Search This Blog

Saturday, September 17, 2011

REDONDO AIPANIA YANGA KESHO


Kiungo Ramadhani Chombo ‘Redondo’ amewatoa hofu mashabiki wa Azam FC kwa kuwa hakikishia ushindi katika mechi zijazo za ligi kuu ukiwepo mchezo wa kesho dhidi ya Yanga utakaochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na tovuti ya Azam,Redondo amesema wamefanya maandalizi ya kutosha kupambana na timu yoyote watakayokutana nayo.

“Timu ina hali nzuri, na kwa kuwa tumekuwa pamoja muda mrefu, tunahitaji ushindi kwa kila mechi tunayokutana nayo ili kufikia malengo yetu, hata kama ni Yanga kwetu ushindi lazima” alisema Redondo.

Redondo ameongeza kuwa baada ya kucheza michezo iliyopita, timu inapigana kadri iwezavyo ili kukaa katika nafasi nzuri. Naye nahodha msaidizi wa timu hiyo, Aggrey Morris amesema wapo katika maandalizi mazuri na mechi dhidi ya Yanga ni sawa na mechi ya kawaida hivyo ushindi utapatikana.

Amesema wapenzi wa Azam FC wasiwe na mashaka, wachezaji wote wapo makini na wajitokeze kwa wingi kwani hawatawaangusha.

Kocha mkuu Stewart Hall amezungumzia mchezo huo kama ni moja ya mechi muhimu kwao ya kupata pointi tatu, kwakuamini kuwa kutokana na wachezaji kuonyesha hali ya kupatikana kwa ushindi.

“Wachezaji wapo kamili, MrishoNgassa na Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ wameshamaliza adhabu zao hivyo watakuwepo katika mchezo huo” alisema Stewart.

Ameongeza kuwa watatumia mapungufu walionayo Yanga kupata ushindi, anaamini safu yake ya ulinzi iliyoko chini ya nahodha Aggrey Morris watahakikisha hakuna madhara katika lango lao litakalosimamiwa na makipa Mwadini Ally na Obren Cuckovic.

Azam FC kesho itacheza mchezo wake wa saba wa ligi kuu dhidi ya Yanga, Azam itashuka katika mchezo huo ikiwa na pointi nane, ikishinda michezo miwili, sare michezo miwili na kupoteza mchezo mmoja, wakati Yanga inapointi 6.

MTIBWA YAITANDIKA 2-0 VILLA SQUAD

MTIBWA SUGAR YA MOROGORO LEO IMEIFUNGA VILLA SQUAD YA DAR MABAO MAWILI KWA BILA KATIKA MCHEZO WA LIGI KUU YA TZ.BARA .MAGOLI YA MTIBWA YAMEFUNGWA NA THOMAS MORRIS, NA SAID RASHID.

MATOKEO MENGINE YA VODACOM PREMIER LEAGUE

TOTO AFRICA 0-0 JKT RUVU

RUVU SHOOTING 2-1 COASTAL UNION

BLACKBURN 4 - ARSENAL

MAGOLI MATANO YALIYOFUNGWA NA WACHEZAJI WA ARSENAL HAYAKUTOSHA KUWAOKOA THE GUNNERS NA KIPIGO KUTOKA KWA BLACKBURN LEO KWENYE EPL. MAGOLI MAWILI YA KUJIFUNGA YA ALEX SONG NA LAURENT KOSCIENLY NA MENGINE MAWILI KUTOKA YAKUBU YAKITOSHA KUPELEKA MSIBA EMIRATES STADIUM.

YAKUBU AKIPEWA "GWALA" NA KOCHA WAKE STEVE KEAN BAADA YA KUFUNGA BAO

MIKAEL ARTETA AKIFUNGA BAO LA KWANZA KWENYE MECHI DHIDI YA BLACKBURN


MASHABIKI WA BLACKBURN WAKIANDAMANA KWA MADAI KUMTAKA KOCHA "STEVE KEAN" AJIUZULU.


MECHI ZA LEO VODACOM PREMIER LEAGUE


TOTO AFRICAN Vs JKT RUVU
Mchezo huu utapigwa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.


VILLA SQUAD Vs MTIBWA SUGAR.
Baada ya kufungwa na Simba na Azam FC, Villa squad itakuwa kibaruani kuwakabili wakatamiwa wa Morogoro, Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Azam uliopo Chamanzi Mbande nnje kidogo ya jiji la Dar es salaam.



RUVU SHOOTING Vs COASTAL UNION.
Coastal union leo watakuwa wanatafuta namna ya kujifariji pale watakapo karibishwa Ruvu Shooting katika dimba la Mlandizi mkoani Pwani.
VILLA SQUAD Vs MTIBWA SUGAR.
Baada ya kufungwa na Simba na Azam FC, Villa squad itakuwa kibaruani kuwakabili wakatamiwa wa Morogoro, Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Azam uliopo Chamanzi Mbande nnje kidogo ya jiji la Dar es salaam.


RUVU SHOOTING Vs COASTAL UNION.
Coastal union leo watakuwa wanatafuta namna ya kujifariji pale watakapo karibishwa Ruvu Shooting katika dimba la Mlandizi mkoani Pwani.

MTIHANI WA KWANZA KWA ANDRE VILLAS-BOAS

Kocha Andre Villas-Boas anakutana na mtihani wa kwanza mgumu akiwa kocha kesho jumapili, na nafikiri tutaona na kujua mengi kuhusu falsafa zake kwenye soka.

