Search This Blog

Saturday, May 4, 2013

LIVE SCORE: AS FAR RABAT 2 - 1 AZAM FC FULL TIME


Mpira unamalizika kwa Azam kutolewa kwa kufungwa mabao mawili kwa moja.

DK 90: Mwamuzi anaongeza dakika 3 za nyongeza.

DK 88: AS FAR Rabat 2 - 1 Azam FC

 DK 82: John Bocco anapiga penati na kukosa

DK 81; Azam wanapata penati baada ya beki wa AS FAR Rabat kuunawa mpira.

 DK 80: Azam pamoja na kuwa pungufu wanajitahidi kwenda mbele kujaribu kutafuta bao la kusawazisha - Ameingia Gaudence Mwaikimba.

 DK 75: AS FAR Rabat 2 - 1 Azam FC

 DK 74: Waziri Omary anapata kadi nyekundu baada ya kumshika mchezaji wa AS FAR Rabataliyekuwa anaelekea langoni mwa Azam.

 DK 68: Waziri Omary wa Azam anapewa kadi ya njano kwa mchezo mbaya.

 DK 65: Anatoka Brian Umony anaingia Khamis Mcha kwa upande wa Azam

 DK 60: Timu zote zinapoteza nafasi kadhaa za kufunga katika kipindi cha dakika 3 zilizopita.

DK 55: Mwamuzi anatoa kadi nyepesi kabisa nyekundu kwa David Mwantika wa Azam

DK 48: Azam bado wanaendelea kucheza kwa kushambulia lango la AS FAR Rabat lakini wanakosa umakini wa kuweza kuingiza mpira kwenye 18 ya wapinzani.

 DK 46: Azam wanaanza kipindi cha pili kwa kasi na kufanikiwa kupata ambayo haizai matunda.

 Kipindi cha pili kimeanza AS FAR Rabat 2 - 1 Azam FC 

 Mpira ni mapumziko

DK 45: Mwamuzi anaongeza dakika 3 

DK 43: Azam wanafungwa bao la pili hapa -AS FAR Rabat 2-1 Azam

 DK 38: Kipre Balou anapewa kadi ya njano - AS FAR Rabat pamoja na kuwa pungufu wanacheza mchezo wa kasi na nguvu.

 DK 35: Mchezaji wa AS FAR Rabat anapewa kadi nyekundu kwa kumpiga teke la uso Brian Umony

 DK 33: Kipre Tchetche anakosa bao la wazi akiwa amebaki na kipa tu wa AS FAR Rabat

 DK 30: AS FAR Rabat wanamiliki mpira kwa muda mrefu huku Azam wakicheza kwa mashambulizi ya kushtukiza

DK 25: Mchezaji yupo akitubiwa baada ya kupata maumivu wakati akizuia shuti liloelekezwa golini kwake

DK 20: A.F.R 1 - 1 Azam FC

DK 12:
AS FAR Rabat 1-1 Azam FC. Dakika ya 12 wanasawazisha.DK 6: Goaaal John Bocco anaipa Azam bao la kuongoza hapa

KICK OFF

1. Mwadini
2. Himidi
3. Waziri
4. Mwantika
5. Atudo
6. Bolou
7. Umony
8. Salum 'sure boy'
9. Bocco (C)
10. Mieno
11. Kipre


Akiba
 

Aishi
Mwaipopo
Mwaikimba
Abdi Kassim
Mcha Viali
Jabir
Luckson

LAWAMA JUU YA UTEUZI WA KIKOSI CHA TAIF STARS KWA KIM POULSEN - KIBADENI ASEMA WA KULAUMIWA NI MARSH

Baadhi ya wadau wa soka nchini wamekuwa wakimlalamikia kocha Mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen kwa uteuzi wa timu hiyo, ingawa kocha wa Kagera Sugar, Abdallah Kibadeni 'Mputa' ametamka kuwa wakulaumiwa ni msaidizi wake.

kocha wa Mkuu wa Ruvu Shooting, Boniface Mkwasa hivi karibuni alisema uteuzi wa kocha huyo umeegemea zaidi kwenye klabu za Simba, Yanga, Azam FC na Mtibwa Sugar.
 
Mkwasa alimtaka kocha huyo kujaribu kuwafuatilia wachezaji wa timu nyingine kwani wapo wenye sifa zote za kuichezea timu hiyo na hata kuwazidi baadhi ya waliopo kwa sasa.
 
Kibadeni alisema jijini Dar es Salaam kuwa kocha Kim hapaswi kulaumiwa kwa hilo isipokuwa msaidizi wake ambaye ni Silvester Marsh kushindwa kumshauri.
 
"Kwa upande wangu lawama hizi nafikiri zinapaswa kubebwa na msaidizi wake (Marsh) kwa kushindwa kumshauri mkubwa wake.
"Siamini kama Marsh amewahi kumshauri kitu halafu akakipinga. Kim ni kocha muelewa isipokuwa amekosa mtu sahihi wa kumshauri." alisema Kibadeni.

Katika hatua nyingine nyota wa timu hiyo Themi Felix alisema; "Nafikiri atueleze kuwa kucheza timu ya Taifa Stars ni mpaka uwe Simba, Yanga au Azam FC ndiyo unaweza kuonekana." alisema
Felix ambaye yupo kwenye kiwango kizuri cha soka.

