Search This Blog

Saturday, January 28, 2012

YANGA WAWAPIGISHA KWATA WANAJESHI WA JKT RUVU: WAWATANDIKA 3-1


Alikuwa mshambuliaji na mchezaji bora wa Uganda, Hamisi Kiiza aliyeokoa jahazi la mabingwa wa Tanzania Bara Yanga kutokomea kwenye gwaride la JKT Ruvu kabla ya Mwasika kuipoteza JKT Ruvu.

Katika mchezo huo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Taifa, JKT Ruvu walikuwa wa mwanzo kupata goli katika dakika ya 33 kupitia kwa Amos Mgisa.

Kama yanga wangekuwa makini wangekwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2 ama zaidi, lakini walikwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa goli moja huku wakipoteza nafasi walizopata kupitia kwa Kenneth Asamoah.

Yanga iliwabidi wangoje mpaka dakika ya 60, ambapo walisawazisha goli kupitia kwa Hamisi Kiiza kwa Mkwaju wa penati, na dakika 19 mbele Kiiza alirejea tena nyavuni kwa kuifungia Yanga goli la pili.

Wakati JKT Ruvu wakiwa wanajiuliza kilicho wasibu walijikuta wanatundikwa msumari wa tatu katika dakika ya 89 kupitia kwa Stephan Mwasika, hivyo kuwaashia indiketor Simba waliopo kileleni.


Katika mchezo mwingine wa ligi kuu uliochezwa Mlandizi ulimalizika kwa sare ya goli 1-1 pale Ruvu shooting ulipo wakaribisha Kagera Sugar.

Katika mchezo huo magoli yote yalifungwa katika kipindi cha kwanza, huku Ruvu Shooting wakiwa wa mwanzo kupata goli katika sekunde ya 33 kupitia kwa Abdurahman Abdurahman.

Kagera Sugar walikuja kusawazisha goli hilo katika dakika ya 26, na kupelekea mchezo kuisha kwa sare ya goli 1-1.


Katika uwanja wa Azam, Toto Africa imekubali kupokea kichapo cha pili mfululizo toka kwa Villa Squad inayoangaika kujinasua toka mkiani, wakati jahazi la Toto likiendelea kuzama.

Magoli ya mshambuliaji wazamani wa Moro united na Yanga Nsa Job na Makundi yalitosha kuwapa point 3 muhimu Villa Squad na kuibuka na ushindi wa magoli 2-0.

MSIMAMO WA VPL.
Kwenye Mabano Idadi ya Mechi Zilizochezwa.
1. Simba SC (14) 31
2. Yanga (15) 31
3. JKT Oljoro (14) 26
4. Azam FC (14) 26
5. Mtibwa Sugar (14) 22
6. Kagera Sugar (15) 20
7. JKT Ruvu (15) 17
8. Ruvu Shooting (15) 17
9. Moro United (14) 15
10. African Lyon (14) 14
11. Toto Africa (15) 13
12. Polisi Dodoma (14) 12
13. Coastal Union (14) 11
14. Villa Squad (15) 10

Aboodmsuni.blogspot.com

LIVERPOOL WAITOA MAN UNITED FA CUP



szólj hozzá: Liverpool vs United 2-1 Goal

CRISTIANO RONALDO AENDELEA KUVUNJA REKODI KWENYE LA LIGA


Winga wa Klabu ya Real Madrdi Cristiano Ronaldo ameendelea kuvunja rekodi katika ligi kuu ya Spain baada ya sasa kuwa ndio mchezaji aliyefunga mabao mengi katika nusu ya msimu kuliko mchezaji yeyote katika historia ya ligi hiyo.

Ronaldo alishinda tuzo ya Pichichi msimu uliopita baada ya kufunga mabao 41, na mwaka huu msimu ukiwa upo katikati mreno huyo tayari ameshatupia kambani mabao 23, na kuivunja rekodi aliyoiweka mwenyewe msimu uliopita ya mabao 22 pamoja na ile mshambuliaji wa zamani wa Barcelona Cesar ambaye nae alifunga mabao 22 katika nusu ya kwanaza ya msimu wa 1950/51.

LA LIGA ALL-TIME TOP SCORER IN 1ST LEG.

