Search This Blog

Saturday, November 12, 2011

UHAI CUPMichuano ya vijana wa umri chini ya miaka ishirini kwa vilabu vya ligi ya Premier ya Tanzania bara Uhai Cup imefunguliwa rasmi hivi leo kwa michezo iliyopigwa kwenye viwanja vya Mbande huko Chamazi na Karume jijini Dar es salaam.

Jumla ya mechi sita zimepigwa hivi leo kwenye ufunguzi wa michuano hiyo, ambapo zimepigwa mechi tatu kwa kila uwanja, kuanzia saa tatu za asubuhi hadi saa kumi na mbili za jioni.

Asubuhi saa tatu ulipigwa mchezo baina ya Azam FC dhidi ya Kagera Sugar kwenye uwanja wa Mbande, na muda huo huo kwenye uwanja wa Karume ukapigwa mchezo baia ya Ruvu shooting starz, mabingwa watetezi dhidi ya JKT Oljoro ya jijini Arusha.

Baadae saa nane mchana wakati Dar es salaam Young Africans wakikabiliana na Moro United kwenye uwanja wa Mbande, katika uwanja wa Karume ukawa ukipigwa mchezo baina ya Ruvu starz dhidi ya Polisi Dodoma.

Mwisho saa kumi alaasiri, wakati Simba wakimaliza udhia na wagosi wa Ndima Coastal Union toka jijini Tanga kwenye uwanja wa Mbande, Toto Africans ya jijini Mwanza wakawa wanapapatuana na waalikiwa wa michuano hiyo, Serengeti Boyz.

Tukianzia na mchezo wa kwanza kule Mbande hapo asubuhi, Azam dhidi ya Kagera ni kuwa dakika tisini zilimalizika kwa Azam FC kuilaza Kagera Sukari mabao mawili kwa moja.

Baadae saa nane mchana kwenye uwanja huo huo Young Africans, walikiona cha mtemakuni mbele ya vijana wa Moro United, baada ya kuzabwa mabao matatu kwa moja, wakionekana kushindwa kabisa kustahmili vishindo vya vijana wa Moro United.

Na hapo saa kumi za jioni kibarua kwenye uwanja huo kwa siku ya leo kikakamilishwa kwa mchezo baina ya Simba dhidi ya Coastal Union na pambano likimalizika kwa Simba kuisasambua Coastal Union mabao matatu kwa sifuri.

Mabao ya Simba kwenye mchezo huo yakiwekwa kimiani kwa ustadi mkubwa na washambuliaji Edo Christopher, Miraji Madenge na Rashid, huku vijana hao wa msimbazi wakipiga soka ya uhakika kabisa.

Vijana wa Moro United wanaonekana kuwa wamejipanga sana na wakiwa na timu ambayo inaonekana kuzoeana kabisa, kama ilivyo kwa wekundu wa msimbazi Simba sports club, ambao inavutia kuwatazama kutokana na kucheza soka la pasi nyingi za uhakika na kuvutia.

Bado yaonekana kana kwamba litakalowakuta Young Africans litakuwa kama lile la msimu uliopita, kutokana na kutokuwa na timu inayocheza kama timu zaidi ya vipaji binafsi, tofauti na timu kama za Moro, Azam, na Simba.

Kati mwa mji kwenye uwanja wa Karume, asubuhi Ruvu shooting dhidi ya Oljoro pambano hilo lilimalizika kwa mabingwa watetezi wa taji hilo Ruvu shooting starz kulambwa mabao mawili kwa moja.

Na saa nane za mchana JKT Ruvu starz dhidi ya Polisi Dodoma..

Mwisho saa kumi za jioni Toto Africans dhidi ya Serengeti Boyz wakaumiza nyasi za uwanja wa Karume jijini kwa kwenda sare ya kufungana mabao mawili kwa mawili, ambapo Serengeti Boyz walilazimika kutoka nyuma na kusawazisha mabao yote mawili.

Kesho ni mapumziko katika michuano hiyo, na jumla ya michez9o mingine sita itapigwa hapo siku ya jumatatu, kwenye viwanja vya Mbande huko Chamazi na uwanja wa Karume kati mwa jiji.

LEO NI MAADHIMISHO YA MIAKA 17 YA KIFO CHA METHOD MOGELLA ' FUNDI'

METHOD MOGELLA ( KUSHOTO ) AKITAMBULISHWA KWA MH JOHN SAMWEL MALECELA NA ZAMOYONI MOGELLA

TAREHE 12/11/1994 MISHALE YA SAA SABA MCHANA MAENEO YA BUGURUNI JAY AMBE NYUMA YA ROZANA ALIYEKUA KIUNGO WA SIMBA NA TIMU YA TAIFA METHOD MOGELLA ' FUNDI ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUUGUA KWA MAJUMA MAWILI. HII ILIKUA NI SIKU YA MAAJABU KWA DADA YAKE MKUBWA ANGELINA MOGELLA WAKATI TAARIFA ZA MSIBA WA MDOGO WAKE ZINAMFIKIA GHAFLA ALIJISIKIA UCHUNGU WA MAMA MZAZI KWASABABU ALIKUA NA UJAUZITO, WAKATI FAMILIA YA MOGELLA IKIWA KWENYE HARAKATI ZA MSIBA, DADA ANGELINA ALIKIMBIZWA KWENYE HOSPITALI YA TMJ NA MNAMO SAA NNE USIKU ALIJIFUNGUA MTOTO WA WAKE WA TATU WA KIUME, MTOTO YULE ALIPEWA JINA LA METHOD ANICETH, ANICETH METHOD AMBAYE KWA SASA NI MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA AZANIA LEO ANATIMIZA MIAKA 17 YA KUZALIWA.
KWAHIYO LEO NI SIKU AMBAYO METHOD MOGELLA ALIFARIKI DUNIA NA BAADA YA MASAA 9 AKAZALIWA UPYA...
METHOD ANICETH ANACHEZA SOKA NA AINA YAKE YA UCHEZAJI NI KAMA MAREHEMU MJOMBA WAKE....

