Search This Blog

Saturday, March 15, 2014

HIVI NDIVYO MTIBWA WALIVYOIVUTA SHATI YANGA MOROGORO LEO


Kikosi cha Timu ya Soka ya Mtibwa Sugar Iliyoanza Leo Dhidi Ya  Yanga.
Waliosimama Kutoka Kushoto : Salum Mbonde,Dickson Daud,Abdalah Juma, Ally Shomary, Shaban Nditi,Walioinama Kutoka Kushoto : Vicent Barnabas, Said Mkopi,ShabanKisiga,Husein Ramadhan, Paul Ngalema 
Kikosi cha Timu ya  Yanga Kilichoanza Leo : Kutoka Kushoto Didier Kavumbangu, Haroub Canavaro,Khamis Kiiza,Oscar Joshua,Frank Domayo,Simon Msuva, Juma Abdul,Nizar Khalifan,Mbeleni Juma Kaseja. 


Ligi Kuu Tanzania Bara Imendelea Leo Ambapo Katiak uwanja wa Jamuhuri Mkoani Morogoro Kulikuwa na Mchezo Mkali Dhidi ya Wenyeji Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani Mkoani Morogogo Dhidi ya Mabingwa Watetezi  Yanga ya Dar es Salaam . Katika Mchezo Huo Hadi Dakika 90 za Mchezo Zinamalizika Matokeo Timu Hizo Zmetoka sare ya Bila Kufungana.Mchezo Ulikuwa Mkali na wakukamiana Pamoja na Hali ya Uwanja Kutokuwa nzuri kutoka na Mvua Zianzoendelea Kunyesha Mkoani Hapa.Timu ya   Yanga walitengeneza Nafasi Nyingi za Kufunga lakini walishindwa Kuzitumia .Wachezaji Emanuel Okwi na Didie Kavumbangu walipata nafasi za kufunga katika dakika ya 80 na 88 lakini awalishindwa kufunga, Yanga walifanya Mabadiliko katika Dakika ya 65 Alitoka Nizar Khalifan  na Kuingia Said Dilunga,Dk78 Alitoka Khamis Kiiza na Kuingia  Husein Javu. 
Mtibwa Sugar Walipata Pigo katika Dakika ya 70 Ambapo Mshambuliaji Wao Abdalah Juma  Alionyeshwa Kadi Nyekundu kwa Kumchezea Rafu mbaya.


 Mashabiki wa Timu ya  Yanga waliojitokeza kwa Wingi katika Uwanja wa Jamuhuri Mkoani morogoro
Benchi la Timu ya Soka ya Mtibwa ya Morogoro  Lilkiongzwa na Kocha wa Timu Hiyo  Meky Mexime Wa Kwanza Kushoto..
Makocha wa  Yanga 
Mashabiki waliojitokeza kwa Wingi Katika Uwanja w Jamhuri Mkaoni Morogoro Leo Katika Mcheza Kati ya Yanga Dhidi ya Mtibwa Sugar 
Mshambuliaji wa Timu ya  Yanga Emanuel Okwi akitafuta Mbinu za Kufunga katika Lango la Timu ya Mtibwa Sugar ya Mkoani Morogoro Katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Jamuhuri Mkaoni Morogoro.
Moja ya Purukushani katika Lango la Timu ya  Yanga Katika Mchezo Uliochezwa katika Uwanja wa Jamuhuri Mkaoni Morogoro  
Mchezaji wa  Yanga Simon Msuva Akitafuta Mbinu za Kumtoka Beki wa Timu ya Mtibwa Sugar Paul Ngalema 


LIVE SCORE: YANGA SC 0 - 0 MTIBWA SUGAR - AZAM FC 4 - 0 COASTAL UNION FULL TIME


FT: Azam 4 Coastal Union 0.

90(+5)’ Azam 4 Coastal 0.
 Mpira umemalizika, Mtibwa Sugar 0 - 0 Young Africans

92(+5)’ Kipa wa Mtibwa kakaa chini anafunga kamba za viatu
Zimeongezwa dakika 5
90’ Mtibwa 0 Yanga 0
81’ Didier Kavumbagu wa Yanga anapoteza nafasi ya wazi.

80’ Mtibwa 0 Yanga 0

75’ Okwi kaponea chupuchupu kupewa kadi nyekundu baada ya kubutua mpira kupinga maamuzi ya refa huku akiwa tayari ana kadi ya njano.

73’ Mtibwa 0 Yanga 0

64’ John Bocco anaipatia Azam bao la tatu.

67’ Emanuel Okwi wa Yanga anaoneshwa kadi ya njano

60’ Yanga sub: Nizar Khalifan anatoka, Hassan Dilunga anaingia. 

56’ Abdallah Juma wa Mtibwa anaoneshwa kadi nyekundu.
Yanga 0 - 0 Mtibwa
Kipindi cha pili kinaanza Chamazi na Jamhuri
HT: Mtibwa Sugar 0 - 0 Yanga, Azam 2 - 0 Coastal Union 

45 Yanga 0 - 0 Mtibwa
Kipre Tchetche azifumania tena nyavu za Coastal Union Dakika ya 38

Dakika ya 34 Azam 1 - 0 Coastal - Yanga na Mtibwa milango bado migumu.

30 Azam 1 - 0 Coastal


31’ Mtibwa 0 Yanga 0


Yanga 0 - 0 Mtibwa Sugar mpira ni dakika ya 25


Kipre Tchetche anaifungia Azam FC bao la kwanza dakika ya 23

RAGE FIKIRIA AJENDA ZA WANACHAMA MKUTANO WA KESHO, MATATIZO YA SIMBA YATATULIWE NA WANASIMBA WENYEWE!!


Mpira ni mchezo unaogusa hisia za watu wengi zaidi Duniani. Ipo michezo mingi, lakini unapozungumzia soka unagusa mamilioni ya watu kuliko mchezo wowote unaoujua.

Wapo mashabiki wengi ambao kila muda wanajadili soka. Hata hapa Tanzania, ukipita kwenye vijiwe mbalimbali, baa, ofisi za watu na maeneo mengi ambayo watu wanakutana kupiga gumzo, hawaachi kuzungumzia kabumbu.

Nchini Tanzania, klabu za Simba na Yanga zina wapenzi wengi zaidi ya klabu yoyote. Unapotaja klabu hizi, unagusa hisia za Watanzania wengi.

