Search This Blog

Saturday, May 25, 2013

KUTOKA LONDON: YANAYOJIRI NJE YA DIMBA LA WEMBLEY KABLA YA MCHEZO WA BVB VS BAYERN











HUU NDIO UCHAMBUZI NA UTABIRI WANGU WA FAINALI YA BORRUSIA DORTMUND VS BAYERN MUNICH

FC Bayern wanakutana na mtihani mgumu usiku wa leo watakapocheza dhidi ya Borussia Dortmund kwenye dimba la Wembley jijini London. Leo ni siku ya kuondokana na mkosi mkubwa unaowatawala mabavarians ambao ndio timu inayoongoza kwa kufungwa kwenye UEFA Champiosn League - leo ni siku ya kufuta machungu kwa kupoteza mechi ya fainali ya mwaka jana ambayo walistahili kushinda ingawa bahati haikuwa upande wao.
Hii ni fainali ya kwanza ya wajerumani ambao wanastahili kuwemo kwenye fainali hiyo. Utakuwa mchezo mzuri wa kukumbukwa.

Dortmund, klabu inayoibuka kuwa na nguvu barani ulaya

Majeruhi: Mario Götze

Baada ya kusemwa kuwa kutolewa kawenye hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa wa ulaya msimu wa 2011-12, Dortmund hatimaye wameyachukulia uamakini mashindano haya kwa gaharama ya kupoteza ubingwa wa nyumbani.
Ingawa, mchezo wao kwenye Champions League umekuwa wa aina yake. Nguvu, ushirikiano, mbinu za mchezo wao zimekuwa nzuri kiasi cha kuvishinda vilabu kama Real Madrid.

Mario Götze, kiungo mchezashaji wao, ataukosa mchezo huo kutokana na majeruhi ya misuli. Alijaribu kurudisha fitness yake kupitia mazoezi, lakini bahati haikuwa yake na akaawambia mchezo wake wa mwisho wa msimu huu ulikuwa pale Santiago Bernabeu. Ujuzi ambao BVB wataukosa ni pasi muhimu, kukimbiza mpira na mashuti yenye madhara

Wachezaji wa kuchungwa.
Kukosekana kwa Gotze kutamuacha mchezashaji Marco Reus. Kiungo huyo mshambuliaji anaweza kufanya runs za hatari pia kupiga mashuti na kutoa pasi za mwisho za hatari. Kazi ya kumzuia Reus kwa hakika atapewa kiungo mkabaji wa Bayern Javi Martinez ambaye aliweza kuwazima Iniesta na Andrea Pirlo kwenye mechi za raundi zilizopita.
Robert Lewandowski amegeuka kuwa mshambuliaji wa kiwango cha dunia, ameonyesha utulivu mbele ya lango la adui ambao washambuliaji wanakosa. Ana control nzuri ya mpira, anapiga mashuti yenye kulenga goli.
Muhimu zaidi, ni hazina ya Dortmund kwenye kulinda lango - golikipa Roman Weidenfeller. Uwezo wake wa kudaka uliinyima Bayern ushindi kwenye michezo kadhaa iliyopita msimu huu.
 Beki wa kati Mats Hummels anaweza akacheza mechi ya fainali pamoja na kuwa na majeruhi. Kitu cha kuvutia kuhusu yeye ni kwamba pamoja na mlinzi kwa ujumla, lakini pia anaweza akaigharimu timu yake kwa makosa ya kizembe.

Ilkay Gündogan ni kiungo mzuri mkabaji ambaye anaweza kufanya dribbling vizuri kuwapita mabeki wa Bayern, lakini sio mzuri kwa mipira ya juu ambao ndio silaha inayohitajika kuweza kuisimamisha Bayern.

Wakati uzuri wa Dortmund inacheza vizuri hata bila kuwa na mpira, mchezo mzuri wa kupasiana unaweza ukawadhuru kwenye nusu yao ya uwanja. Pia wana udhaifu mkubwa kwenye mipira mirefu.

Bayern, wanapaa kwenye muda muafaka

Majeruhi: Badstuber, Kroos.

 Huu ni mchezo unaomaanisha kila kitu kwa Bayern, ambayo ipo kwenye kiwango cha juu kwenye muda sahihi.
The bavarians wapo kwenye moto safari hii kwenye ulinzi na ushambuliaji. Udhaifu wao uliowagharimu msimu uliopita ni nguvu ya akili, udhaifu ambao umeshashughulikiwa. Sasa hivi wana ile hali ya winning mentallity - angalia namna walivyotoka nyuma na kuwafunga Borrusia Monchengladbach 4-3.
Franck Ribéry yupo kwenye kiwango cha dunia akicheza winga ya kushoto, unaweza ukasema hivyo pia kwa Thomas Muller ambaye anashughulika na majukumu ya kushambulia aliyokuwa nayo Toni Kroos.
Bastian Schweinsteiger na kila kitu cha kutoa kwenye mchezo huu. Ni package iliyokamilika kama mchezaji, box to box midle, yupo kwenye kiwango cha juu sana.
Uzuri wa Bayern hivi sasa mpaka wachezaji ambao walikuwa wavivu kama Arjen Robben wanakaba, timu yote inakaba kwa pamoja na wanashambulia kwa pamoja.

MBINU

Mtu yoyote ambaye angeniuliza timu gani yenye mbinu kali kati ya BVB na Real Madrid: jibu lingekuwa Dortmund. Sio tu kwamba wanaijua vizuri Bayern Munich, bali pia ni hatari sana kwenye mchezo wa kushambulia. Ubora wa umewaumiza wapinzaani wengi, lakini staili yao inayofanana na Barca ndio ambayo Bayern wanaiweza kwenye kucheza dhidi nayo.

Dortmund watahitaji kucheza mchezo wa kupelekea mashambulizi mbele, kupitia katikati ya uwanja kwa sababu ndio mchezo wanaouweza zaidi - wakipeleka mipira kwa Robert Lewandoski.

Kwa upande wa Bayern, mshambuliaji Mario Mandzukic (au Mario Gomez) wataungana na mchezeshaji Thomas Müller kuzuia mistari ya pasi kwenye kiungo kwa presha huku wakirudi nyuma taratibu
Hii itaaminisha Dortmund itabidi watumie zaidi winga kwenda mbele. Hivyo ikiwa BVB watapeleka mpira upande wa kushoto Arjen Robben na Javi Martinez wata press upande huo kuzia mashambulizi. Ikiwa watapeleka upande wa kushoto Frank Ribery na Bastian Schweinsteiger watazuia upande huo. Hii itawasaidia Lahm na Alaba kupambana akina Reus.

