Search This Blog

Saturday, October 27, 2012

LIVE MATCH CENTRE: SIMBA SC 3 - 1 AZAM FC


Dk 90+6 MPIRA UMEISHA. SIMBA 3 - 1 AZAM
 
Dk 90+1 Kazimoto anashindwa kupiga mpira langoni kwa Azam akiwa katika nafasi nzuri.
 
Dk 90 wachezaji wa timu zote wanachezeana rafu za hapa na pale na mwamuzi anapeta.

Dk 89 mwamuzi wa akiba anaonyesha muda wa ziada kuwa ni dakika 6

Dk 87 Simba inafanya mabadilko anatoka Ngassa anaingia Edward Christopher.

Dk 85 Azam inatawala mchezo na kuishambulia Simba kwa muda mrefu.

Dk 83 Azam inapata faulo nje kidogo ya eneo la hatari la Simba na mpira unaopigwa unakuwa kona. Kona inapigwa na Azam inakosa bao la wazi baada ya mashuti ya washambuliaji wake kuwababatiza mabeki wa Simba.

Dk 82 Humud anamfanyia madhambi Okwi. faulo isiyo na madhara imepigwa.

Dk 80 Simba inafanya mabadiliko, anatoka Amri Kiemba anaingia Ramadhan Chombo aka Redondo.

Dk 79 Azam wanakosa bao la wazi bada ya Mcha kupiga kichwa amapira wa krosi uliopigwa na Shikanda. Mabeki wa Simba wanaokoa hatari hiyo na wakati huohuo beki Cholo wa Simba ameumia na anatibiwa.

Dk 76 Simba inafanya mabadiliko anatoka Sunzu anaingia Ramadhan Singano aka Messi.

Dk 75 mashabiki wanaokaa majukwaa ya upande wa Yanga wanaanza kuondoka huku wakizomewa na mashabiki wa Simba.

Dk 73 Morad anamchezea rafu Okwi nje kidogo ya eneo la hatari la Azam. Ngassa anapiga faulo na kipa Mwadin anautoa nje mpira na kuwa kona isiyo na madhara.

Dk 72 Simba inafanya shambulizi kali langoni kwa Azam lakini umakini wa mabeki unaokoa.

Dk 68 Kasim anapiga shuti hafifu kuelekea lango la Simba na kipa Juma Kaseja anadaka.

Dk 65 Simba inapata faulo, Baada ya Ngassa kuangushwa nje kidogo ya eneo la hatari la Azam, Okwi anapiga nje faulo hiyo.

Dk 64 Azam inafanya mabadiliko wanatoka Jabir Aziz na Himid Mao, wameingia Abdi Kasim na Kipre Bolou.

Dk 63 Humud anamfanyia madhambi Kazimoto
Dk 62 Mpira umebalance timu Zinashambuliana kwa zamu
Dk 58 Azam inapata faulo nje kidogo ya eneo la hatari la Simba baada ya Mcha kuangushwa na Kapombe.

Dk 53 Simba inatawala mchezo ikicheza soka la kasi sana. Azam imeelemewa.

Dk 50 GOOOO.... Okwi anaifungia Simba bao la tatu kwa shuti kali akiwa nje ya eneo la hatari la Azam baada ya kuwapiga chenga wachezaji watatu wa Azam.

Dk 49 Azam inapata kona, Beki Aggrey Moris wa Azam anakosa bao baada ya mpira wake wa kichwa kutoka nje akiunga kona.
Dk 48 Tcheche anakosa bao akiwa eneo zuri la kufunga langoni kwa Simba.

Dk 46 beki Cholo wa Simba anaumia baada ya kujigonga na mchezaji mwenzake.

Dk 46 Kazimoto anakosa bao la wazi akiwa peke ya na kipa Mwadini ambaye anaudaka mpira.

Kipindi cha pili kimeanza
17:45 timu zinaingia uwanjani
Dk. 45 HALF TIME. Simba 2 - 1 Azam

Dk 45 Sunzu anaumia baada ya kukanyagwa na bek wa Azam, Said Morad.

Dk 44 Himid Mao anamchezea rafu Amir Maftah.

Dk 43 Okwi anaichambua ngome ya Azam, lakini mabeki wa Azam wanaokoa na kuwa kona ambayo haina madhara.

Dk 41 Goooo.... Okwi anaipatia Simba bao la pili kwa kichwa akiunga krosi ya Kazimoto.

Dk 40 Kazimoto wa Simba anachezewa faulo nje kidogo ya llango la Azam.

Dk 39 Okwi anashindwa kuunganisha krosi safi ya Ngassa akiwa peke yake na kipa Mwadin wa Azam.

Dk 37 Amir Maftah wa Simba anaumia na kutibiwa. Aligongana na Ibrahim Shikanda wa Azam.

Dk 36 Ngassa anakosa bao la wazi akiwa amebaki na kipa wa Azam, Mwadin Ally. Mwadin anapangua shuti la Ngassa na mpira unafika kwa Sunzu ambaye shuti lake linaokolewa kwa kichwa na Said Moradi.

Dk 34 Mcha anakosa bao la wazi akiwa amebaki na Kaseja baada ya mabeki wa Simba kujichanganya katika kuokoa.

Dk 30 beki wa Simba, Nasoro Masoud Chollo anajigonga katika miguu ya Himid Mao na kuumia. mpira umesimama, Chollo anatibiwa.

Dk 29 Jabir Aziz anamchezea rafu Amri Kiemba wa Simba. mwamuzi Nkongo anamuonyesha kadi ya njano Jabir.

Dk 28 Okwi anaichambua ngome ya Azam lakini anapiga shuti kali nje ya lango.

Dk 27 Jabir Aziz wa Azam anapiga mpira nje baada ya kutengewa vizuri mpira na Mcha.

Dk 25 Azam ainapata kona mbili katika lango la Simba

Dk 24 Himid Mao anachezewa rafu na Jonas Mkude wa Simba

Dk 22 Azam inapata kona baada ya beki wa Simba, Ochieng kutoa nje mpira kwa kichwa.

Dk 21 Azam wanafanya mabadiliko anatoka Bocco anaingia Khamis Mcha.

Dk 19 Bocco anaanguka mwenyewe na kutibiwa katikati ya uwanja.

Dk 18 Ngassa anachezewa faulo na Himid Mao.

Dk 17 Mwinyi Kazimoto anapiga shuti kuelekea lango la Azam na mpira unatoka nje kidogo ya goli.

Dk 14 Kasi ya mpira imepungua kidogo na timu zinashambuliana kwa zamu

DK 11 Azam inapata kona baada ya Kapombe kutoa mpira nje. Kona butu inapigwa.

