Search This Blog

Saturday, October 15, 2011

TFF YATOA MAJIBU KUHUSU KAMATI YA LIGI


JAMES DANDU JR. KWENYE SOKA SWEDEN

KWANINI MANCHESTER UNITED NDIO TIMU ILIYOPIGIWA MASHUTI MENGI KULIKO TIMU YOYOTE KWENYE EPL?


Wakiongoza ligi, hawajufungwa, uongozi mzuri wa tofauti ya mabao, so far Manchester United sio timu ya kuwa na wasiwasi na performance yao msimu huu.

Defence yao inaweza kuchukua sifa katika uongozi huu wa timu yao, wameruhusu mabao matano tu kwenye mechi 7, ni rekodi ya kuvutia, tena ukizingatia matatizo ya majeruhi kwenye safu ya ulinzi tena kipindi hiki ambacho viraka kama John O’shea na Wes Brown wakiwa wameondoka kwenda Sunderland.

Pamoja na rekodi nzuri kwenye safu ya ulinzi, United msimu huu ndio timu iliyopigiwa mashuti mengi kuliko timu yoyote kwenye ligi, wakipigia mashuti 97 langoni mwao katika michezo 7.

TAKWIMU

Kwenye graph hapo juu takwimu zinaonyesha United wame-concede shots 13 au zaidi katika kila mchezo.Mchezo dhidi ya Stoke City ndio mchezo pekee ambao United hawakuruhusu shots nyingi.

Pia kwenye graph nyingine hapo chini inaonyesha katika michezo saba, United wameruhusu mashuti mengi langoni mwao kuliko waliyopiga.


MAHALI YALIPOPIGWA MASHUTI



KWANINI?

Turudi kwenye swali-kwanini? Kupitia ushahidi wa takwimu unaonyeshwa hapo juu, kwanini United wameruhusu kupigiwa mashuti kutoka kwenye umbali mrefu? Haya ni baadhi ya mambo yanayoweza kuwa majibu kwanini United wamepigiwa sana mashuti mengi langoni mwao.

1: FIKRA ZA DAVID DE GEA KUWA NA UDHAIFU KWA MIPIRA YA MBALI?

Baada ya kufungwa bao la mbali na Edin Dzeko katika mechi ya ngao ya hisani, watu wengi walianza kuhoji udhaifu wa De Gea katika kuzuia mipira ya mbali.Kupitia system ya Opta takwimu zinaonyesha De Gea alikuwa na rekodi mbovu katika kuzuia mashuti ya mbali msimu uliopita katika La Liga.

Je ni kweli De Gea ni mdhaifu kwa mipira ya mbali? Katika kesi hii sio rahisi kupata jibu sahihi ukizingatia kipindi kifupi alichocheza, lakini la kuzingatiwa ni kwamba wapinzani wanafikiri De Gea ana udhaifu huo, na ndio maana wamekuwa wakijaribu kumtungua kutokea umbali wa 20+ yards.Hitimisho ni kwamba Da Gea bado hajafungwa goli nje ya box katika premier league.

2: MAJERUHI KWENYE ULINZI

Rio Ferdinand na Nemanja Vidic wote wamekuwa majeruhi, Chris Smalling na baadae Antonio Valencia wamekuwa wakichezeshwa katika nafasi beki wa kulia.United defence wame-cope vizuri na hali hii ya majeruhi, lakini swali ni kwamba je wameweza kujenga partnership nzuri kwenye ukuta wao, particularly wakati beki wa kati mmoja anapoenda mbele mwingine anakuja na ku-cover, kama goli la Fernando Torres @Old Trafford lilivyoonesha.Ferdinand na Vidic wamekuwa na wakitengeneza partnership nzuri ya namna hiyo tofauti na Phil Jones na Evans.

3: HAKUNA KIUNGO MZURI MZUIAJI

Kuna utata whether Micheal Carrick ni kiungo mzuiaji au sio, lakini ni mzuri zaidi ya wote wawili Anderson na Tom Claverley katika uzuiaji, Ferguson amekuwa akipenda midfield partnership katika msimu huu.Mtindo wa kuvutia wa 4-4-2 wa United msimu uliopita ndio ulikuwa chanzo cha mchezo mzuri wa United msimu uliopita kupitia viungo Micheal Carrick, Paul Scholes, Fletcher, na Anderson ambao Ferguson alipenda kuwatumia kama two passer na two runners kwa pamoja.