ALL-TIME TOP SCORERS IN FIRST LEG OF LA LIGA
SeasonPlayerTeamGoals
2011/12Cristiano RonaldoReal Madrid23
1950/51CesarBarcelona22
2010/11Cristiano RonaldoReal Madrid22
1989/90Hugo SanchezReal Madrid20
1999/00SalvaRacing20
1943/44EchevarriaReal Oviedo19
1943/44M. MartinBarcelona19
1934/35LangaraReal Oviedo18
1978/79KranklBarcelona18
2005/06Eto'oBarcelona18
2008/09Eto'oBarcelona18
1986/87Hugo SanchezReal Madrid18

Kwa namba hizi ya magoli Ronaldo angeweza kuwa mfungaji bora wa La Liga kwa mara 26, kwa sababu washindi wa pichichi wa muda huo hakuwahi hata kufikisha idadi hii ya mabao aliyonayo Ronaldo sasa tena akiwa leg ya kwanza ya msimu.


EDITIONS OF LA LIGA IN WHICH RONALDO WOULD HAVE WON THE PICHICHI TROPHY WITH THESE NUMBERS
SeasonPlayerTeamTotal goals
1928/29BienzobasReal Sociedad14
1929/30GorostizaAthletic19
1931/32GorostizaAthletic12
1932/33OlivaresReal Madrid16
1944/45ZarraAthletic19
1947/48PahiñoCelta23
1957/58Di StefanoReal Madrid19
BadenesValladolid19
Ricardo AlosValencia19
1958/59Di StefanoReal Madrid23
1963/64PuskasReal Madrid20
1965/66VavaElche19
1967/68UruiarteAthletic22
1968/69AmancioReal Madrid14
GarateAt. Madrid14
1969/70AmancioReal Madrid16
GarateAt. Madrid16
AragonesAt. Madrid16
1970/71GarateAt. Madrid17
RexachBarcelona17
1971/72Enrique PortaGranada20
1972/73MarianinReal Oviedo19
1973/74QuiniSporting20
1974/75Ruiz HerreroAthletic19
1975/76QuiniSporting18
1980/81QuiniBarcelona20
1982/83Poli RinconBetis20
1983/84JuanitoReal Madrid17
Da SilvaValladolid17
1984/85Hugo SanchezAt. Madrid19
1985/86Hugo SanchezAt. Madrid22
1990/91ButragueñoReal Madrid19
200/01TristanDeportivo21

KALI YA LEO: MARK VAN BOMMEL APIGWA UWANJANI

CASILLAS NA RAMOS WAMFANYIA SUPRISE MOURINHO MAZOEZINI

Ingawa gazeti la Marca hivi karibuni kuripoti katika makala moja kuwa Jose Mourinho na Sergio Ramos pamoja na Iker Casillas walitoleana maneno ya kashfa, lakini juzi alhamisi katika camp ya mazoezi ya Madrid mambo yalionekana tofauti sana.

Ugomvi ulioripotiwa na Marca ulikuwa ni juu ya mchezaji gani alipaswa kufanya marking kipindi Carlos Puyol alipofunga goli katika mechi ya kwanza ya Copa del rey.

Lakini wachezaji hao wawili ambao walitoleana maneno na kocha wao walionekana wakimpa zawadi ya keki ya birthday kocha wao ‘The Special One’ katika kusherehekea miaka 49 ya kuzaliwa ya mreno huyo.

ANGALIA VIDEO JINSI ILIVYOKUWA

WILSHARE AUMIA TENA: SHAKANI KUUKOSA MSIMU WOTE


Arsenal wanahofu Jack Wilshare atakosa kipindi chote cha msimu kilichobaki baada ya kupata maumivu tena katika majeraha yake ya enka.

Habari hiisio nzuri kabisa kwa Manager wa England Fabio Capello ambaye Wilshare ni mmoja ya viungo wake anaowaamini na kuwategemea katika kikosi cha England ahead of EURO 2012.

Wilshare amekosa msimu mzima mpaka sasa kutokana na majeruhi aliyoyapata mwanzoni mwa msimu na alitegemewa kurudi uwanjani mapema mwezi ujao.

Lakini akiwa mazoezini Jumanne wiki hii aliumia tena.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alisema: “Nipo disappointed sasa na yanayomtokea Wilshare, kwa sababu anapenda sana kucheza soka. Nina huzuni sana kwa kijana umri kama wake kutumia muda mwingi kukaa nje ya uwanja.