Dk 7 Goooo....Sunzu anaifuangia Simba kwa kichwa bao la kusawazisha akiunganisha krosi ya Mrisho Ngassa. Simba 1 - 1 Azam.

DK 6 Kipa wa Azam, Mwadin Ally anaumia na kutibiwa baada ya kugongana na Sunzu

DK 4 Gooo.... Bocco anaifungia Azam bao la kwanza abaada ya kumzidi mbio beki wa Simba Pascal Ochieng

Dk 3 KIEMBA anamwangusha Bocco nje kidogo ya eneo la hatari la Simba. bocco anapiga faulo na mpira unatoka nje

Dk 1 Amri Kiemba wa Simba anachazewa faulo nje kidogo ya eneo la hatari la Azam. Emmanuel Okwi anapiga fauloa ambayo inaokolewa na mabeki wa Azam

Mpira umeanza uwanja wa taifa Simba 0 - 0 Azam 

Mwamuzi wa leo ni Israel Nkongo

16:31 Timu zinaingia uwanjani tayari kwa kukaguliwa

Kikosi cha Simba kitakachoanza dhidi ya Azam: Kaseja, Maftah, Ochieng, Hatib, Mkude, Kiemba, Kazimoto, Sunzu, Ngassa na Okwi

AZAM FC
Ally Mwadini, Ibrahim Shikanda, Sahm Nuhu, Said Morad, Aggrey Morris, Humud, Jabir Aziz, Himid Mao, Bocco, Kipre Tchetche, Salum 

LIVE MATCH CENTRE: JKT OLJORO 0-1 YANGA SC FULL TIME

Mpira umemalizika, JKT Oljoro 0 - 1 Young Africans
Twite dkk 53


 Dakika ya 87, Young Africans inafanya mabadiliko, anaingia Nurdin Bakari anatoka Frank Domayo
Dakika ya 79 Young Africans inafanya mabadiliko, anaingia Jeryson Tegete anatoka Didier Kavumbagu
Dakika ya 75, JKT Oljoro 0 - 1 Young Africans
Twite dkk 53


 Dakika ya 60, JKT Oljoro 0 - 1 Young Africans
Dakika ya 53, Mbuyu Twite anaipatia Young Africans bao la kwanza

Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, JKT Oljoro 0 - 0 Young Africans

Mpira ni mapumziko, JKT Oljoro 0 - 0 Young Africans

Dakika ya 30, JKT Oljoro 0-0 Young Africans
Dakika ya 15, JKT Oljoro Vs Young Africans
Mpira umeanza hapa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kati ya
JKT Oljiro Vs Young Africans

Kikosi cha watoto wa Jangwani kinachoanza leo ambacho tumefanikiwa kukipata muda mfupi kabla ya mchezo kuanza.

1.Ally Mustapha 'Barthez'
2.Shadrack Nsajigwa
3.Oscar Joshua
4.Nadir Haroub 'Cannavaro'

5.Mbuyu Twite
6.Athuman Idd 'Chuji'
7.Saimon Msuva
8.Frank Domayo
9.Didier Kavumbagu
10.Hamis Kiiza
11.Haruna Niyonzima

Susbs:

1.Yaw Berko
2.Nurdin Bakari
3.David Luhende
4.Kelvin Yondani
5.Rashid Gumbo
6.Nizar Khalfani
7.Jeryson Tegete

WAMEPANDA THAMANI: MAN UNITED WANUNUA MKATABA WAO WA UDHAMINI WA JEZI ZA MAZOEZI KUTOKA KWA DHL

Wakiwa na uhakika wa kuweka kibindoni kiasi cha £350million kwa mkataba wa miaka 7 wa udhamini wa jezi na kampuni ya General Motors ambao umepangwa kuanza mwaka 2014, Manchester United wamenunua haki za udhamini wa jezi zao za kufanyia mazoezi walizoziuza kwa kampuni ya DHL mwaka 2010. Dili hilo lilokuwa na thamani ya £40 million kwa miaka minne kwa kuweka tu maandishi matatu tu ya DHL kwenye jezi zao za mazoezi - hiyo ikiwa ni fedha nyingi kuliko wanazopata vilabu vingine kwa udhamini wa jezi zao rasmi za mechi.

Lakini kutokana na tathmini yao, United wanaona fedha hizo ni kidogo kutokana na thamani yao kupanda, ukizingatia walikuwa wakipata kiasi cha £20 million kwa mwaka kwa udhamini wa AON lakini sasa wataanza kuvuta karibia £50 million kwa mwaka kutoka GM.


"Tumefanikiwa vizuri sana kukubaliana na kununua haki zetu za udhamini wa jezi za mazoezi kutoka DHL kuanzia mwakak 2013," klabu hiyo ilisema. "DHL wataendelea kuwa wadhamini wa masuala ya uchukuzi duniani kote.
"Masuala ya ukuaji wa thamani yetu yalikuwepo katika makubaliano ya mwanzo, ni ni kweli thamani yetu imepanda na mfano mzuri ni dili letu la hivi karibuni lilovunja rekodi lenye thamani ya $559 million la udhamini wa jezi na General Motors, hili linatufanya tuamini kutakuwepo na nafasi ya kuongeza thamani ya haki zetu za kibiashara."

MCHEZAJI WA BARCELONA MPIGAJI: ATUHUMIWA KUIBA POCHI YA DEREVA TAXI

Ni vigumu sana kwa wachezaji makinda kuweza kuwa na muda mrefu kwenye soka kwa miaka ya sasa hasa wanapokuwa kwenye klabu kubwa kama Barcelona, mahala ambapo kuna presha kubwa na nafasi hazijitoshelezi. Hivyo kuna wengine wanaamua kutafuta njia mbadala ya kuingiza kipato popote wanapoweza. Na kijana mwenye umri wa miaka 21 anayeicheza Barca ametuhumiwa kuiba pochi ya dereva taxi akiwa njiani kwenda uwanja wa ndege kujiunga na wenzake wa kikosi cha Spain cha under 21.
Kutoka Marca:
Dereva Taxi anaelezea kwamba akiwa anawaendesha mchezaji Montoya, na wachezaji wenzake Cristian Tello na Gerard Deulofeu, pamoja na Daktari Jorge, aliweka pochi yake katika siti ya mbele alipokaa Montoya na ghafla ya ikapotea.
"Nilimwambia mchezaji aliyekaa siti ya mbele kwamba amechukua pochi yangu, then wakaruka kutoka kwenye gari na kukimbilia kwenye uwanja wa ndege wakisema watachelewa ndege yao," dereva taxi aliiambia Radio Marca. "Kwa sababu nilishindwa kuliacha gari nje peke yake na sehemu ambayo haikuwa sahihi, nikaenda kuipaki sehemu nzuri na niliporudi nikaongea na askari akaniambia wameshaondoka."
"Inaonekana alihisi nimemtusi na kumpakaza, hivyo baadae akanipigia simu na kuanza kunitolea lugha chafu, na baadae mtu mwingine akanipigia akisema ni wakala wake, lakini nikagundua hakuwa mwenyewe hivyo nikamripoti ", Taxi dreva aliendelea.I
Kwa mujibu wa dereva, pochi hiyo ilikuwa na kiasi cha €230 na kadi ya hosptali ya mwanae wa kike.
Montoya alijitetea kupitia mtandao wa Twitter, akisema tuhuma hizo ni za uongo  na baadae akatoa taarifa rasmi ya aya tano kwa waandishi wa habari.

