Search This Blog

Saturday, November 24, 2012

STARS WAANZA MAZOEZI - SAMATTA NA ULIMWENGU BADO HAWAJAFIKA KAMBINI

Kipa wa Kilimanjaro Stars, Juma kaseja akitoka Uwanja baada ya
kumalizika kwa mazoezi yaliyofanyika katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha
Kampala Kampasi ya biashara nchini Uganda jana. Stars inadhaminiwa na
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager
Mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars, Edward Christopher
akikokota mpira wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika Uwanja wa Chuo
Kikuu cha Kampala Kampasi ya Biashara nchini Uganda jana kwa kujianda
na mchezo wa michuoano ya Cecafa. Stars inadhaminiwa na Bia ya
Kilimanjaro Premium Lager

Wachezaji wa Kilimanjaro Stars wakitoka Uwanjani baada ya kufanya
mazoezi katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya Biashara
nchini Uganda jana. Stars inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium
Lager


Na mwandishi wetu,
Kampala

Kocha wa Timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen amesema
ana imani na timu yake itakayotupa karata ya kwanza leo (Jumapili) dhidi ya Sudan katika mashindano ya CECAFA Challenge.

Alisema suala la wachezaji  Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kutofika mpaka sasa halimtatizi kwa kuwa ameiandaa timu vizuri na atawatumia wachezaji waliopo.
 “Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaweza wasicheze katika mechi ya kesho kwa sababu hawajafika lakini mimi nikiwa kocha nimejiandaa vizuri na nina imani na wachezaji waliopo,” alisema.
“Nina imani TFF wanafuatilia suala hili na wachezaji hawa watajiunga na wenzao hivi karibuni lakini hii haituzuii kufanya vizuri kwani tumejiandaa vizuri,” alisema.


Kuhusu wachezaji kama Aggrey Morris, Mohamed Nassoro na Mwadini Ali kutoka Zanzibar kujiunga na wenzao kuichezea Zanzibar Heroes, Poulsen alisema pengo lao halitampa tatizo kwa kuwa ni changamoto.


“Timu hii ambayo inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kwa sasa ina wachezaji wengi chipukizi kwa hivyo huu ndio muda wa kuwapima vizuri kwani kwani  haya ni mashindano makubwa,” alisema.
Alisema wachezaji wote wana hali nzuri na wana ari ya kushinda mechi yao ya kwanza  dhidi ya Sudan ambazi zimo katika Kundi B pamoja na Burundi na Somalia ambazo zitacheza leo pia.


Timu za kundi A zilitarajiwa kucheza jana ambazo ni Kenya dhidi ya Uganda na Ethiopia dhidi ya Sudan Kusini.
Kundi C inajumuisha Zanzibar na Eritrea na Rwanda dhidi ya Malawi.

TAIFA STARS ILIVYOWASILI UGANDA TAYARI KWA CHALENJI CUP


Timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars ikiwasili Katika Uwanja wa
Ndege wa Entebe nchini Uganda jana alasiri tayari kwa mashindano ya
CECAFA Senior Challenge yanayotarajiwa kutimua kivumbi Jumamosi. Stars
inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.


MAMLAKA YA MAPATO YAIFILISI TFF KWA MALIMBIKIZO YA KODI


MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeifilisi akaunti ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kuchukua sh. milioni 300.
TRA imechukua fedha hizo katika akaunti ya TFF iliyopo katika benki ya NMB.

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Sunday Kayuni alisema jana kuwa, TRA imechukua fedha
hizo ili kufidia deni lililotokana na malimbikizo ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) inayotokana na mishahara ya makocha wa timu ya taifa.
Kayuni alisema kuwa, TRA inadai sh. 157, 407, 968 za VAT za mishahara ya aliyekuwa
kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Marcio Maximo na msaidizi wake, Itamar Amorin, Jan Poulsen, Kim Poulsen na Jacob Mitchelsen.
Alisema kwa mujibu wa TRA, mishahara ya makocha hao ilitakiwa kukatwa VAT, lakini
kwa kuwa serikali ndiyo iliyokuwa ikilipa mishahara hiyo, hakuna kodi iliyokatwa.
Kayuni alidai kuwa, TRA imeionea TFF kuchukua fedha hizo, ambazo zilitolewa na
mdhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom.
Alisema serikali ilipaswa kulipa kodi hiyo kwa kuwa ndiyo inayolipa mishahara ya
makocha wa timu za taifa, na siyo TFF, ingawa shirikisho hilo ndilo mwajiri wao.
"Kuchukuliwa fedha hizo kutasababisha mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania Bara
kusuasua, hatutakuwa na fedha za kuzilipa klabu kwa maandalizi ya mechi zake,"alisema Kayuni.
Kaimu Katibu Mkuu huyo alisema TFF inawasiliana na serikali kuijulisha hatua ya TRA,
ingawa mara kadhaa waliwahi kuzungumza nao kuhusiana na jinsi ya kulipa deni hilo. (http://liwazozito.blogspot.com)

HATIMAYE YANGA WAANZA MCHAKATO WA UJENZI WA UWANJA WAO

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuph Manji kulia akisaini hati ya makubaliano ya upembuzi akinifu na Mkurugenzi wa Kampuni ya Beijing Construtcion Geng Hijuan
Klabu ya Yanga leo imesaini makubaliano ya upembuzi akinifu na kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) kutoka nchini China, juu ya mradi wa ujenzi wa Uwanja wa kisasa Kaunda katika eneo la makao makuu ya klabu Jangwani

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuph Manji amesema wamefikia hatua hiyo baada ya kukaa uongozi na kamati ya utendaji na kujadili juu ya hatua hiyo ambayo kampuni ya BCEG itaanza kazi wiki ijayo na pindi itakapokamilisha michoro zoezi litakalofuata itakua awamu ya ujenzi wa uwanja.
Hiki ni kipindi cha kufanya shughuli za kimaendeleo,na hasa kipindi hichi ambacho klabu yetu ipo katika amani na mshikamano kwa viongozi na wanachama, hivyo naamini mara tutakapomaliza suala la uwanja tutaanza pia ujenzi wa jengo lakitega uchumi mtaa wa mafia alisema 'Manji'.
Naye Mkurugenzi wa shirika la BCEG nchini, bwana Geng Hijuan amesema amefurahi kufikia hatua hiyo na klabu ya Young Africans, kazi waliyopewa sasa wataifanya kwa uhakika mzuri na kutoa makadirio halisi juu ya gharama ambazo zitagharimu kufanikisha mradi huo.
Kampuni ya BCEG kutoka nchini China ndiyo iliyojenga uwanja wa Taifa wa kisasa jijini Dar es salaam na sasa ndio waliopewa kazi ya ujenzi wa Uwanja wa kisasa wa Kaunda.
Naye makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga amesema, makadirio ya uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji elfu thelathini (30,000) mpaka elfu arobaini (40,000) kutegemea na wataalam watakavyoona, pia utakua na huduma zote za muhimu katika viwanja vya kisasa.
Manji alisema mategemeo ya Kamati ya Utendaji ni kuanza kujengwa kwa uwanja huo mapema kabla ya mwezi juni mwakani, ambapo desemba 8 mwaka huu watasubiria kupata baraka za wanachama katika mkutano mkuu. (http://www.youngafricans.co.tz)

