Search This Blog

Saturday, September 24, 2011

SENDEU APIGWA FAINI SH. 500,000


Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inayoongozwa na Kamishna wa Polisi mstaafu Alfred Tibaigana imempiga faini ya sh. 500,000 na kuwekwa chini ya uangalizi kwa miezi sita Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu baada ya kumuona ana hatia kwa mashtaka yaliyowasilishwa dhidi yake na TFF.

Uamuzi wa kamati hiyo iliyokutana leo (Septemba 24 mwaka huu) umetokana na ushahidi uliowasilishwa na TFF, na pia Sendeu mwenyewe kukiri kuwa alifanya makosa.

Sekretarieti ya TFF ilimshtaki Sendeu kwenye kamati hiyo kutokana na matamshi yake dhidi ya mwamuzi Alex Mahagi mara baada ya mechi kati ya Yanga na Ruvu Shooting iliyochezwa Septemba 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Sendeu aliita mkutano na waandishi wa habari na kumshutumu Mahagi kuwa alisababisha timu yake ikose ushindi kwa kuwabeba wapinzani wao na kudai anamfahamu Mahagi kuwa ni mwanachama wa Simba, kadi nyekundu aliyompa kiungo wao Haruna Niyonzima si halali na alifanya hivyo kwa lengo la kuisadia Simba ili iendelee kukaa kileleni mwa ligi.

Kauli hiyo ililenga kumjengea chuki Mahagi mbele ya mashabiki wa Yanga kama ilivyo kwa viongozi na watendaji wa TFF wakati Sendeu akiwa ofisa wa Yanga alikuwa anajua taratibu za kufanya pale klabu yake isiporidhishwa na uamuzi wa mwamuzi au suala lingine lolote.

Kamati hiyo haikusikiliza mashtaka dhidi ya Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage kwa vile hakufika kwenye kikao kutokana na kuwa katika kampeni za uchaguzi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania ubunge wa Jimbo la Igunga mkoani Tabora.

Pia kamati hiyo haikusikiliza mashtaka ya kwanza ya Sendeu kwa vile yanakwenda pamoja na yale ya Rage. Kamati itapanga tarehe nyingine kwa ajili ya kusikiliza mashtaka dhidi ya viongozi hao ambapo watapewa taarifa.

LIGI DARAJA LA KWANZA KUANZA OKT 15
Wakati michuano ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara inayoshirikisha timu 18 imepangwa kuanza Oktoba 15 mwaka huu timu ambazo hazijakamilisha usajili wa wachezaji zimeongezewa muda hadi Oktoba Mosi mwaka huu.

Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana leo (Septemba 24 mwaka huu) chini ya Mwenyekiti wake Makamu wa Pili wa Rais, Ramadhan Nassib pia imepanga makundi ya ligi hiyo itakayochezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.

Oktoba 3-9 mwaka huu majina ya wachezaji walioombewa usajili na timu zote 18 yatabandikwa kwenye ubao wa matangazo wa TFF kwa ajili ya pingamizi, na Kamati ya Mashindano itakutana Oktoba 10 mwaka huu kwa ajili ya kupitia majina hayo.

Kundi A litakuwa na timu za Mgambo Shooting Stars ya Tanga, Morani ya Manyara, Polisi Dar es Salaam, Temeke United ya Dar es Salaam, Transit Camp ya Dar es Salaam na Burkina Faso ya Morogoro.

Timu zinazounda kundi B ni Majimaji ya Songea, Mbeya City Council, Mlale JKT ya Ruvuma, Polisi Iringa, Small Kids ya Rukwa na Tanzania Prisons ya Mbeya. Kundi C ni 94 KJ ya Dar es Salaam, AFC ya Arusha, Polisi ya Morogoro, Polisi ya Tabora, Rhino Rangers ya Tabora na Samaria ya Singida.

Watanzania wapeta Guiness Football challenge Bondeni


TIMU ya Tanzania inayoshiriki kwa mara ya kwanza kwenye mashindano ya kujibu maswali na kupiga mipira yanayojulikana kama Guinness Mpira Changamoto yanayoendelea huko
Johannesburg Afrika Kusini, wamefanya kufuru isiyotegemewa baada ya kuongoza katika hatua ya tano hapo juzi.