Cleverley ni kiungo mzuri sana, akicheza zaidi kwa mtindo wa kushambulia zaidi kuliko kiungo yeyote aliyetajwa hapo juu, na kumtumia yeye na Anderson kunaacha gap kubwa katika midfield na defence.Carrick, akiwa yupo mbali na kuwa mtu mzuri kufanya tackling, lakini bado kuna wengine wanm-favour yeye kucheza katika nafasi, yupo vizuri katika kufanya tracking and intercepting.United wanaweza kuwa bora bila yeye, lakini katika uzuiaji sio wagumu kabisa.

4: ROONEY HAFANYI KAZI KUBWA?

Kama Stewart Robson alivyosema hivi karibuni, Rooney akiwa katika form nzuri kama true namba 10 amekuwa akimbii sana bila kuwa na mpira.Alikuwa anafanya kazi kubwa kipindi wakati akicheza pembeni kipindi United ilipokuwa dominated na Cristiano Ronaldo na alifanya kazi kubwa zaidi alipokuwa anatumika kama mshambuliaji pekee.Sasa, mfano mzuri wa aina yake ya mchezo kuwa madhara ilikuwa katika fainali ya Champions league dhidi ya Barca, matatizo ya safu ya kiungo cha United yalianzia kutokana na aina hii mchezo, Rooney akiwa hashuki sana kuja kukaba na ku-cover, matokeo yake viungo walikuwa wakifanya kazi kubwa mbele kwenye pitch, na wakiacha gap kubwa nyuma yao.

Sababu nyinginezo.

Performance ya katika kombe la ngao ya hisani ilionyesha utofauti mkubwa kutoka kwa United ya msimu uliopita.In 2010/11walikuwa well defined na organized vizuri.Sasa, wanacheza zaidi wakiwa katika mtindo wa free-flowing and flexible, matokeo yake wanakuwa wanashambulia zaidi kwa pamoja katika ushirikiano mzuri lakini wakiachia nafasi zaidi kwa wapinzani katika midfield.Katika mtindo wa uchezaji wa sasa wachezaji kama Ashley Young na Nani watakuwa favoured kuliko Ji sung Park na Antonio Valencia wachezaji ambao ni wazuri katika kucheza kwa nidhamu kubwa ya ukabaji.

HITIMISHO

Sifa ya De Gea ya kuwa mbovu kwa mipira ya mbali inaonekana wazi kuchangia, na kama Rooney ataendelea kucheza mchezo wa kutokushuka chini, then Cleverley na Anderson watakuja kuwa exposed na timu yoyote nzuri kubwa kama Real Madrid au Barca katika stages za mbele msimu huu.

Tatizo la majeruhi kwa United halionekani kuchangia sana , Evans, Jones na Smalling wanaonekana kucheza vizuri sana.

Friday, October 14, 2011

MTANZANIA AOMBEWA ITC KUCHEZA UJERUMANI


MCHEZAJI Costancia Maringa wa Tanzania ameombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ili aweze kucheza mpira wa miguu wa wanawake nchini Ujerumani.
Chama cha Mpira wa Miguu cha Ujerumani (DFB) kimetuma maombi hayo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ili kumwezesha mchezaji huyo kuichezea timu ya FC 1919 Marnheim ya nchini humo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa DFB, Helmut Sandrock, Maringa mwenye umri wa miaka 12 ameombewa ITC na chama hicho kama mchezaji wa ridhaa. TFF inafanyia kazi maombi hayo na hati hiyo itatolewa mara baada ya taratibu husika kukamilika.

UNAMKUMBUKA HUYU ?

Mhariri wa Gazeti la Dimba Mahmoud Zubeir ( kulia ) akiwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba Mark Sirengo....

SIMBA VS AFRICAN LYON VIINGILIO


VIINGILIO SIMBA VS AFRICAN LYON

Viingilio katika mechi namba 62 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na African Lyon itakayochezwa Oktoba 16 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam vitakuwa kama ifuatavyo;

VIP A itakuwa sh. 15,000, VIP B sh. 10,000, VIP C sh. 7,000, viti vya rangi ya chungwa (orange straight and curve) sh. 5,000 wakati viti vya kijani na bluu itakuwa sh. 3,000.