Ndio maana kwenye mechi zao, ni rahisi kwa watu kuzirai au kupoteza fahamu pale matokeo mabaya yanapoikumba timu moja.
Kama inafika wakati watu wanapoteza fahamu baada ya timu zao kufungwa na wengine kuamua kujiua, utagundua kuwa timu hizi zina mvuto mkubwa kwa mashabiki wake.

Kama mtu anaweza kukumbwa na matatizo hayo ya kiafya kwasababu timu imefungwa, lazima uwe makini unapopewa dhamana ya kuogoza klabu hizi.
Kuwa kiongozi wa Simba na Yanga, kunahitaji uwe na uelewe mkubwa  wa kutambua kuwa nyuma yako kuna watu wengi wenye mapenzi ya dhati na timu zao.

Unapoleta mchezo na mambo muhimu yanayohusu klabu, unawaumiza watu bila sababu ya msingi.
Nirudi kwenye hoja yangu ya msingi iliyonisukuma kuandika makala hii.

Kesho machi 16 klabu ya Simba  itafanya mkutano wa wanachama wake kwa ajili ya kuifanyia marekebisho Katiba yao.
Kuelekea katika mkutano huo, tayari shirikisho la soka la Tanzania, TFF limewatakia kila la heri Simba katika mkutano huo ambao ni muhimu katika kuhakikisha klabu yao inapiga hatua katika maendeleo ya mpira wa miguu na ustawi wake kwa ujumla.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi katika taarifa yake jana 
aliwakumbusha viongozi na wanachama wa klabu ya Simba kuwa marekebisho hayo ni lazima yafanyike kwa kuzingatia Katiba, Kanuni na maelekezo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Afrika (CAF) na Tanzania (TFF).

Aidha taarifa yake ilisema kuwa waraka wa TFF kwa wanachama wake wa Februari 7 mwaka huu uzingatiwe kikamilifu katika marekebisho hayo.
Zaidi Malinzi aliwakumbusha wanachama wa Simba kuzingatia  umuhimu wa kudumisha amani na maelewano katika klabu yao.
Mkutano wa kesho kwa mujibu wa mwenyekiti wa Simba SC, Ismail  Aden Rage utakuwa na ajenda moja ya marekebisho ya katiba.

Lakini tayari yametokea malumbano ambapo wiki hii viongozi  wa matawi ya Simba, walipinga maamuzi ya Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo kuitisha mkutano mkuu wa dharura Jumapili ukiwa na ajenda moja tu badala yake wametaka kuwe na ajenda tano.
Viongozi hao walikutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari (MAELEZO) na kumtaka Rage na kamati yake ya utendaji waongeze ajenda nyingine ili mkutano huo uwe na ajenda tano.

Walisema wanataka kujua uwanja wao  wa kisasa unajengwa lini, mauzo ya jezi, kesi zilizopo mahakamani dhidi ya Simba,  pesa za mauzo ya wachezaji wao na uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti baada ya kujiuluzu kwa Geofrey Nyange.
Mwanachama machachari wa Simba Bi. Chuma Suleiman alienda mbali na kueleza kuwa pasipo kuyafanya hayo, wanaamini kutakuwa na vurugu katika mkutano huo.

Ukifuatalia suala hili, utagundua kuwa Wanachama wana mengi moyoni mwao ambayo wanataka yajadiliwe katika mkutano huo na kujua hatima ya klabu yao.
Rage akiwa mwenyekiti anayo mamlaka kikatiba ya kupanga ajenda za mkutano mkuu wa wanachama.
Kwasababu katiba inamruhusu, basi hakuna jinsi ya kumpinga kama ameamua kuwepo kwa ajenda moja tu katika mkutano.
Katika maisha ya kawaida, kuna wakati unatakiwa kuwa makini unapofanya maamuzi. Sipingi hata kidogo kwa Rage kuwa na ajenda moja ya mabadiliko ya katiba.
Lakini ukitazama kiuhalisia, bado utagundua kuwa Simba wanayo matatizo mengi ya kujadili katika mkutano huo.
Wanachama wanazo ajenda za kuhoji kwa viongozi wao. Wanataka kujua mambo mengi, hivyo wanaamini mkutano huo ndio wenye nguvu kufanya maamuzi.

Nadhani ipo haja kwa kamati ya utendaji chini ya Rage kufikiria upya na kuyaingiza maombi ya wanachama wake.
Mwanzoni mwa makala hii nilisema, kuongoza Simba au Yanga unagusa hisia za watu wengi, hivyo lazima uwe msikivu.
Rage inabidi akae chini na kutathimini, kama atagundua wayatakayo wanachama ni kwa ajili ya faida ya timu,  basi ayaweke katika mkutano huo. Lakini kama anaona hayana maana kujadiliwa kwasasa basi aendelee na ajenda moja tu.

Wanachama ndio waliomuweka madarakani. Wao ndio wenye klabu, wanapohitaji jambo fulani lijadiliwe basi wafikiriwe.
Siandiki haya kwa kujaribu kumshinikiza Rage aongeza ajenda, lakini najaribu kuwaza endapo kutatokeoa vurugu kwenye mkutanao huo kwasababu tu ajenda za wanachama zimekataliwa kujadiliwa, nani atabeba msalaba wa lawama?.

Bado nasisitiza jambo hili, kuongoza Simba na Yanga unagusa maisha ya watanzania wengi. Hakuna tatizo lisilokuwa na chanzo.
Hata kufanya vibaya kwa timu kunachangiwa na viongozi. Jaribu kuwaza mfumo unaotumika kusajili wachezaji kama unaridhisha katika klabu hizi kubwa.
Watu wachache wanakaa chini na kutafuta wachezaji, na wakati mwingine wanasahau hata kupitia ripoti za mabenchi ya ufundi.
Kupigana vikumbo kwa viongozi, kunyang`anyana wachezaji ndio tabia yao. Lakini wanapogundua kuwa walisajili vibaya na benchi la ufundi limeshindwa kuwapa makali `magalasa` wao, basi makocha wanabebeshwa mzigo wa lawama.
Mwisho wa siku timu inacheza vibaya na kuwajeruhi mashabiki moyoni. Watu wanazirai uwanjani kwasababu ya makosa yaliyofanywa na watu fulani.

