Search This Blog

Thursday, May 23, 2013

DAVID MOYES - KWENYE MKATABA WA MIAKA 6 NA UNITED - ASIPOSHINDA KOMBE NDANI YA MISIMU 2 ATAFUNGULIWA MLANGO WA KUTOKEA


David Moyes, mmoja wa makocha bora kabisa katika ligi kuu ya England ameamua kuondoka Everton baada ya miaka 11 akiwa na klabu ya Merseyside na kuhamia Manchester United kwa mkataba wa miaka 6. Tatizo ambalo msotish huyo atakalokumbana nalo kwa mabingwa hao wapya wa England ni kwamba asiposhinda kombe lolote ndani ya misimu miwili basi atakumbana na panga la kufukuzwa.

Moyes alianza kufundisha soka akiwa na klabu ya Preston North End mwaka 1998, kwenye klabu ambayo alimalizia maisha yake ya kucheza soka. Moyes aliiwezesha Preston kuepuka kushuka kutoka daraja kutoka daraja la pili, then msimu uliofuatia akawaongoza Preston kucheza playoffs, lakini wakafungwa. Mscotland huyo alirudi tena msimu uliofuata na kushinda ubingwa, na kuipeleka klabu hiyo ligi ya daraja la kwanza. Mwaka 2001, Preston walifungwa kwenye playoffs na kufeli kupanda daraja kucheza ligi kuu, lakini mafanikio ya Moyes yalionekana, na akasajiliwa Everton mwaka 2002. 

March 14th 2002, Moyes alitambulishwa kama kocha mpya wa Everton. Alianza vizuri na ushindi wa 2-1 dhidi ya Fulham. Klabu hiyo Merseyside ikamaliza msimu kwenye nafasi ya 7 katika msimu wake wa kwanza. Aliiongoza timu kwa kuwatimua akina David Ginola na kuwaleta wachezaji akina Joseph Yobo na Richard Wright. Ingawa hakuwa na msimu mzuri wa pili akimaliza nafasi ya 17 na pointi 39, kiasi kidogo cha pointi kuwahi kutokea kwenye historia ya klabu hiyo, lakini Moyes aliweza kuepuka kuishusha daraja klabu hiyo.
Miaka iliyofuatia alishuka na kupanda, mwaka 2004 alimpoteza Wayne Rooney kwa Manchester United, lakini pamoja na kumpoteza mmoja wachezaji wake muhimu, Everton wakaenda kumaliza msimu kwenye nafasi ya nne na kufuzu kucheza Champions League. Kuonja ladha ya soka la ulaya kukawapanda wachezaji kichwani na kwa mara nyingine tena Everton wakawa wanapigania kutoshuka daraja. Klabu ikamaliza kwenye nafasi ya 11, lakini msimu wa 2005-06 wakamaliza 6th position, hivyo soka la mashindano ya UEFA Cup likahamia Goodison Park.

Mwaka 2007 ulikuwa msimu ambao Moyes aliigeuza Everton kuwa moja vilabu tishio kwenye nafasi za kucheza ulaya na akafanikiwa kumsaini Leighton Baines kwa £6m na Phil Jagielka kwa £4m. Na mwaka 2009, alivunja rekodi ya ada ya usajili ya klabu kwa kumsaini mbelgiji Marouane Fellaini kwa £15m na wakafanikiwa kufika fainali ya FA Cup ambapo wakafungwa 2-1 na Chelsea.
Habari kubwa ilikuja April 21st 2010 ambapo Sir Alex Ferguson alipotangaza kwamba anamtaka maneja wa Everton Moyes awe mbadala wake atakapostaafu. Lakini May 14th 2010, Moyes alielezea matamanio yake ya kutaka kuifundisha klabu ya nyumbani kwao ya Celtic,lakini Neil Lennon akateuliwa badala yake. Kwa mshtuko zaidi  May 8th 2013, Sir Alex aliamua kustaafu na David Moyes akapewa mikoba ya Fergie akisaini mkataba wa miaka 6 na Red Devils, na hapa ndipo wasiwasi wangu ulipo.

Sir Alex amekuwa kocha wa soka kwa miaka 39 na 26 kati ya hiyo ameitumia katika kuifundisha Manchester United. Alifanikiwa kushinda vikombe 49, na 38 kati ya vikombe hivyo ameshinda akiwa na United. Aliwaambia waandishi wa habari kwamba David Moyes alikuwa ndio chaguo lake la asili kabisa lakini Moyes alisema kwamba hakuwa amepanga kuondoka Everton na asingeweza kuikataa Manchester United. 
Akiwa anatajwa kama kocha bora wa muda wote, Ferguson anaacha viatu vikubwa kwa Moyes, lakini je yupo tayari kwa changamoto hiyo. Muda pekee ndio utaongea.

Kuleta kombe kwenye kabati la vikombe Old Trafford ndio kitakuwa kitu muhimu kwake katika kupata sapoti ya mashabiki wa United, aidha kubeba tena ubingwa wa EPL au kushinda Champions League, Moyes atategemewa kubeba kombe mapema, ikizingatiwa kikosi alichoachiwa cha sasa, kilicho na mchanganyiko wa vijana na wachezaji wenye uzoefu, pia tayari amehakikishiwa mzigo wa usajili ambao kuna tetesi anataka kuutumia katika kuwasajili Baines na Fellaini.

Kushinda makombe 38 ni kitu kikubwa sana kwake, lakini mashabiki wa klabu watahisi vibaya ikiwa ndani ya kipindi cha miaka 2 atashindwa kuleta ubingwa Old Trafford na anaweza akaonyeshwa mlango wa kutokea. Manchester United na mashabiki wao hawajozea kumaliza msimu bila kombe. Hii inaweza kuwa safari nyingine ndefu yenye mafanikio kwa Moyes au inaweza kuwa mwanzo wa anguko lake. Vyovyote itakavyokuwa mashabiki wengi wa United wana furaha kwamba meneja wa Everton amekuwa mrithi wa Sir Alex Ferguson.

No comments:

Post a Comment