Chelsea hawajafungwa tangu mreno huyo mwenye miaka 33 alipowasili Stamford Bridge akitokea Porto.

Na nafikiri trip ya Chelsea kwenda Old Trafford itatuthibitishia ubora wa mbinu za Villas Boas.

Tunafahamu nini tutegemee kutoka kwa Manchester united ambao hawajawahi kucheza defensively dhidi ya timu yoyote iwe Barcelona au Wigan.

United hawatobadilisha mchezo wao dhidi ya Chelsea lakini kitachokuwa kinavutiwa zaidi ni kuona jinsi gani wageni watakavyocheza.

Vilas-Boas alipokuwa Porto alikuwa akitegemea kushinda kila mchezo lakini sasa yupo katika sehemu nyingine.

Anai-manage timu kubwa ambayo kesho inasafiri kwenda Theatre of Dreams ambako mwaka huu timu yao ipo katika form nzuri.

Hivyo nafikiri mchezo utatueleza na kutufanya kumjua vizuri Villas-Boas.

Je atafahamu kuwa ni vigumu sana kucheza na United kwa open game?

Au anaweza kwenda na akacheza aina ya mchezo huo na akafanikiwa.?

Nafahamu nini Jose Mourinho ambaye siku zote amekuwa akifananishwa na Villas-Boas-angeenda kufanya kama bado angekuwa kocha wa Chelsea.

Kama Mourinho angekutana na United ambayo ipo kwenye form nzuri, basi ni dhahiri angecheza mchezo wa kuzuia zaidi.

Hivyo natamani kuona je Villas Boas atacheza mtingdo wa 4-3-3 au 4-5-1 au 4-4-2 @ old Trafford.

Kesho naamini AVB atachagua kikosi chake bora kabisa kwa mara ya kwanza kitu ambacho tena kitakuwa cha kutazamwa ili kujua his assessment of his squad.

Haijalishi matokeo ya kesho, nina uhakika AVB atakuwa manager mzuri sana.

MATCH PREVIEW: BLACKBURN VS ARSENAL.

Arsenal wanapata nafasi ya pili ya kuwafurahisha mashabiki wao na kujenga ‘confidence’ muhimu kwenye timu yao wikiendi hii wanapokutana na Blackburn Rovers .

Kikosi cha washika bunduki kinaingia kwenye mchezo huu kikiwa kimesheheni kwa mara ya kwanza msimu huu baada ya kuwakosa nyota wake kwa sehemu kubwa ya michezo minne ambayo imeshachezwa hadi sasa .

Gervinho na Alex Song wanarejea baada ya kuwa nje wakitumikia adhabu huku wachezaji wapya waliosajiliwa wakiendelea kuzoea mazingira ya timu yao mpya wakiwa wamekaa na kikosi cha washika bunduki kwa wiki mbili tangu waliposajiliwa.

Kikosi cha Blackburn bado hakijaa vizuri na imani ya wengi ni kuwa watafungwa na Arsenal tena kirahisi.

Mchezo wa kwanza kwa Arsenal kushinda ulikuwa mwishoni mwa wiki iliyopita walipoifunga timu iliyopanda daraja ya Swansea City tena kwa bao ambalo lilikuja kutokana na boko la kipa wa Swansea.

Kuna mengi ambayo yamefanana kwenye viwango vya timu hizi mbili hadi kufikia wiki ya tano ya ligi kuu ya England . Blackburn wameshinda mchezo mmoja kati ya michezo tisa iliyopita na Arsenal wana rekodi kama hiyo tofauti ikiwa kwenye ukweli kuwa kwao ni rekodi ya michezo ya ugenini na kwa Rovers ni michezo yote.

Kocha wa Blackburn Steve Kean bado ana wakati mgumu sana kwenye kipindi chake kama kocha.

Wakati akiandaa timu ya kucheza na Arsenal, mitaani kuna mashabiki wanaanda maandamano ya kuwashinikiza wamiliki wa timu hii wamfukuze kazi kwa kushindwa kuipa mafanikio timu yao.

Tatizo kubwa linalotazamwa na wataalamu kwa Blackburn ni kwa kocha Steve Kean kuwa na uzoefumdogo.

Kumbuka Steve Kean alikuwa kocha msaidizi kwa Sam Allardyce na alipofukuzwa bosi wake ndipo alipopewa jukumu la kuwa kocha mkuu .

Tayari baadhi ya wachezaji tegemeo wa Blackburn walieleza kukerwa na uamuzi wa kumuondoa kocha Sam Allardyce na mfano mzuri alikuwa nahodha Christopher Samba .

Hapo moja kwa moja utagundua kinachoisibu Blackburn na ndio maana wanaingia kwenye mchezo dhidi ya Arsenal wakiwa kwenye hali mbaya ambayo huenda ikaendelea kwenye mchezo huu.

Kwa jinsi ambavyo michezo yao miwili ya mwisho ilivyoenda unaweza kusema kuwa Rovers hawana bahati .

Wiki iliyopita walicheza na Fulham wakatoka sare 1-1 na kabla ya hapo walicheza katika mchezo ambao wangeweza kuchukua pointi zote tatu kwani walikosa penati mbili na bao lililowaua lilikuwa kwenye dakika ya mwisho ya mchezo lilikuwa bao la penati pia ambayo iliwekwa wavuni na Mikael Arteta mtu ambaye watakutana naye kesho akiwa na timu nyingine .

