Search This Blog

Saturday, June 29, 2013

CHEMSHA BONGO: HAWA NI WACHEZAJI GANI?


*WOTE WANA VIPARA SASA HIVI.

KUELEKEA FAINALI YA BRAZIL VS SPAIN: JE NI BRAZIL YA AKINA PELE AU SPAIN HII YA SASA - IPI NDIO TIMU BORA KABISA KUWAHI KUTOKEA KWENYE SOKA LA KIMATAIFA?Kutoka kwa Pele, Tostao, Rivelino na Gerson mpaka kwa Xavi, Andres Iniesta, Iker Casillas na Sergio Busquets, timu hii ya Spain na Brazil ya wakati ule zote zimeteka hisia za mioyo ya wapenda soka duniani kwa soka lao safi.

Aidha ni rangi za njano na blue za Pele na wenzie au nyekundu za La Roja - timu hizi mbili ndio zinazotajwa kuwa bora kuliko zote kuwahi kutokea katika historia ya mashindano ya kimataifa.


Ni vigumu sana kuweza kuzifananisha timu hizi mbili kutoka kwenye mbili tofauti. Mchezo wa soka umebadilika kabisa ndani ya muda wa zama hizi mbili - ambazo Brazil ya miaka 1970 na Spain ya sasa, zote zikiwa zimechukua kombe kubwa kabisa katika mpira wa miguu.

Kutoka kwenye ubora wa uwanja wa kuchezea na mpira wenyewe mpaka kwenye ukweli kwamba wachezaji wa sasa wanahitajika kukimbia mara mbili zaidi ya ilivyokuwa kwa wenzao wa miaka ya 1970's, soka la kisasa limekuwa gumu na lisilotabirika.

Lakini huku Spain wakijiandaa kupigania ubingwa wa nne mkubwa kabisa katika mashindano ya kimataifa ndani ya kipindi cha miaka mitano tangu walipochukua ubingwa wa Euro mwaka 2008 kwa kuifunga Ujerumani 1-0 jijini Vienna - watapambana na Brazil katika fainali ya kombe la mabara kesho jumapili na kujaribu kuweka rekodi mpya. Lakini Je unadhani ni Spain ya sasa au Brazil 1970 ipi ni bora?

Timu zote zinatajwa kucheza mchezo wa soka unaovutia mno kuuangalia - zikiwa zinamiliki mpira kwa muda mrefu na zikiwa na utajiri wa vipaji vya wachezaji mmoja mmoja.

"Mwaka 1970, tulicheza kwa namna Spain inavyocheza leo hii, lakini sio kwa spidi hii,” kocha wa kikosi cha Brazil ya mwaka 1970, Mario Zagallo, aliiambia BBC wiki hii.

“Lakini, timu yetu ilikuwa nzuri sana katika kuuchezea mpira na kuumiliki kama ilivyo kwa Spain, ambao wamekuwa wakicheza hivi kwa muda mrefu.”

Je ni timu kudumu kwa mrefu na kuendelea kupata mafanikio? Au ni kuchukua makombe mengi? Ni nini hasa kipimo cha ubora kati ya vizazi hivi viwilitofauti vya soka?


MJADALA ULIOFANYWA NA MARCA
Ni wachezaji wangapi wa kikosi cha sasa cha Spain wangeweza kupata namba katika kikosi cha Brazil ya akina Pele, au ni wachezaji wangapi wa Brazil 1970 wangeweza kucheza kwenye kikosi cha Spain hii? Kuna mchezaji wa kushindana na Pele? Je Spain wanamkosa mtu wa aina ya Jairzinho? Brazil ilijaaliwa vipaji vya mchezaji mmoja mmoja wakati Spain mafanikio yao ynayaonekana kutoka kucheza kitimu zaidi. 

Je unadhani ni Brazil 1970 au Spain ya sasa ipi kiboko katika soka la kimataifa? ANGALIA HIZI VIDEO ZINAWEZA KUKUPA MWANGA KIDOGO KUHUSU TIMU HIZI MBILI?

HIVI NI BAADHI YA VIPANDE VYA MECHI ZA BRAZIL 1970 HII NDIO SPAIN YA SASA

ANDRES INIESTA AIOKOA TIMU YAKE YA UTOTONI KUTOKUSHUSHWA DARAJA KWA KUSHINDWA KULIPA MISHAHARA YA WACHEZAJI


Klabu ya Albacente inayoshiriki kwenye ligi ya daraja la 2 nchini Spain maarufu Segunda Division B - ingeweza kushushwa daraja kama isingekuwa kusaidiwa na mchezaji wao wa zamani Andres Iniesta masaa 11 kabla ya muda muda waliopangiwa kulipa madeni ya mishahara ya wachezaji inayofikia kiasi cha €240,000.

Klabu hiyo ingeshushwa mpaka daraja la 3 kama wangeshindwa kulipa deni lao mpaka kufikia Ijumaa saa sita kamili mchana.

Japokuwa, Iniesta, ambaye ana hisa nyingi kuliko watu wote kwenye klabu hiyo ambayo pia ndio alianzia soka lake, alikuja kuokoa jahazi, kwa kulipa madeni yote ya mishahara kutoka kwenye mfuko wako.

Hii sio mara ya kwanza kwa kiungo huyo wa Barcelona kuisadia timu hiyo - mpaka sasa ameshalipa kiasi kipatacho cha €420,000 tangu 2011.

Iniesta, ambaye kwa sasa yupo Brazil, alicheza kwa miaka miwili katika klabu ya Albacente kabla ya kujiunga na Barcelona kwenye academy yao ya La Masia mwaka 1996. 

MARC VIVIEN FOE PART 2: KITUO CHA SOKA ALICHOJENGA KIMEGEUKA KITUKO SASA - MAN CITY PIA WAMTOSAWakati michuano ya kombe la mabara 2013 yakiwa yanavuka hatua ya nusu fainali huko Brazil, miaka 10 iliyopita wakati kama huu michuano hiyo ilikumbwa na majanga.

On 26 June 2003, Marc-Vivien Foe alidondoka uwanjani wakati akiichezea timu yake ya Cameroon katika nusu fainali dhidi ya Colombia na pamoja majaribio ya kujaribu kumtibia, mchezaji huyo akiwa miaka 28 alifariki dunia muda mfupi baada ya kukumbwa na mshtuko wa moyo.

Miaka 10 baadae, ni huzuni kugundua kwamba kumbukumbu ya mchezaji wa zamani wa West Ham na Manchester City inaanza kupotea kwa kiasi fulani - 'legacy' yake imeanza kupotea.

Muongo mmoja baada ya kifo chake, Foe alikuwa na ndoto ya kuwafunza vijana wadogo wa kikameroon na wanasoka wa kiafrika.

