Search This Blog

Saturday, March 17, 2012

MOHAMED BANKA AIBIWA VIFAA MUHIMU VYA GARI YAKE LEO HII.

Kiungo wa zamani wa klabu za Simba na Yanga Mohamed Banka leo amefanywa kitu kibaya na vibaka baada ya kuibiwa vitu mbalimbali katika gari yake. Banka aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
"wezi noma leo wameniliza kila kitu chenye umuhimu ndani ya gari daah wame vunja kioo kidogo cha nyuma basi wakazama ndani ya ndinga asubuh kwenye mechi zetu duuh haya bana alafu nimeambiwa vimepatikana wanataka pesa ni vikomboe"

MGOSI NA TIMU YAKE WAWAFUNIKA SAMATA NA TP MAZEMBE

DC Motema Pembe, klabu inayobebwa na mshambuliaji wa Kitanzania, Mussa Hassan Mgosi hivi sasa ndio inaongoza Ligi Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Timu hiyo ya mfungaji bora wa zamani wa Ligi Kuu hadi jana ilikuwa imekwishacheza mechi tatu, kushinda mbili na sare moja hivyo ina pointi saba.
Katika mechi ya kwanza, DCMP iliifunga Elima 2-0 ugenini na mechi ya pili iliifunga Saint-Luc 3-1 kabla ya kutoa sare ya bila kufungana na Makiso Jumatano.
Wababe hao wa Simba katika Kombe la Shirikisho mwaka jana, kesho wanashuka tena dimbani kumenyana na Muungano.
Timu nyingine katika Ligi Kuu ya DRC yenye washambuliaji wawili chipukizi wa Kitanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu na Mbwana Ally Samatta, Tout Puissant Mazembe inashika nafasi ya tatu kwa pointi zake sita, ingawa yenyewe imecheza mechi mbili tu.
Mechi ya kwanza ilishinda 5-0 dhidi ya Tshinkunku na ya pili 1-0 dhidi ya Sanga Balende, wakati leo inamenyana na Molunge.
Machi 22, TP Mazembe itaanza kampeni zake za kuwania taji la tano la Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kumenyana na Power Dynamos ya Zimbabwe mechi ya kwanza wakicheza ugenini kabla ya kurudiana nyumbani Lubumbashi wiki mbili baadaye.
Source:Bongostaz.blogspot.com

HAMIS KIIZA AIPANDISHA YANGA NAFASI YA PILI NA GOLI LA DK. ZA MAJERUHI

  Goli la dakika ya 89 lililofungwa na Hamisi Kiiza jioni hii wakati Yanga ilipocheza na Villa Squad Uwanja wa Taifa,  Dar es Salaam katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara, liliiwezesha Yanga kutoka kifua mbele kwa kujipatia pointi tatu muhimu katika ligi hiyo.
Yanga sasa inapanda hadi nafasi ya pili, kwa kutimiza pointi 43 baada ya kucheza mechi 20, sawa na vinara Simba SC wenye pointi 44, ambao leo wanacheza mechi ya 21 na Mtibwa Sugar. Azam yenye pointi 41, inashuka hadi nafasi ya tatu na kuwaachia ‘wanaume’ anga zao.
Kiiza aliipatia timu yake bao hilo pekee baada ya kumalizia kazi nzuri iliyoanzishwa na Haruna Niyonzima kisha Godfrey Taita kuachia shuti kali la mbali lililomkuta mfungaji aliyekwamisha wavuni  na kuwainua mashabiki wao katika dakika hizo za lala salama ambao walikuwa vichwa chini wakitarajia mechi hiyo ingekwisha kwa suluhu.
Hasa baada ya Davies Mwape kuwakatisha tamaa kwa kukosa nafasi nyingi za kufunga hasa ile ya dakika 69 baada ya Pius Kisambale kumtengenezea mpira mzuri hivyo kuwakera mno mashabiki wao.
Mbali ya Mwape, Kenneth Asamoah naye alikosa bao la wazi akiwa yeye na kipa wa Villa Squad, Daudi Mwasongwe dakika ya 57 aliposhindwa kuitendea haki krosi ya Haruna Niyonzima.
Villa itabidi ijilaumu kuruhusu nyavu zao kutikiswa dakika za lala salama kwani walikuwa wameishawabana Yanga kwa kuonyesha kandanda safi na kuufanya mchezo huo kuwa mgumu kwa pande zote lakini wakishindwa kuhimili vishindo.
Katika nafasi ambazo Villa itazijutia, ni dakika ya 22 baada ya mchezaji wao, Martin Rupert kupiga mpira nje ya lango  la Yanga akiwa peke yake na kushindwa kucheka na nyavu huku mchezaji huyo akiendelea kufanya makosa ya kushindwa kucheka na nyavu dakika 71 baada ya kumpoka mpira Oscar Joshua.
Hata hivyo pambano hilo ambalo matokeo yake yalikuwa yakisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka, lilikuwa zuri na kuwa kivutio kwa mashabiki waliojitokeza uwanjani.
Katika mchezo mwingine leo, Coastal Union imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya maafande ya JKT Orjolo huo pia ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu.
Bao la Coastal Union lilifungwa dakika ya 18 na Salum Sued kwa penati baada ya  mchezaji mwenzake, Daniel Lyanga kukwatuliwa katika eneo la hatari na mchezaji wa JKT Orjolo, Omary Mswaki.
Ligi hiyo itaendelea leo katika viwanja viwili ambapo katika Uwanja wa Jamhuri Morogoro, Simba itatoana jasho na Mtibwa Sugar huku katika dimba la Chamazi, wenyeji Azam FC ikiwakaribisha maafande wa Ruvu Shooting.

