Search This Blog

Saturday, August 4, 2012

MBWANA SAMATA AENDELEA KUWAFANYA KITU MBAYA WAARABU - APIGA BAO TP MAZEMBE WAKIIFUNGA 2-0 ZAMALEK

PICHA YA SIKU - EMMANUEL OKWI - IANDIKIE CAPTION


DIDIER KAVUMBAGU AKABIDHIWA JEZI NAMBA 21 YANGA



YANGA WATAMBULISHA RASMI KIFAA CHAO KUTOKA ATLETICO - NI DIDIER KAVUMBAGU



Mshambuliaji wa kimataifa kutoka timu ya Olympic Atletico ya Burundi, Didier Kavumbagu amewasili jana usiku na kujiunga na kikosi cha mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati Young Africans Sports Club tayari kwa kuanza kuitumikia timu yake mpya.

Didier Kavumbagu aliyechezea timu ya Olympic Atletico katika mashindano ya Kagame ya mwaka huu na kuifikisha timu yake hatua ya Robo Fainali, kabla ya kutolewa na timu ya URA ya Uganda.


Pamoja na timu yake kutolewa katika hatua ya robo fainali, Didier alionyesha kiwango cha hali ya juu ikiwa ni pamoja kufunga mabao yote mawili katika mchezo wa kwanza wa Ufunguzi wa mashindano ya Kagame dhidi ya Young Africans.

Mchezaji huyu wa timu ya Taifa ya Burundi amesajliwa kuichezea timu ya Young Africans kwa mkataba wa miaka miwili ambapo atakua mitaa ya twiga na jangwani mapaka mwishoni mwa msimu wa 2013-2014.

Kavambagu alizaliwa tarehe 02/05/1988 mjini Bujumbura na kuanza kucheza soka katika timu za mitaani kabla ya kuchaguliwa timu ya taifa ya vijana U-17 mwaka 2006 na kushiriki mashindano ya kombe la vijana CECAFA U-17 visiwani Zanzibar.

Alionyesha kiwango cha hali ya juu katika mashindano hayo na kupelekea kusajiliwa na timu ya Olympic Atletico ambapo ameitumikia mpaka mwaka huu alipoamua kuachana na yo na kujiunga na mabingwa wapya wa kombe la Kagame Young Africans Sports Club.

Young Africans imeanza jana mazoezi yake kwa ajiliya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara unaotazamiwa kuanza septemba mosi, na wachezaji wote wamehudhuria mazoezi jana na leo Didier amejumuika na wachezaji wenzake kufanya mazoezi chini ya kocha Mkuu Tom Saintfiet katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola. 


source:http://lindiyetu.blogspot.com

SIR ALEX FERGUSON - MASHABIKI WA UNITED WANANITUKANA KWA KUNISHUTUMU KWAMBA NITAFAIDIKA NA UUZWAJI WA HISA ZA KLABU

QUOTE OF THE DAY
"Hakuna ukweli wowote kwenye tuhuma ninazotupiwa. Hizi ni tuhuma ambazo zinanitukana....nadhani inabidi ili liwekwe wazi kwa mashabiki wa Manchester United. Kuhusiana na masuala ya kwamba nimewasifia familia ya Glazer kwa nitafaidika  na uuzaji wa hisa za United kwenye soko la hisa la New York, hakuna ukweli wowote katika tuhuma hizi. Sipokei malipo yoyote moja kwa moja au vinginevyo kutokana biashara hiyo ya hisa."

Haya ni maneno ya Sir Alex Ferguson akijibu maswali ambayo mashabiki wa Manchester United wamekuwakiuliza: kwamba je atakuwa akifaidika kutoka na biashara ya kuuza hisa za klabu katika soko la New York .

KALI YA LEO: KWA USHANGILIAJI HUU WACHEZAJI HAWAPASWI KUFUGA NYWELE NDEFU

STEWART DOWNING AFUNGA GOLI LAKE LA KWANZA AKIWA NA LIVERPOOL MWAKA MMOJA BAADA YA KUSAJILIWA

Friday, August 3, 2012

HUYU NDIO SANTI CAZORLA MCHEZAJI MPYA WA ARSENAL - ANGALIA MAVITU




Hatimaye klabu ya Arsenal wamekamilisha usajili wa kiungo wa Hispania, Santiago Cazorla kutoka klabu ya Malaga, mchezaji huyo amesema kwenye ukurasa wake rasmi wa Twitter.

