halitafutika kirahisi katika vichwa vya wapenzi wengi wa soka. Alipoulizwa atoe maoni yake kuhusiana na goli lile, kipa wa Juventus, Gigi Buffon alisema hivi, “Siwezi kusema ni vizuri kufungwa goli lakini ni vizuri kuwa sehemu ya goli bora kama lile. Hongera kwake”. Oscar ni wa 14.

Maroune Fellaini (13)

Mchezaji ghali zaidi wa klabu ya Everton. Huyu ndiye alikuwa gumzo zaidi wakati ligi ya Uingereza ilipokuwa katika wiki za mwanzo mpaka sasa. Akiwa ni mzaliwa Ubelgiji na asili ya Morocco, Maroune Abdellatif Fellaini amekuwa kiwango bora zaidi msimu huu kuliko msimu mwingine wowote katika maisha yake. Watu wengi wamekuwa wakiifuatilia Everton kwa sababu ya huyu mtu na yeye ndiye ubongo nyuma ya mafanikio ya Everton kwa msimu huu. Anazivutia klabu kubwa nyingi huku Chelsea ikiongoza mbio za kumnyakua, si ajabu kuona akihamia kwenye timu inayoendana na kiwango chake. Amekuwa wa 13.

Gonzalo Higuain (12)

Mtambo wa magoli kutoka mzaliwa wa Ufaransa. Huyu ndiye patna wa Cristiano Ronaldo katika kupasia mipira nyavuni pale Real Madrid kwa sasa. Mafanikio ya Gonzalo msimu huu yamechangiwa zaidi na kuumia na kiwango cha Karim Benzema kushuka. Katika siku za hivi karibuni Higuain amekuwa akishirikiana vyema na Lionel Messi katika kutengeza nafasi za magoli katika timu ya taifa ya Argentina. Amekuwa wa 12.

Luis Suarez (11)

Mchezaji ambaye amekuwa akiandamwa na mikasa ya kutosha tangu adake mpira uliokuwa ukiingia nyavuni katika mechi ya robo fainali ya kombe la Dunia pale Afrika Kusini dhidi ya timu ya Ghana. Pamoja na mikasa mingi kuwa upande wake Luis Suarez hajashuka kiwango na msimu huu tofauti na misimu mingine amekuwa akifunga magoli mengi ingawa timu yake ya Liverpool bado mambo hayajawa mazuri. Ndiye mchezaji anayeng’ara zaidi kwa majogoo wa jiji. Amekuwa wa 11.

Andrea Pirlo (10)

Ule usemi wa ng’ombe hazeeki maini uhalisia wake huonekana hapa. Watumiaji wa mvinyo humfananisha Andrea Pirlo na kinywaji hicho, kadri kinywaji kinavyozidi kukaa ndivyo ubora wake unavyoongezeka. Kadri umri wa Pirlo unavyoongezeka ndivyo kiwango chake kinavyoongezeka. Huyu ndiye chachu hasa ya mafanikio ya Juventus katika kumaliza msimu uliopita bila kufungwa na Italia kufika kwenye fainali ya kombe la Ulaya. Amefunga 10 bora.

Juan Mata (9)

Pamoja na kwamba Didier Drogba ndiye aliyeiwezesha Chelsea kushinda kombe la FA na lile la ligi ya mabingwa Ulaya kwa kiasi kikubwa katika mechi za fainali, Mata ndiye aliyekuwa mchezaji bora wa Chelsea kwa msimu uliopita. Msimu uliopita Mata alikuwa kwenye kiwango bora lakini sasa hivi amekuwa zaidi ya alivyokuwa msimu uliopita. Juan Manuel Mata Garcia anaendelea kuwa mchezaji bora wa Chelsea mpaka sasa. Huyu ndiye mchezaji bora wa ligi ya Uingereza kwa mwezi wa 10, mwaka 2012. Amekuwa wa 9.

Bastian Schweinsteiger (8)


Roho ya timu ya Bayern Munchen, akifunga magoli na kutoa pasi za mwisho za kutosha. Basti kama marafiki zake wanavyomwita ametengeneza chemistry katika timu ya Bayern hasa katika sehemu ya kiungo ya timu. Uwezo mkubwa wa kukota aliokuwa nao, pasi kali ‘zenye macho’ , uwezo mkubwa wa kukaba, uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, na mwisho wa yote ni uwezo wake mkubwa wa kupiga mipira iliyokufa unamfanya awe mchezaji wa kipekee. Schweinsteiger ana nafasi kubwa ya kuingia kwenye FIFA FIFPro World XI ya mwaka huu. Amekuwa wa 8.

Andres Iniesta (7)

Mchezaji bora wa Ulaya kwa mwaka 2012, siku zote amekuwa kwenye kiwango bora. Iniesta kwa sasa yupo kwenye kiwango cha juu cha soka katika maisha yake. Yeye ndio mtu anayeng’aa zaidi kwenye timu yenye vipaji lukuki ya Spain. Sababu ya Iniesta kushika namba 7 katika listi hii ni kutokana na makali kupungua kidogo tangu mashindano ya Ulaya kuisha pia ni kutokana na watu waliopo juu yake viwango vyao kuongezeka kwa kiasi kikubwa. Kitu ninachoamini ni kuwa lazima Iniesta atajwe kugombania FIFA Ballon d’Or katika wale watu watatu wa mwisho.