Hili linaweza kuwalazimisha BVB kutumia mipira ya juu ambayo Bayern wanaimudu pia, hivyo kuwafanya Dortmund kuwa na option moja tu kucheza sana mpira kwenye nusu yao ya uwanja na kujaribu kufanya counter. Hivyo nafasi zao za kufunga zitakuwa pungufu - au italawazimu wachezaji wa Dortmund kuwashinda wa Bayern kwenye vita ya one-on-one au kunufaika na makosa ya wachezaji wa Bayern kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Monchengladbach wiki iliyopita. Lakini pia Bayrn wanaweza wakawa wamepata funzo kupitia mchezo huo na kutoruhusu makosa yale yasijirudie dhidi ya Borrusia Dortmund usiku wa leo pale Wembley.

Ikiwa Bayern watacheza kwenye kiwango cha juu usiku wa leo basi itawachukua BVB kutumia vipaji binafsi zaidi vya wachezaji kuweza kushinda.
 
Vita binafsi leo hii itakuwa kati ya winga wa kushoto wa Bayern Frank Ribery vs Lukasz Piszczek. Kwa spidi aliyonayo Mpoland huyo, na uwezo wake wa kuzuia itamchukua uwezo mwingi sana Frank Ribery kuweza kupita.

Mara ya mwisho Bayern wameifunga Dortmund, walimtumia zaidi Toni Kroos na uwezo wake wa kumiliki mpira - Muller hana uwezo mkubwa wa kukaa na mpira kama ilivyo kwa Kroos hivyo mambo yanaweza magumu kiasi.

Utabiri wangu nawapa Bayern nafasi ya kushinda. Mafunzo waliyoyapata miaka iliyopita hasa msimu uliopita dhidi ya Chelsea yatawapa hali ya kupigana zaidi. Hata kama wataanza kufungwa, watashindana na kuhakikisha safari hii wanaepukana na mkosi wa fainali ya Champions League. Dortmund wana mtindo wa kupaniki - angalia katika mechi ya pili dhidi ya Madrid nusura waondolewe pamoja kuwa walikuwa na hazina ya mabao 4-0.

Vikosi vinavyoweza kuanza

FC Bayern (4-2-3-1) Neuer – Lahm, Boateng, Dante, Alaba – Martinez, Schweinsteiger – Robben, Müller, Ribéry – Mandzukic
Borussia Dortmund (4-2-3-1) Weidenfeller – Piszczek, Subotic, Hummels, Schmelzer – Gündogan, Kehl – Blaszczykowski, Reus, Grosskreutz – Lewandowski
Location: Wembley Stadium, London
Referee: Nicola Rizzoli (Italy)

Friday, May 24, 2013

CHAMPIONS LEAGUE FINAL COUNTDOWN: BORRUSIA DORTMUND NA BAYERN ZAWASILI JIJINI LONDON MAPEMA LEO


Shaffih Dauda nikiwa baadhi ya mashabiki wa BVB waliokwenda uwanjani kuilaki timu yao

Borrusia Dortmund wakiwasili London mapema leo

Roberto Lewandoski na wenzie ndani ya Heathrow Airport
Jurgen Klopp kocha wa Borrusia Dortmund

Mario Gomez akiwasili jijini London

Frank Ribery akilakiwa na umati wa mashabiki

AZAM TV NA SUALA LA KUONYESHA LIGI KUU - SIMBA, YANGA HAZINA NIA NJEMA NA SOKA LA TANZANIA




KAMPUNI ya S. S. Bakhressa ilipoanzisha timu ya soka ya Azam FC, viongozi na mashabiki wa klabu kongwe za Simba na Yanga walidhani ni nguvu ya soka.
S. S. Bakhressa ikapiga hatua ya pili kwa kujenga uwanja wa kisasa, Chamazi, Temeke, Dar es Salaam, ikiwa ni ishara ya dhamira ya kufanya mapinduzi ya soka nchini.
Mbali ya kujenga uwanja wa mazoezi (unatumika hata kwa mashindano) na uwanja mkubwa wa kisasa ambao ujenzi wake ulizinduliwa na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni, S.S. Bakhressa imeingia hatua nyingine kubwa kwa kuanzisha kituo cha televisheni cha Azam TV.
Moja ya malengo ya Azam TV inayojenga barabara ya Nyerere ni kutumia kiasi cha Sh. 1.5 bilioni kuonyesha moja kwa moja mechi za Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Ikiwa itapata haki ya kuonyesha ‘live’ mashindano hayo, taarifa zinasema Azam TV imejipanga kutoa Sh. 100 milioni kwa kila timu kati ya 14 zitakazoshiriki msimu ujao wa ligi hiyo. Hii ni neema kubwa kwa klabu zote hasa changa.
Hii ina maana sasa angalau kila timu, itaweza kujikimu kwa kiasi chake na kuweka karibu uwiano sawa wa kuchuana na timu zenye uwezo mkubwa wa kifedha kama Simba, Yanga na Azam FC iliyo chini ya kampuni ya S. S. Bakhressa.
Kwa hiyo, timu zisizo na wadhamini mkubwa na ambazo ndiyo kwanza zimepanda daraja kama Ashanti United ya Ilala, Mbeya City ya Mbeya na Rhino ya Tabora na hata zilizopo kama Coastal Union zitanufaika kwa kiasi kikubwa na ujio wa udhamini wa Azam TV.
Timu zilizoshuka daraja za Toto African, African Lyon na Polisi Morogoro zitakuwa zinasikitika neema kuja kwenye ligi wakati zimetupwa nje.
Msimu uliopita tuliiona Toto ya Mwanza ikishiriki kwa tabu ligi hiyo huku wachezaji wake wakilala katika basi wakati mwingine huku chakula pia kikiwa shida. Hali hii inachangia kwa kiasi kikubwa timu hizi ambazo hazipo chini ya taasisi kubwa kufanya vibaya hasa katika mechi zake za umbali mrefu na wakati mwingine hata zile za katika kituo chake.
Kwa vyovyote vile Azam TV inakuja kuleta ushindani mkubwa siyo katika udhamini tu, bali hata urushaji wa vipindi vya michezo.
Lakini Simba na Yanga zilizoanzishwa kabla ya uhuru ‘zinapanga’ hujuma. Simba wanadai kiasi cha Sh. 100 milioni ni kidogo na hakilingani na hadhi yao na pia hawawezi kulipwa sawa na timu nyingine za ligi hiyo.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage amenukuliwa na gazeti moja la michezo akisema anakubaliana na wazo la Azam TV, lakini kiasi hicho cha fedha ni kidogo kwao na hata siku moja timu haziwezi kulipwa haki sawa ya matangazo huku akitolea mfano katika Ligi Kuu ya England.
Kwa upande wa Yanga, Ofisa Habari wake, Baraka Kizuguto amesema hawezi kuzungumzia vitu vya tetesi kwani Azam TV hadi sasa hawajawapelekea taarifa rasmi kuhusu lengo hilo la kuonyeshwa kwa mechi zao msimu ujao.
“Sipo katika nafasi nzuri ya kuzungumzia jambo hilo, kwani hatujataarifiwa jambo lolote juu ya mpango huo wa Azam TV, wakituletea maombi yao, sisi kama timu tutakaa na kutoa uamuzi,” anasema Kizuguto.
Hii ina maana kwamba, kama Simba na Yanga zitabaki na mawazo hayo, Azam TV inaweza kukwamishwa katika mpango huu na kubaki na ule wa kuonyesha mechi za timu yao tu, kwani lengo lao ni kutangaza biashara zao.
Utaratibu ni kwamba muda ukifika, uongozi wa Azam TV utaomba kibali cha kudhamini Ligi Kuu kutoka Kamati ya Ligi ambayo itapanga kiwango baada ya kuteta na klabu.
Vituo vya TV vikionyesha ‘live’ mechi yoyote ya ligi hupaswa kulipa gharama kufidia kiasi cha watu ambao hawataingia uwanjani na kutumia fursa hiyo kurusha matangazo ya biashara. Azam TV haitazungumza na klabu binafsi.
Lakini kwa desturi za Simba na Yanga, ambazo miaka nenda rudi ni kupanga mikakati ya kuangushana, hata hili zinaweza kukwamisha. Kwa husuda zitaweka mgomo ili mpango huu ufe ili zenyewe zibaki kutawala soka, timu ndogo zibaki zikinyanyasika kama ilivyokuwa kwa Toto African iliyopigana hadi inashuka daraja.
Rai yangu kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Kamati ya Ligi ni kwamba, Simba na Yanga zisiachwe kuharibu mapinduzi ya soka yanayoletwa na Azam TV.
HABARI HII IMETOLEWA KATIKA GAZETI LA MAWIO, IMEANDIKWA NA ELIUS KAMBILI
         