KALI YA LEO: MWENYEKITI WA MAN CITY AFUNGA HAT TRICK KATIKA MECHI YA HISANI

TFF YAWAPA ONYO LA MWISHO RAGE NA SENDEU


Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imetoa onyo la mwisho kwa Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage na Ofisa Habari wa Yanga Louis Sendeu kutokana na kutohudhuria vikao viwili mfululizo kama walivyotakiwa na kamati hiyo.

Rage na Sendeu wanatakiwa kujieleza mbele ya kamati hiyo iliyo chini ya Kamishna mstaafu wa Polisi, (CP), Alfred Tibaigana, kutokana na tuhuma za utovu wa nidhamu baada ya kudaiwa kutoa kauli zenye lengo la kushusha maendeleo ya soka hapa nchini, wakati wa kuelekea mechi ya Ngao ya Hisani, kati ya Simba na Yanga.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, kamati hiyo inatarajiwa kukaa hivi karibuni ambapo imeagiza Rage ataarifiwe kuwa anayepanga vikao vya kamati hiyo sio yeye, hivyo endapo hatatokea siku atakayoitwa, atajadiliwa na mamuzi kutolewa.

Alisema Rage amekosa mara mbili kuhudhuria kikao cha kamati hiyo, hivyo kitakapoitishwa itakuwa ni mara ya tatu, hivyo kutakuwa hakuna samahani.

Septemba 24, mwaka huu, Sendeu alihojiwa na kamati hiyo kutokana na tuhuma nyingine za kutoa matamshi yenye kuhatarisha maisha ya mwamuzi Alex Mahagi, na kuhukumiwa kulipa faini ya sh 500,000.

SAMATTA AGOMA KULA CHAD


Katika hali ya kushangaza, mshambuliaji tegemeo wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na TP Mazembe ya Congo, Mbwana Samatta hajakula chakula chochote cha asubuhi tangu timu hiyo ilipowasili Jumatano usiku.

Samatta hakuonekana katika ukumbi wa chakula wa Hoteli ya Santana ambayo Stars wamefikia jijini N’djamena na wakati wote wa asubuhi huku akilalamika kuwa mazoea ya maisha ya DR Congo yanamuathiri kwa kiasi kikubwa.

“Siwezi kula ndugu yangu. Kule DRC kumenizoesha vibaya. Huwa tunafanya mazoezi kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa sita.

"Tukirudi tunasubiri kidogo tunakwenda kula chakula cha mchana. Huwa hatuli chakula cha asubuhi, muulize Thomas (Ulimwengu),” alisema Samatta.

Alipouliuzwa kuhusu suala hilo , Ulimwengu ambaye pia anaichezea TP Mazembe alikiri kwamba na yeye ameanza kuathirika na hali hiyo ingawa tofauti na Samatta yeye alikuwa anapiga msosi kama kawaida.

“Hata mimi nimeanza tabia hiyo. Sijisikii kula asubuhi kwa sababu ratiba ya Congo ni tofauti kabisa na ya Tanzania au huku” aliongeza Ulimwengu ambaye anakaa chumba kimoja na Samatta.

Katika pambano la jana, kocha wa Stars Jan Poulsen alitarajiwa kumuanzisha Samatta na kumuweka benchi Ulimwengu katika mfumo wa 4-5-1 ambao unamuweka mshambuliaji mmoja tu katika eneo la mbele.

EDO KUMWEMBE, N’DJAMENA

Friday, November 11, 2011

LIVE MATCH CENTRE: CHAD 1-2 TANZANIA FULL TIME.

MPIRA NI MAPUMZIKO SASA, TAIFA STARS 1-1 CHAD.

MRISHO NGASSA NDI AMEFUNGA GOLI LA STARS.

SECOND HALF: MPIRA UMEANZA TIMU ZINASHAMBULIANA KWA ZAMU.

DK 55: STARS 1-1 CHAD.

DK 60: STARS 1-1 CHAD.

DK 67: STARS 1-1 CHAD.

DK 75: STARS 1-1 CHAD.

DK 81: STARS 1-1 CHAD

DK 85: STARS 1-1 CHAD

DK 90: STARS 2-1 CHAD. NURDIN BAKARI ANAIPATIA TZ BAO LA PILI.

YOUNG LIONS WAFANYA MAUAJI

VAN DER SAR: SAFU YA KIUNGO YA UNITED IIMARISHWE.


Edwin van der Sar anaamini safu ya kiungo ya Manchester United inabidi iboreshwe kama klabu hiyo inataka kushindana na Barcelona msimu huu.

Mholanzi huyo ambaye alicheza mechi ya mwisho mwezi May katika mechi ambayo vijana wa Sir Alex Ferguson waliadhiriwa na kipigo cha 3-1 katika fainali ya Champions league na vijana wa Pep Guardiola.

Hata Ferguson alikiri kuwa ilikuwa mechi ya upande mmoja, huku Barcelona wakipiga pasi 662 dhidi ya 301 za United. Hali inayomfanya Van Der Sar aamini mabingwa wa England wajaribu kubadilisha mfumo wa uchezaji wao hasa katika safu ya kiungo kama wanataka kufanikiwa barani ulaya msimu huu.

RASHID MATUMLA ULINGONI NA MTAMBO WA GONGO


MABONDIA Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’ wanatarajia kupanda ulingoni kuzichapa Desemba 25 mwaka huu katika pambano lisilo la ubingwa.

Pambano hilo linatarajia kuwa la raundi 10 uzito wa kati litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Heinken, Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam .

Akizungumza Dar es Salaam jana Ofisa habari wa Kampuni Adios Promotion ambao ndio waandaaji wa pambano hilo, Mao Lofombo alisema pambano hilo limeandaaliwa ili kumaliza ubishi baina ya mabondia hao ambapo katika pambano la mwisho Matumla alimchapa Oswald kwa pointi ambaye aliwalalamikia majaji kuwa hawakumtendea haki wakati walishawai kupigana mara mbili nyuma ambapo Matumla kamshinda Maneno Mara mbili na Maneno kashinda mara moja mpambano huo utakuwa wa kumaliza ubishi baina yao.

