Search This Blog

Friday, May 3, 2013

RASHID MATUMLA: MUDA WANGU WA KUSTAAFU NDONDI BADO HAUJAFIKA

MABONDIA watatu wa ngumi za kulipwa ambao ni wadogo wa veteran wa ndondi hapa nchini, Rashid Matumla wamestaafu kucheza ndondi.

Hata hivyo wakati mabondia hao wakistaafu, kaka yao amedai muda wake wa kustaafu bado haujafika na kusisitiza ataacha ndondi siku atakapopigwa na mabondia chipukizi.

Matumla alithibitisha kustaafu kwa wadogo zake hao na kuwataja kuwa ni Hassan, Mkwanda na Karim ambao waliwahi kufanya vizuri hapa nchini na nje ya nchi.

"Karim alikuwa akicheza Australia na Mkwanda alikuwa Sweden," alisema Matumla na kuongeza kuwa wote waliwahi kucheza hapa nchini kabla ya kuamia kwenye nchi hizo.

"Nje ya nchi kucheza ngumi inakuwa ngumu kutokana na sheria zao hivyo kujikuta wote wakiachana na ndondi hivi sasa hawawezi kabisa kucheza," alisema.

1 comment:

  1. Ulishawahi kuaibika kwa kuendekeza njaa,nadhani next time utapata kichapo kitakachosababisha uzimie ulingoni na hatimaye kuzindukia hospital.Tafuta kazi ufanye hata kama ni kuuza machungwa kuliko kutafuta aibu.

    ReplyDelete