SIMBA MPIRA PESA KUIWEKEA KIKAO MECHI DHIDI YA YANGA JUMAPILI

Wanachama wa Tawi la Simba la Mpira Pesa la Magomeni jijini Dar es Salaam wanatarajia kukutana (Jumapili) kwa ajili ya kuweka mikakati ya kuhakikisha timu hiyo inaibuka ushindi katika mchezo wa mwisho na mtani wake Yanga.
 
Mwenyekiti wa tawi hilo, Ustaadh Masoud alisema jijini Dar es Salaam kuwa wamepanga kukutana wanachama wote wa tawi hilo hiyo kesho kwa lengo la kuweka mikakati yakuifunga Yanga.
 
"Tunafikiri klabu yetu ya Simba imepoteza ubingwa wa ligi. Pia kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi
ambayo ingetupa fursa ya kushiriki Kombe la CAF mwakani. Kwa hiyo, furaha yetu ambayo imebaki
kwa sasa ni kumfunga mtani wetu Yanga katika mchezo wa mwisho wa ligi na kutibua sherehe hizo za ubingwa." alisema Masoud.
 
Pambano hilo la kufunga pazia la msimu wa Ligi soka Tanzania Bara 2012/13 litachezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Mei 18, mwaka huu.
 
Katika mchezo wa kwanza timu hizo mbili kongwe kwa soka zilitoka sare ya kufungana bao 1-1.
Simba ilikuwa ya kwanza kujipatia bao lake lililozamishwa na Amri Kiemba wakati Said Bahanuzi akiisawazishia Yanga bao hilo kwa mkwaju wa penalti.

Friday, May 3, 2013

JAMAL MALINZI AZUNGUMZIA MAAMUZI YA FIFA.


KALI YA LEO: MKURUGENZI WA DORTMUND AJIFUNGIA CHOONI KUOGOPA COMEBACK YA REAL MADRID


Mkurugenzi mtendaji wa Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke alikuwa kwenye hali ngumu mno katika dakika z mwish za mchezo wa pili wa nusu fainali ya Ligi ya mabingwa wa ulaya dhidi ya Real Madrid kiasi cha kuacha kuangalia mpira na kukimbilia chooni.

Borussia Dortmund walikuwa wakishambuliwa kama nyuki huku Madrid wakipata mabao mawili ya haraka haraka hivyo kukaribia kuwatoa Wajerumani hao ikiwa wangepata bao lingine.

Mwishoni Dortmund wakakaza na kufanikiwa kuitoa Real kwa jumla ya mabao 4-3, lakini Watzke anakiri dakika za mwisho za mchezo huo zilikuwa ni ngumu kuliko zote katika maisha yake ya uongozi wa soka.


Alisema: “Inaonekana tunapenda sana kujipa presha wenyewe
“Kwa mara kwenye maisha yangu ya soka niliacha kuangalia mpira kwa kuhofia matatizo ya moyo wangu.

Ilinibidi niende chooni kwenye dakika za mwisho, nikajifungia, nikayafunga masikio yangu na nikawa naangalia tu muda kwenye saa yangu.


“Nilikuwa kwenye hali mbaya sana - mawazo kibao yalikuwa ndani ya kichwa changu kwa muda ule.”

Watzke hakuwa kiongozi pekee wa Dortmund aliyekuwa kwenye hali mbaya kiasi cha kutishia afya yake. Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Michael Zorc alikiri nae nusra apate mshtuko wa moyo.


KOCHA WA SIMBA: MPIRA WA KASI NDIO TUTAOTUMIA KUIMALIZA YANGA

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Liewig ametamka kuwa silaha yake kubwa kwenye mchezo wa Yanga ni kasi ya wachezaji
wake, ingawa amekiri wanatakiwa kuwa makini kwa dakika zote 90 za mchezo.
 

Mfaransa huyo alisema jijini Dar es Salaam kuwa tayari wamepoteza ubingwa wa ligi pamoja na nafasi ya pili ambayo
ingeweza kuifanya timu hiyo ishiriki Kombe la CAF mwakani.
 

"Hatuna nafasi tena ya kushinda taji la ligi kwa msimu huu wala kumaliza katika nafasi ya pili ambayo ingetupa fursa ya kushiriki Kombe la CAF mwakani.
"Kilichobaki ni kulinda heshima yetu kwa kuwafunga mabingwa (Yanga) katika mchezo wetu wa mwisho hiyo Mei 18. Timu yangu ya Simba ina wachezaji wengi vijana ambao wana kasi kubwa kuwazidi Yanga." alisema kocha huyo aliyerithi mikoba ya Mserbia Milovan Cirkovic aliyetupiwa virago na klabu hiyo mwaka jana.
 

Kocha huyo aliongeza; "Yanga ni timu nzuri hakuna mtu anayepinga hilo, lakini haiwezi kumudu kasi ya wachezaji
wangu vijana.
"Nimewaona katika mechi kadhaa za ligi, wanacheza vizuri ingawa sitaki kuamini kwamba watashinda mbele ya vijana wangu imara."
 

Liewig alisema katika kambi ya kujiwinda na mchezo huo ataongeza muda wa programu yake ya mazoezi kuhakikisha kikosi chake kinakuwa katika hali nzuri ya ufiti kabla ya kukutana na watani hao wa jadi katika soka la Tanzania Bara na kuharibu sherehe za ubingwa huo.

