Search This Blog

Saturday, July 20, 2013

MUIGIZA NA MWANACHAMA WA SIMBA BI HINDU - RAGE DIKTETA - ANATUTISHIA POLISI, HATUSIKILIZI WANACHAMA

Muigizaji mkongwe na mwanachama wa klabu ya Simba, Bi Hindu amesema hajaridhishwa kabisa na uendeshaji wa mkutano mkuu wa Simba uliongozwa na mwenyekiti Aden Rage.

Akizungumzia na mtandao huu, Bi Hindu alisema: "Yule bwana Rage leo katupeleka peleka tu, badala ya kutuambia vitu vya msingi analeta porojo, ukimuuliza eti katiba inampa mamlaka. Katuletea polisi ili atutishe, polisi apeleke kwenye siasa za chama chetu CCM na sio kwenye Simba yetu. Sikupenda hata ule mpangilio wa maswali, watu wenye hoja nzito alikuwa akiwakataa na kuchagua wa kwake aliowapanga," alisema Bi Hindu.

MKUTANO MKUU WA SIMBA WAFANYIKA KWA AMANI: RAGE AKIZINDUA MKAKATI MPYA WA MAENDELEO WA SIMBA

Mkutano mkuu wa klabu ya Simba umefanyika leo kwenye ukumbi wa Police Officer's Mess Osteybay jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulihudhuriwa na wanachama wapatao mia 700 ulifanyika kwa lisaa limoja kutoka saa nne kamili asubuhi mpaka saa tano. Mkutano ho ulizungumzia mambo mengi ikiwemo taarifa ya matumizi ya fedha ya klabu, suala la ujenzi wa uwanja wa Simba pamoja na kuzinduliwa kwa mkakati mpya wa maendeleo ya Simba.

Rage na Mzee Kinesi

Ibrahim Masoud Maestro na mwenyekiti wa kamati ya usajili Zakaria Hans Pope

Mwenyekiti aliyepita wa Simba Hassan Dalali alikuwa mmoja wa wahudhuriaji

Wanachama


Katibu Mkuu wa Simba Mtawala

Pamoja na mkutano huo kufanyika kwa amani lakini kulikuwepo na mabishano ya hapa na pale miongoni mwa wanachama
HIZI NDIO BEI ZA TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014: YA BEI YA CHINI KABISA NI $220 MECHI YA UFUNGUZI - FAINALI NI $440

Bei za tiketi kwa ajili ya mashabiki wa kutoka nje ya Brazil watakaokwenda nchini Brazil kuangalia fainali za kombe la dunia zitaanzia bei ya $90 (£59, 69 euros) kwa mechi za makundi.
FIFA imetangaza kwamba tiketi ya bei rahisi kabisa kwa mashabiki wataokwenda Brazil kwa ajili ya mchezo wa fainali ya michuano hiyo itaanzia $440 (£288) na ya bei ghali kabisa itakuwa kiasi cha  $990 (£650) ambayo ni sawa na 1,603,800 kwa fedha za madafu.

Michuano hiyo itaanza mnamo tarehe 12 June mwaka ujao, huku mechi ya kwanza ya ufunguzi ikichezwa jijini Sao Paulo.

Tiketi zitaanza kuuzwa mnamo 20 August mwaka huu.
Mashabiki wana muda mpaka 10 October kutuma maombi ya kununua tiketi na utafanyika uchaguzi wa kuamua maombi yapi yamepita.


Kuna jumla ya tiketi millioni 3 ambazo zipo kwa ajili ya maombi ya manunuzi ya mashabiki. 

BEI ZA TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA (Mashabiki wa nje ya Brazil)

Matches Category 1 Category 2 Category 3

Opening Match
$495
$330
$220
Group Matches
$175
$135
$90
Round of 16
$220
$165
$110
Quarter Finals
$330
$220
$165
Semi Finals
$660
$440
$275
3rd / 4th Place Match
$330
$220
$165
Final
$990
$660
$440

Kwa raia ya wa Brazil tiketi ya bei rahisi kabisa itaanzia kwenye kiasi cha $15. Hizi zinapatikana kwa wanafunzi tu, na wale watu wenye umri zaidi ya miaka 60 ambao wapo kwenye mipango ya kusaidia jamiii. Kwa wabrazil wengine wote bei ya chini kabisa itaanzia kiasi cha $30. 

Bei ya chini kabisa ya tiketi katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 nchini South Africa ilikuwa ni  $20, na pia ilikuwa kwenye mechi za  makundi.
FIFA mwanzoni ilisema kwamba tiketi za kombe la dunia mwaka 2014 zitakuwa za bei rahisi kuliko zote.

Katika mtandao rasmi wa kuuza tiketi wa FIFA kutakuwepo na ramani ya ya uwanja inayokuonyesha sehemu za kukaa kutokana na bei ya tiketi yako.
Hi inamaanisha kwamba hakutakuwa na kuhangaika katika kujua ni wapi unapaswa kukaa, alisema mkurugenzi wa masoko wa FIFA  Thierry Weil, ambaye ndio anayehusika na masuala ya yote tiketi.

Mashabiki wanaweza kuomba angalau siti nne kwa mechi, na kwa mechi saba tu.
Amesema pia kutakuwa na mfumo wa kuuza tena tiketi ikiwa watu waliomba au kununua tiketi kabisa na wakashindwa kufika uwanjani. 
Angalau tiketi 400,000 zitawekwa maalum kwa mashabiki wa nchi mwenyeji, huku karibia tiketi 50,000 zikiwa maalum kwa ajili ya wajenzi wanaojenga viwanja vitakavyotumika kwenye michuano hiyo.