Hakika baadhi ya viongozi hawawezi kukwepa lawama kwa haya, ifike wakati wawe na moyo wa huruma kwa mashabiki wao. Wachezaji hawalipwi mishahara na posho kwa wakati. Unategemea wacheze mpira gani kama wana njaa. Lakini kuna watu wanaohusika na kukwepa majukumu yao.
Nawaasa viongozi wa Simba wawape nafasi wanachama wao kujadili mambo ya klabu. Nafahamu kuwa uhuru wa kutoa mawazo hauzuiliwi hata kikatiba. Katiba inatoa nafasi kwa kila mtu kutoa mawazo yake.
Wape watu nafasi ya kuzungumza, pima uzito wa hoja zao, chukua mazuri achana na pumba.

Kikubwa kwa Rage ni kutumia busara ya utu uzima ili kuepuka mgogoro usiokuwa wa lazima.
Katika utawala wa kidemokrasia, watu wana nafasi kubwa ya kujadili mambo yao, usijaribu kuwanyima fursa.
Migorogoro haina tija kwa klabu. Watu wamechoka kusikia migogoro. Wachezaji wanaathiriwa nayo hata kama si moja kwa moja.

Viongozi mnapolumbana na wanachama kwa masuala fulani, mnatoa mwanya kwa wapinzani wenu kuwapiga bao.
Kila la heri wana Simba katika mkutanao wenu hapo kesho. Tafuteni mwarobaini wa matatizo yenu.

Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
0712461976

Friday, March 14, 2014

TAARIFA RASMI YA ULI HOUNESS KUJIUZULU NAFASI YA URAISI WA FC BAYERN MUNICH.


BODI YA LIGI NA TFF NDANI YA BIFU ZITO: NI BAADA YA BODI HIYO KUKATAA KUFANYIWA UKAGUZI WA MATUMIZI YAO YA FEDHA.

Taarifa za uhakika ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba kuna hali ya kutoelewana kati ya TFF na bodi ya ligi.

Chanzo cha kutokuwepo kwa maelewano mazuri baina ya uongozi wa bodi na TFF ni kutokana na viongozi wa bodi ya ligi kukataa kukaguliwa mahesabu ya matumizi yao ya fedha.

Inasemekana kwamba uongozi wa Jamal Malinzi ulivyoingia madarakani uliwasaliana na bodi ya ligi ukiwaeleza kwamba ungewatumia mkaguzi wa mahesabu bodi ya ligi kwa ajili ya kukagua matumizi yao.

Lakini katika hali ya kushangaza bila sababu ya msingi na yenye mashiko uongozi wa bodi ya ligi ulikataa kumpokea mkaguzi wa mahesabu, hali iliyopelekea kutokuelewana baina ya TFF na bodi hiyo.

HAYA NDIO MABAO 50 BORA KABISA KATIKA KIPINDI CHOTE ARSENE WENGER ALICHOIFUNDISHA ARSENAL

Hii ni listi ya mabao 50 bora ya klabu ya Arsenal katika kipindi chote ilichofundishwa na kocha Arsene Wenger. Video hii imetengenezwa na akaunti rasmi ya Arsenal ya mtandao wa Youtube.

VIONGOZI WA YANGA WAONYESHA MFANO WA KUIGWA KWENYE MATUMIZI YA FEDHA ZA KLABU

Uongozi wa klabu bingwa ya Tanzania bara Dar Young Africans umeonyesha mfano wa kuigwa kwa viongozi wengine wa soka nchini siku moja baada ya kurudi kutoka Misri walipoenda na timu kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha kuaminika kutoka ndani ya  klabu hiyo ni kwamba viongozi wa msafara wa Yanga chini ya mkuu wa msafara huyo makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga umerudisha kiasi cha millioni 39 klabuni kutoka kwenye fedha walizopewa kwa ajili ya matumizi kwenye safari yao nchini Misri.

"Eeh bwana safari hii kweli tuna viongozi wenye nia ya dhati ya kuiongoza vizuri Yanga, Sanga na viongozi wenzie walioenda Misri walipewa fungu la bajeti kwa ajili ya matumizi yote ya klabu nchini Misri, lile fungu lilikuwa litumike lote, lakini tofauti na viongozi wote wa misafara waliopita, Sanga na wenzake wameweza kurudisha millioni 39 kutoka katika fedha walizopewa. Haijawahi kutokea kwenye klabu hii kwa kweli, huko nyuma kitendo kama hichi hakikuwahi kutokea, hapa klabuni kila aliyesikia kuhusu hilo jambo ameshutushwa.
"Zile fedha zilikuwa tayari zimeshatolewa kwa matumizi hivyo hata kama wangeamua kuzila hakuna ambaye angeulizia, hawa jamaa ni waadilifu na wana mapenzi ya kweli na klabu," kilisema chanzo hicho cha habari.

RAIS WA BAYERN MUNICH AJIUZULU BAADA YA KUHUKUMIWA KWENDA JELA


Raisi wa klabu bingwa ya Bayern Munich Uli Hoeness amejiuzulu kwenye nafasi yake ya uraisi wa klabu hiyo na amesema ameamua kutokata rufaa dhidi ya hukumu aliyopewa.

Hoeness, mmoja watu wazito katika soka nchini Ujerumani, alihukumiwa kwenda jela miaka mitatu na nusu baada ya kukutwa na hatia ya kukwepa kodi .

Hoeness alisema kupitia taarifa fupi iliyochapishwa kwenye mtandao wa klabu ya Bayern kwamba amefikia maamuzi hayo baada ya kuzungumza na familia yake na akawaelekeza wanasheria wake wasikate rufaa.

MACHAFUKO YA BRAZIL YAIABISHA FIFA.


MO FARAH ATETEA UAMUZI WAKE.


KAULI YA LEO: ''MOURINHO ANAONGEA SANA'' - YAYA TOURE


MKALI NANI: NANI MWENYE UWEZO ZAIDI KATI EDIBILY LUNYAMILA NA MRISHO NGASSA.


MKALI NANI: IPI SAFU KALI YA USHAMBULIAJI KATI YA SUAREZ NA STURRIDGE VS ROONEY NA VAN PERSIE

Kuelekea mchezo wa watani wa England, Manchester United vs Liverpool wikiendi hii - tujadili ipi ni safu kali ya ushambuliaji baina ya Suarez na Sturridge dhidi ya Van Persie na Rooney

KUELEKEA KOMBE LA DUNIA: HILI NDIO GOLI LA HARAKA ZAIDI KUWAHI KUFUNGWA KATIKA FAINALI YA KOMBE LA DUNIA


Ilikuwa ni kwenye sekunde ya 90 ya mchezo ndani ya dimba la Munich Olympiastadion wakati kiungo wa Uholanza  Johan Neeskens alipofunga goli dhidi ya West Germany tarehe 7 July 1974.