Vilabu 10 bora barani Africa ktk kipindi cha muongo mmoja.

Shirikisho la kimataifa la takwimu na historia za mchezo wa soka ulimwenguni limetoa orodha ya vilabu 300 bora kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita ( 2001-2010 )

1- Al-Ahly (Egypt)
2- Espérance Sportive de Tunis (Tunisia)
3- Etoile Sportive Sahel (Tunisia)
4-ASEC Mimosas (Ivory Coast)
5- Cotonsport FC (Cameroon)
6- Enyimba International FC (Nigeria)
7- Zamalek SC (Egypt)
8-Al-Hilal Omdurman (Sudan)
9- Jeunesse Sportive Kabylie (Algeria)
10- Asante Kotoko SC (Ghana)

MABONDIA WAPIMA UZITO LEO KWA AJILI YA MPAMBANO WAO KESHO

RAMADANI SHAULI GABRIEL OCHIANG WAPIMA UZITO KWA AJILI YA MPAMBANO WAO KESHO
 Bondia Ramadhani Shauli akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Gabriel Ochiang wa Kenya kulia picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/

 Mabondia Ramadhani Shauli wa Tanzania (kushoto) na Gabliel Ochiang wa Kenya wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito, Dar es salaam LEO kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika KESHO katika ukumbi wa friens Coner Manzese. picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/

Mabondia Ramadhani Shauli wa Tanzania (kushoto) na Gabliel Ochiang wa Kenya wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito, Dar es salaam LEO kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika KESHO katika ukumbi wa friens Coner Manzese.picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/


Baadhi ya mabondia pamoja na viongozi wa mchezo wa ngumi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupima uzito leo

SIMBA NAO WAPO MANUNGU KUPAMBANA NA WATEJA WAO MTIBWA.

Kikosi cha Simba
Viongozi wa ligi kuu ya Tanzania bara Simba Sports Club, kesho inatarajiwa kuendeleza harakati zake za kuipokonya Yanga ubingwa wa Yanga, itakapokuwa mgeni wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Wanamsimbazi ambao wanaongoza ligi hiyo kwa pointi zao 44, wakifuatiwa na Azam yenye pointi 41, wakati Yanga, mabingwa watetezi wana pointi 10, mara ya mwisho ilifungwa na Mtibwa, Machi 22, mwaka 2009, bao la Omar Matuta lakini tangu hapo wamekuwa wakishinda mfululizo.

Simba inayonolewa na Mserbia Milovan Cirkovic, pamoja na kutarajiwa kulinda rekodi yake mbele ya Mtibwa inayofundishwa na Mkenya, Thom Olaba lakini pia inahitaji kuendeleza wimbi la ushindi katika mechi za ugenini, ikitoka kuifunga Polisi mjini Dodoma 1-0.

Kesho, wachezaji wa kigeni wanatarajiwa kuendelea kuonyesha umuhimu ndani ya Simba kwa kuifungia timu hiyo mabao.
Hadi sasa mabao ya Simba katika Ligi Kuu zaidi yamefungwa na Mnyarwanda Patrick Mutesas Mafisango na Mganda Emmanuel Okwi.     