Aliianzisha Marc-Vivien Foe Sport Complex, kituo ambacho kilijengwa nje kidogo ya maeneo ya mji wa Yaounde. Lakini kwa bahati mbaya kituo hicho sasa kipo kwenye hali mbaya
Sanamu lilojengwa nje ya sehemu ya kuingilia tayari limeanza kupata ufa, rangi iliyopakwa kwenye majengo ya kituo hicho imeshapauka, pia majengo hayo yakianza kuharibika. Kama hakuna jambo litakalofanywa kushughulikia kituo hicho, siku moja kitageuka kuwa nyumba ya kulala wahuni.

Leo hii kila kitu kipo katika hali mbaya ndani ya kituo hicho - hakuna madirisha, kuta zimejaa mavumbi na huku wadudu wakizidi kuzingira mazingira ya kituo hicho.

Sehemu ilipokuwa limejengwa bwawa la kuogelea, kuna maji machafu yaliyojaa kwenye bwawa hilo, maji yenye rangi ya kijani huku uchafu ukiwa unaelea, pia kuna takataka za plastic na miti mbalimbali. 
Bwawa la Kuogelea 
Kwenye sehemu ya kuchezea kama palivyo sehemu nyingine za Cameroon kuna undogo mgumu, uliochimbwa kutengeneza uwanja miaka kadhaa iliyopita, na nyuma yake uwanja huo kuna pori. 

"Marc angerakabti majengo na eneo hili la kituo, alikuwa na nia ya dhati katika kuwakomboa vijana wa Cameroon na wengine wote Afrika wanaopenda kucheza soka, lakini tangu kifo chake hakuna hata mmoja aliyechangia katika kukiendeleza kituo hichi," anasema kwa masikitiko Amougou Martin Foe baba wa marehemu.  

Miaka minne iliyopita, kulikuwepo na sherehe za kumbukumbu ya Marc katika kituo hicho huku mechi za soka zikichezwa, lakini hilo pia siku hizi halifanyiki. 
Mwaka huu, ilifanyika sala tu katika kaburi la Marc katika kukumbuka siku ya kufa. Shughuli nyingine zinazofanyika katika kumkumbuka kama maandamano, mbio za baiskeli, na michezo mingine yote imeghailishwa na serikali mpaka 27 Julai kutokana mikutano ya kisiasa. 
Hakuna program yoyote rasmi kutoka kwa serikali ya Cameroon. Ahadi zimekuwa zikitolewa kwa takribani miaka 10 sasa, lakini hakuna jambo lolote lilofanyika.

"Serikali haifanyi jambo lolote kama ilivyowahi kuahidi. Ahadi zao zimekuwa hazikamiliki. "Miaka 10 ni kama jana na bado tunaumizwa na kifo cha Foe. Kama Baba ni vigumu kusahau."

Bila kuwa na uwezo wa kifedha ni vigumu kutunza kituo cha Foe za michezo na Amougou Foe anahuzunika sana juu ya jambo hilo. 
"Wasiwasi wa Marc ulikuwa ni vipi kama angeshindwa kumaliza kujenga kituo hichi. Alikuwa anataka kuwafunza vijana wadogo soka lakinijambo hilo kwa sasa halifanyiki. Kama familia yetu ingekuwa na uwezo tungejaribu kufanikisha ndoto yake."

Pia inaonekana wachezaji wenzie wa Cameroon hawana mpango wowote wa kumuenzi 'Marco' kama walivyokuwa wakimuita wenyewe.
Amougou Foe anaamini wachezaji wenzie aliocheza nao wangeweza kufanya kitu kuhusu kituo hicho, ikiwa wangekuwa na nia ya kufanya hivyo kwa sababu baadhi yao wana vituo vya soka hata nje ya Cameroon. 
"Kama angetokea mtu akatengeneza sehemu ya kuchezea, na kuwachukua vijana na kuwafundisha lingekuwa jambo jema sana; matamanio yangu ni kituo hichi kuwa hai." alisema.
Nje ya uwanja wa Etihad jijini Manchester

Kwa upande wa klabu ya Manchester City ambayo yenyewe ilijenga sehemu ya kumbukumbu ya Marc Vivien Foe mbele ya uwanja wa Etihad lakini kwa siku ya juzi ambayo ndio ilikuwa siku ya kumbukumbu ya kifo chake hakukuwa na jambo lolote lilokuwa likiendelea hapo Etihad, kwa mujibu wa mtanzania aishiye nchini UK Johnson Malunda ambaye yeye alifunga safari kutoka London kwenda Manchester akitegemewa kutakuwa na tukio la kumkumbuka mwafrika mwenzie pale Etihad - aliambulia patupu na kujikuta mwenyewe huku kukiwa hamna tukio lolote liloandaliwa na City wenyewe pia hakukuwa na shabiki hata mmoja aliyekuwepo katika eneo hilo lilojengwa maalum kwa kumbukumbu ya Foe.
Johnson Mulunda akiwa kwenye eneo la kumbukumbu ya Foe = Etihad

Friday, June 28, 2013

FALCAO, MOUTINHO NA WENZAO KUANZA LIGI YA UFARANSA WAKIWA NA PENGO LA POINTI 2 - VURUGU ZA MASHABIKI ZAWAPONZA


Monaco tayari wameshatumia kiasi kisichopungua €120 million kama ada ya uhamisho kwa wachezaji wake wampya wakijiandaa na msimu ujao wa  Ligue 1, lakini mapesa yao yote hayotoweza kuwazuia kuanza ligi wakiwa nyuma ya timu zote kwenye ligi kwa pointi 2. Tukio lilotokea wakati wa mchezo wao wa mwisho wa Ligue 2 ambao walishinda ubingwa wa ligi hiyo na kupanda daraja, ambapo kulitokea vurugu uwanjani limesababisha kukatwa pointi 3 (moja imewekwa pembeni, hivyo inamaanisha kwamba itaongezwa kwenye adhabu ikiwa kutatokea tukio la namna hiyo tena.

Kutoka Reuters:
Kuliwashwa moto wakati wa mechi ya mwisho ya ligue 2 Monaco wakicheza kwenye uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Le Mans, kabla ya mshabiki hawajavamia uwanjani baada ya filimbi ya mwisho. Refa aliumizwa na mashabiki kwa mujibu wa ripoti ya kamisaa wa mchzo huo.
"Kwa tukio hilo, Monaco watacheza mechi moja bila uwepo wa mashabiki na pia wamekatwa pointi 3 watakapoanza kucheza kwenye ligue 1 msimu ujao," ilisema taarifa ya shirikisho la soka la Ufaransa LFP .