Friday, October 26, 2012

PICHA YA SIKU! IANDIKIE CAPTION

THE DRESSED IN WHITE PARTY NDANI YA SYNERGY LOUNGE!


LIVERPOOL WALIVYOWAGONGA NA SAMUEL ETO'O NA TIMU YAKE YA ANZHI MAKHACHKALA

HARUNA MOSHI: MCHEZAJI MWENYE KIPAJI, MTUKUTU ANAYEHARIBIWA NA MASHABIKI - SIMBA ILICHELEWA KUMSIMAMISHA



Siku ya juzi klabu ya Simba ambao ndio mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara walitoa taarifa ya kuwasimamisha wachezaji wake wawili wa kikosi cha kwanza Haruna Moshi Shabaan aka Boban na Juma Nyosso kutoka na sababu mbili tofauti.

Juma Nyosso alisimamishwa kuichezea klabu ya wakubwa ya Simba na kupelekwa kufanya mazoezi na timu ya pili ya klabu hiyo ili aweze kurudisha kiwango chake ambacho kimeporomoka sana msimu huu. Huku Haruna Moshi Boban akisimamishwa kuichezea timu hiyo kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu vilivyokithiri.

Masuala ya vitendo vya ukosefu wa nidhamu kwa Boban sio mageni kabisa, pamoja na kipaji kikubwa alichonancho cha soka lakini Boban ni mmoja ya wachezaji wenye nidhamu mbovu katika soka la kizazi hiki.

Boban kwa kipindi cha muda mrefu amekuwa akifanya matukio ya ajabu ndani na nje ya uwanja, na anapoadhibiwa baadhi ya wadau na mashabiki wa soka wanamtetea na kudai anaonewa.

Pamoja na sifa ya utovu wa nidhamu baadhi ya makocha ambao tayari wameshafanya kazi na mchezaji huyu kipenzi cha mashabiki hasa wa klabu yake ya Simba, wanasema kwamba Boban pia ni mchezaji mvivu mno, na hana utaratibu mzuri wa kuishi kama mchezaji wa soka la kisasa, na ndio maana pamoja na kipaji kikubwa alichonacho imeshindikana kwa mchezaji huyu kucheza soka nje ya nchi kwa mafanikio.

Kwa taarifa za uhakika nilizonazo, zipo sababu kadhaa zisizopungua nne ambazo ndizo zimepelekea Boban kusimamishwa Simba.

Wakati Simba ikiwa inajiandaa na mchezo dhidi ya Mgambo JKT, Haruna akidai anaumwa hivyo hatoweza kwenda timu jijini Tanga. Uongozi ukampa ruhusa, lakini wakati timu ikiwa tayari Tanga, Boban akaonekana maeneo ya uwanja wa Muhimbili akicheza ndondo. Kama hiyo haitoshi usiku wake akaonekana katika moja ya kumbi za starehe akijirusha - kwa bahati nzuri hapo katika kiwanja cha kujirusha alikuwepo mmoja wa viongozi wa Simba kutoka kamati ya usajili ambaye alimuona Boban na kuupeleka uongozi wa juu taarifa juu ya mchezaji huyo.

Boban akaitwa na uongozi na kuhojiwa juu ya suala hilo, na baada ya hapo mchezaji huyo akafikia hatua ya kumpigia simu kiongozi aliyemchongea kwa uongozi wa klabu na kumtukana matusi makubwa ya nguoni.

Pia Boban amekuwa akilalamikiwa kufanya mambo anavyojisikia ndani ya Simba, kwanza taarifa kutoka benchi la ufundi mchezaji huyo ni mvivu wa mazoezi na anacheza anavyojisikia yeye, pili hana utaratibu mzuri, kwa mfano timu inapocheza Dar es Salaam wamejipangia utaratibu wa kukutana klabuni na kuondoka kwa pamoja kwenye basi rasmi la timu, lakini Haruna amekuwa akipingana na utaratibu huo na kuacha kupanda basi hilo kisha huenda uwanjani na gari lake binafsi.
Jambo lingine timu yenye udhamini kama Simba imejiwekea sare maalum za kuvaa staffs wa timu hiyo wakati wa kabla ya mechi, kwenye mechi na baada ya mechi, lakini Haruna amekuwa akijivalia vyovyote anavyojisikia hivyo kuharibu utaratibu ambao timu imejiwekea.

Pamoja kuendelea na matendo yake ya utovu wa nidhamu huku akionywa mara kwa mara Boban aliendelea kukaidi na hatimaye juzi uongozi wa Simba ukaamua kumsimamisha mchezaji huyo a.k.a 'kichwa haambiliki'

Boban ni mchezaji tegemeo Simba hivyo anapofanya mambo ya ajabu anaihathiri timu yake ambayo ilianza ligi vizuri lakini sasa mambo yameanza kwenda hovyo. 

Ili mchezaji ucheze kwa kiwango kuzuri inabidi ufanye mazoezi kwa bidii, kusikiliza na kufuata unachofundishwa na mwalimu pamoja na kuwa na nidhamu nzuri na mwisho ndio kinakuja kipaji binafsi. Boban anakosa vyote hivyo anabaki na kipaji tu, kitu ambacho pekee yake hakitoshi kumkamilisha mchezaji wa soka la kisasa.