HAYA NDIO MAPATO YA MECHI YA YANGA DHIDI YA COASTAL UNION - LIGI KUU KUENDELEA WIKIENDI SIMBA VS RUVU

YANGA, COASTAL UNION ZAINGIZA MIL 66
Mechi namba 172 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Coastal Union iliyochezwa juzi (Mei 1 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 imeingiza sh. 66,022,000.

Watazamaji 11,478 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 15,378,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 10,071,152.54.

Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 10,230 na kuingiza sh. 51,150,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 69 na kuingiza sh. 1,380,000.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,819,793.62, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 4,691,876.17, Kamati ya Ligi sh. 4,691,876.17, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,345,938.09 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,824,618.51.


LALA SALAMA VPL KUENDELEA JUMAPILI
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea Jumapili (Mei 5 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya Ruvu Shooting na Simba itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.15 jioni.

Hiyo itakuwa mechi ya raundi ya 24 kwa timu hizo ambapo Simba iko nafasi ya nne ikiwa na pointi 39 nyuma ya mabingwa Yanga wenye pointi 57, Azam yenye pointi 48 na Kagera Sugar ambayo ina pointi 40. Ruvu Shooting iko katika nafasi ya saba ikiwa na pointi 31.

Hadi sasa mabao 348 yameshafungwa katika ligi hiyo huku Yanga ikiongoza kwa kufunga 45. Polisi Morogoro yenye pointi 22 katika nafasi ya 12 ndiyo iliyofunga mabao machache ikiwa nayo 13 tu.

African Lyon yenye pointi 19 katika nafasi ya mwisho ndiyo inayoongoza kwa kuwa na kadi nyingi. Timu hiyo inayofundishwa na Charles Otieno ina kadi 44 ambapo kati ya hizo nne ni nyekundu. Mtibwa Sugar ya Manungu, Turiani mkoani Morogoro yenyewe inaongoza kwa kuwa na kadi nyingi nyekundu ambapo hadi sasa inazo saba.

KAMATI YA UTENDAJI YA TFF SASA KUKUTANA KUPANGA NAMNA YA KUTEKELEZA MAAGIZO YA FIFA KUHUSU UCHAGUZI MKUU

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inakutana Mei 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam kupokea na kupanga utekelezaji wa maagizo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kuhusu uchaguzi wa shirikisho.

Kikao hicho cha dharura chini ya Uenyekiti wa Rais wa TFF, Leodegar Tenga kitakuwa na ajenda hiyo moja tu katika kuhakikisha utekelezaji wa maelekezo ya FIFA unafanyika haraka ili uchaguzi ufanyike ndani ya muda uliopangwa.

FIFA katika maelekezo yake imetaka kwanza ziundwe Kamati ya Maadili na Kamati ya Rufani ya Maadili kabla ya kuingia kwenye mchakato wa uchaguzi wa Kamati mpya ya Utendaji ya TFF. FIFA imeagiza uchaguzi uwe umefanyika kabla ya Oktoba 30 mwaka huu.

KILA LA KHERI AZAM KOMBE LA SHIRIKISHO
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaitakia kila la kheri timu ya Azam katika mechi yake ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika itakayochezwa Morocco kesho (Mei 4 mwaka huu).

Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano hiyo itachezwa jijini Rabat kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Morocco. Timu hizo zilitoka suluhu katika mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita.

Azam iko nchini Morocco kwa karibu wiki nzima sasa ikijiandaa kwa mechi hiyo chini ya Kocha wake Stewart John Hall. Msafara wa Azam nchini humo unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Eliud Mvella.

25 WARIPOTI KAMBINI YOUNG TAIFA STARS
Wachezaji 25 kati ya 30 walioitwa na Kocha Kim Poulsen kwenye kikosi cha pili cha Taifa Stars (Young Taifa Stars) wameripoti kambini ambapo mazoezi yalianza tangu jana jioni (Mei 2 mwaka huu).
Kocha Kim amewaitaka wachezaji katika kambi hiyo ya siku tano ili kuangalia uwezo wao katika maeneo kadhaa kwa lengo la kupata baadhi ambao anaweza kuwajumuisha kwenye kikosi cha Taifa Stars siku za usoni.

Wachezaji watano walioshindwa kujiunga katika kambi ya timu hiyo iliyoko hoteli ya Sapphire jijini Dar es Salaam ni Aishi Manula, David Mwantika, Himid Mao, Samih Nuhu na Seif Abdallah ambao wako Morocco na timu yao ya Azam.

KAMATI YA MASHINDANO KUPITIA MAANDALIZI RCL
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inakutana Jumapili (Mei 5 mwaka huu) kupitia maandalizi ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) iliyopangwa kuanza Mei 12 mwaka huu.

Tayari mikoa 18 kati ya 27 kimpira imeshapata mabingwa wao kwa ajili ya RCL itakayotoa timu tatu zitakazopanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao (2013/2014).

Kamati hiyo chini ya Uenyekiti wa Blassy Kiondo ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF itapokea taarifa ya maandalizi ya ligi hiyo kutoka Idara ya Mashindano ya TFF na kufanya uamuzi juu ya mikoa ambayo haijawasilisha mabingwa wao.