Kinyang’anyiro hicho kinachoshirikisha
jumla ya washiriki 50, 16 wakiwa ni Watanzania na waliobaki ni washiriki wa Kenya na Uganda, kinaendelea hadi hapo kesho kitakapofikia mwisho wa hatua la nane. Mpaka jana kabla ya hatua ya sita timu ya George Lukuba na Freddy Jordan ndio waliokuwa vinara. Vijana hao walishinda katika hatua za tatu
na nne za kinyang’anyiro hicho wakati Sultan Mohamed na Mansoor Seif
walikuwa wa pili. Vijana hao wa Kitanzania ambao walionekana
kuyumba katika hatua ya mazoezi yaliyofanyika kwa siku mbili katika studio za kisasa za Q ( Q-Studios) zilizopo huko
Kew, mpakani na kitongoji cha Alexandra ambacho ni cha pili kwa kukaliwa na
Wazalendo wengi wa asili ya Kiafrika baada ya Soweto kwa jiji la Johannesburg, wamewashangaza waandaazi wa changamoto hiyo ya mpira wa miguu. Watanzania hao wamekuwa wepesi kujibu maswali na kupiga mipira na kuwabwaga Waganda ambao walianza kwa mbwembwe nyingi wakati wa mazoezi.
Lukuba amesema wao nia yao ni lushinda kuvuta fuba (pesa) hayo yanayotolewa na watengenezaji wa kinywaji cha Guinness ambacho kinasambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti hapa nchini. Vijana hao walifanyiwa usaili wiki mbili zilizopita katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam,
walipanda ndege kuelekea Johannesburg siku ya Jumanne wiki liyopita.
Jumla ya hatua nane zinashindaniwa katika kinyang’anyiro hicho ambacho kina toa dola elfu hamsini kila hatua.


Lukuba ambaye tuliwasiliana naye moja kwa
moja jana alisema ndoto ya washiriki wa Kitanzania ni kuendela kuvuta pesa ili kuubwaga umasikini na kuwatoa nishai wenzao wa Kenya
na Uganda ambao wamekuwa wakiwabeza kabla ya mashindano kuanza. Changamoto hiyo ya Guinness itaoneshwa na televisheni inayopendwa na watazamaji wengi nchini, ITV kwa wiki nane mfululizo. Washindi wa hatua zote nane watajiunga na wanasoka wannne waliostafu soka katika onyesho ambalo pia litashirikisha
watazamaji ambao watatuma ujumbe mfupi wa maandishi kupitia simu zao za mkononi kujaribu bahati yao ya kuvuta pesa hapo baadaye. Wachezaji hao ni Jay Jay Okocha wa Nigeria, Rigobert Song wa Cameroon, Kalusha Bwalya wa Zambia na Mfaransa Marcel Desaily aliyekuwa beki mahiri wa timu ya Chelsea
na Ufaransa iliyoshinda kombe la Dubnia mwaka 1998. Desaily kwa sass anaishi Accra, Ghana. Hii imekuwa fursa pekee kwa Watanzania kujiongezea kipato kupitia onyesho hilo.

Labda habari za kusikitisha ni kuhusu mshiriki mmoja wa Kitanzania Juma Nassoro ambaye anaumwa jipu juu ya paja lake la kushoto ambalo limepasuka na anaendelea vizuri. Mshiriki mwingine wa Uganda Daniel Elagon amebanwa na malaria tokea siku ya Jumamosi wakati wa hatua ya mwanzo ambapo kulikuwa na baridi kali jijini Johannesburg. Shindano hili la Guinness limekuwa
likifanyika katika nchi za Ghana na Cameroon pia Kenya na Uganda
walikuwa washiriki kwa mara ya kwanza mwaka jana na hii ni mara yao ya pili
.

MECHI YA MOROCCO VS TAIFA STARS YAHAMISHWA


MECHI STARS v MOROCCO
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco (FRMF) limehamisha mechi ya kundi D ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Morocco kutoka Casablanca na sasa itachezwa Marrakech.
Mechi hiyo itachezwa saa 1.30 jioni Oktoba 9 mwaka huu. Pia Algeria na Jamhuri ya Afrika ya Kati ambazo ziko kundi hilo zitacheza Oktoba 9 mwaka huu na muda huo huo ili kuepuka kupanga matokeo. Mechi hiyo itachezwa jijini Algiers.
Kwa vile hakuna mashirika ya ndege ya kimataifa yanayokwenda Marrakech, FRMF ndiyo itakayogharamia usafiri wa Taifa Stars kutoka Casablanca hadi Marrakech. Kwa mashabiki wa Tanzania wanaotaka kwenda kuishangilia Taifa Stars nauli kwa ndege za Morocco kutoka Casablanca- Marrakech- Casablanca ni dola 120.
Waamuzi wa mechi kati ya Stars na Morocco watakuwa Gassama Bakary, Jawo Dickory, Touray Sulayman na Camara Bakary, wote kutoka Gambia. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Zoumaro Gnofame kutoka Togo.
Kocha Jan Poulsen anatarajia kutangaza kikosi Septemba 26 mwaka huu kwa ajili ya mechi dhidi ya Morocco na kitaingia kambini Septemba 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

KENNY DALGLISH NAE ALIKOSA BAO KAMA LA TORRES

TFF MABINGWA WA KUVUNJA KANUNI LIGI KUU BARA


Pamoja na kuonekana likifuatilia kwa karibu utekelezwaji wa kanuni zake ndogo ndogo katika uendeshaji wa Ligi Kuu msimu huu, blog hii imebaini bado kuna kanuni za msingi ambazo chombo hicho kimekuwa kikizipuuza licha ya kuwa imezitunga yenyewe.