COASTAL UNION WAENDELEZA BALAA KWENYE USAJILI - WAMSAJILI MKENYA ALIYEWAHI KUKIPIGA AZAM, KUUNDA SAFU YA KIUNGO NA BOBAN PAMOJA NA SANTO


Klabu ya Coastal Union imeendeleza harakati za kukijenga vyema kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya Vodacom kwa kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Kenya Crispin Odula kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Bandari ya nchini Kenya.

Crispin Odula ambaye aliwahi kuicheza Azam FC huko nyuma, amesajiliwa baada ya kocha Hemedy Morocco kutoa maagizo kwa uongozi kwamba kiungo huyo wa kikenya anahitajika kwenye timu yake. Akiwa na malengo ya kumtumia Odula, Jerry Santo na Haruna Moshi Boban katika kuunda safu imara ya kiungo ya timu hiyo.

Mkurugenzi wa ufundi wa Wagosi wa Kaya Nassor Ahmed 'Binslum' mwenye kofia akiwa na kiungo mshambuliaji kutoka Bandari ya Mombasa aliyesaini kuungana na kikosi cha Coastal Union CRISTIN ODULA (katikati), kulia ni mwakilishi wa Coastal Union jijini Mombasa Kenya ndugu Hussein Tawakkal.

WACHEZAJI MAKINDA WAWILI WA TANZANIA WAENDA KUJIFUNZA SOKA QATAR KWENYE ACADEMY YA KIMATAIFA YA ASPIRE

Wachezaji wawili kutoka Tanzania wamechaguliwa miongoni mwa 50 waliofanyiwa majaribio nchini Uganda kwa ajili ya kuingia katika kituo cha kuendeleza vipaji (centre of excellence) kilichoko Doha nchini Qatar kupitia mpango wa kukuza vipaji wa Aspire Football Dream.
Abdulrasul Tahir Bitebo (15) ambaye ni mshambuliaji kutoka Kituo cha Uwanja wa Karume, na Martin Omela Tangazi (14) ambaye ni beki kutoka Kituo cha Ukonga ndiyo waliochaguliwa kutoka Tanzania kuingia katika kituo ambapo watakaa kwa mwezi mmoja kabla ya kusaini mkataba rasmi wa kuendelezwa.

Wachezaji wengine walikuwa wakitoka katika nchi za Uganda na Kenya. Mchezaji mwingine aliyefuzu katika nafasi tatu zilizokuwepo ni kutoka nchini Kenya.

Mpango wa Aspire Football Dream unafadhiliwa na Mtoto wa Mfalme wa Qatar katika nchi 16 duniani, na kwa hapa nchini uko chini ya Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

TFF ina jumla ya vituo 14 vya kuendeleza vipaji kupitia mpango huo wa Aspire Football Dream. Vituo hivyo ni Karume, Kigamboni, Tandika, Kawe, Ukonga, Kitunda, Mbagala, Magomeni, Makongo, na Tabata vilivyo katika Mkoa wa Dar es Salaam. Vingine ni Bagamoyo kilichopo mkoani Pwani, Morogoro, Arusha na Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kituo kingine cha kuendeleza vipaji (centre of excellence) cha Aspire kipo Dakar nchini Senegal.

TFF KUENDESHA KOZI SITA KATI YA JULAI- SEPTEMBA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litaendesha kozi sita tofauti za mpira wa miguu kati ya Julai na Septemba mwaka huu.

Kozi hizo ni FIFA 11 For Health itakayofanyika Hombolo mkoani Dodoma kuanzia Julai 8 hadi 19 mwaka huu. Julai 6 hadi 15 mwaka huu kutakuwa na kozi ya mpira wa miguu wa ufukweni (Beach Soccer) itakayofanyika jijini Dar es Salaam.

Waamuzi wa FIFA nao watakuwa na kozi itakayofanyika kati ya Agosti 22 hadi 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati kozi ya ukocha kwa ajili ya Copa Coca-Cola itafanyika jijini Dar es Salaam kati ya Agosti 12 na 17 mwaka huu.

Vilevile kutakuwa na kozi ya mpango wa grassroots unaolenga wachezaji mpira wa miguu (wasichana na wavulana) wenye umri kuanzia miaka 6-12 itafanyika kuanzia Septemba 9 hadi 13 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati tamasha (festival) la grassroots litafanyika Uwanja wa Karume, Septemba 14 mwaka huu.

RCL KUKAMILISHA HATUA YA NNE JUMAPILI
Mechi za marudiano za hatua ya nne ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) zitachezwa Jumapili (Juni 30 mwaka huu) kwenye viwanja vya Sokoine jijini Mbeya, na Kambarage mjini Shinyanga.

Friends Rangers ya Dar es Salaam ambayo katika mechi ya kwanza ilifungwa nyumbani mabao 3-0 itakuwa mgeni wa Stand United FC mjini Shinyanga wakati Kimondo SC itaikaribisha Polisi Jamii ya Mara jijini Mbeya. Katika mechi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.

Hatua ya mwisho ya RCL itachezwa Julai 3 mwaka huu kwa mechi za kwanza wakati zile za marudiano zitafanyika Julai 7 mwaka huu. Timu tatu za kwanza zitapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao.

OFFICIAL: GOLIKIPA WA ZAMANI WA SIMBA AJIUNGA NA YANGA KWA MKATABA WA MIAKA MIWILI

Aliyekuwa golikipa wa timu ya Simba, Azam na Mtibwa Deogratius Munishi maarufu kama Dida amejiunga rasmi na klabu bingwa ya Tanzania bara - Dar Young African.
 
Kwa mujibu wa mmoja wa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga Abdallah Bin Kleb ni kwamba Dida amesaini mkataba wa kuitumikia Yanga kwa miaka miwili akiwa 'free agent' (mchezaji huru).
 
Dida ambaye alisajiliwa na Azam akitokea Mtibwa na kuweza kujijengea nafasi katika kikosi cha kwanza cha AZAM kabla ya miezi kadhaa iliyopita kusimamishwa na wachezaji wenzie Erasto Nyoni, Said Morad, Aggrey Morris kwa tuhuma za kupokea mlungura na kusababisha timu yao kufungwa na Simba katika mchezo wa raundi ya kwanza wa ligi kuu msimu uliopita.
 