Mechi hiyo itaanza saa 10 jioni na tiketi zitauzwa uwanjani kwenye magari maalumu.

YANGA YAIFUMUA KAGERA SUGAR 1-0

Mshambuliaji kutoka Ghana Asamoah leo ameendeleza makali yake na kikosi cha Yanga baada ya kufunga goli pekee na la ushindi kwa timu yake dhidi ya Kagera Sugar katika mwendelezo wa ligi kuu ya Tanzania..

TP MAZEMBE WAENDELEZA UJENZI UWANJA WAO











Thursday, October 13, 2011

LIVERPOOL NA KUPOROMOKA KIUCHUMI


WAINGEREZA WANA MSEMO WAO USEMAO ‘ BE CAREFUL FOR WHAT YOU WISH FOR’ ,,, YAANI KUWA MAKINI NA UNACHOTAKA KWANI WAWEZA KUKIPATA HALAFU KIKAWA MATATIZO KWAKO .

HUU NI MSEMO AMBAO UNAWEZA KUWA SAHIHI KWA HALISI INAYOENDELEA KWENYE KLABU YA LIVERPOOL .

KWA WASIOFAHAMU LIVERPOOL NI MOJA YA KLABU KUBWA NCHINI ENGLAND . UMAARUFU WA LIVERPOOL HAUPO NDANI YA VISIWA VYA MALKIA TU BALI HATA BARANI ULAYA AMBAKO WEKUNDU HAWA NI MABINGWA WA KIHISTORIA WA MICHUANO MBALIMBALI BARANI HUMO IKIWEMO MICHUANO YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE AMBAYO LIVERPOOL NI MABINGWA MARA TANO.

KABLA YA MANCHESTER UNITED KUTWAA UBINGWA WAKE WA 19 WA LIGI KUU NCHINI ENGLAND MSIMU ULIOPITA LIVERPOOL WALIKUWA MKONO KWA MGUU KWENYE KILELE CHA MATAJI YA LIGI HIYO TIMU ZOTE ZIKIWA ZIMETWAA UBINGWA MARA 18 NA KAMA SI KUFANYA VIBAYA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 20 BASI LIVERPOOL WANGEWEZA KUWA JUU YA UNITED KWANI MARA YA MWISHO KWAO KUTWAA HILO TAJI LA 18 ILIKUWA MWAKA 90 WAKATI WA LIGI YA ZAMANI .

LIVERPOOL PIA ILIKUWA TIMU YA KWANZA KWA ENGLAND KUWA NA MKATABA WA UDHAMINI WA JEZI , WAKIFANYA HIVYO MWAKA 1979 AMBAPO KAMPUNI YA VIFAA VYA UMEME YA HITACHI ILIINGIA MKATABA NA KLABU HII BAADA YA KUONA NAFASI YA KIBIASHARA KWENYE MCHEZO WA SOKA.

MASHABIKI WENGI WA LIVERPOOL WANALALAMA KUWA TIMU YAO IMEFANYA VIBAYA KATIKA KIPINDI CHA BAADA YA MWAKA 90 KWA KUWA MFUMO WA LIGI MPYA ULIWANYIMA NAFASI YA KUFANYA VIZURI . WASICHOTAMBUA MASHABIKI HAWA NI KWAMBA LIVERPOOL NDIO HASA TIMU ILIYOCHORA RAMANI YA MFUMO MPYA WA LIGI KUPITIA KWA ALIYEKUWA MWENYEKITI WAKE WAKATI HUO NOEL WHITE . WHITE ALIENDELEA KUWA KIONGOZI WA LIVERPOOL KWENYE NAFASI YA UKURUGENZI HADI MWAKA 2007 .

KIKUBWA AMBACHO MASHABIKI NA WAPENZI WA LIVERPOOL WANASHINDWA KUELEWA NI UKWELI KUWA TIMU YAO IMESHINDWA KWENDA NA NYAKATI MPYA ZA SOKA KWANI KIUKWELI KWA MUDA MREFU TIMU YAO PAMOJA NA KUWA MOJA YA WAJENZI WA LIGI KUU MPYA BADO IMENASA KWENYE SOKA LA ENZI ZILE.

