Search This Blog

Friday, March 22, 2013

KAHAWA vs CHAI - KIPI KINYWAJI BORA KWA MWANAMICHEZO??



Sahau kuhusu Barcelona vs Real Madrid, hii ni kubwa kuliko. Je ni kinywaji gani unapaswa kabla na baada ya mechi kati ya chai na kahawa.

 KABLA YA MECHI?
Kahawa
Kaffeini inayopatikana kwenye kahawa itakupa nguvu zaidi kuelekea kwenye mech, lakini kuwa makini usizidishe. " content of coffee will power you up ahead of kick-off, but be careful not to overdose. “Kiasi kinachoshauriwa kunywa kisizidi 3mg ya kaffeine kwa kila kilo ya uzito wa mwili,” anaelezea Mayur Ranchordas, mtalaam wa lishe ya wanamichezo kwenye kutoka Sheffield Hallam University. Vikombe vidogo viwili vya kahawa ni tosha kwa kwa mwanamichezo wa kiume.

Muda wa Mapumziko?

Kahawa
Lakini muda huu inabidi uongeze vipande viwili vya keki. Utafiti wa Ranchordas na kusifiwa na jarida la madawa ya michezo la Uingereza umeonyesha kwamba kombinisheni sahihi ya kahawa na kabohaidretis inasaidia kuongeza nguvu na uwezo wa akili kufanya kazi vizuri.

Kwa kujilinda na baridi ?

Chai
Takwimu kutoka US National Academy of Sciences zinaonyesha kwamba kitu kiitwacho L-theanine kinachpatikana kwenye chai kinasaidia seli nyekundu za damu kufanya kazi vizuri mara tano zaidi zaidi ya wanywaji wa kahawa.

Lishe baada ya mechi?

Kahawa
“Baada ya mazoezi utataka kuongeza maji na ute uliopotea kwenye mazoezi,” anasema Ranchordas. Kuongeza kahawa kwenye lishe yako baada ya mazoezi kutakufanya urudi kwenye hali ya kawaida kwa haraka. Utafiti umeonyesha kwamba wanamichezo wanaoingiza kaffeine pamoja na kabohaidreti wanakuwa na asilimia 66 zaidi ya glycogen – inayotumika kama kilainishi cha misuli masaa manne baada ya mazoezi magumu.

FINAL SCORE

Kahawa 4 Chai 1: Matokeo yanaonyesha chai imeshindwa. Ingawa pia kaffeine inachukua kuanzia dk 30-60 kusambaa vizuri kwenye damu lakini inakaa kwenye mfumo wa mwili kwa masaa matatu mpaka manne, hivyo kuwa muangalifu.

Thursday, March 21, 2013

SEHEMU YA HOTUBA ILIYONIVUTIA SANA YA MHESHIMIWA RAISI DR JAKAYA MRISHO KIKWETE KWENYE UZINDUZI WA AZAM COMPLEX

MESSI ACHORA TATTOO YA MKONO WA MWANAE THIAGO KWENYE MGUU.







WAKATI KIKWETE AKIPONDA UONGOZI WA SIMBA NA YANGA MWANAE RIDHIWANI APEWA UONGOZI YANGA

 DAKIKA chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kuponda mfumo wa uongozi wa klabu kongwe chini zikiwemo Simba na Yanga, mtoto wake, Ridhiwani leo ametangazwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa kitega uchumi cha Yanga katika eneo la makutano ya Mitaa ya Mafia na Nyamwezi, Ilala jijini Dar es salaam.

Kikwete akiwa katika uzinduzi wa kituo cha michezo cha Azam Complex huko Mbande Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, alisema viongozi wengi wa klabu hizo wapo kwa maslahi yao binafsi na si kuzinufaisha klabu.

“Hawa Azam hawana gozigozi katika utawala tofauti na klabu kubwa za hapa nchini na mimi nawaambia Azam sasa ni timu kubwa na inazisumbua sana hizo mnazoziita timu kubwa,” alisema Kikwete na kuongeza;

“Leo hii ninyi mna kituo cha kukuza vijana, wenzenu Simba na Yanga hawana kitu kama hiki, wamekalia ukiritimba tu siku zote na ndiyo maana hawafanikiwi.”


Kikwete aliyasema hayo leo mchana huko Mbande Chamazi, lakini katikati ya jiji la Das es Salaam kwenye makutano ya mitaa ya Jangwani na Twiga yalipo makao makuu ya Yanga, Mwenyekiti wa timu hiyo, Yusuf Manji alikuwa akimtambulisha Ridhiwani Kikwete kuwa mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa kitega uchumi katika eneo la klabu lililopo makutano ya Mafia/Nyamwezi eneo la Ilala jijini Dar es salaam.

Manji alisema uteuzi wa Ridhiwani umezingatia uwezo wake kwa taaluma yake, na moyo alionao katika kujitolea katika kazi mbalimbali za klabu ya Yanga.

"Wote tunamfahamu Ridhiwani amekua ni mwanachama wa Yanga kwa muda mrefu, amekua akijitoa katika kazi mbalimbali za maendeleo ya klabu, hivyo tumeona ni vizuri kumpa fursa hiyo ili aweze kusaidia katika kuleta maendeleo ya klabu" alisema Manji

Katika kamati hiyo ambayo Ridhiwani ameteuliwa, amepewa fursa ya kuteua/kuchagua wajumbe atakaoshirikiana nao katika ujenzi wa kitega uchumi hicho, pia atakua na uwezo wa kuongeza wajumbe au kupunguza kulingana na mahitaji kwa kipindi hicho.

Mara baada ya kutambulishwa kwa wanachama na waandishi wa habari, Ridhiwani alisema anashukuru kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo na kuahidi kuwa atajitahidi kadri ya uwezo wake kuhakikisha ujenzi huo unafanikiwa.

"Nitakaa na kuangalia ni wajumbe gani ambao tutaweza kukaa pamoja na wajenzi (wakandarasi) ili kuweza kufanikiwa katika ujenzi wa kitega uchumi, kwani napenda eneo hilo liwe sehemu ambayo litasaidia katika uchumi wa klabu" alisema Ridhiwani



Ridhiwan
MASWALI TATA

Je, leo Kikwete amewaponda viongozi wa klabu kubwa nchini, na wakati huo huo mtoto wake anateuliwa kushika nafasi kubwa katika klabu, Ridhiwani ni mmoja kati ya viongozi waliopondwa?

Ridhiwani anaweza kumfanya baba yake ageuze au kupindua kauli yake aliyoitoa leo?

Je, maneno ya Kikwete yalihusiana na uteuzi wa Kikwete?

Au Kikwete alitamka bila kujua kama Ridhiwani amepewa uongozi Yanga?

Kazi kwenu!

MATUKIO MBALI MBALI KTK PICHA KWENYE UZINDUZI WA AZAM COMPLEX!