KWA NDUGU ZANGU WABONGO MNAOTAKA KUOMBA KUNUNUA TIKETI UNAWEZA KUINGIA KWENYE MTANDAO HUU - www.ticket.org/WorldCup

TIMU ZA AFRIKA MAGHARIBI ZIZIDI KUKATWA POINTI MICHUANO YA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2014 - GUINEA NAYO YAKATWA POINTI 3 KWA KUCHEZESHA MCHEZAJI ASIYERUHUSIWA KISHERIA

Kiungo wa Equatorial Guinea Emilio Nsue, mfungaji wa hat trick katika ushindi wa mabao 4-3 katika mechi ya kuwania kufuzu kombe la dunia dhidi ya Cape Verde, alikuwa haruhusiwi kucheza mchezo huo na hivyo timu yake ya Guinea imepokonywa ushindi wa mechi hiyo, Fifa imesema leo Ijumaa.
Cape Verde wamepewa ushindi wa mabao 3-0 wa mchezo huo uliochezwa March 24, hivyo wameongeza matumaini ya kuwang'oa Tunisia kwenye kilele cha kundi B

Pia FIFA imewapa pointi ushindi wa mabao 3 Cape Verde wa mchezo wa marudiano, uliochezwa mwezi uliopita, baada ya mchezaji wa Guinea anayekipiga - Nsue ambaye alicheza katika mchezo huo na akiwa haruhusiwi kisheria. Cape Verde walishinda mchezo huo kwa mabao 2-1. 

MSIMAMO WA KUNDI ULIVYO SASA:
  Team P W D L GF GA GD Pts
1 Tunisia 5 3 2 0 10 6 4 11
2 Cape Verde 5 3 0 2 9 4 5 9
3 Sierra Leone 5 1 2 2 7 8 -1 5
4 Equatorial Guinea 5 0 2 3 4 12 -8 2

Friday, July 19, 2013

TITO VILANOVA ARUDIWA TENA NA KANSA - BARCELONA WAITA MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI HUKU TAARIFA ZIKISEMA KOCHA HUYO AMEJIUZULU

Barcelona wameita mkutano wa waandishi wa habari kwa haraka, huku kocha Tito Vilanova akitegemewa kujiuzulu kutokana kudhoofu kwa afya yake tena.

Raisi wa Barcelona Sandro Rosell na mkurugenzi wa soka Andoni Zubizarreta watakutana na waandishi jioni hii, wakatalunya wametangaza kupitia mtandao wao.

Vilanova alirithi mikoba ya Pep Guardiola mwaka jana lakini utawala wake umefunikwa na wingu la matatizo ya afya yake.

Kocha huyo wa zamani wa Barcelona B alikosa sehemu ya msimu uliopita baada ya kwenda jijini New York kutibiwa kansa.

Aligundulika kuwa na kansa mnamo November 2011.

Vilanova anaaminika kuwa ugonjwa wa kansa umemrudia tena, huku akiwa na jukumu la kuiongoza moja ya klabu kubwa duniani.


Kilimanjaro: Taifa Stars itafanya maajabu Kampala

Na Mwandishi wetu,

Mwanza
Wadhamini wa timu ya Taifa (Taifa Stars) Kilimanjaro Premium Lager, wamesema wana imani Stars itafanya vizuri katika mechi ya marudiano na Uganda Cranes kuwania kucheza katika mashindano ya CHAN kwani maandalizi ni mazuri.
Hayo yalisemwa na Meneja wa Kampuni ya Bia Tanzania Kanda ya Ziwa, Malaki Sitaki wakati  TBL Mwanza  iliwaandalia chakula cha jioni wachezaji wa Stars.
Aliishukuru TFF kwa kuichagua Mwanza tena iwe Kambi ya timu ya Taifa kwani wakaazi wa Mwanza wanaipenda timu yao na wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kuangalia wachezaji wakiendelea na mazoezi chini ya Kocha Kim Poulsen.
“Tuna imani mutafanya vizuri ili twende CHAN….kama Waganda walitufunga bao moja kwetu sisi tuna uwezo wa kuwafunga mawili kwao,” alisema Bw Malaki.
Alisema kocha amefanya kazi nzuri tangu aanze kuifundisha Timu ya Taifa na anastahili pongezi kwa mafanikio aliyopata mpaka sasa.
“Matunda mojawapo tuliyoona ni kuwafunga vigogo kama Zambia, Cameroon na Morocco,” alisema na kuongeza kuwa Kilimanjaro Premium Lager iko pamoja na Stars kwani ushirikiano uliopo ni wa manufaa kwa pande zote.
Naye Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba, aliipongeza Kilimanjaro Premium Lager kwa kuwa karibu na Taifa Stars wakati wote.
Alisema matokeo ya awali ya Stars kufungwa bao moja yasiwakatishe wachezaji na wananchi tama kwani kilichotokea ni matokeo ya mpira na Stars wanaweza kugeuza meza wakiwa Kampala.
Alisema Stars ilivyopiga kambi Mwanza mwaka jana kabla ya kwenda kwenye mashindano ya CECAFA ilishinda mechi tatu mfululizo kwa hivyo wanaamini safari hii pia kutakuwa na matokeo mazuri Kampala Jumamosi Julai 27, Stars itakapocheza na Cranes katika mechi ya marudiano.
Alisema wachezaji wanahitaji sapoti kubwa wakiwa Kampala na ni muhimu watanzania wanaoishi Mwanza na mikoa mingine ya jirani na Uganda wajitokeze kwa wingi katika mechi hiyo.
Naye kocha Kim Poulsen alisema wachezaji wako katika hali nzuri na ana imani watafanya kazi nzuri Kampala.