Stephan El Shaarawy (6)

Mashabiki wake humwita ‘The Pharaoh’ kwa sababu amezaliwa na wazazi wenye asili ya Misri pale Savona, Italia. Huyu ndio nguzo ya Milan kwa sasa katika upachikaji mabao baada ya Zlatan Ibrahimovic kuondoka. Akivaa jezi yenye namba ya mwaka aliozaliwa, # 92 (1992), na ikiwa ndio kwanza katimiza miaka 20 juzi tu mwezi October, Firauni huyu amekuwa tishio sana kwa mabeki wa timu pinzani zinazopambana aidha na Italia ama A.C Milan. Nimempa namba 6 kwa sababu anastahili.

Zlatan Ibrahimovic (5)

Mtaalamu huyu mwenye mkanda mweusi wa mchezo wa karate amekuwa mkubwa kuliko ligi ambayo anacheza ndani yake. Tangu kuhama kutoka AC Milan na kutua PSG mambo yamekuwa rahisi sana kwa Ibracadabra. Kutokana na aina yake ya mchezo na kipaji chake watoto wa mjini wanakwambia, Ibra sio wa leo wala kesho wakimaanisha, Zlatan ataendelea kung’aa kwenye medani nzima ya soka kwa kipindi kirefu kidogo mpaka pale atakapoamua kustaafu. Huyu ndiye mfungaji anayeongoza katika ligi kuu ya Ufaransa kwa sasa. Tarehe 14 mwezi huu wa 11, 2012, goli la 4 aliloifunga Uingereza linasemekana kuwa goli la karne. Zlatan Sefik Ibrahimovic ni namba 5.

Radamel Falcao (4)

Ukiwa ni msimu wake wa pili katika ligi kuu ya Spain, Radamel Falcao ameibuka ghafla na kuwa gumzo katika bara lote la Ulaya. Falcao ndio mpinzani mwenye nguvu wa Ronaldo na Messi ambaye alikuwa akinghojewa katika kugombania kiatu cha dhahabu cha ligi kuu ya Spain. Akiwa tayari ameshinda kombe La UEFA akiwa na Porto ya Ureno pamoja Athletico Madrid aliko sasa ambako pia majuzi alishinda UEFA Super Cup pale alipoichabanga Chelsea goli 3 peke yake katika ushindi wa 4-1, Falcao ameendelea kuwa mchezaji wa kutumainiwa katika kila timu anayoitumikia. Falcao anastahili nafasi ya 4.

Robin van Persie (3)

Huyu ndiye mchezaji bora wa ligi kuu ya Uingereza kwa msimu uliopita, 2011/12, huku akiwa hana muda mrefu tangu ajiunge na mashetani wekundu akitokea kwa mahasimu wao wakubwa, Arsenal, RvP amekuwa ndio nguzo katika mashambulizi ya United msimu huu akiwa ameifungia goli 8 tayari na pasi za magoli 3 kwenye ligi kuu, van Persie ameendelea kuwa moja ya nembo za ligi kuu ya Uingereza kwa wakati huu. Hivi karibuni wakati Sir Alex Ferguson alipochaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi October alimshukuru Robin kwa kutoa mchango mkubwa sana katika tuzo yake hiyo. Robin van Persie anakuwa wa 3 nyuma ya Ronaldo na Messi.

Cristiano Ronaldo (1)

CR7 kama anavyopenda kujiita. Yeye kaiteka dunia ndani ya uwanja na nje ya uwanja. Cristiano Ronaldo ni moja ya wachezaji adimu sana katika kizazi hiki cha leo. Uwezo wake wa kupasia ‘kamba’ umekua ukiongezeka siku baada ya siku. Ronaldo ndiye mchezaji anayetawala vichwa vya habari vya magazeti kila kukicha pamoja na ‘fundi’ mwingine kutoka Italia aitwaye Super Mario Balotelli. Mtupia mabao huyu ambaye ndio anaongoza magoli katika ligi ya mabingwa Ulaya msimu huu akiwa na goli 5 katika mechi 4 alizocheza amekuwa akisifika kwa bidii yake ya kujituma mazoezini na kwenye mechi. Kutokana na yote haya Cristiano pia anashikilia namba moja pamoja na Leo Messi. Ronaldo ndiye mchezaji bora wa mwaka huu, 2012 wa Goal.com, mtandao wa soka wenye heshima kubwa zaidi.

LIONEL Messi (1)

Ameendeelea kuiteka dunia kutokana na kipaji chake ambacho kinawashangaza wadau wengi wa soka. Huku akishikilia rekodi ya kufunga magoli mengi duniani katika msimu mmoja, magoli 73 katika msimu wa 2011/12 na magoli 76 mpaka sasa kwa mwaka huu akiwa nyuma ya Gerd Muller, urafiki wa Messi na nyavu umezidi kudumishwa siku baada ya siku ikumbukwe kwamba kila goli analofunga Messi kwa hivi sasa ni rekodi katika klabu ya Barcelona kwa sababu yeye ndiye mfungaji bora wa klabu kwa wakati huu. Kwa sasa mchezaji huyu bora wa dunia yuko katika kiwango sawa na mshindani wake wa karibu wa siku zote, Cristiano Ronaldo ndio maana wote wamekuwa vinara kwa kushikilia namba moja.Imeandaliwa na Stephen Samuel, napenda kutumia jina la PodoBest zaidi.


Twitter: @iPodoBest

MSIKILIZE RAGE ALIPOONGEA NA WAANDISHI - KUWAFUNGIA WANACHAMA WA TAWI LA MPIRA PESA

VIDEO KWA HISANI YA ITV

MFUPA ULIOMSHINDA DIEGO MARADONA - FILBERT BAYI HAUWEZI

Na Simon Chimbo

Akiaminika kuwa ni mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea katika ulimwengu
  wa soka, baada ya Pele, Diego Almando Maradona alishindwa kuisaidia Argentina pale alipopewa  dhamana ya kuifundisha timu yake ya taifa.
 