VIDEO: SPAIN WAITANDIKA ITALIA KWA 7-6 - WAENDA FAINALI KUCHEZA MECHI YA KIHISTORIA DHIDI YA BRAZILHIGHLIGHTS ZA MECHI HII ILIYODUMU KWA DAKIKA 120
ملخص المباراة + الوقت الاضافي ... اسبانيا x... by kooralive

ANGALIA PENATI ZOTE 14
España vs Italia penalties by Samu30000

HIGHLIGHTS FUPI + PENALTIES
Spain vs Italy MATCH HIGHLIGHTS + PENALTIES by footballdaily1

EXCLUSIVE: JUMA KASEJA AZUNGUMZA KWA MARA YA KWANZA BAADA YA KUTEMWA NA SIMBA - HAJAPEWA TAARIFA RASMI NA SIMBA....
Siku moja baada ya klabu ya Simba kupitia mwenyekiti wa kamati ya usajili Zacharia Hans Pope kuthibitisha kwamba golikipa mkongwe wa timu hiyo Juma Kaseja hatoongezewa mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo aliyoichezea kwa takribani miaka 10, leo hii mtandao huu umepata nafasi ya kuongea na Juma Kaseja kutaka kujua anazungumziaje uamuzi huo wa Simba.

Kaseja ambaye ni golikipa namba moja wa timu ya taifa ya Tanzania kwa sasa yupo kwao mjini Kigoma alipoenda kupumzika baada ya kumaliza majukumu yake timu ya Taifa hivi karibuni, amezungumza na mwandishi wa mtandao huu Johnson Matinde akiwa kwao Kigoma kuhusu mustakabali wake wa soka baada ya kutemwa na Simba pamoja na mambo mengine.

Juma Kaseja akijifua na vijana wadogo mkoani Kigoma wanaotaka kufuata nyayo zake.

Akizungumzia kuhusu suala la kutoongezewa mkataba mpya na Simba, Juma Kaseja alisema kwamba taarifa hizo yeye amezisikia kwenye vyombo vya habari kama watu wengine walivyosikia na hajapata taarifa rasmi: "Jana nikiwa natokea Tanga nilipokuwa nikapata taarifa za kuhusu masuala yangu na Simba. Klabu kupitia viongozi wake imeshaongea kuhusu suala hili na mie itafika siku nitaongelea kwa kina kuhusu jambo hili, ila kwa sasa ni kweli mimi sio mchezaji wa Simba na nisingependa kuzungumzia kuhusu wao."

Akizungumzia kuhusu mustakabali wake wa soka baada ya kuachana na Simba, Kaseja alisema: "Mimi ni mchezaji mpira, hii ndio kazi yangu hivyo nitaendelea kucheza mpira. Sasa kama unavyoniona nipo hapa kwetu nafanya mazoezi ili niwe bora kwenye kazi yangu. Mengine kuhusu ni timu gani nitachezea msimu ujao ningependa tuyaache kwa sasa, utakapofikia muda muafaka wa kuzungumzia then nitaongelea jambo hilo."

Kaseja akiwa mjini Kigoma amekuwa akijifua kwenye uwanja wa Shule ya msingi Kaluta, shule ambayo Juma Kaseja alisoma na uwanja wa shule hiyo ndio ambao alianzia career yake ya soka na ndio maana kila anapokwenda mapumzikoni nyumbani kwao Kigoma hupenda kufanya mazoezi uwanjani hapo na baadhi ya wachezaji chipukizi.

Thursday, June 27, 2013

MIAKA 10 YA KIFO CHA MARC VIVIEN FOE PART 1: SERIKALI YA CAMEROON YAWAKERA WANANCHI KWA KUAHIRISHA MAADHIMISHO KUPISHA MKUTANO WA KISIASA
Tarehe 26 mwezi Juni mwaka 2013, ilitimia miaka kumi tangu kufariki kwa mchezaji wa Kimataifa wa Cameroon Marc Vivien Foe, aliyeanguka uwanjani wakati wa mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FIFA la Mabara mwaka 2003 nchini Ufaransa.

Serikali ya Cameroon hata hivyo iliahirisha shughuli kubwa iliyoandaliwa kwa ajili ya kumbukumbu ya kifo chake, hatua ambayo imezua malalamiko ya wananchi wengi wanaodai kupuuzwa kwa mchezaji huyo.

Amekuwa ni mtu mwenye kuenziwa kwa kiwango cha juu kuanzia FIFA hadi vilabu alivyovitumikia wakati wa uhai wake hususani timu za Olympic Lyon, West Ham United na Manchester City.Kifo cha Foe kiliamsha taharuki kubwa Duniani hasa kwa kuzingatia kilitokea kwenye michuano mikubwa na wakati ambapo Cameroon ilikuwa na mashabiki lukuki kutokana na ubora wa timu yao.

Serikali ya Cameroon ilipanga maadhimisho makubwa ya kumkumbuka Foe akitimiza miaka kumi kaburini hivi leo na maandalizi yote yalikwisha kamilika, lakini imeahirisha na kusogeza mbele hadi mwezi ujao kwa ajili ya kupisha Mkutano Mkuu wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika Magharibi na Afrika ya Kati ulioanza jumatatu wiki hii Jijini Yaunde.

Wananchi wa nchi hiyo wameghadhibishwa na kitendo hicho na baadhi yao wamenukuliwa wakisema kuwa Rais Paul Biya na Serikali yake wameshindwa kuonyesha heshima inayomstahili marehemu Foe. Taarifa ya Serikali imesema kuwa Imeandaa shughuli hiyo kwa wiki nzima kuanzia Julai 20 hadi 27 itakayofanyika kwenye kituo kilichopewa jina la mchezaji huyo katika eneo la Nkomo-Okoui, Jijini Yaunde.

Marc Vivien Foe alikufa kutokana na mshituko wa moyo katika mchezo dhidi ya Colombia na kifo chake kimechukuliwa kama fundisho kwa wadau wa mpira wa miguu duniani kuhakiki afya za wachezaji na hasa vipimo vya moyo kila wakati.

Jambo hilo bado linasugua vichwa vya watafiti wa afya na bado hakuna majibu ya moja kwa moja ya kwa nini wachezaji wanakufa viwanjani kwa matatizo ya moyo ilhali wanapimwa afya zao ipasavyo. Wengi bado wanakumbuka mkasa uliompata mchezaji wa ligi kuu ya England Fabrice Muamba aliyezimia kwa siku kadhaa baada ya kuanguka uwanjani kutokana na matatizo ya moyo, Muamba alisalimika na amejiuzulu kucheza mpira kabisa licha ya umri wake mdogo wa miaka 23.

Rekodi zinaonyesha kuwa tangu mwaka 2003 wanasoka 38 wamekufa viwanjani kutokana na kutatizwa na moyo akiwemo Alen Pamic wa Croatia aliyekufa Ijumaa ya wiki iliyopita baada ya moyo wake kusimama ghafla.

