Search This Blog

Thursday, March 21, 2013

ANTONIO CASSANO AMPA MWANAE JINA LA MESSI KUONYESHA NI NAMNA GANI ANAMKUBALI LIONEL

Mchezaji wa soka wa kiitaliano Antonio Cassano amesema anaamini muargentina Lionel Messi ndio mwanasoka bora wa muda wote, na ndio maana aliweza kumshawishi mkewe kumpa mtoto wao jina mwanasoka huyo bora wa dunia kwa mara nne. 

Mshambuliaji huyo wa  amesema ni mapenzi yake kwa Messi ndio yaliyomfanya ampe mwanae jina lake. 

"Nimempa jina la Lionel kwa sababu mie ni shabiki mkubwa wa huyu mchezaji bora wa soka wa muda wote. Mke wangu hakutaka, lakini nilifanikiwa kumshawishi. Kwa maoni yangu, Messi ni mchezaji muhimu sana kwenye historia ya mchezo huu, nampenda sana anvyocheza soka."

Lionel Cassano, alizaliwa siku ya Jumatatu iliyopita, ni mtoto wa pili wa Cassano baada ya mtoto wake wa kwanza Christopher. 

No comments:

Post a Comment