Search This Blog

Saturday, October 27, 2012

MCHEZAJI WA BARCELONA MPIGAJI: ATUHUMIWA KUIBA POCHI YA DEREVA TAXI

Ni vigumu sana kwa wachezaji makinda kuweza kuwa na muda mrefu kwenye soka kwa miaka ya sasa hasa wanapokuwa kwenye klabu kubwa kama Barcelona, mahala ambapo kuna presha kubwa na nafasi hazijitoshelezi. Hivyo kuna wengine wanaamua kutafuta njia mbadala ya kuingiza kipato popote wanapoweza. Na kijana mwenye umri wa miaka 21 anayeicheza Barca ametuhumiwa kuiba pochi ya dereva taxi akiwa njiani kwenda uwanja wa ndege kujiunga na wenzake wa kikosi cha Spain cha under 21.
Kutoka Marca:
Dereva Taxi anaelezea kwamba akiwa anawaendesha mchezaji Montoya, na wachezaji wenzake Cristian Tello na Gerard Deulofeu, pamoja na Daktari Jorge, aliweka pochi yake katika siti ya mbele alipokaa Montoya na ghafla ya ikapotea.
"Nilimwambia mchezaji aliyekaa siti ya mbele kwamba amechukua pochi yangu, then wakaruka kutoka kwenye gari na kukimbilia kwenye uwanja wa ndege wakisema watachelewa ndege yao," dereva taxi aliiambia Radio Marca. "Kwa sababu nilishindwa kuliacha gari nje peke yake na sehemu ambayo haikuwa sahihi, nikaenda kuipaki sehemu nzuri na niliporudi nikaongea na askari akaniambia wameshaondoka."
"Inaonekana alihisi nimemtusi na kumpakaza, hivyo baadae akanipigia simu na kuanza kunitolea lugha chafu, na baadae mtu mwingine akanipigia akisema ni wakala wake, lakini nikagundua hakuwa mwenyewe hivyo nikamripoti ", Taxi dreva aliendelea.I
Kwa mujibu wa dereva, pochi hiyo ilikuwa na kiasi cha €230 na kadi ya hosptali ya mwanae wa kike.
Montoya alijitetea kupitia mtandao wa Twitter, akisema tuhuma hizo ni za uongo  na baadae akatoa taarifa rasmi ya aya tano kwa waandishi wa habari.

No comments:

Post a Comment