Search This Blog

Friday, March 16, 2012

CHELSEA YAPANGWA NA BENFICA - HUKU BARCELONA AKIWASUBIRI HATUA YA NUSU FAINALI

 Real Madrid v Apoel Nicosia


Barcelona v AC Milan

Marseille v Bayern Munich 

Chelsea v Benfica


Mtanange utakavyokuwa.
 Ratiba ya hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa imepangwa hii Leo huko Munich . 
Ratiba hiyo inaonyesha kuwa Mabingwa watetezi Fc Barcelona watavaana na Ac Milan,
 huku Real Madrid wakicheza na Apoel Tel Aviv , michezo mingine itawakutanisha Chelsea na Benfica huku Bayern Munich wakicheza na Olympic Marseile.
Michezo ya robo fainali itapigwa tarehe 27 na 28 kwa michezo ya kwanza huku ile ya marudiano ukichezwa Kati ya tarehe 3 na 4 mwezi aprili. 


Kwa upande wa robo fainali ya ligi ya Europa , Az alkamaar watacheza dhidi ya valencia cf , schalke 04 watakipiga dhidi ya athletic Bilbao , Sporting Lisbon watacheza na Metalist Kerkiv huku Athletico Madrid wakicheza na Hanover 96 ,michezo hii itachezwa Kati ya tarehe 29 machi na tarehe 5 aprili.

2 comments:

  1. Ratiba hiyo tamu kichizi, ila nina wasiwasi kama ikitokea wakipita round hii na wakakutana Madrid na Bayern Munich naona Madrid anatoka, Bayern wana timu nzuri sana,Natamani Fainali ya Barcelona na Bayern Munich, ana Chelsea na Real Madrid.

    ReplyDelete
  2. kaka Madrid wanakutana na Apoel FC ya Nicosia Cyprus sio Apoel Tel Aviv

    ReplyDelete