
Winga wa kimataifa wa England Stewart Downing amemalizana na klabu ya Liverpoo na leo ametambulishwa rasmi kama mchezaji mpya wa majogoo wa jiji kwa £20million.
Klabu ya Mathare United inayoshiriki katika ligi kuu ya Kenya imefanikiwa kuingia mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja na moja ya makampuni makubwa ya vifaa ya michezo PUMA.
Udhamini huo wa Mathare United kutoka kwa PUMA una thamani ya kshs 3million, huku klabu hiyo ikipata jezi rasmi na za mazoezi, na viatu.
Uhamisho wa mshambuliaji Jerryson Tegete kuelekea Simba kwa klabu hiyo ya msimbazi kumtoa beki Kelvin Yondan pamoja na kiasi cha pesa umeshindakana.
Chanzo cha habri kutoka ndani ya pande mbili za uongozi wa watani wa jadi kinasema kuwa kushindakana kwa dili hilo ni kutokana muda, "Ni kweli Simba walipeleka ofa ya kutaka kumsajili Tegete lakini Yanga wameshindwa kutoa maamuzi kutokana na kwamba suala la zima maamuzi ya usajili linapaswa kutolewa maamuzi na kamati ya utendaji ya klabu hiyo ambao imeshindwa kukutana kwa dharura mpaka dirisha la usajili lilipofungwa leo saa 6 usiku."
Masaa machache baada ya uongozi wa klabu ya Simba kutangaza kumpeleka kwa mkopo katika klabu ya Ruvu Shooting, beki Meshack Abel ameongea na blog hii na kufunguka juu sakata hilo la uhamisho wake.
"Kiukweli nimeshangazwa sana na taarifa hizi za mimi kupelekwa kwa mkopo Ruvu Shooting, kwa sababu mimi nilishakataa kwenda huko.Jumatatu iliyopita Uongozi uliniita na kuniambia juu ya suala hili na mimi nikawaambia siwezi kwenda Ruvu, ni bora wanipe barua ya kuniacha ili niende nikatafute timu ninayoitaka mwenyewe lakini uongozi ukaniambia mimi ndio niandike barua ya kuvunja mkataba.Kutokana na sharti hilo nikashindwa coz sikuwa na uwezo wa kulipia gharama za contract termination, hivuo nikawaomba waniache nitafute timu mwenyewe lakini sitaki kuichezea Ruvu Shooting.
"Kiukweli Simba wamekuwa hawanitendei haki tangu wanisajili, mpaka sasa nawadai fedha zangu za usajili za mwaka jana, waliniahidi kunilipa kwa kunipa gari lakini mpaka msimu unaisha sikupewa kitu, na wakati tunajiandaa kwa ajili ya mechi ya pili ya Motema Pembe niliumia hivyo nikashindwa kuitumikia klabu, lakini cha ajabu mwisho wa mwezi(May) ulipofika walinikata mshahara wangu eti kwa madai walitumia fedha waliyonikata kunitibia majeraha niliyoumia nje ya Simba.
"Mambo yote haya niliyavumilia lakini sasa imefika mwisho, nahitaji uongozi wa klabu ya Simba waniache niende sehemu ninayoitaka kama walivyowaachia Haruna Shamte na Jabu kuchagua sehemu wanazozitaka."
Meshack ambaye alihamia Simba akitokea Mtibwa Sugar anasema tayari amepeleka maombi rasmi ya kuomba Simba wamuandikie barua ya kumuacha kwa sababu ameshapata timu ya kuichezea nchini Botswana, "Niliongea na katibu na nimweleza kuwa nimepata timu inayotaka kunisajili nchini Botswana inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo "Tigers Sports Club, na kama mambo yakienda vizuri Jumapili natarajia kwenda Gabarone kumalizana nao.Naamini bado nina uwezo mkubwa wa kucheza na nitathibitisha uwezo wangu ndani ya msimu mmoja tu."
HIKI NDO KIKOSI CHA KLABU KONGWE KABISA ULIMWENGUNI YA SHEFFIELD FC ILIYOANZISHWA MNAMO MWAKA 1857
Ndani ya kitabu hicho kuna sheria ambazo baadhi ziko hadi leo hii kama vile “in-direct free kick” , kona na matumiz ya sehemu ya juu ya goli maarufu kama mtambaa panya .
Sheria nyingine inaonyesha kuwa mchezaji anaruhusiwa kusukuma kwa kutumia mikono ila sio kumuangusha au kumpiga mchezaji mwenzie mweleka HIKI NDO KITABU CHENYEWE
Majina ya wachezaji hao ni kama ifuatavyo:
1: Kenneth Asamoah
2: Haruna Niyonzima
3: Hamis Kiiza
4: Yew Berko
5: Davis Mwape
Wakati huo huo klabu hiyo ya Yanga imemtoa kwa mkopo mchezaji Idd Mbaga kwa klabu ya African Lyon inayoshiriki katika ligi kuu ya Tanzania.