"Sasa naweza kusema mimi ni mchezaji mpya wa Arsenal," alisema kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27.

Cazorla, ambaye ameichezea timu yake ya taifa mara 47 lakini alikosa ubingwa wa Kombe la Dunia kutokana na kusumbuliwa na ngiri, aliiwezesha Malaga kufuzu kucheza Ligi ya Klabu Bingwa wakati klabu yake ya zamani ya Villarreal ilishuka daraja.



STARS KUIKABILI BOTSWANA TAREHE 15, BINGWA WA KOMBE LA BANCABC SUPER 8 KUPATA MIL.40


LIGI DARAJA LA KWANZA SASA TIMU 24
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kuanzia msimu huu wa 2012/2013 itakuwa na timu 24 kutokana na mabadiliko ya mfumo wa mashindano yaliyofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
 
Kamati ya Utendaji ya TFF ilikutana Julai 29 mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine ilifanya mabadiliko ya mfumo wa mashindano ikiwemo FDL kuchezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini badala ya ule wa awali wa vituo.
 
Kutokana na mabadiliko hayo, timu za FDL zitagawanywa katika makundi mawili ya timu 12 kila moja kutokana na ukaribu wa kanda na kucheza kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
 
Timu ya kwanza kutoka kila kundi itapanda kucheza Ligi Kuu msimu unaofuata wakati ya tatu itakayoungana na hizo mbili itapatikana kwa mechi za nyumbani na ugenini kwa timu zilizoshika nafasi ya pili katika kila kundi.
 
Ili kufikisha idadi ya timu 24 kwenye FDL, Kamati ya Utendaji ya TFF kwa kuzingatia mapendekezo ya Kamati ya Mashindano imeamua timu tatu za juu kwenye Ligi ya Taifa kutoka vituo vyote vitatu vya ligi hiyo zimepanda daraja.
 
Sasa timu 24 za FDL ni Ashanti United (Dar es Salaam), Burkina Moro (Morogoro), Green Warriors (Dar es Salaam), Kanembwa JKT (Kigoma), Kurugenzi Mafinga (Iringa), Majimaji (Ruvuma), Mbeya City (Mbeya), Mkamba Rangers (Morogoro), Mlale JKT (Ruvuma) na Morani (Manyara).
 
Nyingine ni Moro United (Dar es Salaam), Mwadui (Shinyanga), Ndanda (Mtwara), Pamba (Mwanza), Polisi (Arusha), Polisi (Dodoma), Polisi (Iringa), Polisi (Mara), Polisi (Tabora), Rhino Rangers (Tabora), Small Kids (Rukwa), Tessema (Dar es Salaam), Transit Camp (Dar es Salaam), Villa Squad (Dar es Salaam)
 
Timu nne zitashuka daraja kurudi Ligi ya Mkoa. Timu hizo ni mbili zilizoshika nafasi za mwisho kwa kila kundi. Timu nne zitakazopanda kucheza FDL zitapatikana kwa mchujo utakaohusisha mabingwa wa mikoa.
 
Kwa mfumo huo mpya wa mashindano, ligi za mikoa zitakazosimamiwa na kuendeshwa na vyama vya mpira wa miguu vya mikoa zinatakiwa kuwa na timu zisizopungua 16 na zisizozidi 20. Ligi za mikoa pia zitachezwa mwaka mzima kwa mikondo miwili (nyumbani na ugenini).
 
Ligi ya mkoa itashusha timu mbili na kupandisha nyingine mbili kutoka ligi ya wilaya. Ligi za wilaya zitakazosimamiwa na kuendeshwa na vyama vya mpira wa miguu vya wilaya zinatakiwa kuwa na timu zisizopungua 10 na zisizozidi 20.
 
Kwa wilaya zenye timu zaidi ya 20, chama husika cha mpira wa miguu kitapanga utaratibu wa kuzichuja kwa mashindano ili kupata zile bora 20 zitakazocheza ligi rasmi ya wilaya.
 
Mabingwa wa wilaya katika mkoa husika watacheza mechi za kuchujana (play offs) ili kupata timu mbili zitakazopanda daraja kucheza ligi ya mkoa husika.
 
Kutokana na mabadiliko hayo ya mfumo wa mashindano, sasa madaraja rasmi ya ligi ni Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi ya Mkoa (Ligi Daraja la Tatu) na Ligi ya Wilaya (Ligi Daraja la Nne).
 
