Search This Blog

Saturday, July 7, 2012

WEMA SEPETU NA JACK WOLPER WAKIJIFUA DAKIKA CHACHE KABLA YA PAMBANO LAO - TAMASHA LA MATUMAINI


Wema Sepetu akipasha na mwalimu wake Rashid Matumla kabla ya pambano
Wema akijifua.
 
Wolper.
Wasanii mahiri wa Filamu, Wema Sepetu na Jacqueline Wolper wakijifua kabla ya mpambano wao leo.


MATUKIO YOTE YA PICHA KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHER

HIVI NDIVYO WABUNGE MASHABIKI WA SIMBA WALIVYOSHANGILIA USHINDI WAO DHIDI YA WABUNGE MASHABIKI WA YANGA

Mbunge wa Chadema na mshabiki mkubwa wa Simba Zitto Kabwe akishangilia baada ya kufunga penati
Wapinzani Bungeni Washkaji dimbani - Zitto Kabwe na William Ngeleja wakiongoza ushangiliaji wa wabunge wa Simba.
Wachezaji wa Simba (Wabunge) wakishangilia ushindi baada ya kuwafunga watani wao wa Yanga (Wabunge) kwa penalti 3-2.
Add caption
Yanga baada ya kipigo hicho.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mtanange wa watani wa jadi Simba na Yanga (Wabunge) wakati wa TAMASHA LA MATUMAINI ambapo wabunge wapenzi wa timu ya Simba wameibuka kidedea kwa penalti 3-2.  Simba wamefunga penalti 3 wakati Yanga wakifunga 2.

WABUNGE WA SIMBA WAWAKUNG'UTA WABUNGE WA YANGA MABAO 3-2 TAIFA LEO


Mbunge William Ngeleja akiingia dimbani kwenye mchezo wa leo uliofanyika kwenye dimba la taifa.

Benchi la wabunge wa Yanga.

...Kikosi cha Simba.
...Kikosi cha Yanga.


Wachezaji wa Yanga na Simba (Wabunge) wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya mechi kuanza.
Mtanange baina ya wabunge hao ukiendelea.…

Wachezaji wa Yanga na Simba (Wabunge) wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya mechi kuanza.
Mtanange baina ya wabunge hao ukiendelea.
Zitto Kabwe akitoa pasi.
PICHA ZOTE KWA NIABA YA GLOBAL PUBLISHER


BONGO MOVIE WAINYANYASA BONGO FLAVA KWENYE TAMASHA LA MATUMAINI

Wachezaji wa Bongo Movie Ben Kinyaiya na JB wakifanya warm up kabla ya mchezo.
Benchi la Bongo Movie team
BongoMovie wakishangilia goli lao
Wachezaji wa Bongo Movie na mashabiki wake wakishangilia bao lao lililofungwa na Kiduko.

BAADA YA MORRISON, POGBA SASA NI FRYERS - KWANINI MAN UNITED WANAPOTEZA MATUNDA YA ACADEMY YAO?


Ravel Morrison alikuwa wa kwanza kuondoka. Paul Pogba sakata la uhamisho wake  kwenda Juventus limemalizika wiki iliyopita rasmi baada ya Ferguson kuthibitisha ameenda Juve. Sasa jina jipya la mchezaji kinda kutoka kwenye academy ya United, Zeki Fryers  ambaye nae anakaribia kutua Tottenham Spurs. Kwanini Manchester United wanapata wakati mgumu kukaa kwa muda mrefu na wachezaji wake wa kutka kwenye academy yao.

Kwa klabu ambayo imepata mafanikio makubwa na mfumo wa kuingiza wachezaji makinda kutoka kwenye Academy mpaka kwenye timu kubwa ni vigumu kuelewa kwanini hivi karibuni wanashindwa kudumu na makinda yao.

Itakumbukwa kauli ya Alan Hansen alyomwambia Ferguson: "Huwezi kushinda chochote na wachezaji watoto." Na Fergie akafanya kinyume chake na kushinda makombe mengi sana na kikosi kilichoitwa cha watoto kilichowahusisha wachezaji kama Ryan Giggs, Scholes, Beckham na wengine wengi.

Kwenye kipindi cha hivi karibuni United ambao wamepata mafanikio makubwa kupitia mfumo wa wa kukuza vipaji - wamekuwa wakipoteza wachezaji wao makinda ambao wanaonekana kuwa na vipaji vikubwa.

Kwanini mchezaji mwenyewe akataka kuondoka? Tena kwnye klabu inayosadikika kuwa maarufu, yenye mashabiki wengi, mafanikio na tajiri kuliko - huku akiwa na uhakika kupata nafasi ya kuingia kwenye kikosi cha kwanza. Yote haya yamepafanya Old Trafford kuwe sehemu nzuri kwa wachezaji. Kila mtu alilijua hili. Labda hilo ndio lilikuwa tatizo.

Wachezaji wadogo kama Pogba wamekuwa wakichanganywa akili na mishahara mikubwa inayotolewa na vilabu vinginena United wanakuja kugundua kwamba brand ya Red Devils haina ushawishi mkubwa kama iliyokuwa nayo mwanzoni. Kuna taarifa kwamba Pogba alihadiwa kwamba kuanzia msimu wa 2011-2012 angekuwa anapata nafasi mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza lakini mwishowe akaishia kupata kucheza kwenye mechi 7, huku tatu zikiwa kwenye mechi za kombe la Carling.

Ahadi ya kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza ilikuja kuonekana imetimizwa kwa kiasi kidogo sana. Pogba hakuwa tayari kusubiri kwa muda mrefu kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara ndani ya jezi ya United na akaamua kubadilisha upepo kwenda Turin.

Pamoja na matatizo mengine lakini hili na nafasi ya kucheza mara kwa mara limechangia kwa makinda kushindwa kuendelea kubaki Old Trafford.

Wakati hakuna mchezaji anayepaswa kulipwa kulikovile anavyostahili, lakini kuendelea kukataa kuafikiana na wachezaji wake makinda ambao wana vipaji vikubwa kunaweka hatari kubwa kwa klabu hiyo yenye mafanikio makubwa kwenye premier league.

Pogba na Morrison ni vijana ambao walikuwa wakitajwa kuwa ndio nguzo ya miaka kadhaa ijayo ya  safu ya kiungo ya United, walikuwa ndio watakaokuja kuwa waokozi wa safu hiyo ambayo kwa kwa siku za hivi karibuni ndio imekuwa sehemu yenye udhaifu kwenye kikosi cha Red Devils, lakini badala ya kuendelea kuwashikilia vijana waliowakuza huku akitafuta top layers wa muda - United wameacha makinda yao yaondoke huku wakimuachia msala wa kutafuta wachezaji wa bei chee Fergie.

Lakini chini ya utawala wa Glazers United wamekuwa wakishindwa kufanya usajili wa wachezaji wakubwa kutokana na bei pamoja mahitaji binafsi ya wachezaji, mfano mzuri ni akina Wesley Sneijder, Samir Nasri, Eden Hazard na hata hivi sasa Modric anaweza akaongezeka kwenye listi. Hivyo kutokana na kuwa wanyonge kwenye kushindana na timu aina ya Real Madrid, Barelona, Chelsea na City njia rahisi katika kuweza kuendelea kupata wachezaji wazuri ni kupitia mfumo wa wachezaji vijana.
Mahasimu wao Manchester United wanaweza kuja kutamba kuwashinda wengi kwa ubora wa wa academy yao ya kitajiri iliyo njiani, lna huku United wakiwa hawana uwezo wa kushindana na nguvu ya matumizi ya Noisy Neighbours - hivy bado njia nzuri zaidi ya kushindana nao na kuboresha mfumo wao mzima wa kukuza na kuhakikisha na wanadumu na wachezaji ambao ni matunda ya chuo chao.
 