Friday, November 23, 2012

"FILBERT BAYI NA GULAM HAWANA HATA CHEMBE YA HEKIMA"
Naomba kunukuu MAADILI (CODE OF ETHICS) za IOC wao wamezivunja wazi wazi na kwa vile inaonyesha wazi wazi kwamba maisha yao yanategemea ofisi ya TOC wapo tayari kufanya lolote ili warudi, wale na waishi vizuri kwa mika mingine minne; wakidhani serikali haina mkono mrefu wala jicho lionalo mbali!!.

1). Kwa mujibu wa kitabu cha SPORTS ADMINISTRATION MANUAL lililochapishwa na Olympic Solidrity chini ya uangalizi wa INTERNATIONAL OLYMPIC COMMITTEE toleo la 2010; kuna mambo matatu ambayo mimi ninaona wazi kwamba waheshimiwa hao wamekiuka maadili ya IOC ambayo ni sambamba na maadili ya JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA:

  (A). Dignity: Kuna vipengele sita ambavyo mimi naona vyote vimekiukwa, lakini kipengele cha 6 ambacho kinasema; 
7. The Olympic parties shall guarantee the athletes conditions of safety, well-being and medical
care favourable to their physical and mental equilibrium.
Ninathibitisha kipengele hicho maana HAPAKUWA NA DOCTOR KTK KAMBI ILIYOWEKWA KWENYE HOSTEL YA KATIBU MKUU WA TOC!!. Ndo maana mwanariadha MUSANDUKI MUHAMED aliugua alipofika LONDON kwa kukosa matibabu ya awali ambayo angeyapata wakati akiwa mazoezini. 'Hili ni kosa ambalo limeelezewa kuwa ipo katika "read line which must not be breached"
   (B). Integrity: Kuna vipengele vitano pia, lakini twende katika kipengele cha 3  ambacho kinasema; 3. "Any form of conflict of interest must be avoided". 
Kipengele hicho kinajieleza vizuri na ushahidi wake ni wazi; KWAMBA, TIMU YA TAIFA LETU ILIPELEKWA NYUMBANI AMA KATIKA HOSTEL ZINAZOMILIKIWA NA KATIBU MKUU WA TOC, AMBAYE PIA NI MJUMBE WA KUDUMU WA CHAMA CHA RIADHA TANZANIA, HIVYO BASI KATIBU HUYO ALITUMIA INFLUENCE YAKE KUPATA MASILAHI YATOKANANAYO NA MASHINDANO YA OLYMPICS!!. KATAA KUBALI HILINI KOSA LA JINAI HATA HAPA KWETU, AMA KWA JINA LINGINE TUNAITA "ABUSE OF POWER". MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA. PIA KATIBU HUYO MKUU ALIJILIPA MWENYEWE KWA KUJUA NI KIASI GANI KINATOLEWA KWA MAANDALIZI YA TIMU.  Pia ifahamike kwamba hakuna katibu mkuu mwingine duniani wa NATIONAL OLYMPIC COMMITTEE ya nchi zaidi ya 200 duniani zinazoshiriki Olympics amediriki kupeleka timu ya taifa lake katika himaya yake ili afaidike na mapato ya moja kwa moja kutoka Olympic Solidarity.
     (C). Resources: Katika section hiyo kuna vipengele vine lakini mimi niongelee vipengele  1 na 2 inayosema kwamba; 1. The Olympic resources of the Olympic parties may be used only for Olympic purposes.
2.1 The income and expenditure of the Olympic parties shall be recorded in their accounts,
which must be maintained in accordance with generally accepted accounting principles.
An independent auditor will check these accounts.
Nawatuhumu kivipi; kwa sababu: Tumekuwa tukilalamikia mapato na matumizi kutoka kwa Olympic Solidarity na dola 100,000 kutoka India, bila kusahau dola 100,000 ambazo zilitumika kwa maandalizi ya timu(kimsingi mzee alijilipa mwenyewe) fedha ambazo BAYI NA GULAMU wanakuwa bubu pindi wanapoulizwa, pia kuna uwezekano kwamba accountant anayekagua mapato na matumizi ya TOC ni mfanyakazi/mjumbe wa TOC!!. Sasa basi ipo wapi dhana ya IOC inayotaka kuwepo kwa INDEPENDENT AUDITOR ?.

NINI KINAFUATA BAADA YA HAYO YOTE:
A fall from grace, 'Ipo siku, tena hivi karibuni BAYI ataanguka kutoka juu!!, nikimaanisha siri zake zote zitakuwa hadharani na dunia nzima itajua, na tunafahamu kuwa mataifa ya mgharibi haipendi UFISADI, na FILBERT BAYI ana sifa nzuri sana kimataifa kwani anajulikana kama "The miracle miler", ila mimi nasema laiti angelijua jinsi ambavyo heshima yake itakavyoshuka kama ile ya LANCE AMSTRONG, asingekuwa na kiburi cha kuwa kin'gan'ganizi katika uongozi bali aachie madaraka ili aonekane wa maana hadi kufa kwake!!. AMA SIVYO tayari tumeandaa sahii 2,000 za wadau ambao dunia haitawadharau, na tutatuma malalamiko yetu hadi IOC na kopi kwa Olympic Solidarity, ripoti ambayo itaipaka matope serikali sababu kuna VIGOGO WAWILI wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wamehusishwa na ripoti yetu ambayo gharama ya uchunguzi imechangiwa na wazalendo. Asishangae muda mfupi ujao akabatizwa jina la "The criminal Miler badala ya lile zuri la The miracle miler".
Yeye na hela yake SISI na uzalendo wetu na nchi yetu!!.
Mambo mengine yaliyoharibika BAYI na Gulamu walipoingia:
1). Olympic Possible ilifutwa, program ambayo ndio iliwawezesha wao kushinda medali 1980 baada ya kufadhiliwa kupitia program hiyo inayofadhiliwa na IOC kila mwaka. Je wamezi-locate hizo hela wapi?.
2). Matumizi mabaya ya PUMA na LINING ambapo hadi sasa taifa letu halina SPONSOR kutokana na Tanzania kuonekana matapeli sababu ya wawili hao ambao bora wafe kuliko kukosa uongozi TOC.
3). Zanzibar na Bara kutumiwa vibaya kwa madai "TOC INAJALI MUUNGANO", wakati huo ndo uongo wao, tangu waingie madarakani si Zanzibar wala Bara wamejengewa chochote, bali wao wamejijengea mashule, majumba ya kifahari na sasa wanaomba kura ili labda wakamilike kwa kujijengea AIRPORTS KABISA!!.
HII INASIKITISHA, INASHANGAZA, INAKATISHA TAMAA, LAITI BMT WANGETAMBUA HILO TANZANIA TUTASONGA MBELE!!.