Alisema tayari mabondia hao wamekubali kucheza pambano hilo ambalo litakuwa la marudiano na kwamba wameshaanza maandalizi ambapo kila mmoja amejigamba kumstaafisha mwenzie ngumi.

Mao alisema, licha ya pambano hilo linalotarajia kuvuta hisia za mashabiki wa ngumi, pia kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi ambapo Rashidi Ally atachapana makonde na Hassan Sweet, Kalulu Bakari na Athuman Kalekwa na Shabani Kazinga na Kashinde
Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.

'' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani,

DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D DVD hizo za mafunzo zinapatikana makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au katika kambi ya ngumi ILala na klabu ya AShanti nayo ya Ilala.

BARUA YA VIONGOZI WA VILABU KUKATAA WITO WA TENGADOUBLE CLICK TO MAXIMIZE THE PIC.

Thursday, November 10, 2011

UNAWAKUMBUKA HAWA?


SIR ALEX FERGUSON'S GOLDEN GENERATION

JAN POULSEN ATAJA KIKOSI CHA KUIKABILI CHADGOLIKIPA
JUMA KASEJA


MABEKI

SHOMARI KAPOMBE

IDRISSA RAJAB

JUMA NYOSO

AGGREY MORRIS


VIUNGO

SHABAN NDITI

HENRY JOSEPH

ABDI KASSIM

NIZAR KHALFAN


WASHAMBULIAJI

MRISHO NGASSA

MBWANA SAMATTAAdebayor arejea kuitumikia TOGO.

Adebayor met Togo federation and government officials at his house in Accra, Ghana

Stern: League has 'stopped the clock'BREAKING NEWS: VIONGOZI WA VILABU WAKUBALIANA KUTOHUDHURIA MKUTANO WA TENGA KESHO

Masaa machache baada ya Raisi wa shirikisho la soka nchini TFF, Leodgar Tenga kuomba kukutana na viongozi wakuu wa vilabu 14 vinavyoshiriki katika ligi kuu ya Tanzania bara kwa ajili kuzungumzia utata wa namna ya uendeshaji wa ligi kuu ya msimu ujao utakavyokuwa, sasa taarifa za muda huu zilizothibitishwa zinasema viongozi hao wa vilabu wamekutana jioni katika hoteli ya Movenpick na kuamua kuwa hawatokwenda kukutana na Tenga kesho kama alivyoomba.

Viongozi hao wa vilabu wamesema sababu kuu ya kukataa kwenda kufanya mazungumzo na Tenga ni kwa sababu hawadhani kwamba kuna jipya lolote wataloambiwa ili kuweza kubadili msimamo wao wa ligi ya msimu ujao kuendeshwa na kampuni ya vilabu.


“Hatuoni kama kuna umuhimu wowote wa kufanya majadiliano juu ya suala hili, sisi sote tumeshaamua kwamba msimu ujao ligi itaendeshwa na kampuni ya vilabu vishiriki, TFF na Tenga wenyewe hawataki, wanataka kamati itakayoteuliwa na Tenga ndio iendeshe ligi. Tenga anataka tukae tujadili ajenda ipi? Sisi kwa pamoja tumeshaamua kwamba ligi ya msimu ujao itaendeshwa na kampuni yetu na huu uamuzi wetu wa mwisho,” alizungumza Geoffrey Nyange Kaburu ambaye ni mwenyekiti wa Kamati maalum ya kusimamia mchakato wa uanzishwaji wa Kampuni ya kusimamia ligi kuu kuanzia msimu ujao.
BREAKING NEWZ: TENGA KUKUTANA NA VIONGOZI WA VILABU VYA LIGI KUU KESHO


Sekeseke kati ya vilabu vya ligi kuu na shirikisho la soka nchini linatarajiwa kuchukua sura mpya hapo kesho baada ya Raisi wa shirikisho hilo, Leodgar Tenga kuwaita viongozi wote wa vilabu vinavyoshiriki katika ligi kuu kukaa katika meza moja na kujadili juu ya mustakabali wa namna ya kuiendesha ligi.

Mkutano wa Tenga na viongozi wa vilabu unatarajiwa kufanyika kesho katika makao makuu ya TFF-Karume stadium jijini Dar es Salaam.

Madhumuni yanatarajiwa kuwa ni kujadili juu mgogoro unaoendelea kati vilabu na TFF kuhusu namna gani inayofaa kuiendesha ligi kuu ya TZ bara msimu ujao.

Kwa muda mrefu sasa viongozi wa vilabu wamekuwa wakisema kuwa msimu ujao watachukua majukumu ya kuendesha ligi kupitia kampuni yao itakayoundwa na vilabu vishiriki, wakati TFF wakiwa wanataka ligi kuu iendeshwe kupitia kamati ya ligi.

TAIFA STARS YAWASILI SALAMA CHAD


Taifa Stars imewasili jana usiku hapa N'Djamena tayari kwa mechi ya kwanza ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Chad itakayochezwa kesho Uwanja wa Idriss Mahamat Ouya.

Timu imefikia hoteli ya Santana, na leo saa 10 jioni kwa saa za hapa itafanya mazoezi ya mwisho Uwanja wa Idriss Mahamat Ouya. Kesho mechi itaanza saa 10 kamili jioni ambayo kwa nyumbani ni saa 12 jioni.

Wachezaji wote wako katika hali nzuri isipokuwa beki Erasto Nyoni ambaye ameamka leo asubuhi akiwa na malaria. Kocha Jan Poulsen amesema atatangaza kikosi kitakachoanza mechi ya kesho baada ya mazoezi ya leo jioni.

Waamuzi wote wanatoka Nigeria. Mwamuzi wa kati atakuwa Bunmi Ogunkolade wakati wasaidizi ni Tunde Abidoye na Abel Baba. Kamishna wa mechi ni Hamid Haddadj kutoka Algeria.

