Search This Blog

Saturday, December 22, 2012

HIVI NDIVYO STARS ILIVYOMUADHIRI BINGWA WA AFRIKA ZAMBIA

 
Mchezaji wa Taifa Stars Mrisho Ngasa akishangilia na kupongezwa na wenzake mara baada ya kufunga goli la mkwanza katika mchezo huo.
 
Wachezaji wa Taifa Stars wakitoka nje ya uwanja kwa mapumziko baada ya kipindi cha kwanza kuisha kwenye uwanja wa Taifa.
Mashabiki wa timu ya Taifa Stars wakishagilia mara baada ya Mrisho Ngasa kufungo goli la kwanza dhidi ya Chipolopolo katika mchezo huo
Kikosi cha timu ya Zambia kikiwa katika picha ya pamoja.
Kulia ni Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu nchini Zambia Kalusha Bwalya na mabalozi wa Zambia nchini Judith Kangoma-Kapijimpanga na Balozi Tanzania nchini Zambia Bi. Grace Mujumi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mchezo huo.
Mashabiki wa timu ya taifa ya Zambia wakishangilia timu yao katika mchezo huo.

Mashabiki wa Stars wakishangilia timu yao dhidi ya ZambiaMakocha wa Zambia wakitoka uwanjani baada ya mechi kuisha

Mcha akiwapeleka puta mabeki wa Zambia


PICHA KWA HISANI YA Michuziblog na Fullshangwe

STARS NA SOKA LA HATARI WAMTOA KAMASI BINGWA WA AFRIKA - YAITANDIKA 1-0 ZAMBIA

Goli pekee lilofungwa na mchezaji Mrisho Ngassa katika dakika ya 44 ya kipindi cha kwanza umeipatia Tanzania ushindi dhidi ya mabingwa wa Afika timu ya taifa ya Zambia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

Timu zote ambazo zilikuwa zimewakosa wachezaji wao muhimu ziliuanza mchezo wa vizuri huku Stars ikionekana kucheza vizuri kwenye upande wa ulinzi na safu ya kiungo iliyokuwa chini ya wanaume wanne Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Isaac Domayo na Sure Boy.

Tanzania iliishambulia sana Zambia katika kipindi cha kwanza dakika za mwanzo lakini Mrisho Ngassa alikuwa anazidiwa ujanja na mabeki warefu wa Zambia hivyo kupoteza nafasi kadhaa, kabla ya dakika ya 44 kupokea pasi nzuri kutoka kwa Mwinyi Kazimoto na kufumua shuti kali na kuiandikia bao safi Tanzania hivyo kwenda mapumziko wakiwa kifua mbele kwa 1-0.

Kipindi cha pili Zambia walirudi kwa kasi wakiingiza baadhi ya silaha zao walizoziacha nje mwanzoni lakini bado walishindwa kuipita ngome imara ya ulinzi iliyoundwa na Juma Kaseja, Kelvin Yondani, Aggrey Morris , Kapombe na Erasto Nyoni ambao leo hii walicheza vizuri sana kiasi cha kumfunika kabisa mchezaji bora wa Afrika wa BBC Chris Katongo.

Hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa matokeo yakiwa 1-0 kwa bila, Stars ikitoka na ushindi mzuri iliyostahili kwa kucheza soka safi kabisa la kuridhisha.  


DIEGO MARADONA AKANWA NA CHAMA CHA SOKA CHA IRAQ - WASEMA HAWANA MPANGO WA KUMUAJIRIKufuatia ripoti zilizotoka kwamba Diego Maradona alikuwa akikaribia kuwa kocha wa timu ya taifa ya Iraq, chama cha soka cha nchi hiyo kimesema jambo hilo halitotokea kabisa.
Kutoka The National:
"Hakuna mazungumzo yoyote kati ya chama cha soka cha Iraq na Diego Maradona na hakuna nia ya kumuajiri kocha huyo," makamu wa mwenyekiti wa IFA Abdul-Khaliq Masoud alisema jana.
Kukataliwa huku kumekuja siku baada ya afisa mmoja wa shirikisho la soka la Argentina kukaririwa akisema kwamba Maradona ndio anayeoongoza katika mbio za kumrithi Zico, kocha wa zamani wa Iraq, ambao wapo katika nafasi nzuri ya kufika katika fainali za kombe la dunia 2014.