“Hali ya hewa ya Mwanza ni sawa kabisa na Kampala na wachzaji wameshazoea na wako katika hali nzuri ya mchezo,” alisema.

JUAN SEBASTIAN VERON ARUDI DIMBANI - AFUATA NYAYO ZA BECKHAM KWA KUTOA MSHAHARA WAKE WOTE KUCHANGIA KITUO CHA KUFUNDISHIA SOKA

Juan Sebastian Veron alimaliza miaka yake 18 ya kucheza soka akiwa na klabu ya Estudiantes mwaka 2012 — hii klabu ambayo alianzia kucheza soka. Veron aliendelea kuitumikia klabu hiyo akiwa kama mkurugenzi wa michezo, huku akicheza soka la mchangani na timu ya ndogo ya Brandsen. Kwa bahati nzuri akiwa na klabu hiyo ndogo walishinda ubingwa wa ligi ya La Plata na inaonekana ubingwa huo umempa hamasa ya kurudi dimbani kiungo wa zamani wa Man United mwenye miaka 38 ambaye sasa ameamua kuichezea klabu ya Estudiantes.
Kutoka Reuters:
Veron, ambaye ni mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Estudiantes, amesaini mkataba wa kuwa mchezaji wa mwaka mmoja na atacheza msimu wote wa 2013-14 wa ligi kuu ya Argentina.
"Sidhani kama nipo kwenye fomu niliyokuwa nayo mwaka  (2009) wakati tuliposhinda ubingwa wa Libertadores Cup, lakini sasa nimehamasika zaidi kurudi uwanjani kwa sababu napenda kucheza soka," alisema Veron alippongea na Radio Del Plataearlier wiki hii.
Pia labda kwa kufuata mfano wa mchezaji mwenzie wa zamani wa Man United - David Beckham, Veron ameamua kwamba atachangia mshahara wake wote kwenye kituo cha soka ambacho alijifunzia soka miaka 20 iliyopita.

NDOTO ZA KUREJEA UNITED ZAZIDI KUFUTIKA - CRISTIANO RONALDO AIWEKA SOKONI NYUMBA YAKE YA JIJINI MANCHESTER


Matumaini ya mashabiki wa Manchester United kuona kipenzi chao Cristiano Ronaldo akirejea kuitumikia klabu hiyo jana yalizidi kupotea baada ya mchezaji huyo kuiweka sokoni nyumba yake aliyokuwa akiishi wakati yupo nchini England kabla ya kujiunga na Real Madrid.

Ronaldo, 28 — aambaye alijiunga na Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa £80million mnamo mwaka 2009 — amekuwa akiuhusishwa sana kurejea Manchester United.

Lakini mreno huyo sasa ameiweka sokoni nyumba yake yenye vyumba vitano iliyopo kwenye eneo la Alderley Edge, Cheshire, kwa bei ya £3.75million.

Chanzo kimoja cha habari kilisema: “Mashabiki wa United  mara zote walikuwa wanajua hatua ya Ronaldo kutokuiuza nyumba yake iliyopo jijini Manchester ilikuwa ni kwa sababu alikuwa na mpango wa kurejea mjini labda kujiunga na United, lakini baada ya mwenyewe jana kuiweka sokoni nyumba hiyo - inayoonyesha matumaini ya Ronaldo kurudi Old Trafford yanazidi kufutika.

TOP 100 YA WAFUNGAJI BORA WA LIGI KUU YA ENGLAND - THIERRY HENRY NA HASSELBAINK NDIO WACHEZAJI WA KIGENI PEKEE WALIO NDANI YA TOP 10 -


Wakati zikiwa zimebaki takribani siku 30 kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya England - hii ndio listi ya wafungaji bora wa muda wote wa ligi kuu ya England.
Inayoongozwa na Alan Shearer ambaye amefunga jumla ya mabao 260, akifuatiwa na Andy Cole na mfaransa Thierry Henry akishika nafasi ya 3 - huku yeye na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Jimmy Floyd Hasselbaink wakiwa ndio wachezaji pekee kutoka nje ya United Kingdom kuwemo ndani ya Top 10.


L.A LAKERS YATAKA KUMUUNGANISHA KOBE NA AIDHA LeBRON JAMES AU CARMELO ANTHONY


Timu ya mpira wa kikapu Los Angeles Lakers wanajiandaa kuimarisha timu yao kwa kutaka kumsajili LeBron James au Carmelo Anthony baada ya msimu ufuatao wa ligi, ESPN inaripoti. 
Mastaa wote wawili LeBron na Anthony watakuwa huru msimu ujao ikiwa wataamua kutoongeza mikataba yao ya sasa na vilabu vyao. Kunfi la wachezaji wengine wa kikapu, akiwemo Dwyane Wade, Amar’e Stoudemire na Chris Bosh wana kipengele cha uhuru wa kukatisha mikataba yao, katika mikataba ya miaka mitano waliyosaini mwaka  mapema 2010.
Luol Deng, Danny Granger, Andrew Bogut na Dirk Nowitzki watakuwa huru mwishoni mwa msimu ujao wa ligi ya NBA. Pia L.A Lakers itabidi kufanya uamuzi kuhusu hatma ya Kobe Bryant, ambaye yupo atakuwa anaingia kwenye mwaka wa mwisho wa mkataba wake msimu huu unaokuja.