TFF inasisitiza kuwa kwa mujibu wa kalenda yake ya matukio, kipindi cha usajili wa wachezaji kwa madaraja yote ni kimoja, na ligi zitachezwa kwa wakati mmoja.
 
Usajili wa hatua ya kwanza ni kuanzia Juni 15 hadi Agosti 10 mwaka huu wakati kipindi cha pili cha usajili ni Agosti 21 hadi Septemba 4 mwaka huu. Usajili wa dirisha dogo ni Novemba 15 hadi Desemba 15 mwaka huu.
 
Ligi kwa madaraja yote zitaanza Septemba. Ligi Kuu itaanza Septemba Mosi mwaka huu, Ligi Daraja la Kwanza ni Septemba 15 mwaka huu, Ligi ya Mkoa na ile ya Wilaya zenyewe zitaanza Septemba 8 mwaka huu.
 
Mechi za kufungua msimu kwa madaraja yote (Ngao ya Jamii) ambazo kwa sasa zinakutanisha bingwa na makamu bingwa zitachezwa Agosti 25 mwaka huu wakati michuano ya Kombe la FA itaanzia wilayani Septemba 24 mwaka huu.
 
BINGWA MICHUANO YA BANCABC SUPER 8 KUPATA MIL 40/-
Bingwa wa michuano ya BancABC Super 8 inayoanza keshokutwa (Agosti 5 mwaka huu) katika miji ya Dar es Salaam, Zanzibar, Mwanza na Arusha atapata sh. milioni 40 wakati makamu bingwa sh. milioni 20. Pia timu mbili zitakazoishia hatua ya nusu fainali kila moja itapata sh. milioni 15 wakati zilizobaki kila moja itapata sh. milioni 5.
 
Timu zimepangwa katika makundi mawili ya A na B. Kundi A lina timu za Simba (mabingwa wa Tanzania Bara), Jamhuri, Zimamoto na Mtende zote za Zanzibar. Kundi ni Super Falcon (mabingwa wa Zanzibar), Azam, Mtibwa Sugar na Polisi Morogoro zote za Tanzania Bara.
 
Mechi za ufunguzi keshokutwa (Agosti 5 mwaka huu) ni Simba vs Jamhuri (Dar es Salaam), Zimamoto vs Mtende (Mwanza), Mtibwa Sugar vs Polisi Morogoro (Arusha) na Super Falcon vs Azam (Zanzibar). Awali mashindano yalikuwa yaanze Agosti 4 mwaka huu lakini yamesogezwa mbele kwa siku moja.
 
Hatua ya makundi itamalizika Agosti 12 mwaka huu. Mechi za nusu fainali na fainali zote zitachezwa Dar es Salaam. Nimeambatanisha ratiba.
 
Mdhamini bancABC atagharamia usafiri wa ndege kwa timu zote kutoka kituo kimoja hadi kingine, malazi na jezi. Yanga imejitokea kwenye mashindano hayo na nafasi yake imechukuliwa na Mtibwa Sugar ambayo ilishika nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu ya Vodacom.
 
KOZI YA UONGOZI YA FIFA KUANZA AGOSTI 6
Kozi ya Uongozi na Utawala ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) itafanyika Msimbazi Center jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 6-11 mwaka huu ikiwa na washiriki 30.
 
Washiriki wa kozi hiyo itakayonedeshwa na wakufunzi kutoka FIFA ni viongozi kutoka TFF, Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, klabu za Ligi Kuu na viongozi wa mpira wa miguu wa wanawake.
 
Walioteuliwa kushiriki ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani, Rais wa ZFA Amani Makungu, wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF; Ahmed Mgoyi, Blassy Kiondo, Stanley Lugenge, Khalid Abdallah, Hussein Mwamba na Eliud Mvella.
 
Wengine ni Katibu Mkuu wa ZFA, Kassim Salum, Katibu Msaidizi wa ZFA, Masoud Attai, wenyeviti wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Kagera (Jamal Malinzi), Dodoma (Nassoro Kipenzi) na Pascal Kihanga (Morogoro).
 
Makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Mara (Mugisha Galibona), Mtwara (Vincent Majiri), Morogoro (Hamisi Semka), Kagera (Salum Chama), Tanga (Beatrice Mgaya) na Dodoma (Stuart Masima). Pia yumo Mwenyekiti wa Coastal Union, Ahmed Hilal na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga.
Washiriki wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, Mkurugenzi wa Ufundi, Sunday Kayuni, Ofisa Habari, Boniface Wambura, Mkurugenzi wa Masoko na Matukio, Jimmy Kabwe, Mkurugenzi wa Mashindano, Saad Kawemba, Ofisa Sheria wa TFF, Neema Lucumay, Ofisa wa Mpira wa Miguu wa Wanawake, Grace Buretha, Amina Karuma (Mpira wa miguu wa wanawake) na nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa.
 
STARS KUIKABILI BOTSWANA AGOSTI 15
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Agosti 15 mwaka huu itapambana na Botswana (Zebras) katika mchezo maalumu wa Kalenda ya FIFA utakaofanyika jijini Gaborone.
 
Tayari Kocha Kim Poulsen alishatangaza kikosi cha wachezaji 21 kitakachoingia kambini Agosti 8 mwaka huu tayari kwa mechi hiyo ya kirafiki ya kujipima nguvu.
 
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

SALAMA JAY NA MADAM RITHA WAZUNGUMZIA EPIQ BSS DAR

MRISHO NGASSA ATAMBULISHWA RASMI SIMBA - AFANYA MAZOEZI KWA MARA YA KWANZA NDANI YA UZI MWEKUNDU

Mchuma mpya aliopewa Ngassa baada ya kusajiliwa na Simba

Mrisho Ngassa akiingia mazoezini

Mashabiki wa Simba wakiwa wanampokea mchezaji wao mpya Mrisho Ngassa

Ngassa ndani uzi mwekundu akiwa na Uhuru Suleiman

Ngassa akipambana na Amri Kiemba




Na jezi yake ile ile namba 16

Wanasimba wakiwa juu ya mawe ya ufukwe wa COCO wakiwaangalia wachezaji wao wakifanya mazoezi

Hapa Ngassa akiwa amezingirwa na mashabiki wa Simba baada ya kufika makao makuu ya klabu hiyo kutambulishwa

Mrisho Ngassa akiwa na uzi wake mpya baada ya kutambulishwa makao makuu ya Simba

Ujumbe kwa uongozi wa Yanga.


Picha zote zimepigwa na Salehe Ally wa GPL

AZAM: 12 WAMEOMBA KAZI YA UKOCHA - HATUKUMFUKUZA STEWART HALL

Uongozi wa klabu ya Azam umesema tayari imepokea maombi ya makocha  12 wanaowania nafasi ya kukinoa kikosi cha timu hiyo.Maombi ya makocha hayo yanatokana na uamuzi wa hivi karibuni uliotangazwa na uongozi wa klabu ya Azam wa kusitisha mkataba wa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Stewart Hall.

Baada ya kutangazwa kuondolewa kikosini, klabu hiyo ilimtangaza kocha wa muda, Vivek Nagul raia wa India atakayesaidiana na Kalli Ongala.

Mwenyekiti wa Azam, Said Mohamed alisema kuwa miongoni mwa maombi yaliyopokelewa ni ya makocha wazawa na mengine ni ya makocha kutoka nje ya nchi.

"Kikubwa ni kwamba tumepokea maombi ya makocha 12 mpaka sasa miongoni mwao ni  wazawa na wengine kutoka nje ya nchi,".alisema Mohamed.

Hata hivyo, Mohamed hakuwa tayari kutaja majina ya makocha wala  nchi wanazotoka kwa madai kwamba bado wanafanya upembuzi yakinifu na muda si mrefu wataweka bayana.

Aliongeza kuwa, vigezo vitakavyotumika katika kumpata kocha wao mpya ni rekodi zake katika kufundisha soka na si vinginevyo.

Wakati huu huo, Mohamed amekanusha taarifa zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa klabu yake imemtimua  Hall baada ya kumpanga Winga Mrisho Ngasa katika pambano dhidi ya Yanga.

"Niweke wazi kwamba uongozi wangu unafanya kazi kwa kuzingatia ushauri  wa benchi la ufundi ,hakuna tuhuma zozote zilizoletwa kwetu zinazomhusu  Ngassa, sasa kwanini tumfukuze kocha, huo ni uzushi tu. 


Kukanusha huku kwa Azam kwamba walimfukuza Stewart kunakuja siku mbili baada ya baadhi ya vyombo vya habari kuripoti kwambakocha huyo alitimuliwa baada ya kumpanga Ngassa kwenye fainali japokuwa likatazwa kufanya hivyo na uongozi wa AZAM FC.