Bahati mbaya ya Blackburn ina kila dalili za kuendelea unapotazama orodha ya wachezaji watakaokosa mchezo wao dhidi ya Arsenal.

David Hoilett,David Dunn,Morten Gamst Pedersen na Ryan Nelsen wote wataukosa mchezo huu huku beki na nahodha Christopher Samba akiwa na shaka japo kuna uwezekano mkubwa wa kumuona .

Bado mshambuliaji mpya Mauro Formica hajapata muda wa kutosha kuzoeana na wenzie na ndio maana hadi sasa bado ameonekana kupata wakati mgumu kwenye timu yake mpya.

Tegemeo pekee walilo nalo Rovers ni kwa beki mpya Scott Dann aliyesajiliwa toka Birmingham City ambaye anatrajiwa kucheza pembeni ya Christopher Samba .

Katikati ya uwanja Steve Nzonzi atakuwa muhimu sana kwa jinsi anavyoweza kuunganisha sehemu mbili za beki na safu ya viungi wa mbele na washambuliaji na atakuwa msaada mkubwa kwa Mauro Formica ambaye atacheza shimoni.

Rubben Rochina pamoja na Goodwillie watakuwa mbele kusaidiana na Nzonzi na Formica kujaribu kuivuka ngome itakayokuwa chini ya mjerumani Per Mertersecker.

Mashabiki wa Arsenal kwa vyovyote watakuwa na mawazo kuwa timu yao imevuka kipindi cha mpito na matatizo yake yameisha lakini ukweli ulioonyeshwa na mchezo wa wiki iliyopita dhidi ya Swansea ambapo Arsenal walishinda kwa bao la ‘kidizaini’ kama wasemavyo vijana wa mtaani ni kwamba bado hali sio nzuri kama ambavyo wangependa iwe.

Kikosi cha Arsenal kitawakosa Thomas Vermaelen ambaye amerudi kwenye meza ya wagonjwa na kiungo Abou Diaby pamoja Jack Wilshere bado wataendelea kuwa nje .

Nafasi zao zitachukuliwa na watu wale wale ambao wamekuwa wakijaza mashimo yaliyopo kina Thomas Rosicky na Aron Ramsay endapo atakuwa amepona haraka kama inavyotaarifiwa kuwa .

Viungo Gervinho na Alex Song watarudi kuungana na kinda Emanuel Frimpong ambaye ametokea kuwa tegemeo kwa Arsenal lakini faida iliyopo ni kwamba wachezaji wapo na washika bunduki hawatalazimika kutumia vijana kama walioonekana kwenye kipigo cha bao nane toka kwa Man United.

Mikael Arteta atakuwa kwenye sehemu ya kiungo kuendeleza kazi iliyomleta Emirates ya kujaza nafasi ya Cesc Fabregas na pia inaweza kuwa nafasi ya wachezaji wapya kina Yossi Benayoun na Andre Santos na hata mshambuliaji Park Chu Young kuonyesha uwezo wao.

Timu hizi zote mbili kwa pamoja zinaweza kusema kuwa huu ndio mwanzo mbaya wa msimu kuliko misimu yote katika historia zao ambapo Rovers wanashika mkia wakiwa na pointi moja tu waliyoipata wiki iliyopita mikononi wa Fulham na Arsenal wako kwenye nafasi ya 12.

Katika michezo minne iliyopita Blackburn wameruhusu wavu wao kutikiswa mara 7 na Arsenal wameruhusu wavu wao kutikiswa mara nyingi zaidi .

Blackburn wana rekodi mbaya sana katika michezo yao dhidi ya Arsenal na wamefungwa michezo 21 huku wakishinda mechi 17 kati ya mechi 53 ambazo zimechezwa kwenye uwanja wao.

Arsenal wao wamefungwa na Blackburn mara moja katika michezo 10 iliyopita na Arsenal wameshinda mara saba mfululizo huku wakifunga mabao 212 katika michezo yote waliyocheza kwenye historia ya ligi ya England huku Blackburn wao wakifunga mara 145.

Endapo Arsenal itafungwa katika mchezo huu itakuwa mara yao ya 100 kupoteza mchezo kwenye ligi kuu ya England .

Hadi sasa hakuna mchezaji yoyote wa Arsenal ambaye amefunga zaidi ya bao moja na pia hakuna mchezaji ambaye ametoa pasi ya bao zaidi ya moja .

Friday, September 16, 2011

WAZEE WA KUBET HAYA MZIGO HUU HAPA !!