Ligi hiyo itachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini, na ratiba (draw) itapangwa wakati wowote. Ada ya kushiriki ligi hiyo kwa kila klabu ni sh. 100,000 na usajili utakaotumika na ule ule wa ligi ngazi ya mkoa. Hakutakuwa na usajili mpya wa wachezaji.

SERIKALI NA FIFA ZIMEIUMBUA TFF, ANGETILEH IOMBE RADHI SERIKALI!

Mh Amos Makalla (kushoto ) akiwa na Angetileh Oseah

SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (Fifa) limeliagiza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuanza upya mchakato wake wa Uchaguzi Mkuu baada ya kubaini mambo kadhaa lilipokuja kusilikiza malalamiko ya baadhi ya wagombea wa uchaguzi huo.
Uamuzi huo wa Fifa ni kama ulikuwa ukitabiriwa na wadau wengi wa michezo nchini kutokana na madudu yaliyofanywa na Kamati ya Uchaguzi na ile ya Rufaa ya TFF, kiasi cha baadhi ya wagombea kuamua kupeleka malalamiko yao Fifa baada ya kutokuwa na chombo chenye mamlaka mengine hapa nchini.
Mvutano ulizidi kupamba moto baada ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuingilia kati.
Kutokana na hali hiyo, serikali ilipitia upya malalamiko hayo ambayo yalilenga kubatilisha uamuzi wa TFF kuendesha uchaguzi huo kwa kutumia marekebisho ya katiba yaliyofanyika mwaka 2012 kwa njia ya waraka uliosambazwa kwenye mikoa yote wanachama wa TFF.
Tofauti na katiba inavyosema kwamba, ili marekebisho ya katiba yafanyike, ni lazima mkutano mkuu ukae, TFF ilipitisha marekebisho hayo bila ya mkutano mkuu kukaa kwa maelezo kwamba hawana fedha za kuendesha mkutano huo.
Serikali iliagiza kutotumiwa kwa katika hiyo ya mwaka 2012, hapo ndipo palipoibuka malumbano kati ya Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Amos Makalla na Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah.
Angetile ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari alikuwa akijibizana wazi wazi na Mh. Makalla huku akijua kwamba kinachofanywa na waziri huyo ni maagizo ya mabosi wake ambao ni waziri husika, Dr Fenella Mukangara na serikali kwa ujumla.
Hatukupenda majibizano hayo kwa kuzingatia vitu viwili, kwanza, TFF ipo chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, hivyo kuendeleza malumbano kwa Angetile na Mh. Makalla hakukuwa na manufaa ya kukuza soka la Tanzania.
Ni malumbano ambayo Angetile hakupaswa kuyapa nafasi kwa kuwa serikali ndiyo inayoratibu kila kitu kinachohusu michezo nchini na hata uamuzi wa kuipiga ‘stop’ katiba ya 2012 lilikuwa jambo sahihi ambalo hata Fifa waliliona baadaye.

ANGETILEH ALIKUWA AKIBISHANA NA SERIKALI
Angetileh alipokuwa akilumbana na kujibizana na Mh. Makalla tunadhani alisahahu kwamba Makalla anafanya kazi chini ya serikali ya Rais Jakaya Kikwete, hivyo kupingana na kujibizana na mtu kama huyo ni sawa na kujibizana na serikali iliyo chini ya Mh. Kikwete.
Kama chombo cha habari, www.shaffihdauda.com tunadhani Angetile atakuwa amejifunza kutokana na jambo hili na kwa kuzingatia taaluma yake anapaswa kuviomba radhi vyombo vya habari, kwani wadau wa soka walikuwa wakimtazama Angetileh kwa macho mawili kwanza akiwa kama katibu mkuu wa TFF pili akiwa kama mwandishi ‘ Senior ‘ wa habari za michezo.
Kitendo kile kilitoa picha mbaya kwa waandishi wa habari karibu wote, hasa wanaondika habari za michezo. Tunasisitiza hii haikuwa picha nzuri kwa taaluma.
Hakukuwa na haja ya Angetile kubishana na Mh. Makalla kama angekuwa anafahamu anayebishana naye ni naibu waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, ambayo kimsingi hata yeye Angetile, Mh. Makalla ni kama bosi wake.
Hatujuhi ilipopatikana nguvu ya Angetile kubishana na Mh. Makalla huku akimdharau naibu waziri huyo kwa kusema hata akienda wizarani atazungumza na waziri husika na siyo msaidizi wake.
Hoja ya kwamba, Mh. Makalla alikuwa akiegemea upande mmoja haikuwa na mashiko kwani uamuzi wa kutotumia katiba ya mwaka 2012, ulipata pia baraka za Mh. Dr Mukangara na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

MSIMAMO WETU
Tunaamini kwamba, Angetile ni binadamu kama walivyo binadamu wengine hivyo atakuwa amebaini kosa alilofanya katika jambo hili hivyo kutorudia tena endapo hali kama hii itajitokeza hapo baadaye (kama atabaki madarakani).
Tutaendelea kusimamia haki katika michezo bila kupindisha ukweli na kamwe hatuwezi kuzifanyia kazi kelele za watu wengine ambao kwa namna moja au nyingine hawana nia nzuri na soka la Tanzania.

NSA JOB AUSHUKURU UONGOZI WA COASTAL UNION KWA MATIBABU WALIYOMPATIA.