LeBron James, ambaye ni mshindi wa tuzo ya NBA Finals MVP, alisema hivi karibuni kwamba hafikirii kabisa kuhusu mkataba wake utakapoisha mnamo mwaka 2014.
Lakers walimpoteza Dwight Howard wakati alipoamua kusaini mkataba wa na Houston Rockets badala ya kuongeza mkataba wa miaka mitano na timu hiyo ya L.A. 

WAKATI KOCHA WAO AKIUGULIWA NA MAMA YAKE - MAN CITY WAZIDI KUIMARISHA TIMU YAO - NEGREDO NA JOVETIC WASAJILIWA


MANUEL PELLEGRINI amesafiri kwenda kwao Chile jana usiku wakati Manchester City ikikamilisha usajili wa £39million wa washambuliaji wa wawili.

Kocha huyo aliiacha klabu yake ikiwa kwenye kambi ya mazoezi nchini South Africa kwa sababu anauguliwa na mama yake mazazi.

City wana matumaini Pellegrini, 59, ataungana na kikosi chake tena huko Hong Kong jumanne ijayo — akiungana na washambuliaji wapya wa timu hiyo Alvaro Negredo na Stevan Jovetic.
Negredo akienda kufanyiwa vipimo vya afya
Bosi msaidizi wa klabu hiyo Brian Kidd alisema: “Manuel imembidi arudi nyumbani kwao Chile. Tuna matumaini ataungana nasi tukiwa Hong Kong jumanne lakini hatuna uhakika." 

Mshambuliaji wa kihispaniola Negredo, 27, jana mchana alikuwa jijini Manchester kwenye hosptiali ya Bridgewater akifanyiwa vipimo kukamilisha uhamisho wake wa kutoka Seville kwa ada ya uhamisho ya kuanzia ya £16.4m — huku £4.2m zitalipwa kutokana na kiwango cha mchezaji.
City pia tayari wameshakubalina ada ya usajili ya £22.4 kwa ajili ya mshambuliaji wa Fiorentina Stevan Jovetic.
Mshambuliaji huyo wa Montenegro, 23, atawasili jijini Manchester leo kukamilisha dili hilo la usajili. 
Jovetic alisema: “Mimi bado kijana na nataka kubadilisha maisha yangu ya kisoka.
“City ni timu kubwa na muhimu ndani ya Premier League.
“Nataka kushinda makombe na pia nitakuwa na rafiki yangu mkubwa Matija Nastasic.”

SAKATA LA USAJILI WA ROONEY : FAMILIA YAANZA KUATHIRIKA - MKEWE HATAKI WAHAMIE NJE YA NCHI

Sakata la usajili la mshambuliaji WAYNE Rooney jana usiku lilitishia kuivunja familia yake — kwa sababu mkewe wake Coleen hataki kuhamia nje ya nchi hiyo.

Man United jana ilikataa ofa inayotajwa kuwa £20million kutoka Chelsea, mahala ambapo mshambuliaji huyo inasemekana yupo radhi kwenda kwa kuwa Coleen, 27, ataendelea kuwa karibu na wazazi wanaoishi huko Liverpool.
Coleen Rooney with eldest son Kai
Lakini United wanaonekana hawapo tayari kuwauzia silaha wapinzani wao wa moja kwa moja ndani ya ligi kuu ya England - hivyo kufanya kuwepo na uwezekano mkubwa wa uhamisho wa kwenda Paris Saint-Germain kufanikiwa kama Moyes akiamua kumuuza Rooney.
Wayne Rooney at training ground 
Chanzo kimoja cha habari kilisema: “Suala hili la uhamisho wa Rooney linasababisha hali tete baina ya Wayne na Coleen. Hawataki kuhamia nje ya nchi. Lakini ikiwa hatashindwa kuhamia Chelsea basi mambo yatazidi kuwa magumu kwao. 
“Chaguo la kwanza la Wayne ni Chelsea kwa sababu wakihamia kusini mwa nchi bado wataendelea kuwa karibu na Liverpool wakiendesha masaa kadhaa kwenda mahala wazazi wao wanapoishi.
“Lakini United wamesema kwamba, ikiwa watamuuza - itakuwa ni kwa klabu ya nje tu, hivyo PSG wanaweza wakarudi na ofa nzuri. 
"Coleen hataki kabisa kwenda Ufaransa kwa sababu anadhani ni mbali sana na ilipo familia yake, ambao wanamsaidia sana katika kulea wanae Kai na Klay.
"Hivyo ikiwa atauzwa, Wayne itabidi atumie ndege binafsi kutoka Paris-Liverpool, au aende kuishi mwenyewe hotelini.”

Mchana wa jana mke wa Rooney, Coleen alijikuta tena kwenye majibizano makali na baadhi ya mashabiki kwenye mtandao wa Twitter ambao walikuwa wakimtumia meseji ampelekee Rooney kuhusu suala la uhamisho wake - hali ambayo inazidi kuleta hali tete.

PAUL MFEDE 'BOLINGO' - SIMBA ASIYESHINDIKA ALIYESHINDWA NA KIFO - SHUJAA WA CAMEROON MWAKA 1990 KWENYE KOMBE LA DUNIA ALIYEPOTEZA MAISHA BAADA YA KUSHINDWA KULIPIA MATIBABULouis Paul Mfede alikuwa gwiji wa soka nchini Cameroon , alikuwa shujaa ndani ya uwanja na balozi mzuri nje ya uwanja .