Jamii ya wapenda soka duniani imeendelea kumkumbuka na kumuenzi Foe kwa matukio mbalimbali na mwezi Mei mwaka huu, Mchezaji wa Kimataifa wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang alishinda tuzo ya Marc Vivien Foe inayotolewa kwa mchezaji bora kutoka Afrika miongoni mwa ambao wanacheza ligi kuu ya Ufaransa.

Barabara jirani na ulipo uwanja alipofia Stade de Gerland mjini Lyon imepewa jina lake wakati mjini Lens huko huko Ufaransa Mtaa unaolekea uwanja mkubwa wa soka Stade Bollaert umebatizwa jina lake pia. Kadhalika kwenye uwanja wa City of Manchester umejengwa mnara mdogo kwa ajili ya kumbukumbu yake.

Kijana mmoja mjini Garoua nchini Cameroon ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa Simba huwa hafi bali anasinzia tu, akimaanisha kwamba Wacameroon bado wapo na kipenzi chao Marc Vivien Foe wanayeamini kuwa amesinzia tu.

EDIBILY LUNYAMILA, MOHAMED HUSSEIN MMACHINGA WARUDI DIMBANI


Timu ya wachezaji wakongwe waliowahi kutikisa katika soka la Tanzania - Wakongwe FC wameunda timu ambayo imeingia kwenye kombe la mchangani linaloitwa Beira Cup linalofanyika viwanja vya Beira maeneo ya Kigogo hapa jijin dar es salaam.


Timu hiyo inaundwa na wachezaji wengi wa zamani kama vile Mtwa Kihwelu, Jemedari Said Kazumali mshambuliaji wa zamani wa kariakoo ya lindi, 82 Rangers ya Shinyanga na JKT Ruvu ambaye kwa sasa ni meneja Azam, kiungo wa zamani wa Ushirika ya Moshi na Yanga Steven Nyenge, winga wa zamani wa biashara ya Shinyanga, Yanga, Simba na Malindi Edibily Lunyamila, mshambuliaji wa zamani wa Bandari ya Mtwara, Yanga na Simba Mohamed Hussein 'Mmachinga', kiungo wa zamani wa Simba George Lucas "Gazza", Ally Yusuf 'Tigana', Ngade Chabanga, Bakari Idd, Benny Mwalala, mshambuliaji wa zamani wa Cosmopolitan ya jijini Dar Shaffih Dauda, kiungo wa zamani wa Miembeni ya Zanzibar Ibrahim Masoud 'maestro' na wengineo kibao

 Kutoka kushoto: Steven Nyenge,Dauda na Mohamed Hussein' Mmachinga'

Timu hii ya Wakongwe FC jana ilicheza mechi yake ya kwanza na kuifunga Young Kids ya Tabata kwa bao 1-0 - goli lilofungwa na Ben Mwalala.
Shaffih Dauda na Lunyamila

OFFICIAL: ISCO ASAINI MKATABA WA MIAKA 5 KUJIUNGA NA REAL MADRID.

Klabu ya Real Madrid imedhibitisha kumsajili kiungo mshambuliaji Isco kutoka klabu ya Malaga kwa mkataba wa miaka mitano.
Real Madrid imetangaza taarifa hizi kupitia kwenye tovuti yake na kusisitiza kilichobaki sasa ni kufanyiwa vipimo vya afya.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 alikuwa pia anawaniwa na klabu ya Manchester City inayonolewa kwasasa na kocha wake wa zamani Manuel Pellegrini aliyekuwa Malaga.

YANGA YAPANGA KWENDA KANDA YA ZIWA KUJIANDAA KUTETEA UBINGWA WAO WA VODACOM

Timu ya Young Africans inatarajiwa kwenda kanda ya Ziwa mwishoni mwa wiki ijayo kwa ajili ya kucheza michezo ya kirafiki ya kujiandaa na maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu 2013/2014, ambapo itatumia fursa hiyo kuwaonyesha  kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom na kusherehekea pamoja na wpenzi, washabiki na wanachama wake.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga, mkurugenzi wa kampuni ya Nationwide ambao ndio waandaji wa ziara hiyo Frank Pangani amesema wao wanatumi afurs ahiyo kwa wakazi wa kanda ya ziwa kupata fursa ya kuwaona wachezaji wa Yanga wakiwa na kombe lao la Ubingwa wa Vodacom pamoja na kushuhudia michezo ya kirafiki ya kimataifa.
Naye Afisa Habari wa klabu ya Yanga Baraka Kizuguto amesema ziara hiyo wataitumia kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom, wanachama na wapenzi wa Yanga kuliona kombe la Ubingwa ikiwa ni pamoja na kucheza michezo ya kirafiki ambayo mwalimu ataitumia kwa ajili ya kukiandaa kikosi chake.
Ziara ya Mabingwa au Champions Tour ni tukio la kila mwaka linalowahusishwa mabingwa wa soka wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na mabingwa wa soka waalikwa wa kutoka nchi jirani za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na pia timu alikwa ya nyumbani. 
Mara ya kwanza tukio hili lilifanyika mwaka jana 2012, kwa bingwa wa Tanzania Bara wa msimu uliopita, timu ya Simba Sports Club (SSC) ya Dar Es Salaam kushiriki ziara hiyo kucheza na mabingwa wa Uganda wa msimu uliopita timu ya The Express ya Kampala na Toto African ya Mwanza.
Mwaka jana 2012 ziara hiyo ya mabingwa ilifanyika katika mikoa ya Mwanza (Uwanja wa CCM Kirumba), Simba ilicheza na Toto African ya Mwanza, Shinyanga (Uwanja wa CCM Kambarage) Simba vs Express, na Dar Es Salaam (Uwanja wa Taifa) Yanga vs Express na Simba vs Express.
Mwaka huu 2013 itakuwa ni mara ya pili kwa tukio hili la Ziara ya Mabingwa kufanyika chini ya uandalizi wa taasisi ya michezo ya Natiowide Entertaiment Centre (NEC) yenye makao yake jijini Mwanza.
Ziara ya Mabingwa mwaka huu wa 2013 itawahusisha mabingwa wa Tanzania Bara, Young Africans Sports Club (YASC) ya Dar Es Salaam na waalikwa mabingwa wa mwaka huu wa Uganda timu kongwe na mashuhuri  ya Kampala City Council (KCC) ya jijini Kampala na pia timu alikwa ya ndani inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo itatangazwa ndani ya muda wa siku mbili kutoka leo.
Mechi za Ziara ya Mabingwa mwaka huu wa 2013 zitachezhwa katika mikoa ya Mwanza (CCM Kirumba) Jumamosi 06/07/2013 Yanga vs KCC, Shinyanga (CCM Kambarage) Jumapili 07/07/2013 Yanga vs KCC marudiano, na Tabora (Ali Hassan Mwinyi) Alhamisi 11/07/2013 Yanga vs timu ya nyumbani itakayotangazwa siku mbili zijazo. Baada ya mechi hizo ziara hiyo inatarajiwa kuendelea katika mikoa itakayotanagazwa baadae.
Nationwide Entertainment Centre pia inazishukuru timu zote zinazoshiriki ziara hii ya mabingwa kila mwaka wakiwemo mabingwa wa msimu huu Yanga na mabingwa wa msimu uliopita watani wao wa jadi Simba ambao wametoa ushirikiano mkubwa, na wadhamini wa mwaka huu Kilimanjaro Premium Lager na vyombo vya habari.
Source: http://youngafricans.co.tz

MJADALA:NINI MAONI YAKO BAADA YA UONGOZI WA SIMBA KUTANGAZA KUTOMSAJILI TENA JUMA KASEJA!