Thursday, October 25, 2012

MKE WA SHABIKI WA MAN UNITED ACHOSWA NA VIPIGO VYA MUMEWE KILA MAN U INAPOFUNGWA

Mara kadhaa tumekuwa tukisikia vitu kadhaa vya kushangaza juu ya mashabiki wa soka kwa sababu tu ya mapenzi ya timu zao. Ingawa matukio hayo yanaweza yakawa yanachekesha lakini uda mwingine inakuwa ni vigumu kuelewa ni soka linaweza kuingiliana na maisha yetu binafsi kwa kiasi kikubwa namna. Hi hapa ni barua iliyoandikwa na mwanamke mmoja kutoka Kenya ambaye amekuwa akigeuzwa 'punching bag' na mume wake kila mara klabu ya Manchester United inaofungwa.

Habari,

Nimeanza kufikiria kwa kina juu ya kuomba talaka kwa mume wangu kwa sababu sifikirii kama naweza nikaendelea na ndoa ya namna hii. Nilifunga ndoa miaka 4 iliyopita na kila mara mara wakati wa mechi za ligi kuu ya England, FA Cup, Capital One Cup au UEFA Champions league ninakuwa katika kipindi kigumu sana katika maisha yangu ya ndoa.
Mume wangu ni shabiki wa kufa wa Manchester United na anaweza kufanya chochote kwa ajili ya timu yake pindi inapofungwa au kushinda.  Pindi Man U inapofungwa mwisho wake huwa naambulia vipigo, na nimekuwa nikisikia hii timu jina lake la utani ni Red Devils(Mashetani wekundu) nimeanza kujiuliza maswali kama mume wangu ni mfuasi wa dini ya shetani.

Anyway mie nimechoswa na uso wangu kuwekwa bandeji kila mara Manchester United inapofungwa kwa sababu huwa napokea vipigo vizito sana jambo ambalo linaniathiri kisaikolojia na kimwili. Sasa hivi namuogopa sana ingawa pindi Manchester United inaposhinda kama juzi usiku, mume wangu alikuwa ndio mume bora duniani.

Kiukweli hali hii inanichanganya. Nimechoka kupigwa kwasababu ya klabu ya soka.

Na hawa Manchester United kwanini wasiwe wanashinda kila siku wanapocheza?

Jane.”

SD TV: KAMA HUKUANGALIA SIMBA TV WIKI HII JIMWAGE!

ARSENAL HALI TETE: WAPIGWA 2-0 NYUMBANI KWAO EMIRATES NA SCHALKE

MANCINI AKALIA KUTI KAVU: MAN CITY YAGONGWA 3-1 NA AJAX NA KUJIWEKA HATARINI KUTOKA KWENYE CHAMPIONS LEAGUE

REAL MADRID WALA KIPIGO CHA KWANZA KWENYE CHAMPIONS LEAGUE


Borussia Dortmund 2-1 Real Madrid (Özet - 24/10/2012) |izlesene.com

HIVI NDIVYO YANGA ILIVYOZIDI KUICHIMBIA KABURI POLISI MOROGORO

 Kikosi cha Yanga kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya pambano lao na Polisi Morogoro katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Yanga ilishinda 3-0. (Picha na Habari Mseto Blog)
 Kikosi cha timu ya Polisi Morogoro
 Golikipa wa Yanga, Ali Mustafa akiwa katika harakati za kuokoa moja ya hataroi zilizoelekezwa langoni mwake. Kulia ni mshambuliaji wa Polisi Morogoro, Bantu Admin (PICHA KWA HISANI YA http://francisdande.blogspot.com/)
 Paschal Maige akichuana na beki wa Yanga, Shadrack Nsajigwa
 Nsajigwa akimiliki mpira huku akizongwa na mchezaji wa Polisi Moro, Keneth Masumbuko

TANZIA

FAMILIA YA  MAREHEMU MCHUNGAJI MWAKIPUNDA WA NGAMANGA IPINDA KYELA WANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MZEE NSUBISI SAMUEL MWAKIPUNDA (MKURUGENZI WA ZAMANI WA IDARA YA MAELEZO)  KILICHOTOKEA SIKU YA JUMATANO TAREHE 24/10/2012.

MIPANGO YA MAZISHI INAFANYIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU PUGU KINYEMWEZI DAR ES SALAAM.
HABARI ZIWAFIKIE NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI POPOTE PALE WALIPO.

KWA MAWASILIANO ZAIDI
+255655994499
BWANA AMETOA BWANA, AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE
AMEN

BREAKING NEWS! KIKOSI CHA PRISONS FC CHAPATA AJALI TANGA!

Timu ya prison ya Mbeya imepata ajali eneo la Hare mkoani Tanga,wachezaji Issa Mwantika,Lugano Mwangama,Khalidi Fungabreki,Daudi Masungwe wamepoteza fahamu na kukimbizwa hospitali ya Tanga, Kiungo wa Prisons Diego Magai akiongea na blog hii kutoka eneo la tukio amesema chanzo cha ajali iyo ni baada gari aina ya COaSter kuacha njia na kupinduka baada kupigwa na mwanga mkali wa taa za gari walilokua wanapishana nalo usiku huu,hadi saa tano na dk hamsini usiku huu majeruhi walikuwa wakikimbizwa hospitali teule ya Muheza.

Wednesday, October 24, 2012

BAO LA WIKI VPL: DAN LYANGA vs MTIBWA SUGAR.

SIKU KAMA LEO: MIAKA 13 ILIYOPITA NWANKWO KANU ALILIVUNJA DARAJA LA CHELSEA KWA HAT TRICK - ARSENAL IKITOKA NYUMA NA KUSHINDA 3-2

LIVE MATCH CENTRE: YANGA SC 3 - 0 POLISI MOROGORO FULL TIME



Kutoka Mkwakwani Coastal Union wameendeleza wimbi la ushindi kwa kuwafunga African Lyon 1-0 - Goli likifungwa na Nsa Job.
 
Mpira umemalizika, Young Africans 3 - 0 Police Morogoro
Msuva DK 4
Didier DK 6
Kiiza DK 58


 Dakika ya 80, Young Africans 3 - 0 Police Morogoro

Dakika ya 65, Young Africans 3 - 0 Police Morogoro

Kutoka Chamazi mechi imemalizika kwa sare. AZAM FC 1 - 1 RUVU SHOOTINGS.