Fefe aka Bolingo alikuwa sehemu muhimu ya kikosi kilichoipeleka Cameroon kwenye robo fainali ya kombe la dunia mwaka 1990 na kuweka historia ambayo haijafikiwa mpaka hii leo .

Lakini tarehe 10 mwezi uliopita alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 52 kutokana na maradhi ya mapafu kwenye hospitali moja huko Yaounde na sababu za kifo chake zaidi ya maradhi ilikuwa ukweli kuwa alishindwa kugharamikia dawa na matibabu ya maradhi yake . 


Jeneza la Mfede wakati akienda kuzikwa

Ulikuwa ni mwisho wa kuhuzunisha kwa maisha ya mtu ambaye aliifanyia Cameroon makubwa sambamba na watu kama Roger Milla , Thomas Nkono, Libih Thomas, Maboang Kessack na wengineo hasa miaka 23 iliyopita nchini Italia kwenye kombe la dunia.

Mafanikio ya Mfede na wenzie yaliwafanya Wacameroon wote kujawa na matumaini na kumbukumbu ya wengi waliomshuhudia akiwapiga chenga wachezaji watatu pamoja na tabia yake ya kuwafanya wenzie wajiamini hadi kuwafunga Argentina 1-0 kwenye mchezo wa kwanza wa kombe la dunia mwaka 90 haitafutika vichwani mwa watu wa Cameroon.

Pamoja na yote haya, viongozi wa chama cha soka cha Cameroon na wizara ya michezo waliotaarifiwa na mkewe Paul juu ya hali ya mumewe hawakufanya chochote .

Mtoto wa Mfede anayeitwa Frederick alifichua kuwa msaada pekee ulitoka kwa Roger Milla ambaye alisaidia kulipa gharama za hospitali wakati familia yake ikiwa imekosa msaada. Siku ya mazishi yake, waziri wa michezo Adam Garoua alimtunuku Mfede medali ya heshima kwa mchango wake kwa taifa la Cameroon huku akiweka shada la maua kwenye kaburi lake kwenye kijiji cha Nkol-kosse huko Lekie kwenye jimbo la kati la Cameroon lakini watu wamehoji kwanini Mfede hakupewa huduma wakati akiwa mgonjwa huduma ambayo ni muhimu kuliko hata nishani isiyo na maana wakati huu akiwa amekufa.


Kikosi cha Cameroon kilichofanya maajabu 1990 - Mfede aliyechuchuma wa kwanza mkono wa kulia.

Thomas Nkono alilalamika, "Kwanini watu ambao tuliwahi kuitwa mabalozi leo hii maisha yetu yanafifia kwa aibu na shida . Ninapoona watu wachache ambao ni mashabiki halisi wa soka wakiwa wamelizunguka jeneza la Mfede nasikititka huku nikisema kuwa hii ni mbaya kwa shujaa wa taifa . Inauma kuona akiondoka duniani kama mtu ambaye hakuna anayemfahamu."

Thomas Nkono ambaye anaaminika kuwa kipa bora wa afrika kwa miaka yote aliongeza kuwa, "Watu ambao walijitoa kwa ajili ya soka wanapaswa kutambuliwa na serikali lakini kumuona Mfede anakufa mtaani namna hii inaniuma sana."

Beki wa zamani Benjamin Massing alisema, "Ni huruma sana kumuona mwenzetu amekufa kwa namna kama hii akiwa ametelekezwa na kauchwa mwenyewe."Mfede akimtuliza Rigobert Song baada ya kupewa kadi nyekundu kwenye moja ya mchezo wa kombe la dunia 1990

 

Pamoja na kukosekana kwa huduma na mazishi ya kitaifa kwa Mfede au the magic foot yaani guu la kushoto la kichawi kama alivyokuwa akifahamika enzi za miaka ya themanini jina ambalo alipewa na mchezaji bora wa afrika mwaka 1980 Jean Manga Onguene atakumbukwa na wenzie kama mtu mwenye furaha na aliwaunganisha wachezaji wenzie .

"Kesi ya Mfede ni kesi ambayo inawakuta wachezaji wengi wa zamani wa Cameroon hasa wale wa miaka ya tisini .

Sisi wanasoka hakuna anayetujali
," anasema mchezaji wa zamani Libih , anaongeza, "Mbaya zaidi hakuna umoja miongoni mwetu kwa kuwa sio serikali pekee ambayo itafanya kila kitu . Ni kweli kuwa tunajitolea maisha yetu kupigania bendera ya taifa letu lakini baadaye tunakuwa watu wa kawaida lazima tukutane na maisha ya baada ya soka. 

Inatia huruma kuwa wachezaji wakubwa hawaweki misingi yoyote ya kulinda maslahi yetu . Tunakimbilia maisha mabaya ambayo hayafahamiki na ndio maana tunapambana kwenye televisheni kwa kuwa tunataka kurudi mahala fulani, inatia huruma na maisha ni magumu, tunapigana sisi kwa sisi badala ya kujenga."

Mchezaji mwingine Youmbi Ayakan ambaye alicheza kwenye miaka ya tisini aliungana na Libih ambapo alisema kuwa kuna haja ya wachezaji kujipanga na kuweka hali zao za baadaye kuwa nzuri zaidi. "Ni muhimu kwa wale wanaocheza sasa na hata wale waliostaafu, wachezaji wengi wa sasa hata hawafahamu kaka zao waliocheza kabla yao, sisi ndio tuliwafanya waote kufikia mahali hapa walipo leo hii lakini hakuna anayefanya kitu kwa ajili yetu."