Sio yeye tu, wapo wengi lakini umewahi kujiuliza kuwa kwanini Pele sio kiongozi mkubwa wa soka duniani? Na pengine sijui kama Ronaldinho Gaucho anaweza?

Hapa nyumbani Tanzania, ukimzungumzia Filbert Bayi {Kiongozi wa
Tanzania Olympic Commision TOC} pengine ni kipaji 'adimu' zaidi kuwahikutokea kwa wanamichezo wote huku Sunday Manara akiwakilisha kwa soka.

Miaka ya 1970+  Bayi aliweka rekodi adimu katika michuano mbalimbali ya riadha ikiwemo jumuiya ya Madola, All Africa Games na mingine mingi. Je hiyo ni tiketi ya yeye kuwa kiongozi bora wa TOC? Jibu wanalo Waagentina walipo muamini  Diego Maradona na kuvuna matokeo hasi.


Ndio maana haikuhitaji Sir Alex  kuwa mchezaji bora wa dunia ili
awafikishe Manchester United mahali walipo.
Uongozi ni 'committment na Accountability' au kwa maneno mengine ni wito Watanzania wanao jua hawapo kwenye system na hilo lina tutafuna hadharani.
Ni wakati wa Bayi kuwaachia wengine waende Singida na Arusha
kuwachukua wanariadha Mungu ibariki Tanzania

JOSEPH OWINO NJIANI KURUDI NYUMBANI MSIMBAZI

Zoezi la klabu bingwa ya Tanzania bara Simba kupata mbadala wa beki wake aliyetimkia Yanga, Kelvin Yondani linaendelea, baada ya Lino Musombo kutemwa na kusajiliwa kwa Keita na Ocheing ambao wameonekana kuhangaika kuziba pengo la Yondani, sasa klabu hiyo ya Simba inasemekana wapo katika harakati za kumrudisha moja wa mabeki wao bora katika kipindi cha miaka 10 iliyopita mganda Joseph Owino.

Simba ambao walianza ligi vizuri na kuongoza ligi kwa muda mrefu kabla ya kupoteza muelekeo mwishoni mwa mwa raundi ya kwanza ya msimu wa VPL. Sasa katika kujaribu kuimarisha safu ya ulinzi ya timu hiyo ambayo imeonekana kuyumba sana msimu huu, uongozi wa Simba umeona bora ufanye mpango wa kumrudisha kundini Owino ambaye amesajiliwa Azam lakini amekuwa akikosa namba ya kudumu baada ya kurudi kutoka kwenye majeruhi yaliyomuweka nje kwa muda mrefu.

Taarifa ambazo hazijathibitishwa ni kwamba Simba tayari wapo kwenye mazungumzo na Azam ili kuweza kuona uwezekano wa kumsaini Owino.

Owino ambaye aliondoka Simba baada ya kupata majeraha ya goti ambayo yalimuweka nje kwa muda mrefu, na Azam wakamsajili akiwa mgonjwa wakamtibu lakini baada ya kupona amekuwa na urafiki mzuri na benchi la Chamazi.

                                                                 

Thursday, November 15, 2012

AZAM KUSAJILI WAKENYA WATATU - KUJIIMARISHA LIGI KUU RAUNDI YA PILI NA MICHUANO YA KIMATAIFA

Katika kujiimarisha kwa ajili ya michuano ya kimataifa na ligi kuu ya Tanzania raundi ya pili, klabu ya Azam FC imetajwa kuwa katika mazungumzo na wachezaji watatu kutoka Sofapaka ya Kenya.

Taarifa za kuaminika kutoka kwa chanzo kilicho karibu na Azam ambayo wiki iliyopita  waliwasimamisha wachezaji wao wanne, Dida Munishi, Said Morad, Aggrey Morris na Erasto Nyoni kwa tuhuma za kupokea rushwa, kimesema majina ya wachezaji watatu kutoka Sofapaka ni Eugene Ambuchi Asike, James Situma na Humphrey Mieno

Wachezaji hao watatu wa kikenya inasemekana ni kocha Stewart Hall ndio aliyetoa maombi ya kusajiliwa kwa wachezaji hao ambao alifanya nao kazi wakati akiwa kocha wa Sofapaka baada ya kutimuliwa Azam FC miezi kadhaa iliyopita.

GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE IMEREJEA TENA.

THE LEGEND IS BACK!

MATAIFA HURU YA AFRIKA: MAREFA KUFICHWA KUEPUSHA UPANGAJI WA MATOKEO

Marefa  wa fainali zijazo za kombe la mataifa huru ya Afrika watawekwa mbali na watu wengine wakati wa michuano hiyo nchini South Africa ili kuzuia upangaji wa matokeo.

Hali ya ulinzi ilitumika pia katika fainali ya za kombe la dunia mwakak 2010 zilizofanyika nchini SA.

CEO wa kamati ya ndani ya uandaaji Mvuso Mbebe alisema: "Marefa watakuwa mafichoni katika hotel mojawapo ambayo hakuna mtu atakuwa na uwezo wa kuwafikia.

"Hawatokuwa na uwezo wa kuwasiliana na mtu yoyote kutoka nje, kwa sababu hatuwezi kujua nini kinaweza kufanyika katika mawasiliano yao na watu wasioruhusiwa.