COASTAL UNION WAIGONGA SIMBA - KUCHEZA FAINALI YA UHAI CUP NA AZAM FC

Azam ya Dar es Salaam na Coastal Union ya Tanga ndizo zitakazoumana kwenye fainali ya michuano ya Kombe la Uhai 2012 itakayochezwa kesho jioni (Desemba 23 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.

Timu hizo zimepata fursa hiyo baada ya kushinda mechi zao za nusu fainali ya michuano hiyo inayoshirikisha timu za vijana wenye umri chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom. Michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Said Salim Bakhresa kupitia maji Uhai.

Azam ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata tiketi ya fainali baada ya kuitoa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwa mikwaju ya penalti 3-2. Matokeo ya dakika 90 yalikuwa bao 1-1. Nayo Coastal Union iliivua ubingwa Simba kwa kuifunga mabao 2-1.

Mechi ya fainali itaanza saa 10 kamili jioni, na itatanguliwa na ile ya kutafuta mshindi wa tatu kati ya Mtibwa Sugar na Simba ambayo itachezwa saa 2 kamili asubuhi kwenye uwanja huo huo.

Mbali ya kombe, bingwa wa michuano hiyo atapata sh. milioni 1.5, makamu bingwa sh. milioni 1 wakati mshindi wa tatu atajinyakulia sh. 500,000. Timu iliyoonesha zaidi mchezo wa kiungwana (fair play) itapata sh. 400,000, mchezaji bora wa mashindano sh. 350,000, mfungaji bora sh. 300,000 na kipa bora sh. 300,000.

Naye kocha bora katika mashindano hayo atazawadiwa sh. 300,000 kama itakavyokuwa kwa refa bora.

Friday, December 21, 2012

MKE WA SNEIJDER ASEMA "TUNAONDOKA MILAN MWEZI JANUARY"

Mke wa Wesley Sneijder amesema kwamba mumewe ataondoka Inter wakati dirisha la usajili la mwezi January.

"Tunakaribia kuondoka Milan," Yolanthe Cabau aliviambia vyombo vya habari vya Uholanzi. "Kila kitakuwa kimewekwa vizuri katika siku za mwanzo za mwezi January.

"Tutakapohamia? Tunaangalia mahala pazuri kwa ajili ya familia yetu. Kwa sasa hivi sijali sana kuhsu kazi yangu."

Sneijder amekuwa kwenye kutokuelewana na Inter katika siku za hivi karibuni baada ya kukataa ombi lao kwa mchezaji apunguze kiasi cha €2m kutoka kwenye mshahara wake.

Hajaichezea timu hiyo ya Serie A tangu alipocheza dhidi Chievo, kwanza kwa sababu ya majeruhi na baadae kwa sababu za kiufundi za boss Andrea Stramaccioni.

Sneijder aliruhusiwa kuanza mapumziko yake ya Christmas mapema wiki hii pamoja na kwamba Inter bado wana mechi mbili  za kucheza.

HIVI NDIVYO TUZO YA BALLON D'OR INAVYOTENGENEZWA - RONALDO, MESSI, AU INIESTA NANI KUIBUKA KIDEDEA WIKI 2 ZIJAZO????

RONALDO, INIESTA OR MESSSI

Golden balls: The world's oldest jewellers have a team of six working on the Ballon d'Or trophy
Timu ya masonara sita ndio wanashughulikia utengenezwaji wa tuzo ya Ballon d'Or

Golden balls: The world's oldest jewellers have a team of six working on the Ballon d'Or trophy
Utengenezaji wa Ballon d'Or ukiendelea

Golden balls: The world's oldest jewellers have a team of six working on the Ballon d'Or trophy
Ufaransa ndio imekuwa nchi inayotengeneza tuzo tangu mwaka 1956.


Piece by piece: The same family-run store in Paris have built the trophy every year since 1956
Mtengenezaji akiweka kipande kimojawapo kwenye tuzo hiyo

Craftsman: All the finishing touches are applied by hand... but who will get their hands on the trophy?
Craftsman: All the finishing touches are applied by hand... but who will get their hands on the trophy?

ROONEY KAMA BECKHAM: MKEWE ATANGAZA JINSIA YA MTOTO WAO ANAYETARAJIWA KUZALIWA MAY 2013

Tayari wameshafanikiwa kuwa na mtoto wa kiume katika familia yao, lakini kama vile haitoshi Collen na Wayne Rooney wanategemea kumkaribisha dume lingine katika familia yao hvi karibuni.

