Search This Blog

Friday, January 10, 2014

HATIMAE SIMBA NAYO YAFUZU FAINALI MAPINDUZI CUP.

Klabu ya Simba imefanikiwa kukata tiketi ya kucheza fainali ya kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga URA ya Uganda mabao 2-0.
mabao ya Simba kwenye mchezo huo yamefungwa na beki Joseph Owino pamoja na kiungo Amri Kiemba huku kiungo Owen Kasule wa URA akilimwa kadi nyekundu kwa kumchezea madhambi Ramadhani Singano.
Simba sasa itacheza fainali siku ya Jumatatu na timu ya KCC pia toka nchini UGANDA iliyoitoa AZAM kwa mabao 3-2.

YANGA DIMBANI KESHO DHIDI YA ANKARA SEKER SPOR.


Wakati mabingwa wa soka wa Tanzania Bara, Yanga kesho wanacheza mechi yao ya kwanza dhidi ya timu daraja la kwanza ya Ankara Seker Spor, uongozi wa timu hiyo leo utatangaza jina la kocha mkuu katika mkutano na waandishi wa habari.
Mechi hiyo itachezwa saa 9.00 za Tanzania kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mashindano wa kimataifa wa Yanga, Seif “Magari” Ahmed amesema kuwa mazoezi ya jana yalifanyika asubuhi kutokana na jua kuwahi kuzama na hali ya hewa kubadilika.
Ahmed alisema kuwa wachezaji wanaendelea vizuri na mpaka sasa wamepania kufanya vyema katika mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua.Alisema kuwa baada ya mechi hiyo, timu hiyo itaendelea na mazoezi kabla ya kucheza mechi nyingine mbili na timu za madaraja ya juu.
“Timu imeanza kambi rasmi, na mazoezi mazuri na maandalizi yametupa moyo japo ka siku ya kwanza, kesho (leo) watacheza mechi ya kirafiki ya kwanza na timu ya daraja la kwanza, n mechi nzuri kwani timu hiyo inashika nafasi za juu katika ligi hiyo,” alisema Seif.
Alisema kuwa kwa sasa timu yao inakaa mji mwingine tofauti na Antalya ambao upo kilometa 70 kutoka mji wao wa zamani. Wamefikia hotel ya ufukweni ijulikanayo wa jina la Suino Beach Hotel and Site ambayo ina hadhi ya kimataifa.Wakati huo huo;  uongozi wa klabu hiyo kesho utamtambulisha kocha mkuu wa klabu hiyo katika mkutano maalum na waandishi wa habari makao makuu ya klabu hiyo.
Seif alisema kuwa wamepitisha majina matano na walikuwa kwenye makubaliano nao mmoja wao ambaye kesho (leo) tutamtangaza rasmi.
Alisema kuwa wamepata kocha mzuri ambaye anajua mazingira ya Afrika na anajua maisha ya mpira kwa bara hili.

KCC YAIVUA AZAM FC KOMBE LA MAPINDUZI, YAIFUNGA MABAO 3-2.
David Mwantika na Kipre Tchetche wakimpongeza Joseph Kimwaga baada ya kuifungia Azam bao...


ROBERTO CARLOS USO KWA USO NA YANGA NCHINI UTURUKI.


Beki wa kushoto wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil Robert Carlos leo asubuhi  amekutana na wachezaji na viongozi wa Yanga kabla ya mazoezi.

Carlos Kwa sasa ni kocha wa timu ya Sivasspor iliyopo Ligi Kuu nchini Uturuki, Yanga pamoja na Sivasspor zimeweka kambi kwenye hotel ya Sueno Beach zikijiandaa na mashindano mbali mbali yanazikabil,Yanga wakiwa wameweka kambi kujiandaa na raundi ya pili ya ligi kuu ya Vodacom wenzao Sivasspor wanajiandaa na mchezo kombe la chama cha soka nchini humo ambao utachezwa siku ya jumanne.

Roberto Carlos akiwa na wachezaji wa Yanga nchini Uturuki.

    Nizar Khalfan na kocha Charles Boniface Mkwasa wakiwa na Roberto Carlos nchini Uturuki.
Roberto Carlos akiwa na Baraka Kizuguto pamoja na Juma Pondamali.

 IMEANDALIWA NA BARAKA KIZUGUTO

NUKUU ZA SOKA LEO!