Stars imekuja hapa na kikosi cha wachezaji 21 ambacho kitarejea nyumbani siku moja baada ya mechi kwa ndege ya Ethiopian Airlines kwa kupitia Addis Ababa, Ethiopia. Timu itawasili Novemba 13 mwaka huu saa 7.25 mchana na kwenda moja kwa moja kambini.

NEWCASTLE UNITED YABADILI JINA LA UWANJA


Mike Ashley jana usiku alimaliza historia ya miaka 119 ya Newcastle United baada ya kuupa jina jipya uwanja wa St.James’ Park kwa kuuita Sports Direct Arena.

TEENSPOT MAGAZINE !! ON SALE .. WE DO IT FOR THE YOUTH


Magazine yetu sasa ipo mtaani ! Pata Copy yako SASA

Miss Tz part 1: Watanzania Tumechoka kuwa Wasindikizaji Miss World…

Miss Tanzania 2011 Salha Israel

Hivi karibuni darbase.com ilikuwa ni mmoja ya mamilioni ya watu duniani ambao nilishuhudia mashindano ya Miss world yakitimiza miaka 60 na fainal zake kufanyika London Uingereza na Kama kawaida Tanzania tulipeleka Mwakilishi wetu Salha Izrael, na Kilichotokea ni kile ambacho tumekizoea na Mwakilishii wetu akabaki kuwa mshiriki na sio mshindani, ni hadithi ambayo imezoeleka,
Miss Venezuela, Ivian Lunasol Sarcos Colmenares,aliwashinda washiriki wengine kutoka nchi 113 na kutwaa taji hilo baada ya kuwaridhisha majaji katika mashindano hayo kwa kufanya vizuri katika categories zote starting with beach beauty, top model, talent, sports, and beauty with a purpose - where the contestants must demonstrate involvement in a charity project.
Shindano la Miss Tanzania lina historia kubwa na inayovutia ambapo mshindi wa Kwanza kabisa anayetambulika alikuwa ni Bi Theresia Shayo ambaye alijinyakulia Taji hilo rasmi mwaka 1967, Shindano hilo lilipita kipindi cha kufungiwa na serikali mpaka mwaka 1994 pale akina Uncle Hashim Lundenga na kamati ya Miss Tanzania walipolifufua tena na kulijenga kulipa umaarufu mkubwa ulionao hivi sasa. Kuanzia mwaka huo ambako Aina Maeda alipata nafasi ya Kuiwakilisha Tanzania Miss world, Haijatokea mrembo wa Tanzania Kufanya vizuri katika mashindano ya dunia ukiondoa Mwaka 2005 ambapo mrembo Nancy Sumari aliweza Kunyakua taji la Miss Afrika kwa kufika Fainali ya top 7, darbase.com haitakuwa na fadhila kama haitotambua mafanikio mengi ambayo kamati ya Miss Tanzania imeyapata katika kipindi hicho, kubwa ikiwa ni kufanya Miss Tanzania kuwa shindano kubwa la urembo afrika mashariki na kati, uendeshaji wa ufanisi wa kamati pamoja na kufungua njia kwa warembo wengi ambao wamepata nafasi kupitia miss Tanzania, wengi wamepata kazi katika mashirika, wamefanikiwa katika fani ya modelling duniani na wamekuwa wakipewa zawadi ambazo zilianzia nyumba mpaka magari, ni mafanikio makubwa yanayostahili kuthaminiwa na wote wanaopenda maendeleo,darbase.com kama mdau wa urembo chini Tanzania inatoa pongezi kubwa kwa Hashim Lundenga na timu yake kwa mafanikio hayo
Miss Tanzania kutokana na mafanikio yake imeweza kuvutia Mashirika makubwa hapa nchini kutoa udhamini wa uhakika kitu ambacho wenzetu Kenya na Uganda hawajaweza kukifikia, Akina Lundenga na Timu yake wamefanya kazi kubwa, hili hakuna ubishi.
Kama ulipata nafasi ya kuangalia fainali za mwaka huu utagundua kuwa mashindano hayo yamebadilika sana, sio urembo pekee but it is beauty with purpose, Mashindano yamekuwa na vipengele vya beach beauty, top model, talent, sports, and beauty with a purpose - where the contestants must demonstrate involvement in a charity project.

Ukiangalia washiriki wa Nchi nyingine walivyojiandaa utaona kuwa sisi tunafanya mzahaa, Japo mrembo wetu alikuwa miongoni mwa walioingia fainali za Kipengele cha beauty with a purpose utagundua kuwa kazi yake ya siku moja tuu aliyoifanya hospital ya watoto haiwezi kufua dafu hata kidogo na kazi zilizoshinda za Miss Ghana Stephanie Karikari ambaye alipresent kazi yake ya ukarabati wa Kituo cha watoto yatima, pamoja na Miss Indonesia Astrid Ellena ambaye alionyesha kazi yake ya kuhudumia watu wenye matende zilikuwa ni kazi ambazo zinaonyesha ziliandaliwa vizuri na washiriki waliokuwa na wataalamu ambao wanajua ni nini cha kufanya ambacho kita katch judge emmotions and attention kila aliyeangalia zile clips aliguswa, na hii inatokana na maandalizi ya kutosha pamoja na kutumia wataalam.