Nahodha wa Taifa Stars Juma Kaseja akiwa na kocha wa timu hiyo Kim Poulsen.

Wednesday, June 26, 2013

OFFICIAL: TEVEZ AKABIDHIWA JEZI YA DEL PIERRO JUVENTUS BAADA YA KUSAINI MKATABA WA MIAKA 3

Mshambuliaji wa kiargentina Carlos Tevez amekamilisha uhamisho wa kujiunga na Juventus kwa ada ya uhamisho ya paunfi millioni 10. Tevez aliwasili leo jijini Turin na moja kwa moja akaenda kufanyiwa vipimo kisha kusaini mkataba wa miaka 3 wa kuitumikia Juventus.

   
Tevez ambaye ni mchezaji wa zamani wa West Ham, Man United na Man City amepewa jezi 10 aliyokuwa akivaa gwiji wa Juventus Alesandro Del Pierro.

BREAKING NEWS: SIMBA WATANGAZA RASMI KUMUACHA JUMA KASEJA

Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa mwenyekiti wa kamati ya usajili Zacharia Hans Pope umetangaza rasmi kuachana na mlinda mlango mkongwe wa timu hiyo  Juma Kaseja.

Akizungumza na kipindi cha Sports Leo cha Radio One, Hans Pope amesema hawatomuongezea mkataba Kaseja na wamempa baraka za kutafuta timu nyingine.

Kwa muda mrefu Simba ilikuwa ikisuasua kumpa mkataba Kaseja aliyeidakia Simba kwa takribani miaka 10, na hatimaye leo wamethibitisha rasmi kumuacha Kaseja.

Kwa hanari zaidi kuhusu suala hili endelea kufuatilia mtandao huu.

Makumbusho mabingwa Airtel Rising Stars Kinondoni

Nahodha wa timu ya Makumbusho United Hamza Mohamed akipokea kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, kutoka kwa Ofisa Maendeleo wa TFF Bw. Salum Madadi baada ya kuibamiza timu ya Mtakuja 5-1 katika mchezo wa mwisho wa mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 uliofanyika kwenye uwanja wa Mwanyamala shule ya msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 25, 2013.
 

Nahodha wa timu ya Makumbusho United Hamza Mohamed akinyanua juu kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, baada ya kuibamiza timu ya Mtakuja 5-1 katika fainali ya mashindano hayo ngazi ya mkoa iliofanyika kwenye uwanja wa Mwanyamala shule ya msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 25, 2013.

Wachezaji wa timu ya Makumbusho United wakishangilia baada ya kutwaa kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, kwenye uwanja wa Mwanyamala shule ya msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 25, 2013. Makumbusho walishinda 5-1 dhidi ya Mtakuja.
 

Baadhi ya mashabiki wa kishangilia timu zao katika michuano ya Mkoa ya Airtel Rising star 2013

Timu ya Makumbusho United imetawazwa kuwa mabingwa wa Airtel Rising Stars mkoa wa kisoka wa Kinondoni baada ya kuwafunga bila huruma Mtakuja Beach 5-1 katika mchezo wa fainali wa mashindano hayo ya vijana chini ya umri wa miaka 17. Mchezo huo ulifanyika kwenye kiwanja cha shule ya Msingi Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo Juni 25 ,2013.

Mabingwa hao wapya wa ARS ngazi ya mkoa walianza michuano hiyo kwa kishindo walipoitandika Sifa United 3-1 katika mchezo wa ufunguzi uliopigwa katika uwanjwa huo huo Jumapili. Katika mchezo wa leo, Makumbusho wamepata magoli kupitia kwa Premji Stephano (dk 12), Ally Amin (dk 35), Rashid Ngone (dk 38 na 71) na  Wllie Kalolo (dk 53) wakati Mtakuja walipata goli la kufutia machozi dakika ya 78 kwa njia ya penati iliyopigwa na Steven Munyu.

Jijini Mbeya, timu ya Mbasco ilitoshana nguvu na timu ya Mbosa Jumatatu Juni 24 baada ya kutoka sare ya 3-3 katika mchezo wa vuta nikuvute wa Airtel Rising Stars. Mbasco walipata magoli yao kupitia kwa Jasco Mwaibabe (dk 20 na 50) na Joel Kasimila dakika ya 68. Mchezo huo ulifanyika kwenye kiwanja cha Magereza Mbeya.
Kwa upande wao, Mbosa walipata magoli yao kupitia kwa Michael Mwashilanga (dk 5), Richard Kalinga (dk 49) na Enock Chikaonga (dk 9).

Mjini Morogoro; timu ya Moro kids iliishinda Anglikana 3-0 katika mchezo mwingine wa Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya seconday ya Morogoro. Magoli ya Moro kids yaliwekwa kimiani na Abdul Rashid, Robert Nashon na Evans Nashon. Robert na Evans ni mapacha.

Katika mkoa wa kisoka wa Ilalan, Msimamo Youth Academy walipata ushiindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Buguruni Youth Center katika mchezo mgumu iliofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam. Goli hilo la ushindi lilifungwa dakika za majeruhi na nahodha wa timu hiyo Rajab Mohamed katika dakika ya 89

Mkoa wa kisoka waTemeke ulitarajiwa kuanza mechi zake za Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa jana (leo) katika uwanja wa Twalipo na mkoa wa Mwanza vile vile ulitarajia kuanza mechi zake kwenye uwanja mkongwe wa Nyamagana jana (leo). 

Programu hii ya Airtel Rising Stars ni ya Afrika nzima likiwa na lengo la kuendeleza na kukuza  mpira wa miguu katika bara la Afrika kwa vijana wanaochipukia waweze kupata nafasi ya kuendeleza vipaji vyao.