Dakika ya 58, Hamis Kiiza anaipatia Young Africans bao la tatu - Young Africans 3 - 0 Police Morogoro
Dakika ya 57, Shadrack Nsajigwa anaonyeshwa kadi ya njano
Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza,
Young Africans 2 - 0 Police Morogoro
Mpira ni mapumziko, Young Africans 2 - 0 Police Morogoro
Msuva dkk 4, Didier dkk 6


 Dakika ya 38, Haruna Niyonzima anakosa penati
Dakika ya 30, Young Africans 2 - 0 Police Morogoro
Police Morogoro wanafanya mabadiliko dakika ya 19, anatoka golikipa. Manji Kulwa aliyeumia anaingia Kondo Salum

Dakika ya 15, Young Africans 2-0 Police Morogoro
Dakika ya 6, Didier Kavumbagu anaipatia Young Africans bao la pili

Dakika ya nne, Saimon Msuva anaipatia Young Africans bao la kwanza

Mpira ndio umeanza hapa Uwanja wa Taifa kati ya
Young Africans Vs Police Morogoro


Kutoka Chamazi: 25MINS AZAM FC 1 - 1 RUVU SHOOTINGS

Kikosi cha Yanga kinachoanza leo dhidi ya maafande wa Polisi wa Morogoro.

1. All Mustapha 'Barthez'
2. Shadrack Nsajigwa
3. Oscar Joshua
4. Nadir Haroub 'Cannavaro'
5. Mbuyu Twite
6. Athuman Idd 'Chuji'
7. Saimon Msuva
8. Haruna Niyonzima
9. Didier Kavumbagu

10. Jeryson Tegete
11. David Luhende

Subs:
1. Yaw Berko
2. Ladislaus Mbogo
3. Nurdin Bakari
4. Rashid Gumbo
5. Frank Domayo
6. Nizar Khalfani
7. Hamis Kiiza

MJADALA: ANGALIA VIDEO HII THEN UTOE MAONI YAKO JE NI KWELI AZAM WALINYIMWA NA GOLI NA PENATI DHIDI YA PRISONS?

BREAKING NEWS: SIMBA YASIMAMISHA BOBAN NA JUMA NYOSSO



KLABU ya soka ya Simba inapenda kutoa taarifa zifuatazo kwenu siku ya leo.

1.    Kuhusu Boban na Nyoso

Wachezaji wawili wa Simba, Haruna Moshi Shaaban (Boban) na Juma Said Halfan (Nyoso), wamesimamishwa kuitumikia timu ya wakubwa (senior) kwa sababu na nyakati tofauti.

Moshi amesimamishwa kuichezea timu ya wakubwa kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu na kutokuwa na heshima kwa mwajiri (timu). Klabu imempa Haruna muda wa siku 21 kutoa maelezo kuhusu makosa yake na iwapo atashindwa kutoa maelezo ya kuridhisha, klabu inaweza kumchukulia hatua zaidi.

Katika kipindi hicho (siku 21 kuanzia jana), Boban atapokea nusu ya mshahara wake wa kila mwezi na hatapata marupurupu yoyote yanayohusiana na timu ya wakubwa.

Kwa upande wa Nyoso, uongozi umemwagiza afanye mazoezi na kikosi cha timu ya pili (Simba B) hadi hapo atakapoimarisha kiwango chake cha uchezaji.

Hatua hii imetokana na ripoti ya benchi la ufundi iliyoonyesha kwamba mchezaji huyo amekuwa akifanya makosa mengi ya kiuchezaji yanayoigharimu na ingawa amekuwa akipewa maelekezo na walimu, bado amekuwa akirudia makosa yaleyale.

Kutokana na hilo, Nyoso atafanya mazoezi na wachezaji wa kikosi cha pili hadi walimu watakaporidhika kwamba amejirekebisha na yuko tayari kutumikia kikosi cha wakubwa.

Katika muda wake wote huo akifanya mazoezi na timu B, Nyoso atakuwa akipata mshahara wake wa kila mwezi kama kawaida na pia atapata marupurupu wanayopata wachezaji wa Simba B.

Emmanuel Okwi

Klabu ya Simba inaeleza kusikitishwa kwake na taarifa za vyombo vya habari vyenye lengo la kuuza magazeti pasipo kujali athari za habari zenyewe.

Kwa mfano, habari ya kwenye gazeti la CHAMPIONI la leo ina kichwa cha habari KATIBU MKUU AMFUKUZA OKWI SIMBA. Hata hivyo, kilichoandikwa ndani ya habari yenyewe kinamnukuu aliyewahi kuwa Katibu Mkuu kwenye miaka ya nyuma.

Gazeti hilo linafahamu kabisa kwamba Simba ina Katibu Mkuu mmoja tu kwa sasa na anaitwa Evodius Mtawala. Simba haijawahi kuwa na makatibu wakuu wawili kwa wakati mmoja.

CHAMPIONI linafahamu ukweli huu lakini kwa sababu inazozijua lenyewe, imeamua kuandika habari hiyo na kuweka kichwa cha habari cha namna hiyo pasipo kujali athari zake kwa wanachama wa Simba, Katibu Mkuu aliyepo madarakani kwa sasa na weledi wa fani ya uandishi wa habari

Kilichoandikwa kwenye habari hiyo ya CHAMPIONI ni maoni binafsi ya mwanachama wa Simba na kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake kuhusiana na jambo lolote ali mradi halivunji sheria za nchi.

Simba SC inarudia wito wake wa kuvitaka vyombo kubaki kwenye misingi ya kitaaluma na kuacha kuandika habari zilizotiwa chumvi na kuleta mitafuruku isiyo na sababu yoyote.

Kikosi

Simba inaendelea vizuri na mazoezi visiwani Zanzibar kujiandaa na mechi dhidi ya Azam itakayopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi hii.

Hata hivyo, mchezaji Salim Kinje ameruhusiwa kuondoka kambini Zanzibar leo kutokana na kupata msiba wa baba yake mkubwa uliotokea Dar jana.

Uongozi, kwa namna ya kipekee kabisa, unatoa salamu za pole kwa familia ya Kinje kutokana na msiba huu.

Boniface Wambura

Kwa niaba yangu binafsi na klabu ya Simba, napenda kumpongeza Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura, kwa kuteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuwa miongoni mwa wasimamizi wa shirikisho hilo katika michuano ya Wanawake itakayofanyika nchini Guinea ya Ikweta (Equatorial Guinea).

Wambura ndiye Mtanzania pekee aliyeteuliwa na CAF kutumika kwenye michuano hiyo na jambo hilo ni la faraja kwa tasnia ya habari nchini ambako Wambura ametokea.

Imetolewa na

Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC






BARCELONA WAIHUKUMU CELTIC DAKIKA YA MWISHO YA MCHEZO

CHELSEA WACHEZEA KICHAPO CHA KWANZA ULAYA - WATANDIKWA 2-1 NA SHAKHTAR

CHICHARITO AIOKOA UNITED NA AIBU NYUMBANI - SAFU YA ULINZI KIMEO

MANCHESTER UNITED YASEMA TAYARI TUNA LISTI YA MAKOCHA WATAKAOFAA KUMRITHI FERGUSON

Manchester United leo wamesema kwamba mipango ya kupata mbadala wa Sir Alex Ferguson imeshajadiliwa na mpaka sasa kila kitu kipo tayari lakini mipango hiyo sasa imefungiwa kwenye makabati ya ofisi za klabu hiyo huko Old Trafford.

Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Ed Woodward amesema kwamba listi ya watakaowania nafasi ya Fergie ipo tayari na wanaijua watu wachache sana lakini hakuna tarehe inayojulikana kuwa ndio itakuwa mwisho wa kocha Mscotland pale Theatre of Dreams.
Alisema: "Tayari tuna mtazamo wa namna mchakato mzima wa kumpata mbadala wa SAF utakavyokuwa na ni aina gani ya mwalimu tunataka na vipi tutampata huyo mwalimu.
Wants it: Jose MourinhoClose to home: David MoyesOut of work: Pep Guardiola



'Lakini kila kitu kuhusu jambo hilo kipo kwenye makabati na mipango yote itakaa huko hata zaidi ya tunavyofikiria."

Majina kama Jose Mourinho na Pep Guardiola, vilevile David Moyes, mara nyingi yamekuw yakihusishwa na kazi ya kumrithi Fergie katika klabu yenye mafanikio kuliko zote pale Uingereza, japokuwa bado haijajulikana lini babu huyo atastaafu.

Akiongea mapema mwaka huu wakati akisherehekea miaka yake yake 25 ndani ya klabu hiyo, babu mwenye miaka 70 alisema: " Sijui ni muda gani nitaweza kuwa hapalakini kama afya yangiu itaniruhusu sidhani kama miaka mingine mitatu au miwli  itakuwa shida.
I'm the boss: United boss Sir Alex Ferguson recently celebrated 25 years at the helm'Nafikiri unahitaji nguvu katika kazi hii. Nimebarikiwa kitu hicho. Nitafahamu wakati utakapofika sifurahii kazi na ikifia hatua hiyo kwa hakika nitastaafu.

KAULI YA SIKU: MICHEAL LAUNDRUP MPYA "CHRISTIAN ERIKSEN" - KWANINI NILIKATAA KUJIUNGA NA MAN CITY

“Hana tamaa ya fedha. Alichagua kubaki hapa kwa maendeleo yake  na kwa sababu ya hilo bado yupo hapa Ajax. Ana mahusiano mazuri sana na kocha Frank De Boer na anafurahia maisha hapa Amsterdam. Christian hakuchukua hata sekunde 10 kuamua kwamba haitaki Manchester City walipomtaka."

Maneno ya wakala wa Christian Eriksen Martin Schoot akiliambia gazeti la De Telegraff na kuelezea kwanini mchezaji wake alikataa kujiunga na mabingwa wa Uingereza Manchester City.

TEKNOLOJIA YA MSTARI WA GOLI KUANZA KUFUNGWA KWENYE VIWANJA VYA SOKA DUNIANI KOTE BAADA YA FIFA KUSAINI MKATABA RASMI

Teknolojia ya mstari wa goli kwenye viwanja vya soka imekaribia kuanza baada ya leo FIFA kusaini mkataba na makampuni mawili makubwa yatakayosimamiwa teknolojia hiyo.

GoalRef na Hawk-Eye wamepewa ruhusa ya kuanza kufunga mifumo yao ya teknolojia dunaini kote baada ya kusaini mkataba huo na chombo kinachosimamia soka ulimwenguni.

Taarifa ya FIFA ilisema: “Kuanzia October 2011 mpaka June 2012, kampuni zote mbili zilipita katika majaribio ya nje ya ya maabara, pia majaribio katika mechi za moja kwa moja.
"Mjaribio yote yalifaulu kwa maana hiyo sasa mchakato huu ulioanza mwaka 2011 unakaribia kumalizika, na kampuni zote mbili zimepewa mamlaka ya kufunga teknolojia hiyo dunini kote." 

Lakini FIFA wakasema pia kwamba: "Pindi teknolojia hiyo inapofungwa uwanjani, itafanyiwa uchunguzi kuangalia namna inavyofanya kazi.

"Uchunguzi huo utafanywa na taasisi huru na majibu yatakayotolewa lazima yawe chanya juu ya mashine hiyo na hapo ndipo pekee teknolojia hiyo inaweza kutumika katika mechi rasmi."

Tuesday, October 23, 2012

MASWALI MAGUMU JUU MAKATO 17 YA UWANJANI KATIKA MECHI ZA LIGI KUU - NA JINSI YANAVYOVIUMIZA KIUCHUMI VILABU


MAKATO ya ajabu ajabu, yasiyo na msingi na mengine mengi yanayofanana, ambayo yanabadilishwa-badilishwa majina tu licha ya kubeba maana moja, yameendelea kuzikamua hadi tone la mwisho klabu za ligi kuu katika kampeni "nzito" ya kuhakikisha haziendelei.
Katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom baina ya Simba na Kagera Sugar iliyochezwa Oktoba 17 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2, Sh. milioni 58.5 zilipatikana lakini kila klabu iliambulia mgawo kiduchu wa Sh. milioni 11.1 tu.
Hali hiyo iliendelea pia katika mechi ya Yanga dhidi ya Ruvu Shooting iliyochezwa Jumamosi Oktoba 20 kwenye Uwanja wa Taifa na kumalizika kwa wenyeji kushinda 3-2.
Licha ya mechi hiyo kuingiza Sh. milioni 47.6, Yanga na Shootings kila moja iliambulia mgawo kiduchu wa Sh. milioni 8.4.
Ni makato makubwa yanayozua maswali tele ambayo majibu yake hayajawahi kutolewa.
Kwa kutumia mfano wa mechi ya Simba dhidi ya Kagera Sugar, makato halisi yalikuwa kama ifuatavyo:
1. Maandalizi ya uwanja (pitch preparation) Sh. 400,000
2. Uwanja Sh. 3,671,261.85
3. Usafi na ulinzi wa uwanja Sh. 2,350,000
4. Ulinzi wa mechi Sh. 3,500,000
5. Gharama za mchezo Sh. 3,671,261.85
6. Umeme Sh. 300,000
7. Wachina (stadium technical support) Sh. 2,000,000
8. Tiketi ni Sh. 3,183,890.
9. Posho ya msimamizi wa kituo Sh. 120,000
10. Kamishna wa mechi Sh. 250,000
11. Waamuzi Sh. 440,000
12. Mwamuzi wa akiba Sh. 70,000
13. Mtathimini wa waamuzi Sh. 254,000
14. Kamati ya Ligi Sh. 3,671,261.85
15. Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) Sh. 2,202,757.11
16. Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) Sh. 1,468,504.74.
17. Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni Sh. 8,924,491.53.