Mashindano haya yamenifungua macho haswa pale nilipowaona washiriki wengine wakishiriki Midahalo katika Cambridge society, Topic zilizokuwa zinazungumziwa ni kuhusu masuala ya kijamii na dunia kwa ujumla, umahiri wa waliozungumza unaonyesha kuwa walishafanya hivyo huko makwao kabla ya kwenda fainali sidhani kama Salha wetu alipata hata nafasi kwenda kwenye jumuia za chuo kikuu hapa nyumbani kuzungumza na vijana masuala yanayowakaboli kama mtoa mada au mchangiaji kitu ambacho darbase.com tunaamini ni msingi mkuu kutayarisha kwa mashindano makubwa ya Miss world, hakika hakutayarishwa!
Washiriki toka Afrika kusini Bokang Montjane(Miss Africa) pamoja Miss Zimbabwe Malaika Mushandu na mshindi hawakunishangaza pale walipofika top 15 kwani kama ulipata nafasi kuangalia wakati wanaonyesha utamaduni wa kwao kwa ngoma lazima ukubali, walitayarishwa kwa mavazi ya asili pamoja na kuwa mahiri kuzicheza ngoma hizo. Hauwezi kuwa na utaalamu huo kwa kipindi kifupi tuu cha mwezi mmoja ni lazima walitumia muda mrefu kujiandaa.Inauzunisha Salha alishindwa hata kucheza sindimba loh.
Hili jambo linakera na kama lisipofanyiwa marekebisho tutakuwa wasindikizaji, hebu nasi tujifunze kwa wenzetu kama India, Afrika Kusini, hata alipotoka mshindi wa mwaka huu ambapo mshiriki wa mwaka huu alishinda taji hilo tangu mwaka Jana hivyo basi alikuwa na muda wa Zaidi ya mwaka kujiandaa. Kamati ya Miss Tanzania, wadau na wadhamini inabidi waangalie uwezekano wa kubadili ratiba ili mshindi wetu apate nafasi kubwa kujiandaa. Vilevile hii itasaidia mrembo kujiheshimu na kujilinda kwani kama ameshinda mwaka huu itambidi ashiriki fainali za mwaka ujao, na kama hatakuwa na maadili ni rahisi kumdhibiti kwa kumyima nafasi ya kushiriki fainali, ukomo wa muda wake uwe ni pale anaporudi Miss world, darbase.com inaamini nchi ya Venezuela itakuwa ni sehemu nzuri kujifunza kwani hii ni mara yao ya 6 kunyakua taji la miss world.
Nafikiri umefika wakati Kamati ya miss Tanzania kubadili mashindano ili yafanane na vipengele vinavyotumika Miss world, Washiriki ambao wanawakilisha mikoa / kanda kwenye mashindano ya Taifa ni Lazima wawe ni washiriki wazuri kwenye michezo, Kila Mshiriki ni Lazima awe amejihusisha moja kwa moja na Kazi za Kujitolea huko alikotoka na zaidi ya yote BASATA na serikali inabidi wakaze buti kuhakikisha kila mshiriki anajua japo kucheza ngoma moja ya kitamaduni ili atuwakilishe vyema; it is a matter of National pride, Kushiriki kazi za kijamii kutoka mikoani itaongeza credibility kwa shindano na washiriki na wazazi watakuwa na furaha kuona watoto wao wakijitolea moja kwa moja katika jamii yao. Ukiangalia washiriki wa mwaka huu zaidi ya nusu wanasoma vyuo vikuu na mmoja katika kila washiriki wanne ana elimu ya chuo kikuu. Basi na kwetu profile ya washiriki wa fainali za Miss Tanzania inabidi japo iwe na nusu ya washiriki wenye diploma, inawezekana!
Mshiriki wetu hakuandaliwa vizuri, jaribu kuangalia website ya Miss world uangalie her profile na za wengine mfano, Miss Kenya, Catherine Susan ANYANGO, Future ambitions? I would love to start a cancer foundation in Kenya.Favourite food? Pilau. Miss South Africa, Bokang Ramaredi MONTJANE .Future ambitions? To own a top arts and confidence school for girls in South Africa. To have my own talk show tackling social issues. Favourite food? I love pap and tribe which is a traditional meat. Miss World, Venezuela, Ivian Lunasol SARCOS COLMENARES,Future ambitions ? Promote NGOs and work with children. Favourite food? My favourite food is chicken soup and the traditional pabellon of my country. Miss Tanzania, Salha Israel KIFAI, Future ambitions? To become a lawyer.Favourite food? My favourite food is Chinese pilau. Simlaumu Salha kwa kuwa na ambition za kuwa Lawyer katika shindano ambalo theme yake ni beauty with the purpose na Simlaumu kwa Kupenda Chinese pilau na sio any other Tanzania traditional food kama makande,ugali dagaa n.k, kama washiriki wa nchi nyingine wanavyopenda vyakula vya kwao, hii imetokea kwa sababu Salha hakuandaliwa, muda haukutosha!
La Mwisho nadhani sasa umefika muda wa Lino Agency kuweka utaratibu wa Kupanua wigo wa kuongeza na kubadili members wa kamati ya miss Tanzania, Damu mpya na mawazo mapya yanahitajika kutuvusha na kuleta mafanikio zaidi, Miss Tanzania ni shindano la Kitaifa na linahusu taifa zima lazima kuwe na watu wanaowakilisha makundi tofauti katika kamati ya miss Tanzania na wajumbe hao wasiwe wa Kudumu,Umefika muda kwa kamati ya Miss Tanzania to implement Salha motto ‘Think Big, Dream Big, Achieve Big.’
Nawakilisha…Tony.for.www,darbase.com, wadau wa urembo na burudani nchini ,tell 0718-144 133

TENGA AOMBA MIAK 4 MINGINE YA UONGOZI CECAFA ILI AMALIZE KAZI


Publish Post

Raisi wa shirikisho la soka nchini (TFF) na mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodegar Tenga amesema atagombea tena kuliongoza Baraza hilo na kwamba miaka minne mingine itamtosha kuweza kumalizia yale anayoyaona bado katika kuendeleza soka la ukanda huu.

Tenga alisema hayo jana alipokuwa akizungumzia uchaguzi mkuu wa baraza hilo unaotarajiwa kufanyika Novemba 24, siku moja kabla ya kuanza kwa mashindano ya Kombe la Chalenji,

Dar es Salaam.


Tenga, anayetetea nafasi yake atapambana na Makamu Mwenyekiti wake, Faoul Hussein kutoka Djibout, alisema kwamba dhamira yake ilimtuma kuomba miaka minne mingine ya

kulitumikia baraza hilo.