BREAKING NEWS............AMRI KIEMBA ASAINI YANGA

WAKATI Haruna Niyonziam akiwa amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga, habari zilizotufikia hivi punde zinasema kiungo wa Simba, Amri Kiemba amesajiliwa na Yanga tayari kwa kuitumikia timu hiyo kwa msimu ujao.
Akizungumza na mtandao huu, mtu mmoja kutoka kamati ya usajili ya Yanga, amesema Kiemba amesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili ili kuongoza nguvu katika safu ya usajili ya Yanga.
Mtandao huu unaahidi kuwasiliana na Kiemba muda mfupi atakapotoka mazoezini katika kambi ya Taifa Stars kujiandaa na mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2014.
Atakapotoka mazoezini mtandao huu utawasiliana naye kiungo huyo ili aweze kueleza ukweli juu ya usajili wake kwa Yanga.
Kiemba aliwahi kuichezea Yanga miaka ya nyuma kabla ya kutimka katika timu hiyo.

KUELEKEA FAINALI YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE - RIPOTI KUTOKA JIJINI LONDON NA SHAFFIH DAUDA

Yakiwa yamebaki masaa kadhaa kabla ya fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya kufanyika mmoja wa waandishi wa mtandao huu Shaffih Dauda atakuwa akiripoti matukio na taarifa muhimu kuhusu mpambano huo utakawakutanisha wapinzani wa ligi ya Ujerumani Borrusia Dortmund vs Bayern Munich.

JUPP HEYNCKES - HUU NDIO MSIMU WANGU BORA KULIKO YOTE

Akiwa na miaka 68, na zaidi ya miongo hata mitatu kwenye kufundisha soka. Kocha wa FC Bayern Munchen Jupp Heynckes anafurahia msimu wake bora kabisa kwenye maisha yake ya ufundishaji soka.
Heynckes, yupo katika mwaka wake wa 3 kwenye mkataba wake na Bayern na tayari ameshaiongoza Bayern Munich kutwaa ubingwa wa Bundesliga. UEFA Champions League - ubingwa ambao Heynckes alishinda na Real Madrid CF mwaka 1998 - anaweza kushinda kwa kuifunga Bayern mbele ya Borrusia Dortmund siku ya jumamosi, wakati kuna fainali ya kombe la Ujerumani dhidi ya VfB Stuttgart inamsubiri ili kuweza kushinda treble. Itakuwa jambo la kuvutia kwa Heynckes kumuachia nafasi Josep Guardiola.
"Sijawahi kuwa na msimu kama huu, ni kitu kizuri kuwahi kunitokea kwenye maisha yangu ya soka," alisema. "Tumevunja karibia rekodi zote. Kawaida unapofunga mabao mengi pia unaruhusu mengi, lakini wachezaji kama Arjen Robben, Franck Ribéry, Mario Gomez, [Mario] Mandžukić, Thomas Müller, [Xherdan] Shaqiri, wote wameshajivunza namna kuzuia. Hilo ni jambo muhimu kwenye soka la leo.
"Fainali itakuwa ngumu ila tumejipanga kuweza kuepeukana na machungu ya msimu uliopita. Dortmund ni timu nzuri naamini fainali itakuwa mchezo wa kuvutia."

DORTMUND - KUNDI GUMU LILIWAPA HALI YA KUJIAMINI


Kama Borussia Dortmund itashinda ubingwa UEFA Champions League pale Wembley siku ya jumamosi, kwa hakika watakuwa wameshinda kwa njia ngumu.
Wakiwa wamepangwa kwenye kundi gumu lilohusisha timu zilizobeba ubingwa msimu uliopita AFC Ajax, Manchester City FC na Real Madrid CF, ambao walikuja kukutana nao kwenye nusu fainali na Robert Lewandowski akaisaidia timu yake kuidhalilisha Madrid.
Lakini mechi nyingine za kusisimua walizofanya maajabu kwa mabao ya dakika za mwisho kwenye mechi hatua ya mtoano na robo fainali dhidi ya Malaga na Shakhtar Donetsk. 
"Tumekuwa na wakati mzuri mpaka sasa kwenye michuano hii, kuanzia kwenye hatua ya makundi mpaka tulipofika fainali. Mechi za makundi zilitufungua macho na kutupa mwanga wa namna ya kupambana na vilabu bora barani ulaya na namna ya kuweza kuvishinda.
Wanaosimama mbele ya Dortmund ni washindi wa pili wa msimu uliopita FC Bayern Munich. Wanaweza wakawa wamemaliza lgi wakiongozwa kwa pointi 25 na vijana wa Jupp Heynckes na walipoteza mechi zao mbili kati ya nne za mwisho walizokutana, lakini kocha Klopp hatishwi na hali hiyo. Anasema kwamba inawezekana huu ndio ukawa mchezo mkubwa zaidi wa BVB tangu ushindi wa fainali ya UCL mwaka 1997.  