By: Gidabuday.
NB: Niliyoyasema nimeyanukuu kutoka kwenye kitabu cha IOC, ukihitaji kopi za kurasa muhimu za kitabu hicho please be free to ask me at any time:

VILLAS-BOAS NA DI MATTEO - MAJENEZA YAO STAMFORD BRIDGE YALICHONGWA NA WEST BROM NA TIMU ZA SERIE A


Najua unajua kwamba Andre Villas-Boas ndiye aliyempeleka Robert Di Matteo, Chelsea, kama msaidizi wake. Kabla, Di Matteo alikuwa ni kocha mkuu wa West Bromwich Albion, huko alifukuzwa baada ya timu kufanya vibaya kwenye ligi kuu msimu wa 2010/11. Baada ya Villas-Boas kufukuzwa Chelsea, Di Matteo alitajwa kuwa kocha wa muda wa Chelsea baada ya kupata mafanikio makubwa katika muda mfupi, msimu wa 2011/12 ulipoisha, alipewa kazi ya kuwa kocha mkuu wa Chelsea kuanzia msimu wa 2012/13. Di Matteo naye sasa hivi ameshatimuliwa Chelsea.

Nataka ujue jinsi Villas-Boas na Di Matteo kufukuzwa kwao katika klabu ya Chelsea jinsi kunavyofanana;

MECHI ZAO ZA MWISHO ZA LIGI KUU NA LIGI YA MABINGWA ILIZIHUSISHA KLABU YA WEST BROMWICH ALBION NA NCHI YA ITALIA:

Andre Villas-Boas

Tarehe 21 February, 2012, Chelsea ilifungwa 3-1 na Napoli kule Italia kwenye mechi ya ligi ya mabingwa wa Ulaya. Lavezzi alifunga mara mbili na Cavani huku goli la Chelsea likifungwa na Mata.

Tarehe 4 March, 2012, Chelsea ilifungwa 1-0 na West Bromwich Albion, hii ndio ilikuwa mechi ya mwisho ya Villas-Boas, Gareth McAuley. Siku hii Villas-Boas alifukuzwa.

Roberto Di Matteo

Tarehe 17 November, 2012, Chelsea ilifungwa 2-1 na West Brom, Di Matteo, kwanza alikuwa amefungwa na timu yake ya zamani pili kwa mara nyingine Chelsea ilikuwa inafungwa kwa tofauti ya goli moja WBA. Shane Long na Odemwingie waliwaua Chelsea, Hazard aliwapatia Chelsea bao la kufutia machozi. Game ilipigwa pale pale kwenye uwanja wa WBA, The Hawthorns.

Tarehe 20 November, 2012, Chelsea inafungwa goli 3 kwa mara nyingine kwenye ardhi ya Italia huku wenyewe wakiambulia patupu safari hii, walipokuwa wakicheza dhidi ya Juventus. Quaglirella, Vidal na Giovinco. Kesho yake tarehe 21, Di Matteo alikuwa amefukuzwa.

Imeandaliwa na PodoBest

Twitter: @iPodoBest

MESSI NA RONALDO WATOSWA NA CRUYFF KATIKA KIKOSI CHAKE BORA CHA MUDA WOTE

BeckenbauerYashinCarlos Alberto

Beckenbauer

KrolDi StefanoGuardiola


Di Stefano

KeizerGarrincha Pele


Star man: Diego Maradona terrorises the England defence at the 1986 World Cup

Katika hali ya kushangaza gwiji wa soka wa Uholanzi na Barcelona Johan Cruyff ametangaza kikosi chake bora cha muda wote na amewatosa wachezaji bora wa kizazi hiki kuanzia Ronaldo De Lima, Ronaldinho, Zidane, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Katika kikosi hicho kuna muingereza mmoja tu - Sir Bobby Chalrton ambaye ni mshindi wa kombe la dunia pekee kwa England.
'

CRUYFF'S ALL-TIME XI (3-4-3)

Yashin (USSR); Carlos Alberto (Bra), Beckenbauer (Ger), Krol (Hol); Guardiola (Sp), Charlton (Eng), Di Stefano (Arg/Col/Sp), Keizer (Hol); Maradona (Arg), Pele (Bra), Garrincha (Bra)


Read more: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2237293/Johan-Cruyffs-world-XI-No-Lionel-Messi-Cristiano-Ronaldo.html#ixzz2D3Q6V6wo
Follow us: @MailOnline on Twitter | DailyMail on Facebook

CRUYFF'S ALL-TIME XI (3-4-3) Yashin (USSR); Carlos Alberto (Bra), Beckenbauer (Ger), Krol (Hol); Guardiola (Sp), Charlton (Eng), Di Stefano (Arg/Col/Sp), Keizer (Hol); Maradona (Arg), Pele (Bra), Garrincha (Bra)

MAPENZI YA ABRAMOVICH NA TORRES CHANZO CHA KUONDOKA KWA MAKOCHA WATATU CHELSEA


Mapenzi ya ROMAN ABRAMOVICH na straika mwenye jina kubwa kwa mara nyingine yamemgharimu kazi kocha mwingine wa Chelsea.

Roberto Di Matteo alitimuliwa saa nne asubuhi akitokea nchini Italia alipoiongoza Chelsea kudungwa 3-0 na Juventus, Fernando Torres amecheza part kubwa sana katika kufukuzwa kazi kwa makocha watatu waliopita wa The Blues - Di Matteo, Andre Villas-Boas na Carlo Ancelotti.
Ungeweza kufikiria kwamba Abramovich anaweza alijifunza kitu kutoka kwenye sakata la Andriy Shevchenko.
Jose Mourinho, akijiandaa kwa msimu wa wa 2006-2007 baada ya kushinda ubingwa wake wa pili, akasajiliwa mchezaji ambaye hakuwa hata akimtaka.
Lakini mmiliki wa kirusi aliendelea kumng'ang'ania: "Ni mchezaji wangu mwenye gharama ya £30million na yupo kwenye timu. 