Moja ya kanuni hizo za msingi ambazo TFF imeshindwa kuitekeleza ni pamoja na ile ya 12 inayozungumzia bima.
Kipengele cha kwanza cha kanuni hii kinasema kuwa viongozi na wachezaji wote lazima wawekewe bima na klabu zao na kuongeza kuwa klabu itakayokiuka kanuni hiyo haitashirikishwa katika michuano yoyote inayosimamiwa na TFF.

Aidha kipengele cha pili cha kanuni hiyo kinatoa maagizo kwa Chama cha Walimu wa Mpira wa Miguu (TAFCA) kuhakikisha wanachama wake wanawekewa Bima na klabu husika.Pia Chama cha Madaktari wa Michezo Tanzania (TASMA) na wenyewe wanatakiwa kuhakikisha kwamba wanachama wake wanawekewa bima na klabu husika.

Hata hivyo licha ya TFF kusisitiza utekelezwaji wa kanuni hiyo, uchunguzi iliofanywa na blog hii baada ya kufanya mahojiano na baadhi ya wachezaji na viongozi wa klabu 14 zinazoshiriki Ligi Kuu umebaini kuwa kanuni hiyo haitekelezwi kwa asilimia 100 kanuni na bado klabu zinaendelea kushiriki Ligi Kuu kama kawaida bila hatua zozote kuchukuliwa na shirikisho hilo.

Mchezaji mmoja wa safu ya ushambuliaji ya Yanga mbali ya kukiri kutokuwa na bima pia alisema hajawahi kusikia suala hilo likizungumziwa katika klabu yake.

Msemaji wa klabu ya African Lyon, Sherally Abdallah alizungumzia suala hilo kwa kusema kuwa wachezaji waliokatiwa bima ni wale waliosajiliwa misimu ya nyuma, lakini kwa wale wa msimu huu bado suala lao linashughulikiwa.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, Boniface Wambura baada ya kuulizwa ni kwa nini shirikisho lake limeshindwa kusimamia kanuni ilizozitunga lenyewe badala ya kutoa majibu yeye alimtaka mwandishi wa habari hii aziulize klabu ni kwa nini zimeshindwa kutekeleza kanuni hiyo na baada ya hapo ndio atafutwe yeye.

Source:Mwananchi.co.tz

ADHABU ZA OKOCHA KWA OLIVER KHAN- WE MISS U JAY JAY

KALI YA LEO: CARLO ANCELLOTI BADO KOCHA WA CHELSEA? ONA HII

HII NI KARATASI YA MAJINA YA KIKOSI CHA CHA WACHEZAJI NA MAKOCHA KATIKA MECHI YA CARLING CUP ILIYOCHEZWA JUMATANO KATI YA CHELSEA NA FULHAM.

SIO WABONGO TU HATA RIHANNA ANAIPENDA BRAZIL

Friday, September 23, 2011

ON THIS DAY: CARLOS TEVEZ AFUNGA GOLI LAKE KWANZA AKIWA NA UNITED DHDI YA CHELSEA

MANCHESTER UNITED KIBOKO YA STOKE CITY KWENYE EPL



Tokea mwaka 2008, Stoke City ndio timu ambayo imekuwa ikizisumbua sana timu kubwa maarufu kama Big Six katika ligi kuu ya England katika uwanja wao wa nyumbani “The Britannia Stadium”.

Mchezo wa kukaba na kutumia nguvu zaidi chini ya kocha wao Tony Pulis umeonekana kama ndio dawa sahihi ya kuwazuia timu kubwa kuondoka na ushindi hasa wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Tangu waingie kwenye premier league mwaka 2008, Stoke wamepoteza mechi 15 kati ya 59 za mechi zao za nyumbani na wakishinda mechi 28 ukilinganisha na kufungwa mechi 34 kati ya 59 nje wa uwanja wao, hivyo hali hii inaonyesha ni jinsi gani vijana wa Tony Pulis walivyo imara wakiwa ndani Britannia Stadium.

Pamoja na ugumu wao wakiwa nyumbani kwao Stoke City wana mbabe wao naye ni Manchester United.

Vijana wa Sir Alex Ferguson wanaelekea Britannia kesho Jumamosi wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi wakifunga mabao 15 katika mechi zao 3 za mwisho za ligi.Pia United wana rekodi nzuri dhidi ya Stoke wakishinda kila mchezo waliocheza na timu ya vijana wa Tony Pulis kwenye premier league, kitu ambacho mwanachama wa Big Six ameweza kufanya.