"Mpango wetu ni kuufanya huu mchezo kama mwingine, hatutaki kujipa presha, ingawa tutacheza kwa namna ya tofauti ili kuweza kujihakikishia ushindi."

HARUNA NIYONZIMA ASAINI MIAKA MIWILI YANGA SC


Uongozi wa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom  klabu ya Young Africans leo umekata mzizi wa fitina kwa kiungo mchezeshaji kutoka nchini Rwanda Haruna Niyonzima kuendelea kuitumikia timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili kufuatia kumalizika kwa mkataba wake awali.
Akiongea na waandishi wa habari makao ya klabu ya Yanga, katibu mkuu Lawrence Mwalusako amesema wameamua kumuongezea mkataba mchezaji huyo kufuatia kuuhitaji mchango wake kwani katika kipindi chake cha miaka miwili ameonyesha kiwango cha hali ya juu na kutoa mchango mkubwa.
 Mwalusako amesema kumekua yakiongelewa mengi juu ya mchezaji wetu Niyonzima, baadhi ya vyombo vya habari vimekua vikitoa taarifa za kupotosha juu yake ukweli leo umedhihirika kwamba Niyonzima ni mchezaji wa Yanga na ataendelea kuitumikia kwa miaka miwili.
Haruna Niyonzima alijiunga na Yanga kwa mara ya kwanza Julai 2011 akitokea katika timu ya APR nchini Rwanda ambapo katika miaka yake miwili aliyoichezea timu ya Yanga amefanikiwa kuisadia kupata makombe mawili ya ubingwa wa Ligi Kuu 2012-2013 na Kombe la Kagame 2011-2012.
Naye Niyonzima amesema anawashukuru wanachama, washabiki na wapenzi wa klabu ya Yanga kwa kuwa naye muda wote, Yanga ni nyumbani kwangu kwani najisikia furaha kuichezea timu hii na malengo yangu ni kuisadia ili iweze kufanya vizuri katika upatashindano ya kimataifa.
Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya klabu ya Yanga Abdallah BinKleb amesema palikua na propaganda nyingi juu ya Niyonzima, lakini ukweli ndio huu Niyonzima ataendelea kuitumikia klabu ya Yanga kwa miaka miwili.
"Tunautambua mchango wake alioutoa kwa miaka mwili kwani ameweza kutupatia vikombe viwili vya Ligi Kuu ya Vodacom na Kombe la Kagame hivyo tumemuongezea mkataba wa miaka miwili tena ili aendelee kutoa mchango wake na kuisadia timu katika michezo ya kimataifa" alisema BinKleb

Thursday, May 23, 2013

TATHMINI YA LIGI KUU 2012/03 - UKATA, MIGOGORO VILIATHIRI LIGI KUU



UKATA na migogoro isiyoisha baina ya viongozi na wanachama ndiyo ilichangia baadhi ya timu kufanya vibaya na nyingine kushuka hadi daraja la kwanza.
Timu pekee ambazo hazikuathiriwa na migongano kati ya viongozi na wanachama au viongozi na wachezaji ni zile zinazomilikiwa na mashirika kama Kagera Sugar na Mtibwa Sugar, na zinazomilikiwa na majeshi.
African Lyon, licha ya kuwa na wadhamini pamoja na Coastal Union, Toto African na matajiri wa udhamini Simba na Yanga zilikumbwa na migogoro iliyoziathiri kwa namna moja au nyingine.
Yanga, pamoja na kutambia Kocha Tom Saintfiet wa Ubelgiji, ilianza ligi kwa kutoka suluhu na Prisons na ilipochapwa 3-0 na Mtibwa Sugar akatimuliwa akaajiriwa Mholanzi Ernie Brandts, aliyeiwezesha kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Bara baada ya kufikisha pointi 60.
Simba ilianza kwa shangwe, lakini ilipotoka sare kadhaa na kuambulia vichapo, wanachama wa tawi la Mpira Pesa wakaujia juu uongozi, baadhi ya viongozi wakaachia ngazi na kocha Mserbia Milovan Cirkovic akafukuzwa akaajiriwa Mfaransa Patrick Liewig ambaye alifurukuta na kuiwezesha kushika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 45. Bila migogoro huenda Simba ingemaliza nafasi nzuri zaidi.
Azam FC isiyo na mashabiki wengi, ilianza msimu ikiwa chini ya Mserbia Boris Bujak 'Buka' lakini ghafla alitimuliwa na nafasi yake ikajazwa na kocha wake za zamani Mwingereza Stewart Hall aliyeisaidia kushika nafasi ya pili baada ya kufikisha pointi 54. Vilevile timu hiyo ilivurugana na wachezaji watatu ikidai wamepokea rushwa.
Kwa tathmini, timu hizo zenye ukwasi wa fedha ndizo kwa mara nyingine zimeshika nafasi tatu za kwanza. Msimu uliopita Simba ilikuwa bingwa ikafuatiwa na Azam na Yanga.
Wakati Simba na Yanga zilikuwa na uwezo wa kutimua makocha na kuajiri wengine, Toto African ya Mwanza ilikosa uwezo huo ikabaki ikipigania kutoshuka daraja. Ukata ulipoielemea Toto ilibaki ikilalamikia ugumu wa ratiba na waamuzi hadi imeshuka daraja la kwanza.
African Lyon ilianza ligi ikiwa na mikakati ya kujinasua kwenye ukata lakini ilikwama. Kwanza kampuni ya Zantel iliyotaka kuidhamini iliwekewa kauzibe na pili kocha Muarentina Pablo Ignacio Velez aliyeajiriwa kuiboresha kikosi alitupiwa virago.
Timu ikabaki chini ya msaidizi wake Jacob Otieno naye aliposhindwa ikaachwa kwenye mikono isiyo salama ya Salum Bausi aliyeshuka nayo. Coastal Union chini ya Hemed Morocco ilianza vizuri na hata kutamba kuwania nafasi tatu za juu, lakini imeishia nafasi ya sita huku mchezaji wake Nsa Job akikabiliwa na tuhuma za kupokea mlungula kutoka moja ya klabu kubwa.
Timu ndugu za Kagera Sugar na Mtibwa Sugar, zote zikimilikiwa na kampuni ya Super Doll, zimejitokeza kuwa kiboko cha vigogo baada ya kutoa vichapo kwa nyakati tofauti. Kagera chini ya Abdallah Kibadeni ilishika nafasi ya nne ilhali Mtibwa chini ya Mecky Mexime iliishia nafasi ya tano.
Kagera Sugar na Mtibwa Sugar hazina ukata lakini pia hazina mafungu makubwa kwa ajili ya kufanya usajili wa wachezaji ghali wanaoweza kuzisaidia kutwaa taji la Ligi Kuu.
Katika kipindi chote cha ligi, hayakusikika malalamiko wala manung’uniko ya hali ya kambi kutoka timu za Jeshi la Kujenga Taifa kama Ruvu Shooting, Oljoro JKT, Mgambo na JKT Ruvu. 
Aidha, hayakusikika malalamiko kutoka Prisons iliyo chini ya Jeshi la Magereza wala Polisi Moro iliyo chini ya Jeshi la Polisi hadi imeshuka daraja.
Hata hivyo, ushiriki wa kusuasua na uwezo mdogo wa kusajili wachezaji wenye majina makubwa umeziathiri. Kisheria, timu hizo hazipaswi kusajili wachezaji nyota kutoka nje ya nchi.
Timu hizo, ambazo kwa muundo ni kwa ajili ya kutoa burudani kwenye majeshi, zimekuwa zikitoa mchango mkubwa katika Ligi Kuu japokuwa kwa ushindani wa wastani tu. Ni mara chache sana zimekuwa na uwezo wa kuzifunga timu kubwa za Simba, Yanga na Azam ila humudu kutoa sare.
Mara nyingi ushindani fulani huonekana zinapokutana zenyewe. Wakati fulani zimekuwa na matokeo mazuri kwenye viwanja vya nyumbani na nyingine kama Mgambo imeponea chupuchupu.
Polisi Moro, Toto na African Lyon zimeshuka daraja na kwa utaratibu zimepisha nafasi kwa Ashanti United ya Ilala, Mbeya City na Rhino ya Tabora zilizopanda daraja. Nazo zisipokuwa na mafungu ya kusajili wenye uwezo au zikiendekeza migogoro kwa muda mrefu zitajikuta zikirejea daraja la kwanza.
MAKALA HII IMETOLEWA KATIKA GAZETI LA MAWIO, IMEANDKWA NA ELIUS KAMBILI