England Premiership

Aston Villa v Newcastle - Small Stake on Draw 1-1

Everton v Wigan - Small Stake on Home Win 1-0

Blackburn v Arsenal - Small Stake on Away Win 0-1

Wolverhampton v QPR - Small Stake on Home Win 1-0

Bolton v Norwich - Small Stake on Draw 2-2

Swansea v West Brom - Small Stake on Away Win 0-1


Scotland Premier

Dundee Utd v Inverness CT - Small Stake on Away Win 0-1

Motherwell v St Johnstone - Small Stake on Draw 1-1

Hearts v St Mirren - Small Stake on Home Win 1-0

Aberdeen v Kilmarnock - Medium Stake on Draw 1-1

Dunfermline v Hibernian - Large Stake on Home Win 3-0


Italy Serie A

Cagliari v Novara - Medium Stake on Home Win 2-1

Inter Milan v Roma - Medium Stake on Home Win 2-0


Spain Primera Liga

Sporting Gijon v Valencia - Small Stake on Away Win 0-1

Mallorca v Malaga - Small Stake on Away Win 0-1

Granada v Villarreal - Medium Stake on Draw 1-1

Barcelona v Osasuna - Large Stake on Home Win 2-0

Sevilla v Real Sociedad - Medium Stake on Home Win 2-1


Germany Bundesliga

Bayer Leverkusen v FC Koln - Large Stake on Home Win 1-0

Hamburg v Borussia Monchengladbach - Large Stake on Away Win 0-1

Nurnberg v Werder Bremen - Large Stake on Away Win 0-1

Kaiserslautern v Mainz - Large Stake on Away Win 1-2

Hoffenheim v Wolfsburg - Medium Stake on Home Win 2-0

Hertha Berlin v Augsburg - Large Stake on Home Win 1-0


France Ligue 1

Valenciennes v Dijon - Medium Stake on Draw 1-1

Nice v AC Ajaccio - Small Stake on Draw 1-1

Toulouse v Bordeaux - Medium Stake on Away Win 0-1

Brestois v Montpellier - Large Stake on Away Win 0-1

Lille v Sochaux - Large Stake on Away Win 1-2

Auxerre v Caen - Large Stake on Home Win 3-2

Lorient v St Etienne - Small Stake on Draw 1-1


Holland Eredivisie

FC Groningen v Excelsior Rotterdam - Large Stake on Home Win 3-0

Vitesse v Roda JC - Large Stake on Home Win 3-0

VVV Venlo v Heerenveen - Large Stake on Draw 2-2

Feyenoord v De Graafschap - Large Stake on Home
Win 2-0


Portugal Superliga

Nacional v Pacos Ferreira - Large Stake on Away Win 0-1

Kesho ndo kesho: FLOYD Mayweather vs Victor ORTIZ



Matokeo ya Michezo ya Europa League.

Hapo jana kwa mara ya kwanza nilibashiri matokeo ya michezo ya Europa League na mchezo mmoja wa ligi kuu ya Vodacom kama ifuatavyo:
1. Matokeo yaliyopo kwenye mabano ndio matokeo halisi ya michezo ilipigwa hapo jana usiku.
2. Matokeo yaliyopo kwenye mabano na yana rangi ya bluu yametokea kama ambavyo nilibashiri.
3. Mchezo wa YANGA na African Lyon ndio pekee uliotoa matokeo halisi niliyobashiri
4. kati ya michezo 25 niliyobashiri hapo jana michezo 13 nimepatia na mchezo mmoja tu umetoa matokeo halisi niliyoyabashiri

Besiktas v Maccabi Tel Aviv - Home Win 2-1 ( 5:1 )

FC Copenhagen v Vorskla - Home Win 2-0
( 1:0 )

PAOK Salonika v Tottenham - Draw 1-1
( 0:0 )

PSV v Legia Warsaw - Home Win 2-1
( 1:0 )

PSG v SV Salzburg - Home Win 2-0
( 3:1 )

Hapoel Tel Aviv v Rapid Bucharest - Home Win 2-1 ( 0:1 )

Shamrock v Rubin Kazan - Away Win 1-2
( 0:3 )

Slovan Bratislava v Athletic Bilbao - Draw 1-1 ( 1:2 )

Lazio v Vaslui - Home Win 2-0 ( 2:2 )

Hannover 96 v Standard Liege - Home Win 2-1 ( 0:0 )

FC Zurich v Sporting Lisbon - Draw 1-1 ( 0:2 )

Dynamo Kiev v Stoke - Home Win 1-0 ( 1:1 )

Anderlecht v AEK Athens - Home Win 2-1
( 4:1 )

Austria Vienna v Metalist Kharkiv - Draw 1-1 ( 1:2 )

Maccabi Haifa v AEK Larnaca - Home Win 3-1 ( 1:0 )

Wisla Krakow v Odense BK - Draw 1-1 ( 1:3 )

SK Sturm Graz v Lokomotiv Moscow - Draw 1-1 ( 1:2 )

Udinese v Rennes - Home Win 1-0
( 2:1 )

Birmingham v Braga - Home Win 2-1 ( 1:3 )

Fulham v FC Twente - Home Win 2-0 ( 1:1 )

Club Brugge v Maribor - Home Win 2-1 ( 2:0 )

AZ v Malmo - Home Win 3-0
( 4:1 )

Steaua Bucharest v Schalke 04 - Draw 2-2
( 0:0 )

Atletico Madrid v Celtic - Draw 1-1 ( 2:0 )

African Lyon v Yanga - Away Win 2-1 ( 2:1 )

CHAMPIONS LEAGUE: BARCELONA VS AC MILAN MATCH RPORT


Barcelona 2-2 Milan:

September 13, 2011

http://i1231.photobucket.com/albums/ee512/zonal_marking/barca-milan.jpg

Timu zilizoanza

Milan walifunga kwenye dakika ya kwanza ya mchezo na kwenye dakika ya mwisho katika mchezo uliotawaliwa na Barcelona kwa asilimia kubwa ya mchezo.

Timu ya Pep Guardiola iliwatumia Sergio Busquets na Javier Mascherano kama mabeki wa kati na Seydou Keita alicheza kama kiungo mkabaji na Barcelona ilitumia mfumo wa 4-3-3.