Aliongeza: "Watakuwa wanaondoka hotelini, chini ya ulinzi mkali utakaokuwa ukisindikizwa na vikosi maalum vya ulinzi, hali itaendelea mpaka mwisho wa michuano."

Shrikisho la soka la Afrika limepitisha hatua hiyo ya ulinzi wa marefa ambao utaanza kuanzia January 19 mpaka February 10

MANCHESTER UNITED YAPUNGUZA DENI WANALODAIWA

Klabu ya soka ya Manchester United imepunguza deni lake katika robo ya kwanza ya mwaka huu, baada ya familia ya Glazer inayomiliki timu hiyo, kulipa milioni 62.6.
Kwa jumla, deni lilipungua na kusalia pauni milioni 359.7, katika kipindi cha miezi mitatu kabla ya tarehe 30 mwezi Septemba, mwaka 2012.
Deni hilo limepungua kwa asilimia 17, ikilinganishwa na mwaka mmoja uliopita.
Mapato ya Manchester United yalipanda kwa asilimia 3.4, na kufikia faida ya pauni milioni 76.3, klabu hiyo ya Old Trafford imeelezea.
Lakini faida kutokana na utangazaji wa mechi zake ilipungua kwa asilimia 37.4, na kufikia pauni milioni 13.7, hasa kutokana na kubadilishwa kwa ratiba za mechi.
Klabu kilicheza mechi moja ya klabu bingwa, ilhali msimu uliopita ilicheza mechi mbili, na vile vile ilipungukiwa kwa mechi mbili zilizotangazwa moja kwa moja, ikilinganishwa na msimu wa awali.
Tofauti hizo zilisababisha hasara ya pauni milioni 5.6, ilhali klabu kina matumaini kitakuwa katika hali bora zaidi kwa kucheza mechi zaidi za klabu bingwa.
Manchester United ilipungukiwa kwa milioni 2.6, kwa kucheza mechi chache za klabu bingwa, hasa kwa kumaliza katika nafasi ya pili katika ligi kuu ya Premier, msimu 2011-12, ilikilinganishwa na msimu 2010-11.

EXCLUSIVE: MWAKALEBELA KUANZA HARAKATI ZA KUMNG'OA BAYI TOC LEO HII

Habari za uhakika kutoka kwa aliyekuwa katibu mkuu wa TFF katika awamu ya kwanza ya uongozi wa Leadgar Tenga, Bwana Frederick Mwakalebela ni kwamba kesho asubuhi ataenda kuchukua fomu za kugombea uongozi wa ukatibu mkuu wa kamati ya Olimpiki Tanzania.

Mwakalebela ambaye ni mmoja ya wadau wenye kuonyesha nia ya dhati katika kukuza michezo kwa kutoa misaada mbalimbali pamoja na kuandaa michuano kama 'Mwakalebela CUP' ambayo imekuwa ikitoa vipaji vingi amesema ameamua kuchukua fomu ya kugombea ukatibu mkuu kwa sababu anaamini ana uwezo na nia ya dhati ya kuongoza kamati hiyo ili kuiwezesha nchi yetu ipige hatua zaidi katika michezo.

Kuchukua fomu kwa Mwakalebela kunamaanisha katibu mkuu huyo wa zamani wa TFF, ameanza mbio za kumng'oa madarakani kidemokrasia Fibert Bayi ambaye amekuwa kiongozi wa kamati hiyo kwa muda mrefu sasa.

Leo ndio siku ya mwisho ya kuchukua fomu.

Wednesday, November 14, 2012

EPISODE 2: SALVADOR CABANAS MWANASOKA ANAYEISHI NA RISASI KICHWANI
Nchi mojawapo ambayo iliweza kupambana na vita dhidi ya madawa na vurugu zake ni Colombia. Kwenye miaka 1980 na 90, nchi hiyo ilikuwa ndio sehemu inayopendwa zaidi na wauza madawa ya kulevya ambao waliyachukua maisha ya mcheza soka Andres Escobar, miongoni mwa wahanga wa wauza madawa hao.

Escobar, akiwa na miaka 27 wakati alipouliwa, alijifunga goli katika michuano ya kombe la dunia 1994 dhidi ya USA, na Colombia wakapoteza mechi na kutolewa kwenye hatua ya makundi.

Wauza madawa, inaaminika waliweka fedha nyingi kwenye kamari kwa ajili ya timu ya taifa ya Colombia kufanya vizuri, hivyo walihakikisha Escobar analipa kwa kuwapotezea fedha zao na wakamuua. Mazishi ya Escobar yaliudhuriwa na watu wapatao 120,000.


Kwa upande wa Cabanas akiwa anapigania maisha yake kwenye Hospitali ya Angeles Predregal, alipata sapoti kubwa, watu takribani 5,000 walikusanyika kwenye uwanja wa timu ya taifa na kufanya sala la kumuombea kipenzi chao, hali hiyo pia ilitokea Mexico kwenye uwanja wa Azteca.