Goli hilo linabakia kuwa goli lilofungwa kwa haraka zaidi katika mchezo wa fainali ya kombe la dunia, hata hivyo goli halikuweza kuwasaidia Wadachi kushinda mechi hiyo na kubeba ubingwa.

Wajerumani walirudisha goli kupitia Paul Breitner na Gerd Muller akafunga goli la ushindi kuihakikishia Ujerumani Magharibi ubingwa wa pili wa dunia. 

VAN PERSIE: NINA FURAHA MAN UNITED, NA NINATAKA KUENDELEA KUWA HAPA HATA BAADA YA MKATABA KUISHA."

Mshambuliaji Manchester United Robin van Persie amesema rasmi kwamba anataka kubakia Old Trafford kwa muda mrefu. 
Mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 30 amekanusha kwamba haelewani na kocha David Moyes na imekuwa ikisemekana kwamba angeondoka kwenye timu hiyo kipindi kijacho cha usajili.  
Lakini nahodha wa Uholanzi anasisitiza kwamba anapendelea kubakia United.
"Ukweli ni kwamba nina furaha sana," Alisema. "Nilisaini mkataba wa miaka minne na nina furaha kuendelea kukaa hapa kwa muda mrefu, hata baada ya miaka yangu miwili iliyobaki." 
Pia tetesi zimekuwa zikisema kwamba Van Persie havutiwi na mbinu za ufundishaji za Moyes. 
Lakini akiongea katika interview aliyofanyiwa na United Review, kuelekea mchezo dhidi ya mahasimu wao Liverpool, aliongelea juu ya saula la mbinu za Moyes. 
"Hakuna shaka kwamba ninajifunza mbinu mpya na ninaendelea vizuri chini ya David Moyes," alisema. "Vipindi vya mazoezi tunavyokuwa kuwa navyo ni vizuri mno na ninajifunza vitu vingi kutoka kwenye mazoezi hayo kila siku. 
"Kuna hali nzuri ya kuheshimiana baina yetu na mazingira yetu ya kufanya kazi ni mazuri. Moyes anataka sana kazi iende vizuri na mie ninataka hivyo pia."

PICHA YA SIKU: DANNY MRWANDA KAMA XABI ALONZO!USHAHIDI WA PICHA ZA KUKAMATWA KWA ERIC CANTONA

Mwanasoka wa zamani wa Ufaransa na klabu ya Manchester United Eric Cantona akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kukamatwa baada ya kumfanyia shambulio la mwili mtu mmoja huko London Uingereza.

MIYEYUSHO KUZIPIGA NA MUDDY MATUMLA APRIL 26


Promota Ally Mwazoa katikati akiwatambulisha mabondia Fransic Miyeyusho kushoto na Mohamed Matumla wakati wa kutangaza mpambano wao utakaofanyika April 26 katika ukumbi wa PTA Sabasaba  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Bondia Fransic Miyeyusho kushoto na Mohamed Matumla wakikumbatiana baada ya kukubaliana kuzipiga April 26 katika ukumbi wa PTA Sabasaba picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Fransic Miyeyusho wakitunishiana misuli na Mohamed Matumla wakati wa utambulisho wa mpambano wao mbele ya waandishi wa habari Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe' na Mohamed Matumla 'Snake JR' leo wamesaini mkataba wa kupambana april 26 katika ukumbi wa PTA Sabasaba 

Akizungumzia mpambano huo promota wa mchezo wa masumbwi nchini Ally Mwazoa amesema ameingia nao mkataba mabondia hawo kwa kuwa anajua wanaweza mchezo wa masumbwi na ni mafundi wa mchezo huo najua kuna watu wengi walitamani kudhamini mchezo huo lakini bahati imeniangukia mie

mpambano uho utakaopigwa april 26 katika ukumbi wa pta sabasaba kutakuwa na mapambano mengine makali ya utangulizi ambapo mwana dada Lulu Kayage atamvaana na Halima Ramadhani siku hiyo kwa ajili ya kuhamasisha wanawake wenzao wajitokeze katika mchezo wa masumbwi

baada ya kusaini mkataba huo bondia Miyeyusho alijitamba kuendeleza ubabe katika familia hiyo ambapo alisema atamchakaza kama alivyo mchakaza baba yake mdogo Mbwana Matumla ambaye amecheza nae mara tatu na kupigwa mara mbili ambapo mpambano wa mwisho ulikuwa na shamu shamu nyingi kila upande miyeyeyusho alibuka mshindi kwa point

nae Matumla alijibu mapigo kwa kusema Miyeyusho anamuheshimu kwa kuwa yeyey ni mkubwa kiumri ata hivyo atampa kichapo kikali kama alivyompatia mdogo wake Doi Miyeyusho ambaye mara ya kwaza alipigwa kwa K,O raundi ya pili DDC Keko na mara ya pili pia K,O ya raundi ya pili katika ukumbi uho uho uho wa PTA Sabasaba hivyo siwezi kushusha rekodi yangu kwa kupigwa na miyeyusho akitaka kujua mimi ni mkali zaidi yao amulize pia Nassibu Ramadhani ambaye nilimpatia kipigo kibaya sana na kunifanya ninyakue pikipiki ,            Mwazoa

aliongeza kuwa ulizi na usalama wa mali zako ni wa huwakika hivyo familia nzima mnaweza kuja kushudia mpambano huo wa masumbwi bila shaka 
 
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Thursday, March 13, 2014

ERIC CANTONA ARIPOTIWA KUKAMATWA KWA KUMSHAMBULIA MTU LONDON

Mchezaji wa zamani wa Manchester United Eric Cantona amekatwa jijini London akituhumiwa kufanya shambulio la mwili. 
Mwanasoka huyo wa zamani wa Ufaransa ambaye aligeukia uigizaji wa filamu alikamatwa na polisi kuafuatia ripoti aligombana na na mwanaume mwingine. 
Polisi waliitwa kwenye eneo la tukio Primrose Hill kufuatia ugomvi uliotokea wakati wa chakula cha mchana jana jumatano. 
Msemaji wa polisi wa Metropolitan: “Tuliitwa kwenye eneo la tukio 12.55pm kufuatia ripoti ya shambulio. Maofisa wa polisi walifika eneo la tukio na kumkamata mwanaume mmoja mwenye miaka 40."
Mashabiki kadhaa kupitia Twitter waliripoti kwamba walimuona Cantona jana katika kituo cha polisi huko Primrose Hill.
Cantona, 47, aliichezea United kwa miaka sita 1990s, akiifungia timu hiyo mabao 64.