KIONGOZI WA LIVERPOOL WAKATI LIGI MPYA INAANZA DAVID MOORES ALIJARIBU KUIJENGA UPYA LIVERPOOL LAKINI MAWAZO YAKE YALISHINDWA . MOORES ALIWALETA WAMILIKI WAPYA WA KLABU HIYO WAMAREKANI TOM HICKS NA GEORGE GILLET , WATU AMBAO ALMANUSRA WAITIE SHIMONI TIMU HII.

HIVI KARIBUNI MMOJA WA VIONGOZI WA KAMPUNI INAYOIMILIKI KLABU HII YA KIHISTORIA KAMPUNI YA FENWAY SPORTS GROUP AMETOA WAZO LA VILABU VYA LIGI KUU KUFANYA MAKUBALIANI BINAFSI KWENYE MIKATABA YA TELEVISHENI , KINYUME NA MFUMO WA SASA AMBAPO TIMU ZA LIGI KUU ZINAFANYA MAKUBALIANO YA HAKI ZA MATANGAZO YA TELEVISHENI KWA PAMOJA HUKU ZIKIGAWANA MAPATO KUTOKANA NA HESABU ZA MASOKO AMBAPO TIMU YENYE SOKO KUBWA NDIO HUPATA MGAO MKUBWA .

HILI NI WAZO ZURI AMBALO LINAWEZA KUZIKOMBOA BAADHI YA KLABU AMBAZO HAZINA SOKO KUBWA KIUSHABIKI LAKINI ZINA TIMU YA WATU WA MASOKO WENYE MIPANGO THABITI.

KWA LIVERPOOL AMBAO WAZO HILI LIMETOKA KUNAWEZA KUWA NA MADHARA MAKUBWA . LIVERPOOL PAMOJA NA UKUBWA WAKE KAMA KLABU BADI HAINA UWANJA KAMA WA ARSENAL AMBAO UNAIFANYA IWE NA UHAKIKA WA KUWA KWENYE HALI NZURI YA KIUCHUMI KWA MIAKA MINGI IJAYO . ENEO AMBALO LIVERPOOL IPO LEO HII NI ENEO AMBALO HALIVUTII KIUTALII NA ANGUKO LA KIUCHUMI LIMELIATHIRI JIJI HILI KULIKO MAHALI KOKOTE ULAYA .

HALI HII INAIFANYA LIVERPOOL KUWA MOJA YA KLABU AMBAZO HAZIFANYI VIZURI KIBIASHARA . UKIONGEZA UKWELI KUWA TIMU HII HAIJATWAA UBINGWA WA LIGI YA ENGLAND KWA MIAKA 20 NA NA KWA HALI YA LIGI KUU YA ENGLAND KWA SASA BADO HAINA UHAKIKA WA KUCHEZA LIGI YA MABINGWA AMBAYO THE REDS HAWAJACHEZA KWA MISIMU MIWLI SASA .

HAYA YOTE YANAIFANYA LIVERPOOL IPOTEZE MVUTO ILIYOKUWA NAYO WAKATI ULE ILIPOKUWA TIMU KUBWA NA HAPA NDIO LINAPOKUJA SWALI KUWA JE SOKO LA TELEVISHENI LITATOSHA KWA LIVERPOOL ENDAPO KILA TIMU ITAFANYA MAKUBALIANO YAKE YENYEWE , LIVERPOOL HAWANA BUDI KUWA WAANGALIFU KWA WANCHOTAKA KWANI KINAWEZA KUWA LAANA BADALA YA MBARAKA KWAO ?

PHOTOS: CARLOS TEVEZ 'CARLITOS' AREJEA MAN CITY

CARLITOS AKIINGIA KATIKA UWANJA WA MAZOEZI WA CITY @CARRINGTON LEO JIONI

ROBERTO MANCINI NAE AKIINGIA CARRINGTON AKIWA ANA-RIDE BAISKELI

TEVEZ: MANCINI ANIOMBE RADHI


Carlos Tevez jana usiku ali-demand kuombwa radhi na kocha wake wa Manchester City Roberto Mancini.

Tevez, 27, amekasirika kwamba amebebeshwa mashtaka ya kukataa kucheza katika mechi dhidi ya Bayern Munich, na ikiwa leo adhabu yake ya kusimamishwa kwa wiki mbili inaisha, Carlitos yupo tayari kurejea kucheza katika ligi kuu ili kudhihirisha hakugoma kucheza dhidi ya The Bavaria.