BIG SIX vs STOKE IN THE PREMIER LEAGUE | Home & Away

PWDLFAGDPts
Manchester Utd6600162+1418
Chelsea
7520163+1317
Arsenal6402127+512
Tottenham6402118+312
Manchester City6321103+711
Liverpool723274+39


REKODI YA BIG SIX KATIKA UWANJA WA BRITANNIA

BIG SIX vs STOKE IN THE PREMIER LEAGUE | At Stoke

PWDLFAGDPts
Manchester Utd330051+49
Chelsea
422052+38
Tottenham320154+16
Arsenal310256-13
Manchester City302123+42
Liverpool402214-32

ZANETTI NA MIAKA YAKE 16 NA INTER MILAN CHINI MAKOCHA 17

Javier Zanetti alifungua ukurasa mpya katika historia ya klabu ya Inter Milan Jumanne baada ya kuipita rekodi Giuseppe Bergomi ya michezo 756 kwa klabu hiyo ya Italia.Ingawa mafanikio ya Muargentina huyu yalifunikwa na kipigo cha 3-1 kutoka kwa Novara na kichapo ambacho kilipelekea kufukuzwa kwa kocha Gian Piero Gasperini.

Zanetti alikuwa ni moja wachezaji wa kwanza kusajiliwa kipindi Mssimo Moratti anaingia madarakani, Raisi huyo aliingia madarakani mwak 1995, miezi michache kabla Zanetti hajajiunga na Inter kutokea Banfield.

Kwa miaka 16 aliyokuwa na Inter Milan, Javier Zanetti ameichezea klabu hiyo mechi 757 chini makocha 17 na amefanikiwa kushinda makombe 16 yakiwemo matano ya Serie A, manne ya Coppa Italia, manne ya Supercoppa Italiana, moja la Champions league, UEFA Cup 1, FIFA Club World Cup 1.

YEW BERKO NA NIYONZIMA NDIO MAPROO WANAOKULA MISHAHARA KIHALALI YANGA

Mchezaji Athuman Iddi 'Chuji' amesema hakuna kiungo mzalendo wa kumzidi kiwango chake ndani ya Simba na Yanga huku akiwasifu Haruna Niyonzima na Yaw Berko kuwa ndio wachezaji pekee wa kigeni waliostahili kusajiliwa na Jangwani wala sio wengine wanaolipwa mamilioni.

Chuji aliachwa na Simba na kutimkia Villa Squad kabla ya TFF kumzuia kucheza Ligi Kuu na sasa yuko mtaani akifanya shughuli zake ingawa ametangaza kwamba atarudi uwanjani kwenye dirisha dogo.

"Ukiangalia namba ambazo mimi nilikuwa nacheza Simba na Yanga sasa hivi zimeshikwa na wachezaji wa kigeni, hiyo inamaanisha kwamba hakuna mzalendo yeyote wa kunifikia."
"Waliopo wameshindwa kuhimili vishindo ndio maana wamebadilishwa namba na wengine wako benchi, Yanga nafasi yangu imechukuliwa na Niyonzima 'Fabregas' na Simba yupo Patrick Mafisango ambao wote ni raia wa Rwanda,"alisema Chuji ambaye yupo Kinondoni, Dar es Salaam ingawa muda mwingi kwa sasa anaishi Tanga.

Kiungo huyo wa zamani wa Taifa Stars, hakusita kuwapongeza nyota wawili waliosajiliwa na Yanga ndio wachezaji kigeni wanaokula mshahara kihalali.

"Yanga imesajili wachezaji watano wa kigeni, lakini ni wawili tu wanaokula mshahara kihalali kutokana na msaada wao kwa timu, ambao ni Haruna (Rwanda) na Berko (Ghana), hao wachezaji wanaisaidia sana Yanga na unaona kweli ni watu wanaofanya kazi tofauti na wenzao."

"Haruna akicheza kiungo kinatulia sana na hata Berko unaona kwamba kweli huyu ni kipa hata kama timu haifanyi vizuri, lakini hao wengine hawana jipya, kuna wachezaji wengi sana wa Tanzania waliokuwa wanaweza kucheza sehemu zao,"alisisitiza Chuji.

Wachezaji wengine wa kigeni wa Yanga ambao Chuji haridhiki na uwezo wao tofauti na wanavyokuzwa na mashabiki ni Hamis Kiiza wa Uganda, Kenneth Asamoah wa Ghana na Davis Mwape wa Zambia.

Habari za ndani zinasema kuwa mchezaji huyo amefanya mazungumzo na Coastal Union ingawa bado hawajafikia muafaka na huenda akasaini wakati wa dirisha dogo la Desemba na kurudi uwanjani.

BASENA KUWAPIGA BENCHI SUNZU NA MAFTAH DHIDI YA MORO


Kocha wa Simba, Moses Basena amesema atampumzisha mshambuliaji wake tegemeo Felix Sunzu katika mchezo wa kesho dhidi ya Moro United baada ya kuumia wakati wa mechi kati yao na Toto African.