HATIMAYE RAISI WA BAYERN MUNICH AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 3 KWA KUKWEPA KODI

Rais wa Bayern Munich amehukumiwa kwenda jela kwa kifungo cha miaka mitatu na miezi sita kutokana na kosa la kukwepa kodi.

Uli Hoeness, 62, alikiri kukwepa kodi inayofikia kiasi cha €18.5 million kupitia akaunti zake za benki za siri lakini utetezi wake wa kukiri kosa akidhania ungemsaidia kuepukana na adhabu ya kifungo ulishindwa kumsaidia. 

Mwndesha mashtaka alitaka Hoeness afungwe jela miaka mitano na nusu kwa kutokana na kupatikana na hatia ya kukwepa kodi.

Mwishowe, jaji wa mahakama iliyokuwa ikisikiliza kesi hiyo akaamuru mwanasoka huyo wa zamani wa Ujerumani Magharibi atumikie kifungo cha miaka 3 na miezi sita.

ALEX MGONGOLWA MWENYEKITI MPYA WA KAMATI YA UCHAGUZI YANGA!


BARUA YA YANGA KUOMBA KUANDAMANA TAREHE 17 KUPINGA UCHELEWESHAJI WA MAOMBI YA UJENZI WA KIWANJAGOLI LA 91 KWA UBORA KATIKA KOMBE LA DUNIA - DIEGO MARADONA VS ENGLAND MWAKA 1986

)

NIONAVYO MIMI: MOURINHO NI KOCHA WA SAYARI NYINGINE.


Na Oscar Oscar Jr
 
0789-784858 

Kuna watu wengi sana katika medeni ya soka wanaamini kuwa kocha wa sasa wa Chelsea Jose Mourinho,alishindwa kupata mafanikio akiwa na timu ya Real Madrid huko nchini Hispania ambako ameinoa timu hiyo kwa misimu mitatu. Hii imetokana na pengine kocha huyo kushindwa kuwapatia klabu ya Real Madrid ubingwa wa 10 wa klabu bingwa Ulaya ambapo mpaka sasa timu hiyo inashikilia rekodi ya kutwaa taji hilo mara 9, kushindwa kuvunja ubabe wa Barcelona nchini Hispania na mvurugano baina ya kocha huyo na watawala, wachezaji wake kama nahodha Iker Cassilas, beki mreno mwenzie Pepe na Sergio Ramos kwa nyakati tofauti ni kati ya sababu ambazo watu wengi wanazitumia kumkosea heshima kocha Jose Mourinho! 

Ni kweli hayo yote yalitokea lakini, unamjua Mourinho au unamsikia? Jose Mourinho ni mshindi wa Ballon D'or kama kocha bora wa dunia mwaka 2010, ametwaa taji la ligi kuu katika nchi 4 tofauti, alifanya hivyo akiwa na timu za Fc Porto ya nchini Ureno, Chelsea ya Uingereza, Inter Millan ya Italia na Real Madrid ya huko Hispania. Mourinho ni miongoni mwa makocha wanne waliowahi kutwaa kombe la klabu bingwa Ulaya wakiwa na klabu mbili tofauti, alifanya hivyo akiwa na klabu ya Porto ya huko Ureno na Inter Millan ya Italia. Unapoamua kumbeza Jose Mourinho, hakikisha umefikiria mara mbili au mara tatu. 

Msimu wa 2010/2011 wakati Jose Mourinho anaanza kazi pale kwenye dimba la Estadio Santiago Bernabeu kuinoa timu ya Real Madrid, nchi ya Hispania ilikuwa imetoka kutwaa kombe la dunia kule nchini Afrika ya kusini na chachu ya mafanikio hayo ni wachezaji wa kutoka klabu ya Fc Barcelona. Ni muda ambao Barcelona ilikuwa haikamatiki, Xaiv Hernandez, Andres Iniesta, Pedro Rodriguez, Sergio Busquets na Lionel Messi walikuwa kwenye kilele cha ubora wao. 

Barcelona ilikuwa ni timu ambayo kwa lugha rahisi,utasema ilikuwa imeshindikana duniani. Kocha wa Zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson alikutana na Barcelona hiyo iliyoshindikana kwenye fainali ya klabu bingwa ulaya mara mbili mwaka 2009 na 2011 lakini hakufua dafu, na kibaya zaidi mzee huyo mwaka 2011, alijikuta akitetemeka mikono huku akiwa haamini kile anachokiona kwa watoto hao wa Katalunia. Arsenal na mzee wao Arsene Wenger,walikutana mara mbili kwenye robo fainali ya UCL na timu hiyo iliyoshindikana, waliteketezwa kama mkate kwenye chai! 

Pamoja na ubora wote ule wa Barcelona,Jose Mourinho katika misimu yake mitatu pale Bernabeu,alifanikiwa kutwaa Kombe la Mfalme kwenye msimu wake wa kwanza tu taji ambalo Real Madrid walilikosa kwa miaka 18, Mourinho msimu wake wa pili aliweza kutwaa taji la La Liga mbele ya Barcelona. Wakati dunia ikiogopa kupangwa na Barcelona hasa kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya, Mourinho alikuwa anakutana na Barcelona ile hatari mara 4 hadi mara 6 kwa msimu mmoja! 

Tangu mwaka 2003, Real Madrid ilikuwa haijawahi kutinga hatua ya nusu fainali za klabu bingwa Ulaya lakini ndani ya misimu mitatu ya Mourinho,wamecheza mfululizo nusu fainali hizo. Utakumbuka msimu wa 2010/2011 walifika nusu fainali na kutolewa na Barcelona ambao walienda kutwaa taji hilo,2011/2012 walifika na kutolewa na Bayern Munich na 2012/2013 walitolewa na Borrusia Dortmund. Ulitaka Jose Mourinho afanye nini zaidi? 

Mourinho amerejea msimu huu kuinoa kwa mara nyingine tena klabu ya Chelsea. Mmiliki wa klabu hiyo Roman Abromovic kwa nyakati tofauti,amekuwa akibadili malengo yake. Abromovic wakati ameinunua klabu ya Chelsea,lengo lake ilikuwa ni kuifanya timu hiyo kutamba kwenye ligi kuu ya Uingereza na Kocha Jose Mourinho aliifanya kazi hiyo kwa kuwapatia Ubingwa wa EPL mara mbili mfululizo mwaka 2005/2006 na 2006/2007. Unamjua Mourinho au Unamsikia? 