Mahusiano ya Mourinho yakaharibika na hawakuweza kuwa vizuri tena.
Mpaka Mourinho anatimuliwa baada ya michezo sita ya msimu wa 2007-2008, Shevchenko alikuwa amefunga mabao manne katika premier league ndani ya michezo 31 - na hatimaye aliondoka Stamford Bridge akiwa amefunga mabao 9 katika mechi 48.
 
Abramovich, akaendelea kuwa mbishi.
Na historia ikajirudia tena kwa Fernando Torres.
Akitiwa upofu na rekodi nzuri ya magoli ya mhispania alipokuwa Liverpool ingawa katika mwaka wake wa mwisho hakuwa kwenye kiwango kizuri, Abramovich akaweka mezani £50million mwezi  January 2011 kwa matumaini Torres angeongeza makali katika kikosi cha Carlo Ancelotti kilichoshinda makombe mawili.
 limekuwa janga lisilotibika.
Torres alienda na kufunga bao 1 tu katika mechi 14 za ligi na hakupata chochote katika champions league ambapo Chelsea walitolewa na Manchester Unitedo fainali. Ancelotti nae akaenda na maji.
 
Akaingia AVB ambaye alianza kwa kuleta mabadiliko ndani ya kikosi - jaribio ambalo lilidumu kwa mechi 27 huku Torres akifunga mara moja tu katika mechi 22. Akatimuliwa AVB. 

Na sasa ameondoka Di Matteo. Katika mechi kadhaa zilizopita ambazo mambo yamekuwa magumu kwa Di Matteo - Torres hakuwa kwenye kiwango kizuri kabisa. Hakuna la kushangaza.

Pamoja na jitihada zote za meneja kumpa nafasi nyingi kadri iwezekanavyo lakini wachezaji wenzake wameshapoteza matumini nae - kiasi kwamba Di Matteo alijaribu kumuacha katika kikosi chake kilichocheza Turin dhidi Juve japokuwa alionywa kwamba jambohilo lingempotezea kazi yake.

Di Matteo siku zote amekuwa ni jaribio kwa Abramovich. Kwanza kabisa hakuwahi kumtaka kwenye nafasi ya kocha mkuu hasa pale aliposhinda Champions league - na hilo kidogo lilimfanya awe na uzito katika kuchukua makocha wenye majina makubwa.

Alimuacha Di Matteo na kumpa mkataba wa miaka miwili kama zawadi. Lakini siku zote alikuwa anatafuta sababu ya kumtimua.

Wakati huo huo Torres aliendelea kuwa na kiwango kibovu.

Torres ni mchezaji ambaye siku zote maisha yake yamekuwa ya umimi, yakimzunguka mwenyewe tu.

Mfano mzuri tuliiona tabia yake muda mfupi baada ya fainali ya Champions league jijini Munich.

Badala ya kushangilia ushindi mkubwa zaidi katika historia ya Chelsea, Torres alikuwa akilalamika kuhusu kutopewa nafasi ya kupiga penati na kuachwa kwenye benchi akicheza kwa dakika sita tu za dakika za kawaida

Alisema: “Nimekuwa kwenye kipindi kigumu cha maisha yangu ya soka msimu huu na sipo tayari kukirudia tena. Msimu ujao nataka mtu aniambie nini kitatokea, jukumu lipi nitakuwa nalo kwenye timu, nini nitegemee na nione kama kitakuwa na thamani hiyo."

Japokuwa aliambiwa kabisa nini kitatokea na jukumu gani atakalokuwa nalo kwenye timu. Na kumpa sapoti yote aliyotaka Abramovich akaenda kumuongezea watengenezaji magoli wengine pembeni ya Juan Mata - Eden Hazard na Oscar.

Kama vile haikutosha Abramovich akamruhusu Didier Drogba kuondoka ili kumpa nafasi zaidi Torres kwenye timu.Torres akashinda vita ambayo hakufanya chochote kushinda.

Sasa, ingawa amekuwa na nafasi ya kuonyesha nini anaweza kufanya na kulipa fadhila ya imani anayopewa na mmiliki wa klabu lakini bado ameendelea kuwa Sheva namba 2.

Na bado Abramovich akaendelea kumsisitiza na kumuelekeza  Di Matteo kwamba Torres aanze kwenye kikosi cha kwanza. Kocha akaendelea kufuata maelekezo ya bosi kinyume na mapenzi yake.

Na matokeo yake - timu imepoteza muelekeo.

BAADA YA DI MATTEO - MARK HUGHES NAE AENDA MAJI QPR

MARK HUGHES ametimuliwa kazi ya kuwa kocha wa QPR.

Mmiliki wa QPR Tony Fernandes amemfukuza kazi kuelekea mchezo dhidi ya Manchester United.
Harry Redknapp ndiye mtu ambaye anatajwa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Hughes pale Loftus Road.
  Taarifa rasmi ya QPR statement ilisema: "Uamuzi huu umechukuliwa kwa uangalifu mkubwa na bodi ya wakurugenzi, kufuatia mikutano iliyofanyika kwa siku kadhaa zilizopita.

"Bodi ya wakurugenzi inamtakia kila la kheri na kumshukuru Mark kwa aliyoifanya katika kipindi cha miezi 10 iliyopita.
"Mark ameonyesha ueledi na uaminifu katika kipindi chote alichokuwa hapa, lakini kwa hali iliyopo tumejikuta hatuna chaguo zaidi ya kufanya mabadiliko.
"Bodi sasa itafanya kazi kwa nguvu katika kuweka meneja mpya kwa haraka zaidi."

Thursday, November 22, 2012

PHOTOZ: RAFAEL BENITEZ ATAMBULISHWA RASMI KUWA KOCHA WA MPYA WA CHELSEA - MASHABIKI WAMPOKEA NA MABANGO YA KUMKATAA

.
I'm back! Rafael Benitez held his first press conference as Chelsea manager at Stamford Bridge on ThursdayI'm back! Rafael Benitez held his first press conference as Chelsea manager at Stamford Bridge on Thursday

Remember me? Rafa Benitez takes his first Chelsea training session on Thursday afternoon


Revival bid: Benitez gets to work on making Torres score goals again for the BluesRemember me? Rafa Benitez takes his first Chelsea training session on Thursday afternoon 
 
Making his point: A Chelsea fan stands outside the training ground with an anti-Benitez sign
Making his point: A Chelsea fan stands outside the training ground with an anti-Benitez sign

No thanks: Chelsea fan protested when Rafa Benitez was linked in March

 

REAL MADRID NDIO TIMU YA WAFUNGAJI WENGI KWENYE LA LIGA


Baada ya mechi 12 za msimu wa ligi, Real Madrid ndio timu yenye wafungaji wengi wa magoli: 12.