 MC wa shughuli alikuwa ni PJ wa Power Breakfast ya Clouds FM.
    Hafisa habari wa Azam FC Jaafar Maganga.
    Mimi pia nilikuepo na mwanangu TUPATUPA...
    Dr Jakaya Kikwete akipita kwenye Bwawa la kuogelea....


    Hapa anakata utepe kuifungua rasmi Azam Complex...

JE LIONEL MESSI ATAIVUNJA REKODI YA CRISTIANO RONALDO KUZIFUNGA TENAZOTE ZA LA LIGA

Leo Messi anaweza kuifikia rekodi ya Cristiano Ronaldo kwa kuwa mchezaji wa pili kuifunga kila kitu kwenye La Liga ikiwa ataweza kufunga goli kwenye mechi dhidi ya Celta Vigo

Pia atakuwa mchezaji wa kwanza kufunga kwenye 19 mfululizo kwenye ligi, maana nyingine kufunga timu zote pinzani.


Tangu Barça waliposhinda 4-2 dhidi ya Mallorca, November 11, Messi amefunga kwenye kila mchezo wa La Liga, mechi 18 mfululizo. Katika mechi ijayo dhidi ya Celta Vigo akifunga atakuwa ameweka rekodi ya kufunga kwenye mechi 19 mfululizo.

Celta Vigo huwa wanamsumbua Messi
Mara ya mwisho Messi kushindwa kufunga kwenye La Liga ilikuwa kwenye mechi dhidi ya Celta, ambayo ndio pekee ambayo iliweza kumzuia Messi kugusa nyavu zao msimu huu. Timu zote zilizobakia zinajua balaa la Baba Tiago.

KIKWETE AZIPONDA SIMBA, YANGA HUKU AKIIPA SHAVU KUBWA AZAM FC.


KLABU kubwa za soka nchini zikiwemo Simba na Yanga, zimetakiwa kuachana na ukiritimba katika uongozi ili ziweze kupata maendeleo na kuinua soka la Tanzania.

Rai hiyo imetolewa leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete wakati akizindua kituo cha michezo cha Azam Complex kilichopo Mbande Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Kikwete alisema kwa kujenga kituo hicho, Azam iliyoanzishwa mwaka 2004 imezishinda klabu kongwe zilizoanzishwa muda mrefu na hadi leo hii hazina viwanja vya mechi zake.

Azam Complex ipo chini ya timu ya soka ya Azam ambayo ni moja kati ya makampuni ya S. S Bakhresa, kampuni kubwa inayomiliki kampuni za utoaji huduma za usafiri na uzalishaji wa vyakula na vinywaji.

“Azam ni timu iliyoanzishwa mwaka 2004 tu, lakini leo hii ina mafanikio makubwa na kuwa mfano wa kuigwa kwa klabu nyingine. Siri kubwa ya mafanikio haya ni nia thabiti ya uongozi na watendaji wake.

“Hawa hawana gozigozi katika utawala tofauti na klabu kubwa za hapa nchini na mimi nawaambia Azam sasa ni timu kubwa na inazisumbua sana hizo mnazoziita timu kubwa,” alisema Kikwete.

Alisema uongozi wa Azam una nia ya kuendeleza soka la Tanzania ndiyo maana umeanzisha kituo hicho ambacho kitazalisha wachezaji wazuri watakaolisaidia taifa siku za usoni.

“Leo hii ninyi mna kituo cha kukuza vijana, wenzenu Simba na Yanga hawana kitu kama hiki, wamekalia ukiritimba tu siku zote na ndiyo maana hawafanikiwi,” alisema Kikwete.

Kabla ya kutoa hotuba yake, Kikwete alitembelea maeneo kadhaa ya kituo hicho ikiwemo viwanja vitatu vya soka ambavyo viwili kati yake havijakamilika, bwawa la kuogelea, hosteli za wachezaji na canteen ya kisasa.

APONDA UCHAWI KATIKA SOKA
Kikwete alitumia nafasi hiyo kuponda klabu zinazoendekeza ushirikina katika soka na kusema kwa kufanya hivyo kunarudisha nyuma maendeleo ya soka nchini.

“Mimi nashangaa sana eti hadi leo hii, timu haina mipango ya maana na viongozi wake wamekalia kuamini mambo ya uchawi tena wanatumia fedha nyingi kutekeleza hazima hiyo, hawa huwa hawafiki mbali na ni ujinga kuamini hivyo.

“Katika Karne hii, uchawi hauna nafasi kabisa zaidi ya mipango thabiti ya kuinua soka. Kama wanaamini uchawi unasaidia basi wawakusanye wachawi wote wa Tanzania halafu wawaingize uwanjani wacheze, tuone kama watafanikiwa.

“Kama uchawi ungekuwa na nguvu, basi Afrika tungechukua Kombe la Dunia tangu zamani na lisingeondoka hapa,” alisema Kikwete na kufanya umati kuangua kicheko.

AWATOLEA MACHO VIONGOZI WABABAISHAJI
Kikwete alisema viongozi wengi wa klabu wanaingia madarakani kwa ubabaishaji mkubwa huku wakitumia rushwa kwa wanachama wasio waaminifu na matokeo yake wanashindwa kupata mafanikio.

“Kila siku migogoro ni sehemu ya maisha ya klabu hizo mnazoziita kubwa. Hawapigi hatua, hawana mbinu za uongozi na wengi wao wapo katika uongozi ili wanufaike na siyo wainufaishe timu, hawa hawafai,” alisema Kikwete.

KIKWETE ‘ANAIPENDA’ ARSENAL
Katika hali ya kushangaza, mara kadhaa Kikwete alikuwa akitoa mifano ya soka la Ulaya na aliitaja sana Arsenal badala ya Barcelona hali iliyowafanya watu mbalimbali kuamini Kikwete ana mapenzi na timu hiyo.

“Tazama wenzenu timu za Ulaya kama Barcelona ilivyokuwa na mifano mizuri ya kuthamini soka la vijana, wale walimkuza (Cesc) Fabregas kisha Arsenal ikamchukua na baadaye akarudishwa Barcelona, hii inaonyesha Arsenal (badala ya Barcelona) ina mfumo mzuri wa kukuza vijana.

“Hiki kinachofanywa na Arsenal (akimaanisha Barcelona) aahh…. Nini Barcelona kinafaa kuigwa na timu zote na Azam imeonyesha nia ya kuiga hali hiyo. Barcelona walimsimamia (Lionel) Messi hadi akafikia mafanikio ya leo hii,” alisema Kikwete.

RAISI DR JAKAYA MRISHO KIKWETE AKIZINDUA RASMI KITUO CHA SOKA CHA AZAM COMPLEX.

Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete akikizindua rasmi kituo cha soka cha Azam Complex hii kilichopo maeneo ya Mbande,Chamazi. Pembeni yake ni Makamu Mwenyekiti wa AZAM FC ndugu Said Mohammed.
 Mheshimiwa Dr Jakaya M Kikwete akikata utepe kuashiria kukifungua rasmi kituo cha Azam Complex,kulia kwake ni Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dr Fenella Mukangara
   Mheshimiwa Raisi J.M. Kikwete akiwa kwenye Gym...

 Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya SSB na Mwenyekiti wa Azam FC Ndugu Abubacar Bakhressa akimkaribisha Mheshimiwa Raisi Jakaya Kikwete
 Kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Azam Fc ndugu Said Mohamed,Dr Fenella Mukangara,Ndugu Abubacar Bakhressa na mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Ndugu Sadick Mecky Sadick

BODI YA WADHAMINI YATAMBULISHWA RASMI

 






















Wajumbe wa Bodi ya wadhamini kutoka kushoto ni Francis Kifukwe, Captain George Mkuchika na Balozi Ami Mpungwe

























Uongozi wa klabu ya Yanga chini ya mwenyekiti wake Yusuf Manji juzi uliwatambulisha rasmi wajumbe wa Bodi ya Baraza la Wadhamiini ambao watafanya kazi zote ambazo zitahusiana na klabu ya Yanga (Mali na Ufilisi) kufuatiwa kupitishwa na wanachama katika mkutano mkuu.
Yanga ilifanya mkutano mkuu mwezi Januari 20, 2013 mkutano uliofanyika katika ukumbi wa bwalo la Polisi Oysterbay ambao wanachama wa klabu walilridhia kuwaongezea tena mda Mama Karume na Francis Kifukwe amabao awali walikua wamemaliza mda wao wa miaka miwili.
Katika mkutano huo wanachama waliridhia kwa mwenyekiti kuongeza idadi ya wajumbe wa bodi ya wadhamini kutoka wawili waliokuwepo na kufikia wajumbe saba, ambapo kwa sasa klabu itakua na wajumbe wanne na kamati ya utendaji itapata fursa ya kuongeza wengine watau ili kufikia idadi ya wajumbe saba.
Akiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya klabu ya Yanga, Manji amesema uteuzi huo wa bodi ya wadhamini umezingatia wasifu wa wajumbe hao ambao wamewahi kufanya kazi katika sekta mbali mbali ndani na nje ya nchi.
Klabu ya Yanga awali ilikua na wajumbe wawili wa Bodi ya wadhamini ambao ni Mama Fatma Karume na Injinia Francis Kifukwe.
Kwa sasa bodi ya wadhamini itakua na wajumbe wa wanne (4) ambao ni Mama Fatma Karume, Francis Kifukwe, na wajumbe wapya waliotambulishwa leo ni Balozi Ami Mpungwe na Kaptain George Mkuchika.
Akitoa wasifu wa wajumbe hao, Manji alisemaBalozi Amir Mpungwe amekua ni kiongozi wa serikali kwa nyadhifa mbali mbali kwa miaka kadhaa, amekua Balozi wa kwanza Tanzania nchini Afrika Kusini mara baada ya nchi hiyo kupata uhuru na kwa sasa anafanya shughuli zake binafsi.
Kaptain George Mkuchika ni waziri wa nchi ofisi ya waziri utawala bora pia amekua kiongozi wa serikali kwa nyadhifa mbalimbali na hata katika chama chake amekua kiongozi makini kwa muda mrefu.
Aidha kuhusu Mama Fatma Karume na Mzee Kifukwe mwenyekiti amesema wanafahamika kwa kazi zao walizozifnya kwa maendeleo ya klabu ya Yanga hali iliyopelekea mkutano mkuu wa wanachama kuwaongezea muda tena wa miaka miwili.
Mara baada ya kutambulishwa rasmi na kupewa katiba za Yanga mwenyekiti alitumia fursa hiyo kuwazungusha wajumbe kuona majengo na mali za klabu kabla ya kupiga picha ya pamoja. 

















Wajumbe wa Bodi ya wadhamini wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa klabu ya Yanga

Source: www.youngafricans.co.tz

SERIKALI IMERIDHIA MCHAKATO WA UCHAGUZI WA TFF UENDELEE KWA KATIBA IPI ?

 WAKATI Serikali na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakikubaliana mchakato wa uchaguzi wa TFF uendelee kwa sharti la kuhakikisha haki inatendeka kwa wagombea waliokatwa kufanyiwa mapitio ya mchakato wa kuwaondoa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kuna jambo halipo sawa.

Ikumbukwe kwamba, serikali ilisitisha uchaguzi huo baada ya kupokea malalamiko yaliyohusu utumikaji wa katiba mpya ya TFF ya mwaka 2012 ambayo ilipitishwa isivyo halali bila mkutano mkuu kukaa.

Serikali ilielekeza kutumika kwa katiba ya mwaka 2006 ambayo ilipitishwa na mkutano mkuu wa TFF, au mkutano mkuu ukutane kupitisha katiba ya 2012 ndipo mchakato wa uchaguzi uendelee.

Jana, wakati Rais wa TFF, Leodegar Tenga akitangaza kufikia makubaliano hayo yaliyofikiwa baada ya kikao cha pamoja kati ya TFF, uongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo chini ya Waziri Dk. Fenella Mukangara na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), HAKUWEKA wazi kwamba mchakato huu wa uchaguzi unaoendelea unafanyika kwa kutumia katiba ipi.

Tenga alienda mbele kwa kusema baada ya makubaliano hayo, TFF itaiandikia barua Fifa ambayo itasimamisha mchakato wa review ili iweze kutuma ujumbe wake kwa ajili ya kusikiliza malalamiko ya wagombea walioenguliwa.

KUNA NINI KATIKA KATIBA?
Kama serikali awali ilitoa maelekezo ya katiba ya mwaka 2012 kutotumika kwa kuwa ni batili, sasa kwa nini Tenga ameshindwa kuweka wazi kwamba uchaguzi huu unafanyika kwa katiba ipi?

Kama Fifa wanakuja kufanyia kazi malalamiko ya wagombea ambao hadi wanachinjwa katika uchaguzi huu, mchakato wake ulikuwa unafanyika chini ya katiba ya mwaka 2012, ina maana Fifa watafanya kazi kwa kutumia katiba ya mwaka 2012 ambayo serikali imeipinga.

Je, uhalali wa katiba ya mwaka 2012 umetoka wapi? Maana serikali ilipofanya mapitio ya kupitisha hadi kusajiliwa kwa katiba hiyo ya mwaka 2012, iligundua upungufu kiasi cha kumsimamisha kazi mtu aliyeipitisha.

Usafi wa katiba ya mwaka 2012 umetoka wapi? Ni nini kilizungumzwa zaidi katika kikao hicho na kuamua suala la katiba kuachwa hewani wakati serikali ilishatoa msisitizo wa kutoitambua katiba ya mwaka 2012?

MSISITIZO WA UCHAGUZI KABLA YA MEI 25

Tenga amesisitiza huku akiahidi kuwa uchaguzi wa TFF utafanyika kabla ya Mei 25 mwaka huu kama walivyokubaliana na Serikali, na kuwa haki si tu itatendeka bali ionekane imetendeka.