Tevez anasema alikuwa radhi kuomba msamaha kwa kukataa ku-warm up ikiwa Mancini nae ataomba radhi kwa kusema uongo kuwa alikataa kucheza.

Tevez sasa anatarajiwa kuhojiwa na klabu on Monday.

Chanzo cha habari cha gazeti la ‘The Sun’ kilisema: “Tevez amekasirika.Anataka Mancini amuombe radhi kwa kusema uongo kuwa alikataa kucheza.

“Mambo yote yangekuwa yameisha kama wote wawili wangeomba radhi lakini City walikataa wazo hilo.”

Taarifa kutoka kambi ya Tevez zinasema kuwa Carlitos alikataa kupasha kwa sababu tayari alishafanya hivyo, lakini upande wa Man City wanaonekana wapo upande wa Mancini na leo uongozi wa klabu hiyo ulimzuia mshambuliaji huyo asiudhurie mazoezi ya asubuhi ya kikosi cha kwanza.

City wamedhamiria kumpiga faini ya £1.5milllion na kumfungia zaidi kwa wiki nne.

CHICHARITO ASAINI MKATABA MPYA WA MIAKA 5 NA UNITED


Siku chache baada ya kutoka kwa taarifa kuwa Real Madrid wametenga kiasi cha £30 million kwa ajli ya kumsajili Javier Hernandez, klabu ya Manchester United leo imetangaza kuwa mchezaji huyo kutoka Mexico amesaini mkataba wa mpya wa miaka 5.

WAYNE ROONEY: NILIANZA KWENDA ANFIELD NIKIWA NA MIAKA 10

WAYNE ROONEY ALIPOKUWA MIAKA 10 NDANI YA JEZI YA EVERTON, MWAKA 1996 .

Ronaldinho is back in the Business

YANGA WAKIRI KUFULIA, WAMPIGIA MAGOTI MANJI NA KUTOA SALAMU ZA BIRTHDAY


Kutokana na hali ya kifedha kuzidi kuwa ngumu, uongozi wa Klabu ya Yanga chini ya mwenyekiti wake Lloyd Nchunga umemwangukia aliyekuwa mfadhili na mdhamini wao, Yusuf Manji, ili aweze kurejea kuokoa jahazi.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga, alisema kuwa wamefikia uamuzi wa kumsihi Manji arejeshe ufadhili na udhamini baada ya mambo kuanza kwenda mrama.


Nchunga alisema baada ya uongozi kuona wameshindwa kumpata mfadhili wa kuchukua nafasi ya Manji, ambaye alijiondoa kudhamini na kuifadhili Yanga na kubaki mwanachama wa kawaida, waliona ni vema kumuomba arudi.

“Baada ya kutafakari kwa kina, tuliona tuna kila sababu ya kumsihi na kumwomba Manji arejee na napenda kuwaambia kuwa tumekuwa na majadiliano ya muda mrefu na ndugu Yusuf Manji na kimsingi amekubali,” alisema Nchunga.


Alifafanua kuwa baada ya uongozi kumwandikia barua rasmi Manji, kumuomba arejee kuidhamini, mfanyabiashara huyo aliomba muda wa kutafakari ili aweze kujadiliana na familia yake, pamoja na wafanyabiashara wenzake kabla ya kuridhia.


Aliongeza kuwa Manji amesema kabla ya kutoa uamuzi wa ama kurudi ama kutorudi, ameomba kwanza kukutana na Kamati ya Utendaji na baada ya mazungumzo hayo, ndipo atafikia uamuzi wa mwisho juu ya maombi hayo.

“Pia nichukue fursa hii kwa niaba ya Yanga, kumtakia ‘birthday’ siku njema ya kuzaliwa ndugu yetu Manji, ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani na anatarajia kurudi nchini Ijumaa, huku akiwa katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, kwani alizaliwa Oktoba 14, pia tujitokeze kumpokea siku atakaporudi,” alisema Nchunga.

