Search This Blog

Friday, November 23, 2012

MAPENZI YA ABRAMOVICH NA TORRES CHANZO CHA KUONDOKA KWA MAKOCHA WATATU CHELSEA


Mapenzi ya ROMAN ABRAMOVICH na straika mwenye jina kubwa kwa mara nyingine yamemgharimu kazi kocha mwingine wa Chelsea.

Roberto Di Matteo alitimuliwa saa nne asubuhi akitokea nchini Italia alipoiongoza Chelsea kudungwa 3-0 na Juventus, Fernando Torres amecheza part kubwa sana katika kufukuzwa kazi kwa makocha watatu waliopita wa The Blues - Di Matteo, Andre Villas-Boas na Carlo Ancelotti.
Ungeweza kufikiria kwamba Abramovich anaweza alijifunza kitu kutoka kwenye sakata la Andriy Shevchenko.
Jose Mourinho, akijiandaa kwa msimu wa wa 2006-2007 baada ya kushinda ubingwa wake wa pili, akasajiliwa mchezaji ambaye hakuwa hata akimtaka.
Lakini mmiliki wa kirusi aliendelea kumng'ang'ania: "Ni mchezaji wangu mwenye gharama ya £30million na yupo kwenye timu. 

Mahusiano ya Mourinho yakaharibika na hawakuweza kuwa vizuri tena.
Mpaka Mourinho anatimuliwa baada ya michezo sita ya msimu wa 2007-2008, Shevchenko alikuwa amefunga mabao manne katika premier league ndani ya michezo 31 - na hatimaye aliondoka Stamford Bridge akiwa amefunga mabao 9 katika mechi 48.
 
Abramovich, akaendelea kuwa mbishi.
Na historia ikajirudia tena kwa Fernando Torres.
Akitiwa upofu na rekodi nzuri ya magoli ya mhispania alipokuwa Liverpool ingawa katika mwaka wake wa mwisho hakuwa kwenye kiwango kizuri, Abramovich akaweka mezani £50million mwezi  January 2011 kwa matumaini Torres angeongeza makali katika kikosi cha Carlo Ancelotti kilichoshinda makombe mawili.
 limekuwa janga lisilotibika.
Torres alienda na kufunga bao 1 tu katika mechi 14 za ligi na hakupata chochote katika champions league ambapo Chelsea walitolewa na Manchester Unitedo fainali. Ancelotti nae akaenda na maji.
 
Akaingia AVB ambaye alianza kwa kuleta mabadiliko ndani ya kikosi - jaribio ambalo lilidumu kwa mechi 27 huku Torres akifunga mara moja tu katika mechi 22. Akatimuliwa AVB. 

Na sasa ameondoka Di Matteo. Katika mechi kadhaa zilizopita ambazo mambo yamekuwa magumu kwa Di Matteo - Torres hakuwa kwenye kiwango kizuri kabisa. Hakuna la kushangaza.

Pamoja na jitihada zote za meneja kumpa nafasi nyingi kadri iwezekanavyo lakini wachezaji wenzake wameshapoteza matumini nae - kiasi kwamba Di Matteo alijaribu kumuacha katika kikosi chake kilichocheza Turin dhidi Juve japokuwa alionywa kwamba jambohilo lingempotezea kazi yake.

Di Matteo siku zote amekuwa ni jaribio kwa Abramovich. Kwanza kabisa hakuwahi kumtaka kwenye nafasi ya kocha mkuu hasa pale aliposhinda Champions league - na hilo kidogo lilimfanya awe na uzito katika kuchukua makocha wenye majina makubwa.

Alimuacha Di Matteo na kumpa mkataba wa miaka miwili kama zawadi. Lakini siku zote alikuwa anatafuta sababu ya kumtimua.

Wakati huo huo Torres aliendelea kuwa na kiwango kibovu.

Torres ni mchezaji ambaye siku zote maisha yake yamekuwa ya umimi, yakimzunguka mwenyewe tu.

Mfano mzuri tuliiona tabia yake muda mfupi baada ya fainali ya Champions league jijini Munich.

Badala ya kushangilia ushindi mkubwa zaidi katika historia ya Chelsea, Torres alikuwa akilalamika kuhusu kutopewa nafasi ya kupiga penati na kuachwa kwenye benchi akicheza kwa dakika sita tu za dakika za kawaida

Alisema: “Nimekuwa kwenye kipindi kigumu cha maisha yangu ya soka msimu huu na sipo tayari kukirudia tena. Msimu ujao nataka mtu aniambie nini kitatokea, jukumu lipi nitakuwa nalo kwenye timu, nini nitegemee na nione kama kitakuwa na thamani hiyo."

Japokuwa aliambiwa kabisa nini kitatokea na jukumu gani atakalokuwa nalo kwenye timu. Na kumpa sapoti yote aliyotaka Abramovich akaenda kumuongezea watengenezaji magoli wengine pembeni ya Juan Mata - Eden Hazard na Oscar.

Kama vile haikutosha Abramovich akamruhusu Didier Drogba kuondoka ili kumpa nafasi zaidi Torres kwenye timu.Torres akashinda vita ambayo hakufanya chochote kushinda.

Sasa, ingawa amekuwa na nafasi ya kuonyesha nini anaweza kufanya na kulipa fadhila ya imani anayopewa na mmiliki wa klabu lakini bado ameendelea kuwa Sheva namba 2.

Na bado Abramovich akaendelea kumsisitiza na kumuelekeza  Di Matteo kwamba Torres aanze kwenye kikosi cha kwanza. Kocha akaendelea kufuata maelekezo ya bosi kinyume na mapenzi yake.

Na matokeo yake - timu imepoteza muelekeo.

No comments:

Post a Comment