Mechi ya Athletic Bilbao iliwawezesha Ramos, Özil na Khedira kuongeza majina yao katika listi ya majina ya wachezaji ambao wamefunga mabao katika ligi na kuonyesha njaa ya wachezaji wa Real mbele ya goli.

Walinzi na viungo pia wapo katika orodha ya wafungaji wa Real. Washambuliaji wamefunga mabao 22, wakiwakisha asilimia 70% ya ujumla, na yaliyobakia yamefungwa kutoka na viungo na mabeki, na kuweka ujumla wa mabao 32 kwa Real kwenye La Liga. Mbao saba kati ya hayo yamefungwa na wachezaji kutoka safu ya ulinzi

REALMADRID LEAGUE GOAL SCORERS
Players Goals
Cristiano Ronaldo 12
Higuaín 7
Benzema 2
Di María 2
Sergio Ramos 1
Pepe 1
Özil 1
Khedira 1
Modric 1
Essien 1
Callejón 1
Morata 1

MOURINHO AWEKA REKODI KWENYE CHAMPIONS LEAGUE: AWAFUNIKA FERGUSON NA WENGER

Usiku wa jana Jose Mourinho aliiongoza timu yake Madrid kufuzu kucheza hatua ya 16 bora ya Champions league katika mchezo dhidi ya Manchester City ambao kwa upande wake ilikuwa mechi yake ya 29 kuiongoza Madrid katika UCL, ukiongeza mechi 33 alizoingiza Chelsea, 21 alizoiongoza Inter, na 17 alizoiongoza Porto zinamaanisha jana alitimiza mechi yake ya 100 katika Championse league.

 Jose Mourinho ndio kocha mwenye umri mdogo zaidi kuweza kufikisha idadi ya mechi 100 katika historia ya Champions league.

Mou ni kocha wa tano kuweza kufikisha idadi hiyo ya mechi na akiwa na umri wa miaka 49 tu

 Ancelotti alifikisha idadi ya mechi 100 ya UCL akiwa na miaka 51, wakati Wenger (58), Hitzfeld (58) na Ferguson (62) walifanya hivyo wakiwa na miaka zaidi ya Mourinho

MAKOCHA WALIOTIMIZA MECHI 100 KATIKA CHAMPIONS LEAGUE NA MIAKA YAO WAKATI WALIPOFIKISHA IDADI HIYO
MANAGERS AGE
Ancelotti 51
Wenger 58
Hitzfeld 58
  Ferguson 62

Mreno huyo ambaye mechi yake ya kwanza Champions league ilikuwa katika uwanja wa Santiago Bernabéu mnamo tarehe 19 February 2002, katika mechi 100 alizoziongoza timu nne tofauti katika Champions league ana rekodi ushindi mechi 54, 26 droo, na akafungwa mechi 20, magoli ya kufunga 167 na magoli ya kufungwa 85.

He has managed most victories, scored most goals and lost fewest matches with Madrid

THE 99 GAMES OF MOURINHO IN THE CHAMPIONS LEAGUE
Season Team Total Won Drawn Lost GF GA
2001-2002 Oporto 4 1 0 3 3 6
2003-2004 Oporto 13 7 5 1 20 12
Total Oporto 17 8 5 4  23 18
2004-2005 Chelsea 12 6 2 4 21 13
2005-2006 Chelsea 8 3 3 2 9 4
2006-2007 Chelsea 12 7 3 2 17 9
2007-2008 Chelsea 1 0 1 0 1 1
Total Chelsea 33 16 9 8   48 27
2008-2009 Inter 8 2 3 3 8 9
2009-2010 Inter 13 8 3 2   17 9
Total Inter 21 10 6 5   25 18
2010-2011 Real Madrid 12 8 3 1  25 6
2011-2012 Real Madrid 12 10 1 1  35 9
2012-2013 Real Madrid 5 2 2 1  11 8
Total Real Madrid 29 20 6 3   71 23
TOTAL 100 54 26 20 167 86


Barcelona ndio timu ambayo amekutana nayo mara nyingi katika mechi zake 100.
José Mourinho amekutana na timu tofauti 33 katika kipindi chote alichoanza kufundisha soka katika champions league. Katika timu zote alizokutana nazo,  Barcelona ndio timu ambayo amekutana nayo mara nyingi (12), wakifuatiwa na Liverpool, Lyon na CSKA Moscow alizokutana nazo mara sita. Amecheza dhidi ya Bayern na Ajax mara tano tano, timu ambazo amekutana mara nne ni pamoja na Werder Bremen, Manchester United na timu mbili amezifundisha Porto na Real Madrid zimecheza na Chelsea mara mbili, lakini hajawahi kukutana na timu yake nyingine Inter Milan.

TIMU 33 ALIZOWAHI KUCHEZA NAZO
TEAM MATCHES
Barcelona 12
Liverpool   6
Olympique de Lyon   6
CSKA de Moscú   6
Bayern   5
Ajax   5
Oporto   4
Real Madrid   4
Werder Bremen   4
Manchester United   4
Panathinaikos   3
APOEL   2
Chelsea   2
Dínamo de Kiev   2
Dínamo de Zagreb   2
Rubin Kazan   2
Anorthosis   2
Levski Sofía   2
Betis   2
Anderlecht   2
Partizán de Belgrado   2
Olympique de Marsella   2
Tottenham   2
Deportivo   2
PSG   2
Valencia   2
Auxerre   2
Milan   2
Borussia Dortmund   2
Manchester City   2
Mónaco   1
Sparta de Praga   1
Rosenborg   1

OMBI LA DROGBA KUJIUNGA KWA MKOPO NA KLABU NYINGINE LAKATALIWA NA FIFA

Ombi la uhamisho wa usajili wa mkopo nje ya dirisha la usajili la Didier Drogba limekataliwa na FIFA.
Gwiji huyo wa zamani wa The Blues amekuwa akihusishwa na kurudi Chelsea kwa uhamisho wa mkopo wa muda mfupi wakati wa mapumziko ya ligi kuu ya China lakini FIFA leo wamekataa maombi ya nahodha huyo wa Ivory Coast.
Shirikisho hilo la soka duniani lilisema kwenye taarifa yake: "Tunathibitisha kwamba tulipokea maombi ya mchezaji Didier Drogba kuomba ruhusa ya kusajiliwa nje ya kipindi cha usajili kwa mkopo.
"FIFA imemualifu mchezaji juu ya kanuni zilizopo.....kwamba wachezaji wanaweza kusajiliwa katika vipindi viwili tu vya mwaka vya usajili vilivyowekwa na vyama vya soka."
FIFA ilisema ingewezekana tu kwa Drogba kuhama kama asingekuwa na mkataba na kalbu nyingine ndio angeweza kusajiliwa kwa wakati ulio nje ya dirisha la usajili.
Drogba alikuwa anahitaji kupata sehemu ya kuendelea kujifua kabla ya kwenda kwenye michuano ya mataifa huru ya Afrika 2013.