KAGO AREJEA MSIMBAZI, TIMU IPO KAMBINI


Straiker wa kimataifa wa Simba, Gervas Kago, amerejea jana jijini Dar es Salaam na kujiunga na kambi ya timu hiyo kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya African Lyon inayotarajiwa kupigwa Oktoba 16 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga ‘Mr. Liverpool’, alisema kurejea kwa Kago ambaye alikuwa Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa ajili ya kuichezea timu ya taifa ya nchi hiyo ambayo ilikuwa ikitafuta tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika (CAN), kutaiongezea makali timu yao ili iweze kufanya vema katika mechi zake za kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Alisema, tayari Kago ameshajiunga na wenzake ambao wamepiga kambi Bamba Beach, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi zilizobaki, ambapo alibainisha kuwa wachezaji wa timu hiyo waliokuwa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ nchini Morocco, ambao ni Juma Kaseja, Said Nassor ‘Cholo’, Juma Jabu na Juma Nyoso nao wameshaingia kambini.

WACHEZAJI YANGA WALETA MGOMO KUTOKANA NA UKATA KLABUNI


Hali mbaya ya ukata ndani ya klabu bingwa ya Tanzania na Afrika Mashariki na kati, jana asubuhi ilisababisha mgomo wa wachezaji wa klabu hiyo wakitaka kugomea mazoezi huku wakishinikiza kulipwa mishahara yao kuanzia Septemba na kutafutiwa kambi sehemu nyingine, kwani klabuni kuna matatizo ya huduma ya maji.

Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kwamba wachezaji hao waliamua kuendesha mgomo huo baada ya kupigwa danadana za mara kwa mara na viongozi wa klabu hiyo, kuhusiana na mustakabali mzima juu ya ulipwaji wa mishahara yao.

Habari hizo zilibainisha kuwa, kutokana na hali hiyo, uongozi wa Yanga ilibidi ukae kikao na wachezaji hao ili kufikia muafaka kuhusiana na mustakabali mzima wa mgomo huo, ambapo jioni walianza kulipwa huku mafundi pia wakijipanga kutatua tatizo hilo la miundombinu ya maji.

Alipotafutwa msemaji wa Yanga, Louis Sendeu, kuzungumzia kitendo hicho, alisema kuwa: “Hizo ni propaganda tu ambazo ni za kupuuzwa, si kweli leo wachezaji asubuhi hawakufanya mazoezi kwa sababu uwanja wetu ulijaa maji, lakini jioni walifanya mazoezi kama kawaida kabla ya kuingia kambini.”

Kuhusiana na kikao baina yao na wachezaji, Sendeu alisema kuwa kilikuwa cha kawaida katika kupeana mikakati ya kuelekea katika mechi ya kesho na michezo mingine iliyobaki.

MECHI YA UGANDA VS KENYA YAINGIZA MAPATO YA BILLION MOJA


Pamoja na kutofanikiwa kupata nafasi ya kushiriki katika kombe la mataifa huru ya afrika litakalofanyika mwakani, shirikisho la Soka la Uganda Fufa limesema limepata mapato ya kiasi cha zaidi ya 1bilioni za Uganda katika mechi dhidi ya Kenya iliyokuwa ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwenye uwanja wa Namboole.

Fufa imesema imepata jumla ya shilingi 1.024bilioni baada ya kutengeneza tiketi za dhahabu 610 ambazo zilikuwa zikiuzwa kwa shilingi 120,000 za Uganda, ambapo zilibaki tiketi 10 tu.

Tiketi zote 38,865 zilizokuwa zikiuzwa kwa shilingi 20,000 za Uganda ziliuzwa, lakini tiketi 503 za VIP hazikuuzwa kwa mujibu wa Fufa.

"Hatuna hizo fedha hivi sasa, tumetumia kiasi cha shilingi 561milioni za Uganda kwa mambo mbalimbali hivyo tutabakiwa na kiasi kisichozidi shilingi 500 za Uganda,"alisema Makamu wa Raisi wa Shirikisho la Soka la Uganda, Anthony Kimuli.

Alisema,"kiasi hicho cha fedha tumekitumia kwa ajili ya tiketi za kitaalamu, kambi ya timu ya Taifa, waamuzi, uwanja wa Namboole na walinzi 4,000."

Raia wengi wa Uganda walikosa tiketi za mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa matokeo ya 0-0 dhidi ya Kenya na hivyo Uganda kushindwa kufuzu Fainali za Nataifa ya Afrika wakati ilikuwa ikishinda mechi hiyo kwa idadi yoyote ya mabao inafuzu.