DAVID MOYES - KWENYE MKATABA WA MIAKA 6 NA UNITED - ASIPOSHINDA KOMBE NDANI YA MISIMU 2 ATAFUNGULIWA MLANGO WA KUTOKEA


David Moyes, mmoja wa makocha bora kabisa katika ligi kuu ya England ameamua kuondoka Everton baada ya miaka 11 akiwa na klabu ya Merseyside na kuhamia Manchester United kwa mkataba wa miaka 6. Tatizo ambalo msotish huyo atakalokumbana nalo kwa mabingwa hao wapya wa England ni kwamba asiposhinda kombe lolote ndani ya misimu miwili basi atakumbana na panga la kufukuzwa.

Moyes alianza kufundisha soka akiwa na klabu ya Preston North End mwaka 1998, kwenye klabu ambayo alimalizia maisha yake ya kucheza soka. Moyes aliiwezesha Preston kuepuka kushuka kutoka daraja kutoka daraja la pili, then msimu uliofuatia akawaongoza Preston kucheza playoffs, lakini wakafungwa. Mscotland huyo alirudi tena msimu uliofuata na kushinda ubingwa, na kuipeleka klabu hiyo ligi ya daraja la kwanza. Mwaka 2001, Preston walifungwa kwenye playoffs na kufeli kupanda daraja kucheza ligi kuu, lakini mafanikio ya Moyes yalionekana, na akasajiliwa Everton mwaka 2002. 

March 14th 2002, Moyes alitambulishwa kama kocha mpya wa Everton. Alianza vizuri na ushindi wa 2-1 dhidi ya Fulham. Klabu hiyo Merseyside ikamaliza msimu kwenye nafasi ya 7 katika msimu wake wa kwanza. Aliiongoza timu kwa kuwatimua akina David Ginola na kuwaleta wachezaji akina Joseph Yobo na Richard Wright. Ingawa hakuwa na msimu mzuri wa pili akimaliza nafasi ya 17 na pointi 39, kiasi kidogo cha pointi kuwahi kutokea kwenye historia ya klabu hiyo, lakini Moyes aliweza kuepuka kuishusha daraja klabu hiyo.
Miaka iliyofuatia alishuka na kupanda, mwaka 2004 alimpoteza Wayne Rooney kwa Manchester United, lakini pamoja na kumpoteza mmoja wachezaji wake muhimu, Everton wakaenda kumaliza msimu kwenye nafasi ya nne na kufuzu kucheza Champions League. Kuonja ladha ya soka la ulaya kukawapanda wachezaji kichwani na kwa mara nyingine tena Everton wakawa wanapigania kutoshuka daraja. Klabu ikamaliza kwenye nafasi ya 11, lakini msimu wa 2005-06 wakamaliza 6th position, hivyo soka la mashindano ya UEFA Cup likahamia Goodison Park.

Mwaka 2007 ulikuwa msimu ambao Moyes aliigeuza Everton kuwa moja vilabu tishio kwenye nafasi za kucheza ulaya na akafanikiwa kumsaini Leighton Baines kwa £6m na Phil Jagielka kwa £4m. Na mwaka 2009, alivunja rekodi ya ada ya usajili ya klabu kwa kumsaini mbelgiji Marouane Fellaini kwa £15m na wakafanikiwa kufika fainali ya FA Cup ambapo wakafungwa 2-1 na Chelsea.
Habari kubwa ilikuja April 21st 2010 ambapo Sir Alex Ferguson alipotangaza kwamba anamtaka maneja wa Everton Moyes awe mbadala wake atakapostaafu. Lakini May 14th 2010, Moyes alielezea matamanio yake ya kutaka kuifundisha klabu ya nyumbani kwao ya Celtic,lakini Neil Lennon akateuliwa badala yake. Kwa mshtuko zaidi  May 8th 2013, Sir Alex aliamua kustaafu na David Moyes akapewa mikoba ya Fergie akisaini mkataba wa miaka 6 na Red Devils, na hapa ndipo wasiwasi wangu ulipo.