Kocha wa Ac Milan Maximiliano Allegri alimkosa Zlatan Ibrahimovic na hii ilimaanisha kuwa Alexandre Pato alianza kama mshambuliaji pekee akisaidiwa na Antonio Cassano nyuma yake . Antonio Nocerino na Gianluca Zambrotta pia walianza .

Mchezo huu ni mgumu sana kuuelezea , swali la kujiuliza ni hili , ni vipi mbinu za Milan zilifanikiwa kwenye mchezo huu? Kuna baadhi ya mbinu zilionekana kufanya kazi , mfano ni wembamba wa uwanja kwa jinsi walivyopanga wachezaji kujaribu kudhibiti njia za Barca kupenyeza mipira, mfumo wa Milan kwa jumla,pamoja na kujaribu kuwaadhibu Barca kwa jinsi walivyokosa kasi kwenye upande wa mabeki, hivi vyote vilifanya kazi, lakini Barcelona wangeweza kuua mchezo kama si uzembe wao wenyewe . Guardiola alikuwa anatumia mbinu zake za siku zote , ukiacha mabeki wa kati ambao wamekuwa tatizo kwa Barca hivi karibuni mbinu za Milan zilifanya kazi kwa kiasi Fulani.

Vitu vilivyofanikiwa kwa upande wa Milan

1 Mfumo kwa ujumla

Timu za Italia zimekuwa zikigharimiwa na kucheza kwa kukosa wachezaji wa pembeni haswa kwenye ligi ya mabingwa.Timu ya mwisho kuondoka na pointi tatu kwenye uwanja wa Nou Camp ilikuwa Hercules ambao walishinda msimu uliopita kwa mabao 2-0 kwenye ligi ya Hispania . Hercules walitumia mfumo wa 4-4-2 ya mtindo wa Diamond na Milan walijaribu kufanya kitu kama hiki ili kushindana na viungo wa Barcelona ambao wanamiliki mpira kwa kiasi kikubwa .Mabeki wa Milan walicheza vizuri wakijitahidi kujenga ukuta ambao ulionekana kuwabana wachezaji wa Barcelona, viungo watatu waliosimama mbele ya mabeki walifanya kazi yao vizuri kwa kuweka ukuta wa ziada mbele ya mabeki wa Ac Milan huku kiungo ambaye alifanya kazi ya ubunifu nyuma ya Cassano na Pato Kevin Prince Boateng na baadae Clarence Seerdorf walicheza kwenye eneo ambalo alisimama Seydou Keita . Tatizo kubwa ambalo liliwakumba Barca kwa kumchezesha Keita mbele ya mabeki kama kiungo mkabaji ni kwamba wachezaji wa Barca walishindwa kwenda kwa Keita kuchukua mipira na hali hii iliwapa uhuru Boateng na Seerdorf.

2.Kumdhibiti Messi.

Siku zote utakapocheza dhidi ya Messi ukae ukijua kuwa lazima yeye ang’ae mwisho wa siku na ukishindwa kumhimili hakuna atakayekulaumu kwa sababu kila mtu anajua uwezo wake na sio mabeki wengi wameweza kumzuia kwa mafanikio . Milan mwanzoni mwa mchezo kuanzia dakika waliyopata bao mpaka kwenye dakika ya 30 waliweza kummudu na kumzuia kwa kiasi fulani, Alesandro Nesta alimkaba na Messi na alihakikisha kuwa alimkera . Haikuwa lengo au mbinu ya Milan kumkaba Messi yeye kama yeye au peke yake . Waliweka nidhamu yao ya ukabaji kama kawaida yao ila kila alipopata mpira walihakikisha kuna watu wawili au zaidi wamemzunguka ,kilichomzuia messi kufanya vitu vyake mwanzoni ni viungo watatu wa Milan waliokuwa wamesimama mbele ya mabeki ambao uwepo wao ulimnyima Messi nafasi ya kurudi hadi katikati ya uwanja kufuata mipira kama anavyofanya siku zote. Barca walicheza sana mbele ya wachezaji nane waliokuwa mbele ya goli na nyuma ya mpira na ndio maana mchezo ulikuwa mgumu kwa Barca mwanzoni . Lakini ndio kama ilivyosemwa awali kwamba utamkaba Messi unavyotaka lakini mwishowe lazima atakudhuru na ndio kilichotokea kwani mwishowe alitengeneza bao lililofungwa na Pedro.

3.Kumhimili Dani Alves

Hasara mojawapo ya kuchezesha mfumo wa 4-3-1-2 dhidi ya timu kama Barcelona au timu nyingine yoyote ile ni ukweli kuwa unawapa uhuru mkubwa sana mabeki wa pembeni . Ila Milan walitumia mfumo huu na hawakupata tabu kwani waliridhika na kuwapa uhuru mabeki wa pembeni wa Barcelona . Alves alikuwa akipambana na Gianluca Zambrotta na Pedro alikuwa akiingia mpaka katikati ya uwanja , Dani Alves hakuwa anakimbia pembeni sana na Zambrotta alikuwa anamruhusu aingie ndani sana kwa kuwa ndio upande ulipo mguu wake wenye nguvu mguu wa kulia japo anatumia miguu yote miwili na upande huo ndio upande ambao Dani Alves hautumii sana na kwa sababu hii Barcelona walijikuta wakipunguza uwanja wao wenyewe huku wakishindwa kutanua uwanja.