Simba ambao leo hii pia wamefanikiwa kukamilisha usajili wa Felix Sunzu wanamhitaji Tegete aje kuziba pengo lilioachwa na mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi anayekaribia kujiunga na DC Motema Pembe.
Sekeseke la usajili wa kiungo Wesley Sneijder kutoka Inter Milan kuelekea Manchester United limechukua sura mpya baada ya taarifa za kampuni kubwa mavazi ya Nike kuingilia kati juu ya kukamilisha kwa usajili huo unaotajwa kuwa wenye thamani ya £35.2million.
Kampuni hiyo kubwa ya kimarekani ambayo ndio mdhamini wa jezi za mabingwa wa England inasemekana wapo tayari kulipa kiasi cha pesa kilichopungua katika matakwa ya mshahara anaotaka Sneijder ili kuhakikisha uhamisho huo unafanikiwa.
Nike waliwahi kufanya kitu cha namna hii wakati mbrazili Ronaldo De Lima alipohama kutoka Barcelona kwenda Inter wakati mahasimu wao wa kibiashara Adidas, ambao wanaidhamini Real Madrid, walihusika kwa kiasi kikubwa katika kurahisha mambo kwenye usajili wa Cristiano Ronaldo na David Beckham kwenda Benebeu.
United wamekuwa wakijaribu kukamilisha dili la usajili wa Sneijder ndani ya wiki hii, huku CEO David Gill akikacha safari ya US ili aweze kupata muda wa kuongea na Inter Officials jijini Milan.
Taarifa zisizo rasmi zinasema kuwa United wapo tayari kulipa £35.2m wanayoitaka Inter lakini mazungumzo yamekwama katika matakwa binafsi ya mchezaji.Kambi ya mchezaji wanataka mshahara wa £200,000 kwa wiki huku Red Devils wakiwa tayari kulipa mshahara wa £170,000 per week.
Mchezaji wa zamani wa mabingwa wa Tanzania na CECAFA Kagame Cup Athumani Idd Chuji leo ametangazwa rasmi kuwa mchezaji wa klabu ya Villa Squad ya Dar Es Salaam.
Chuji ambaye baada ya kutoka Yanga alirudi Simba na kuitumikia klabu hiyo katika michuano Kagame iliyomalizika last weekend amejiunga na Villa baada ya kukatwa katika usajili wa Simba,blog hii imepewa taarifa na msemaji wa timu hiyo bwana Idd Godgod.
Wakati huo huo Villa Squad leo wamethibitisha rasmi kuwa watatumia uwanja Chamazi wa Mbagala unaomilikiwa na matajiri wa ligi kuu klabu ya Azam kama uwanja wao wa nyumbani kwenye michezo ya ligi kuu ya vodacom msimu ujao .
Klabu ya Juventus nayo imeingia rasmi katika vita ya kutaka kumsaini Manchester City star Carlos Tevez baada ya kutuma ofa ya £45million, kwa mujibu kwa Corinthians.
City juzi walikataa ofa ya £35million kutoka kwa wakatoliki wa Brazil kwa ajili ya Carlos Tevez, lakini sasa ofa mpya iliyo mezani imeongezeka kwa £10million.
Ingawa raisi wa Corinthians Andres Sanchez amesisitiza kuwa hatoongeza ofa lakini anaamini kuwa Carlotos ana matamanio ya kurejea South America na kuwa karibu na familia yake, hivyo bado ana imani kuwa Tevez atachagua kujiunga na timu yake ya zamani.
Alisema: "Hakuna kilichobadilika, hajaamua kumuuza wala kuendelea kuwa nae.
"Wamepokea ofa ya £45m kutoka Juventus, lakini Tevez hataki kuendelea kubaki ulaya.
"Naendelea kuamini ofa niliyotuma ni nzuri, lakini inategemea na City wataamuaje.Kama ningekuwa raisi wa klabu anayochezea Tevez, basi nisingekubali kumuuza lakini kauli ya mchezaji ina uzito zaidi.Kama anataka kuondoka then ataondoka tu kwa njia yoyote.Katika soka mikataba imewekwa ili kuvunjwa."
Mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia Felix Sunzu anatarajiwa kuwasili nchini kuja kujiunga na Simba asubuhi hii.
Sunzu ambaye ni moja ya wachezaji waliong'ara katika michuano ya CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP yaliofanyika mwishoni mwaka jana, ameachwa na timu yake ya Al Hilal ya Sudan baada ya kushindwa kuonyesha uwezo mkubwa na hivyo kupelekea nafasi yake kuchukuliwa na raia mwingine wa kigeni ndani ya timu hiyo.
Mshambuliaji Rademel Falcao amemaliza utata juu ya tetesi zinahusu kuhama Porto baada ya kusaini mkataba wa mpya na mabingwa wa Ureno.