Suluhisho la tatizo hili kwa mujibu wa Libih ni kwa wachezaji waliostaafu kutumia uwezo wao kuwasaidia wachezaji wachanga ama kuwa viongozi wa chama cha soka na tawala nyingine za michezo na hata kuingia kwenye ukocha

"Kuna haja ya chama cha soka kulinda maslahi ya wachezaji kwa kuwa sisi wote tumefanya makubwa kwa niaba ya taifa na kuna haja ya wanamichezo wote kwa pamoja kulindwa."

Thursday, July 18, 2013

PHOTOS: TAIFA STARS IKIJIFUA KIRUMBA TAYARI KWENDA KUWAMALIZA UGANDA KWAO

Add captionWENGER: HATUJAKARIBIA KUMSAJILI MCHEZAJI YOYOTE MPAKA SASA - TUNAO UWEZO WA KULIPA MSHAHARA WA WAYNE ROONEY'

Wakati wa mashabiki wa klabu ya Arsenal wakiwa wanasubiri kwa hamu usajili wa wachezaji kwenye klabu yao - kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema kwamba klabu hiyo mpaka sasa haipo karibuni kumsajili mchezaji yoyote.

Kocha huyo wa kifaransa ambaye ndio kocha aliyedumu muda mrefu na timu kuliko kocha yoyote kwenye ligi kuu ya England, amepewa fedha nyingi za usajili msimu huu, na mpaka sasa amemsajili mchezaji mmoja tu - mshambuliaji wa timu ya Ufaransa chini ya miaka 20 Yaya Sanago kwa uhamisho wa bure kutoka  Auxerre.

Wakati mashabiki wakiwa na tumaini la kusajiliwa kwa mchezaji mkubwa, kocha huyo mwenye miaka 63 ameonya kwamba mpaka sasa hawajakaribia kumsaini mchezaji yoyote.

“Ushindani barani ulaya ni mkubwa kwa sasa. Kuna fedha nyingi lakini hakuna wachezaji wengi wa kuwasajili. Tunajitahidi sana kufanikisha usajili lakini mpaka sasa hatupo karibu kusajili mchezaji yoyote.

Wenger pia alimzungumzia mchezaji wa Manchester United Wayne Rooney ambaye amekaririwa akisema yupo tayari kumsajili mchezaji huyo kwenye timu yake ya Arsenal.

"Ilitokea kwetu msimu uliopita na inaweza ikawatokea wao United msimu huu. Rooney yupo kwenye mkataba wa miaka mwili na United, hivyo sasa kilichobaki ni maamuzi ya United. Lakini sisi kama Arsenal tuna uwezo wa kumsajili na kumlipa mshahara wake mkubwa Wayne Rooney."

KOZI YA WAAMUZI NA MAKOCHA WA MCHEZO WA BEACH SOCCER ILIVYOMALIZIKA NCHINI TANZANIA

MABADILIKO YA VIONGOZI WA KAMATI NDOGO ZA ZA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI TFF

JAJI Steven Ihema na wakili mwandamizi, Bi. Jesse Mguto wataongoza kamati muhimu za za maadili za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zilizoundwa baada ya kufanya mabadiliko kwenye katiba ya Shirikisho hilo mwishoni mwa wiki iliyopita, Rais wa TFF Leodegar C. Tenga alitangaza jana.


Shirikisho hilo pia limemteua Jaji Bernard Luanda kuongoza Kamati ya Rufaa za Uchaguzi wakati Profesa Mgongo Fimbo ataendelea kuongoza Kamati ya Rufaa za Nidhamu na Kamanda Mstaafu, Alfred Tibaigana akiendelea kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu.

Rais Tenga alisema hayo wakati alipoongea na waandishi wa habari jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati ya Utendaji, ambacho kikatiba kina jukumu la kuunda Kamati Ndogo za TFF na vyombo vya maamuzi.

“Tulitaka tuwe na watu solid (imara) na makini ambao watatuhakikishia tunakwenda vyema,” alisema Tenga akizungumzia uteuzi huo ambao unahitimisha mchakato wa mageuzi kwenye Shirikisho baada ya Uchaguzi Mkuu wa TFF uliopangwa kufanyika mwezi Februari kusimamishwa kutokana na baadhi ya wagombea kupinga kuenguliwa na baadaye kwenda FIFA.

Katika kumaliza tatizo hilo, FIFA ilituma ujumbe wake kusikiliza walalamikaji na watu wengine na baadaye kuagiza kuundwa kwa Kamati za Maadili na kufanyika kwa Mkutano Mkuu Maalum wa TFF kwa ajili ya kuingiza vyombo hivyo kwenye katiba kabla ya kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa TFF.

“Tumezingatia pia maoni ya wajumbe wa Mkutano Mkuu ambao walitaka kamati ziwe na majaji... lakini si rahisi kupata seating judges (majaji walio kazini) ndio maana tunawashukuru wale waliotuambia kuwa wako tayari kutusaidia.

“Tumetafuta majaji na mawakili waandamizi ambao tunaamini watatuhakikishia haki inatendeka na inaonekana inatendeka,” alisema Tenga na kuongeza kuwa pia walizingatia maombi ya wajumbe wengine watatu ambao walitaka kupumzika, akiwataja kuwa ni Deo Lyatto, Sylvester Faya na Idd Mtiginjollah.