Coolen, 27, ambaye ni mjamzito wa mtoto wake wa pili, alitangaza jinsia ya mtoto wake aliye tumboni kwenye mtandao wa kijamii wa Twiter na akasema mshambuliaji wa United, Rooney amezipokea taarifa hizo kwa furaha kubwa.

Aliandika hivi kwenye akaunti yake ya Twiiter
 
Coleen na Wayne tayari ni wazazi wa Kai, na sasa wanategemea kuongeza kidume kingine ndani ya nyumba mnamo mwezi wa tano mwakani.

REAL MADRID VS MAN UNITED: RONALDO "SITOSHANGILIA GOLI ENDAPO NITAFUNGA DHIDI YA UNITED"

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amesisitiza kwamba hatoweza kushangilia ikiwa atafunga katika hatua ya 16 ya UEFA Champions league dhidi ya Manchester United.

 Nahodha huyo wa Ureno ambaye alicheza kwa mafanikio makubwa akiwa na United katika kipindi cha miaka 6 kabla ya kuondoka na kujiunga Los Blancos katika kipindi cha kiangazi mwaka 2009 kwa ada iliyovunja rekodi ya dunia ya £80 million.

"Sitoshangilia goli nikiweza kufunga dhidi ya Man United," Ronaldo alikaririwa akisema siku ya alhamisi na mtandao wa AS.


Ronaldo, 27, hivi karibuni alielezea hisia zake juu ya kocha wa Manchester United na kusema kocha huyo raia wa Scotland amecheza part kubwa katika kumfanya mchezaji ambaye alivyo sasa.

"Ferguson ni mtu mzuri sana. Mwanadamu mwema. Amenifundisha vitu vingi," Ronaldo aliiambia The Sun.


"Kama nilivyosema huko nyuma, Fergie ni kama baba yangu kwenye soka. Nammisi sana yeye na mahusiano tuliyokuwa nayo."

TETESI - WIKI MOJA BAADA YA KUBADILISHIWA MASHTAKA - LULU AACHIWA KWA DHAMANA KWENYE KESI YA MAUAJI YA KANUMBA

Chama cha umoja wa waandishi wa habari kimeripoti kwamba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam asubuhi ya leo imempa dhamana msanii Elizabeth Michael baada ya kupitia vifungu kadhaa na kuona kesi yake ya kuua bila kukusudia inadhaminika.

Kwa maana hiyo, Lulu sasa atasherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka na mwaka mpya wa 2013 akiwa na familia yake, ndugu, jamaa na marafiki.

Msanii huyo ambaye anatuhumiwa kuhusika na kifo cha msanii mwenzake, Steven Kanumba - The Great, alibadilishiwa kosa la kuua na kuwa kuua bila kukusidia, ambalo, kwa mujibu wa sheria linadhamnika na kwamba ikiwa mtuhumiwa atapatikana na hatia, adhabu ya juu kabisa ni kifungo cha maisha, miaka kadhaa au kuachiwa huru.


Mtandao haujaweza kuthibitisha taarifa hizi kama ni za kweli...........

YAYA TOURE MCHEZAJI BORA WA AFRIKA TUZO ZA CAF - AWAFUNIKA DROGBA, NA ETO'O - ABOUTRIKA MCHEZAJI BORA NDANI YA AFRIKA - ZAMBIA KIBOKO YAO

Kiungo wa Ivory Coast  na Manchester City Yaya Toure ametajwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa mara ya pili mfululizo usiku wa Alhamisi, akimshinda mmpizani wake wa karibu Didier Drogba 

Kiungo huyo mwenye miaka 29 ambaye katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, alichangia kwa kiasi kikubwa kuisadia Ivory Coast kucheza fainali ya AFCON 2012 pai alikuwa ndio mhimili wa Manchester City mpaka walipochukua ubingwa wa England mwezi June mwaka huu.

Pia alikuwa mmoja wa wafungaji katika mechi ya ushindi wa kombe la hisani dhidi ya Chelsea ambapo City walishinda kwa 3-2 - huku akitoa mchango mkubwa kwa timu yake ya taifa kufuzu michuano ya AFCON 2013.

Didier Drogba alishika nafasi ya pili, huku kiungo wa Barcelona Alexander Song akikamata nafasi ya 3 katika tuzo hizo zilizotolewa mjini Accra usiku wa kuamkia leo.