Tayari wameshapoteza viungo wao wenye vipaji vikubwa, sasa ni Fryers, kinda lingine lenye kipaji aliyekuwa akitaarishwa kuja kuchukua nafasi kwenye kikosi cha kwanza kumrithi Patrice Evra anaelekea uzeeni - naye yupo njiani kuondoka. Ndio maana wapo tayari kulipa "kodi ya England' kumsanini Leighton Baines.

Lakini hili sio kusema kwamba hakuna wachezaji wengine wakali wanaokuja kutoka kwenye academy, Commitment ya United kwenye kukuza vipaji bado ipo safi kama mawingu. Will Keane amekuwa akifanya mambo makubwa kwenye timu ya reserve na ameichezea England under 21 mwaka huu, ingawa mwezi uliopita alipata majeraha ya goti na atakuwa nje kwa muda kidogo.

Muitaliano aliye na kipaji kikubwa Davide Petrucci ni staa mwingine aliyepo kwenye academy ya United - inaonekana anaweza kuanza kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza msimu wa 2012-13 , kinda lenye akili sana kwenye upande wa kushambulia na vision za hatari dimbani - huku beki wa kati Tom Thorpe tayari amecheza kwa kiwango kikubwa mpaka amepewa unahodha wa England under 21.

Pogba, Morrison na Fryers wameondoka, na hili linawapa nafasi United waanze kujifikiria upya. Kuondokewa na wachezaji wake muhimu ni tatizo ambalo limeandama sana Arsenal na limewagharimu sana. United inabidi wajipange na kuweza atleast kuweza kuwalipa vizuri na kuwapa nafasi vijana wao ili wasiendelee kupoteza matunda ya academy yao ambayo kwa hali ya uchumi ilivyo chini ya Glazer - academy ndio nguzo yao kwa sasa.

Vinginevyo wajiandae kuwa chini ya utawala wa mahasimu wao wakubwa wenye misuli ya pesa ambao tayari wamewapora ubingwa wa England msimu uliopita huku wakiwapa kipigo cha aibu.

FELIX SUNZU ARUDI DIMBANI NA KUIPELEKA SIMBA NUSU FAINALI YA URAFIKI CUP

Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba na Zambia Felix Muamba Sunzu leo amerudi dimbani kuitumikia tena klabu yake ya Simba na kuifungia goli la pekee na la ushindi kwenye mchezo wa kombe la Urafiki linaloshindaniwa huko Zanzibar.

Simba imeifunga timu ya vijana ya Zanzibar Karume Boys kwa bao 1-0 liliowekwa kimiani na Mzambia huyo.

Kwa matokeo hayo Simba ambao walianza vyema michuano hiyo inayofanyika kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa kwa ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya mabingwa wa Zanzibar, Mafunzo kabla ya kuja kushikiliwa kwa sare ya 1-1 na Azam, ambao ni washindi wa pili wa Ligi Kuu ya Bara.

Azam FC ilimaliza ikiwa ya pili kwa kuwa na pointi 5 baada ya sare mbili na ushindi katika mechi iliyochezwa mapema jana.


Katika mechi hiyo, Azam iliilaza Mafunzo ya hapa kwa mabao 3-2.

HUYU NDIO KOCHA MPYA WA VAN PERSIE NA WENZIE

Kwa mara ya pili kwenye maisha yake ya soka - kocha mkongwe Luis Van Gaal hatimaye amepata nafasi ya kusahihisha makosa yake aliyoyafanya miaka sita iliyopita kwa kuiongoza Uholanzi kukosa nafasi ya kucheza kwenye kombe ladunia kwa mara ya kwanza.

Siku kadhaa baada ya kocha Bert van Marwijk kujiuzulu kuifundisha Uholanzi baada ya kucheza kwa kiwango kibovu kwenye Euro 2012, leo hii amepata mrithi wake - Luis van Gaal.

Van Gaal kocha wa zamani wa Ajax, Barcelona na Bayern Munich anamrithi Bert, huku ikiwa ni kipindi chake cha pili kuiongoza Holland.

Baada ya kutambulishwa kwa waandishi wa habari Van Gaal alisema: "Ni changamoto niliyokuwa nikiisubiri sana, nashukuru nina nafasi ya kurekebisha palipoenda vibaya mara mwisho nilivyokuwa mwalaimu wa timu ya taifa."

Kocha huyu mwenye miaka 60 amesaini mkataba wa ambao utampeleka mpaka kwenye fainali za kombe la dunia 2014.

MCHAKATO WA LIGI KUENDESHWA KAMPUNI WAFIKIA ASILIMIA 95 SASA

Hatimaye mchakato wa vilabu kuweza kufungua kampuni itakayosimamia umeanza kufikia mwishoni.

Kwa taarifa nilizonazo leo kumekuwepo na kikao cha mwisho kilichokaa kwa kuwahusisha viongozi kutoka kwenye vilabu vyote vya ligi kuu ambao ndio wanaounda kampuni itayosimamia ligi kuu ya Tanzania bara msimu ujao.


Kwenye kikao hicho mambo yote muhimu katika kuelekea kwenye mchakato huo wa kuanzishwa kwa kampuni na sasa kilichobakia ifikapo wiki ijayo - viongozi hao wa vilabu watapeleka mfumo mzima na utaratibu waliopanga kwa namna ya kuendeshwa kwa ligi msimu kwa kamati ya utendaji ya shirikisho la soka kwa ajili ya kupata mawazo tofauti ili kuleta maboresho kama yatakuwepo - na mchakato wa kuifungua kampuni kuanza mara moja.

Friday, July 6, 2012

HII NDIO SIRI YA MAFANIKIO YA BARCELONA : TIMU YA WATOTO WA MIAKA 11 INAVYOKIPUTA

CHEMSHA BONGO: HIKI NI KIKOSI CHA TIMU GANI KUTOKA TANZANIA??


YANGA WAMSAINISHA TOM SAINTIFIET KWA MIAKA MIWILI

Hatimaye siku mbili baada ya kutua nchini kocha Tom  Saintifiet kutoka nchini Ubelgiji, leo ameingia mkataba wa kuifundisha klabu ya Yanga kwa kipindi cha miaka miwili.

Akizungumza mara baada ya kuingia mkataba huo katika Makao Makuu ya klabu ya Yanga , Mwalimu huyo amesema anatarajia kufanya kazi kwa nguvu sana ili kuhakikisha Yanga inafanikiwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania

Saintifiet amesema Mkataba huo wa miaka miwili amesema anatarajia  kuutumia katika kuleta maendeleo katika Klabu ya Yanga ikiwemo kukuza vipaji katika soka la Vijana.
 
Naye Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwesiga Selestine amesema Mkataba huo huenda ukawa ni endelevu iwapo uongozi utaridhishwa na mwenendo wa Kocha huyo.
 

KWANINI IKER CASILLAS ANASTAHILI KUSHINDA TUZO YA UCHEZAJI BORA WA DUNIA

Mjadala ulishaanza. Huku Spain wakisherehekea ushindi wao wanusu fainali  dhidi ya Ureno kwenye Euro 2012, mjadala ukawa ukageukia kwenye tuzo ya Ballon d'Or.  Cristiano Ronaldo alicheza kikubwa cha kutosha kwenye michuano hiyo kiasi cha kumfanya achukue tuzo ya uchezaji bora wa dunia? Au itakuwa Lionel Messi kwa mara ya nne mfululizo?