“Serikali imetuelekeza uchaguzi ufanyike kabla ya Mei 25. Tumewaambia kwetu huko ni mbali. Fifa wakija hata kesho wakituambia endeleeni sisi tuko tayari.

Hesabu zetu ziko tayari, makabrasha yote yako tayari yanasubiri mkutano tu. Labda itakuwa kutoa muda tu kwa wajumbe walioko mbali waweze kujiandaa, maana wajumbe huwezi kuwaita ghafla,” amesema.

Hapa inawezekana kweli Tenga ana nia thabiti ya kuhakikisha mkutano unafanyika kabla ya Mei 25, tatizo linakuja uchaguzi utafanyikaje bila ya maswali muhimu kujibiwa hasa kuhusu katiba?

MSIMAMO WA MTANDAO HUU
Tunaamini Tenga na TFF ni watu wanaojua kile wanachofanya katika uongozi wao, sasa ni muhimu kwao kuweka wazi kuhusu katiba itakayotumika katika uchaguzi huu japokuwa hadi kauli ya jana ya TFF ni wazi katiba ya mwaka 2012 ndiyo itakayotumika.

Kama katiba itakayotumika ni ya 2012, tuelezwe sababu za kufanyika hivyo, nayo serikali itueleze imekubali vipi kuendelea na uchaguzi kwa kutumia katiba ambayo awali iliikataa.

Tunaamini uchaguzi wa TFF utafanyika kwa haki na anayestahili ndiye atakayeshinda lakini ni muhimu kwenda huko huku mambo yaliyotatiza hapo awali yakashughulikiwa mapema ili kutoweka mkanganyiko hapo baadaye.

KUTOKA MAKTABA: TANZANIA VS CAMEROON 1:0

ANTONIO CASSANO AMPA MWANAE JINA LA MESSI KUONYESHA NI NAMNA GANI ANAMKUBALI LIONEL

Mchezaji wa soka wa kiitaliano Antonio Cassano amesema anaamini muargentina Lionel Messi ndio mwanasoka bora wa muda wote, na ndio maana aliweza kumshawishi mkewe kumpa mtoto wao jina mwanasoka huyo bora wa dunia kwa mara nne. 

Mshambuliaji huyo wa  amesema ni mapenzi yake kwa Messi ndio yaliyomfanya ampe mwanae jina lake. 

"Nimempa jina la Lionel kwa sababu mie ni shabiki mkubwa wa huyu mchezaji bora wa soka wa muda wote. Mke wangu hakutaka, lakini nilifanikiwa kumshawishi. Kwa maoni yangu, Messi ni mchezaji muhimu sana kwenye historia ya mchezo huu, nampenda sana anvyocheza soka."

Lionel Cassano, alizaliwa siku ya Jumatatu iliyopita, ni mtoto wa pili wa Cassano baada ya mtoto wake wa kwanza Christopher. 

PICHA YA SIKU: SERGIO RAMOS NA PICHA YA FERNANDO TORRES


Wednesday, March 20, 2013

MJADALA: ZIDANE, INIESTA NANI ZAIDI?


ZINEDINE Zidane ni mmoja wa wachezaji wenye kipaji cha aina yake waliowahi kucheza soka akiwa na Ronaldo De Lima.

Akiwa na umri mdogo, Zidane alikuwa na uwezo mkubwa wa kuongoza mashambulizi kupitia katikati ya uwanja huku akitumia uwezo binafsi na nguvu ipasavyo.

Wakati huo alikuwa akichezea klabu ya Bordeux ya Ufaransa kabla hajasajiliwa na Juventus ya Italia kwa ada ya uhamisho ya thamani ya pauni milioni tatu ambazo ni zaidi ya Sh. 7.5 Bilioni.

Akiwa na Juventus, Zidane hakuanza maisha vyema na kulikuwa na watu wengi ambao walikuwa na walakini na uwezo wake.

Kadri msimu wa mwaka 1996/97 ulivyozidi kwenda, Zidane taratibu alianza kuonekana muhimu na alikuwa na mchango mkubwa kwa kikosi kilichofika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambacho kwa bahati mbaya kilifungwa na Borussia Dortmund ya Ujerumani.

Kipigo hicho kilipokewa kwa mshangao na wengi hasa baada ya Zidane maarufu kama Zizzou kukabwa ‘man to man’ kwenye mchezo huo na kiungo wa Dortmund, Paul Lambert ambaye hii leo ni kocha wa Aston Villa.

                
Msimu uliofuata, Juventus ilifungwa katika fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid kwa bao la Predrag Mijatovic. Kikosi hiki cha Juventus kilichokuwa na Didier Deschamps, Edgar Davids, Alesandro Del Piero na Zizzou kilikuwa kinaonekana kama kitatawala soka la Ulaya kwa muda mrefu ujao.


Kwenye fainali za Kombe la Dunia 1998, Zidane alilazimika kungoja hadi mchezo wa fainali kisha kufunga mabao yake ya kwanza ya michuano hiyo. Mabao hayo ndiyo yaliyoipa Ufaransa ubingwa wa Dunia kwa mara ya kwanza, na hapa hakukuwa na ubishi kuwa, Zidane alikuwa mchezaji bora mbele ya kizazi cha dhahabu cha wachezaji wa Les Bleus.


Miaka miwili baadaye, Ufaransa ilitwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Ulaya licha ya Zidane kutofunga bao hata moja. Hakuna ubishi kuhusu mchango alioutoa katika mafanikio hayo ya Ufaransa mwaka 2000.



MCHEZAJI GHALI KULIKO WOTE DUNIANI

 

Mwaka 2001 Zidane aliuzwa kwenda klabu ya Real Madrid kwa dau lililoweka rekodi ya Dunia kwa wakati huo la pauni milioni 42 ambazo ni zaidi ya Sh. 105 Bilioni.

Msimu wake wa kwanza akiwa na Real Madrid, ulikuwa mgumu na kulikuwa na taarifa kuwa, presha ya matarajio makubwa yaliyokuwepo mabegani mwake kutokana na fedha nyingi zilizotumika kumsajili ilikuwa kubwa kwake.

Hata hivyo, Real Madrid ilifika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2002 na kwenye fainali yake ya tatu, Zidane alifanikiwa kutimiza ndoto zake.


Kwenye fainali hiyo, Zidane alifunga bao ambalo linaweza kuwa bora kwa miaka yote ya michuano hiyo.

Zidane alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Dunia mwaka 2003, ikiwa mara yake ya tatu kupewa tuzo hiyo. Kabla ya hapo aliwahi kutwaa tuzo hiyo kwenye miaka ya 1998 na 2000.


Uwezo wake wa kubadili matokeo ya mechi ngumu uwanjani, ulimfanya adhihirishe ubora wake mbele ya kila mtu. Kwenye klabu yake, kulikuwa na ‘issue’ za mradi wa Galactico ambazo ziliathiri mafanikio ya klabu.