ROONEY AONGEZEKA KATIKA LISTI YA MAJERUHI UNITED: KUUKOSA MCHEZO WA LEO DHIDI YA LIVER.


Wayne Rooney ana asilimia kubwa ya kukosa mchezo wa leo raundi ya nne kati ya Manchester United na mahasimu wao Liverpool.

Rooney hajafanya mazoezi na United wiki hii yote baada ya kupata majeruhi ya goti na enka katika mchezo wa wiki iliyopita wa premier league dhidi ya Arsenal @Emirates.

Chini ya sheria na taratibu za United, hali hiyo itamuweka nje ‘Baba Kai’ katika mechi ya leo @Anfield, ingawa inaweza ikawa vigumu kwa Sir Alex Ferguson kumuacha nje mshambuliaji mwenye mabao mengi msimu huu ukizingatia mchezo wenyewe unachezwa katika uwanja ambao siku za hivi karibuni pamekuwa sio mahala pazuri.

Hii inaamanisha kwamba kama Rooney hatocheza leo, kikosi cha Red Devils kitakuwa bila wachezaji 11 wa kikosi cha kwanza. “Hiii sio hali nzuri kabisa kwetu”, alikiri Fergie.

TUNISIA YAFUATA IVORY COAST HATUA YA PILI AFCON

CHAMAKH ARUDI ARSENAL: MOROCCO NJE KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA

Friday, January 27, 2012

KALI

AZAM NA SIMBA ZAONGOZA KUDAI MAMILIONI TFF


Chairman wa Kamati ya Ligi, Wallace Karia amethibisha Azam, Mtibwa Sugar na Simba kwa pamoja zinalidai Shirikisho la Soka Tanzania zaidi ya shilingi 63 milioni kati ya sh 121 milioni inazodai TFF huku akisema klabu nyingine za Ligi Kuu zinadai pia.

Klabu ya Azam inaongoza kwa kudai sh 24,066, 619 huku Mtibwa Sugar ikishika nafasi ya pili kwa kudai sh 20,976,426 wakati Simba inakamata nafasi ya tatu kwa kudai sh 19, 731,887 na timu ya JKT Oljoro ikidai kidogo zaidi sh 465.

Tathmini iliyofanywa hivi karibuni na Kamati mpya ya kuendesha ligi hiyo iliyoteuliwa na rais wa TFF, Leodegar Tenga na Mwenyekiti wake Karia imebaini kuwa klabu zote 14 zinaidai TFF jumla ya shilingi 121,979,048.

Fedha zinazodaiwa na klabu hizo na klabu za Ligi Kuu ni zawadi na fedha za nauli za maandalizi zinazotolewa na wadhamini wa Ligi hiyo kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom.

Kwa upande wa Azam wanadai fedha za zawadi ya mshindi wa tatu wa Ligi msimu wa 2009/10, Sh10 mil ni fedha za udhamini wa Vodacom na sh 4, 789,166 za mgawo wa mwezi Novemba mwaka jana.

Simba inaidai TFF, sh 19,731,887mil na kati ya hizo Sh 8mil ni za zawadi ya ushindi wa pili Kombe la Kagame lililofanyika katikati ya mwaka jana, Sh 6mil ni baki la mshindi wa pili wa zawadi ya Ligi Kuu msimu wa 2009/10.

Pia, sh 4 mil ni ambazo zimetokana na tiketi walizochukua kwenye pambano la Simba na TP Mazembe mapema mwaka jana.

Mbali na timu hizo timu nyingine zinazoidai TFF na madeni yao kwenye mabano ni Ruvu Shooting (sh 15,137,507ml), Kagera Sugar (Sh 14,725,431ml), Yanga (Sh 9,323,322ml), Polisi Dodoma (Sh 8,359,621ml), Moro United (Sh 5,653,074ml), Toto Afrika (sh 3,255,650), Ruvu JKT (sh 3,255,650) Samai Magereza - Tanzania Prisons (Sh 3,228,512), AFC (sh 2,005,400), Maji Maji (Sh 2,462,334), Afrika Lyon (Sh 1,878,631ml), Villa Squad (Sh 1,907,738ml) na Coastal Union (Sh 532,535).