“Mimi ni muumini wa vipindi, nadhani nikipata miaka minne zaidi itanitosha,” alisema Tenga ambaye aliweka bayana kuwa hana nia ya kugombea tena baada ya kipindi cha miaka minne

mingine kuisha.


Tenga alisema kwamba haamini juu ya kukaa madarakani muda mrefu mpaka watu wanakuchoka na kuamua kukuondoa kwa aibu.


Alisema wapo watu wengi wenye uwezo wa kuongoza hivyo ni muhimu kwa kiongozi kuongoza kwa mtindo ya kuachiana madaraka.


Aliongeza kama atachaguliwa kwa miaka minne inayokuja baada ya kipindi hicho kuisha hatogombea tena na kwamba ataendelea kuchangia mawazo yake kama mwanamichezo yeyote yule katika maendeleo ya mpira wa miguu.


Kuhusiana na mpinzani wake, Tenga alisema ni haki ya kila mtu kikatiba kugombea kwa nafasi yoyote kama akipata ridhaa ya chama cha soka cha nchi yake.


Alisema yeye binafsi amepata ridhaa ya Shirikisho la Soka nchini TFF na ndio maana anagombea tena kutetea nafasi yake.

NEYMAR AZITOLEA NJE BARCA NA REAL - ASAINI MKATABA MPYA

Mshambuliaji kinda wa kibrazil Neymar amesaini mkataba mpya na klabu yake ya Santos na kumaliza uvumi wa miezi kadhaa kuwa alikuwa akijiandaa kujiunga na aidha Real Madrid au Barcelona.

Baada ya wiki iliyopita kutoka kwa taarifa kuwa Neymar atajiunga na Madrid katika uhamisho wa dirisha dogo mwezi January mwakani, leo hii imedhihirika kuwa Neymar amekubali kuuboresha mkataba wake na mabingwa wa uchampioni wa Copa Libertadores.

Mkataba wa Neymar ambao unaishia 2015, utaendelea kama ulivyo lakini mbrazili huyo ameongezea kiasi kikubwa katika mshahara wake aliokuwa analipwa kwa wiki.

Wakala wa mchezaji huyo Wagner Ribeiro amethibitisha kuwa makubaliano yamefanyika na kwamba mteja wake alikuwa na furaha sasa kuendelea kubaki Santos.

“Neymar ana furaha sana kuweza kuendelea kubaki hapa mpaka 2014 baada ya World Cup, baada ya hapo labda anaweza kufikiria kuondoka.” Alisema Wagner.

Mbrazili huyo anategemea kuvuna mshahara £1.1 million kwa mwezi na thamni yake inategemea kupanda kutoka £35.7m mpaka atleast £45million.

Wednesday, November 9, 2011

Fifa allow England to wear poppy on black armbands


Fifa has agreed that the England team can wear poppies on their black armbands during Saturday's friendly against Spain at Wembley.

The move came after Prince William and Prime Minister David Cameron wrote to Fifa asking that England be allowed to wear shirts embroidered with poppies.

Fifa bans political, religious or commercial messages on shirts.

The Football Association of Wales is now considering its position ahead of Wales' game against Norway.


Mr Cameron said "The idea that wearing a poppy to remember those who have given their lives for our freedom is a political act is absurd.

"Wearing a poppy is an act of huge respect and national pride."

WATANZANIA TUSAHAU WORLD CUP 2014.

Mbio za kwenda Brazil zinaanza mwishoni mwa juma hili na kuna nchi zaidi ya 200 zitakua zinagombania nafasi 31 huku nafasi moja ikiwa tayari imeshachukuliwa na mwenyeji.

Ni kama mwezi tangu tumefungwa na Morocco katika mechi ya mwisho ya kufuzu CAF 2012, Tulienda Morocco tukiomba miujiza na kwa bahati mbaya miujiza haikutokea, ukweli ulionekana kwamba Morocco walikuwa wazuri kuliko sisi, Kocha wetu mkuu Jan Poulsen pamoja na wachezaji wetu walikiri wenyewe kuzidiwa kimpira.

Sasa tunaenda kuwakabili Chad hata kama tukifanikiwa kuwatoa kwenye hii raundi ya awali lakini bado tutakaokutana nao mbeleni ni hao hao Morocco pamoja na miamba mingine kama Ivory Coast kwenye hatua ya makundi.

Hivi ni kweli watanzania wangapi wanaoweza kujiangalia kwenye kioo na kusema wana imani na sisi kwenda katika fainali za Kombe la Dunia Brazil, Tuwe wakweli kwanza na Hatuweza kabisa kwenda Brazil kwani Itakuwa ni miujiza ya hali ya juu.
Sasa kama we Malinzi unatambua hilo, na we Tenga unatambua hilo na viongozi wote wa Serikali wanatambua hilo kwanini tunatumia kile kidogo tulichonacho katika kushindana kwenye mashindano ambayo tunajua hatufiki popote ? Kwanini umlipie Nizar Khalfan kutoka Canada,Henry Joseph,Abdi Kassim waje kujiunga na timu wakati tunajua hatuendi kokote?

Mheshimiwa Pinda, kwa nini uwahimize watanzania wasaidie kwa hali na mali timu yetu wakati sote tunajua hawawezi kwenda Brazil bila miujiza?

Tukubali kwamba 2014 hatuendi Brazil hivyo mtuondoe mzigo wa matumaini ya kufuzu kwa miujiza na Kwanini tusitumie kile kidogo kilichopo kujenga timu ambayo mategemeo yake hayatategemea miujiza kufuzu fainali za kombe la mataifa afrika na kombe la dunia katika miaka kadhaa ijayo.

Nafasi ya kujenga timu kama hiyo ipo, lakini kwa nchi masikini kama yetu hatuwezi kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja, inabidi tukubali moja na hamna muda mzuri kama huu kukubali kwamba nafasi pekee tuliyonayo ya kwenda kombe la dunia au hata kombe la CAN ni kwa kujenga timu mpya, tukitumia vijana wetu wadogo.