Mohamed Aboutrika alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani ya bara, huku timu yake ya Al Ahly ikichaguliwa kuwa timu bora kwa upande wa vilabu wakati mabingwa wa Afrika kitaifa Zambia wakichaguliwa timu bora ya taifa. Tuzo zilikuwa kama ifuatavyo

CAF AWARDS
Player of the Year - Yaya Toure
African based Player of the Year - Mohammed Aboutrika
Women's Footballer of the Year - Genoveva Anonma (Equatorial Guinea)
National team of the Year - Zambia
Coach of the Year - Herve Renard (Zambia)
Club of the Year - Al Ahly
Legends Award: Mahmoud El Gohary (Egypt) and Rigobert Song (Cameroon)
National Women's Team of the Year - Equatorial Guinea
Fair Play Award - Gabon national team supporters
Most Promising talent of the Year - Mohamed Salah (Egypt and FC Basel)

Thursday, December 20, 2012

CRISTIANO RONALDO ANARUDI OLD TRAFFORD - TUJIKUMBUSHE MARA MWISHO KUCHEZA DHIDI YA MAN UNITED ILIVYOKUWA


TAIFA STARS VS ZAMBIA - KIM POULSEN NA RENARD KUZUNGUMZA NA WAANDISHI KESHO - NUSU FAINALI YA UHAI CUP KARUME

Makocha wa Tanzania (Taifa Stars), Kim Poulsen na Zambia (Chipolopolo) watakuwa na mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika kesho (Desemba 21 mwaka huu) kuzungumzia pambano lao litakalochezwa Jumamosi (Desemba 22 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mkutano huo utafanyika saa 5 asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Makocha hao watazungumzia maandalizi yao ya mwisho kabla ya pambano hilo litakalochezeshwa na mwamuzi Sylvester Kirwa kuanzia saa 10 kamili jioni.

Pia makocha hao watajibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari kuhusu pambano hilo litakalokutanisha timu hizo ambazo zimefanya vizuri kwenye orodha ya viwango vya ubora vya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) vilivyotolewa jana (Desemba 19 mwaka huu).

Wakati Zambia ambao ni mabingwa wa Afrika wamepanda juu kwa viwango vya ubora kwa nafasi nne, Taifa Stars ambayo katika mchezo uliopita iliifunga Kenya (Harambee Stars) bao 1-0 imepanda kwa nafasi nne.

Taifa Stars ambayo inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini tangu Desemba 12 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo kubwa ya kirafiki inayotarajiwa kuwa ya kuvutia.

TENGA ATOA NOTISI YA MKUTANO MKUU TFF
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ambaye ndiye Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho hilo tayari ametoa notisi ya mkutano huo utakaofanyika Februari 23 na 24 mwakani jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo utafanyika Februari 23 mwakani na kufuatiwa na ajenda ya uchaguzi siku inayofuata. Ajenda ya uchaguzi iko chini ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF.

Notisi hiyo imetumwa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu ambao ni kutoka vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki, klabu za Ligi Kuu ya Vodacom na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF.

Ajenda za Mkutano Mkuu zitatumwa kwa wajumbe siku 15 kabla ya mkutano huo wenye wajumbe zaidi ya 100.

NUSU FAINALI UHAI CUP KUPIGWA KARUME
Mechi za nusu fainali ya michuano ya Kombe la Uhai 2012 inayoshirikisha timu za vijana wenye umri chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom zitachezwa kesho (Desemba 21 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.

Nusu fainali ya kwanza ya michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Said Salim Bakhresa kupitia maji Uhai itazikutanisha timu za Mtibwa Sugar ya Morogoro na Azam na itafanyika kuanzia saa 2 kamili asubuhi.

Simba na Coastal Union zitacheza nusu fainali ya pili kuanzia saa 10 kamili jioni kwenye uwanja huo huo. Mtibwa Sugar imepata tiketi ya nusu fainali baada ya kuichapa African Lyon mabao 3-1 wakati Simba iliilaza Oljoro JKT mabao 2-0.

Nayo Azam iliindoa JKT Ruvu kwenye robo fainali kwa bao 1-0 huku Coastal Union ikipata ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mechi ya mwisho ya robo fainali.

Mechi ya fainali na ile ya kutafuta mshindi wa tatu zitachezwa Jumapili (Desemba 23 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam. Mechi ya mshindi wa tatu itaanza saa 2 kamili asubuhi wakati ya fainali itakuwa saa 10 kamili jioni.