BINAMU YAKE MESSI AMPELEKA FIFA RAISI WA KLABU YAKE KWA KUMTOLEA MANENO YA UBAGUZI WA RANGI

Wakati Lionel Messi akiendelea kuweka rekodi za kufunga - akiongeza mawili na kumpita Ruud Van Nisterlooy kama mfungaji bora wa pili katika historia ya Champions league  - binamu yake, Maxi Biancucchi, amemtuhumu Raisi wa klabu ya Paraguay kwa ubaguzi wa rangi.

Raisi wa Olimpia Marcelo Recanate anatuhumiwa kwa kumtukana Biancucchi baada ya mchezaji kusema anafikiria kuhamia nchini Qatar. 

“Tumetuma barua na nyaraka zote. FIFA watazipokea leo," wakili wa Biancucchi aitwaye Ricardo Scarane aliiambia Radio 970 AM.
“Maxi anayajua yote yaliyosemwa. Ameumizwa sana na maneno ya Marcelo lakini ataendelea kutimiza matwaka ya mkataba wake kwa mapenzi aliyonayo kwa timu na mashabiki wa klabu."

DRFA EPISODE 3: Mayai, Tully na Ntahilaja wapeleka mapingamizi yao

Wagombea walioenguliwa wamewasilisha kwa TFF rufaa zao za kupinga majina yao kuenguliwa katika uchaguzi wa DRFA.

Ally Mayai, Said Tully na Philemon Ntahilaja ndiyo wagombea waliowasilisha rufaa zao kwa TFF kupinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA kukata majina yao kwa kigezo cha kutokuwa na uzoefu wa uongozi katika soka.

Katibu wa kamati ya uchaguzi ya DRFA, Hella amethibitisha rufaa hizo zilizowekwa na wagombea hao.

RONALDO ATOA KIATU CHAKE CHA DHAHABU KIUZWE MAPATO YAENDA KUSAIDIA WATOTO GAZA

Vyombo vya habari vingi barani ulaya vimeripoti kwamba Cristiano Ronaldo ametoa msaada wa €1.5 million kwa watoto wa mji wa  Gaza. Lakini ukweli ni kwamba msaada huo umetoka kwa Real Madrid foundation ambao walichangisha kiasi hicho kutokana na mauzo kiatu cha dhahabu alichoshinda Ronaldo msimu wa 2010-11.

Mwaka jana Mreno huyo aliuza viatu vyake vingi vya michezo na fedha zilizopatikana alizitoa kwa Real Madrid Foundation ambao wakazipeleka kwa shule za watoto huko Gaza.

 Real Madrid Foundation imesaidia kujenga shule 167 katika nchi 66 tofauti.

MAONI YA MDAU OMARI ISSA


HII NI KWA WADAU NA VILABU VYOTE.

Msimu uliopita 2011-2012 wa ligi kuu Tanzania Bara ilipokua imemaliza mzunguko wa kwanza tuliambiwa mzunguko wa pili ligi itaendeshwa na chombo huru(kampuni) lakini mzunguko wa pili ulipoanza hakukua na hicho kitu.Tukaambiwa ligi ya 2012-2013 itaendeshwa na chombo huru cha ajabu hadi mzunguko wa kwanza unaisha hatujaona hicho chombo huru ila tunaambiwa tena kuwa mzunguko pili league itaendeshwa na chombo huru. Sasa tujiulize je club zipo kwenye huo mchakato wa kuunda hicho chombo huru au wako busy na mambo yao tu? Je TFF wanania ya kweli kuachia ligi? Nakumbuka kuna kipindi vilabu vionyesha umoja wa hali ya juu sana na mchakato ulikua katika hatua nzuri sana cha ajabu Raisi wa TFF alivyoona umoja wa vilabu umedhamilia kufanya kweli aliamua kuuvunja umoja ule kwa kuunda kamati ambayo haina maana.Nawakumbusha vilabu na wadau muda wa mapinduzi umefika tena ya lazimaaa. Vilabu amkeni upya kwa kasi ya ajabu mnanyonywa wenyewe hamuoni au viongozi mnashiriki kuvinyonya vilabu vyenu?

DRFA EPISODE 2: MAZWILE AJITOA DRFA, NANI ANAYEFUATA?

     Risiti niliyopewa mara tu baada ya kukata Rufaa.

Baada ya jana Shaffih Dauda kuwasilisha rufaa kwa kamati ya uchaguzi ya TFF iliyo chini ya mwenyekiti Deo Lyatoo  ya kuipinga kamati ya uchaguzi ya DRFA kuwapitisha  wagombea  Issack Mazwile na Muhsin Said.
MGOMBEA wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na mwakilishi wa mkutano mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Isaac Mazwile, amejitoa katika uchaguzi wa chama hicho uliopangwa kufanyika 12 Desemba, mwaka huu.
 Gazeti la Mwananchi la leo 22 Novemba, 2012, limeandika, Mazwile ambaye jina lake lilipitishwa kuwania uongozi bila ya kufanyiwa usaili, amejitoa katika kinyang’anyiro hicho kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kubanwa na majukumu ya kazi kwa muajiri wake, ambaye ni benki ya National Microfinance (NMB).
 Mazwile alipitishwa na Kamati ya Uchaguzi ya DRFA iliyo chini ya Mwenyekiti, Juma Simba ‘Gaddafi’ kuwania uongozi katika nafasi zilizotajwa hapo juu huku akiwa na amewekewa pingamizi na mgombea mwenzake (wa uwakilishi wa mkutano mkuu wa TFF), Shaffih Dauda.
 Mapingamizi aliyowekewa Mazwile ni kutokuwa muadilifu katika uongozi wa soka hasa alipokuwa akiongoza katika Chama cha Soka Kinondoni (KIFA), kutokana na kitendo chake cha kumuacha mtu aliyefahamika kwa jina la Seif Ally Mailo 'Saddam' akisaini nyaraka mbalimbali za chama hicho huku akiwa hana madaraka yoyote ndani ya chama.
 Pingamizi hilo, lilitupwa na viongozi wanne wa kamati ya uchaguzi ya DRFA ambao ni Makamu Mwenyekiti, Abdallah Faraji, Katibu Mkuu, Peter Hella na wajumbe Mwarami Ally Kobe na Said Rubeya. Mwenyekiti Gaddafi hakuwepo katika kikao hicho kutokana na kutingwa na mambo ya chama (CCM).
 Mazwile pia, alipitishwa na kamati hiyo kuwania uongozi wa DRFA bila hata ya kuhudhuria usaili uliofanyika kwenye ukumbi wa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam hivi karibuni hivyo kuibua minong’ono miongoni mwa wadau wa michezo.
 Hata hivyo, Shaffih Dauda tayari alikuwa ameshawasilisha rufaa  kwenye  kamati ya uchaguzi ya TFF kupinga Mazwile pamoja na Muhsin kupitishwa kuwania uongozi ndani ya DRFA.
 Pia Shaffih Dauda aliweka pingamizi kwa Muhsin Said kutokana na kutokuwa na elimu ya kidato cha nne. Awali Shaffih Dauda alimuwekea pingamizi Balhabou lakini kamati ya uchaguzi ilitupa pingamizi hilo kwa kumpitisha Balhabou huku ikiahidi kufuatilia vyeti vya mgombea huyo katika taasisi husika.
N.B
Shaffih Dauda jina lake halikuondolewa kwenye mchakato ila anapigania haki tu za wapenda soka!
TUENDELEE KUWA PAMOJA...........