Baada ya Mourinho kuondoka,Abromovic alitaka timu yake ipate mafanikio ya Ulaya na kupitia kwa kocha Roberto Dimateo na Rafael Benitez kwa nyakati tofauti,waliweza kutimiza ndoto za Bosi huyo toka Urusi kwa kutwaa kombe la klabu bingwa Ulaya na lile la Europa. Pamoja na hayo yote, Abramovic hakuridhika na sasa akasema anataka timu icheze kama Barcelona na hapo ndipo ujio wa Mata, Hazard na Oscar ulipolenga kutimiza matakwa ya bosi huyo. 

Ujio mpya wa Jose Mourinho kwenye EPL akiwa na Chelsea,ulianza huku akiwa anatamani kuifanya chelsea icheze kama Abromovic anavyotaka lakini, ilishindikana baada ya Mourinho kujikuta akipata sare nyingi na vipigo kutokana na aina hiyo ya uchezaji. Baada ya kupata ushindi wa mabao 4-3 pale Stadium of Light dhidi ya Sunderland na kupokea kichapo cha mabao 3-2 pale kwenye dimba la Britania dhidi ya Stoke City, Mourinho aliamua kubadilika na kuachana kabisa na ule mfumo wa burudani na kurudi kwenye mbinu yake ya kulinda zaidi na kushambulia kwa kushtukiza ambayo imempa mafanikio duniani. 

Msimu huu Mourinho ndiye kocha pekee aliyeweza kuifunga timu ya manchester city nyumbani na ugenini kwenye ligi kuu ya Uingereza na tangu mwaka 2014 uanze, hajapoteza mchezo wowote wa ligi huku dunia ikishuhudia kila mwezi mchezaji mmoja wa Chelsea akifunga ''Hat-Trick", alifunga Samwel Et'oo dhidi ya Manchester united mwezi Januari, akaja Eden Hazard akufunga dhidi ya Newcastle United mwezi Februari na huu ni mwezi machi huku Mjerumani Andre Schullre akifanya hivyo dhidi ya Fulham. Unamjua Mourinho au Unamsikia? 

Jose Mourinho anajua namna ya kwenda na wakati uwanjani na namna ya kufanya mabadiliko ya kiufundi wakati mchezo unaendelea. Msimu uliopita aliwaondoa Man United kwenye michuano ya UCL na katika mechi hiyo, dunia ilishuhudia mabadiliko ya wachezaji uwanjani yenye tija.Wakati Mourinho anajiandaa kumuingiza Karim Benzema, winga wa man united Luiz Nani alipewa kadi nyekundu, Mourinho naye fasta akabadilika na kumtoa beki Alvaro Abeloa ambaye alikuwa anamkaba Luiz Nani na Kumuingiza Luke Modric badala ya Benzema. Baada ya dakika "sifuri' Man United waliangamizwa na goli la kusawazisha la  Modric kabla ya Christiano Ronaldo, kumalizia bao la pili na kupigilia kabisa msumari. Hivi unamjua Mourinho au Unamsikia? 

Jose Mourinho anajua pia namna ya kucheza na maneno.Pamoja na kuongoza ligi kwa sasa, bado ameendelea kudai kuwa timu yake haiko kwenye mbio za ubingwa na ushindi wake dhidi ya Spurs mwishoni mwa juma, ilikuwa ni kuwahakikishia nafasi ya kumaliza ndani ya timu nne za juu. Mourinho bado hajapoteza mchezo wowote wa ligi kuu anapocheza uwanja wa nyumbani pale Stanfford Bridge tangu msimu wake wa kwanza wa 2005/2006 mpaka leo. Huyu mwanaume anachofanya hapa ni kuwaondolea presha wachezaji wake ili waone hata wanapoukosa ubingwa,sio tatizo huku akiwawashia moto Arsenal na Manchester city ambao wanaonekana kucheza kwa presha ya kutaka ubingwa bila kumsahau Liverpool ambaye pengine wengi hawampi nafasi.

Kuna muda mwingine hutakiwi kuamini sana maneno ya Mourinho, baada ya kulazimishwa sare tasa pale Stanfford Bridge na West Ham United ambao walionekana kutumia mbinu ya "kupaki Bus" aliibuka na kusema kuwa wanacheza soka la karne ya 19! Kauli hii ni wazi kuwa Mourinho anahitaji pointi 3 kwenye kila mchezo ili ikiwezekana apate ubingwa mwishoni mwa msimu huu ingawa ameendelea kukanusha jambo hilo.

Wenzetu Ulaya wachezaji ndiyo wanaolipwa fedha nyingi kuliko makocha, tofauti na hapa kwetu Tanzania ambapo ni kinyume chake. Mourinho ni kocha anayesifika kwa kutengeneza nidhamu ndani ya timu na haoni tabu kumuwajibisha nyota yoyote kwenye kikosi chake. Wakati akiwa Real Madrid, kipa na nahodha wa timu hiyo Iker Cassilas, beki mreno mwenzie Pepe na Sergio Ramos kwa nyakati tofauti,walikutana na rugu la Mourinho.

Eden Hazard kwa sasa ndiye tegemeo kwenye kikosi cha Chelsea lakini kutokana na utovu wake wa nidhamu, Mourinho alimuacha nje Star huyo kwenye mechi ya ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Schalke 04. Ashley Cole naye aliachwa nje kwenye mchezo dhidi ya Arsenal baada ya kugundulika kuwa beki huyo alionekana siku chache kabla ya mchezo huo akiserebuka disco na baadhi ya wachezaji wa Arsenal. Hivi unamjua Mourinho au Unamsikia?

Jose Mourinho ni aina ya kocha ambaye kila shabiki wa soka, angependa aifundishe timu anayoshabikia. Mourinho ni mpiganaji na siku zote anawaza ushindi.Unapokuwa na Mourinho siku zote unakuwa na roho ya upambanaji huku ukiamini ushindi unapatikana muda wowote. Namuheshimu sana Sir Alex Ferguson, Juup Heynches, Pep Gaudiola, Arsene Wenger, Carlo Ancelloti na makocha wengine wenye historia kwa nyakati hizi lakini, Jose Mourinho ni kocha wa sayari nyingine.