REKODI YA SIMBA NA MTIBWA TANGU 2005:
                        P      W     D     L      Gf    Ga   Pts
Simba SC        12    8      3      1      19    6      27
Mtibwa Sugar 12    1      3      8      6      19    6
Septemba 25, 2011
Simba 1-0 Mtibwa Sugar
Feb 27, 2011
Simba 4-1 Mtibwa Sugar
Sept 29, 2010
Mtibwa Sugar 0-1 Simba              
Machi 22, 2009
Mtibwa Sugar    1-0 Simba  
Sep 28, 2008
Simba 1-0 Mtibwa Sugar  
Apr 21, 2010    
Mtibwa Sugar    0-4 Simba  
Nov 15, 2009
Simba 3-1 Mtibwa Sugar 
Feb 20, 2008
Simba 1-1 Mtibwa Sugar 
Okt 7, 2007
Mtibwa Sugar    1-3 Simba
2007: Hazikukutana kwenye Ligi ndogo
Sept 10, 2006
Mtibwa Sugar       1-1 Simba
Apr 9, 2006
Simba 1-1 Mtibwa Sugar
Okt 5, 2005
Simba 2-1 Mtibwa Sugar
Mei 22, 2005
Mtibwa Sugar 0-1 Simba  

YANGA KUENDELEZA VIPIGO KWA VILLA SQUAD LEO?

Mabingwa wa soka wa Afrika mashariki na kati na Tanzania Bara, Yanga leo wanaingia uwanjani kucheza na Villa Squad kwenye mechi ya marudiano ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salam.

Mechi hiyo inakutanisha timu hizo zikiwa kwenye mazingira tofauti, Yanga ikiwania kutetea taji lake na Villa ikipambana kubaki kwenye Ligi Kuu msimu ujao, mazingira hayo ndiyo yanaufanya mchezo huo kutotabirika.

Kocha wa Villa Squad, Habib Kondo ambaye timu yake inashika nafasi ya pili kutoka chini ikiwa na pointi 16 kwa michezo 19 wana kila sababu ya kupambana kwa nguvu leo kuhakikisha wanaibuka na ushindi.

Kondo alikaririwa wiki chache baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba akisema watapambana kuibakisha timu hiyo kwenye Ligi Kuu, hivyo ni wazi atataka kuendeleza rekodi hiyo kwa kuifunga na Yanga, ambayo pia ni moja ya vigogo vya soka hapa nchini.

Yanga inayoshika nafasi ya tatu baada ya michezo 19 ikiwa na pointi 40 nyuma kwa mchezo mmoja na hasimu wake Simba yenye pointi 44 inayoongoza ligi hiyo na nyuma kwa mchezo mmoja dhidi ya timu inayoshika nafasi ya pili ya Azam yenye pointi 41 ni wazi itataka kuendeleza ushindi wa bao 1-0 ilioupata dhidi ya African Lyon Jumatano ili kuisogelea Simba na kuwa mbele kwa pointi mbili dhidi ya Azam.

Kwenye mchezo dhidi ya Lyon, Yanga ilicheza bila ya nyota wake tisa wa kikosi cha kwanza kwa kufungiwa na Shirikisho la Soka nchini(TFF) na wengine wakitumikia adhabu ya kadi nyekundu ama kuwa majeruhi.
Wachezaji hao ni Haruna Niyonzima, Athumani Idd, Hamisi Kiiza, Juma Seif, Nurdin Bakari, Omega Seme, Jerry Tegete, Nadir Haroub na Stephan Mwasika.
Lakini kwenye mchezo wa leo inatarajia kuwa na Athumani Idd, Hamisi Kiiza na Juma Seif ambao wamemaliza kutumikia adhabu ya kadi zao, huku ikiendelea kuwakosa Nurdin Bakari, Nadir Haroub na Omega Seme waliofungiwa kutocheza mechi tatu, huku Tegete na Mwasika wakifungiwa kwa kipindi cha miezi sita na mwaka mmoja kila mmoja.
Kurudi kwa baadhi ya nyota hao kunaweza kuwa faraja kwenye kikosi cha timu hiyo, kwani kilionekana kucheza vibaya kwenye mechi iliyopita dhidi ya African, aidha kuendelea kukosekana kwa baadhi ya nyota hao kwenye mchezo huo kunaweza kuwa faida kwa Villa Squad kwenye mchezo wa leo.
Kwenye mchezo wa awali uliochezwa Uwanja wa Azam Chamazi, Yanga iliifunga Villa mabao 3-2, mabao ya Niyonzima, Asamoah na Kiiza.

REKODI YA YANGA NA VILLA SQUAD:
P  W     D     L      Gf    Ga   Pts
Yanga SC        3  2      -       1      12    7        9
Villa Squad     3  1      -       2      7      12    3
Septemba 21, 2011
Yanga 3-2 Villa Squad
Aprili 27, 2009
Yanga  4-5 Villa Squad   
Septemba 21, 2008
Villa Squad 0-5 Yanga

Friday, March 16, 2012

WEZI WAINGIA CHUMBA CHA KUIFADHIA MAKOMBE UWANJA WA EMIRATES - WATOKA KAPA.

