Search This Blog

Saturday, January 28, 2012

ROONEY AONGEZEKA KATIKA LISTI YA MAJERUHI UNITED: KUUKOSA MCHEZO WA LEO DHIDI YA LIVER.


Wayne Rooney ana asilimia kubwa ya kukosa mchezo wa leo raundi ya nne kati ya Manchester United na mahasimu wao Liverpool.

Rooney hajafanya mazoezi na United wiki hii yote baada ya kupata majeruhi ya goti na enka katika mchezo wa wiki iliyopita wa premier league dhidi ya Arsenal @Emirates.

Chini ya sheria na taratibu za United, hali hiyo itamuweka nje ‘Baba Kai’ katika mechi ya leo @Anfield, ingawa inaweza ikawa vigumu kwa Sir Alex Ferguson kumuacha nje mshambuliaji mwenye mabao mengi msimu huu ukizingatia mchezo wenyewe unachezwa katika uwanja ambao siku za hivi karibuni pamekuwa sio mahala pazuri.

Hii inaamanisha kwamba kama Rooney hatocheza leo, kikosi cha Red Devils kitakuwa bila wachezaji 11 wa kikosi cha kwanza. “Hiii sio hali nzuri kabisa kwetu”, alikiri Fergie.

No comments:

Post a Comment