4 Pressing ya Milan.

Milan mwanzoni walikuwa wameridhika na kukaa kwenye nusu yao ya uwanja na kuwaachia Barcelona waje , walikuwa wameridhika kukaba na kuutafuta mpira ulioko kwenye himaya ya Barcelona . Kwenye dakika ya 50 walilazimika kutoka pangoni baada ya kufungwa bao la pili . Hapa Allegri hakuona faida ya kukaa nyuma tena na akabadili mfumo na kuwaelekeza wachezaji wake kutoka na kushambulia . Bado Barcelona waliendelea kutawala mchezo kwenye kipindi hiki ila kiu ya Milan ya kujaribu kuchukua mipira miguuni mwa wachezaji wa Barcelona ilionekana wazi. Hakuna haja ya kuendelea kubaki nyuma ukiwa umefungwa katika hali ya kawaida.

5.Kuanzisha mchezo kutoka nyuma .

Kama ilivyoonekana kwenye bao la mapema la Pato , Milan wangefaidika kwa kutumia wachezaji wenye kasi dhidi ya wa Barcelona ambao hawana kasi hasa mabeki wa kati.

Kikosi cha Guardiola kwa kawaida huwa kinacheza kwa kukaba kuanzia sehemu ya juu ya uwanja lakini Sergio Busquets na Mascherano walionekana kuwa wangelazimika kurudi nyuma kulinda lango lao. Hivyo tangu mwanzoni mwa kipindi cha pili ilionekana wazi kuwa Christian Abbiati , Nesta na Thiago Silva walikuwa wakianzisha mipira kuanzia langoni mwao na si kupiga mipira mirefu ili kuwatamanisha wachezaji watatu wa mbele wa Barca wafuate mipira toka kwao (kina Nesta) ili kutengeneza nafasi nyuma yao.

6 .Mabao ya wazi.

Milan walikuwa na vyanzo viwili vya wazi vya mabao(A) Kasi kupitia katikati na (b)mipira iliyokufa. Hivi vyote viwili vilifanya kazi kwani bao la kwanza Milan walifunga kwa kutumia kasi ya Pato na bao la pili lilifungwa kupitia kona .

Kilichoenda vibaya kwa Milan.

1.Kutoa faulo nyingi .

Timu yoyote inayomtumia Mark Van Bommel kwenye sehemu ya kiungo wa kukaba siku zote lazima itagawa faulo nyingi,wachezaji wa Milan walikuwa wanajitupa kupita kiasi wakidhani kuwa kucheza rafu ni mojawapo ya njia za kuwapunguza kasi Barcelona.Alesandro Nesta alicheza rafu za akili tofauti na wenzie hasa pale ambapo lango la Milan lilipokuwa hatarini lakini viungo waliokuwa mbele yake hawakufuata mfano wake , walikuwa wanacheza rafu zisizo na msingi na kiranja katika hilo alikuwa Mark Van Bommel na ndio maana alipewa kadi ya njano mapema kwennye dakika ya 18. Unapocheza dhidi ya Barcelona siku zote uko hatarini kupata kadi, sasa unapopata kadi ya njano kwenye dakika ya 18 halafu bado una muda mrefu wa kukimbizana na Xavi, Iniesta na Messi unategemea nini kama si kadi nyekundu. Hili liliigharimu Milan kwani baada ya kupewa kadi Van Bommel hakufanya ‘tackling’ nyingine yoyote kwa kuhofia kuonyeshwa kadi nyingine na hili liliidhuru timu yake.

2.Kuruhusu mashuti mengi.

Moja ya sifa nyingi za Xavi kama mchezaji si upigaji wa mashuti ya mbali, hizo ni sifa za kina Lampard na Steven Gerard, lakini cha ajabu ni kwamba Xavi alipiga mashuti matatu ya mbali kwenye mchezo huu, hii ni kwa sababu kulikuwa na nafasi ya kufanya hivyo ambayo ilitengenezwa na viungo wa Milan .

3.Hakukuwa na pasi za mwisho za uhakika(hasa pasi za kupitia katikati ya mabeki)

Barcelona walikuwa wadhaifu kwenye safu ya ulinzi hasa kwenye mashambulizi ya moja kwa moja lakini Milan hawakuwa na ujanja wa kupenyeza mipira katikati ya mabeki kwa kuwa wachezaji wa mbele hawakuwa wamejipanga vyema kufanya hivyo. Hakuna aliyejua jukumu alilopewa Antonia Cassano kwenye mchezo huu.Cassano alikuwa akicheza kama mshambuliaji anayeshuka mpaka chini , sawa lakini mchezaji huyu anapaswa kufanya nini au ana jukumu gani la kutimiza hasa pale ambapo timu yake haina mpira .Alichotakiwa kufanya Cassano ni kurudi ndani zaidi au kusogea pembeni kumvuta Mascherano atoke kwenye eneo lake na kuanzisha mashambulizi ya ghafla. Pengine Urby Emmanuelson angeweza kupangwa tangu mwanzoni kwa kuwa ana kasi na angeweza kuyapa mashambulizi ya Milan mlengo tofauti kidogo akitokea pembeni ya uwanja, hapa Barca wangejaribiwa zaidi kutokana na kukosa kasi kwenye timu yao.

4 .Uchovu

Cassano , Pato na Seerdorf mwisho wa siku walichoka na upande pekee wa Milan ambao haukuwa na wachezaji waliochoka ulikuwa upande wa kulia na ni kwa sababu Antonio Nocerini na Ignazio Abate walikuwa na uwezo wa kukimbizana na Barca na hata bao la kusawazisha kwa Milan lilipatikana baada ya ubishi wa Nocerino ambaye alilazimisha kona iliyozaa bao.