COSTA ARUDISHWA KIKOSINI NA MASHARTI YA KUKATWA NUSU MSHAHARA


Uongozi wa klabu ya Simba umemrudisha kundini beki wake Victor Costa kwa sharti la kumlipa nusu mshahara mwezi huu kama sehemu ya adhabu yake kwa kosa lake la kutoroka kambini.

Mbali na Costa naye Salum Machaku ameandikiwa barua ya onyo kwa kitendo chake cha utovu wa nidhamu alichokionyesha kwenye mazoezi ya timu hiyo ilipokuwa ikishiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi mwezi huu visiwani Zanzibar.

Akizungumza jana mmoja wa viongozi wa Simba alisema Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo ilikaa na kujadili suala la Costa na kuamua kumkata mshahara wake wa mwezi huo ikiwa ni onyo kwa wachezaji wengine na kuamua kumrudisha kambini ili aweze kuendelea na mazoezi na wenzake.

Alisema baada ya mchezaji huyo kuondoka kambini bila taarifa kwa viongozi wake iliamriwa apumzishwe kuendelea na kambi wakati wa michuano hiyo kabla ya kutoa hukumu ya mwisho ambayo ni kumkata mshahara wake.

"Mwezi huu tutamlipa nusu mshahara ikiwa sehemu ya adhabu yake na kutakiwa kuendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mechi za ligi, lakini kwa mwenzake Machaku ameandikiwa barua ya kutakiwa kujirekebisha," alisema kiongozi huyo.

Kuhusu suala la Emmanuel Okwi, chanzo hicho kilidai uongozi ulimsikiliza na uamuzi zaidi utachukuliwa hapo baadaye.

WACHEZAJI BORA WA LIGI KUU YA ENGLAND KUTOKA KWENYE KILA TIMU.




Mpaka kufikia sasa ligi kuu ya England imefikia katikati katika msimu huu wa 2011-2012, hivyo wacha leo tufanye review ya kuchagua mchezaji bora kutoka kwenye kila klabu katika premier league.

Tutawapanga wachezaji hawa kutokana na nafasi za timu zao katika msimamo wa ligi ulivyo.

20: WIGAN ATHLETIC: MOHAMED DIAME

Performance ya Mohamed Diame ndani ya kikosi cha Wigan inaonekana itamuongoza na kumletea mafanikio makubwa Msenegali huyu mzaliwa wa Ufaransa.

Sio tu anaongoza kwa kufanya tackles nyingi lakini pia ndio mchezaji wa pili wa timu hiyo ambaye anaongoza kwa kufanya dribbling nyuma ya Victor Moses.


19: WOLVES: WAYNE HENNESSEY

Ben Watson na Sebastian Larsson wanaweza kuwa mashahidi wazuri juu ya uwezo Wayne Hennessey katika kuokoa penati.

So far , mchezo bora kabisa wa Hennessey ulikuwa dhidi ya Arsenal.

Aliokoa magoli ya wazi zaidi ya 9 na kufanikiwa kuwa mchezaji bora wa mechi katika mechi ambayo Wolves walimaliza wakiwa 10 uwanjani ni kujipatia pointi moja kibindoni.


19: BLACKBURN: YAKUBU

What a comeback kutoka Yakubu.

Wengi tulifikiri his top flight career ilikuwa imeisha baada ya kufunga goli 11 katika misimu mitatu iliyopita akiwa Everton.

Msimu huu, Yakubu amefunga magoli 12 mpaka sasa akiwa na Blackburn, ambao wapo katika kupambana na vita ya kushuka daraja.



18: BOLTON WANDERERS: IVAN KLASNIC

Kwa asilimia 44 Ivan Klasnic ameisadia indirectly na directly upatikanaji wa magoli yote ya Bolton msimu huu katika premier league.

Huku Kevin Davies akipoteza nafasi yake kikosini na David Ngog akionekana kutojitosheleza kama mshambuliaji wa Premier league – Bolton wanamhitaji Klasnic katika kila mchezo.


17: QPR: ALEJANDRO FAURLIN

Kama Queens Park Rangers watakuja kushuka daraja, then kukosekana kwa Alejandro Faurlin kutokana na majeruhi inaweza ikawa sababu.

16: QPR wana tatizo la kutokufunga magoli, hivyo wanahitaji kuwa na uwezo wa kuzuia kiushindani.

