Search This Blog

Thursday, November 15, 2012

EXCLUSIVE: MWAKALEBELA KUANZA HARAKATI ZA KUMNG'OA BAYI TOC LEO HII

Habari za uhakika kutoka kwa aliyekuwa katibu mkuu wa TFF katika awamu ya kwanza ya uongozi wa Leadgar Tenga, Bwana Frederick Mwakalebela ni kwamba kesho asubuhi ataenda kuchukua fomu za kugombea uongozi wa ukatibu mkuu wa kamati ya Olimpiki Tanzania.

Mwakalebela ambaye ni mmoja ya wadau wenye kuonyesha nia ya dhati katika kukuza michezo kwa kutoa misaada mbalimbali pamoja na kuandaa michuano kama 'Mwakalebela CUP' ambayo imekuwa ikitoa vipaji vingi amesema ameamua kuchukua fomu ya kugombea ukatibu mkuu kwa sababu anaamini ana uwezo na nia ya dhati ya kuongoza kamati hiyo ili kuiwezesha nchi yetu ipige hatua zaidi katika michezo.

Kuchukua fomu kwa Mwakalebela kunamaanisha katibu mkuu huyo wa zamani wa TFF, ameanza mbio za kumng'oa madarakani kidemokrasia Fibert Bayi ambaye amekuwa kiongozi wa kamati hiyo kwa muda mrefu sasa.

Leo ndio siku ya mwisho ya kuchukua fomu.

1 comment:

  1. kaka kila la kheri mpiganaji wetu naamini mbuyu wa TOC ukidondoshwa tutegemee mwanzo mzuri

    Hapa nachokoza tu kaka--Vip kwenye chama chetu utasitisha harakati,,,nimesikia bado wanakupenda and na wewe bado unalitaka jimbo au utapiga kote ote,,,

    ReplyDelete