Fainali za ARS Taifa vile vile zitatumika kuchagua timu bora za wavulana na wasichana ambao wataiwakilishaTanzania katika mashindano ya kimataifa ambapo nchi mwenyeji wa michuano hiyo itatangazwa mwezi ujao. Wachazeaji wengine watachaguliwa kwenda kwenye kliniki itakayoendeshwa na makocha kutoka klabu maarufu duniani ya Manchester United

ZINEDINE ZIDANE ATEULIWA KOCHA MSAIDIZI WA REAL MADRID - ATAMBULISHWA PAMOJA NA CARLO ANCELOTTI


Real Madrid wamemtambulisha rasmi kocha wao mpya Carlo Ancelotti na pia wametangaza kwamba Zinedine Zidane na Paul Clement watakuwa ndio makocha wasaidizi.

Ancelotti alitambulishwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu na raisi wa klabu hiyo Florentino Perez mapema leo mchana.
 
Ancelotti atasaini rasmi mkataba wa miaka mitatu na Madrid July 3 akitokea Paris St Germain.

WAKATI WACHEZAJI WENGINE WAKILA BATA IBIZA - DEMBA BA AENDA KUFANYA IBADA MAKKA NA MEDINAMAANDALIZI YA SOKA LA UFUKWENI YAZIDI KUPAMBA MOTO - VIWANJA VYAANZA KUTENGENEZWA

Maandalizi ya mradi wa Tanzania Beach Soccer unaoratibiwa na kampuni ya Prime Promotion kwa kushirikiana na shirikisho la soka nchini TFF yanaendelea vizuri sana.
Kwa mujibu wa mwakilishi wa Primetime Promotion Shaffih Dauda ni kwamba sasa mradi huo umefikia katika hatua nzuri ya ujenzi wa viwanja vitakavyotumika katika michuano ya mchezo huo.
"Kwa sasa tumeanza kazi ya kutengeneza viwanja pembezoni mwa ufukwe wa bahari hindi katika eneo la Mikocheni ulipo mgahawa wa Escape 1. Tunashukuru ushirikiano mzuri tunaopata kutoka kwa TFF chini ya mkurugenzi wa ufundi Sunday Kayuni. Kama maandalizi na mipango yote ikienda kama ilivyopangwa tunategemea michuano hii itaanza mwishoni mwa mwaka huu."


Utengenezaji wa viwanja ukiendelea Mikocheni pembezoni mwa bahari ya Hindi.

EXCLUSIVE INTERVIEW: AMRI KIEMBA

CHEMSHA BONGO: HUYU NI MCHEZAJI GANI WA LIGI KUU YA ENGLAND ANAYECHEZEA KLABU ILIYOPO KWENYE BIG 4


PAMOJA NA TISHIO LA USALAMA - KAGAME CUP YAENDELEA HUKO DARFUR - TIMU ZA RWANDA, UGANDA, SUDAN, DJIBOUT NA BURUNDI ZASHIRIKI I


Mashindano ya kandanda ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati ya kuwania kombe la Kagame yameingia robo fainali nchini Sudan sehemu ya Darfur Kaskazini na Kordofan Kusini.
Mashabiki wakiwa uwanjani kuangalia mojawapo ya mtanange wa CECAFA Kagame Cup

Jumatano wiki hii Express ya Uganda inapimana nguvu na APR ya Rwanda kisha wenyeji Al Ahly Shandy dhidi ya Al Merreikh ya kutoka El Fashir, mji mdogo ambao una uwanja wa kimataifa wa ndege pamoja na viwanja vya kisasa vya voliboli, mpira wa kikapu na kandanda.
 
Mechi hiyo ya wenyeji inasubiriwa kwa hamu. Al Merreikh ina mashabiki wengi na wachezaji kadhaa wa nje baadhi yao Joseph Kabagambe ambaye ni mchezaji kutoka Uganda wa kiungo cha kati na Adam Williams wa Nigeria. Mchezaji mwingine wa Nigeria David Nwosu anayechezea Merreikh hatacheza kwa sababu ya kuonyeshwa kadi mbili za manjano..
Kabla ya mechi jioni ya saa 10 mashabiki wanapata nafasi ya kushiriki swala ya Alsir

Alhamisi wiki hii Vital'O ya Burundi inapepetana na Ports ya Djibouti mechi ya kwanza ya robo-fainali, na ya pili ni kati ya Rayon ya Rwanda na URA ya Uganda. Mechi za nusu-fainali ni Ijumaa na Jumamosi kisha Julai tarehe mosi ni mechi ya fainali.


BAADA YA KUSHINDWA KUIPELEKA CONGO BRAZIL 2014 - KOCHA LEROY AJIUZULU

Claude LeRoy ameachia ngazi kama kocha wa timu ya taifa ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Kocha huyo kutoka Ufaransa mwenye umri wa miaka 65 alichukua wadhifa huo wa kuifundisha timu ya Congo kwa mara ya pili mwezi Septemba mwaka 2011.

"Niliwambia wachezaji wangu kwamba nitaachia ngazi baada ya miaka miwili," alisema Le Roy, ambaye mechi yake ya mwisho ilichezwa jumapili iliyopita dhidi ya Cameroon. Timu mbili zilitoka sare ya bila kufungana, katika mechi za mchujo wa kutafuta tiketi ya fainali za kombe la dunia.

Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DR Congo haitafuzu katika fainali za kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014 na kama ilivyotarajiwa Timu ya taifa ya Cameroon ilipewa alama tatu baada ya Togo kukiri kwamba mapema mwezi huu ilimtumia mchezaji ambaye hakuruhusiwa kucheza.

LeRoy alisaidia Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo kufuzu kwenye fainali za kombe la mataifa ya bara la Afrika mwaka 2013 nchini Afrika kusini, lakini ikashindwa kuvuka hatua ya makundi licha ya kutopoteza mechi hata moja.

Ni kwa mara ya saba LeRoy akisaidia timu kufuzu kwenye fainali za kombe la Afrika baada mafanikio yake akiifundisha Cameroon na kunyakua kombe hilo mwaka 1988. Pia alizifundisha Senegal na Ghana.

KALI YA LEO: (VIDEO)GOLIKIPA WA BARCELONA U14 ADAKA PENATI SITA DHIDI YA ATLETICO NA KUIPA KOMBE TIMU YAKE (VIDEO)

MKATABA MNONO WA CHELSEA NA ADIDAS WAMPA MOURINHO MSULI WA KUPAMBANA KWENYE SOKO LA USAJILI BILA KUHOFIA 'FINANCIAL FAIR PLAY'

JOSE MOURINHO amewashiwa taa ya kijani ya kuanza kufanya balaa kwenye usajili baada ya Cheslea kusaini mkataba mnono wa £300million na kampuni ya utengenezaji wa mavazi ya kawaida na kimichezo ya adidas.