HATIMAYE BALOTELLI APIGWA KIBUTI NA DEMU WAKE ALIYESEMA ANGEMTOA SADAKA KWA WACHEZAJI WA REAL MADRID


MARIO Balotelli ameachwa na aliyekuwa mchumba Fanny Neguesha — siku chache baada ya kuripotiwa kusema kwamba kikosi kizima cha Real Madrid kingeweza kulala nae ikiwa wangeitoa Borussia Dortmund.
Mwanamitindo Fanny, 22, aliondoka kwenye nyumba ya mshambuliaji huyo huko Italia baada ya kugombana kutokana kutoelewana baina ya wawili hao.

Straika huyo wa AC Milan Balotelli, 22, alisema wachezaji wote wa Madrid — akiwemo Cristiano Ronaldo — wangeweza kufanya mapenzi na demu wake Fanny ikiwa juzi wangeweza kufanya maajabu ya kugeuza matokeo ya mechi ya kwanza (4-1) na kufanikiwa kwenda Wembley.

Balo alikaririwa na gazeti la Marca akisema: “Ikiwa Real Madrid wataenda kucheza fainali ya  Champions League, nitamtoa mchumba wangu alale nao wote." Ingawa baadae alikana kutoa kauli hiyo.

Balotelli  aliachana na mama wa mtoto wake wa kike mtangazaji wa TV  Raffaella Fico, 25, kisha ndio akaanzisha mahusiano na mwanamitindo Fanny ambaye ana asili ya Ubelgiji.

TANZANIA YAPENYA NUSU FAINALI PAN-AFRICAN GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE


Jana usiku timu kutoka Kenya na Tanzania ziliwakilisha vizuzi Afrika mashariki katika sehemu ya saba ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™. Timu ya Kenya ilifanikiwa kuzishinda timu nyingine na kufikia hatua ya mwisho ya ukuta wa pesa wa Guinness. Kenneth kamau na Wills Ogutu wote kutoka Nairobi wamefuzu nusu fainali pamoja na watanzania Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad ambao walipata nafasi ya pili jana usiku.

Timu hizi mbili kutoka Kenya na Tanzania sasa zina nafasi ya kuwakilisha Afrika mashariki na kushinda hadi dola za kimarekani 250,000 pamoja na kuvikwa taji la ushindi wa Pan-African, watakapoendelea hatua z juu zaidi. Timu hizi zitahitaji kujiandaa vizuri zaidi na kujiamini ili kufanya vizuri katika hatua ya nusu fainali.

Timu zingine nne zitakutana katika robo fainali ijayo ili kuwania nafasi ya kuingia nusu fainali ya mashindano ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE.

Usikose kuangalia robo fainali za Pan-African kupitia televisheni za ITV na Clouds TV ambapo timu za Africa Mashariki zinapokutana na timu na timu zingine kutoka Afrika Magharibi huku ukiburudika na kinywaji cha GUINNESS.

Hakikisha kuufwatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali.

-www.facebook.com/guinnesstanzania

GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol. Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku.

Tafadhali kunywa kistaarabu - Hairuhusiwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.

RASHID MATUMLA: MUDA WANGU WA KUSTAAFU NDONDI BADO HAUJAFIKA

MABONDIA watatu wa ngumi za kulipwa ambao ni wadogo wa veteran wa ndondi hapa nchini, Rashid Matumla wamestaafu kucheza ndondi.

Hata hivyo wakati mabondia hao wakistaafu, kaka yao amedai muda wake wa kustaafu bado haujafika na kusisitiza ataacha ndondi siku atakapopigwa na mabondia chipukizi.

Matumla alithibitisha kustaafu kwa wadogo zake hao na kuwataja kuwa ni Hassan, Mkwanda na Karim ambao waliwahi kufanya vizuri hapa nchini na nje ya nchi.

"Karim alikuwa akicheza Australia na Mkwanda alikuwa Sweden," alisema Matumla na kuongeza kuwa wote waliwahi kucheza hapa nchini kabla ya kuamia kwenye nchi hizo.

"Nje ya nchi kucheza ngumi inakuwa ngumu kutokana na sheria zao hivyo kujikuta wote wakiachana na ndondi hivi sasa hawawezi kabisa kucheza," alisema.

ANNA KIBIRA KUKABIDHIWA RASMI MADARAKA CHANETA MEI 11

MWENYEKITI mpya wa Chama cha netiboli Tanzania (Chaneta), Anna Kibira atakabidhiwa rasmi madaraka Mei 11 tayari kuanza kukitumikia chama hicho.

Kibira aliyechaguliwa hivi karibuni kwenye uchaguzi mkuu akichukua mikoba iliyoachwa na Anna Bayi  alisema baada ya makabidhiano hayo amepanga kuandaa mpango mkakati wa kuendeleza mchezo huo kimataifa.

"Mara nitakapokabidhiwa nitakaa na kamati ya utendaji na kuweka mikakati ya kuendeleza yalemazuri yote yalioachwa na wenzetu ikiwamo kuhakikisha timu ya taifa inafuzu kushiriki kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola ya mwakani," alisema

Katibu mkuu wa Chaneta aliyemaliza muda wake, Rose Mkissi aliliambia gazeti hili jana kuwa wamechelewa kumkabidhi Kibira na kamati yake ofisi kutokana na michezo ya Mei Mosi iliyomalizika jana.