Kwa mchanganuo huo inamaanisha kwamba zaidi ya Sh. milioni 36 zilimezwa katika makato wakati klabu ziliambulia jumla ya Sh. milioni 22.
Vilio vimekuwa vikubwa sasa kwa sababu ni makato mengi mno yanayoua timu zetu changa ambazo zinahitaji sapoti ya serikali, ambayo badala yake imekuwa ikizikamua.
Miongoni mwa makato yanayochefua ni ya "Uwanja", "Maandalizi ya Uwanja", "Usafi wa Uwanja na Ulinzi" na "Ulinzi wa mechi". Ni kwa vipi unaweza kumshawishi mtu kwamba hivyo ni vitu vinne tofauti?

Miongoni mwa maswali magumu ambayo hayajatolewa majibu ni haya:

UWANJA

Makato ya "Uwanja" peke yake, yanathibitisha kwamba uwanja huo unakodishwa, hivyo ili kuutumia ni lazima ulipie. Ndio maana Simba na Kagera Sugar wakatozwa Sh. milioni 3.6. Je, klabu zinaruhusiwa kuukodi kwa kulipa mapema kiasi hicho cha pesa na kisha waone wenyewe kama watahitaji kulipia umeme, kama watahitaji sapoti ya kiufundi kutoka kwa Wachina? 

MAANDALIZI YA UWANJA
Malipo ya "Uwanja" yanatumika kufanya kazi gani ikiwa pia kuna malipo ya "Maandalizi ya Uwanja" na "Gharama za Mchezo"?
Tofauti ya malipo haya iko wapi? Je makato ya 'Usafi wa Uwanja na Ulinzi" siyo "Maandalizi ya Uwanja"? Kwani mtu anaposema maandalizi ya uwanja huwa anamaanisha nini?

USAFI WA UWANJA NA ULINZI
Licha ya kuwapo kwa makato ya "Maandalizi ya Uwanja" pia kuna makato haya ya "Usafi wa Uwanja na Ulinzi". Je, wanapofanya usafi uwanjani hayo siyo maandalizi ya uwanja? Na kama usafi ni maandalizi ya uwanja, kwanini ni makato tofauti? Na "ulinzi' huu ni upi ambao kwa pamoja na usafi unagharimu jumla ya Sh. milioni Sh. 2,350,000 ikiwa vyoo ni vichafu na unaweza ukazimia ukipita nje tu, acha kuingia ndani?

ULINZI WA MECHI
Licha ya kwamba makato ya ulinzi yameshakatwa katika kategori iliyopita ya "Usafi na Ulinzi", pia kuna makato mengine tofauti ya "Ulinzi" pekee ambayo yanagharimu Sh. milioni 3.5. Kama uwanja unalindwa na askari polisi ambao wanalipwa mishahara na serikali iliyowaajiri kwa ajili ya kulinda nchi, fedha hizi Sh. milioni 3.5 zinakwenda wapi?

GHARAMA ZA MCHEZO
Makato ya zilizopewa jina la "gharama za mchezo" katika mechi ya Simba dhidi ya Kagera Sugar zilikuwa Sh. milioni 3.67. Je, gharama za mchezo hazipaswi kujumuisha malipo ya waamuzi, ulinzi wa mechi, usafi na maandalizi ya uwanja? Kwanini haya ni makato tofauti?

UMEME
Kwa mfano umeme hulipiwa Sh. 300,000 katika takriban kila mechi ilhali mechi karibu zote huchezwa mchana? Fedha hizi zinazokatwa pengi mara tatu (Sh. 900,000) katika siku 8 zinaenda kulipia umeme upi? Wa Tanesco au wa jenereta? Ni kweli umeme wa kila saa 2 kwenye uwanja ule ni Sh. 300,000? Au klabu zinakamuliwa ili kulipia umeme wa hata siku ambazo hawautumii?

WACHINA
Wachina hawa wapo kutoa sapoti ya kiufundi. Je, anayepaswa kuwalipa ni mmiliki wa uwanja ama anayeukodi? Hii sapoti ya kiufundi inayogharimu Sh. milioni 2 mara tatu (Sh. milioni 6) ndani ya siku 8 ni ipi? Wanatoa sapoti gani ya kiufundi katika mechi hizi zinazochezwa mchana kweupe? Ikiwa mechi zenyewe hazirushwi na kituo chochote cha TV na hata wakirusha hawatumii chumba (control room) cha uwanja wanatumia magari yao ya 'van', ni sapoti gani wanayotoa Wachina hawa?
Makato ya Wachina yanashangaza, kwani wao ndiyo waliojenga uwanja kwa pesa ya msaada wa nchi yao na pia Serikali ya Tanzania. Sasa cha kujiuliza ni kwamba uwanja ule bado uko mikononi mwao?
Je, walipomaliza kujenga uwanja hawakuukabidhi kwa Watanzania na badala yake wakaingia ubia kuumiliki?
Ina maana Uwanja wa Taifa unamilikiwa na Wachina upande mmoja na Serikali upande mwingine ndiyo maana kila mmoja anakuwa na makato yake?

VAT
Makato ya ongezeko la thamani (VAT) katika mechi hii ya Simba dhidi ya Kagera Sugar yalikuwa Sh.8,924,491.53. Kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria za kodi hapa. Ikiwa pia kuna makato ya umeme, ambapo kwenye umeme pia huwa kuna VAT, je, ni sahihi kulipa VAT mara mbili katika 'bidhaa' (mechi) moja?