Thursday, September 15, 2011

BREAKING NEWS: MWENYEKITI WA TEFA AVULIWA URAIA WA TANZANIA.




Taarifa nilizozipata hivi punde Mwenyekiti wa chama cha soka Manispaa ya Temeke jijini Dsm, Bwana PETER STEPHEN MHINZI ametenguliwa uraia wake wa Tanzania baada ya uchunguzi wa kina kubaini kuwa wazazi wake hawakuwa Watanzania ingawa yeye binafsi alizaliwa nchini Tanzania.


kwa mujibu wa kifungu cha 5(2) (a) cha sheria ya uraia No. 6,1995.










HATIMAYE YANGA YAPATA USHINDI WA KWANZA WA MABAO 2-1...

Taarifa kutoka Uwanja wa Azam Rashidi Gumbo ameipatia Yanga bao la pili na la ushindi mnamo dk ya 63.
Huu ulikuwa ni mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Davis Mwape aliipatia Yanga bao la kuongoza dakika ya 35 kabla ya Lyon kusawazisha kupitia kwa Hamis Shengo kupitia mkwaju wa adhabu ndogo.
hivyo basi Yanga imefanikiwa kupata ushindi wa kwanza wa msimu mabao 2-1 dhidi ya African Lyon.



NYAKATI TANO ZILIMJENGA SAMUEL ETO'O



Wakati nyota wa soka la Cameroon Samuel Eto’o Fils akianza hatua nyingine kwenye safari yake ndefu ya maisha yake ya soka hebu tutazame nyuma kwenye matukio mbalimbali ambayo yameliweka soka lake kwenye ramani.

Etoo hivi karibuni alikamilisha usajili wake toka Inter Milan kwenda kwenye klabu ya Urusi Anzhi Makhachkala .Thamani ya Ada ya uhamisho haijatajwa rasmi ila inaaminika kuwa kwenye maeneo ya Euro Milioni 25 au 28 , huku mshambuliaji huyo akisaini mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo ya Urusi.

Mshambuliaji huyu alisajiliwa Inter Milan mwaka 2009 kama sehemu ya uhamisho wa Zlatan Ibrahimovic toka Inter kwenda Barcelona alikotoka Etoo na huko alifanya vizuri ambako alitwaa ubingwa wa Ulaya , Serie A na kombe la Italia. Alikuwa mfungaji bora kwa Inter msimu uliopita ambapo alifunga jumla ya mabao 37 kwenye michuano yote na aliibeba klabu hiyo kutwaa Kombe la italia.

Maisha ya soka la Etoo yamedumu kwa karibu miaka 15 ambapo amefanikiwa kutwaa mataji mbalimbali akiwa na vilabu na timu yake ya taifa pamoja na tuzo mbalimbali binafsi katika muda wote huo.

Wakati Eto’o akianza kuzoea maisha mapya huko Urusi tunatazama nyakati tano bora katika maisha ya soka ya Eto’o .

UBINGWA WA KOMBE LA MATAIFA IN 2000

Etoo aliingia kwenye soka la kimataifa akiwa na timu yake ya taifa ya Cameroon mwaka 2000 ambapo alitoa mchango mkubwa kwa timu yake ya taifa ya Cameroon The Indomitable Lions .

Cameroon ilizitoa Algeria na Tunisia kuelekea kwenye fainali ambako ilicheza na mahasimu wao wa miaka yote Nigeria . Cameroon iliwafunga Nigeria kwa penati baada ya sare ya 2-2 kwenye dakika 90 na muda wa nyongeza . Etoo hakupiga penati lakini alifunga kwenye hatua za robo fainali , nusu fainali na kwenye fainali pia ambapo alimaliza michuano hiyo akiwa na jumla ya mabao manne akiwa nyuma ya mfungaji Bora Shaun Bartlett kwa bao moja.

Etoo alikuwa na umri wa miaka 18 wakati huo na juhudi zake zilimpa tuzo ya mchezaji bora kijana na Cameroon yote ilitambua kuwa shujaa mpya amepatikana.

MATAJI MATATU AKIWA NA BARCELONA 2008/09.

Msimu wa mwaka 2008/09 ulikuwa wa aina yake kwa Etoo. Akiwa na timu yake ya Barcelona Eto’o aliisaidia kutwaa mataji matatu La Liga , Copa Del Rey na lile la ligi ya mabingwa .

Mchango wa Etoo ulikuwa mkubwa pengine kuliko mtu yoyote na mnamo Oktoba 25, Eto’o alifunga hat-trick ya haraka kwenye historia ya klabu ya Barcelona baada ya kufunga mabao matatu ndani ya dakika 23 katika mchezo dhidi ya Almeria . Etoo pia alifunga mabao manne kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo dhidi Real Valladolid siku chache zilizofuata.

Etoo alifunga mabao 30 kwenye La Liga na alitoa pasi nne za magoli kwa wachezaji wengine , mabao yake hayo yaliisaidia Barca kutwaa ubingwa wa La Liga huku mabao yake manne kwenye Ligi ya Mabingwa ya ulaya yakiisaidia klabu yake kutwaa taji hilo .

MATAJI 3 NA INTER MILAN

Mwaka uliofuata baada ya kuipa taji Barca, Etoo alihamia Inter Milan na hakupoteza muda kwani msimu huo huo aliipa Inter mataji matatu ya Ligi ya mabingwa , Coppa Italia na Serie A.