Source: Sky Sports.

HASHEEM THABEET AONDOKA HOUSTON ROCKETS - AJIUNGA NA PORTLAND TRAIL BLAZERS

 Ligi kuu ya Mpira wa kikapu NBA hapo Jana ilifunga dirisha lake la Usajili wa wachezaji ambapo kwa sasa timu hazitaruhusiwa tena Kufanya mabadilishano ya wachezaji hadi hapo msimu utakapomalizika. 


 Kufungwa kwa dirisha Hilo kunamaanisha kuwa mchezaji aliyekuwa anatarajiwa kuihama timu Yake Dwight Howard ataendelea kubaki na Orlando Magic hadi mwisho wa msimu huu ambapo mkataba wake utakuwa unakamilika. 


Taarifa toka kwa wawakilishi wa Howard zinasema kuwa mchezaji huyo ameeleza dhamira yake ya kutaka  kuongeza mkataba wake kwenye timu hiyo japo wengi wanaamini kuwa Orlando Magic itampoteza mchezaji huyu kwani anaona kubakia kwenye timu hiyo kutamzuia kupata nafasi ya kutwaa ubingwa wa ligi ya NBA.


Hata hivyo tarehe hiyo ya mwisho ya mabadilishano ya wachezaji imeshuhudia Mtanzania anayecheza kwenye ligi hiyo akibadilisha timu kwa mara ya tatu, Hasheem Thabeet amehamishwa kwenye timu ya Portland Trail Blazers akitokea kwenye timu ya Houston Rockets .

WATU 75 WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA KESI YA VURUGU UWANJANI NCHINI MISRI

Nchini Misri huku familia mbalimbali zikiendelea kuomboleza vif via wapendwa wao waliopoteza maisha kwenye vurugu zilizozuka uwanjani katika Mchezo wa ligi kuu Kati ya national al ahly na al masry, watu 75 wamepandishwa kizimbani kujibu tuhuma za kushiriki kwenye vurugu hizo.


Waliopandishwa kizimbani ni pamoja na maafisa tisa wa jeshi la polisi akiwemo mkuu wa jeshi Hilo meja jenerali Issam samakk. Kwa kujibu wa taarifa ya mwendesha mashtaka wa mahakama kuu nchini misri, vurugu zilizotokea siku ya mchezo zilipangwa kabla  na ushahidi wa kila mikanda ya televisheni unaonyesha baadhi ya mashabiki wakitumia silaha walizoingia nazo uwanjani wakiwa na malengo ya kuwadhuru mashabiki wa timu pinzani.


 Kwa upande wa washtakiwa ambao ni maafisa wa jeshi la polisi wanatuhumiwa kwa kushindwa kudhibiti hali iliyotokea huku wakijua kuwa baadhi ya mashabiki walikuwa na lengo la kuanzisha vurugu. 


 Nayo timu timu ya Al Masry ambayo mashabiki wake ndio walioanzisha vurugu hizo, inatarajiwa kupewa adhabu kali ambayo wengi wanaamini adhabu hiyo huenda ikawa ya kushushwa daraja huku uwanja wake ukifungiwa kutotumika kwa michezo yoyote ya kiushindani.

CHELSEA YAPANGWA NA BENFICA - HUKU BARCELONA AKIWASUBIRI HATUA YA NUSU FAINALI

 Real Madrid v Apoel Nicosia


Barcelona v AC Milan

Marseille v Bayern Munich 

Chelsea v Benfica


Mtanange utakavyokuwa.
 Ratiba ya hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa imepangwa hii Leo huko Munich . 
Ratiba hiyo inaonyesha kuwa Mabingwa watetezi Fc Barcelona watavaana na Ac Milan,
 huku Real Madrid wakicheza na Apoel Tel Aviv , michezo mingine itawakutanisha Chelsea na Benfica huku Bayern Munich wakicheza na Olympic Marseile.
Michezo ya robo fainali itapigwa tarehe 27 na 28 kwa michezo ya kwanza huku ile ya marudiano ukichezwa Kati ya tarehe 3 na 4 mwezi aprili. 


Kwa upande wa robo fainali ya ligi ya Europa , Az alkamaar watacheza dhidi ya valencia cf , schalke 04 watakipiga dhidi ya athletic Bilbao , Sporting Lisbon watacheza na Metalist Kerkiv huku Athletico Madrid wakicheza na Hanover 96 ,michezo hii itachezwa Kati ya tarehe 29 machi na tarehe 5 aprili.