‘’UKIONA EMBE LINAFANA NA MAJANI UJUE HALIJAIVA’’- AMIR MHANDO


 

MTANZANIA CHECHE KAGILE ALIFUNGA MABAO 16 NDANI YA SIKU MBILI...HAYA WAZEE WA KUWEKA MIZIGO,TAKWIMU HIZO KWA AJILI YA KUWASAIDIA KUTENGENEZA MIKEKA.....

     MSIMAMO WA VILABU BORA KWASASA BARANI ULAYA


 BARCELONA PIA INAONGOZA KWA KUKABA BARANI ULAYA 


TAKWIMU ZINAONYESHA FC BARCELONA INAONGOZA KWA KUTENGENEZA MASHAMBULIZI..BARANI ULAYA

 
BAYERN MUNICH NDIYO TIMU INAYOONGOZA KUCHEZA VIZURI UGENINI....

 
MANCHESTER CITY NDIYO INAONGOZA KWA KUUTUMIA VIZURI UWANJA WAKE WA NYUMBANI....


WANASOKA NA MITINDO YA NYWELEMJADALA:KWELI DAVID MOYES ANASTAHILI KUBEBESHWA LAWAMA ZA MAN UTD KUFANYA VIBAYA KWASASA ?
BOFYA HAPA CHINI KUSIKILIZA MAONI YA BWANA CEASAR

USHIRIKIANO WA KIBIASHARA WA MESSI, ADIDAS NA FIFA UTAKAVYOMUATHIRI RONALDO KIBIASHARA HATA KAMA AKISHINDA BALLON D'OR


Cristiano Ronaldo amekumbana na habari mbaya kuelekea utoaji wa tuzo ya Ballon d'Or wiki ijayo baada ya kutoka kwa taarifa kuhusu makubaliano ya dili baina ya adidas - wadhamini wakuu wa Lionel Messi - na FIFA.


Katika vipengele vipya vya makubaliano, Adidas wana haki zote za kipekee za promotion ya bidhaa za Fifa Ballon d'Or , wakati Nike, wadhamini wakuu wa Ronaldo na mgombea mwingine wa tuo hiyo Franck Ribery, hawana haki za kibiashara kama ilivyo kwa Adidas kwenye tuzo hiyo.

Kwama maana hiyo inamaanisha kwamba mshambuliaji huyo wa Real Madrid, ambaye anapewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo, hatoweza kutengeneza fedha nyingi kutoka kwenye ushindi wa tuzo hiyo kama ambavyo Messi amekuwa akitengeneza.

"Ushirikiano huu rasmi wa kibaishara na FIFA Ballon d'or ndio sababu sisi tunaweza kutumia tuzo hii kwa ajili ya shughuli zetu za promotion na kwa maana hiyo, kupitia makubaliano hayo, Nike hawawezi kupata nafasi hiyo," Ben Goldhagen, Senior PR Manager wa Adidas UK na Ireland, alisema
     

Adidas walitengeneza toleo maalum la kiatu cha f50 katika kusindikiza ushindi wa nne wa Ballon d'or wa Messi mwezi January 2013 na wamepanga kutengeneza tena kiatu hicho kwa ajili ya Messi bila kujali matokeo ya tuzo za Ballon d'or yatakuwaje.


Ronaldo na wadhamini wake Nike, hawaruhusiwi kisheria kutengeneza na kuuza kiatu cha namna hiyo ikiwa nahodha huyo wa Ureno atashinda tuzo hiyo.

REAL MADRID YAIFUNGA OSASUNA MABAO 2-0 KWENYE KOMBE LA MFALME,


Jana usiku kwenye mchezo wa kombe la mfalme la Hispania Cristiano Ronaldo alifanya kitendo ambacho mwanandamu wa kawaida anaweza kukifanya katika mazingira ya kawaida,Ronaldo aliruka juu umbali wa futi nne zaidi ya mabeki wa Osasuna na kuupiga mpira kichwa ambacho hakikuzaa matunda,kwenye mchezo huo wa raundi ya 16 bora Real Madrid walishinda mabao 2-0 yaliyofungwa na Karim Benzema na Jesse Rodrigez huku Gareth Bale akicheza dakika 90 kwa mara ya kwanza kwa mwaka 2014 baada ya kutoka kwenye maumivu.