Alisema kutokana na mfumo huo mpya, mambo yote yanayohusu masuala ya ndani ya uwanja sasa yatashughulikiwa na Kamati ya Nidhamu, wakati yale ya nje ya uwanja, ambayo yanawahusu viongozi na wanafamilia ya mpira wa miguu kwa ujumla, yatashughulikiwa na Kamati za Maadili.

Tenga alisema mabadiliko hayo pia yamegusa kamati nyingine mbili, yaani Kamati ya Nidhamu na Kamati ya Uchaguzi ambayo sasa itaongozwa na Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Zanzibar, Hamidu Mbwezeleni

Jaji Ihema ataongoza Kamati ya Rufaa za Maadili akisaidiwa na mwanasheria mwingine mwandamizi, Victoria Makani, huku Bi. Mguto, ambaye anakuwa mwanamke wa kwanza kuongoza vyombo vya vya maamuzi ataongoza Kamati ya Maadili akisaidiwa na makamu wake Francis Kabwe, ambaye Msajili wa Mahakama Kuu.

Katika uteuzi huo, baadhi ya wajumbe wamehamishwa kutoka kamati moja hadi nyingine. Mhe. Murtaza Mangungu, ambaye awali alikuwa Kamati ya Rufaa za Uchaguzi, sasa ataingia kwenye Kamati ya Rufaa za Maadili; Kamanda Mohamed Mpinga na Prof Madundo Mtambo wamehamishwa kutoka Kamati ya Rufaa za Uchaguzi kwenda Kamati ya Maadili.

Wajumbe wapya kwenye Kamati hizo ni pamoja na kocha wa zamani wa Taifa Stars na Reli ya Morogoro, Mshindo Msolla na Kamanda Mstaafu Jamal Rwambow wanaingia kwenye Kamati ya Nidhamu; mwanasheria maarufu Evodi Mmanda anaingia kwenye Kamati ya Maadili; mwanasheria mwandamizi Mustapha Kambona ambaye anaingia kwenye Kamati ya Nidhamu; Mhe. Mohamed Misanga ambaye anaingia kwenye Kamati ya Maadili na Kanali Iddi Kipingu, ambaye anasifika kwa kuendesha soka la vijana, anaingia kwenye Kamati ya Rufaa za Nidhamu.

Pia Mwanasheria Anne Steven Marealle anakuwa mjumbe kwenye Kamati ya Rufaa za Uchaguzi; Yohane Masale (Rufaa za Uchaguzi), Allen Kasamala (Rufaa za Uchaguzi); Francis Kiwanga ambaye pia aningia kwenye Kamati ya Rufaa za Uchaguzi na mkufunzi wa FIFA, Henry Tandau ambaye anaingia kwenye Kamati ya Rufaa za Maadili.

Kamati ya Utendaji pia imefanya mabadiliko kwenye Kamati ya Waamuzi ambako mwenyekiti Said Nassoro na katibu Charles Ndagala wa Chama cha Waamuzi wanaingia kwenye kamati hiyo kushika nafasi ya Joan Minja na Riziki Majala.

Wajumbe wa Kamati hizo ni kama ifuatavyo:

Kamati ya Rufaa za Maadili ni Jaji Steven Ihema (mwenyekiti), Victoria Makani (m/mwenyekiti), Mhe. Mohamed Misanga, Henry Tandau na Mhe. Murtaza Mangungu.

Kamati ya Maadili: Bi Jesse Mguto (mwenyekiti), Francis Kabwe (m/mwenyekiti), ACP Mohamed Mpinga, Prof. Madundo Mtambo, na Evod mmanda.

Kamati ya Rufaa za Nidhamu: Prof. Mgongo Fimbo, Ong’wanuhama Kibuta (m/mwenyekiti), Kanali Mstaafu Idd Kipingu, Dk. Mshindo Msolla, ACP Jamal Rwambow.

Kamati ya Nidhamu: Kamanda Mstaafu Alfred Tibaigana (mwenyekiti), Mustafa Kambona (m/mwenyekiti), Azzan Zungu, Yussu Nzowa na Mohamed Msomali.

Kamati ya Rufaa za Uchaguzi: Jaji Bernard Luanda (mwenyekiti), Francis Kiwanga (m/mwenyekiti), A. Steven Semu, Yohane Masalla na Allen Kasamala.

Kamati ya Uchaguzi: Hamidu Mbwezeleni (mwenyekiti), Moses Kaluwa (m/mwenyekiti), Mustafa Siani, Hassan Dyamwale na Kitwana Manara.

Kamati ya Waamuzi: Kapteni Mstaafu Stanley Lugenge (mwenyekiti), Omar Kasinde (m/mwenyekiti), Said Nassoro, Charles Ndagala na Mohamed Nyama.