Sunzu aliyekwamisha mabao mawili kati ya matatu yaliyosababisha Simba kupata sare ya mabao 3-3 dhidi ya Toto African katika mchezo uliofanyika juzi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, aliumia dakika ya 42 ya pambano hilo na kutolewa nje kisha kukimbizwa hospitali kwa kwa ajili ya matibabu zaidi.

Akizungumza kwa simu akiwa jijini Mwanza jana, Basena alisema hali ya afya ya Sunzu inaendelea vizuri, lakini anakusudia kumpumzisha katika mechi hiyo dhidi ya Moro United ili aweze kupona kabisa.

"Kimsingi Sunzu anaendelea vizuri, leo alienda tena hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa mwisho kwa kuwa aliumia sana.

"Ni kwamba alipasuka sehemu ya kichwa, hivyo pamoja na hali yake kuendelea vizuri sifikirii kumtumia katika mechi ya Jumamosi dhidi ya Moro United,"alisema Basena.

Aliongeza kuwa mbali ya Sunzu, pia beki wake tegemeo Amir Maftah ambaye hakucheza katika mechi dhidi ya Toto African ataukosa pia mchezo huo na anaweza hata kukosa mechi ya timu ya taifa,'Taifa Stars' dhidi ya Morocco.

"Kwa kweli nina majeruhi wengi sio Sunzu tu, hata Maftah atakosekana kwani bado hajarejea katika hali yake ya kawaida na inawezekana hata timu ya taifa ikamkosa, tuna wakati mgumu, tunafurahia kurudi kwa Mwinyi wengine wanatoka, lakini hakuna jinsi tutapigana na kuhakikisha hatupotezi mchezo,"alisema Basena.

Wakati huo huo, Basena alizungumzia sare yao ya mabao 3-3 na Toto African kwa kusema walicheza vizuri licha ya kwamba wachezaji wake walifikiri zaidi katika kushambulia na kusahau kujilinda ambapo aliahidi kurekebisha hali hiyo.

Katika hatua nyingine Basena alitoa wito wa askari wanaosimamia usalama kwenye viwanja vya soka kuwajibika kila mmoja kwa nafasi yake ili kuepusha hatari kama iliyojitokeza katika mechi kati yao na Toto African ambapo mbwa alimponyoka askari na kuingia uwanjani na kuwafukuza wachezaji wake akiwamo Haruna Moshi 'Boban' na Sunzu.

YANGA WAIWEKEA NGUMU TFF


Uongozi wa mabingwa wa Tanzania Bara Yanga SC, imepinga mabadiliko ya ratiba ya ligi kuu ya Tanzania Bara, kwa mchezo wao kusogezwa mbele mpaka jumatano badala ya jumamosi hii.

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, TFF limesogeza mbele mchezo wa Yanga na Coastal Union mpaka september ya 28 siku ya jumatano, badala ya siku ya jumamosi september 24 mwaka huu.

Yanga wamepinga mabadiliko hayo ya ratiba kwa kusema kitendo cha kubadilisha ratiba ovyo ovyo kwa sasa hautumiki, huku wakitumia kielelezo cha TFF kukataa kuwasogezea mchezo baina yake na Kagera sugar msimu uliopita kutokana na wao kuwa na mchezo wa kimataifa.

Hata hivyo walisema kuwa hakuna haja ya kusogeza mchezo mbele wakati kuna uwanja wa Azam unaweza kupokea mchezo huo badala ya Taifa kama uwanja unavyo onyeshwa.

WADAU PROJECT YA UWANJA WA SIMBA IMEFIKIA WAPI ?













Thursday, September 22, 2011

MABEKI BORA WA KIAFRIKA WALIOCHEZA BARANI ULAYA


SAMUEL OSEI KOFFOUR (GHANA)

Koffour alipelekwa ulaya na Torino akiwa na miaka 13 baada ya kucheza michuano ya watoto kwa timu za nchini Ghana.Koffour ambaye anatajwa kama ndio beki bora muda wote barani Afrika, alishinda tuzo ya BBC kama mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2001.

Alicheza miaka 12 kwa mafanikio akiwa na Bayern Munich ambapo alishinda makombe 6 ya Bundersiliga na makombe 4 ya Kombe la Ujerumani.

Koffour anakumbukwa sana kwa kulia mpaka kutoa makamasi baada ya kufungwa na Manchester United katika dakika za mwisho katika fainali ya champions league mwaka 1999.


NOUREDDINE NAYBET (MOROCCO)

Naybet alicheza michezo zaidi ya 100 ya kimataifa na Morocco na akicheza kwa mafanikio timu ya La Liga Deportivo La Coruna ambapo alishinda kombe la ligi.Uzoefu na kucheza kwa timing ndizo zilikuwa nguzo zake kwenye soka.