Faurlin amefanikiwa kushinda kurudisha possession mara 146.


15: WEST BROM: CHRIS BRUNT

Magoli mengi yaliyofungwa na West Brom msimu huu yametokana usaidizi wa kutoa za mwisho za Chris Brunt, ambaye ametoa assists nyingi kuliko Graham Dorrans, Jerome Thomas, Peter Odemwingie, Shane Long, Somen Tchoyi na Zoltan Gera wakijumlishwa.

Ama kwa hakika West Brom watapata tabu sana kutokana na kukosekana kwa Brunt ambaye amepata matatizo ya enka.



14: EVERTON: LEIGHTON BAINES

Ni lazima iwe aidha Jose Enrique au Leighton Baines pale linapokuja suala la beki wa kushoto wa bora wa Premier kwa sasa.

Baines yupo balanced, anajua kusambaz mipira vizuri, kukaba, kupandisha timu na kuongoza mashambulizi yote ya Everton, pia ni hatari sana kwa set-piece.

Kama Fabio Capello anaagalia form katika kuchagua wachezaji wake then Leighton Baines anastahili kuanza mbele ya Ashley Cole in Three lions squad.



13: SWANSEA CITY: MICHEL VORM

Kama David De Gea angekuwa anacheza kama Michel Vorm, media zingekuwa zinamsifia sana ni ujio wa pili wa Lev Yashin katika premier league.

On form, Vorm kwa sasa ndio golikipa bora katika premier league.


12: FULHAM: CLINT DEMPSEY

Mousa Dembele yupo na kipaji kikubwa sana, ana ujuzi zaidi, pia ni hatari sana lakini kwa sababu zisizoelezeka amekuwa hatoi matunda ya mwisho ya kipaji chake.

Huku tofauti, Clint Dempsey, ambaye uwezo wa unazaa matunda makubwa nadani watoto wa Mohamed Al Fayed.

Minf you, ana wastani wa mashuti manne kila mechi, na goli 6 kati ya shots 79. Dempsey mpaka sasa ndio mfungaji bora wa Fulham akiwa magoli 9 in EPL.

Kama ulikuwa unajiuliza vipi kuhusu Andy Johnson na Bobby Zamora wote kwa pamoja wana wastani wa goli 7 katika shots 54.


11: ASTON VILLA: STILIAN PETROV

Nani anaongoza kwa kufanya interceptions katika premier league? Jibu ni Stilian Petrov.

Inaeleweka kama utakuwa una unafikiria kasi ya Gabriel Agbonlahor, lakini amekuwa akifanya nini msimu huu?

Amefunga magoli au kutoa asisists ngapi dhidi ya Arsenal, Chelsea, Manchester City, Manchester United na Tottenham Hotspur? Jibu ni zero.

Petrov hajasaidia katika midfield pia anatoa msaada wa nguvu katika kutoa pasi zinazoaa matunda, lakini pia kazi anayoifanya katika kukaba ni exceptional.



10: SUNDERLAND: STEPHEN SESSEGNON

Stephen Sessegnon ndiye best dribbler at Sunderland, na anamzidi Sebastian Larsson linapokuja suala la kupiga key passes.

Alikuwa yupo vizuri @Paris Saint Germain na hata sasa anaendeleza makali akiwa Sunderland.

Ingawa kwa mtu mwenye kipaji cha aina yake inilibidi awe na assists na magoli mengi pia.


9: NORWICH CITY: STEVE MORISON

Kijana huyu ndio nguzo kuu ya mashambulizi ya Norwich City, mipira yote ya Norwich inayoenda mbele inamlemnga yeye. NDio maana aliwapa tabu sana mabeki wa timu kubwa kama Manchester United, Chelsea, na hata Arsenal ambao aliwafunga.

Morison ndio top scorer wa Norwich City akiwa tayari ameshafunga magoli 7 katika premier league.



8: STOKE CITY

Stoke City wamefunga magoli ya penati kuliko ya kawaida.

Katika upatikanaji wa magoli hayo Jonathan Walters amekuwa na mchango mkubwa wa magoli na assists 10 katika mashindano yote.



7: NEWCASTLE UNITED: DEMBA BA

Rekodi zake Demba Ba zinaongea zenyewe hahitaji maelezo mengi.