MKAKATI WA MAENDELEO YA MCHEZO WA SOKA LA UFUKWENI ' BEACH SOCCER ' WAZINDULIWA RASMI.

 Beki wa YANGA na nahodha wa zamani wa TAIFA STARS Shadrack Nsajigwa akisikiliza kwa umakini mkubwa wakati wa mchakato wa kutengeneza mchakato maendeleo ya Beach Soccer wa miaka minne, anayemfuatia Nsajigwa na winga wa zamani wa YANGA na RIVATEX ya nchini Kenya.
 Mkufunzi anayetambuliwa na FIFA wa mambo ya Utawala na uongozi michezoni Bwana Henry Tandau akitoa somo kwa wadau waliohudhuria washa hiyo ya siku moja kwenye Hotel ya Escape Two iliyopo Mbezi Beach jijini Dar Es Salaam.
 Mimi pia nilikuepo kutoa mchango wangu wa nini kifanyike ktk kipindi cha miaka minne ijayo walau Tanzania iweze kushiriki kombe la Dunia kupitia mchezo huu.
 wewe mdau pia unaweza kuongezea madini hapa!
 Ibrahim Masoud 'Maestro' alikuepo pia,pembeni yake ni Stewart Kambona kutoka Prime Time Promotions.
Mkurugenzi wa ufundi wa TFF Bwana Sunday Kayuni pia alikuepo kwenye huo chakato wa kutengeneza.

MTANZANIA APEWA MKATABA EA SPORTS KWA AJILI YA GAME ZA FIFA.

Wednesday, November 21, 2012

DROGBA AOMBA KUSAJILIWA KWA MKOPO - KURUDI CHELSEA??

DIDIER DROGBA amefungua mlango wa kurudi kwenye premier league baada ya kuomba ruhusa ya kujiunga na klabu nyingine nje ya dirisha la usajili.

FIFA ilisema kwamba inafikiria ombi la mshambualiaji wa Shanghai Shenhua katika siku moja ambayo kocha wa zamani wa Chelsea Di Matteo alipofukuzwa.
  Taarifa ya FIFA ilisema: “Tunaweza kuthibitisha kwamba mchezaji Didier Drogba ametuma ombi la kuruhusiwa kusajiliwa nje ya dirisha la usajili na klabu kwa mkopo."


Drogba, ambaye aliondoka Chelsea baada ya kufunga penati ya ushindi katika fainali ya champions league, amekuwa akifikiria kurudi kufanya mazoezi na klabu yake ya zamani wakati ligi kuu ya China itakapokuwa imeisha - kitu ambacho Di Matteo alisema atakukaribisha vizuri kabla ya kutimuliwa leo asubuhi.
Kwa sheria zilizopo za FIFA haziruhusu Drogba kuhamia timu yoyote mpaka January 1.

BECKHAM ATANGAZA KUONDOKA L.A GALAXY BAADA YA MIAKA 6

Siku moja baada ya mabingwa watetezi L.A. Galaxy kuingia kwenye fainali ya pili mfululizo ya MLS, David Beckham ametangaza kwamba fainali hiyo itakuwa ya mwisho japokuwa amebakiwa na mwaka mmoja katika mkataba wake.
Beckham alisaini mkataba wa miaka miwili mwezi January baada ya kumaliza wa kwanza miaka 5 mwaka uliopita ambapo Galaxy walibeba ubingwa wao kwanza tangu alipojiunga na timu hiyo. Mwaka 2012, Beckham amekuwa na msimu mzuri katika ligi ya MLS akifunga mabao 7 na kutengeneza mengine matano katika mechi 28. Lakini wiki iliyopita, tetesi za kumhusu kiungo huyo wa miaka 37 kuondoka kwenda Australiakwenye A-LEAGUE zilianza kusambaa lakini kwa haraka zikakanushwa na msemaji wake.

Sasa akiwa anaondoka Galaxy, uhamisho wa kwenda A-League sasa unawezekana, lakini pia anaweza kwenda kwenye klabu nyingine ya MLS au mahala pengine popote duniani ambapo wanataka kuuza jezi za David Beckham.

Monday, November 19, 2012

EXCLUSIVE:MADUDU YA UCHAGUZI DRFA YAENDELEA


Mjumbe Mwarami Kobe Ally ( kushoto ),mwenyekiti,Juma Simba (kati ) na Katibu wa kamati bwana Peter Hella (kulia ) .