Usiku uliofuatia, Andrea Pirlo alionyesha kiwango cha hatari na kuiongoza Italy kupata ushindi wa usiotegemewa dhidi ya Ujerumani kwenye hatua ya nusu fainali. Na baada ya fainali, Kiungo wa Spain Andres Iniesta akaingia kwenye mchuano wa tuzo hiyo baada ya kuiongoza La Roja kutoa kipigo cha mbwa mwizi kwa Italia huku akimfunika Andrea Pirlo.

Lakini vipi kuhusu mwanaume aliyebeba kombe la Euro kwa Spain jumapili iliyopita?

Iker Casillas ndio jina jipya ambalo limeibuka katika mchuano huu wa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa FIFA. Akiwa amepewa sifa na Pele huku Di Stefano akimuondoa - mawazo tofauti yameshaanza kujitokeza.

Golikipa huyo wa Spain aliiongoza La Roja kupata ushindi mkubwa michuano hiyo iliyofanyika Oland na Ukraine, akiweka rekodi mbalimbali ambazo hakuna magolikipa wengine duniani wamewahi kuzifikia.

Jaokuwa timu yake mara nyingi imekuwa ikitawala mpira, lakini pale anapohitajika kuzuia mashambulizi hufanya hivyo kwa usahihi mkubwa. Kipa huyo mwenye miaka 31, aliokoa vizuri sana mpira uliopigwa na Ivan Rakitic wakati mchezo ukiwa 0-0 dhidi ya Croatia - goli ambalo kama wangefungwa lingeweza kuwaondoa kwenye michuano hiyo mabingwa hao kwenye hatua ya makundi. Pia kuokoa mkwaju wa penati ya Joao Moutinho uliwazuia kuwapa uongozi Ureno kwenye hatua ya penati na kuwapa nguvu zaidi baada ya Xabi Alonso kukosa penati yake ya kwanza kwa Spain iliyokolewa na Rui Patricio.

Kwenye fainali, Iker aliokoa michomo kadhaa ya hatari iliyoelekezwa golini kwake, wakati Spain wakiongoza kwa 2-0, kabla ya mchezo kuendelea na kuisha kwa Italy kufungwa 4-0.

Mechi hiyo ilikuwa ya 137 kwa Ikerkuichezea Spain na sasa amebakisha mechi 11 kumfikia golikipa Andoni Zubizarreta. Lakini kubwa zaidi mafanikio ya kwenye mchezo huo wa fainali - ulimfanya golikipa huyo wa Madrid kuwa mchezaji wa kwanza kushinda mechi 100 kwenye level ya kimataifa. Alivunja rekodi ya Dino Zoff ya kucheza dakika 494 bila kufungwa goli kwenye Euro, huku Casillas akicheza dakika 511 bila kufungwa goli - Antonio Di Natale alikuwa ndio mshambuliaji wa mwisho  kumfunga Iker.

Pia Saint Casillas alikuwa na msimu mzuri sana na Real Madrid, akikumbukwa zaidi kwa kuiongoza Blancos kuifunga Barca 2-1 huku akiokoa mpira muhimu wa Xavi mwezi wa nne pale Nou Camp.

Casillas akiwa kiongozi wa timu chini Jose Mourinho waliongoza Los Blancos kubeba kombe la kwanza la La Liga  tangu mwaka 2008.

Mchezaji mwenzie wa Madrid, Cristiano Ronaldoanaweza akawa ndio mtu aliyechangia zaidi mafanikio ya Madrid, lakini kushindwa kwake kuiongoza Ureno vizuri dhidi ya Spain kwenye Euro 2012 kunaweza kumuangusha, wakati Messi akishinda kombe moja tu dogo la mfalme huku akivunja rekodi ya mabao ulaya kwa kufunga mabao 73 lakini pia akakosa  kushinda kombe muhimu la La Liga - huku akiwa hajacheza michuano ya mashindano ya kimataifa. Performance ya Pirlo pia haikutosha, baada ya Spian kuwaaibisha waitaliano mjini Kiev jumapili iliyopita, kwa maana mchezaji mmoja wa La Roja anastahili kubeba tuzo hiyo.

Xavi na Iniesta wamecheza vizuri na kiukweli wanastahili kuwemo kwenye mchuano, lakini ukiangalia kimafanikio Casillas anastahili kuchukua tuzo hii ya Ballon d'Or.

SABA WAPATA ITC KUCHEZA KENYA, MSUMBIJI


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa Watanzania saba kucheza mpira wa miguu katika nchi za Kenya na Msumbiji.

TFF imetoa hati hizo kwa wachezaji hao baada ya kuombewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Msumbiji (FMF) ili waweze kucheza katika klabu za nchi hizo.

Wachezaji waliokwenda Bandari ya Kenya na klabu walizokuwa wakichezea nchini kwenye mabano ni David Naftali (huru), Meshack Abel (huru), Mohamed Banka (huru) na Thomas Mourice (Mtibwa Sugar).

Klabu ya CD Madchegde ya Msumbiji imewachukua wachezaji Hassan Hassan Mustapha kutoka Mgambo Shooting ya Tanga, na Abdallah Ally Abdallah na Thobias David Silas kutoka klabu ya daraja la kwanza ya Transit Camp ya Dar es Salaam.

ODHIAMBO WA AZAM APATA ITC

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ya mchezaji George Odhiambo, raia wa Kenya aliyejiunga na klabu ya Azam.

Hati hiyo imetolewa na Chama cha Mpira wa Miguu cha Denmark (DBU) ambapo Odhiambo alikuwa akicheza nchini humo kabla ya kutua Azam kwa ajili ya msimu wa 2012/2013.

Klabu nyingine zinazosajili wachezaji kutoka nje ya Tanzania zinatakiwa kuhakikisha zinakamilisha uhamisho wao (transfer) kabla ya Julai 30 mwaka huu ambayo ndiyo siku ya mwisho kufanya hivyo.

Kanuni ya 41 ya Ligi Kuu kuhusu ITC inasema: “(1) Maombi ya ITC kwa wachezaji wa kigeni wa kulipwa yatawasilishwa kupitia mtandao wa kompyuta kwa kutumia program ya ‘Transfer Matching System-TMS’ baada ya klabu zinazohusika na mchezaji huyo au wachezaji hao kukubaliana nje ya mtandao.

(2) Maombi ya ITC kwa wachezaji wa kigeni wasio wa kulipwa yatawasilishwa kwa barua TFF baada ya klabu zinazohusika na mchezaji huyo au wachezaji hao kukubaliana. Chama cha Soka kinachotoa ITC kwa njia hii kitapeleka nakala FIFA. (3) ITC haihitajiki kwa mchezaji mwenye umri chini ya miaka kumi na mbili (12).”

Tunapenda kuzikumbusha klabu kuwa kwa mujibu wa Kanuni ya 53 ya Ligi Kuu, wachezaji wa kigeni ni lazima wawe wanachezea timu ya Taifa au klabu za Ligi Kuu huko wanakotoka.