VILLA SQUAD, YANGA KUCHEZA TAIFA

Timu za Villa Squad na Yanga zinapambana kesho (Machi 17 mwaka huu) katika mechi namba 142 ya Ligi Kuu ya Vodacom itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Viingilio katika mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Oden Mbaga mwenye beji ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) vitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B na sh. 15,000 kwa VIP A. Mechi hiyo itaanza saa 10 kamili jioni.

Mechi nyingine ya kesho namba 144 itachezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga ambapo Coastal Union watakuwa wenyeji dhidi ya Oljoro JKT ya mkoani Arusha.

Ligi itaendelea tena Jumapili (Machi 18 mwaka huu) kwa mechi mbili. Mtibwa Sugar itaikaribisha Simba kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati Azam watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting Stars kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam.


WATANZANIA WATEULIWA KUCHEZESHA CONGO
Mwamuzi Waziri Sheha wa Tanzania ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuchezesha mechi namba 51 ya Kombe la Shirikisho kati ya AC Leopards ya Jamhuri ya Congo na Club Sportif Sfaxien ya Tunisia.

Katika mechi hiyo itakayochezwa jijini Brazzaville kati ya Machi 23, 24 na 25 mwaka huu, Sheha atasaidiwa na waamuzi John Kanyenye na Ferdinand Chacha wakati mezani atakuwa Ramadhan Ibada. Waamuzi wote hao wasaidizi pia wanatoka Tanzania. Kamishna atakuwa Zeli Sinko kutoka Ivory Coast.

Naye Hafidh Ally wa Tanzania ameteuliwa kuwa Kamishna wa mechi namba 53 ya Kombe la Shirikisho kati ya Lydia LB Academic ya Burundi na Enppi ya Misri itakayochezwa jijini Bujumbura kati ya Machi 23, 24 na 25 mwaka huu.


Powered by Sorecson : Creation de site internet
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

AZAM FC ITAWEZA KUTIMIZA MALENGO?

Jina la Timu
Azam Football Club
Kuanzishwa
24 June 2007
Uwanja

Chamanzi Complex, na Taifa Dar es Salaam
Mwenyekiti
Abubakar Bakhresa
Kocha
Stewart Hall
Ligi
Vodacom Primier League
       