"Tulitaka kuukabidhi uongozi mpya ofisi mapema tangu tulipomaliza uchaguzi Dodoma ingawa ilishindikana kutokana na michezo ya mei mosi," alisema Mkissi.

Kwa mujibu wa Mkissi makabidhiano hayo yatafanyika jijini Dar es Salaam tayari kwa uongozi huo kuanza kuitumikia Chaneta.

SERIKALI YAKIRI KUTOWASAIDIA WANAMICHEZO WALIOLITUMIKIA TAIFA

Serikali imekiri kuwa haina utaratibu rasmi wa kuwasaidia wanamichezo waliolitumikia taifa, pindi wanapokumbwa na matatizo.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa Bungeni na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla wakati akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni Idd Azan.

Azan alitaka kujua ni utaratibu gani ambao serikali imekuwa nao juu ya kuwasaidia wananichezo wenye matatizo waliyowahi kuzitumika timu za taifa, kama vile nahodha wa Taifa Stars, Jellah Mtagwa ambaye kwa sasa anasumbuliwa na maradhi.

Akijubu swali hilo, Makalla alisema kuwa serikali haina utaratibu rasmi wa kuwasaidia wanamichezo wake waliowahi kuzitumikia timu za taifa pindi wapokuwa na matatizo isipokuwa imekuwa ikiwaenzi kupitia utaratibu usio kuwa rasmi.

"Serikali haina utaraibu rasmi wa kuwasaidi wanamichezo waliowahi kuzitumikia timu za taifa wakati wanapokuwa na matatizo.

"Hata hivyo imekuwa ikiwaenzi kupita kwa vyama mbalimbali vya michezo hapa nchini kwa kuwapa tuzo kutokana na kutambua mchango wao," alisema Makalla.

Katika hatua nyingine serikali kupitia kwa Naibu huyo wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo haikuweza kuweka wazi kama itamsaidia Mtagwa mara baada ya Azan alipouliza swali la
nyongeza kuwa serikali inampango gani katika kumsaidia mchezaji huyo wa zamani ambaye alitumikia Taifa Stars kwa zaidi ya miaka 15 na kuingizia serikali mamilioni ya fedha kupitia shirika lake la posta lililokuwa likiuza stemp zilizokuwa na picha yake.

Mtagwa ni miongoni mwa wachezaji wa Taifa Stars waliyoiwezesha Tanzania kushiriki katika Fainali za Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza mwaka 1980 nchini Nigeria.

Hata hivyo tangu mwaka huo Tanzania hajawahi tena kushiriki katika fainali hizo na mara kwa mara imekuwa ikishia njiani.

Thursday, May 2, 2013

EXCLUSIVE: HATIMAYE NSA JOB APELEKA JINA LA KIGOGO ALIYEMPA RUSHWA TFF

MSHAMBULIAJI wa Coast Union, Nsa Job amewasilisha barua kwenye Shirikisho la soka (TFF) ambayo inamtaja kigogo ambaye alimpa rushwa.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lilimtaka mchezaji huyo kujieleza kutokana na kukaririwa akiongeza katika kituo kimoja cha radio akikiri kupokea rushwa ya sh2mil kwa mmoja wa kiongozi wa timu kubwa ili acheze chini ya kiwango pindi walipokuwa wanacheza na timu hiyo.

Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, alisema kuwa tayari mchezaji huyo amekwisha tuma barua ya kujieleza nao wameamua kulipeleka suala hilo katika kamati ya nidhamu ambayo inatarajiwa kukutana wiki ijayo.

Alisema mbali na suala hilo pia kamati hiyo itapitia mambo mbali mbali ya ligi kuu ambayo yametokea ikiwemo suala la viongozi ambao walikuwa wanatoa maneno ya uchochozi.

Alisema viongozi wanatakiwa kufuata taratibu na kanuni za soka sio kuongea ongea vitu visivyo na maana ambavyo vitaleta matatizo katika soka.

Moja ya Viongozi ambao watajadiliwa ni Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga baada ya kudaiwa kutoa maneno ya uchochezi pindi TFF, walipohairisha mechi yao dhidi ya Mgambo JKT ya Tanga.  

GOLI LA WIKI:HAROUN CHANONGO ( SIMBA vs POLISI MORO )

MAAGIZO YA FIFA KUHUSU UCHAGUZI WA TFF


Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuanza upya mchakato wa uchaguzi baada ya kubaini kasoro iliyotokana na ukosefu wa kutokuwepo vyombo vya kushughulikia ukiukwaji wa maadili.

FIFA ambayo ilituma ujumbe wake katikati ya mwezi uliopita kufanya utafiti kuhusu mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa TFF ambao ulisimamishwa baada ya baadhi ya wagombea kulalamika, imetaka uchaguzi ufanyike kabla ya tarehe 30 Oktoba 2013, lakini ukitanguliwa na mabadiliko ya katiba ambayo yatahusisha uundwaji wa vyombo vya kushughulikia ukiukwaji wa maadili.

Raiswa TFF, Leodegar Tenga aliwaambia waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa shirikisho hilo kuwa suala la Tanzania lilijadiliwa kwenye kikao cha Kamati ya Dharura ya FIFA kilichofanyika tarehe 28 Aprili 2013 na maamuzi yake kutumwa juzi kwa barua iliyosainiwa na KatibuMkuuwa FIFA, Jerome Valcke.