Kanuni hiyo inasema: “Klabu inaruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni wa ngazi ya kimataifa ambao ni wa timu za Taifa na Ligi Kuu kutoka nje ya nchi wasiozidi watano (5). Wachezaji kutoka Ulaya na Marekani ya Kusini wanweza kuwa wa daraja la pili na kuendelea, na klabu inaruhusiwa kuchezesha wachezaji walioorodheshwa wasiozidi watano (5) wa kigeni katika mchezo mmoja. Wachezaji hao watasajiliwa baada ya TFF kuhakikisha usahihi wa taarifa zao na kukamilika kwa taratibu za uhamisho wa kimataifa.”

16 BORA COPA COCA-COLA KUANZA J’MOSI

16 bora ya michuano ya Copa Coca-Cola 2012 inaanza kesho (Julai 7 mwaka huu) kwa mechi nne zitakazokutanisha timu nane kati ya 16 zilizofuzu hatua hiyo. Mechi hizo za 16 bora zitachezwa kwenye viwanja vya Kumbukumbu ya Karume na Tanganyika Packers vya Dar es Salaam.

Ruvuma iliyoongoza kundi A itacheza na Temeke iliyoshika nafasi ya tatu kundi C. Mechi hiyo itaanza saa 2.30 asubuhi Uwanja wa Karume. Mechi nyingine ya asubuhi itakayochezwa Tanganyika Packers itawakutanisha washindi wa pili kundi A Kigoma dhidi ya Mara walioshika nafasi ya nne kundi C.

Mechi za jioni kwa kesho zitakazoanza saa 10 kamili jioni zitakuwa kati ya Mjini Magharibi na Kagera kwenye Uwanja wa Karume wakati Morogoro na Pwani zitaumana kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers ulioko Kawe, Dar es Salaam.

Hatua ya 16 bora itakamilika keshokutwa (Julai 8 mwaka huu) kwa mechi za asubuhi kati ya Kinondoni na Rukwa kwenye Uwanja wa Karume, na Dodoma dhidi ya Arusha kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers. Mechi za jioni siku hiyo ni kati ya Kilimanjaro na Mwanza (Uwanja wa Karume) na Tabora na Tanga (Tanganyika Packers).

Timu zitakazoshinda zitaingia hatua ya robo fainali itakayochezwa Julai 10 na 11 mwaka huu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Nusu fainali itachezwa Julai 13 mwaka huu, na kufuatiwa na mechi ya mshindi wa watatu na fainali ambazo zote zitachezwa Julai 15 mwaka huu.

KIBONZO CHA LEO!

DEBATE: GOAL LINE TECHNOLOGY ITAONGEZA RADHA AU ITAPUNGUZA ?


Hivi hii Teknolojia ya kubaini iwapo mpira umevuka mstari wa goli maarufu kama Goal Line Technology iliyoidhinishwa na bodi ya kimataifa inayosimamia sheria za Soka Ulimwenguni IFAB, Itaongeza radha ya mpira au Itapunguza??....Na vipi kuhusu sisi tuliopo huku Ulimwengu wa tatu, teknolojia hii itatufikia lini??...TUNAKARIBISHA MAONI YENU.

Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’- EPISODE 9

*Awachezea kindava wachezaji wa Vital’O, washinda
*Yanga yatainga fainali, kazi ni dhidi ya wenyeji SC Villa
 Na Saleh Ally
WIKI ILIYOPITA, Malima na wachezaji wenzake wa Yanga walipata faraja baada ya Francis Kifukwe akiongozana na mfadhiri Abbas Gulamali kutua mjini Kampala na kuwapa dola 200 kila mmoja. Mbele yao kuna mechi ya nusu fainali. Je, itakuwaje?
FURAHA ilikuwa ni kubwa kupita kiasi, tulivuka hadi kuingia nusu fainali bila ya kupata posho na maisha yalikuwa magumu sana. Dola 200 kwa kila mchezaji kwetu ni sawa na milioni mbili.
Tulikuwa na furaha sana na kila mtu niliyepishana naye alikuwa akiimba nyimbo kuonyesha ana furaha kubwa. Tuliishi angalau maisha mapya na mechi yetu ya nusu fainali ilikuwa ni dhidi ya Vital’O ya Burundi.
Wale Warundi walikuwa fiti sana, kila mmoja alikuwa akihofia kukutana nao. Lakini Yanga yetu, ilitaka kukutana na kila timu, hakuhakikishia kipindi kile hata wangekuja Man United wangesema kazi haikuwa ndogo, hata kama wangetufunga lakini wangelala na viatu.
Jamaa walikuwa fiti halafu walicheza kwa kasi sana, lakini nasi tulijibu mashambulizi. Tulianza kupata bao sisi katika dakika ya 19, Kally Ongala aliwatoka na kupachika bao safi sana.

Jamaa waliendelea kutushambulia mfululizo hadi walipopata bao katika dakika ya 31, nakumbuka alifunga jamaa anaitwa Olivier Nyangeko . Unajua nilikuwa naandika kila baada ya mechi, (Malima anatoa kitabu na kumhakikishia mwandishi kuwa kweli yeye ni mtu wa data). Baada ya bao hilo jamaa waliendelea kulisakama lango letu.
Vital’O walifanikiwa kupata bao la pili katika dakika ya 51, Saleh Omar akafunga bao la pili. Lakini ‘hatukulowa’ tulijua tuko vitani na tulitaka kwenda fainali. Tuliendelea kupambana na dakika ya 78, nikawazisha.
Ulikuwa ni mpira wa kona, kawaida nilikuwa nafunga mabao mengi ya vichwa lakini siku hiyo nilifunga kwa mguu. Baada ya kona kuchongwa, kipa alipangua na ule mpira ulinikuta mimi.
(Malima anavuta pumzi kwa nguvu halafu anatabasamu), aisee! Nilipiga shuti kali ambalo sijawahi kupiga maishani mwangu na sidhani kama nitapiga tena. Ngoma ikajaa wavuni na mimi nikakimbia kwenye kibendera.
Bao letu lilionekana kama kuwachanganya Vital’O, kila mmoja mchezaji alianza kumlaumu mwenzake. Sisi tuliona ulikuwa ni wakati wa kuwamaliza maana jamaa walikuwa kama wamekubali vile.
Tuliendelea kushambulia kwa kasi kubwa, Lunyamila na Kally walikuwa aakiwasumbua sana mabeki wa Vital’O ambao walitumia muda mwingi wakiwachezea faulo.
Mimi huku niliendelea kutandaza ubabe kwa mafowadi wao, niliwapa maneno ya kuwaudhi lakini nilicheza kindava ili kuwapoza. Mara nyingi niliwaita watoto ili kuwaudhi.
Ilionekana kama tutakwenda katika dakika 30 za nyongeza, kwani hadi dakika 87 kulikuwa hakuna bao tena. Kila upande ulitaka kwa kushinda lakini mimi niliona kama jamaa walikuwa tayari wameshachoka ingawa walisifiwa kwa kuwa na pumzi na stamina tokea kuanza kwa michuano hiyo.
Huku mashabiki wakionekana wanasubiri kwa hamu dakika ya 30 za nyongeza, Said Mhando alitufungia bao maridadi katika dakika za 90. Uhakika tulikuwa tumesonga hadi fainali.
Tulishajua tunacheza fainali dhidi ya wenyeji SC Villa ambao waliingia baada ya kuwafunga Rayon Sports kwa mabao 2-0. Nakumbuka waliotupia wavuni ni Hassan Mubiru na Charles Kayemba.
Jamaa nao walikuwa fiti sana, halafu ndiyo wenyeji wa michuano hiyo na walichotaka ni kulibakiza kombe nyumbani kwao. Hawakuwa na kitu kingine zaidi.
Lakini kiasi fulani nao waliingia hofu kwetu kutokana na namna tulivyokuwa tumeanza michuano hadi kufikia hapa tulipo. Waliona kama tulibadilika na kuwa hatari sana.
Pamoja na hivyo, walikuwa na hofu kubwa na washambuliaji wetu hasa Kally na Lunyamila aliyekuwa gumzo kubwa pale Kampala kutokana na kazi aliyokuwa anaifanya.
Pia walijua kwenye ulinzi, nilisimama mimi pamoja na watu kama Shabani Ramadhani, kiungo tuna mtu kama Salvatory Edward, haikuwa kazi lahisi.
Wangesema hao Villa wawalete hata baada ya kuwa tumemaliza mechi ngumu dhidi ya Vital’O, sisi hatukuwa na shida. Tungepambana nao na kuwachakaza.
KAZI ni kubwa, Yanga imetinga fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (sasa Kombe la Kagame) dhidi ya wenyeji SC Villa ya Uganda. Malima na wachezaji wenzake wakawa tayari kupambana. Je, watawaweza wenyeji na nini kitatokea siku ya fainali. USIKOSE MWENDELEZO.