VIDEO: BARCA NA PSG WALIVYOPITA KWENDA ROBO FAINALI YA CHAMPIONS LEAGUE - CITY NA LEVERKUSEN WAAGA

Wednesday, March 12, 2014

FC BARCELONA VS MANCHESTER CITY - TIMU YA MWISHO YA ENGLAND KUIFUNGA BARCELONA CAMP NOU ILIKUWA LIVERPOOL - CITY WATAWEZA LEO?Barcelona wamepoteza mchezo mmoja tu kati ya 18 ya mwisho waliyocheza katika hatua ya mtoano ndani ya dimba la Camp Nou kwenye michuano ya Champions League (0-3 v Bayern Munich msimu uliopita).

Kati ya michezo 30 ya hatua ya mtoano ya michuano ya Champions League iliyopigwa Nou Camp, Barcelona wamepoteza michezo miwili tu kwa angalau mabao yasiyopungua mawili (0-2 v Real Madrid in April 2002 na 0-3 v Bayern Munich in May 2013).

Ni klabu moja tu ya kiingereza iliyoweza kufanikiwa kuifunga Barcelona katika dimba la Camp Nou kwenye Champions League (kwenye michezo 17): Liverpool mnamo February 2007 (1-2).

Mechi 3 za mwisho za Champions League kati ya Barca dhidi ya timu za England ndani ya dimba la Camp Nou zimezalisha mabao 13.

Manchester City hawajawahi kushinda dhidi ya klabu ya Uhispania kwenye michuano ya Champions League.

Manchester City wameshinda mechi zao tatu za ugenini kwenye Champions League msimu huu, ukiwemo ushindi wa 3-2 dhidi ya mabingwa watetezi Bayern Munich.

Manchester City wameweza kuzuia wavu wao kuguswa mara moja katika mechi 13 za mwisho za Champions League (ushindi wa 3-0 dhidi ya Viktoria Plzen)

Barcelona ndio timu yenye rekodi nzuri zaidi ya kufunga katika uwanja wa nyumbani kwenye michuano ya Champions League msimu wakiwa wameshafunga mabao 13.

Barcelona wamefanikiwa kufika nusu fainali ya ligi ya mabingwa ya ulaya mara sita mfululizo, rekodi bora kabisa katika michuano hii.

Lionel Messi (mabao 66) amebakiza mabao matano 5 tu kufikia rekodi ya mabao Raul ya kufunga mabao mengi katika Champions League (mabao 71). Amefunga mabao 7 katika mechi 4 msimu huu - akiwa kapiga mashuti 9 tu langoni.

Xavi ameshaichezea Barcelona mechi 138 katika Champions League. Ikiwa atacheza leo ataifikia rekodi ya kucheza mechi nyingi katika michuano hii inayoshikiliwa na Ryan Giggs aliyecheza 139.

SIKU YA 92 KABLA YA KOMBE LA DUNIA - GOLI LA 92 KWA UBORA KATI YA 100 YALIYOWAHI KUFUNGWA KWENYE HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA

)

UNALIZUNGUMZIAJE HILI BAO,UNALIFANANISHA NA BAO LIPI

SIKU CHACHE BAADA YA KUTAJWA KUWA MWANASOKA TAJIRI - RONALDO AMSAIDIA MTOTO WA MIEZI 10 KUFANYIWA UPASUAJI WA KUOKOA MAISHA YAKE


Gazeti la kihispania AS linaripoti kwamba mwanasoka tajiri zaidi na bora Cristiano Ronaldo anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ameamua kumlipia fedha za matibabu mtoto mwenye miezi 10 Erik Ortiz Cruz ambaye ni mgonjwa sana akisumbulia na matatizo kwenye ubongo wake (Cortical dysplasia.)

Ugonjwa huu unamfanya mtoto huyo awe anazimia au kupata mshtuko mara 30 kwa siku na hivyo anahitaji kufanyiwa upasuaji ili kuondoa hali hiyo isiyo ya kawaida kwenye ubongo. (Kufahamu zaidi kuhusu cortical dysplasia ingia hapa the Wikipedia entry here.)

Kila kipimo anachofanyiwa mtoto huyo kina gharama ya 6,000 euros na upasuaji mzima unagharimu kiasi cha 60,000 euros hivyo watu wa kijiji cha Villaluenga de la Sagra, Spain, wamekuwa wakijaribu kukusanya fedha kwa ajili ya matibabu ya mtoto huyo kupitia michango.

Jambo hili lilipomfikia Ronaldo ambaye alifuata aweze kutoa jezi yake na viatu vyake ili vipigwe mnada, akawapa walichotaka kwa ajili ya mnada na kisha akalipia gharama zote za matibabu ya mtoto huyo.

Hii si mara ya kwanza kwa Ronaldo kusaidia watu wasiojiweza, kitendo hiki kinakuja siku chache baada ya kutajwa kuwa manasoka tajiri zaidi duniani.

GARY NEVILLE AMTETEA MESUT OZIL,WEWE NINI MAONI YAKO JUU YA KIWANGO CHA OZIL....
PHILLIP COCU- KIUNGO FUNDI WA UHOLANZI ALIYEGEUKIA UKOCHADunia na wapenzi wa soka kiujumla wamepata fursa ya kuona na kushuhudia vipaji na ufundi mbalimbali unaoonyeshwa au uliowahi kuonyeshwa na wanasoka mbalimbali ulimwenguni kiasi ambacho baadhi ya majina ya wanasoka ambao wameamua kutundika daruga la kusakata mchezo huo wa kabumbu ulimwenguni yakiendelea kukaa vichwani na kutajwa midomoni mwa wapenzi na mashabiki wa soka ulimwenguni.
Miongoni mwa wachezaji ambao licha ya kuamua kupumzika na mikikimikiki ya mchezo wa soka bado wamebakia kuwepo katika ubongo wa wapenzi wa soka ulimwenguni ni kiungo fundi wa ushambuliaji wa vilabu vya Barcelona na PSV Eindhoven, Phillip John William Cocu ambaye dunia ilimtambua kwa kifupi cha jina lake Phillip Cocu.