Mkataba wa miaka 10 baina ya Chelsea na Adidas ndio unaoshika nafasi ya kwanza kwa thamani baina ya klabu na kampuni ya utengenezaji jezi za klabu husika.

Mkataba huo umeondoa wasiwasi wa Chelsea kuvunja sheria za  Financial Fair Play.
Dili hilo la Chelsea na Adidas limevunja rekodi ya dili la Manchester United na Nike lilokuwa na thamani ya  £287m ambalo lilisainiwa miaka 13 iliyopita na linaisha mwaka 2015. 

Mkataba unamaanisha Chelsea hawatokuwa wakimtegemea zaidi Abramovich kuvunja benki katika kuiwezesha timu hiyo.
Mkataba uliopita na Adidas ulisainiwa mwaka 2006 ulikuwa na thamani ya £20million kwa mwaka.

LIVERPOOL WAENDELEZA VURUGU KWENYE USAJILI: WAKAMILISHA USAJILI WA MCHEZAJI WA NNE - GOLIKIPA MIGNOLET WA SUNDERLAND

Liverpool wamekamilisha usajili wa nne katika dirisha hili la usajili baada ya kutangaza kukamilisha usajili wa golikipa Simon Mignolet kutoka Sunderland kwa ada ya uhamisho ya £9million.

Golikipa huyo amekuwa akitamaniwa na Brandan Brendan Rodgers kwa muda mrefu, na sasa anatajwa kuja kuchukua nafasi ya kwanza kwenye kikosi cha Liverpool mbele ya Pepe Reina.
 

Tuesday, June 25, 2013

ANDRE SCHURRLE - MCHEZAJI WA KWANZA KUSAJILIWA NA MOURINHO CHELSEA MSIMU HUU - ANGALIA UWEZO WAKE

Jose Mourinho amefungua rasmi akaunti ya Chelsea na kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kijerumani ANDRE SCHURRLE - ambaye leo hii amefaulu vipimo vya afya na kujiunga rasmi na Chelsea akitokea Bayern Leverkusen.

Chelsea wamempa mjerumani huyo mkataba wa miaka mitano, na kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Jose Mourinho tangu arejee kutoka Santiago Bernabeu mapema mwezi uliopita.

Schurrle, 22, alisema: “Nina furaha kusajili hapa. Ni heshima kubwa kwangu kuichezea klabu hii, ninaangalia mbele kuitumikia timu hii.”

Schurrle ana uwezo wa kucheza aidha kama winga au mshambuliaji wa kati akiungana na wachezaji wengine kama  Juan Mata, Eden Hazard, Oscar na Kevin De Bruyne katika kugombea nafasi ya kuwemo katika kikosi cha kwanza cha Mourinho. 

Schurrle amepewa jezi namba 14.

ANGALIA MAVITU YAKE KWENYE VIDEO HII HAPA CHINI

ETHIOPIA WANYANG'ANYWA POINTI NA KUWEKA REHANI NAFASI YA KUFUZU KOMBE LA DUNIA - KATIBU MKUU WA SHIRIKISHO ATIMULIWA

Shirikisho la soka nchini Ethiopia limemfukuza kazi katibu mkuu wake siku ya jumatatu baada ya taifa hilo kukumbwa na skendo iliyothibitishwa ya kuchezesha mchezaji asiyestahili kwenye mechi ya za mashindano ya kufuzu kombe la dunia, kosa ambalo limewagharimu kukatwa pointi 3. 
 
Shirikisho hilo lilifanya mkutano na kupiga kura ya kumtimua  Ashenafi Ejigu lakini wakaikataa barua ya kujiuzulu ya makamu wa raisi wa shirikisho hilo Berhanu Kebede, ambaye huko nyuma nae aliingizwa kwenye mkenge wa lawama. 


Baadhi ya wajumbe wa shirikisho na waandishi waliokuwepo kwenye mkutano huo walitaka uongozi mzima wa shirikisho hilo uondolewe. 


Sahilu Gebremariam, Raisi wa shirikisho hilo, alisema kwamba alikuwa anajiandaa kutuma barua ya kujiuzulu katika uchaguzi ujao wa kugombea siti katika kamati kuu ya shirikisho hilo. 

 
"Hili ni kosa kubwa kutokea kwenye soka, hivyo inabidi viongozi wote tuwajibike kwa makosa haya kwa kujiuzulu," Sahilu aliiambia Reuters. "Lakini tuna majukumu mengine mbele yetu hivyo ikaamuriwa tubaki mpaka September."


Ushindi wa Ethiopia wa 2-1 dhidi ya South Africa jijini Addis Ababa katika mechi ya June 16 uliwapa Ethiopia uongozi wa pointi 5 kwenye kundi lao ambazo zisingeweza kufikiwa na timu yoyote hivyo wakawa wamefuzu rasmi kwenda kwenye hatua ya mtoano kwa ajili ya kufuzu kwenda michuano ya kombe la dunia 2014 nchini Brazil.


Lakini masaa kadhaa baadae, FIFA ikasema kwamba inachunguza tuhuma za Ethiopia kumchezesha mchezaji ambaye alikuwa kasimamishwa - kiungo Minyahile Beyene ambaye alicheza kwenye mechi dhidi ya Botswana  June 8.


Minyahile alikuwa na kadi mbili za njano katika mechi zilizopita za kufuzu, na sheria za World Cup zinasema kwamba mchezaji ambaye amepewa kadi mbili za njano kwenye mechi zilizopita za kufuzu anapaswa kutokucheza mechi moja inayofuatia.

 
Alionyeshwa kadi ya njano kwenye mchezo wa sare ya 1-1 dhidi ya South Africa mwaka mmoja uliopita na mara nyingine alionyeshwa kwenye mechi ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Botswana mwezi March mwaka huu.


Ethiopia, ambao hawajawahi kufuzu fainali za kombe la dunia, wanategemewa kunyang'anywa pointi 3 hivyo kumaanisha kwamba nafasi ya kusonga mbele kwenye kundi lao (A) sasa imebaki wazi.


Maofisa wa Ethiopia walisema kwamba walikosea kumchezesha mchezaji kwa bahati mbaya. Makamu wa Raisi wa shirikisho Berhanu, ambaye pia alikuwa kiongozi wa timu wakati wa mechi dhidi ya Botswana, alisema kwamba walipoteza barua ya FIFA ya kuwataarifu kuhusu kadi za Minyahile.


Ikiwa Ethiopia watanyang'anywa pointi 3 basi watabakia na pointi 10, huku South Africa wakiwa na 8, na Botswana wakiwa 7 - huku kila timu ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Ethiopia watacheza mechi yao ya mwisho na  Jamhuri ya Afrika ya Kati mwezi wa tisa tarehe 6, wakati South Africa watatimbana na Botswana.