Baada ya kupokea barua hiyo, Rais wa TFF alifunga safari kwenda Dodoma jana kukutana na Mheshimiwa Waziri na Naibu wake pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT). 

“Matarajio yetu sote yalikuwa kupokea majina ya waliopitishwa ili tufanye uchaguzi. Kinyume chake tumepokea maagizo hayo. Hata hivyo tumeona kuwa hili ni jambo la kheri kwa vile siyo tu haki itatendeka bali pia itaonekana imetendeka.” alisema Tenga, ambaye alishatangaza kuwa hatagombea tena urais baada ya kuliongoza Shirikisho kwa vipindi viwili vya miaka minne kila kimoja.

“Lengo letu ni kuhakikisha maagizo hayo yanatekelezwa na uchaguzi kufanyika mapema iwezekanvyo kabla ya tarehe iliyotolewa. Yale mambo nayoweza kufanyika kwa pamoja yatafanyika ili tuharakishe utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na FIFA.”
Uchaguzi wa TFF ulipangwa kufanyik tarehe 23 na 24 Februari 2013 na ulikuwa ukielekea ukingoni, lakini baadhi ya wagombea walienguliwa katika hatua ya mwisho na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF na ndipo walipo andika barua FIFA kuomba iingilie kati.

Rais Tenga alisema kuwa ujumbe wa FIFA ulikutana na pande zote zilizoathiriwa na mchakato wa uchaguzi na kwamba baada ya kukusanya taarifa hizo, maagizohayo ya FIFA sasa yatakuwa ni suluhisho la matatizo ya muda mrefu katika uendeshaji wa mpira wa miguu nchini.

Katika barua hiyo, FIFA imeiagizaTFF:
1.   Kuunda vyombo sahihi (Kamati ya Maadili itakayokuwa na vyombo viwili ambavyo ni cha kutoa maamuzi ya awali na cha rufaa) ambavyo mamlaka yake yatakuwa ni kushughulikia masuala ya ukiukwaji wa maadili;
2.   Kufanya mabadiliko ya katiba kwa kuzingatia uundwaji wa vyombo hivyo;
3.   Kuanza upya kwa mchakato wa uchaguzi wa Kamati ya Utendaji kwa kufungua milango kwa wagombea ambao walishachukua fomu na wagombea wapya:
4.   Shughuli hiyo ikamilike ifikapo tarehe 30 Oktoba 2013.
Katika kutekeleza hayo, TFF inatakiwa iitishe Mkutano Mkuu wa Dharura kwa ajili ya kufanya mabadiliko ya Katiba kwa ajili ya kuunda kamati hizo za maadili na Kanuni za Uchaguzi kabla ya kuendelea na Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Kamati Mpya ya Utendaji.

Katika maoni yake FIFA imeeleza kuwa katika mchakato, Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliwaengua au kupitisha baadhi ya wagombea kwa kubaini kuwa walikiuka Ibara ya 9 (7) ya Kanuni za Uchaguzi na pia Ibaray a 29 (7) ya Katiba ya TFF ambavyo vinahusisha suala la kufungua kesi mahakamani, kufuja fedha za shirikisho na ukosefu wa uwajibikaji wa pamoja.

Hata hivyo, FIFA ilisema kuwa watu hao walitakiwa waadhibiwe kwanza na kamati husika (kamati za maadili) kabla ya kuenguliwa na kamati za uchaguzi za TFF.

“Kutokana na ukosefu wa kamati za maadili matokeo yake, mmoja wa wagombea amekuwa akienguliwa kwenye uchaguzi kila anapombea bila ya kujua adhabu yake ni ya muda gani,” inasema barua hiyo ya FIFA.

Rais Tenga ameagiza kuitishwa kwa kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji ya TFF kupokea maagizo ya FIFA na kupanga ratiba ya utekelezaji wake kwa lengo la kuhakikisha kuwa mchakato huu unatekelezwa mapema iwezekanavyo.


Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

BREAKING NEWS: FIFA YAAMURU MCHAKATO WA UCHAGUZI MKUU WA TFF UANZE UPYA - MALINZI, WAMBURA, WOTE NDANI SASA

Wiki kadhaa baada ya shirikisho la soka duniani kutuma ujumbe wake kuja kufuatilia suala la uchaguzi mkuu wa TFF uliogubikwa na matukio kadhaa ya utata, leo hii shirikisho hilo la soka duniani limetoa maamuzi ya mchakato wote wa uchaguzi mkuu wa TFF kuanza upya, kwa maana wale wagombea wote waliokatwa wanaweza kurudi kwenye mchakato wa uchaguzi.

Taarifa nilizonazo FIFA imeshatuma barua ya kuelezea uamuzi kwa TFF na muda mchache ujao TFF inatarajiwa kutoa taarifa rasmi kuhusu uamuzi huo wa FIFA.