Lazima tujipe nafasi ya kwenda huko kwa uwezo wetu. Na njia pekee ni moja na haijabadilika katika swala la mpira. Njia pekee ni kujenga upya mfumo wa mpira wa Tanzania kuanzia ngazi chini.

Kwa wafadhili wetu NMB, SERENGETI na wengineo. Kama kweli mnapenda maendeleo ya mpira wa nchi yetu? Basi fanyeni maamuzi ya kibiashara maana kama wafanya biashara najua mtawekeza pale mnapojua kuna nafasi kubwa ya mafanikio. Invest for the future, italipa maana wapenzi wa mpira hapa tuko nanyi kwa muda mrefu sana, bia zenu tutazinywa bado na benki tutaweka hela zetu.

Msaada wenu kwa miaka ya karibuni imetusogeza sana mbele na tunawashukuru sana kwa hilo, lakini hapo ndio tumefika mwisho kwa vipaji tulivyonavyo, hata mkiongeza mara tatu mnachotoa.

Sisemi tusishiriki kwenye haya mashindano, nachosema tushiriki na timu zetu changa ili ushiriki wetu uwe kwa madhumuni ya kuwapa vijana wetu uzoefu (experience) sio kwa madhumuni ya kujaribu kwenda Brazil 2014 au CAN 2015…

TUSAHAU! TUSAHAU! TUSAHAU KWENDA BRAZIL 2014!! ITATUSAIDIA KUJIPANGA ILI TWENDE RUSSIA 2018 AU QATAR 2022 KWA KUTEGEMEA UWEZO WETU NA SIO MIUJIZA KAMA ILIVYO SASA.

JERRY SANTO ATOA SHUKRANI, APATA TIMU ULAYA, KUJIUNGA NAYO JANUARY


Kiungo wa kimataifa wa Kenya na mchezaji wa zamani wa klabu ya Simba, Jerry Santo ameongea exclusively na blog hii kuwashukuru watanzania na wapenzi wa soka hapa nchini kwa kumpa ushirikiano na kumuonyesha mapenzi kwa muda wote aliokuwa akicheza hapa Tzee.


Pia Santo ambaye aliichezea Simba katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Tz Bara msimu huu amesema tayari ameshapata timu ya kuichezea barani ulaya inayoshiriki katika ligi kuu ya nchini Albania iitwayo KF Tirana.


Santo anasema anategemea kujiunga na timu hiyo mwezi January mwakani na anategemea kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia klabu hiyo ambayo wakenya wenzie Moses Arita na James Situma.


KF Tirana ni moja ya timu zenye mafanikio makubwa nchini Albania.IVO MAPUNDA AENDELEA KUTESA MOMBASA KENYA AKIWA BANDARI FCTANZANIA YAPANGWA KUNDI MOJA NA AKINA NIYONZIMA CHALLENGE CUP

Mabingwa watetezi na mwenyeji wa michuano ya CECAFA-Tusker Challenge cup timu ya taifa ya soka ya Tanzania wamepangwa katika kundi A linalohusisha timu za Rwanda, Ethiopia, na Djibouti.

Michuano hiyo ya Tusker Challenge cup ambayo itaanza November 25 mpaka December 10 mwaka huu, pia itashirikisha timu za Uganda, Burundi, Zanzibar na Somalia katika kundi B,

Kundi C linaundwa na timu za Sudan, Kenya, Malawi na Eritrea.Guinness Football Challenge Marcel Desailly


Guinness Football Challenge

Marcel Desailly

They say good things come in threes and if recent events are anything to go by,
it seems that the saying is true! I have just spent three very enjoyable days at
my sports facility in Accra, where I have had the immense pleasure of working
alongside three absolute legends of African football - Rigobert Song, Jay Jay
Okocha and Kalusha Bwalya. Together we have been filming for the GUINNESS®
FOOTBALL CHALLENGE™, which, I’m delighted to say, will be back on TV screens
very soon for its second season.

Like all lovers of the beautiful game, I was a huge fan of the first series which
is why I was so delighted to be asked to be involved in the show’s new season.
It’s very flattering and great fun to be working alongside such greats as Jay Jay,
Rigobert and Kalusha and I’m honoured that the Lizzy Sports Complex was
chosen as the location for the filming. It’s been a real pleasure to host both the L
egends and the team from the GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™.

If you’ve never seen the show, it’s all about achieving greatness by combining
football brains and football brawn to overcome trivia and physical challenges
as teams shoot for glory and the cash prizes on offer. As Legends, our role is to
show the contestants how best to take on the physical challenges, and having
spent the last three days filming them I’ve got to admit that some are pretty
tough! We gave them our best shot but I’m really hoping the contestants don’t
end up showing us up with their skills!

We also spent some time making the GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™
viral and all I can say is if the result is anywhere near as much fun as we had
filming it, then audiences everywhere are in for a treat! And you probably won’t
be surprised to know that we ended the final day doing what we love the most.
Wherever you find a group of ex-footballers and a ball, there’s a pretty high
chance some kind of game will happen – so we challenged some of the media and
crew toa game of 4-a-side, which was great fun. The other teams put up a good
challenge, but I’m delighted to say that we were on fire!

All in all it was a thoroughly enjoyable three days. It was great to pull the boots
on once again alongside the other guys and now I can’t wait for the show to start
so we can see all the contestants in action. And of course I’m especially excited
about the Legends Special episode at the end of the series where Rigobert, Jay
Jay, Kalusha and myself get partnered with the top scoring consumers who have
been playing the GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ game on their mobile
handsets. We’ll be showing off our fancy footwork and they’ll be showing the
nation just how much they know about football! If you want to be in with a
chance of playing the game with us, make sure you sign up to m.guinnessvip.com.
I need a good partner as I’m determined to show the other Legends how it
should be done – so get playing!

Please remember to drink responsibly, strictly 18/21+.

Tuesday, November 8, 2011

BOSINGWA AFUATA NYAYO ZA CARVALHO-AASTAFU SOKA LA KIMATAIFA.Mlinzi wa Chelsea Jose Bosingwa ameweka wazi kuwa hatoichezea tena timu yake ya taifa ya Ureno mpaka kocha wa sasa wa timu hiyo Paulo Bento atakapoondoka kwenye nafasi hiyo.