KIPAJI TOKA EINDHOVEN

Phillip Cocu alizaliwa mnamo tarehe 29,Oktoba 1970 katika kitongoji cha Zevenaar kilichopo katika jii lenye wanazi sugu wa soka la Eindhoven. Ikumbukwe kwamba jiji la Eindhoven ndipo inapotoka timu iliyoweza kutikisa nchini Uholanzi na Ulaya kwa ujumla mwishoni mwa miaka ya tisini na mwanzoni mwa miaka ya elfu mbili ya PSV Eindhoven.
Kama ilivyo ada kwa watoto wengi wanaozaliwa wakiwa na vipaji vya soka, Cocu alijiunga na timu ya watoto ya mtaani kwao ya DCS  kabla ya baadae kujiunga na timu nyingine iliyopo katika mtaa huo ya De Graafschap ambayo aliichezea mpaka mwaka 1988 ambapo alijiunga rasmi na soka la kulipwa katika timu ya AZ Alkmaar ambayo aliichezea kwa muda wa miaka miwili tu ambapo baadaye alijiunga na klabu ya Vitesse .
Akiwa Vitesse, Cocu alipata majeruhi mwanzoni tu mara baada ya kujiunga na klabu hiyo jambo lililopelekea kutishia kipaji chake lakini alifanikiwa kupigana na majeruhi hayo ya goti ambayo na kurudi uwanjani kwa kishindo na kupata nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

AJIUNGA  NA KLABU YA NDOTO ZAKE

Baada ya kuichezea timu ya Vitesse kwa muda wa miaka mitano katika michezo 137 na kufanikiwa kuifungia timu hiyo jumla ya magoli 25, Cocu alisajiliwa rasmi na klabu maarufu ya PSV Eindhoven ambayo inatoka katika jiji alilozaliwa la Eindhoven mnamo mwaka 1995.
Cocu aliuelezea uhamisho huo kuwa ni ukamilisho wa ndoto zake za muda mrefu za utotoni huku akiishukuru klabu ya Vitesse na mashabiki wake kwa kumsapoti katika matukio shida na furaha aliyowahi kukutana nayo ikiwemo majeruhi ya muda mrefu aliyopata pindi alipojiunga na timu hiyo huku wakimchukulia kama miongoni mwa mashujaa wao klabuni hapo.

APIGA SOKA LA UHAKIKA PSV, ATUA BARCELONA

Mara baada ya kujiunga na klabu ya PSV Eindhoven, Cocu alifanikiwa kupata alifanikiwa kujitengenezea namba ya kudumu katika timu hiyo akicheza katika nafasi ya kiungo mshambuliaji nafasi ambayo alikuwa akiimudu vilivyo na kufanikiwa kutwaa mataji mawili maarufu nchini humo ya KNVB na lile la ligi kuu nchini humo lijulikanalo kwa jina la Eredivisie mnamo mwaka 1997.
Akiwa hapo, Cocu alifanikiwa kucheza jumla ya mechi 95 huku akifanikiwa kuifungia timu hiyo jumla ya magoli 31 katika mechi hizo alizocheza.
Kutokana na uwezo wake mkubwa wa kusakata kabumbu, vilabu mbalimbali barani Ulaya vilianza kuinyemelea saini yake lakini ilikuwa ni klabu ya Bercelona iliyofanikiwa kuinasa saini yake mnamo mwaka 1998.

ATESA BARCELONA , APEWA UNAHODHA

Cocu katika misimu yote aliyoichezea klabu hiyo ya Hispania inayotokea katika kitongoji cha Catalan, alifanikiwa kuteka nyoyo za wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza soka jambo ambalo lilipelekea Mdachi huyo kupewa unahodha klabuni hapo, huku akifanikiwa kuisaidia timu hiyo kutwaa taji la nchi hiyo maarufu kama La Liga, huku Barcelona ikifanikiwa kucheza katika nusu fainali mbili za mashindano makubwa na maarufu ya vilabu barani Ulaya yajulikanayo kama Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Pia akiwa Barcelona, Cocu alifanikiwa kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa kigeni kuweza kuichezea mechi nyingi timu ya Barcelona, ambapo aliichezea timu hiyo jumla ya mechi 205 huku akifunga jumla ya magoli 31

AAMUA KURUDI NYUMBANI

Baada ya miaka  sita ya mafanikio ndani ya Barcelona, Phillip Cocu aliamua kurudi katika klabu aliyoipenda ya PSV Eindhoven ambako aliweza kuisaidia timu hiyo kushinda jumla ya mataji matatu ya ligi kuu nchini humo huku pia akiisaidia timu hiyo kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, huku ikiwa ni nusu fainali yake ya tatu katika mashindano hayo.
Inasemekana, Cocu aliamua kurudi zake nyumbani Uholanzi ikiwa ni kama njia ya kumpisha nyota wa Kihispania aliyekua anachipikia klabuni hapo ambaye baadae ametokea kuwa staa na nahodha wa tim hiyo, na huyu si mwingine bali ni Xavi Hernandez.

AMALIZIA SOKA UARABUNI,ANG’ARA TIMU YA TAIFA

Mara baada ya awamu ya pili ya mafanikio ndani ya klabu ya PSV,Cocu aliamua kutimkia zake Uarabuni ambako alikwenda kumalizia soka lake katika klabu ya Al Jazira.
Kutokana na soka lake la uhakika alilolionyesha katika timu mbalimbali, Cocu alifanikiwa kujiwekea nafasi ya kudumu katika timu ya Taifa ya Uholanzi ambayo aliichezea jumla ya mechi 101 na kuifungia jumla ya magoli 10.
Miongoni mwa matukio ya kusisimua ya Phillip Cocu akiwa na timu ya Taifa ya Uholanzi, ni kuifungia timu hiyo magoli mawili katika Fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika nchini Ufaransa mwaka 1998 lakini baadae akaja kukosa penati muhimu dhidi ya Brazil katika mchezo wa nusu fainali ambapo Uholanzi iliondolewa kwa mikwaju ya penati na miamba hiyo ya soka ulimwenguni.

AGEUKIA UKOCHA

Mara baada ya kuamua kutundika daluga la kucheza soka, kama ilivyo kawaida ya wanasoka wengi waliostaafu kucheza soka, Cocu aliamua kujikita katika ukocha wa mchezo huo wenye mashabiki wengi ulimwenguni ambapo hivi sasa anainoa klabu anyoihusudu ya PSV Eindhoven ambayo ameiwezesha kufika katika hatuanya mtoano ambayo walitolew na timu ya AC Milan hivi karibuni, huku wakipata nafasi ya kushiriki katika mashindano ya Europa League.


Imeandaliwa:
CHARLES ABEL-SAUT
0713 923276
Email: charlesabel46@yahoo.com