DRFA
Lakini pia hivi makato ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam DRFA ni ya nini na yanakwenda kufanyia kazi gani ikiwa kwa sasa vyama vya soka vya wilaya za Dar es Salaam (KIFA - Kinondoni, TEFA - Temeke na IDFA - Ilala) vyote vimeshapewa hadhi ya mikoa na vinaendesha ligi zao.
Mratibu wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser alisema makato hayo yanawaumiza na kuwakwaza kiuchumi, hivyo akazitaka klabu kuungana ili kulipatia ufumbuzi suala hilo ambalo limekuwa tatizo kubwa kwa maendeleo ya klabu za soka nchini.
Naye meneja wa Azam, Patrick Kahemele anazigeukia klabu kuwa zenyewe ndizo zinapaswa kujilaumu kwa kuipa madaraka makubwa TFF katika kupanga gharama za tiketi, kiingilio na makato mengine ya gharama za mechi husika, hali ambayo mwishowe huwaacha wakiambulia fedha kidogo mno kutokana na mapato ya milangoni.
“Haya yote yanatokea kwa sababu mwanzo wetu haukuwa mzuri. Klabu hazina umoja. Kama tungeungana katika hili, kusingekuwa na malalamiko,” alisema Kahemele na anaongeza
“Vitabu vya tiketi za uwanjani viko TFF na klabu hazioneshwi, kuna gharama za waamuzi, ulinzi, gharama za mchezo, maandalizi ya uwanja, gharama za mchezo, pesa ya Kamati ya Ligi. Katika hali kama hii tunategemea klabu itanufaika na kiingilio cha mechi."
Mmoja wa wamiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangezi naye anasema wamekuwa wakisikitishwa na hali ya makato inayofanywa na TFF na serikali dhidi ya klabu za Ligi Kuu.
Afisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga anasema klabu yao pia imekuwa ikiathiriwa na makato makubwa.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari hivi karibuni, Rais wa TFF, Leodgar Tenga alisema kuwa makato yote katika kila mechi yanafuata sheria na taratibu zilizopo.
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema asilimia 60 ya makato yote inakwenda serikalini na kwamba pia wanalazimika kutoa fedha Sh. 200,000 kwa ajili ya mafuta ya magari ya polisi.
Simba na Yanga ziliwahi kutishia kutocheza tena kwenye Uwanja wa Taifa kuepuka makato makubwa misimu kadhaa iliyopita na Serikali iliwapoza kwa kuahidi kushughulikia suala hilo.
Hata hivyo, inaonekana hakuna juhudi za kulishughulikia suala hilo hivi karibuni, licha ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sethi Kamuhanda, kuiambia NIPASHE hivi karibuni kwamba wanaweza kukaa chini kuliongelea jambo hilo.
Lakini pamoja na hayo, kinachoonekana hapa bila klabu kuunganisha nguvu na kupinga hili hakuna chochote kitakachofanyika.

Source: Gazeti la Nipashe

KAZI NA DAWA: SUPERMODEL LIONEL MESSI A.K.A BABA THIAGO








SIKU KAMA LEO: MANCHESTER CITY ILIVYOIDHALILISHA MAN UNITED OLD TRAFFORD KWA KUITANDIKA 6-1

Leo tarehe 23 mwezi wa Kumi, Manchester City wanaadhimisha mwaka mmoja tangu walipotoa kipigo cha mbwa mwizi kwa mahasimu wao wakubwa Manchester United katika dimba la Old Trafford.

EPIQ BONGO STAR SEARCH YAZIDI KUTISHA - UPINZANI WAONGEZEKA


Master Jay na Ritha wakimsema Salama kwa kufanya uchaguzi mbaya wa nyimbo kwa washiriki waliopo chini yake

TeamRithaPoulsen
TeamSalama

Madam Ritha akiwafanyia make up washiriki walioko chini yake.


Team Master Jay

AZAM KUIPIKU SIMBA KILELNI KESHO - YANGA DHIDI YA VIBONDE POLISI MOROGORO

Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Oktoba 24 mwaka huu) kwa mechi nne za raundi ya tisa huku Azam ikiusaka usukani wa ligi hiyo ikiwa mwenyeji wa Ruvu Shooting.
 
Mechi hiyo namba 60 ambayo kama Azam itashinda itafikisha pointi 20, hivyo kuwa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom itachezwa Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam. Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 3,000 kwa sh. 10,000.
 
Yanga itawakaribisha Polisi Morogoro ambao ndiyo wa mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom hivi sasa katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa kiingilio cha sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
 
Alex Mahagi kutoka Mwanza ndiye atakayepuliza filimbi kwenye mechi hiyo namba 62. Waamuzi wasaidizi ni Frank Komba na Michael Mkongwa, wote kutoka Iringa wakati mwamuzi msaidizi ni Oden Mbaga anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) wa Dar es Salaam.
 
Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya African Lyon ya Dar es Salaam ambao ni wageni wa Coastal Union inayonolewa na Hemed Moroco. Nayo Mtibwa Sugar itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Manungu ulioko kwenye mashamba ya miwa Turiani mkoani Morogoro.
 
MTIBWA SUGAR, JKT RUVU SASA KUCHEZA NOV 7
Mechi namba 79 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Mtibwa Sugar na JKT Ruvu iliyopangwa kuchezwa Novemba 3 mwaka huu Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro, sasa itafanyika Novemba 7 mwaka huu.
 
Mabadiliko hayo yamefanyika kwa vile Novemba 4 mwaka huu, Mtibwa Sugar itacheza mechi namba 30 dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro. Mechi hiyo awali ilikuwa ichezwe Oktoba 3 mwaka huu lakini ikabadilishwa ili kutoa fursa kwa mechi za Super Week zilizooneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Super Sport cha Afrika Kusini.
 
VITAMBULISHO FAINALI ZA AFCON 2013 MWISHO NOV 7
Waandishi wa Habari wanaotaka kuripoti fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini wanatakiwa kutuma maombi ya kupatiwa vitambulisho (Accreditation) kabla ya Novemba 7 mwaka huu.
 
Maombi hayo yatumwe Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kupitia CAF Medial Channel inayopatikana katika mtandao wa Shirikisho hilo wa www.cafonline.com
 
FDL KUANZA KUTIMUA VUMBI OKT 24
Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaanza kutimua vumbi kesho (Oktoba 24 mwaka huu) kwenye viwanja mbalimbali nchini.
 
Kundi A kutakuwa na mechi tatu ambapo Burkina Faso itacheza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati JKT Mlale itakuwa mwenyeji wa Small Kids kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea.
 
Nayo Kurugenzi itaumana na Majimaji katika Uwanja wa Wambi ulioko Mufindi mkoani Iringa. Kundi hilo litamaliza raundi ya kwanza keshokutwa (Oktoba 25 mwaka huu) kwa mchezo kati ya Mkamba Rangers na Polisi Iringa utakaofanyika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
 
Mechi za kundi B kwa kesho ni Ndanda dhidi ya Transit Camp katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara na Villa Squad itakipiga na Moro United kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi. Oktoba 25 mwaka huu ni Green Warriors v Tessema (Mabatini, Mlandizi) na Polisi Dar v Ashanti United (Uwanja wa Chamazi).
 
Kundi C kesho (Oktoba 24 mwaka huu) ni Kanembwa FC v Polisi Dodoma (Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma), Mwadui v Morani (Kambarage, Shinyanga), Pamba vs Polisi Mara (Kirumba, Mwanza) na Rhino Rangers vs Polisi Tabora (Ali Hassan Mwinyi, Tabora).