Sir Alex amekuwa kocha wa soka kwa miaka 39 na 26 kati ya hiyo ameitumia katika kuifundisha Manchester United. Alifanikiwa kushinda vikombe 49, na 38 kati ya vikombe hivyo ameshinda akiwa na United. Aliwaambia waandishi wa habari kwamba David Moyes alikuwa ndio chaguo lake la asili kabisa lakini Moyes alisema kwamba hakuwa amepanga kuondoka Everton na asingeweza kuikataa Manchester United. 
Akiwa anatajwa kama kocha bora wa muda wote, Ferguson anaacha viatu vikubwa kwa Moyes, lakini je yupo tayari kwa changamoto hiyo. Muda pekee ndio utaongea.

Kuleta kombe kwenye kabati la vikombe Old Trafford ndio kitakuwa kitu muhimu kwake katika kupata sapoti ya mashabiki wa United, aidha kubeba tena ubingwa wa EPL au kushinda Champions League, Moyes atategemewa kubeba kombe mapema, ikizingatiwa kikosi alichoachiwa cha sasa, kilicho na mchanganyiko wa vijana na wachezaji wenye uzoefu, pia tayari amehakikishiwa mzigo wa usajili ambao kuna tetesi anataka kuutumia katika kuwasajili Baines na Fellaini.

Kushinda makombe 38 ni kitu kikubwa sana kwake, lakini mashabiki wa klabu watahisi vibaya ikiwa ndani ya kipindi cha miaka 2 atashindwa kuleta ubingwa Old Trafford na anaweza akaonyeshwa mlango wa kutokea. Manchester United na mashabiki wao hawajozea kumaliza msimu bila kombe. Hii inaweza kuwa safari nyingine ndefu yenye mafanikio kwa Moyes au inaweza kuwa mwanzo wa anguko lake. Vyovyote itakavyokuwa mashabiki wengi wa United wana furaha kwamba meneja wa Everton amekuwa mrithi wa Sir Alex Ferguson.

MWISHO WA AIBU WA ZAMA ZA JOSE MOURINHO NDANI YA REAL MADRID






May 21st 2003 ni tarehe ambayo Jose Mourinho akiwa na kikosi cha FC Porto alishinda ubingwa wa UEFA Cup kwa kuwafunga Celtic. Tangu wakati huo alienda na kushinda makombe mawili ya Champions League na makombe ya ligi katika nchi nne tofauti. Kunaweza kukawa na ubishani mdogo tu kwamba ndiye kocha aliyetawala katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, japokuwa muda wake ndani ya Madrid umeisha vibaya.
2013 umekuwa mwaka wa mwisho wa zama za makocha wengi na wachezaji. Kwa baadhi yao wamekuwa wakisifiwa kwa kazi zao ingawa kwa mtu mmoja - Special One,wakati wake ndani ya Madrid unaangaliwa kama wakati ambao umemfelisha Mourinho kama kocha.

Baada ya kipigo kutoka kwa Atletico kwenye fainali ya Copa Del Rey Jose Mourinho aliulezea msimu huu kama ndio m'bovu kuliko yote kwenye maisha yake ya soka. Ulikuwa wa shetani kwa Madrid huku michezo miwili ikiwa imebakia, Mourinho alitolewa nje kwa kumtusi mwamuzi akiiacha Madrid ikiwa imeghafirika dimbani dhidi ya wapinzani wao wa jadi. Mafanikio pekee aliyoyapata ndani ya msimu huu ni ubingwa  Spanish SuperCup. 

  Msimu uliopita Madrid walikuwa makini, wenye hamu ya kufanikiwa na wakiwa na umoja katika kuuvunja utawala wa Barcelona. Pointi zao walizopata kwenye LA LIGA zilivunja rekodi, walifunga mabao mengi na wangeweza kuzidisha idadi hiyo kama wangekuwa makini. Wangeweza kufanikiwa zaidi msimu uliopita kama wangeshinda kwenye penati kwenye nusu fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya - kufungwa kwao usiku ule ulikuwa mwisho wa umoja wao. ere driven, determined and importantly together in their quest to overcome Barcelona.

Madhara ya kutokuwa na umoja yalionekana msimu huu. Hamu ya kutaka kufanikiwa ulaya zaidi ilizaa sumu iliyokuwa ikimtafuna Mourinho, ligi ikaonekana haina umuhimu hivyo ndivyo atleast kiwango na matokeo yalivyokuwa yakionyesha. Real walikuwa kwenye kiwango cha kawaida sana kwenye ligi wakikosa nguvu na muamko. Kama mlengo ulikuwa ni UCL, basi approach haikuwa sahihi, nguvu nyingi zilitumika mwanzoni na wakati wakielekea mwisho ndivyo nguvu ilivyopungua. Kiwango walichoonyesha kwenye mechi dhidi ya Manchester United na Galatasary kilikuwa cha wastani, aibu ikawakumba kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali dhidi ya Dortmund waliocheza kitimu dhidi ya Madrid waliokuwa wakicheza kibinafsi

NUSU FAINALI 3 ZA CHAMPIONS LEAGUE HAYAKUWA MAFANIKIO NDANI YA MADRID

Nguvu ya Mourinho ilianza kufifia mwaka uliopita, tabia yake ilianza kuchosha na kutambua kwake kwamba msimu huu utakuwa wa mwisho kwake ilizidi kufanya hali kuwa mbaya. Alianzisha vita ambazo zilikuwa ngumu kwake kushinda na mwishowe wake zikaleta mgawanyiko kwa wachezaji na yeye mwenyewe.

Kama hii ilikuwa ndio plan yake ya kulazimisha kuondoka Madrid anaweza akawa amefanikiwa. Timu yake ilikuwa imesambaratika msimu mzima na anaiacha klabu hiyo kwenye hali mbaya. Ndio kuna wachezaji wa kiwango cha dunia kwenye timu hii ya sasa, lakini inahitaji kuundwa upya iwe kitimu zaidi. Kuondoka kwa Mourinho ni jambo zuri kwa pande zote

Kipigo cha Copa Del Rey kimeonyesha kwa picha safi nini kilikuwa tatizo msimu huu na Mourinho ndio mtu wa kulaumiwa. Ataondoka Madrid mwishoni mwa msimu huu, na mabaya yake yamemfanya kuonekana amefeli kufanya kile alicholetwa kufanya ndani ya Madrid. Jukumu kubwa lilikuwa kushinda ubingwa wa Champions League ambao ameshindwa, nusu fainali 3 zinaweza zikawa rekodi nzuri kwa timu nyingine lakini sio Madrid.