Alipohamia kwenye English premier league akiwa na Tottenham alitengeneza ukuta madhubuti kwa pamoja na Ledley King na Micheal Dawson.Pia Naybet alicheza kwenye Ligue 1 na Nantes, na alicheza nchini Ureno akiwa na Sporting Lisbon.


SUNDAY OLISEH (NIGERIA)

Kama ilivyo kwa wachezaji wengi maarufu, safari ya kufanikiwa kwenye soka ya Oliseh ilianzia kwenye mitaani, akicheza soka la kuvutia katika mji mkuu wa Nigeria, Lagos.Ilipofika mwaka 1993 alisajiliwa na timu ya Ubelgiji Liege na kumfanya aitwe kwenye kikosi cha timu super eagles na mechi yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya Ethiopia katika mchezo muhimu wa kugombea nafasi ya kucheza African Cup of Nations ambapo Nigeria walishinda kwa 6-0.

Oliseh pia alicheza kwenye Serie A akizitumikia klabu za Juventus na Reggiana, Ujerumani alizichezea FC Koln na Borussia Dortmund na Uholanzi aliichezea Ajax.

Pia Sunday Oliseh anakumbukwa sana kwa kufunga moja ya mabao bora katika kombe la dunia la mwaka 1998 nchini Ufaransa katika mechi ambayo Nigeria waliifunga Spain kwa mabao 3-2.


LUCAS RADEBE (SOUTH AFRICA)

Alijulikana zaidi kwa jina la ‘Rhoo’, alianza kucheza soka kama golikipa kabla hajabadilishwa na kuwa kiungo na akahamia katika nafasi ya ulinzi wa kati ambayo anatajwa kama moja walinzi bora kuwahi kutokea duniani.

Radebe aliibuka na kujulikana zaidi mwaka 1989 aliposajiliwa na moja ya klabu kubwa barani Afrika , Kaizer Chiefs.

In September 1994, Lucas Radebe na Phil Masinga walihamia Leeds United nchini England.Inasemekana Radebe aliingizwa kwenye hilo dili ili kumfurahisha tu Masinga, lakini alikuja kuwa bora na dhahabu kwenye safu ya ulinzi ya timu hiyo kutoka Yorkshire na hatimaye alipewa unahodha wa klabu hiyo na mashabiki wa timu hiyo wakampachika jina la utani ‘The Chief’

Alikuwa moja ya wacheza soka walioheshimiwa kwa kiasi kikubwa kwenye kizazi chake, aki-deal na majeraha lakini alijituma na kuweka mbele maslahi ya nchi yake na klabu yake.


RIGOBERT SONG (CAMERRON)

Song anabakia kuwa moja ya walinzi bora waliowahi kuvaa jezi ya Indomitable Lions.Amecheza zaidi ya mechi 100, huku akicheza michuano ya kombe la dunia ya mwaka 1994, 1998, na 2002.

Mchezaji huyo wa zamani wa Metz, Salernitana, Liverpool, West Ham United, Cologne, Lens na Galatasary alijulikana zaidi kwa mchezo wake wa nguvu na kujituma, akiwa mfano mzuri kwa kwa uongozi bora uwanjani.

Sambamba na Zinedine Zidane, Song naye amewahi kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika michuano miwili ya World Cup, dhidi ya Brazil kwenye USA 94 na dhidi ya Chile mwaka 1998 nchini Ufaransa.

Mpwa wake, Alex Song, sasa yupo nchini England akiitumikia klabu ya Arsenal.


TARIBO WEST (NIGERIA)

Maarufu zaidi kwa mitindo yake ya ajabu na nywele zenye rangi. Career ya Taribo West barani ulaya ilianza mwaka 1993 alipojiunga na Auxerre, ambapo aliichezea klabu hiyo kwa miaka 4 na nusuna kuisadia timu hiyo kushinda kombe la ligi pamoja na kombe la French Cups.

Uwezo wake wa kuzuia mashambulizi ulimfanikishia ndoto yake na kuhamia Inter Milan, ambapo pia alicheza kwa mafanikio kwa kuisadia timu hiyo kushinda kombe la Uefa Cup mwaka 1998.

Baada ya kuhusishwa sana na kuhamia Liverpool na Juventus, mlinzi huyo aliondoka Giuseppe de Meazza na kwenda San Sirro kwa AC Milan.

West alikuwa moja ya wachezaji wa Nigeria waliocheza kombe la dunia mwaka 1998, na pia alikuwa kwenye the Dream Team ya Nigeria iliyoshinda medali ya dhahabu kwenye Olimpiki mwaka 1996 jijini Atlanta.

Dr. Emmanuel John Nchimbi (Mb) amemteua Bw. Dionis Malinzi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Emmanuel John Nchimbi (Mb) amemteua Bw. Dionis Malinzi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Aidha pia amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Baraza la Michezo la Taifa.

Mhe. Jenister Mhagama (Mb) Mhe.