Neno ‘mwisho’ ni rafiki na adui wa Cristiano Ronaldo

Na Arone Mpanduka-Radio Tumaini
Nimetumia muda mwingi sana kumchunguza Cristiano Ronaldo na matukio yake na leo hii nimepata kitu fulani cha kukuelezea juu ya hilo.Je unafahamu kwamba neno ‘mwisho’linaweza kuwa rafiki na wakati huohuo pia kuwa adui mkubwa kwa nyota huyu? Fuatana nami katika hilo.
NI MTOTO WA MWISHO KUZALIWA
Cristiano Ronaldo ni mtoto wa mwisho kuzaliwa katika familia ya mzee Jose Dinis Aveiro ambaye sasa ni marehemu.Katika familia hiyo Ronaldo ana kaka yake mmoja mkubwa aitwaye Hugo sanjari na dada zake wakubwa wawili Elma na Liliana.Kitendo cha kuzaliwa wa mwisho kilimfanya apendwe na wazazi wake ambapo ilimlazimu mama yake mzazi Maria Alveiro kumpa jina la Ronald Reagan, jina ambalo lilikuwa la rais wa Marekani kwa wakati huo.Hiyo ndiyo sababu ya Cristiano Alveiro kuitwa Cristiano Ronaldo ambapo jina Ronaldo linatokana na ‘Ronald’.
AWEKA REKODI KWENYE MECHI YA MWISHO YA LIGI
Katika mechi ya mwisho wa msimu wa ligi wa 2011-2012, siku ya Mei 13 mwaka 2012, Ronaldo aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao katika kila mechi hasa kwa ligi kuu ya soka ya Hispania.Aliweka rekodi hiyo baada ya kufunga bao kwenye mechi hiyo dhidi ya Mallorca na kushangilia vizuri ubingwa wao ambao walikuw awameutangaza kabla ya ligi kumalizika.
ALIKOSA BAO MUHIMU KATIKA DAKIKA ZA MWISHO
Katika dakika ya 90 Cristiano Ronaldo alishindw akufunga bao muhimu ambalo pengine bila ubishi lingeipeleka Ureno katika hatua ya fainali ya euro 2012 baada ya shuti lake kukosa muelekeo wakati walipokuwa wakicheza na Hispania katika mechi ya nusu fainali.Kitendo cha kukosa bao katika dakika za mwisho kwa namna moja ama nyingine kiliipeleka Ureno kwenye muda wa nyongeza na baadae mikwaju ya penati ikawaondoa Ureno kwenye michuano.
ALIPENDA KUPIGA PENATI YA MWISHO AMBAYO HAKUPIGA
Baada ya dakika 120 kumalizika za mchezo kati ya Ureno na Hispania, iliamriwa zipigwe penati tano tano ili kupata mshindi.Cristiano Ronaldo aliomba awe mtu wa mwisho kupiga penati.Lakini kinyume na maratajio wareno wenzake Joao Moutinho and Bruno Alves walishindwa kukwamisha wavuni mikwaju yao ya penati na kufanya kusiwe na ulazima kwa Ureno kumalizia penati ya tano ambayo ilipaswa kupigwa na Ronaldo.
Hatua hiyo ilimazilika kwa Hispania kushinda kwa penati 4 dhidi ya mbili za Ureno.
ALIACHWA NA NDEGE BAADA YA KUTAKA KUKAA SITI ZA MWISHO
Siku moja baada ya Ureno kutolewa katika michuano ya euro 2012 huko Poland na Ukraine, Cristiano Ronaldo aliachwa na ndege iliyokuwa inawarudisha wachezaji nchini Ureno.
Wakati wakiwa uwanja wa ndege wa Ukraine, Cristiano Ronaldo alimtaarifu mtu anayepanga safari kwamba angependa kukalia moja kati ya siti za mwisho za ndege hiyo.
Baada ya kukubaliwa Ronaldo aliomba ruhusa ya kwenda kwenye mgahawa kuchukua vyakula vyake huku akimsisitiza muhusika wa usafiri wa anga kwamba kama ndege inataka kuondoka basi amshitue.
Matokeo yake ni kwamba ile ndege iliondoka na kumuacha Cristiano Ronaldo akishangaa shangaa kwenye uwanja wa ndege.
SAFARI YAKE YA SOKA KWA UJUMLA
Ronaldo alianza maisha ya soka katika klabu ya soka ya Andorinha ambako alicheza kwa miaka miwili kabla ya kuhamia katika timu ya soka ya Clube Desportive Nacional.Mwaka 1997 alitimkia katika klabu ya soka ya Sporting Club de Portugal.Umahiri wake ulimvutia kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson ambaye mwaka 2003 alimsajili kwa ada ya paundi milioni 12.24 ambazo ni sawa na euro milioni 15 na wakati huo Ronaldo alikuwa na umri wa miaka 18.Msimu uliofuata Ronaldo alishinda taji la FA na na baadae alishiriki fainali za EURO za mwaka 2004 akiwa na taifa lake la Ureno na kwenye michuano hiyo nyota huyo alifunga bao lake la kwanza katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Ugiriki na aliisaidia Ureno kutinga fainali.Ronaldo alikuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo za PFA na FWA akifanya hivyo mwaka 2007 na mwaka 2003 alishika nafasi ya tatu kwenye kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa dunia wa mwaka.Mwaka 2008 nyota huyo alishinda taji la klabu binga barani Ulaya akiwa na Manchester United na alitangazwa kuwa mshambuliaji bora pamoja na mchezaji bora wa michuano hiyo na pia alikuwa mfungaji bora wa michuano hiyo na kutwaa kiatu cha dhahabu.Ronaldo pia aliwahi kuweka rekodi nzuri ya kufunga bao kwa kupiga shuti umbali wa yadi 40 wakati timu yake ya Manchester United ilipokuwa ikicheza na FC Porto katika mchezo wa robo fainali wa Chamions League mwaka 2008.Hii ilimfanya bingwa mara tatu wa tuzo ya Balon dOr Johan Cruyff kusema kwenye mahojiano maalum kwamba “Ronaldo ni bora kuliko George Best na Denis Law ambao walikuwa wachezaji wakubw akatika historia ya Manchester United”.
MAISHA BINAFSI
Baba mzazi wa Ronaldo Jose Dinis Alveiro alifariki dunia mwaka 2005 kwa tatizo la ini ililotokanana unywaji wa pombe kupita kiasi na wakati huo alifariki akiwa na umri wa miaka 52 huku mwanae Ronaldo akiwa na miaka 20.Ronaldo ana maduka makubwa mawili ya kifahari yote yakiwa nchini Ureno ambapo moja lipo mjini Lisbon na lingine lipo pale Madeira.Maduka hayo huuza bidhaa mbalimbali hasa mavazi yenye lebo yake ya CR7.Hadi kufikia mwezi Agosti mwaka 2010,Cristiano Ronaldo alifikisha jumla ya mashabiki milioni 10 katika mtandao wa kijamii wa Facebook.Ronaldo awali alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamitindo wa Uingereza Alice Goodwin na baadae Gemma Atkinson na mwanzoni mwa mwaka 2010 alikuwa na mahusiano na mwanamitindo mwingine kutoka nchini Urussi Irina Shayk.
mpanduka@yahoo.com(0713 896320)