Ajax Cape Town ya Afrika ya Kusini,  Ajax ambayo ilianzishwa mwaka 1999 kwa muunganiko wa klabu za Merger of Seven Stars na Cape Town Spurs ambayo iliwaibua nyota wanaotamba duniani kama Steven Piennar, na Obi Mikel hivi sasa ni moja kati ya timu zenye kutazamwa kama kiini cha uzalishaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo, pia timu hiyo imekuwa ikipata nafasi ya kucheza michuano ya CAF.
Azam FC ambao lengo lao kubwa ni kutwaa ubingwa na kutinga katika michuano ya Afrika msimu huu, imeonesha mwanga na hivi sasa ina wachezaji wengi ambao wanaichezea timu ya taifa. Uwezo mdogo wa kiuzohefu unafunikwa na mafanikio ya klabu hiyo kucheza kama timu isiyo na staa, Azam wanacheza kwa ushirikiano mzuri na wachezaji wake wanacheza kwa viwango bora kama timu moja, ambayo inafanya kazi kwa pamoja. Baada ya misimu mitatu ya kumaliza katika nafasi ya tatu sasa “Wana lamba lamba” hao wanasaka taji la kwanza la ligi kuu, Bara. Hivi sasa wapo pointi sawa na Simba katika kilele cha uongozi katika ligi kuu.
         IMETOKEA WAPI TIMU HII?
“Wafanyakazi wa moja ya viwanda waliamua kuanzisha timu hii kwa blengo la kujifurahisha mwaka 2004. Ikiitwa Mzizima FC . Mwaka 2005 tuliamua kuisajili na kushiriki katika ligi daraja la tatu, na tukafanikiwa kuwa mabingwa wa Mkoa wa kisoka, Ilala.” Anasema kocha msaidizi wa  zamani wa klabu hiyo Mohammed Seif King. “Msimu wa mwaka 2006 wakati tukiwa katika maandalizi ya ligi daraja la pili TFF ikafuta ligi za madaraja, kuanzishwa hii ligi ya TFF kuanzia ngazi ya wilaya. Mwaka 2007 hatukufanya vizuri, nkatika ligi hiyo ya TFF, hapo ndipo tukamuomba Kurugenzi atusaidie katika kutafuta wachezaji wenye uwezo na kuwagharamikia ili tupate nafasi ya kucheza ligi kuu” anaeleza kocha huyo ambaye alikuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa kwanza wa Azam FC.
JUlai, 27 mwaka 2008 baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Majimaji kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma, Azam FC ikapanda daraja na kuwa miongoni mwa timu za ligi kuu.  Kwa sasa Azam ni moja ya timu nne zenye nguvu nchini, na wamekuwa washindani wa kuwania ubingwa kwa msimu wa tatu sasa, uku tangu wapande daraja wamemaliza katika nafasi ya tatu mara tatu. Azam ambayo ilipandishwa daraja na wachezaji nyota waliotamba miaka ya nyuma kama Suleiman Matola, Shekhan Rashid, Kamba Lufo, Boniface Pawassa, Steven Nyenge, Salehe Hilal na wengineo inaweza kufikia matarajio yao hayo kama wachezaji wa sasa wataweka nia nia kwa dhati na kufanya kazi uwanjani. WAkifaidikika na uwepo wa Mwalimu wa kigeni kutoka nchini England, Stewart Hall, Azam FC hivi sasa timu hii inanufaika na uwepo wa vifaa vya kisasa, uwanja  wa kisasa, zaidi ni kwamba wanaingiza pesa nyingi. “Walimu wa kigeni wana faida kubwa sana nchi kwani kila ambacho wamekuwa wakihitaji hupatiwa, tofauti na walimu wazawa ambao ni mara chache husikilizwa na kutimiziwa vitu muhimu anavyokuwa akihitaji, nakumbuka kuwa sisi wakati tunapandisha timu tulikabiliwa na changamoto nyingi, hasa kwenye masuala ya uhitaji wa vifaa, na mambo mengine muhimu, nakumbuka tulikuwa tukienda uwanjani tunapata katoni mbili tu za maji, lakini tazama sasa wanapata kila kitu, hiyo ni sababu moja wanayotakiwa wawe makini na kufanya kazi uwanjani, mana ubingwa hauji kwa kuongea katika vyombo vya habari. WAtambue kuwa kuna timu nyingine tatu ukitoa wao zina uwezo wa kutwaa ubingwa huo hivyo ni lazima wafanye kazi” anasema Mohammed Seif King ambaye alikuwa mukusanya “data” wa Neidor Dos Santos wakati alipokuwa kocha wa Azam na Itamor Amourin.
Wengi waichukulia Azam kama timu ambayo haitaweza kupambana na nguvu ya klabu kubwa za Simba na Yanga. Kwani timu kama Moro United ilishindwa kufanya hivyo katikati ya miaka ya 2000, Moro iliyokuwa na mkusanyiko wa wachezaji nyota nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla , ilikuwa pesa, na uwezo mzuri ndani ya uwanja, wakamaliza raundi nya kwanza kwa tofauti ya pointi 15 na aliyekuwa akishika nafasi ya pili, Yanga. Wakati huo ligi ikiwa na timu 16 uku kila timum ikicheza michezo 15 kwa kila raundi, Moro ilishindwa kiukusanya pointi 15 tu katika michezo 15 ya mzunguko wa pili, kwaqni Yanga walimaliza mabingwa wakiwa na pointi ambazo hazikuzidi 55, na Moro walikuwa na pointi 40 katika baada ya mzunguko wa kwanza tu, Je, “fitna” ambazo zimekuwa zifanywa na baadhi ya vilabu katika ligi kuu yetu vinaweza kuzuhia matarajio ya Azam FC kama ilivyowahi kutokea kwa timu kama, Pallsons, Moro United?
“Malengo ya mmiliki ni kuifanya klabu ya mfano, Tanzania na Afrika ya Mashariki yote. Hivi sasa ameamua kuwekeza kwa kiasi kikubwa cha pesa, amekamilisha awamu ya kwanza ya ujuenzi wa uwanja wa kisasa, ameamua kuwekeza katika soka la vijana, na uku akichukua wachezaji bora kutoka kila vsehemu anayoweza kufanya hivyo kutokana na mfuko wake ulivyo, tazama hata basi lao, ni la kisasa sana hiyo yote ni kwa sabababu mmiliki anataka timu yake iwe ya mfano na bora bzaidi katika ukanda huu na Afrika, kuhusu  kuchukua ubingwa msimu huu? Nadhani wanaweza, ila wanatakiwa watambue ubingwa hauji kwa maneno, bali ni kujiuliza mmejipanga vipi, kuchukua kombe la Mapinduzi ni mafanikio, lakini si kigezo cha kuchukua ubingwa wa ligi kuu, muhimu ni kufanya kazi na kupunga kuongea”  anasema kocha huyo, msaidizi wa zamani wa klabu hiyo, Seif King
     MATATIZO
Mohammed ambaye anakumbuka kuwa wakati wao wakipanda ligi kuu kulikuwa na ushirikiano mkubwa na umoja ndani ya timu, pamoja na matatizo madogomadogo bado timu iliweza kupanda na kucheza ligi kuu. Mara baada ya kupanda daraja, wachezaji wengi nyota walikuja ndani ya timu hii, mfano ni kama Osborn Monday, Cripsian Odula, Francis Ouma , Ibrahimu Shikanda ambao walikuwa ni wachezaji nyota wa Harambee Stars (timu ya taifa ya Kenya), Danny Wagaruka, Peter SenyondoBen Kalama, ambao walikuwa wachezaji wa Uganda, na wengineo lakini haraka nyota hao waliondolewa baada ya kushindwa kufanya mambo makubwa katika miaska yao ya mwanzo. Ni Ouma pekee ambaye aliuzwa, lakini ni wazi hata Shikanda ataondolewa ndani ya timu hiyo msimu ujao mana hana nafasi.
King ambaye alikuwa sehemu ya benchi la ufundi la timu hiyo kwa muda mrefu anasemaje kuhusiana na tatizo la wachezaji wa kigeni kushindwa kufanya vizuri ndani ya kabu hiyo. “ Ni kweli wachezaji hao walisajiliwa Azam wakiwa na viwango vizuri, nadhani kushindwa kwao kuwika kulitokana na haraka yetu ya kutaka kuona mafanikio ya haraka, kuna baadhi wangeweza kufanya vizuri kama vwangepata muda zaidi, na hilo ndiyo tatizo ambalo limekuwa liliikabili timu hii, wachezaji hawapewi muda wa kuzoea mazingira mapya”
Itamor Amourin aliweza kuwapatia nafasi nwachezaji vijana kama Himid Mao, Abubakary Salum “Sure Boy Jr” na wengineo, lakini pamoja na uwezo mzuri walionao nyota chipukizi ndani ya timu hiyo bado hawajaweza kuaminiwa na kocha wa sasa Stewart Hall, japo ni nyota hao wachanga ndiyo walikuwa sehemu ya timu ambayo ilimaliza katika nafasi ya tatu kwa mara ya kwanza wakiwa na wachezaji wazohefu kama kina Sghekhan, Shaban Kisiga, Salum Sued, Said Sued na wengineo. Azam ilishuhudia timu yao ya vijana ikifanya vizuri mfululizo katika michuano ya Uhai Cup kwa miaka miwili mfululizo na Itamor kuwapatia nafasi baadhi yao katikia timu ya wakubwa. Vijana kama Sino Agustino, Seleman Kassim “Selembe”, Tumba Sued, Jamal Mnyate, Salumu Machaku wote hawa wameanza kucheza ligi kuu wakiwa hapo, hivyo kuna haja ya Azam kuangalia aina yake ya usajili, Je usajili unafanywa na kocha au kuna mtu mwingine nje ya benchi loa ufundi? “ Mpira ni kitaru hivyo Azam wanatakiwa waweke malengo kuwa baada ya muda fulani hatutasajili tena kwa gharama kubwa, kwani watakuwa na yosso wao wanaowazalisha. Usajili watafanya kama sehemu ya kuongeza nguvu sehemu zenye mapungufu, pia wanatakiwa kuywapatia nafasi vijana wao chipukizina wachezaji wakigeni wanaokuwa wakiwasajili” anasema, Mohammed.
Azam inaweza kufanya vizuri na kutimiza lengo walilojiwekea, kwani wanacheza vizuri ndani ya uwanja, lakini kuna muda wa wenyewe, ukifika lazima wakaze “buti” na bukta zao kwani msimu uliopita waliokuwa watatu wakawa wa kwanza, na wa kwanza akamaliza wa tatu.