Falcao amesaini mkataba wa wa miaka 4 utakaomuweka Estadio do Dragao mpaka mwaka 2015, mabingwa hao Portugal wameithibitishia soko la hisa la Ureno.
The Colombia international ambaye alikuwa amebakiza mkataba wa miaka 2 katika mkataba wake wa mwanzo, ambao ulikuwa una kipengele cha kumruhusu kuondoka kwa euro millioni 30, lakini mkataba mpya wa Falcao una kipengele cha kumruhusu kuondoka kwa euro million 45, fedha ambayo itakuwa ni kizingiti kikubwa kwa timu zitakazomtaka.
Chelsea ni moja ya timu kubwa zinazohusishwa kwa kiasi kikubwa kutaka kumsaini mcolombia huyo mara baada tu ya kumteua Andre Villas Boas, ambaye aliiongoza Porto kushinda makombe 3 msimu uliopita.
Mabingwa wa ligi kuu ya England Manchester United wametajwa na jarida la FORBES kuwa ndio klabu ya michezo yenye thamani kubwa zaidi duniani.
The Red Devils wanatajwa kuwa na thamani paundi billion 1.165 ikiwazidi vilabu tajiri kama Dallas Cowboys na New York Yankees.
Thamani ya United inahusisha timu, uwanja, mapato na mikataba ya udhamini.
Taarifa hizi ni nzuri kwa familia ya Glazer ambayo ilinunua klabu hii kwa £790m in 2005, ingawa bado wana deni la linalokaribia £500.
Mapato ya matangazo ya United yamechangia sana kwa timu hii ku-top the chart, wakiwa wanapata £80m kwa mkataba wa miaka 4 kwa udhamini wa jezi waliosaini na kampuni ya bima ya Aon pamoja na mkataba mwingine Nike wa miaka 13 wenye thamani ya £300m.
Real Madrid walishika nafasi ya pili kwa vilabu vya soka wakiwa na thamni ya £900m.
Huku habari nzuri kwa wapenzi wa Arsenal ni baada ya timu yao kushika nafasi ya saba wakiwa na thamani ya £740m.
Chelsea walishika nafasi ya 46, na timu nyingine za soka zilizoingia katika top 50 ni Bayern Munich(19), AC Milan(34) na Juventus wakashika nafasi ya 49.
Jambo la kushangaza ni kwamba timu inayoaminika kuwa ni bora ulimwenguni kwa sasa Barcelona wameshika nafasi 26 wakiwa na thamani ya £606million.
LIST YA VILABU 10 VYA MICHEZO VYENYE THAMANI KUBWA
1. Manchester United £1.165billion
2. Dallas Cowboys £1.13bn
3. New York Yankees £1.06bn
4. Washington Redskins £960million
5. Real Madrid £900m
6. New England Patriots £850m
7. Arsenal £740m
8. New York Giants £734m
9. Houstan Texans £727m
10. New York Jets £708m
The deal will be completed once Boateng has passed a medical in Bavaria.
Manchester City wameambiwa na Corinthians: Ofa yetu kwa Tevez ndio ya mwisho chukueni au iacheni.
Ofa ya wabrazili hao ya paundi million 35 ilikataliwa na Eastlands club jana usiku.
City wanataka kupata angalau paundi million 50 na inaamnika klabu mbili za jiji la Milan zinafuatilia kwa karibu.
Raisi wa Corinthians Andre Sanchez alisema: “Ikiwa uhamisho wa Tevez hautokamilika mpaka kufikia Jumapili basi dili hili halitakuwepo mwaka huu.Tevez amekubali kusaini kwa miaka 4 na kupunguza kiwango cha mshahara kwa sababu anatamani kurudi hapa.
“Kama City wanataka paundi 50m basi atabaki England, Corinthians hatutoongeza ofa hiyo.”
Emmanuel Adebayor amekubali kurudi katika mazoezi ya Manchester City Jumatatu, ingawa amehuzunishwa sana na taarifa aliyopewa na klabu hiyo.
Adebayor amekasirika sana na jinsi alivyoondolewa kutoka ziara ya America ya timu hiyo, Manu anahisi kudhalilishwa baada ya kupokea email akiwa mapumzikoni akiambiwa anaweza kufanya mazoezi na reserves tu na kwamba hatakuwa na nafasi katika kikosi cha kwanza.
The straiker , ambaye alikataa kuhudhuria mazoezi wiki hii, anaamini hakutendewa sawa: "Sijui nimewakosea nini.Nilipata email kutoka kwa klabu, nikiwa kwenye mapumziko akiniambia kuwa sitoweza ku-train na kikosi cha kwanza.Hili ni tusi kwangu kwa kuniambia kuwa na-fit kufanya mazoezi na reserves tu.
"Nitarudi mazoezini lakini nimejisikia kutukanwa na kukosewa heshima."