Mkiwa A. Kimwanga (Mb)
Bw. Jamal Rwambow
Bw. Venance Mwamoto
Bw. Juma Pinto
Dkt. Cyprian Maro
Bw. Kanali Eliot Makafu
Bibi Jeniffer Mmasi
Bw. Ramadhani Dau
Bw. Alex Mgongolwa
Bw. Maulid Kitenge

Wengine ni Wajumbe wa kuteuliwa kutokana na nafasi zao:

Mkurugenzi Mkuu - Bodi ya Michezo ya Kubahatisha

Kamishna wa Elimu - Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Mwakilishi - TAMISEMI
Mkurugenzi wa Michezo – Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Mwakilishi - Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Wajumbe kutoka Wawakilishi wa Vyama vya Michezo (Makatibu) ni:

CHANETA - Chama cha Netiboli Tanzania

TPC - Tanzania Paralympic Committee
AAT - Automobile Association of Tanzania
TSA - Tanzania Swimming Association
BFT - Boxing Federation of Tanzania
RT - Riadha Tanzania
TFF - Tanzania Football Federation
TBF - Tanzania Basketball Federation
TOC - Tanzania Olympic Committee
TTTA - Tanzania Table Tennis Association

Uteuzi huu umefanywa kwa kuzingatia Mamlaka ya Waziri chini ya kifungu cha 3(2) cha nyongeza ya Katiba ya Sheria ya BMT Na. 12 ya mwaka 1967 na marekebisho yake katika Sheria Na. 6 ya mwaka 1971.

Wajumbe hao watalitumikia Baraza kwa kipindi cha miaka mitatu.



Imetolewa na Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo22.09.2011

MATCH LIVE CENTER: POLISI TZ 1:1 MTIBWA SUGAR

Mchezo mmoja tu unachezwa leo kwenye muendelezo wa Ligi kuu ya VODACOM Tanzania Bara.

POLISI TZ 1: 1 MTIBWA SUGAR ( FT )
mfungaji: Juma Semsuye ( dk 13 )-Polisi
Shabani Nditi ( dk 70)-Mtibwa

huyu ndo Mbwa aliyeingia Uwanja wa CCM Kirumba.

Hapa alikuwa anamkimbiza Kiungo Haruna Moshi 'BOBAN' .




Huyu Mbwa alimtoroka Askari na kuingia uwanjani na kuwakimbiza wachezaji kama unavyomuona hapo pichani.








Hapa ilikuwa kabla hajakata kamba....cheki anavyowaangalia Raia....anaonekana ana uchu kweli...



*Tukio hili lilitokea Mkoani Mwanza kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom kati ya TOTO AFRICANS na SIMBA Uliomalizika kwa timu hizo kufungana mabao 3-3.

Chuo cha Louisiana cha nchini Marekani kufungua shule ya michezo Tanzania.

PRESS RELEASE: FOR IMMEDIATE RELEASE
Contact Allison Bruchhaus, (318) 487-7194
bruchhaus@lacollege.edu

HIS EXCELLENCY, PRESIDENT KIKWETE OF TANZANIA MEETS WITH LOUISIANA COLLEGE DELEGATION
New York City, NY – It is a distinguished honor for the administration of Louisiana College, an institution internationally renowned for education, to have been granted the time to meet with His Excellency, President Kikwete of Tanzania.
First and Foremost I would like to extend our word of gratitude to the following people.
1. His Excellency, President Jakaya Mrisho Kikwete for making time off his busy schedule to me
5. Mr. Rahim Zamunda Kangezi-for arranging our meeting-
Members of the delegation, Dr. Randall Esters, Dean of Education and Presidential Envoy for International Affairs, and Joseph Cole, Coordinator for Presidential Affairs, presented a proposal to His Excellency for an international education partnership bringing greater strength to a strong educational system. The proposal included a secondary school, university credits, an athletic academy with both basketball and soccer, and a film program.
His Excellency, President Kikwete, was extremely gracious in giving his time to have a wonderful meeting of intelligent minds. Furthermore to show his support, President Kikwete generously committed at least 150 acres of land for the development of the Louisiana College: Tanzania campus. Louisiana College administrators are incredibly grateful and humbled by the opportunity to meet His Excellency as well as discuss educational opportunity.




Rahim akimkabi Mhe Rais Proposal ya Chuo.




Joseph Cole coordinator of President Affairs ,Alan Barkley Excutive Director Opportunity Education, Mhe Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Dr.Randall E. Esters Dean of education LOUISIANA COLLEGE na Rahim Kangezi Zamunda

AFRICAN LYON BADO WANATAKA CHAO KWA MBWANA SAMATTA



Uongozi wa klabu ya soka ya African Lyon, unajipanga ili kufikisha malalamiko yao Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kushindwa kupatia ufumbuzi suala lao la madai ya mgao wa mauzo ya Mbwana Samata aliyeuzwa na klabu ya Simba katika klabu ya TP Mazembe.