GALILE VS MASHALI WATAMBIANA KILA MMOJA KUNYAKUA UBINGWA

MABONDIA Selemani Galile na Thomas Mashali wanatarajia kupanda ulingoni Aprili 9 kuwania mkanda wa ubingwa wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBO) litakalofanyika katika ukumbi wa Friends Corner, Manzese Dar es Salaam.
Pambano hilo linatarajiwa kuwa kati uzito wa kg 75 raundi 10 likiratibiwa na TPBO.
Wakitambiana Dar es Salaam jana, wakati wa kuonyeshwa mkanda huo Galile alisema atahakikisha anafanya mazoezi ya kutosha ili kuweza kuunyakua mkanda huo kwani anauhakika atauchukua kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao.
"Mkanda lazima niiuchukue kwani najua Mashali haniwezi na hataweza kunifanya nisichukue mkanda hivyo najiamini na mkanda ni wangu," alisema Galile.
Naye kwa upande wake Mashali alisema raundi 10 ndio zitaamua mkanda ni wanani lakini anaimani ataunyakuwa kwani anamazoezi ya kutosha na bado ataendelea kujifua na kuhakikisha anaibuka bingwa.
"Ninauwezo, nimejipanga na ninauhakika nitaunyakua mkanda lakini yote raundi 10 ndio zitaamua nani bingwa," alisema.
Naye kwa upande wake Rais wa TPBO, Yassin Abdalah alisema mkanda huo ulikuwa wazi hivyo wakaamua kuwaambia mapromota ambapo alijitokeza Prospa Rweyomamu ambaye ndio ameandaa pambano hilo hivyo bingwa atakayepatikana ndio utakuwa kwake akisubiri mpinzani