MILOVAN CIRKOVIC BADO NA MAPENZI KIBAO NA SIMBA YAKE


UEFA RAUNDI YA 16 BORA: REAL MADRID VS MAN UNITED - ARSENAL VS BAYERN MUNICH

Ratiba ya hatua ya 16 ya ligi ya mabingwa wa ulaya imetoka na ipo kama ifuatavyo

 Galatasary vs Schalke

Celtic vs Juventus

Arsenal vs Bayern Munich

Shakhtar Donetsk vs Borussia Dortmund

AC Milan vs Barcelona

Real Madrid vs Manchester United

Valencia vs Pars Saint Germain

Porto vs Malaga

 

  


MAN UNITED KATIKA HAFLA YA KUCHANGIA UNICEF: NANI KAMFUNIKA MWENZIE KWENYE MAVAZI???

Questioning: Rio Ferdinand is joined on stage by Nemanja Vidic, Wayne Rooney and co at Unted's gala dinner as they are interviewed by BBC political editor Nick RobinsonCheer up, Ryan: A rather glum looking Giggs poses for a picture with team-mates Rooney and FletcherRio Ferdinand and Wayne Rooney Chris Smalling


Patrice Evra Darren Fletcher
 Patrice Evra, Darren Fletcher na wapenzi wao 

Happy: Hernandez shares a joke with Valencia while Cleverley, Young and Welbeck are all smiles (below)
Happy: Hernandez shares a joke with Valencia while Cleverley, Young and Welbeck are all smiles (below)

Happy: Hernandez shares a joke with Valencia while Cleverley, Young and Welbeck are all smiles (below)


SHINJI KAGAWA
Jonny Evans
Thumbs up: Shinji Kagawa (left) and Jonny Evans with his girlfriend Helen McConnell
In the swing: United veteran Ryan Giggs arrives at the star-studded evening at Old Trafford
In the swing: United veteran Ryan Giggs arrives at the star-studded evening at Old Trafford

Men in black: Tom Cleverley, Ashley Young and Danny Welbeck pose for the assorted media
Men in black: Tom Cleverley, Ashley Young and Danny Welbeck pose for the assorted media
Nick Powell Alexander Buttner

SHENHUA YATHIBITISHA ANELKA YUPO NJIANI KUONDOKA CHINA - DROGBA NAE NJIANI KUSEPA

Inaonekana waliokuwa washambuliaji wa Chlesea msimu uliopita Didier Drogba na Nicolas Anelka wameingia choo cha kike kama watoto wa uswahilini wanavyosema. Hiyo imekuja baada ya taarifa za wachezaji hao kutolipwa mishahara yao na klabu ya Shanghai Shenhua.
 
 Vyombo vya habari vya China vimeripoti kwamba management ya Nicolas Anelka ipo katika mazungumzo na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya China ili kusitisha mkataba baina yao huku mshambuliaji Didier Drogba amekuwa akihusishwa kurudi barani ulaya.
 

Drogba alisaini mkataba wa miaka miwili na nusu ambayo inaripotiwa una thamani ya $300,000 kwa wiki mwezi June mwaka huu, lakini Oriental Sports Daily limesema kwamba mshambuliaji huyo mwenye 34 amekuwa akiidai mishahara yake ya wiki kadhaa.

Wakati huo huo, msemaji wa Shenhua amethibitisha Anelka yupo katika mazungumzo ya kusitisha mkataba wake.

ZIDANE BADO ANATISHA, FALCAO, FUTSAL NA BEBETO WATUPIA WAKATI TIMU YA RONALDO ILIPOIFUNGA TIMU YA ZIZZOU 3-2 KWENYE MECHI YA HISANI

Z

CHELSEA YATIMIZA MABAO 126 NDANI YA MWAKA HUU - WAKIITUNGUA LEEDS 5-1

Klabu ya Chelsea jana usiku ilitoka nyuma ya goli 1-0 na kwenda kushinda 5-1 dhidi ya Leeds United katika mchezo wa robo fainali ya kombe la Capital One uliofanyika katika uwanja wa Elland Road. Kwa ushindi wa jana Chelsea kwa jumla imefunga mabao 126 ndani ya kalenda ya mwaka mmoja(2012) ikiwa bado bao moja tu kuvunja rekodi yao ambayo ni mabao 127 waliyoiweka mwaka 2010.
แอิืืืืืืืืืืืืืืืืืืืืืืืิิืททท้เำ by footyroom