JE HII NDIO PENATI BORA KUWAHI KUPIGWA ?

Hallo Shaffih mi nimfuatiliaji mzuri sana wa website yako naweza sema ndio bora au namba 1 kwa habari za sports Tanzania,jana uliweka video zinazoonyesha baadhi ya best penalties zilizowahi kupigwa ukauliza ipi bora?kwa upande wangu mimi mtazame dogo Ezequiel Calvante wa Spain kwenye hii hink  http://www.youtube.com/watch?v=6ObuMb1KCrk  is the best penalt ever.

Mimi mdau wa Shaffih Dauda in sports.
Ukraine

KALI YA LEO: SHABIKI MKUBWA WA ARSENAL NA MTANGAZAJI WA CNN PIERS MORGAN AMTISHA ROBIN VAN PERSIE
CRISTIANO RONALDO AWAZIDI MESSI NA BECKHAM KWA KUWA NA MASHABIKI WENGI FACEBOOK


Hii ndio listi ya wachezaji maarufu zaidi kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook,Baada ya kuibuka wa pili kwa wachezaji wenye fedha nyingi zaidi nyuma ya David Beckham - Cristiano Ronaldo ameonekena kuwa maarufu zaidi kwenye mtandao huo kwa kuwa na mashabiki millioni 46.3, huku akifuatiwa na mpinzani wake Lionel Messi. Tajiri Beckham amekata nafasi ya tatu huku Kaka na Iniesta wakifunga Top 5.
 
1) Cristiano Ronaldo - 46.3m
2) Lionel Messi - 37m
3) David Beckham - 19.5m
4) Kaka - 17.3m
5) Andres Iniesta - 10.2m
6) Fernando Torres - 10.1m
7) Wayne Rooney - 9.4m
8) Steven Gerrard - 7.1m
9) David Villa - 6.1m
10) Mesut Ozil - 5.7m

Thursday, July 5, 2012

JOAO MOUTINHO NA WACHEZAJI WENZAKE WANNE WALIOPANDA THAMANI BAADA YA EURO 2012

Michuano ya Euro 2012 ilikuwa mizuri sana labda uwe muitaliano, na baada ya kuangalia mataifa 16, mechi 31 na magoli 76, Spain wakatawazwa kuwa mabingwa wa ulaya tena.

Wachezaji kama Andres iniesta na Jordi Alba ambao walicheza vizuri sana kwenye mchuano hiyo huku wakicheza kwenye kila mechi, lakini hawakuwa wahispania hao pekee ambao waling'arahuko Poland na Ukraine.

Poland, Russia, Sweden na Denmark wote waliichangamsha michuano hii kwenye hatua ya makundi, lakini pia walikuwa na achezaji ambao walionyesha viwango jinsi vilivyo hatari katika harakati za kusaidia mataifa yao.

Tukiwa nalo hilo kichwani, na ufunguzi wa dirisha la usajili likifunguliwa, hawa ni wachezaji watano - nje ya vikosi vilivyocheza fainali  ambao waliongeza thamani yao kwenye soko la usajili kupitia michuano ya Euro 2012.

ALAN DZAGOEV - KIUNGO MSHAMBULIAJI -URUSI


Akiwa amefunga mabao matatu kwenye hatua za makundi, Alan Dzagoev aljidhihirisha kuwa mmoja ya vijana wadogo wenye future nzuri kwenye soka baada ya kuisadia Russia kupata ilichopta kwenye hatua ya makundi.

Dzagoev, ambaye anaitumikia CSKA Moscow, alianza kufanya balaa kwenye mchezo wa kwanza wa michuano hiyo akiiongoza Russia kuitandika Czech 4-1. Lakini kwa bahati huo ndio ulikuwa ushindi wa mwisho kwa vijana hao kutoka ulaya mashariki.

Alifunga kwenye mchezo dhidi ya Poland ambao uliisha kwa sare ya 1-1 na kuonyesha kiwango kikubwa, alikuwa na control kubwa ya mpira na jicho zuri la kupiga pasi kwenye michezo yote mitatu

Akiwa amebakiza miezi sita kwenye mkataba wake, thamani yake kwenye soko la usajili  haitakuwa kubwa sana kwa sasa. CSKA watafanya kila kitu kuweza kumfunga na mktaba wa muda mrefu.

Ikiwa watafanikiwa, wataweza kupandisha thamani ya mchezaji huyo mpaka kufikia £12million. Ikiwa watashindwa watamuuza kwa bei ya kawaida kuliko inavyopaswa kipindi kijacho cha kiangazi.

THEODOR GEBRE SELASSIE - BEKI WA KULIA - CZECH


Czech Republic walifika robo fainali za Euro, japokuwa walifungwa mabao 4-1 na Urusi, baada ya hapo wakaenda kuwafunga Ugiriki 2-1 na Poland 1-0.

Moja ya sababu kubwa ya kuboreka kwa kiwango chao ilikuwa ni fomu nzuri ya beki wao kulia Theodore Gebre Salassie, ambaye siku kadhaa kabla ya michuano alikubali kuhamia Werder Bremen kutoka Slovan Liberec.

Inaonekana ilikuwa faida kubwa kwa timu hiy ya Bundesiliga kukamilisha uhamisho wa mchezaji huyo kabla ya michuano ya Euro 2012, wakiwa wamelipa $1.6million kwa ajili ya kupata huduma za beki huyo mwenye kukaba na kushambulia kwa kasi.

Kutokana kiwango chake alichokionyesha akiwa Czech, kwa hakika thamani yake ingekuwa imepanda zaidi ya aliyonunuliwa.

Kwa kiwango alichonacho, nguvu na kuwa nautayari wa kusapoti mashambulizi kwenye tatu ya mwisho - Gebre Selassie kwa sasa ana soko kubwa. Kwa hakika akiendelea kuwa hivi alivyo Bremen watapata fedha nzuri sana kama wataamua kumuuza.


ANDRIY YARMOLENKO - WINGA - UKRAINE
Mfumo wa Ukraine wa kiufundi, ulikuwa ume-based. kwenye kushambulia zaidi, kupitia mawinga wao.

Huku winga anyetumia mguu wa kushoto Andriy Yarmolenko akicheza upande wa kulia  na winga anayetumia mguu wa kushoto Yevhen Konoplyanka akicheza winga ya kushoto, Ukraine mara kadhaa walikuwa wakiwatumia mawinga hawa kwenye tatu ya mwisho kutengeneza mipira ya kupiga mashuti ya kupiga krosi.