6: LIVERPOOL: LUIS SUAREZ

Angalia hali mabayo amekutana nayo Suarez ndani ya Liverpool msimu.

Amecheza na mtu ambaye hayupo kabisa kwenye form, na asiye msaada wa maana Andy Carrol. Pia kuna huyu Stewart “Nothing” Downing ambaye ni winga ambaye hana goli wala assist mpaka sasa.

Lakini na hali hiyo Suarez ameibeba Liverpool katika mashabulizi na kufunga magoli 5 na kutoa assist 3 katika michezo 16 ya epl msimu huu. Na angekuwa na magoli mengi zaidi kama sio mashuti yake matano kugonga mwamba.

Suarez anaofa vision na pasi nzuri, huku uwezo wake wa kufanya dribbling ukiwa excellent.



5: ARSENAL: ROBIN VAN PERSIE

Kwa statistic, Robin Van Persie yupo katika mstari mmoja na Lionel Messi na Cristiano Ronaldo. Hii inaonyesha ni msimu mzuri kiasi gani alionao Van Persie.

Huyu ndio nguzo ya mashambulizi ya Arsenal. Akiwa ndio Top scorer wa ligi kuu ya England.

Kupata maumivu kwa Van Persie kunaweza kuharibu shughuli kabisa pale Emirates. Lakini sio mbaya Thierry Henry yupo pale.

Ukimuongelea Henry, ilimchukua dakika 10 tu kufunga bao, lakini ilimchukua Fernando Torres dakika 903 kufunga goli lake la kwanza la msimu.


4: CHELSEA: JUAN MATA

Nani aliyepiga key passes nyingi kuliko wote katika premier league? Juan Mata.

Huyu ndio mtu pekee anayeweza kumchezesha Fernando Torres, lakini bado Andre Villas Boas anakataa kumchezesha Mata nyuma ya Torres.

Kama sio Mata, Chelsea sasa hivi wangekuwa katikati mwa msimamo wa ligi na Villas-Boas angekuwa ameshafukuzwa.

Ndio mtu anayeipa uhai mkubwa safu ya ushambuliaji ya Chelsea.


3: TOTTENHAM HOTSPUR: LUKA MODRIC

Luka Modric kwa Tottenham ni kama Xavi kwa Barcelona.

Gareth Bale amesaidiwa sana na uwezo wa Modric kupiga accurate long balls kwa kwake.

Modric amepiga pasi zilizofanikiwa 1,074, na 140 kati ya hiyo ni mipira mirefu inayozaa matunda kwa timu. Form aliyonayo Modric ndio moja ya sababu kuu kwanini Spurs sasa nao wanagombea ubingwa na timu za jiji la Manchester.



2: MANCHESTER UNITED: WAYNE ROONEY

Katika mechi tano za mwanzo za Wayne Rooney msimu huu, alifunga mabao 8 na kutoa assist moja.

Rooney ameendela kuwa world class player ndani kikosi cha United. Sir Alex Ferguson alimuacha Rooney baada ya kutoka usiku na mkewe na adhabu hiyo ya Babu kwa Rooney iliishia kuwagharimu United dhidi ya Blackburn.

Hiyo pekee inaonyesha ni kiasi gani Rooney ana umuhimu ndani ya kikosi cha Mashetani Wekundu.


1: MANCHESTER CITY: DAVID SILVA

Ukiwa unapima kuhusu uzuri wa kiungo cha timu za premier league, hapo ndio utamkuta mtalaam David Silva.

Anfanya kila kitu ambacho Luka Modric anafanya, lakini pia kwa kuwa na consistency pia anafunga magoli na kutoa assists.

Huyu jamaa ni genius wa soka, ni anapaswa kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa ndani ya Manchester City.

Roberto Mancini kwa sasa, anaye golikipa bora wa kiingereza, pia ukuta bora wa katika ligi, safu bora kiungo katika premier league na pia the best forward line katika ligi.

Lakini kwa sababu zisizoelezeka Manchester City wapo nje ya Champions league, FA Cup, na Carling Cup.

Ningekuwa mimi ndio Shekhe Mansour ningeshamtimua Mancini, ana kila kitu ambacho Arsenal hawana lakini bado The Gunners wapo katika michuano mitatu msimu huu.