Watu wengi waliopata tiketi waliweza kuzipata kwa gharama za juu kwa sababu tiketi hizo zilikuwa zikiuzwa nje ya uwanja kwa gharama ya juu.
Wakati huo huo kocha wa timu ya Taifa ya Uganda, Bobby Williamson amesema kocha yeyote angefanya uamuzi kama wake wa kumtimua kambini nyota wa timu hiyo David Obua kutokana na vitendo vyake vya utovu wa nidhamu.

"Kitu kibaya ni kwamba Obua anasema uongo, nilimtumia ujumbe wakati alipokuwa akisema uongo katika radio moja wakati akihojiwa, nilimuambia aseme ukweli ili jamii ifahamu ukweli halisi,"alisema Williamson.

Alisema,"nilijaribu kuzuia ili tusimtimue kwenye kambi, lakini vitendo vyake vya utovu wa nidhamu vilizidi huku akielewa yeye alikuwa ni mchezaji wa kuigwa na vijana wengine waliokuwa kwenye kambi ya timu ya Taifa."

Williamson alisema,"katika timu ya Taifa tunafanya kazi kitimu, lakini yeye alikuwa hataki hilo na kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu."

Hivi sasa mashabiki wa soka nchini Uganda wanata ka kocha Williamson pamoja na Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka la Uganda, Lawrence Mulindwa kujiuzuru baada ya kumfukuza kambini Obua saa 24 kabla ya pambano lao dhidi ya Kenya.

Baadhi ya mashabiki wa soka nchini Uganda wanaamini kukosekana kwa Obua kulisababisha Uganda kushindwa kufuzu Fainali za Afrika kwa sababu katika mechi dhidi ya Kenya timu ya Uganda ilikosa nfasi nyingi za kufunga na kujikuta wakitoka sare ya 0-0 na Kenya.

Wednesday, October 12, 2011

TAIFA STARS YA UKWELIIII IYO !!!



MAN UNITED YATHIBITISHA KUMFUATILIA VAN WOLFSWINKEL


Manchester United wamethibitisha kwamba wanamuangalia kwa karibu mshambuliaji wa Sporting Lisbon Ricky Van Wolfswinkel.

Gazeti la Sportsmail walitoa siri kuwa United wamekuwa wakimchunguza kwa karibu mshambuliaji huyo wa kidachi kwa muda mrefu sasa.

The 22-year old straiker amejiunga na Sporting kipindi cha kiangazi kilichopita kutoka Utrecht kwa £5.5m lakini sasa Ricky anatajwa kuwa na thamani ya £11m baada ya kufunga magoli 6 katika mechi zake 8 za mwanzo.

Kocha msaidizi wa United Mike Phelan alisema: “Tumemfahamu Van Wolfswinkel kwa muda mrefu sasa.Ni kijana mdogo mwenye kipaji kikubwa ambaye ana maendeleo mazuri sana.”

VICTORIA SAVARIN USINGIZI MPYA WA DIEGO FORLAN

Diego Forlan alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mashindano katika kombe la dunia mwaka jana-na sasa mshambuliaji huyo wa Inter Milan ameshinda trophy nyingine.

The Uruguayan striker sasa yupo katika penzi zito na model Victoria Saravia, ambaye alikuwa anatoka na mchezaji mwenzie wa timu ya taifa Carlos Bueno.

Pamoja na kuwa Forlan ni bwana wake wa pili mcheza soka, Saravia amesisitiza haikuwa dharma yake ku-date na wacheza soka ila ametokea kumpenda sana Forlan.

DK 14 ZA MAGOLI 219 YA RONALDO DE LIMA AKIWA NA BARCA, INTER NA MADRID

BREAKING NEWS: VIDIC AASTAFU SOKA


Nahodha wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Serbia Nemanja Vidic ametangaza kustaafu kucheza soka la kimataifa baada ya timu yake ya Serbia kukosa nafasi ya nafasi ya kushiriki michuano ya ulaya mwakani.

Vidc ambaye alikosa penati na kupelekea timu yake kufungwa 1-0 na Slovenia jana Jumanne hivyo kuikosesha Serbia nafasi ya kucheza play offs kwa ajili ya EURO 2012.Estonia walimaliza wa pili huku Italy wakishika usukani mwa kundi C.

