Search This Blog

Friday, December 21, 2012

YAYA TOURE MCHEZAJI BORA WA AFRIKA TUZO ZA CAF - AWAFUNIKA DROGBA, NA ETO'O - ABOUTRIKA MCHEZAJI BORA NDANI YA AFRIKA - ZAMBIA KIBOKO YAO

Kiungo wa Ivory Coast  na Manchester City Yaya Toure ametajwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa mara ya pili mfululizo usiku wa Alhamisi, akimshinda mmpizani wake wa karibu Didier Drogba 

Kiungo huyo mwenye miaka 29 ambaye katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, alichangia kwa kiasi kikubwa kuisadia Ivory Coast kucheza fainali ya AFCON 2012 pai alikuwa ndio mhimili wa Manchester City mpaka walipochukua ubingwa wa England mwezi June mwaka huu.

Pia alikuwa mmoja wa wafungaji katika mechi ya ushindi wa kombe la hisani dhidi ya Chelsea ambapo City walishinda kwa 3-2 - huku akitoa mchango mkubwa kwa timu yake ya taifa kufuzu michuano ya AFCON 2013.

Didier Drogba alishika nafasi ya pili, huku kiungo wa Barcelona Alexander Song akikamata nafasi ya 3 katika tuzo hizo zilizotolewa mjini Accra usiku wa kuamkia leo.

Mohamed Aboutrika alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani ya bara, huku timu yake ya Al Ahly ikichaguliwa kuwa timu bora kwa upande wa vilabu wakati mabingwa wa Afrika kitaifa Zambia wakichaguliwa timu bora ya taifa. Tuzo zilikuwa kama ifuatavyo

CAF AWARDS
Player of the Year - Yaya Toure
African based Player of the Year - Mohammed Aboutrika
Women's Footballer of the Year - Genoveva Anonma (Equatorial Guinea)
National team of the Year - Zambia
Coach of the Year - Herve Renard (Zambia)
Club of the Year - Al Ahly
Legends Award: Mahmoud El Gohary (Egypt) and Rigobert Song (Cameroon)
National Women's Team of the Year - Equatorial Guinea
Fair Play Award - Gabon national team supporters
Most Promising talent of the Year - Mohamed Salah (Egypt and FC Basel)

3 comments:

  1. Hadi leo hii bado naumiza kichwa kutaka kujua ni vigezo vipi vinatumika kumpata mchezaji bora wa Afrika..Lakini kama CAF wanaangalia sifa ya mchezaji kwa mwaka uliopita,basi bila kificho kabisa Katongo alistahili kupata kutokana na mafanikio makubwa aliyopata kupitia timu yake ya taifa ya Zambia,ila kwa kumuengua katongo nilishangazwa sana,pia kitendo cha kumuweka Song ndio kikazidi kuumiza akili yangu kwa kufikiria mazuri aliyofanya,,au labda CAF waseme sifa kubwa ni lazima ucheze ulaya..Haya,,tuje kwa Yaya,pia kwa kuangalia makubwa aliyofanya hayalingani na mafanikio na msaada mkubwa alioutoa Drogba kwa klabu yake na taifa lake,bahati mbaya wote wanatoka taifa moja,,Drogba kafunga fainali mbili,FA na UEFA,tena magolu muhimu na ya ushindi,shindano ambalo ni kubwa sana kwa ngazi ya vilabu,,Yaya kaisaidia City kutwaa ligi,zaidi ya hapo hakuna..leo hii kapewa uchezaji bora,kwa sifa zipi..?km walimtoa katongo kwa fitina zao,basi mbadala wake aliyemfatia kwa karibu ni Drogba na wala si Yaya..YAYA TOURE HAKUSTAHILI KUPATA TUZO HII...MTAZAMO WANGU...

    ReplyDelete
  2. UKWELI NI KWAMBA WANAANGALIA MCHANGO PIA WA MCHEZAJI KWA CLUB YAKE. DROGBA KUONDOKA KTK LIGI BORA YA ULAYA KUMEMPOTEZA SAWA NA ETOO NAE. TOURE KSEMA KWELI ANASTAHILI KUTWAA KWANI NI MCHEZAJI MUHIMU KTK KIKOSI CHAKE CHA CITY.

    ReplyDelete