EXCLUSIVE INTERVIEW NA MFUNGAJI BORA WA VPL 2012-13 KIPRE TCHETCHE

BENEDICT CHALES LUKUMAY WA CLUB MASAI AFARIKI KWA AJALI YA GARI


clip_image001Marehemu Benedict (Kulia)
 
  Habari nilizozipata muda mchache uliopita na kuthibitishwa na ndugu na jamaa wa karibu zinasema Benedict Chalres Lukumay amefariki kwa ajali ya gari eneo la Mikumi mkoani Morogoro usiku huu.
Chanzo cha kifo chake kimeelezwa kuwa ni ajili ya gari iliyotokea eneo la Mikumi mkoani Morogoro majira ya saa mbili usiku. Meneja mkuu wa Meridian Hotel LTD Mzee Mponda amethibitisha juu ya kifo hicho, huku akinieleza kuwa ilitokana na ajali ya gari.
"Wakiwa na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Adrian na gari binafsi wakielekea mkoani Iringa gari aliyokuwamo marehemu iligonga nyuma ya roli lililokuwa limesimama njiani." alisema Mzee Mponda.
Adrian ambaye ndiye aliyekuwa anaendesha gari alinusurika kwenye ajali hiyo.
Benedict alikuwa ni mmoja kati ya Wakurugenzi watendaji wa kampuni ya Meridian Hotel LTD inayomiliki na kuendesha kumbi za burudani zikiwemo Masai Kinondoni, Masai Ilala na Masai Galapo Ilala.
Kifo chake kimeacha pengo kubwa si tu kwa familia bali hata wapenda burudani, akifahamika kimchango katika kusimamia na kuendeleza burudani na yakiwemo maonyesho mbalimbali ya wanamuziki wa bongo fleva na fani nyinginezo.
Ndugu Benny (Chief ) a.k.a Abogaa alikuwa shabiki wa kutupwa wa klabu ya Yanga.
Mungu alaze Pema ROHO ya Marehemu Ben.....

PAPIS CISSE AGOMA KUVAA JEZI ZA KUTANGAZA KAMPUNI YA MIKOPO - ASEMA DINI YAKE HAIMRUHUSUHatma ya mchezaji PAPISS CISSE kuendelea kuwa ndani ya klabu ya Newcastle ipo shakani baada ya mshambuliaji wa kisenegali kujitoa kwenye safari ya kwenda Urenokwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.


Kwa muda mrefu sasa mshambuliaji huyo amekuwa kwenye hali ya kutokuelewana na klabu yake kutokana na suala la kuvaa jezi zenye nembo ya kampuni ya mikopo ya riba ya Wonga.


Cisse, 28, amegoma kuvaa jezi za mdhamini mpya wa Newcastle kwa sabau kampuni hiyo inafanya biashara ambayo ipo kinyume na imani ya dini yake. 

Kutokana na suala hilo, mchezaji huyo aliomba avae jezi ambayo haina logo ya mdhamini huyo au jezi iwe na logo yoyote ya hisani ambayo haiendi kinyume na imani yake. 
Wawikilishi wake wamekuwa kwenye mazungumzo na Newcastle wiki hii kuhusu suala la Cisse kulazimishwa kuvaa jezi za mdhamini - Wonga mazoezini na kwenye mechi. 

Chama cha wanasoka wa kulipwa wa England pia kiliingilia majadiliano hayo lakini mpaka sasa hakuna maafikiano juu ya suala hilo, kitu kilichopelekea mshambuliaji huyo kuamua kubaki England wakati kikosi kizima cha Newcastle kikielekea Braga - Ureno.
Cisse aliwajulisha mapema Newcastle kuhusu kuvaa jezi zenye nembo ya Wonga mara tu baada ya klabuhiyo kuingia mkataba na kampuni hiyo ya mikopo. Hata baadhi ya wachezaji wengine waislam wa Newcastle akiwemo kiungo Hatem Ben Arfa wemeendlea kuvaa jezi zenye nembo ya Wonga.
  
Mchezaji wa zamani wa West Ham Frederic Kanoute - ambaye ni muislam pia - aliruhusiwa na klabu yake ya Sevilla kuvaa jezi isiyokuwa na nembo ya mdhamini ambayo ilikuwa kampuni ya kamari ya 888.com

Newcastle na Wonga zilisaini mkataba wa udhamini wa jezi wenye thamani ya £24m mwishoni mwa msimu uliopita.

AZAM WAJIBU SHUTUMA ZA HUMUD NA SAKATA LA USAJILI WA KWENDA JOMO COSMOS

Humud akiwa na John Bocco
Siku moja baada ya mwanasoka Abdulhalim Humud kuishutumu timuyake ya Azam kumletea longlongo katika usajili wake wa kwenda kujiunga timu ya Jomo Cosmos ya Afrika - leo hii klabu ya Azam imejibu mapigo kwa kutoa kauli nane kuhusu sakata la mchezaji huyo.

 1. Ana Barua Mkononi aliyopewa na Uongozi wa Azam Kumfahamisha kuwa yupo huru kujiunga na Jomo Cosmos,

 
2. Ana mkataba mkononi aliosaini kati yake na Jomo Cosmos

3. Azam FC wameshamwaga wino kwenye transfer contract kumruhusu akajiunge na Jomo Cosmos
on free transfer tangia April 2013

4. Analalamika eti Azam FC inatangaza kumuondoa kwenye usajili kwa kuwa ameuzwa South Afrika badala ya kufurahi

5. Analalamika eti Azam FC haijamsafilisha… tangia lini uliona timu inayomuuza mchezaji inamsafirisha? Kimsingi wa kuulizwa ni Jomo Cosmos kwa nini hawatumi ticket

6. Muda wa usajili bado unaendelea tena unafungwa Septemba yeye analalamika kwenye vyombo vya habari badala ya kwenda klabuni kuuliza hatma yake.

7. Ili kumpa uhuru wa 100% Azam FC leo imeamua kumlipa kilichobaki kwenye mkataba wake na kuachana naye ili kumpa uhuru kamili… sasa ni mchezaji huru… wanaosema Azam FC inambania sijui wanatoa wapi hizo hoja?


8. Tunamtakia kila la kheri Abdulhalim Humoud katika maisha yake kama mchezaji huru 100%