Huku wachezaji wengi kwa ujumla wakikosa kipaji cha kuchezea mpira kulikuwa kizingiti cha Ukraine kusonga mbele, lakini Yarmolenko, kipekee, alikuwa mchezaji aliyecheza vizuri sana ambaye alionekana muda wowote angeweza kuwadhuru wapinzani.

Akiwa mtulivu alikuwa akiingia katikati kupiga mashuti au kwenda pembeni kuruhusu kutoa sapoti ya kulisha washambulaiji wa kati, Yarmolenko alikuwa mzuri katika kumiliki mpirra na alikuwa mchezaji wa kwanza wachezaji wenzie walikuwa wakimtafuta mara walipopata mpira ili aweze kufanya utundu wake.

Yarmolenko kwa sasa anaichezea Dinamo Kyiv kwenye nchi yake ya ukraine, ambapo huwa anachezeshwa katikati nyuma ya mshambuliaji wa kati. Atakuwa na timu kibao zitakazowatuma mawakala ikiwa taonyesha nia ya kuondoka kwenda kucheza nje ya mipaka ya nchi hiyo.

Kyiv sasa watakuwa wakitegemea ada kubwa ya uhamisho baada ya kiwango alichoonyesha Euro.

JOAO MOUTINHO - KIUNO WA KATI - URENO

Moja kati ya wachezaji wachache kwenye michuano hii wenye uwezo wa kupiga pasi vizuri tu kama ilivyo kwa viungo wa Spain, Joao Moutinho alikuwa nyota iliyoangaza mafanikio ya Ureno kwenye Euro 2012, na ikiwa ataamua kuhama kutoka klabu yake ya sasa ya Porto, atakuwa hajajitendea kitu kibaya kwani kwa hakika atazivutia timu nying sana zenye majina makubwa.

Tofauti na wachezaji wengine kwenye listi hii, Moutinho tayari alikuwa na bei kubwa kabla ya michuano baada ya kucheza vizuri kwa misimu kadhaa akiwa na Porto.

Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa za vilabu vya Uingereza Manchester United na Tottenham Hotspur zikiwania saini yake kwenye soko la usajili la hivi sasa 0 huku thamani yake ikitajwa kufikia paundi millioni 32 .

MATS HUMMELS - BEKI WAKATI - UJERUMANI

Hatimaye tumekutana na moja kati wachezaji walioifanya Ujerumani kuwa tishio kwenye michuano ya Euro 2012 - huyu ni beki wa kati Mats Hummels.

Beki huyo wa Borussia Dortmund amekuwa na michuano mizuri. Alizuia kwa kiwango cha juu sana huku hali ya kuweza kuongoza safu ulinzi akionekana kuwa nguvu na ufundi.

Ujerumani wakati wanaingia kwenye michuano hii, safu ya ulinzi ndio iliyoonekana kuwa dhaifu, lakini chini ya ulinzi wa Hummels, Ujerumani walionekana kubadilika na kuwa imara sana kwenye safu ya ulinzi.

Amekuwa akionekana kuwa na thamani ya £20million kwa sasa, Hummels hajaonyesha nia yoyote kuondoka Dortmund, pia klabu yake haijaonyesha nia ya kumuuza.

Ukiangalia kiwango chake kwenye Euro 2012, umri wake na potential aliyonayo huko mbeleni inaonekana kipaji chake kitazidi kukuana kama ikiwa hivyo basi anaweza kuja kuvunja rekodi ya usajili kwa mabeki ambayo kwa sasa inashikiliwana Rio Ferdinand ambayo alisajiliwa na United kwa gharama ya £29million.

KUTOKA KWA GEORGE BEST MPAKA CRISTIANO RONALDO - JEZI NO.7 YA MAN UNITED YAMUANGUKIA VALENCIA KUFUTA NYAYO ZA AKINA CANTONA AU AKINA OWEN?Kwenye soka la dunia kuna jezi chache zilizo na historia kubwakuliko jezi namba 7 ya Manchester United, ikiwa imevaliwa na mastaa wakubwa sana walipokuwa pale Old Trafford, baada ya kuondoka kwa Micheal Owen sasa namba hiyo imeangukia kwenye umiliki wa Luis Antonio Valencia.

Tanguwakati wa msimu wake wa kwanza pale Theatre of Dreams, Raia huyu wa Ecuador amekuwa kipenzi cha mashabiki kwa sababu nyingi. ni mchezaji anayetoa mchango mkubwa sana kuchangia ushindi wa United, na nguvu na uwezo mkubwa kukaba.

Uamuzi wa kumpa mchezaji huyo wa Wigan jezi namba 7 utampa umaarufu zaidi Valencia   kwa mashabiki wa klabu hiyo ambao wengi wamekuwa wakimpenda, wakati huo huo atakuwa na mzigo mkubwa wa kuweza kufuata nyayo za baadhi ya wachezaji wakubwa waliowahi kuivaa jezi hiyo.

Katika tukio hili kubwa kwa career ya Valencia - ebu tujikumbushe wachezaji waliong'ara na waliovurunda wakiwa wamevaa jezi namba saba kwenye kikosi cha Manchester United.

WALIOFANYA VIZURI NA JEZI NAMBA 7
GEORGE BEST
Ingawa alikuwa anacheza sehemu moja kama ilivyo kwa Valencia - tofauti yao kubwa ni kwamba Best alikuwa maarufu zaidi kwa kuandikwa kwa mambo ya nje ya uwanja kuliko dimbani.

Alikuwa malaya mwenye kubadilisha wanawake kila kukicha huku akiwa mlevi namba moja, Best alikuwa kila siku kwenyekurasa za mbele za magazetikutokana na staili yake ya maisha, akiwa kwenye mahusiano na wasichana wa jumba la Playboy, kamari ulikuwa ndio mchezo wake huku akitumia vibaya fedha nyingi alizokuwa akipata kwenye manunuzi ya magari na vitu vingine vya anasa.

Pamoja na matukio yake yote uwanjani - Best alikuwa hatari dimbani. Alifanya mpira uonekane rahisi kucheza, akititirika kutoka winga ya kushoto na kuwapita mabeki shukrani kwa uwezo wake mkubwa wa kuchezea mpira na kasi. Lakini uwezo wake wa kuchezea miguu yote miwili ulimfanya atishe zaidi kwa kushindwa kutabirika - jambo ambalo lilimsaidia kufunga mabao mengi zaidi.

Wakati wa enzi za Best pale United, makombe waliyoshinda ni mataji mawili ya ligi na ngao mbili za hisani, wakati alimaliza kama mfungaji bora kwenye misimu sita mfululizo kabla ya kuondoka Old Trafford mwaka 1974 akiwa na miaka 27. Akaenda kuzichezea klabu nyingine 14 na hatimaye akastaafu mwaka 1984 na kufariki mwaka 2005 baada ya kuugua kwa muda mrefu matatizo ya ini.


BRYAN ROBSON
Hakukuwa na jambo kubwa ambalo Bryan Robson alishindwa kufanya, alikuwa mchezaji aliyekamilika na aliweza kuukabili mchezo na kuubadilisha huku akiongoza vizuri timu yake.

Maarufu zaidi kama nahodha aliyeitumikia kwa muda mrefu zaidi klabu hiyo kwenye historia, Robson alikuwa maarufu zaidi kwa kuwa kiungo ambaye alikuwa anafunga mabao mengi zaidi - lakini uwezo ake wa kukaba, stamina aliyonayo, na hali ya ushindani ilimfanya awe mchezaji wa aina yake.