Ulikuwa wakati mgumu kwa Zidane kwa kuwa hata timu yake ya taifa ilikuwa na matatizo kwenye michuano mikubwa. Majeraha aliyopata mwaka 2002 yalishuhudia timu yake ikitemeshwa ubingwa wa Dunia kwenye hatua ya makundi.Ufaransa ilishindwa kupata hata bao moja.

Timu zote mbili za Zidane, kwa maana ya Ufaransa na Real Madrid zilikosa ‘balance’ na hii ilimnyima mafanikio japo aliyopata kwenye tuzo binafsi mojawapo ikiwa ya kuteuliwa kuwa mmoja wa wachezaji 50 bora wa miaka yote.



Mwaka 2006 ulikuwa wa aina yake kwenye historia ya mchezo wa soka. Mwaka 2003 Barcelona walimnunua Ronaldinho Gaucho wakati Real Madrid walimnunua David Beckham. Wachezaji hawa wawili walikuwa gumzo na walionyesha mwelekeo wa mchezo wa soka kwa kipindi hicho.


Beckham alionekana kuwa mtu aliyejengwa kwenye miaka ya 90 na Gaucho akionekana wa miaka ijayo. Wakati Madrid na mradi wao wa Galactico wakionekana ‘wana-flop’, Barcelona walikuwa wakicheza soka safi na la kuvutia.

Mwaka 2006 walitwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya wakiifunga Arsenal mabao 2-1. Mtindo wao wa soka lao la kushambulia kwa pasi nyingi huku ukiongozwa na Samuel Eto’o na Gaucho, ulivutia machoni kwa watazamaji. Haya yalikuwa mapinduzi ya soka.

Mwaka huo pia kulikuwa na Kombe la Dunia huko Ujerumani. Zidane aliamua kurejea kwenye timu ya taifa na kuiongoza Ufaransa kwa mara ya mwisho. Mkataba wake na Real Madrid uliisha msimu wa 2005/06 na katika michuano ya Kombe la Dunia 2006, ndipo alipocheza soka kwa mara ya mwisho.


MCHEZO ULIOLETA MABADILIKO.


Kama ndoto, Zidane aliiifikisha Ufaransa hadi fainali ya Kombe la Dunia 2006. Mechi ambayo itakumbukwa na wengi ilikuwa robo fainali dhidi ya Brazil, ambapo ilikuwa vita yake na Ronaldinho Gaucho.

Ilikuwa inaonekana kama imepangwa kwa Ufaransa na Zidane kutwaa ubingwa wa Dunia na kwenye fainali alifunga bao la mkwaju wa penati ambalo lilimfanya kuwa mmoja wa wachezaji wanne pekee ambao wamewahi kufunga kwenye fainali mbili tofauti.


Hata mchezo huo ulipomalizika katika muda wa kawaida, ulilazimika kuamuliwa kwa muda wa nyongeza ambako Zidane almanusra afunge bao kwa kichwa lakini mpira aliopiga uligonga mwamba. 


Kwa mshangao wa wengi, Zidane alionyeshwa kadi nyekundu zikiwa zimebaki dakika kumi fainali ifikie hatua ya matuta baada ya kumpiga kichwa beki wa Italia, Marco Materazzi.

Ufaransa iliishia kufungwa kwa mikwaju ya penalti na wengi walifikiri kuwa endapo Zidane asingetolewa, Ufaransa ingekuwa na nafasi ya kutwaa ubingwa wao wa pili.

Fainali hiyo ilikuwa siku ambayo mabadiliko yalifanyika ambapo ‘master’ wa soka kwa muongo uliopita yaani Zidane, alikuwa anamaliza zama zake na kijana ambaye anakuja kurithi nafasi yake alikuwa anaanza taratibu.


KIUNGO MCHEZESHAJI BORA


Mwaka 2006 kundi la watu liliamua kuanzisha tuzo maalum kwa viungo wachezeshaji, tuzo ambayo ilipewa jina la WORLD PLAYMAKER AWARD yaani kiungo mchezeshaji bora, na tuzo ya kwanza kwa mwaka huo ilikwenda kwa Zidane.

Ilikuwa njia nzuri ya kumuenzi kiungo mchezeshaji bora wa kizazi cha hivi karibuni. Kaka alishinda mwaka uliofuatia na kwa upande wake alikuwa kama Zidane kwa njia nyingi.

Mwaka 2008, kiungo mchezeshaji wa aina mpya aliibuka. Aliwahi kuwepo tangu awali, ila kwa mwaka huo alianza kuchukua nafasi yake kama mtu muhimu kwenye timu alizochezea, alianza kutawala mechi alizocheza katika njia ambayo ilisababisha ushindi kwa timu yake.


Mashabiki walianza kuona kile ambacho anafanya akiwa uwanjani, jinsi alivyokuwa akiwaongoza wenzake uwanjani. Xavi Hernandez ndiye kiungo mchezeshaji anayezungumziwa.

Mwaka 2006 pia ulikuwa mwaka ambao Barcelona walianza kutambulika kama timu ya kuogopwa Ulaya, na mwaka 2008 timu ya taifa ya Hispania kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya, ilianza rasmi safari yake kuelekea mafanikio ya kiwango cha juu.

Mchezo wa soka ambao ulikuwa ukitegemea zaidi nguvu katika miaka iliyopita ulianza kubadilika. Barcelona na Hispania zikiwa na wachezaji wadogo kimaumbo lakini wenye uwezo mkubwa kimbinu na kiuwezo kama Xavi Hernandez, Andres Iniesta na Lionel Messi zilibadilisha jinsi soka la Ulaya lilivyochezwa na wachezaji hawa wakiibuka kama wachezeshaji wapya kwenye soka.

Xavi Hernandez alishinda tuzo ya kiungo mchezeshaji bora kwa miaka minne mfululizo kuanzia mwaka 2008 mpaka 2011. Alistahili tuzo hiyo na alistahili tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya mwaka 2008.


Xavi aliziongoza Barcelona na Hispania kupata mafanikio kwa miaka minne akitwaa mataji karibu yote kwenye soka la klabu na timu ya taifa. Xavi alikuwa kama funguo iliyofanya wenzie wacheze vizuri.
     

 
Mwaka 2012, tuzo ya kiungo mchezeshaji bora ilihamia kwa mwenzie Andres Iniesta. Michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya 2012 ilimshuhudia Xavi akitwaa tuzo ya mchezaji bora na alimaliza kwenye nafasi ya tatu nyuma ya Cristiano Ronaldo na Messi kwenye tuzo za Ballon D’or.

Hatimaye Iniesta alitambuliwa kama mmoja wa wachezaji bora. Miaka kumi ikiwa imepita tangu Zidane alipotwaa ubingwa Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Real Madrid pamoja na tuzo ya mchezaji bora wa dunia, kiungo mchezeshaji wa aina mpya alichukua mikoba ya Zidane akiwa anacheza kwa staili tofauti na Zidane lakini kwa ubora, kiwango na matokeo yale yale .