Mgombea asiyeudhuria usaili apitishwa kugombea
WAKATI majina ya wagombea katika uchaguzi mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) yakiwekwa hadharani, majina ya wagombea Said Tully,Ally Mayay na Philemon Ntahilaja yamekatwa huku Isaac Mazwile akipitishwa bila hata ya kuwepo katika usaili.
 Awali Tully ambaye ni wakala anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) aliwekewa pingamizi la kutokuwahi kufanya kazi katika klabu ya Ashanti United ya Ilala na hata alipowasilisha barua ya kuchaguliwa katika moja ya kamati za timu hizo, alitupwa nje.
 Mbali ya Mazwile kupitishwa kuwania nafasi ya mwakilishi wa mkutano mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na makamu mwenyekiti, mtu mwingine aliyepitishwa ni Muhsin Balbhou anayewania nafasi ya mwakilishi wa mkutano mkuu huku akiwa amewekewa pingamizi.
 Uteuzi wa Mwarami Ally Kobe kwa mara ya pili katika kamati ya uchaguzi
Kwa mujibu wa mmoja wa wagombea wa nafasi ya uwakilishi wa mkutano mkuu, Shaffih Dauda, mjumbe wa kamati hiyo Ally Kobe, hakustahili kuchaguliwa tena kuwamo ndani ya kamati hiyo kwani alishiriki madudu ya awali yaliyoifanya kamati iliyokuwa chini ya Mwenyekiti, Muhidin Ndolanga kuvunjwa na TFF.
 Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Deo Lyato alivunja kamati ya uchaguzi ya DRFA iliyokuwa chini ya Ndolanga kutokana kukiuka kanuni mbalimbali za uchaguzi huku kubwa likiwa kutia kasoro fomu za wagombea kadhaa.
 Kobe anadaiwa kuhusika kwa kiasi kikubwa katika madudu hayo, lakini Mwenyekiti wa DRFA anayemaliza muda wake, Said Bakhressa ambaye ameenguliwa na kamati ya Lyato kutetea nafasi yake, alihakikisha Kobe anabaki katika kamati ili tu kuhakikisha mtandao wake wa viongozi unapitishwa kuwania uongozi DRFA.
 Hivyo, Kobe aliachwa ili kuwalinda baadhi ya wagombea wanaodaiwa kuwa ama wafuasi au kupandikizwa na Bakhressa katika mchakato wa usaili hata mapingamizi wanayowekewa.
 Ili haki itendeke, ilitakiwa Kobe asiwepo tena katika kamati mpya ili kufanya mambo yaendelee katika mstari mnyoofu kwani lengo la Lyato lilikuwa kuhakikisha haki inapatikana katika mchakato wa uchaguzi huo. Hii ina maana si Ndolanga peke yake aliyekuwa na matatizo katika kamati hiyo.
 Inaweza hata mambo yaliyotokea wakati mwenyekiti akiwa Ndolanga, yalisababishwa na wajumbe kama kina Kobe. Kwa hali hii, hakuna jipya lililofanywa na Lyato, kwani madudu yameendelea. 
 Miongoni mwa mambo yaliyofanywa na kamati ya sasa ya uchaguzi ya DRFA iliyo chini ya Mwenyekiti, Juma Simba ‘Gaddafi’ ni kupitisha majina ya Mazwile na Balhabou huku wakiwa wamewekewa mapingamizi na wagombea wenzao.
 Gaddafi kutokuwepo katika kamati kwaruhusu madudu
Katika kikao cha kupitia mapingamizi yaliyowekwa kwa baadhi ya wagombea wa uchaguzi wa DRFA, mwenyekiti, Juma Simba hakuwepo kutokana na udhuru aliotoa ili kuhudhuria mambo ya siasa katika Chama cha Mapinduzi (CCM) ambako ana majukumu.
 Kwa kutumia mwanya huo, wajumbe Said Rubeya na Kobe walitumia kila njia kuhakikisha wanawabeba baadhi ya wagombea ambao ndani yake wapo Mazwile na Balhabou.
 Hata katibu wa kamati, Peter Hella alizidiwa nguvu na Rubeya na Kobe katika kuhakikisha haki inapatikana jambo lililomfanya achukue uamuzi wa kujiuzulu kwa kutokubaliana na kilichokuwa kikifanywa na wajumbe hao.
 Kuona hivyo, mwenyekiti Gaddafi alipopewa taarifa hizo na Hella, alimsihi katibu huyo asijiuzulu kwa ahadi ya kuzidi kuuchafua uchaguzi huo. Hella bado yupo mguu ndani mguu nje kuhusu nafasi yake kwenye kamati hiyo.
 Pingamizi la Mazwile lilivyozimwa.
Mgombea Mazwile aliwekewa pingamizi na Shaffih Dauda linalohusu kitendo chake cha kutokuwa mwadilifu katika kazi zake akiwa mtendaji wa Chama cha Soka Kinondoni (KIFA) kwa kumruhusu mtu asiye kiongozi kusaini kazi za chama hicho.
 Inadaiwa kuwa, Mazwile akiwa mtendaji wa KIFA alitakiwa kusaini fomu za wagombea mbalimbali waliokuwa wakitakiwa kuhalalishwa kugombea katika vyama mbalimbali vya soka ikiwemo DRFA ili kuthibitishwa uhalali wao.
 Akijua ni kinyume na taratibu, Mazwile akiwa safarini mkoani Dodoma aliruhusu mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Seif Ally Mailo 'Saddam' alisaini fomu na karatasi nyingine zilizopita KIFA kwa niaba yake, ikimbukwe Saddam hana madaraka yoyote KIFA.
 Katika pingamizi hilo, vithibitisho vilitolewa ikiwemo karatasi zilizosainiwa na Saddam kwa niaba ya Mazwile lakini kamati ya uchaguzi kupitia wajumbe wakina Rubeya na Kobe, walitupilia mbali pingamizi hilo. Hata katibu ambaye ni Hella alipowataka wajumbe wenzake kutazama kwa mara ya pili pingamizi hilo, alipingwa vikali. Hatimaye, pingamizi la Mazwile lilitupwa mbali.
 Pingamizi la Balhabou nalo utata mtupu  
Katika pingamizi lake kwa Balbhou, Shaffih Dauda alikuwa alipinga mgombea huyo kuwa na elimu ya kidato cha nne inayotakiwa kwa kila mgombea wa uongozi wa DRFA kwa sasa.
 Kamati ilitoa jibu la kuhakika vyeti vya Balbhou lakini ikimruhusu kuendelea na mchakato wa uchaguzi jabo ambalo ni kinyume na taratibu za uchaguzi huo. Hivyo pingamizi hilo nalo lilitupwa na kamati huku nguvu kubwa ikitoka kwa Rubeya na Kobe.
 Kwa kawaida taasisi inayotakiwa kuthibitisha elimu ya kidato cha nne nchini ni Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) na mchakato huo unaweza kuchukua siku saba hadi 14 tu.
 Mazwile hakuhudhuria usaili lakini kamati yampitisha
Madudu mengine yaliyofanywa na kamati ya uchaguzi ya DRFA ni kupitisha jina la Mazwile kuwania nafasi ya uwakilishi wa mkutano mkuu na makamu mwenyekiti bila ya kuhudhuria usaili wa wagombea wote uliofanyika katika ukumbi wa Uwanja wa Uhuru.
 Mmoja wa wagombea wa uchaguzi wa DRFA, Shaffih Dauda alikuwepo ukumbini tangu mwanzo hadi mwisho na hakumuona Mazwile kuhudhuria usaili huo, lakini jambo la ajabu jina la mgombea huyo limeorodheshwa katika majina ya wagombea waliopitishwa kuwania uongozi DRFA.
 Hayo ni baadhi tu madudu yaliyofanywa na kamati ya uchaguzi ya DRFA ambayo inasimamia uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
 ENDELEA KUWA NASI UPATE MADUDU MENGINE YA UCHAGUZI HUO