Kutwaa mataji matatu mara mbili mfululizo ni rekodi ya kipekee kwa Etoo na juhudi zake kwenye msimu wa mwaka 2009/10ulikuwa ushahidi tosha wa kumpa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2010.

Eto’o alifunga mabao 12 na kutengeneza mengine matano huku bao lake lingine akifunga kwenye Coppa Italia na kwenye ligi ya mabingwa alifunga kwenye ligi ya mabingwa katika msimu ambao Inter waliweka na kuvunja rekodi nyingi.

UBINGWA WA KOMBE LA DUNIA LA KLABU

Mabingwa wa Ulaya na Italia Inter pia walitwaa ubingwa wa Dunia kwa vilabu baada ya kuwafunga mabingwa wa Afrika Tp Mazembe 3-0 kwenye fainali mwezi desemba mwaka 2010.

Inter walitwaa ubingwa huu kwa mabao ya kipindi cha kwanza yaliyofungwa na Goran Pandev, Samuel Etoo na Jonathan Biabiany.

Kwa mara nyingine Eto’o alikuwa na mchango mkubwa kwa timu yake akitengeneza bao la kwanza kabla ya kufunga la pili mwenyewe.

TUZO YA 4 MCHEZAJI BORA WA AFRIKA

Etoo alitwaa taji bora kwenye orodha ya mataji ya CAF kwa wachezaji binafsi baada ya kutunukiwa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2010, Hii ilikuwa mara ya nne kwa Etoo kutwaa tuzo hii baada ya kuitwaa kwenye miaka ya 2003,2004 na 2005.

Katika wachezaji waliokuwa kwenye orodha ya wachezaji wanaowania tuzo hii Etoo alikuwa anastahili kuliko wenzie Didier Drogba na Asamoh Gyan. Etoo aliifungia timu yake ya Taifa mabao mawili kwenye kombe la dunia lakini ilikuwa mchango wake kwenye klabu yake uliompa tuzo hii.

Taji la Serie A , Ligi ya mabingwa , Coppa Italia ,na lile la Super Coppa Italia yaliongeza idadi yake ya mataji pamoja na lile la kombe la dunia kwa vilabu.

WALE WANAOPENDA KU-BET MZIGO HUU HAPA..

Besiktas v Maccabi Tel Aviv - Home Win 2-1

FC Copenhagen v Vorskla - Home Win 2-0

PAOK Salonika v Tottenham - Draw 1-1

PSV v Legia Warsaw - Home Win 2-1

PSG v SV Salzburg - Home Win 2-0

Hapoel Tel Aviv v Rapid Bucharest - Home Win 2-1

Shamrock v Rubin Kazan - Away Win 1-2

Slovan Bratislava v Athletic Bilbao - Draw 1-1

Lazio v Vaslui - Home Win 2-0

Hannover 96 v Standard Liege - Home Win 2-1

FC Zurich v Sporting Lisbon - Draw 1-1

Dynamo Kiev v Stoke - Home Win 1-0

Anderlecht v AEK Athens - Home Win 2-1

Austria Vienna v Metalist Kharkiv - Draw 1-1

Maccabi Haifa v AEK Larnaca - Home Win 3-1

Wisla Krakow v Odense BK - Draw 1-1

SK Sturm Graz v Lokomotiv Moscow - Draw 1-1

Udinese v Rennes - Home Win 1-0

Birmingham v Braga - Home Win 2-1

Fulham v FC Twente - Home Win 2-0

Club Brugge v Maribor - Home Win 2-1

AZ v Malmo - Home Win 3-0

Steaua Bucharest v Schalke 04 - Draw 2-2

Atletico Madrid v Celtic - Draw 1-1

African Lyon v Yanga - Away Win 2-1

Zlatan Ibrahimovic analipwa Mshahara mkubwa Serie A.



Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic analipwa na klabu yake ya AC Milan kiasi cha Euro milioni tisa kwa mwaka.

Ibrahimovic raia wa Sweden anafuatiwa na kiungo wa Inter Milan Wesley Sneijder toka nchini Uholanzi anayepokea kitita cha Euro milioni sita.


Hii ndiyo orodha ya wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa kwenye Serie A.
1 Ibrahimovic AC Milan € 9,000,000
2 Sneijder Internazionale
€ 6,000,000
3 Buffon Juventus
€ 6,000,000
4 Totti Rome
€ 5,200,000
5 De Rossi Rome
€ 4,600,000
6 Flamini AC Milan
€ 4,500,000
7 Julius Caesar Inter
€ 4,500,000
8 Milito Inter
€ 4,500,000
9 Amauri Juventus
€ 4,000,000
10 Cambiasso Inter
€ 4,000,000
11 Maicon Inter
€ 4,000,000
12 Gattuso AC Milan
€ 4,000,000
13 Mexes AC Milan
€ 4,000,000
14 Duck AC Milan
€ 4,000,000
15 Robinho AC Milan
€ 4,000,000
16 Thiago Silva AC Milan
€ 4,000,000
17 Chivu Internazionale
€ 3,500,000
18 Forlan Internazionale
€ 3,500,000
19 Pike Internazionale
€ 3,500,000
20 Pirlo Juventus
€ 3,500,000
21 Chiellini Juventus
€ 3,500,000
22 Van Bommel AC Milan
€ 3,500,000
23 Zambrotta AC Milan
€ 3,500,000

DAY 2: Uefa Champions League Highlites!