KIUNGO MCHEZESHAJI ALIYEKAMILIKA


Andres Iniesta alianzia soka lake akiwa kwenye Academy ya La Massia inayomilikiwa na Barcelona. Uwezo wake wa kucheza kwenye nafasi tofauti, kujituma, na umuhimu kwenye mchezo, ulimfanya achukua nafasi kwenye kikosi cha kwanza akiwa na umri wa miaka 18 na alianza kucheza mechi mfululizo kwenye msimu wa mwaka 2004/05.

Akiwa kama mchezaji mchanga, Iniesta alianza kufanya mazoezi akiwa na kikosi cha kwanza na Pep Guardiola (kocha wa zamani wa Barcelona wakati akiwa bado mchezaji) alimwambia Xavi kuwa, yeye (Xavi) angemfanya Guardiola astaafu lakini Iniesta atawafanya wote wawili yaani Xavi na Pep wastaafu.


Pep Guardiola na Andres Iniesta

Guardiola aliona mbali na hakukosea kwa kauli aliyoitoa, Iniesta hakuwa bora kwenye pasi pekee bali alikuwa mzuri kwenye ukokotaji wa mpira, alikuwa na uwezo mkubwa wa kucheza maeneo tofauti ya uwanja na alikuwa na uwezo mkubwa wa kufunga mabao na kutoa pasi muhimu.


Ilikuwa chini ya Guardiola ambapo Iniesta aliuteka ulimwengu. Guardiola alimtengeneza Iniesta na kumfanya kuwa mchezaji muhimu kwa Barcelona na Hispania na kubwa alilofanya Guardiola ni kumfanya Iniesta ambaye kwa kawaida ni mtu mkimya, kuwa kiongozi kwenye timu yake.


Chini ya nahodha huyu wa zamani wa Barcelona, soka la Iniesta lilifikia kiwango cha juu kupita hata Xavi na Guardiola kama ilivyokuwa kauli ya Guardiola. Alikuwa kiungo mchezeshaji aliyekamilika na hadi sasa ameingia kwenye orodha ya wachezaji bora waliowahi kucheza Barcelona.


MFUNGAJI WA MABAO MUHIMU

Iniesta siyo mfungaji wa mabao mengi, lakini ni mfungaji wa mabao mazuri na muhimu kwa timu yake kama Zidane. Iniesta alikuwa akifunga kwenye mechi muhimu na kubwa.

Moja ya mabao ambayo yatakumbukwa na wengi ni bao alilowafunga Chelsea mwaka 2009 kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ulikuwa mpira wa mwisho kwenye mechi hiyo na ulikuwa mpira ambao Iniesta alifunga bao lililoivusha Barcelona hadi fainali.


Kwenye Kombe la Dunia 2010, Iniesta alifunga bao muhimu kwenye historia ya soka la Hispania. Huku ubao wa matokeo ukisomeka 0-0 wakati wa fainali hiyo dhidi ya Uholanzi, mpira ulimfikia Iniesta upande wa kulia wa eneo la 18, halikuwa bao kama la Zidane kwenye fainali ya mwaka 2002 wakati Real Madrid walipocheza na Bayer Leverkusen, lakini umuhimu wake ulikuwa ule ule.

Zidane alitwaa Kombe la Dunia na ubingwa wa Ulaya akiwa na Ufaransa, lakini hakuweza kutwaa mataji matatu mfululizo na hakuna yeyote aliyewahi kufanya hivyo kabla.


Hispania waliweka historia hiyo na Iniesta alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya 2012. Aliiongoza timu yake akiwa ndani ya uwanja kwa uwezo wake na miaka minne baada ya Xavi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya 2008, Iniesta alitimiza utabiri wa Guardiola.


 

Kabla ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2011, Kocha wa Manchester United, Sir. Alex Ferguson alisema kuwa, kwake Messi si mchezaji anayemuogopa, anamuogopa zaidi Iniesta kwani ndiye hasa mwenye funguo za Barcelona kwa jinsi anavyotafuta upenyo wa kupitisha mipira kwa wenzake na mabao yake muhimu.


Vicente Del Bosque ambaye aliwahi kufanya kazi na Zidane kwenye klabu ya Real Madrid, alimtaja Iniesta kama mchezaji aliyekamilika kuliko wote aliowahi kuwaona.

Na mchezaji mwingine, Samuel Eto’o alimtaja Iniesta kama mchezaji bora duniani kwani kila awapo uwanjani huwa anatengeneza maajabu.

Hakuna ubishi kuwa Iniesta amekuwa akibadilika kwenye nafasi ya kiungo mchezeshaji bora kuendana na mchezo wa soka kwa zama za sasa.

Akiwa kwenye mfumo wa Barcelona huku akicheza soka kuendana na umbo lake dogo, Iniesta alijifunza kumiliki mpira na kuuelewa mchezo kwa jinsi anavyotengeneza ‘movement’ zake, mbinu na hata maamuzi ambayo anayafanya, kitu kinachofanya soka kuonekana rahisi kwake. 

n

HUU NDIO UNDANI YA MARIDHIANO YA TFF NA SERIKALI KUHUSU UCHAGUZI WA TFF

HATIMAYE Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, zimekubaliana ujumbe kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kufika nchini muda wowote kuanzia sasa na kufanya mapitio upya (review) kwa wagombea walioenguliwa katika mbio za uchaguzi wa TFF.
Rais wa TFF, Leodegar Tenga, leo hii amesema kimsingi wamekubaliana na wizara baada ya kikao cha jana kilichowaushisha Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fennela Mukangara, naibu wake, Amos Makalla, Tenga na viongozi wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), kwamba Fifa waje kufanya review halafu uchaguzi uendelee.
“Tumeangalia mambo mengi ya msingi kwa mustakabali wa mpira wa miguu Tanzania, tuna  heshima kubwa ya uongozi bora katika soka duniani. Hivyo tusingependa sifa hii ipotee kienyeji, ndiyo maana TFF, wizara na BMT tulikutana na kukubaliana kwamba, Fifa waje kufanya review ya kile kilichotokea halafu majibu yakipatikana tuendelee na uchaguzi,” amesema Tenga.
 Tenga amesema, wamefikia uamuzi kwa kuwafikiria pia Watanzania wapenda michezo na hata wagombea ambao wana haki ya kupigiwa kura huku wakiwa hawahusiki na hiki kinachoendelea sasa.
“Kuna watu hawahusiki na jambo hili kwa namna yoyote ile, sasa hawa tumewafikirai sana na tumeamua tuwape haki yao haraka iwezekanavyo. Nina imani nchi itabaki kuwa salama katika soka na upepo huu utapita,” amesema Tenga.
Awali Tenga alikuwa ameridhia kufanyika kwa review za mapingamizi ya wagombea mbalimbali wa TFF, lakini ushauri wake huo ulitupwa mbali na Kamati Huru ya Uchaguzi ya TFF na ile ya Rufaa. Baada ya hapo, ndipo serikali ikaiagiza TFF kufuata katiba ya mwaka 2008 baada ya kupokea malalamiko ya baadhi ya wagombea walioenguliwa.
Baadhi ya wagombea waliochinjwa katika uchaguzi huo ni Jamal Malinzi anayewania nafasi ya rais, Michael Wambura anayewania nafasi ya makamu wa rais ma wengineo.