Mwaka 1983 Robson alikuwa ndio nahodha wa kwanza kiingereza kubeba kombe la FA Cup kwa United, wakati mwaka uliofutia uhamisho wa kwenda Juventus nusra ukamilike. Ingawa aliendelea kubaki Old Trafford mpaka mwaka 1994, akiisaidia timu yake kubeba kombe la UEFA Cup mjini Rotterdam in 1991, kwa kuwafunga Barcelona kwenye fainali.

Akiitwa 'Nahodha mwenye maajabu', alicheza mechi 461 akiwa na United, akatia kambani magoli 99, huku mchezo wake wa mwisho dhidi ya Coventry City mwezi May 1994 uliisha kwa sare tasa. Amekuwa akisifiwa kwamba ni bora kuliko wote - kwa kura zilizopigwa na wachezaji wa zamani wa United mwaka 2011.

ERIC CANTONA
'Mfalme Eric' ni mmoja kati ya wachezaji aliocheza kwa vipindi vifupi na kupata mafanikio wakiwa wamevaa jezi namba 7 ya Manchester United.

Cantona aliipokea jezi namba 7 kipindi cha kiangazi akiwasili kutokea Leeds United - uhamisho ambao ulileta maneno kwamba alikuja kuchukua nafasi ya Robson aliyekuwa akiendea mwishoni. Robson alibadilishiwa jezi na kupewa namba 12 na no.7 akachukua King Eric ambaye alikuja kufanya mambo makubwa sana akiwa na United - akiwasumbua mabeki kwa miaka mitano mpaka alipokuja kustaafu mwaka 1997.

Akitokea kutoka kwa mahasimu wakubwaLeeds, Cantona hakuchukua muda mrefu kuweza kupazoea Old Trafford. Kwa fomu aliyokuwa nayo Mark Hughes na Brian McClair pamoja na kuumia kwa Dion Dublin, kulimuhakikishia nafasi ya kucheza sana na kwa bahati nzuri akawa mchezaji wa kwanza kushinda taji la ligi kuu mara mbili mfululizo na klabu mbili tofauti.

Pamoja na mafaniko yake yote kwenye klabu hii, Cantona anakumbukwa sana kwa kitendo chake cha kumpiga shabiki wa Crystal Palace kwa staili ya kung-fu wakati alipotolewa nje kwa kadi nyekundu.

Cantona alifungiwa kwa miezi nane kucheza soka duniani kote huku akipigwa faini tofauti, na baadae akajaribu kuondoka United kwa mara kadhaa. lakini alibaki OT na kwenda kushinda makombe manne ya premier league, mawili ya FA na ngao tatu za hisani - pia alikuwa mchezaji bora namba tatu wa dunia mwaka 1993.


DAVID BECKHAM
Kama George Best alileta maisha ya ustaa kwa wanasoka, David Beckham alikuwa master wa maisha namna hiyo. Ndoa yake kwa muimbaji wa kundi la Spice Girls ndio ilikuwa moja ya chanzo kikubwa cha ustaa wake kukua, na kwa mujibu wa Sir Alex Ferguson suala la kuoa halikuwa zuri kwa avid Beckham.

Mapaparazi na wanahabari walikuwa wakimfuaa Beckham kila mahali alipokwenda huku kiungo huyo wa England akawa maarufu kupitiliza zaidi huku akifanya maajabu uwanjani - tukio la kukumbukwa zaidi ni lile goli alilofunga kati kati mwa uwanja dhidi ya West Ham mwaka 1996.

Beckham alianza kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza cha United kwenye msimu wa 1996-97 mpaka katikati mwa miaka ya 2000 alikuwa atayari ameshabeba makombe manne ya premier league, huku la tatu kati ya hayo likiwa la kukumbukwa zaidi kwa sababu lilikuwa ni moja kati ya matatu waliyobeba United mwaka 1999.


 CRISTIANO RONALDO
Mchezaji wa kwanza wa kireno kuichezea United, akiwa amesajiliwa haraka baada ya David Beckham kuondoka kwenda Madrid.

Usajili wake uliogharimu United paundi millioni 12 uliwashangaza washabiki wengi wa United, lakini dakika 30 alizocheza kwenye mechi dhidi ya Bolton ambayo United walishinda kwa 4-0 - ziliwapa majibu yote waliyohitaji kuhusu bei yake.

 Pamoja na kuanza kucheza kibafsi zaidi kwenye miaka yake miwili ya kwanza akiwa United, lakini aliimarika kiakili na kimwili na kuanza kuisadia klabu yake kuanza kukusanya mataji kama lilivyo ada. Ronaldo akishirikiana na wachezaji wenzie kama akina Wayne Rooney waliiwezesha United kushinda makombe matatu ya premier league, kombe la klabu bingwa ya ulaya na dunia, pamoja na makombe mengine manne tofauti - huku Ronaldo akifunga mabao 127 huku akitoa assits nyingi zilizochangia mafanikio makubwa kwa Manchester United.
Mafanikio ya Ronaldo akiwa na United hayakuhusiana na timu tu baada ya kuwa mchezaji wa kwanza premier league kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa dunia wa FIFA, na mchezaji wa kwanza wa United kushinda Ballon d'Or tangu Best alivyoshinda mwaka 1968.

Ronaldo akiuja kuwaachia huzuni mkubwa mashabiki wa United baada ya kufuata nyayo za Beckham  kujiunga na Real Madrid mwezi June 2009 baada ya Real kulipa ada ya uhamisho iliyoweka rekodi ya dunia ya paundi millioni 80.

WALIOVURUNDA

MICHEAL OWEN
Kutoka siku ya kwanza Micheal Owen alikuwa akipigania nafasi ya kuwa mchezaji anayeanza kwenye kikosi cha kwanza cha United. Ukweli wa kwamba tayari alishakuwa akifikiriwa kwamba ni gwiji wa soka wa Liverpool lilikuwa tatizo la kwanza, lakini pia kushindania namba na Wayen Rooney na Dimitar Berbatov.

Majeruhi pia yalikuwa ndio kikwazo kikuu kwa Owen akiwa na United. Kuibuka kwa Danny Welbeck na Federico Macheda pia kukatishia uwepo wa mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid, ingawa goli la dakika za majeruhi dhidi ya Man City pale Old Trafford litamfanya akumbukwe sana mashtani wekundu.

Pia alikuwa nyota wa mchezo kwenye mechi ya mabingwa wa ulaya dhidi ya Wolfsburg ,wezi December 2009 baada ya kufunga mabao matatu muhimu, ingawa majeruhi yaliendelea kumuandama msimu huo wote na akakosa miezi mitatu ya msimu.

Kwenye msimu wa pili akiwa na United alishinda medali yake ya kwanza ya premier league akicheza mechi 11 tu. Ingawa msimu uliopita Owen alicheza mechi moja tu kwa msimu mzima, na hatimaye United wakaamua kutomuongezea mkataba mpyana huo ndio ukawa mwisho wa wake na United.

Owen anawakilisha kundi la wachezaji wanne waliovaa jezi namba 7 kwa united ambao walivurunda wakiwemo wafuatao.

WALIOCHEMSHA WAKIWA WAMEVAA JEZI NO.7
1 - Micheal Owen

2 - Ralph Milne

3 - Keith Gillespie

4 - Ashley Grimes