Mbali ya kuwepo na mpambano huo siku hiyo kutakuwa na huuzwaji wa DVD za Mafunzo ya Mchezo wa Masumbwi wakiwemo mabondia Lenox Lewis, Evander Holfiled,David Haye, Waldmil Klitichiko,Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roj Jones na wengine wengi
Zitakuwa zikisambazwa kwa ajili ya kuwapa mabondia,mashabiki marefarii kutambua sheria na kanuni za mchezo huo Duniani ambazo zimeandaliwa na Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini, Rajabu Mhamila Super D Alisema kuwa tangia aanze kutoa mafunzo kwa njia hiyo watu wengi wameanza kuwa na uwelewa wa mchezo wa masumbwi nchini kwa kutambua sheria na mambo mbalimbali ya mchezo alisema Super D boxing Coach ambapo mpaka sasa ameweza kutoa matoleo nane tofauti ya mabingwa wa ngumi Duniani Akichanganya na mabondia wa Nchini.


 Mabondia, Selemani Galile kushoto na Tomasi Mashali wakitazamana kwa usongo wa kila mmoja kutaka kuchukua mkanda wa ubingwa wa mchezo wa masumbwi wa Oganaizesheni ya ngumi za Kulipwa Nchini TPBO walipokuwa wakitambulisha mpambano wao. Dar es Salaam jana, utakaofanyika Apri 9.katikati ni Rais wa Oganaizesheni hiyo Yasin Abdallah Mwaipaya.(Picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/)


USHIRIKIANO KUTOKA LA MASIA - MESSI NA FABREGAS NA MAAJABU YAO NDANI YA BARCELONA.


Ushirikiano wao ulianzia miaka mingi iliyopita wakiwa timu ya watoto pale La Masia.
Wanaume hawa wawili mpaka sasa kwa pamoja wameshatupia kambani magoli 65 kati ya 143 yaliyofungwa na timu yao msimu huku wakiwa na jumla ya assists 47 kwa pamoja.
Waite Lionel Messi na Cesc Fabregas marafiki wa miaka mingi iliyopita wanaondelea kuwaumiza watu na uwezo wao wa kucheza soka.


Messi pia kwa pamoja na Xavi ndio wachezaji wanaongoza kwa kutoa pasi nyingi katika tatu ya mwisho ya uwanja katika ligi kubwa barani ulaya.
Messi mpaka amefunga magoli 50 katika mashindano yote msimu huu, huku akitoa assists 21, huku Fabregas akifunga magoli 15.

WAPIGA PASI BORA BARANI ULAYA
The top five passers ndani ya 3 ya uwanja katika ligi barani ulaya
1.- Messi : 911
2.- Xavi: 844
3.- Silva: 763
4.- Pirlo: 731
5.- Hazard: 704
(Font: Opta Sports)

MAN CITY NAO WAWAFUATA MAHASIMU WAO UNITED NJE YA EUROPA LEAGUE - MAGOLI YA UGENINI YAWAONDOA KWENYE MASHINDANO.

HAUKUWA USIKU MZURI KWA VILABU VVYA MJI WA MANCHESTER BAADA YA MAN CITY PIA KUTOLEWA KWENYE KOMBE LA EUROPA - JAPOKUWA WAKIPATA USHINDI WA 3-2 KWA DHIDI SPORTING LISBON.  

AGUERO AKISHANGILIA BAOLAKE LA PILI NA LA KUSAWAZISHA KWA CITY.

SPORTING LISBON WAKIWA WANASHANGILIA BAADA YA KUWATOA MAN CITY.

MARIO BALOTELLI AKIFUNGA PENATI NA KUFANYA MATOKEO YA UBAO YASOMEKE 3-2, LAKINI HADI MWISHO WA SIKU WALIKUWA NI SPORTING WALIOKUWA WAKISHANGILIA KWA KUWA NA FAIDA YA GOLI 2 ZA UGENINI.