Kombe moja la ligi ndani ya miaka 3 na moja la Copa Del Rey ni mafanikio kidogo kwa kocha wa aina yake aliyepewa matumaini makubwa kutokana na kauli zake mwenyewe. Mourinho ni kocha anayejijali yeye zaidi kuliko timu yake, napenda kuwa juu ya klabu - hii inatajwa kuwa sababu mojawapo iliyomnyima kazi Manchester United. Anakosa ujuzi au hali ya kujtaka kujenga timu kwa malengo ya muda mrefu. Hili ndio limemwangusha ndani ya Madrid.
BARCELONA

Ukweli ni kwamba sababu nyingine kuu iliyomleta Mourinho Bernabeu ilikuwa ni kuuvunja utawala wa Barcelona. Alijaribu lakini hali imerudi vilevile sasa hivi wamerudi kwenye kivuli cha wapinzani wao. Alipowasili Santiago Bernabeu alikumbana na kipigo kibaya cha 5-0 na matokeo yake yake mbinu za mchezo wa Mourinho zikabadilika ndani ya Madrid.

Mbinu zake za kucheza dhidi ya Barcelona zilibadilika kabisa na badala ya kufanya mabadiliko kadhaa kwenye timu yake, alikiri kwamba timu yake ni haiwezi Barca na njia pekee ya kucheza dhidi yao na kuwashinda ilikuwa kwa mbinu chafu za vurugu na udanganyifu.Ikiwa tu angeweza kuiendeleza timu yake kwa mfano wa Dortmund na Bayern Munich labda tayari angeweza kuumaliza utawala wa Barcelona kwa kupata mafanikio zaidi hata kwa kubeba kombe la ulaya.
Baada ya majaribio kama 10 kwa mbinu zake Mourinho akaanza kufanikiwa lakini alikuwa ameshachelewa. Barca walionyesha kuwa na mentallity na imani kwenye aina ya mchezo wao na kuwa na mchezaji aina ya Messi waliweza kufanya visivyowezekana pale ilipohitajika. Pamoja na vita ya umalaika vs ushetani baina ya Mourinho dhidi ya Guardiola uliifanya El Classico izidi kuandamwa na vituko, lakini mwisho wa siku Guardiola alimshinda mpinzani wake.

Vita hii ilimfanya Mourinho aonekane mkorofi mwenye mbinu chafu hata ushindi wake ulikuwa wenye malalamiko. Huyu hakuwa kocha mwenye heshima bali mwenye wivu na majivuno. Mourinho aliwasili Santiago Bernabeu akiwa bingwa wa ulaya kama ilivyokuwa wakati akiwasili Chelsea ingawa muda huu alikutana na kiboko yake ambaye hakumpata England.

Alidhalilishwa na Guardiola, aliyekataa kucheza mchezo alioutaka Mourinho. Hivyo ikazaliwa vita ya class vs fashion kati yao. Katika miaka iliyopita Mourinho alionekana kama kocha kijana mnadhifu mwenye kuvaa Armain Suit lakini bado Guardiola alimshinda hata kwenye vita hiyo. Ukweli ni kwamba Barcelona na Guardiola walionyesha dhahiri ya ubovu wa Mourinho.

VITA BINAFSI MBELE YA MASLAHI

Vita ya Mourinho dhidi ya Barcelona, ilipelekewa na mreno huyo kunyimwa kazi mwaka 2008, alisahau kuweka umakini wake kwenye klabu yake aliyoifundisha kwa miaka 3. Vita yake na Barcelona haikuharibu sifa yake binafsi bali pia na ile ya Madrid.

Unaweza ukajaribu kubisha kwa namna alivyoileta uimara kwenye ambao haukuwepo miaka mingi iliyopita, lakini Pellegrini angeweza kufanikiwa zaidi ikiwa angepewa nafasi ya kuendelea kuwa kocha baada ya msimu wake aliomaliza na pointi 96. Pia Pellegrini asingeweza kusababisha migongano na matatizo kwa wachezaji na klabu kwa ujumla.

Ndio maana haikushangaza kuona wachezaji wake wenyewe wakikosana nae - pia haikushangaza kuona wale wachezaji wanaoijua Madrid haswa kiundani walianza kutofautiana nae. Wachezaji ambao tayari walishakuwa na medali za ubingwa wa dunia waliambiwa wacheze mchezo ambao hawakuupenda ili kuweza kuwashinda Barcelona. Haikuwa kama ilivyokuwa kwenye vilabu alivyopitia huko nyuma ambapo aliweza kuwashawishi kuamini kwenye mbinu zake. Kwa sababu tofauti na Porto, Chelsea na Inter, wachezaji wa Madrid tayari walishakuwa washindi. Na baadhi ya wachezaji wa kihispania walikuwa kwenye timu ambayo inasifika kwa kucheza soka safi kuliko timu zote ulimwenguni. 

Kwenye macho yao waliona mbinu za Mourinho zilikuwa zinatofautiana na utamaduni wa Spain na ule wa Madrid. Ugomvi wake na Ramos na Casillas ulikuwa kielelezo tosha. Alipoteza imani ya wachezaji muhimu ndani ya timu, matamanio ya Mourinho yalikuwa kuwadhibiti wachezaji hao ili kuweza kutawala vizuri. Lakini hili ndio likazidisha tatizo, wachezaji hawa haswa Casillas alikuwa mkubwa na mwenye umuhimu ndani ya klabu kuliko Mourinho. Kama ingetakiwa mmoja aondoke baina yao basi Casillas angebaki.

Ndio mwanzoni alipewa rungu na akaweza kumuondoa Raul, lakini kadri siku zilizovyokuwa zikienda ndivyo alivyozidi kugundua Casillas ni kizingiti kikubwa katika utawala wake - na hii ni moja ya sababu zilizomuangusha Mourinho ndani ya Madrid.