"Najisikia faraja sana kwa mapenzi makubwa ninayopewa na watu kila ninapoenda hapa nchini Paraguay," anasema Cabanas. "Mapenzi yananisukuma sana na pia ujumbe mbalimbali ninaopokea kutoka kwa wacheza soka mbalimbali duniani, hasa kutoka kwa wachezaji ndio walionisaidia kwa kiasi kikubwa pamoja na maombi ya mashabiki."Cabanas na Raisi wa Paraguay Fernando Lugo

Mwezi mmoja baada ya kuanza kupata nafuu alitembelewa na raisi wa Paraguay Fernando Lugo. Kabla ya kushambuliwa Cabanas  alifunga mabao 10 katika mechi 44 za Paraguay. Mjini Auancion, watu wanaamini timu ya taifa isingefungwa na Spain  kwenye robo fainali ya kombe la dunia 2010 kama angecheza. Oscar Cordozo alikosa penati amabyo kama Cabanas angeipiga angefunga, mashabiki wanasisitiza. Lakini Cabanas anakataa kukubalina na hisia hizo za mashabiki na kusema kilichotokea kilipangwa kutokea, huku akisisitiza nia yake ni kurudi kuichezea timu yake ya taifa: "Wakati tu ndio nimetoka hosptali nikawa nipo nyumbani naangalia timu yangu ta Taifa ikicheza kwenye kombe la dunia. Nilikuwa naomba itendeke miujiza nipone haraka niende kuiwakilisha nchi yangu. Sikufanikiwa wakati ule lakini sasa nashukuru mungu nimepata nafuu kabisa, ninachokitaka na kuwa fiti na kuitumikia timu yangu ya taifa. Naamini siku si nyingi wakati wangu utafikia ninachopaswa kufanya ni kuonyesha uwezo wangu tu kwa kocha."

Akiwa amezaliwa kwenye familia ya kimaskini katika eneo la Itaugua, akiwa mvulana alikuwa akiuza 'Chipa' mkate wa kiparaguay: "Ilibidi kufanya kazi bado nikiwa mdogo ili kuweza kula kila siku," - anakumbuka.
Mtu ambaye aligundua kipaji chake, kocha wa Kiargentina Mariano  Falcon, alijua Cabanas ana kipaji cha aina yake na hivyo akamchukua kinda lenye miaka 10 wakati huo na kulipeleka kwenye klabu ya de Octubre, ambapo alifunga mabao 31 katika mechi 14 wakati wa msimu wake wa kwanza na timu ya vijana ya klabu hiyo.

Magoli hayo aliyafunga ndani ya 18 na mengine mashuti ya mbali, huku akitumia miguu yote miwili. Akiwa na miaka 15, Cabanas akaanza kuichezea timu ya wakubwa, na akaisadia timu yake hiyo kufika kwenye ligi kuu ya Paraguay kwa mara ya kwanza mwaka 1997. Kwa pesa waliyopokea Octubre kwa mauzo ya Cabanas kwenda klabu ya Chile Audax Italiano 12 de Octubre walifanikiwa kujenga jukwaa kwenye uwanja wao wa Juan Pettengill.

Na alipoenda Amerika, Cabanas akijiweka kuwa moja ya namba 10 bora kabisa huko Latin Amerika na alikuwa mfungaji bora mara mbili - 2007 na 2008 katika Copa Libertadores ambalo ni kombe la mabingwa wa Amerika ya kusini.

Baada ua kupigwa risasi, madaktari walimwambia Cabanas  kwamba hatocheza kabisa soka: "Walisema itakuwa haiwezekani mie kucheza soka. Niliwaambia kwamba hawapo sahihi. Niliongea na mke wangu na wazazi wangu na nikasema nitarudi tena uwanjani. Sikuwahi kuwa na mashaka juu hilo."

Kwa sasa anasumbuliwa na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu ikiwa na kutokana na majeruhi ya ndani aliyoyapata. "Kitu cha kwanza nilichokumbuka baada ya kuzinduka alikuwa ni bibi yangu akiongea na mie. Alifariki mwaka mmoja kabla. Aliniambia itabidi nicheze tena mpira kwa sababu watu wengi bado walikuwa wananitegemea mimi.

"Hilo lilinipa nguvu kubwa sana. Nilipokuwa mdogo nilikuwa nalala nyumbanikwake kwa sababu alikuwa anakaa peke yake  na siku zote alipenda kuwa karibu na mimi. Pia kuwaona watoto wangu wawili kulinipa nguvu sana."

Cabanas anaongea huku akiwa na matumaini na nia ya kweli ya kurudi kuichezea timu ya taifa, lakini kocha wa 12 de Octubre, mdogo wake golikipa wa zamani wa Paragauay Chilavert, aitwaye Jose Luis, anasisitiza hawezi tena kuwa mchezaji yule yule aliyekuwa mwanzo. "Ukweli ni kwamba sababu za kibinadamu, na sio za kisoka. Tunataka kumsaidia aweze kuwa na kiwango kizuri, lakini haiwezekani. Huyu sio Salvador  yule wa zamani."

Changamoto kubwa aliyonayo Cabanas kwa sasa ni kuweza kupona kabisa ugonjwa wake wa kupooza upande wa kushoto. "Alipoanza kufanya mazoezi na sisi hakuweza kabisa kurusha mguu wala mkono wake wa kushoto vizuri, lakini ameendelea kuwa na maendeleo mazuri sana yanatia moyo," Chilavert anasema.

"Upande wa kushoto wa mwili wangu bado mdhaifu, bado ninahitaji mazoezi sana lakini nitapona kwa baraka za mungu. Nataka kupona kabisa niwe na uwezo wa kupiga mashuti kama nilivyokua mwanzoni." - Anaongea Cabanas 

Japokuwa kuna tatizo kubwa ambalo linaweza kuwa kikwazo kikubwa kwa Cabanas kurudi kama alivyokuwa mwanzoni, Risasi aliyonayo kichwani. "Inabidi niwe muangalifu sana wakati ninapopiga kichwa mpira ambao unasafiri kwa haraka. Inabidi nifanye niwezavyo kutuliza mpira ule na paji langu la uso kwa sababu ikiwa tofauti unaweza ukasababisha risasi iliyomo kwenye ubongo kuhama na kusababisha matatizo mengine."

Katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Club Martin Ledesma, Chilavert na makocha wenzake walipata wasiwasi mkubwa pale Cabanas alipongongana na mchezaji wa timu pinzani, lakini kwa bahati nzuri hakuguswa kichwani akasalamika na kuendelea mchezo.

Kwa sasa, Cabanas anacheza mechi za nyumbani tu tena kwa dakika 45. "Akili yake ya kucheza soka itakuwepo pale siku zote,"  anasema kocha Chilavert.
"Anacheza vizuri sana kuunganisha safu ya kiungo na ushambuliaji, lakini anacheza taratibu kidogo."
Hata hivyo kwa sasa hivi kocha Chilavert ameacha kazi yake kwenye klabu akitoa sababu kwamba mabosi wa klabu yake wanamlazimisha amuweke Cabanas kwenye timu. Wachezaji wenzie pia wamekuwa na la kusema kwamba ule uwezo wa zamani wa Cabanas bado sana kurudi. Lakini baada ya kuweza kurudi uwanjani tu, Cabanas anaamini atatisha tena kama ilivyokuwa mwanzoni. "Hakuna aliyepona kutokana na jeraha nililolipata mie. Ilikuwa miujiza ya mungu. Na mungu huyo huyo ataniwezesha muda mfupi ujao niweze kucheza dakika zote 90, na muda wowote kutoka sasa nitaanza kufunga mabao."
Akiwa amesimama kwenye mlingoti wa goli kwenye mazoezi jua linampiga kichwani tena mahala pale kwenye kovu la risasi aliyopigwa - alama ya milele atakayokaa nayo ambayo itamkumbusha tukio la usiku ule kwenye ile bar jijini Mexico. Lakini pamoja na hayo yote Cabanas hamtakii mabaya aliyempiga risasi.

Balderas, anayejulikana kama 'JJ', alienda kujificha  kwa miezi mitatu baada ya kumtundka risasi ya kichwa Cabanas. Bosi wake muuza madawa ya kulevya La Barbie alikiri kwamba alimficha Balderas kwenye  kwenye ofisi zake zilizopo karibu na mji mkuu wa Mexico, mpaka pale alipokuja kukamatwa.

Mwaka jana mwezi wa 9, Balderas alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kutumiwa dokumenti za uongo, lakini  bado anakabiliwa na mashtaka ya uingizaji silaha za magendo na jaribio la kumuua Cabanas.

"Nimemsamehe Balderas," anasema Cabanas. "Ataitumikia adhabu yake kwa kile alichofanya. Kama ambavyo mungu amenisadia mimi kuwa hapa sasa hivi, yeye ndio atamhukumu Balderas. Chochote kitakachotokea namuombea kwa mungu familia yake iwe vizuri."

Cabanas bado ana mkataba  na Club American na ana matumaini ya mbali kuweza kurudi nchini Mexico, lakini timu ilikataa kumlipa kwa miezi nane baada ya kupigwa risasi, ambo ambalo lilipelekea mkewe Maria Lorgia Alonso afungue kesi dhidi ya klabu.

Alonso anasema kwamba familia yake ilikuwa kwenye hali mbaya ya kiuchumi na hatimaye wakafikia makubaliano kwamba na American mwaka jana, ambayo yalihusisha mechi kati ya timu ya taifa ya Paraguay nchini Mexico kwa ajili ya kukusanya fedha za kumsaidia Cabanas na familia yake.

"Nilichokihitaji kutoka kwao ni ukamilishaji wa haki zangu zote zilizo kwenye mkataba ambazo ni kunilipa," anasema Cabanas. Sasa yameisha sina hasira tena juu yao."

Leo hii akiwa na afya njema japo sio sana, ameweka akili yake katika kuisadia klabu yake ya 12 de Octubre kufanikisha malengo yake  ya kupata mafanikio. "Unajua nilipoanza matibabu yangu nilikuwa naweza kusimama kwa kutumia magongo tu. Hivyo kuamka na kuweza kusimama na kucheza uwanjani kumenifurahisha sana. Nitafanya kila niwezalo niweze kuisadia klabu yangu kupanda daraja na kurudi kwenye daraja la kwanza."

Cabanas ambaye bado anakunywa dozi ya kutwa mara 3, alipewa ruhusa mwezi January kurudi dimbani na kwa haraka akawasiliana na Raisi wa klabu  ya De Octubre Luis Salinas kuandaa kurudi kwake klabu hiyo katikaUwanja wa Juan Pettengill, ambao una jukwaa moja la kuingiza mashabiki 500, mbali kabisa na ule wa Azteca nchini Mexico ambao unaingiza mashabiki 104,000 - uwanja pekee duniani kuchezwa fainali mbili za kombe la dunia.

"Ni tofauti  sana hapa," anasema. "akini hapa ni nyumbani kwetu kabisa. Ni mahala pazuri kwangu kwa sababu ndipo nilipojifunza mpira na kukuzwa kama mchezaji. Ninatoa shukrani kubwa sana kwa klabu kunipa hii nafasi. Siku zote nimekuwa kuwa mcheza soka na nina furaha sana kuanza kucheza tena ."BY AIDAN SEIF CHARLIE

SD TV: MGAMBO VS AZAM

KALI YA LEO: FIFA YAMTISHIA KUMPA ADHABU ZAIDI KOCHA WALIYEMFUNGIA MAISHA.

Kocha wa zamani wa Zimbabwe Sunday Chidzambwa, ambaye sasa anatafuta namna ya kusafisha jina lake katika kesi ya upangaji matokeo, ameonywa na FIFA anaweza akakutana na adhabu kali zaidi ikiwa ataendelea na harakati zake za kupeleka kesi mahakamani kama alivyofanya wiki iliyopita.