TENGA AKATAA KUZUNGUMZIA KATIBA

Katika hali ya kushangaza, Tenga alikataa kujibu maswali ya waandishi wa habari yaliyokuwa yakihoji kuhusu katiba itakayotumika katika uchaguzi huo baada ya awali serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, kuigiza TFF kutumia katiba ya mwaka 2008 na kuiacha ile ya 2012 inayoelezwa kupitishwa isivyo halali.
“Jamani swali kuhusu katiba sitalijibu hapa, hapa tunazungumzia uchaguzi na mambo mengine yahusuyo,” amesema Tenga na hata aliposisitizwa kuhusu umuhimu wa swali hilo, alijibu: “Hapa si mahala pake jamani.”

SERIKALI YAZIDI KUIKOMALIA TFF

Mwenyekiti wa BMT, Dioniz Malinzi alisisitiza kwamba, Fifa watafika nchini na kufanya review yao kisha wao kama wasimamizi wa serikali wataipitia ripoti ya kazi hiyo kisha kuitolea maamuzi zaidi.
“Tumekubaliana hapa kwamba Fifa waje kufanya review, hawa mabwana wakimaliza kazi yao sisi tutaiangalia na kutazama kama haki imetendeka halafu ndipo tutaruhusu taratibu za uchaguzi kuendelea,” amesema Malinzi.
Malinzi alisema, kimsingi kikao chao na wizara na TFF kilikuwa cha amani na ana uhakika mambo yataenda vizuri na kila mmoja atapata haki yake ipasavyo.
FIFA WANAKUJA, UCHAGUZI SI ZAIDI YA MEI 25

Tenga baada ya maafikiano hayo, TFF itaiandikia Fifa ambao ndiyo wanaosimamisha mchakato huo ili watume wajumbe wake kwa ajili ya kusikiliza malalamiko ya wagombea walioenguliwa.
Tenga ambaye ameishukuru Serikali kwa kuruhusu mchakato huo uendelee, pia ameahidi kuwa uchaguzi wa TFF utafanyika kabla ya Mei 25 mwaka huu kama walivyokubaliana na Serikali, na kuwa haki si tu itatendeka bali ionekane imetendeka.
“Serikali imetuelekeza uchaguzi ufanyike kabla ya Mei 25. Tumewaambia kwetu huko ni mbali. Fifa wakija hata kesho wakituambia endeleeni sisi tuko tayari. Hesabu zetu ziko tayari, makabrasha yote yako tayari yanasubiri mkutano tu. Labda itakuwa kutoa muda tu kwa wajumbe walioko mbali waweze kujiandaa, maana wajumbe huwezi kuwaita ghafla,” amesema Tenga.
Amesisitiza kuwa TFF ilishapanga tarehe ya uchaguzi, lakini ukasimamishwa na Fifa baada ya baadhi ya walioenguliwa kulalamika huko. Hivyo maneno kuwa TFF hawataki uchaguzi kwa sababu wanataka kuendelea kubaki madarakani haya maana hata kidogo.

WAGOMBEA KUHOJIWA NA FIFA NA KAMATI YA RUFAA

Tenga amewataka wagombea wote waliofika kwenye Kamati ya Rufani ya Uchaguzi na wakaendelea kujiandaa vizuri, kwani Fifa watakapofika watawasikiliza wao na vyombo vilivyowaengua.
Pia amesema TFF ina heshimu Serikali na itaendelea kufanya hivyo, lakini vilevile lazima iheshimu FIFA sababu iko kwenye mpira wa miguu, na FIFA ndiyo wasimamizi wa mchezo huo duniani. 
Amewakumbusha wanachama wa TFF, hasa wajumbe wa Mkutano Mkuu kufahamu kuwa TFF ina katiba, lakini ni lazima pia wafahamu kwanini kuna Fifa.

NANI ANAMKUMBUKA HUYU JAMAA NILIYESIMAMA NAYE.

PIA TUAMBIE NI TUKIO LIPI LINALOKUFANYA UMKUMBUKE....

ILI KUZIDI KUVUTIA MASHABIKI KWENDA UWANJANI - MAN UNITED KUANZA KUONYESHA FILAMU ZA HOLLYWOOD OLD TRAFFORD HADI MWISHO MWA MSIMU

Huku wakiwa wanaongoza ligi kwa pointi 15 zikiwa zimebaki mechi tisa ligi kumalizika, Manchester United wametangaza plan mpya ya kibiashara kuvutia mashabiki wao kuingia uwanjani kuelekea mwishoni mwa msimu. 
Wakati wa mechi zao nne za nyumbani zilizobakia, ikiwemo mechi yao dhidi ya mahasimu wao Man City na Chelsea, Man United wataonyesha moviez ya kutoka Hollywood kwenye screen kubwa  kwenye dimba la Old Trafford. Klabu hiyo imesema lengo ni kuwapa burudani zaidi wanunuzi wa tiketihuku wakielekea kushinda taji lao 20 ikiwa watashinda mechi nne au tano zijazo za ligi.  

"Tuna furaha sana kuwepo kwenye nafasi tuliyopo kwenye ligi," manager wa Man United aliwaambia waandishi wa habari wakati akitangaza uamuzi huo. "Huwezi kuchoka kushinda ligi, lakini suala la kushinda ligi mapema kukiwa kumebakiwa na mechi nyingi, mashabiki wanaweza wakapoteza hamu ya kwenda uwanjani kwa kiasi fulani. Hivyo tumeamua kuanza filamu ili kuzidi kuwaburudisha mashabiki. Nadhani wakati wa mechi na Man City tutakuwa tukionyesha filamu iitwayo You Got Served, then kwenye mechi  ya Aston Villa tutaonyesha Apocalypse Now, na Chelsea tutaonyesha Run Fatboy Run na dhidi ya Swansea itakuwepo filamu ya The Silence of the Lambs."

Msimu uliopita, Man United walipoteza taji kwa Man City kwenye dakika ya mwisho ya msimu. Ingawa Red Devils wanaonekana kuwa vizuri tofauti na msimu uliopita.

HATIMAYE SERIKALI NA TFF ZAFIKIA MUAFAKA KUHUSU UCHAGUZI MKUU

Serikali imekubali mchakato wa uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uendelee kwa sharti la kuhakikisha haki inatendeka kwa wagombea waliofika mbele ya Kamati ya Rufani ya Uchaguzi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mchana, Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao kati ya uongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo chini ya Waziri Dk. Fenella Mukangara, TFF na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Amesema baada ya maafikiano hayo, TFF italiandikia barua Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo ndilo lililosimamisha mchakato huo ili litume ujumbe wake kwa ajili ya kusikiliza malalamiko ya wagombea walioenguliwa.