Kwa taarifa zaidi kuhusu suala hili endelea kutembelea www.shaffihdauda.com

CHEKA HANA MPINZANIA TANZANIA - AMKUNG'UTA MASHALI KWA KNOCKOUT


Bondia Fransic Cheka Kushoto akipambani na Thomas Mshali wakati wa mpambano wao uliofanyika katika sikukuu ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam Cheka alishinda kwa KNOCKOUT raundi ya kumi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Fransic Cheka Kushoto akimshambilia kwa makonde ya nguvu Thomas Mshali wakati wa mpambano wao uliofanyika katika sikukuu ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam Cheka alishinda kwa KNOCKOUT raundi ya kumi Picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Yusuph Jibaba wakati wa mpambano wao uliofanyika mei mosi katika ukumbi wa PTA Saba saba Dar es salaam Star Boy alishinda kwa KNOCKOUT raundi ya nne Picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Yusuph Jibaba wakati wa mpambano wao uliofanyika mei mosi katika ukumbi wa PTA Saba saba Dar es salaam Star Boy alishinda kwa KNOCKOUT raundi ya nne Picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Yusuph Jibaba wakati wa mpambano wao uliofanyika mei mosi katika ukumbi wa PTA Saba saba Dar es salaam Star Boy alishinda kwa KNOCKOUTraundi ya nne Picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' akishangilia ushindi uku akiwa amebebwa juu juu kama mkungu wa ndizi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Cosmas Cheka kushoto akipambana na Charles Mashali wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba siku ya mei mosi Cheka alishinda kwa ponti mpambano huo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' akimsindikiza wakati wa kupigana bondia Ibrahimu Class 'King class Mawe wakati wa mpambano wake na amos mwamakula
Bondia Amos Mwamakula kushoto na Ibrahimu Class 'King Class mawe' wakisubili matokeo ambapo class alishinda kwa point Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Thomas Mashali kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fransic Cheka katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam Cheka alishinda kwa KNOCKOUTShomari kimbau akiwa na Cheka baada ya kumvisha ubingwa wa IBF Africa aliokuwa akiutetea
Kotoka kushoto ni Kocha wa mchezo wa ngumi Kimataifa Rajabu Mhamila 'Super D' mdau ambaye ajajulikana jina Mtaalishaji wa mpambano kati ya Fransic Cheka Vs Thomasi Mashali Adamu Tanaka 'Tunaluza' na MC wa mpambano huo COOL p
Rashidi Mhamila 'Ngade akiwa amepozi na Bady Boy wakati wa onesho hilo

TAKWIMU: BARCA VS BAYERN - MAN UNITED NDIO ILIKUWA TIMU YA MWISHO KUITOA BARCA KWENYE UCL BILA NYAVU ZA KUGUSWA - BAYERN WAWEKA REKODI KUFUZU KUCHEZA FAINALI KWA USHINDI WA MABAO MENGI


Takwimu ziliuzunguka ushindi 7-0 wa FC Bayern Munich dhidi ya Barcelona katika hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya

* Bayern wameweza kufuzu kwenda fainali kwa jumla ya ushindi mkubwa kuliko wowote kuwahi kutokea kwenye historia ya ligi ya mabingwa wa ulaya.

* Kiungo wa Bayern Munich Thomas Mueller amefunga mabao nane na kutoa assists mbili katika ligi ya mabingwa wa ulaya msimu huu

Barcelona walikuwa hawajafungwa katika michezo 12 ya Champions League kwenye uwanja wao wa nyumbani - mara ya mwisho walifungwa 2-1 na Rubin Kazan mwezi October 2009.

* Mara ya mwisho Barcelona kufungwa katika mechi zote mbili za hatua ya mtoano kwenye ligi ya mabingwa wa ulaya ilikuwa ni mwaka 1987, wakifungwa na klabu kutoka Scotland ya Dundee United.

* Manchester United ndio ilikuwa klabu ya mwisho kuizuia FC Barcelona kutokufunga bao katika nusu fainali ya klabu bingwa ya ulaya - mwaka 2008. Mechi ya kwanza Nou Camp walitoka sare 0-0, mechi ya pili Old Trafford Scholes akafunga bao pekee la mchezo na kuwatoa Barca.

*Barcelona wameshindwa kufunga goli katika kipindi cha kwanza katika mechi nne zilizopita.

* Wachezaji wa Barca Victor Valdes na Xavi wameweza kuifikia rekodi ya Edwin Van Der Sar ya kucheza mechi nyingi za nusu fainali ya UEFA Champions league. Mechi 14.

KALI YA LEO: ANGALIA NAMNA MASHABIKI WA REAL MADRID WALIVYOIDHIHAKI BARCELONA KWA KUFUNGWA JUMLA YA 7-0

 Pictures: The photoshoppers rip into Barcelona after their mega loss against Bayern Munich
Hapa wanamaanisha kwamba kinywaji cha 7up kimekuwa mdhamini mpya wa jezi za Barcelona


 Pictures: The photoshoppers rip into Barcelona after their mega loss against Bayern Munich Pictures: The photoshoppers rip into Barcelona after their mega loss against Bayern Munich Pictures: The photoshoppers rip into Barcelona after their mega loss against Bayern MunichScreen+Shot+2013 05 02+at+12.43.15+AM Pictures: The photoshoppers rip into Barcelona after their mega loss against Bayern Munich Pictures: The photoshoppers rip into Barcelona after their mega loss against Bayern Munich
bjnc0oncqaeggcg Golazo! Israel Damonte 30 yard bullet (Nacional) v River Plate
Mchezaji wa zamani wa Bayern Munich Bixente Lizarazu akiwa na jezi ya Barcelona - alisaliti chama