Chidzambwa alifungiwa maisha na Chama cha soka cha Zimbabwe kwa kuhusika kwake na kupanga matokeo ya timu yao ya taifa kupoteza mechi kwa kudhamiria huko barani Asia katika kipindi cha kati 2007 na 2009 kwa malipo ya pesa kutoka kwa wacheza kamari wa huko Asia.

Kocha huyo wa zamani alituhumiwa kuwa ndio aliyepanga mchongo mzima kwa pamoja na Method Mwanjali wa Mamelodi Sundowns na mlinzi BidVest Wits Thomas Sweswe, ambao nao wamefungiwa maisha.

Lakini swali la kujiuliza ikiwa Chidzambwa tayari anatumikia adhabu ya kufungiwa maisha na FIFA, je shirikisho hilo la soka ulimwenguni ambalo mamlaka yake yanaishai kwenye soka tu, litampa adhabu gani nyingine kubwa kuzidi hiyo?

NASSIBU RAMADHANI NA FRANSIC MIYAYUSHO KUGOMBANIA UBINGWA WA WBF DESEMBA 9


Mabondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyayusho wakitunishiana misuri wakati wa kutambulisha mpambano wao wa ubingwa wa WBF utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mwandaji wa mpambano wa ubingwa wa WBF Mohamed Bawazir katikati akiwa ameshika mkanda na mabondia Nassibu Ramadhani kushoto na Fransic Miyayusho kulia wengine kulia ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa ambao na wasimamizi wa mpambano huo na Kushoto ni Mratibu Paul Kunanga na Kocha wa Nasibu Christopher Mzazi

Mabondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyayusho wakitunishiana misuri wakati wa kutambulisha mpambano wao wa ubingwa wa WBF utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mabondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyayusho wakitunishiana misuri wakati wa kutambulisha mpambano wao wa ubingwa wa WBF utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


KAMPUNI YA Darworld Links imeandaa mpambano mwingine wa ubingwa wa masumbwi utakaowakutanisha bondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyayusho mpambano utakaofanyika katika Ukumbi wa PTA Sabasaba akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Mohamed Bawazir


Amesema amewakutanisha mabondia hawo kutaka kujua nani zaidi ya mwenzake kwa kuwa viwango vyao vina fanana na vinatambulika kimataifa hivyo amewataka watanzania kujitokeza kuwapa sapoti hususani kudhamini mchezo huo wa masumbwi ata kwa bondia mmoja mmoja kuwagea changamoto mbalimbali mabondia hawa vijana wana uwezo mkubwa wa kutangaza biashara mbalimbali kupitia mchezo wao wa masumbwi kwani makampuni mengi yamekuwa yakiupiga danadana mchezo huu ni mchezo kama michezo mingine nashangaa sana kuona tunakosa


Udhamini tunapoomba sehemu ya makampuni mbalimbali ukienda wanasema hatuhusiki na mchezo huo.

Wengine wanasema kabisa wadhamini wa michezo wakati wanabagua michezo mingine kama ngumi awapewi kipaumbele kabisaa
amewaomba wapenzi na mashabiki kujitokeza siku tarehe 9 Desemba kuja kuangalia ngumi ili zisonge mbele watakaosindikiza mpambano huo wa masumbwi ni 
Fadhili Majia VS Juma Fundi

Moh'd Rashid Matumla VS Doi Miyayusho

Ibrahimu Class 'King Class Mawe' VS Said Mundi wa Tanga

Fred Sayuni VS Deo Samweli

Hassani Kidebe VS Baina Mazola


Mapambano yote ya utangulizi ni mazuri na vijana wanaotakiwa kuendelezwa katika elimu ya masumbwi Duniani ili wawe mabondia wazuri 


Mpambano huo umedhaminiwa na JB BELMONT HOTEL gazeti la Jmbo Leo, Times FM


Na wengine wameobwa kujitokeza katika udhamini huo kwa mawasiliano zaidi 

0716 332933

0784 426542

BARUA YA WAZI KUTOKA KWA WADAU WA SOKA KWENDA TENGA KWA UKIUKWAJI WA KATIBA YA TFF

-->

Bwana Leodger Chilla Tenga
Rais wa TFF

Ndugu Tenga,

YAH: UKIUKWAJI WA KATIBA YA TFF

Sisi wadau wa mpira wa miguu Tanzania tunakuandikia barua hii tukiwa na uchungu mkubwa kuhusu mwenendo wa uongozi wako.  Ulipoingia madarakani kwa mara ya kwanza Golden Tulip tarehe 27 Desemba 2004 ulitoa matumaini makubwa kuhusu kuleta mabadiliko makubwa katika uendeshaji wa mpira wetu.  Pamoja na mapungufu mengi yaliyojitokeza ndani ya miaka minane ya uongozi wako haya mawili tutakayoyaeleza hapa chini hayawezi kufumbiwa macho na wanaoutakia mema mpira wa Tanzania.