Lyon kwa muda mrefu imekuwa ikidai mgao wao baada ya mshambuliaji Samata kuuzwa TP Mazembe, lakini wamekuwa wakizungushwa na wamefikisha madai yao TFF muda mrefu ila hakuna majibu ya msingi waliyopata.

Akizungumza jijini jana Mkurugenzi wa African Lyon, Rahim Kangezi alisema TFF imekuwa ikipuuza madai yao na kushindwa kuyapatia ufumbuzi jambo hali inayosabisha wachukue uamuzi wa kwenda mbele zaidi kutafuta haki yao.

Alisema moja ya madai wanayoidai TFF ni pamoja fedha za zawadi ambazo walizipata mwaka juzi baada timu hiyo kufanikiwa kuibuka timu yenye nidhamu katika michuano ya Ligi Kuu ya Tanzania msimu fedha ambazo hawajazipata mpaka hivi sasa."Tumevumilia vya kutosha na sasa tunataka kusonga mbele zaidi ili kuhakikisha tunapata haki zetu za msingi ambazo tunastaili kupata.

"Tumekuwa tukiwasilisha malalamiko yetu kila wakati TFF kwa lengo la kuhakikisha tunapata haki zetu, lakini shirikisho hilo limekuwa halitoi ushirikiano wa kutosha kwetu na kushindwa kuyapatia ufumbuzi madai yetu tunayolidai hivyo kutokana na hali hiyo tunaona ni bora kusonga mbele," alisema Kangezi.

Katika hatua nyingine Kangezi alisema pia wanatarajia kuifikisha Fifa klabu ya Simba baada ya kushindwa kuwapa mgao wao baada ya kuuzwa Samatta katika timu ya TP Mazembe.

Alisema kufuatia hali hiyo walifikisha malalamiko yao TFF ikiwa ni pamoja na kulitaka shirikisho kuwaita meza moja viongozi wa Simba na African Lyon ili kuzungumza juu ya jambo hilo, lakini mpaka sasa suala hilo halijapatiwa ufumbuzi na haijulikani ni lini watapata haki yao.


UGANDA YAENDELEA KUWA NAMBA 1 WA SOKA AFRIKA MASHARIKI


Tanzania imeshuka kwa nafasi moja katika viwango vipya vya Shirikisho la Soka Duniani FIFA, ambapo imetoka nafasi ya 125 mpaka 126.Mwezi uliopita Tanzania ilipanda kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya 127 iliyokuwa ikishikilia mwezi Julai mpaka nafasi ya 125.Kwa mujibu wa Fifa, Tanzania imeshuka kwa viwango hivyo kwa nafasi moja baada ya kushindwa kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani na kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Algeria katika mechi ya kufuzu kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika mwanzoni mwa mwezi huu.

Uganda ambayo inaongoza katika viwango vya Fifa katika Ukanda wa Ukanda wa Afrika Mashariki yenyewe vilevile imeshuka kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya 80 mpaka 82.

Kenya yenyewe imepanda kwa nafasi tatu kutoka nafasi ya 133 mpaka 130, wakati Burundi imepanda kwa nafasi tano kutoka nafasi ya 145 mpaka 140 na Rwanda inashika nafasi ya mwisho katika Ukanda huu baada ya kushuka kwa nafasi nne kutoka nafasi ya 138 mpaka nafasi ya 142.

Tanzania inatarajia kucheza mechi ya mwisho ya kufuzu kushiriki fainali za mataifa dhidi ya Morocco hapo Oktoba 9 mjini Casablanca.Katika viwango vya Fifa, Morocco inaonekana imepanda kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya 61 mpaka nafasi ya 59.

Nchi ya Afrika inayoongoza katika viwango hivyo vya Fifa ni Ivory Coast ambayo ipo katika nafasi ya 16 ikifuatiwa na Misri ambayo ipo katika nafasi ya 36, Ghana ipo katika nafasi ya 37, Burkina Faso ipo katika nafasi ya 41 na Senegal ipo katika nafasi ya 42.

Mabingwa wa dunia Hispania wameendelea kuongoza viwango hivyo vya Fifa ikiwa katika nafasi ya kwanza, ikifuatiwa na Uholanzi, Ujerumani, Uruguay na Ureno.Nchi inayoshika mkia katika viwango hivyo vipya vya Fifa ni San Marino ambayo inashika nafasi ya 203.

Februari 1995, Tanzania ilishika nafasi ya 65 katika viwango vya Fifa, hicho ndiyo kiwango cha juu Tanzania kuwahi kushika katika viwango vya FIFA na kiwango cha chini kabisa Tanzania ilishika nafasi ya 175 mwezi Oktoba 2005.Mwezi Januari mwaka huu Tanzania ilikuwa nafasi ya 120, Februari 123, Machi 121, Aprili 112, Mei 117, Juni 127, Julai, Agosti 125 na mwezi huu 126.