Vidic mwenye miaka 29 alisema: “Muda wa mabadiliko ya kizazi kipya na wachezaji wakubwa kusema kwaheri kwa jezi ya Serbia.

Pia kiungo wa Inter Milan Dejan Stankovic mwenye miaka 33 ambaye nae ametangaza kustaafu alisema: “Nimecheza mechi nyingi, nimeisaidia timu ya taifa na sasa ni muda wangu kugeukia majukumu yangu katika klabu yangu ya Inter MiLAN.

Vote Khalfan for Goal of the Week



MLSsoccer.com have unveiled that Vancouver Whitecaps FC midfielder Nizar Khalfan is one of five nominees for Goal of the Week.

VOTE FOR KHALFAN HERE OR TEXT G2 TO 22442

Voting runs until 11:59 pm PT on Thursday.

After a long kick up field from goalkeeper Joe Cannon, rookie striker Omar Salgado flicked a header over to Khalfan, who controlled the ball on the bounce before unleashing a dipping volley into the bottom corner to cap off a 3-0 Whitecaps win against Real Salt Lake.








This is Khalfan’s first Goal of the Week nomination of the season and the eighth nomination overall for Whitecaps FC, including a Week 13 winner from Eric Hassli against Seattle Sounders FC and a Week 27 winner from Davide Chiumiento against New York Red Bulls.

CRISTIANO RONALDO KATIKA HATIHATI YA KUKOSA EURO 2012


Pilika pilika za kugombea nafasi ya kushiriki katika michuano ya mataifa ya ulaya maarufu kama Euro 2012 imefikia ukingoni jana usiku huku baadhi ya mataifa makubwa barani humo yakifuzu lakini kuna baadhi ya nchi kama Ureno ikiwa hatihati ya kutoshiriki michuano hiyo ikiwa itafungwa katika play off.

Group A
Teamv · d · e
PldWDLGFGAGDPts
Germany101000347+2730
Turkey105231311+217
Belgium104332115+615
Austria103341617−112
Azerbaijan102171026−167
Kazakhstan10118624−184

Group B

Teamv · d · e
PldWDLGFGAGDPts
Russia10721174+1323
Republic of Ireland10631157+821
Armenia105232210+1217
Slovakia10433710–315
Macedonia10226814−68
Andorra100010125−240

Group C

Teamv · d · e
PldWDLGFGAGDPts
Italy10820202+1826
Estonia105141514+116
Serbia104331312+115
Slovenia10424117+414
Northern Ireland10235913−49
Faroe Islands10118626−204

Group D

Teamv · d · e
PldWDLGFGAGDPts
France10631154+1121
Bosnia and Herzegovina10622178+920
Romania10352139+414
Belarus1034387+113
Albania10235714−79
Luxembourg10118321−184

Group E

Teamv · d · e
PldWDLGFGAGDPts
Netherlands10901378+2927
Sweden108023111+2024
Hungary106132214+819
Finland103161616010
Moldova103071216−49
San Marino100010053−530

Group F

Teamv · d · e
PldWDLGFGAGDPts
Greece10730145+924
Croatia10712187+1122
Israel105141311+216
Latvia10325912−311
Georgia1024479−210
Malta10019421−171

Group G

Teamv · d · e
PldWDLGFGAGDPts
England8530175+1218
Montenegro833277012
Switzerland83231210+211
Wales8305610−49
Bulgaria8125313−105

Group H

Teamv · d · e
PldWDLGFGAGDPts
Denmark8611156+919
Portugal85122112+916
Norway8512107+316
Iceland8116614−84
Cyprus8026720−132

Group I

Teamv · d · e
PldWDLGFGAGDPts
Spain8800266+2024
Czech Republic8413128+413
Scotland8323910−111
Lithuania8125413−95
Liechtenstein8116317−144

BEST LOSERS WATAKAOCHEZA PLAY-OFF

Group
Teamv · d · e
PldWDLGFGAGDAGPts
E Sweden108023111+201324
F Croatia10712187+11822
B Republic of Ireland10631157+8621
D Bosnia and Herzegovina10622178+9720
A Turkey105231311+2417
H Portugal85122112+9816
C Estonia105141514+1716
I Czech Republic8413128+4913
G Montenegro8332770212

*Mstari wa kijani unaonyesha timu ambazo tayari zimeshafuzu

*Mstari wa bluu unaonyesha timu itakayocheza play off.