Search This Blog

Wednesday, November 9, 2011

TANZANIA YAPANGWA KUNDI MOJA NA AKINA NIYONZIMA CHALLENGE CUP

Mabingwa watetezi na mwenyeji wa michuano ya CECAFA-Tusker Challenge cup timu ya taifa ya soka ya Tanzania wamepangwa katika kundi A linalohusisha timu za Rwanda, Ethiopia, na Djibouti.

Michuano hiyo ya Tusker Challenge cup ambayo itaanza November 25 mpaka December 10 mwaka huu, pia itashirikisha timu za Uganda, Burundi, Zanzibar na Somalia katika kundi B,

Kundi C linaundwa na timu za Sudan, Kenya, Malawi na Eritrea.



No comments:

Post a Comment