Bosingwa aliachwa katika kikiosi kitakachocheza play off ya Euro dhidi ya Bosnia and Herzegovina, huku Bento akiwa na mashaka huu ya mentality na tabia ya Bosingwa.


Akizungumza leo Bosingwa alisema: “Sijui nini anaongea kuhusu maoni yake juu mentality na altitude yangu. Nahisi kudhalilishwa na kutoheshimiwa kutokana na maneno yake. Sitovaa tena jezi ya Portugal ikiwa huyu Bento ataendelea kuwa kwenye benchi,” Bosingwa alikaririwa na A Bola.


“Jamii nzima inatambua juu ya tabia ya kocha huyu, haelewani na wachezaji na anagombana nao kila mara. Ana uwezo wa kiakili wala kihisia kuongoza kundi la wanaume na hafai kabisa kuiongoza timu ya taifa.”


Bosingwa anakuwa mchezaji wa pili wa Ureno kuamua kustaafu kuichezea Ureno, baada ya beki wa Real Madrid Ricardo Carvalho kujiondoa katika timu hiyo baada ya kugombana na kocha Bento.

UHAI CUP: SERENGETI BOYS KUPAMBANA NA VILABU VYA LIGI KUU.
Timu 15 zinazoshiriki michuano ya mwaka huu ya Kombe la Uhai zimepangwa katika makundi matatu ambapo mechi zitachezwa katika viwanja viwili; Uwanja wa Karume na Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Mbande.

Mashindano hayo yanashirikisha timu zenye umri chini ya miaka 20 za klabu zote 14 za Ligi Kuu ya Vodacom wakati timu mwalikwa mwaka huu ni timu ya Taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys).

Mabingwa watetezi Ruvu Shooting Stars ndiyo wanaoongoza kundi A katika michuano hiyo inayodhaminiwa na Kampuni ya Said Salim Bakhresa kupitia bidhaa yake ya maji Uhai. Timu nyingine katika kundi hilo ni Oljoro JKT, Kagera Sugar, Azam na Mtibwa Sugar.

Kundi B lina timu za JKT Ruvu Stars, Polisi Dodoma, Moro United, Yanga na Villa Squad wakati kundi C ni Simba, Coastal Union, Toto Africans, African Lyon na Serengeti Boys. Mbali ya sh. milioni moja za maandalizi kwa kila timu, mdhamini pia anatoa zawadi kwa washindi watatu wa kwanza, mchezaji bora, mfungaji bora, timu yenye nidhamu na nauli za kuja Dar es Salaam na kurudi kwa timu kutoka mikoani.

Campaign Against Malaria yenyewe inatoa seti moja ya jezi kwa kila timu inayoshiriki mashindano hayo ambayo yataanza Novemba 12 na kumalizika Decemba 13 mwaka huu.

Kila siku kutakuwa na mechi tatu katika kila uwanja. Siku ya ufunguzi Toto Africans itacheza na Serengeti Boys saa 3 asubuhi Uwanja wa Karume, Ruvu Shooting Stars vs Oljoro JKT (saa 8 mchana- Karume) na Kagera Sugar vs Azam (saa 10 jioni- Karume).

Simba vs Coastal Union (saa 3 asubuhi- Chamazi), JKT Ruvu Stars vs Polisi Dodoma (saa 8 mchana- Chamazi) na Moro United vs Yanga (saa 10 jioni- Chamazi).

TAIFA STARS KWENDA CHAD KESHO


Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajia kuondoka kesho (Novemba 9 mwaka huu) saa 9 alasiri kwa ndege ya Kenya Airways kwenda N’Djamena kwa ajili ya mechi ya kwanza ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Chad itakayochezwa Novemba 11 mwaka huu.

Msafara wa Stars wenye watu 40 ukiongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Eliud Mvella utawasili N’Djamena kesho hiyo hiyo saa 1.15 usiku kwa saa za huko ambapo kwa hapa nyumbani ni saa 3.15 usiku.

Wachezaji katika msafara huo watakuwa wote 21 walioko kambini, watu sita kutoka Benchi la Ufundi wakiongozwa na Kocha Jan Poulsen, wajumbe wawili wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na washabiki.

Stars ambayo iliagwa jana saa 1 usiku kwa kukabidhiwa bendera na Mwenyekiti wa BMT, Dioniz Malinzi itarejea nchini Novemba 13 mwaka huu saa 7.25 mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines na kwenda moja kwa moja kambini New Africa Hotel kujiandaa kwa mechi ya marudiano itakayochezwa Novemba 15 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

KAMATI: HATUNA MAMLAKA YA KUSIKILIZA RUFAA YA WAMBURA

Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imesema haina mamlaka (jurisdiction) ya kusikiliza shauri lililowasilishwa mbele yake na aliyekuwa mgombea uenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM), Michael Richard Wambura.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kamishna Mstaafu wa Polisi Alfred Tibaigana, Wambura aliwasilisha rufani mbele yao akipinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF kumuengua kugombea uongozi katika chama hicho.

Tibaigana alisema Kamati yake ambayo ina wajumbe saba, kabla ya kusikiliza shauri hilo ilitaka kwanza kujua kama ina mamlaka (jurisdiction) hayo. Kamati ilizitaka pande zote (bothi parties)- mlalamikaji na mlalamikiwa kueleza kama ina jurisdiction au la.

Mwanasheria wa Wambura, Audax Kahendaguza aliwasilisha hoja zake za kwa nini anadhani Kamati ina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo wakati Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alieleza kwa nini anaamini Kamati hiyo haina mamlaka hayo.

Baada ya hapo, Kamati ilizitoa nje pande zote mbili na baadaye kufanya uamuzi. Uamuzi wa Kamati kuwa haina mamlaka hayo ulikariri Ibara ya 12(4) ya Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF inayosema: “The decisions of the TFF Elections Committee are final and conclusive and shall not be monitored by any body.”