Ingekuwa Mourinho angeweza kumtumia vizuri kipa basi angeweza kujiletea mafanikio binafsi na ya timu lakini badala yake akaamua kuwa na vita nae . Ukosefu wa umoja na ushirikiano ndani ya kikosi ndio sabau kuu ya anguko la Madrid msimu huu na mtu wa kumlaumu ni Mourinho mwenyewe.
Sio "Special One" tena

Mwanaume huyu aliyewasili mwaka 2010 akiwa bingwa wa ulaya, The Special One anaondoka Madrid akiwa amefeli na chini ya kivuli cha kocha aliyefanikiwa zaidi kwenye kipindi cha miaka 10 iliyopita. Swali ni - je tumeshaona ubora wote wa Mourinho? Makocha kama Guardiola na Klopp wanaonekana kuwa makocha wa kisasa zaidi wenye kujiheshimu. Tunashuhudia kizazi cha makocha wapya na nina mashaka kwamba Mourinho atapata mafanikio yoyote yatakayokaribia mafanikio aliyoyapata muongo mmoja uliopita.

Ikiwa atarudi Chelsea kama inavyotegemewa itadhihirika kwamba amefeli kwenye levo ya juu, ndio alikuwa bora kwa miaka kadhaa iliyopita lakini amefeli ndani ya Madrid na kuvionyesha vilabu kama United, Barcelona na Bayern Munich kwamba hafai kuwa kiongozi ndani ya timu zao. Hata Man City ambapo wafanya maamuzi ni watumishi wa zamani wa Barca inaonekana hawataki kujihusisha nae. Ukweli ni kwamba Madrid imempotezea sifa yake kama kocha bora kutokana na kufeli kufanya kazi kama ilivyopaswa.


Wednesday, May 22, 2013

VIBONZO VYA LEO



NGASSA ASAJILIWA BILA KUPIMWA, FEDHA ZA EL MERREIKH ZIMEMPONZA, NI HALALI KUCHEZA YANGA


LAZIMA tuamini kwamba aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngassa amejiunga na Yanga na ataichezea timu hiyo michuano yoyote itakayoshiriki kuanzia sasa.
Ngassa amejiunga na Yanga huku kukiwa na vitimbi kadhaa vilivyotokea tangu anaondoka katika timu hiyo miaka michache iliyopita, wakati huo Yanga ilikuwa chini ya Mwenyekiti, Iman Madega.
Winga huyo aliondoka Yanga na kujiunga na Azam FC katika usajili ambao haukutarajiwa na wengi kutokana na mapenzi ya Ngassa kwa Yanga, bila shaka fedha iliongea. Azam ililipa zaidi ya Sh. 90 milioni ili kumnasa mchezaji huyo.

Mwaka jana katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, akiwa anaichezea Azam, Ngassa baada ya kuifungia bao muhimu timu hiyo katika nusu fainali, alikwenda kwenye kibendera cha kona na kukibusu. Kibendera hicho kina rangi ya kijani na njano, rangi hizo zinatumiwa na Yanga.
Hiyo ilionekana kama ishara ya kuitukuza Yanga na kuidharau Azam timu inamlipa mshahara na posho nyingine, kwa kifupi ni mwajiri wake. Azam haikupendezwa na hali hiyo, kabla ya kuanza kwa msimu huu ikatangaza kumtoa kwa mkopo kwa Simba.
Wakati Azam inatangaza kumtoa kwa mkopo au kumuuza Ngassa, nilijua fika kwamba Yanga inaweza kutia mkono wake hivyo ikatazama mazingira ya kumkwamisha kurejea katika klabu yake na kuhakikisha anakwenda Simba.
Alipokuwa Simba, Ngassa alipata ‘deal’ la kujiunga na klabu ya El Merreikh ya Sudan, viongozi wa Simba walizungumza na El Merreikh bila ya kupata ridhaa ya Ngassa. Mwisho wake mchezaji alikataa kujiungana timu hiyo ya Sudan.
Azam ambayo nayo ingefaidika kama Ngassa angejiunga na El Merreikh, ni wazi haikupendezwa na hali hiyo ya Ngassa kukataa kuiunga na klabu hiyo. Mkakati ukapangwa.

Lakini wakati haya yakitokea siku za nyuma hebu tutazame namna Ngassa alivyosajiliwa na Yanga huku kukiwa na mambo kadhaa ya kushangaza;

NGASSA HAJAPIMWA AFYA

Kama ilivyo kawaida ya timu nyingi za Tanzania, safari hii Ngassa amesajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili bila ya kupimwa afya…!
Jambo hili la wachezaji kusajiliwa bila kupimwa afya sasa linaonekana la kawaida ambalo klabu zimerithi utaratibu huo toka zamani, Dunia imebadilika lakini viongozi wengi wa soka hapa nchini hawatazami hili.
Kwa mfano Ngassa anaweza kuwa na matatizo ya afya katika viungo vyake vya mwili ambavyo baadaye anaweza kuigharimu klabu kumgharamia matibabu kwa mfano matatizo ya goti.
Matibabu hayo yanaweza kuigharimu klabu kiasi kikubwa cha fedha ambacho kingeweza kufidiwa wakati wa usajili wake.

FEDHA ZA EL MERREIKH ZAMPONZA
Kama inavyodaiwa kwamba, Ngassa amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia Simba, baada ya deal la kumpeleka El Merreikh kushindikana, Simba na Azam ziliamua kupeleka mkataba huo wa Simba kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kuusajili ili Ngassa asiwe na uamuzi mwingine atakapoamua timu ya kujiunga nayo mkataba wake utakapoisha Azam.  
Lengo la Azam na Simba lilikuwa ni kuona Ngassa hajiungi na Yanga na anaichezea Simba msimu ujao pia, HATA KAMA BILA RIDHAA YAKE.
Kwa kuwa Ngassa anafahamu anachofanya na anaheshimu maamuzi yake, aliamua kusaini kuichezea Yanga ili acheze soka kwa amani zaidi.
Usajili wa Ngassa kwa Simba (kama kweli alisaini) ulikuwa wa kama ‘kishika uchumba’ ili awe na uhakika na ahadi ya kusajiliwa na klabu hiyo, hivyo baadaye angeweza kuwa na maamuzi mengine kama alivyofanya sasa.

NGASSA NI HALALI YANGA
Kama kweli TFF itafuata hatua kwa hatua katika kile kinachoitwa mkataba wake na Simba, Ngassa ataichezea Yanga msimu ujao, kwani kuna vitu vingi vilifanyika katika mkataba huo bila ridhaa ya mchezaji.
Jambo hili linaweza kuwa kama la usajili wa Kelvin Yondani na Mbuyu Twite.