Rais Tenga ambaye ameishukuru Serikali kwa kuruhusu mchakato huo uendelee, pia ameahidi kuwa uchaguzi wa TFF utafanyika kabla ya Mei 25 mwaka huu kama walivyokubaliana na Serikali, na kuwa haki si tu itatendeka bali ionekane imetendeka.

“Serikali imetuelekeza uchaguzi ufanyike kabla ya Mei 25. Tumewaambia kwetu huko ni mbali. FIFA wakija hata kesho wakituambia endeleeni sisi tuko tayari. Hesabu zetu ziko tayari, makabrasha yote yako tayari yanasubiri mkutano tu. Labda itakuwa kutoa muda tu kwa wajumbe walioko mbali waweze kujiandaa, maana wajumbe huwezi kuwaita ghafla,” amesema.

Amesisitiza kuwa TFF ilishapanga tarehe ya uchaguzi, lakini ukasimamishwa na FIFA baada ya baadhi ya walioenguliwa kulalamika huko. Hivyo maneno kuwa TFF hawataki uchaguzi kwa sababu wanataka kuendelea kubaki madarakani haya maana hata kidogo.

Hivyo amewataka wagombea wote waliofika kwenye Kamati ya Rufani ya Uchaguzi na wakaendelea kujiandaa vizuri, kwani FIFA watakapofika watawasikiliza wao na vyombo vilivyowaengua.

Pia amesema TFF ina heshimu Serikali na itaendelea kufanya hivyo, lakini vilevile lazima iheshimu FIFA sababu iko kwenye mpira wa miguu, na FIFA ndiyo wasimamizi wa mchezo huo duniani.  

Amewakumbusha wanachama wa TFF, hasa wajumbe wa Mkutano Mkuu kufahamu kuwa TFF ina katiba, lakini ni lazima pia wafahamu kwanini kuna FIFA.

Rais Tenga amewahadharisha watu wanaopitapita mikoani kuomba saini za wajumbe ili kuita Mkutano Mkuu wa dharura wakati wanajua mkutano ulishaitishwa, lakini ukasimamishwa na FIFA. Jambo hilo kikatiba ni kosa.

HIKI NDIO KIKOSI CHA MOROCCO KINACHOKUJA IJUMAA KUUMANA NA STARS - CHAMAKH NA TAARABT WATOSWA

Taarabt ambaye ameachwa kwenye kikosi cha Morocco akipambana na Van Persie
Timu ya Taifa ya Morocco (Lions of the Atlas) inatarajiwa kuwasili nchini keshokutwa Ijumaa kwa ndege ya Emirates tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Tanzania (Taifa Stars) itakayochezwa Jumapili katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Msafara wa timu hiyo yenye watu 58 wakiwemo maofisa 19 na waandishi wa habari 12 utawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 8.55 mchana na utafikia hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency.

Siku hiyo Morocco inatarajia kufanya mazoezi jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, na Jumamosi itafanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa saa 9 kamili alasiri.

Wachezaji walioko kwenye kikosi hicho chini ya Kocha Rachid Taoussi ni Nadir Lamyaghri, Anas Zniti, Yassine Bounou, Younnes Bellakhadar, Abdellatif Noussair, Abderrahim Achchakir, Zoheir Feddal, Younnes Hammal, Zakarya Bergdich na Abdeljalil Jbira.

Issam El Adou, Kamel Chafni, Salaheddine Saidi, Mohamed Ali Bamaamar, Abdelaziz Barrada, Salaheddine Aqqal, Abdessamad El Moubarky, Nordin Amrabat, Chahir Belghazouani, Abdelilah Hafidi, Youssef Kaddioui, Brahim El Bahri, Hamza Abourazzouk na Youssef El Arabi.

Wakati huo huo, tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zitaanza kuuzwa keshokutwa katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Uwanja wa Taifa na Dar Live Mbagala.

Milango siku ya mechi kwa ajili ya watazamaji itafunguliwa saa 6 kamili mchana.

KUTOKA MAKTABA: TUJIKUMBUSHE- TANZANIA Vs GAMBIA

YAYA TOURE: HIZI NDIO NJIA YA KUTAWALA DIMBA LA KATI


  • Know when to stick or twist
    Know when to stick or twist
  • Don’t be too forceful with your challenges
    Don’t be too forceful with your challenges
  • Doing light weights will keep you light
    Doing light weights will keep you light
  • Barbell squats and box jumps
    Barbell squats and box jumps
  • Know when to stick or twist
    Know when to stick or twist

Yaya Toure anaelezea siri ya mafanikio yake kwenye kutawala nafasi ya kiungo kwa kutumia nguvu, kujipanga na namna ya kutoa pasi

Kujipanga

“Nikiwa Barcelona, nilianza kwenye nafasi ya kiungo na nilimaliza kwenye nafasi hiyo hiyo. Hawakunihataji niende mbele. Kazi yangu ilikuwa kutawala nafasi ya kiungo, kunyang'anya mpira kutoka kwa adui na kuigawa kwa mchezangu mwenzangu.I started in midfield and finished in midfield. Nilipaswa kuifanya kazi hiyo kwa muda muafaka, ingawa inabidi nifanye lolote ili kutengeneza nafasi kubwa. Ukiona nafasi ifuate, ikiwa hakuna tengeneza ulinzi wa nafasi yako na toa pasi. Haupaswi kwenda mbele tu ili mradi umeenda. Muda mwingine ni vizuri kufanya hivyo lakini muda mwingine inabidi utumie uwelevu wako vizuri na kutoa pasi kwa haraka.”

Tumia nguvu lakini kucheza madhambi

“Inabidi uwe mwangalifu sana ukiangalia ni nani unakabiliana nae. Wakati unapopambana na wapinzani imara, labda unaweza ukawalazimisha kutenda madhambi, sio kwa vurugu lakini inabidi utumie nguvu. Lakini kwa wachezaji wafupi, wepesi, inabidi uwe mwangalifu zaidi. Inabidi usubiri, na kukabiliana nae huku ukiwa mwangalifu kutokutumia nguvu sana. Ni rahisi sana kupewa kadi siku hizi. Pia kuna ukweli kwamba kuna wanakuwa wanakutegemea hivyo unapopata kadi nyekundu ya moja kwa moja , unakuwa unawaletea ugumu usiohitajika kwa upande wao."

 

Jenga mwili gym

“Makocha wa viungo ndio watu muhimu zaidi kwangu klabuni; wananisaidia kuuweka mwili wangu vizuri, kitu ambacho ni muhimu kwa kazi yangu ya uwanjani. Nafanya mazoezi ya kila kiungo changu kila siku; mikono na miguu, mgongo, mabega - na vingine muhimu. Lakini jambo muhimu sio vizuri kubeba vitu vizito sana, ila inabidi nibebe vitu vyepesi kiasi mara nyingi sana. Huwa nafanya marudi zaidi ya mara 10 au 12 inategemea na zoezi, lakini sizidishi sana, kwa sababu sitakiwi kuwa mzito uwanjani. Uzito mwepesi unamaanisha unakuwa mwepesi uwanjani."