1.     Kupitisha muda wa uongozi wako bila kibali cha mkutano mkuu.
Mkutano mkuu uliokuingiza madarakani ulifanyika siku ya Jumapili tarehe 14 Desemba 2008.  Kifungu 33(1) cha Katiba ya TFF kinatamka kuwa kipindi cha uongozi ni miaka minne tu.  Hivyo ukomo wa uongozi wako na kamati yako ya utendaji ni saa sita za usiku tarehe 13 Desemba 2012.  Aidha kifungu cha 10(1) cha kanuni za uchaguzi wa TFF kinatamka kuwa tangazo la uchaguzi litatolewa siku 40 kabla ya uchaguzi.  Kwa mantiki hii kamati yako ya uchaguzi ilitakiwa itangaze tarehe ya uchaguzi siku ya Jumatatu tarehe 05 Novemba 2012 au kabla ya hapo.   Leo ni tarehe 13 Novemba 2012 na ofisi yako iko kimya!  Hii haikubaliki, haiwezekani ujiongezee muda wa uongozi bila kibali cha Mkutano Mkuu.  Tutawaomba wajumbe wa Mkutano Mkuu wakuadhibu kwa kosa hili la ukiukwaji wa Katiba.  Pamoja na mapungufu haya ni vyema ukatufahamisha uchaguzi umepanga ufanyike lini au unasubiri wajumbe wa mkutano mkuu wakulazimishe kwa maandishi?

2.     Kufuta nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais wa TFF
Yapo maneno yanasemwa eti uongozi wako unataka kufuta nafasi ya pili ya Makamu wa Rais wa TFF kinyemela.  Kama tuhuma hizi ni za kweli tunaoma tukukumbushe yafuatayo:
2.1.1      Nafasi ya makamu wa pili wa Rais wa TFF iko ndani ya Katiba ya TFF kifungu 31(1)
2.1.2      Kifungu cha katiba 30(1) kinatamka wazi kuwa ni mkutano mkuu pekee wenye mamlaka ya kubadili Katiba ya TFF.  Hivyo hakuna njia mbadala ya kubadili Katiba ya TFF.
2.1.3      Kifungu cha Katiba 30(2) kinatamka kuwa tangazo lolote la nia ya kubadili Katiba ya TFF litatolewa siku 45 kabla ya mkutano mkuu.  Uongozi wako utawezaje kutoa tangazo hili ndani ya kipindi cha uongozi wako kilichobakia?
2.1.4      Kifungu cha Katiba 30(6) kinatamka kuwa ombi la kubadili katiba litapigiwa kura NDANI YA MKUTANO MKUU na ili lipite theluthi mbili ya wajumbe sharti iridhie.  Zingatia utashi huu wa Katiba.

Bwana Tenga kama kweli wazo hili lipo basi achana nalo, usijidhalilishe kwa kukiuka Katiba iliyokuweka madarakani.  Nafasi za uongozi katika uchaguzi ujao zitangazwe kwa mujibu wa Katiba iliyokuweka madarakani.  Kama kuna umuhimu wa kubadili Katia hakuna uharaka wowote, subiri awamu ijayo ifanyie kazi wazo hilo, awamu ambayo huenda wewe mwenyewe ukaingoza pia kama ukigombea tena.

Tunasubiri majibu ya hoja zetu za majibu haya tunaomba uwajulishe watanzania wote.

Nakala ya barua hii tunawapelekea wajumbe wote wa Mkutano Mkuu kwa taarifa.

Ni sisi kwa niaba ya wadau wa mpira wa Tanzania.

MILOVAN CIRKOVIC: NIONDOKE AMA NISIONDOKE ?


after 2 losses,stay or not?
after 2 losses,stay or not?
Kocha wa klabu ya SIMBA raia wa Serbia,Milovan Cirkovic amewauliza mashabiki wa MNYAMA kwenye mtandao wa kijamii wa facebook kwamba baada ya timu yake kupoteza michezo miwili ya ligi kuu ya Vodacom,wanaamuaje AOONDOKE ama ABAKI ?
kazi kwenu wadau kupiga kura za kutosha hapa!

STARS WAJIFUA KIRUMBA TAYARI KUIVAA HARAMBEE STARSTuesday, November 13, 2012

GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE YARUDI TENA

Washiriki wa mwaka huu
GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™
SEASON 2
KEY MESSAGES – EA
CORE
·         The GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™, the TV game show phenomenon which has excited audiences across Africa for the last two years, is back for an incredible 2nd Season, and this time around, it’s going to be Pan-African!
·         Guinness® is calling upon football fans to play for their country in the new Pan-African show, as contestants from Kenya, Tanzania, Uganda, Cameroun and Ghana go head-to-head
·         Successful teams could win up to 900,000 USD in Season 2, as contestants represent their nation to find out who is Made of More and has the skill and knowledge to go all the way and be crowned Pan-African champions
·         In the new Season even more people can get involved in the GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ in a number of different ways.  Alongside the exciting new TV show there will be the return of the GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ mobile phone game so that fans can test their football trivia on their mobile phone; and live GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ quizzes in bars
AUDITION EVENTS
·         Guinness® is searching for football lovers who have what it takes to represent Tanzania on a Pan-African stage, and show that they can achieve their potential and be recognised as players, rather than spectators in life
·         Players can try out for a chance to appear in the show at the GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ audition events.  Three events to search for the stars of Season 2 of the GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ will be held in:
-          At Leaders Club, Dar es Salaam on 24th November
·         Teams of two football fans who think they have the brains and the brawn to step up and represent Tanzania in the GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ should come along and try out for the show.  One of you will need to demonstrate great skill with a ball at your feet, and your partner should know everything there is to know about the beautiful game. You will be put through your paces in a series of challenges to see if you could represent your nation and be in with a chance of winning up to 900,000 USD.
·         The GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ audition events will be a fun day out for everyone, with football activities, music and entertainment. Entry is free but will be restricted to only those 18+.
TV SHOW / BROADCAST
National Series
To be broadcast on ITV & Clouds TV. Details to be shared in a while.