GOLI LA SIKU: KIPA MKONGWE WA BRAZILI ROGERIO CENI

HUYU NDIO LIONEL MESSI ANAYEFUATIA BARCELONA - ANAITWA GERARD DEULOFEU

Ni kijana mwenye miaka 18, aliyeanza kuitumikia klabu ya Barcelona kwa takribani miaka 10 iliyopita. 
Kinda la kihispania ambaye anatabiriwa na wengi kuwa Lionel Messi au Cristiano Ronaldo mpya katika ulimwengu wa soka duniani. 

 Hii hapa ni video yake inayomuonyesha tangu alipokuwa mdogo akaiichezea timu ya Barcelona ya watoto wa chini ya miaka 11 mpaka alivyopandishwa  kuichezea Barcelona B. Angalia video hii then utoe maoni yako kwamba ni kweli anastahili sifa anazopewa. 

By Aidan Charlie

MSAADA TUTANI: HUYU NI NANI





TSC MWANZA YAENDELEZA BALAA - UJERUMANI - YAITANDIKA 3-1 NUARBERG NA KUTWAA KOMBE LINGINE

Timu ya kituo cha TSC Mwanza imeendelea kutoa dozi katika michuano mbalimbali inayoshiriki hapa Ujerumani.


Baada ya wiki iliyopita kufanikiwa kutwaa ubingwa wao kwanza tangu waanze ziara yao hapa Ujerumani, kisha kufungwa katika fainali ya kombe Fallerhof kwa penati na FC Basel siku nne zilizopita, siku ya jana klabu hiyo ya academy ya watoto wa mitaani iliyopo jijini Mwanza iliifunga klabu ya Nuarnberg kwa mabao 3-1 katika mechi ya kugombea ya kugombea kikombe cha hisani hapa nchini Ujerumani.


Katika mchezo TSC Mwanza waliwazidi wapinzani katika dakika takribani zote za mchezo na wakafanikiwa kufunga mabao yao yote matatu kupitia kinda lenye hatari mbele ya nyavu Miraji Madenge aka Shevchenko ambaye ni mchezaji wa Simba B.



Shaffih Dauda nikiingia uwanjani kuangalia mechi


Thursday, August 2, 2012

HIVI NDIVYO ADEN RAGE ALIVYOWAPIGA BAO YANGA NA KUMSAINI MBUYI TWITE

Wakati makamu mwenyekiti wa Simba Geodfrey Nyange Kaburu na mwenyekiti wa kamati ya usajili Zakaria Hans Pope wakiwa wanamalizana na kiungo mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa na mabingwa wa Tanzania bara, upande mwingine mwenyekiti wa klabu hiyo Mheshimiwa Aden Rage nae alisafiri umbali wa kilomita zipatazo 1,459.7, kutoka Dar kwenda Kigali kukamilisha usajili wa beki wa kati wa APR Mbuyi Twite.

Wakati Rage akiwa anamsainisha Twite ambaye pia alikuwa akiwindwa na mabingwa wa Africa mashariki na kati Yanga - upande mwingine Ngassa alikuwa anatia saini kuitumikia Simba kwa miaka 2.

Kwa maana hiyo Simba wakawa wameipiga bao wapinzani wao Yanga ambao wao pia walikuwa wakiwahitaji wachezaji hao wote wawili Twite na Ngassa.

Na haya ndio matambo ya Simba kupitia msemaji wao Ezekiel Kamwaga kuhusu kuwapiga bao wapinzani wao.




Kigali, saa nne kasoro asubuhi ya leo....Mbuyi Twite anasaini mkataba wa kuitumikia Simba mbele ya Mhe; Ismail Aden Rage...Wakati akipata kahawa, jamaa mmoja anaitwa Bin Kleb akapiga simu, "Twite, siye Yanga tunakutaka sana tuambie tu tuje lini ili tumalizane....Akawekewa loud speaker; akaambiwa Mzee, hapa napata cappuccino nikiwa na Mwenyekiti wa Simba...Kleb akakata simu....2-0....1-0 ilikuwa Ngassa.......Jamani Simba ina watu kibao....Jamani Simba...Mi Casa Es Su Casa
By Aidan Charlie

EXCLUSIVE: MRISHO NGASSA AMALIZANA NA SIMBA - ALIPWA MILLIONI 30, GARI NA MSHAHARA WA MILLIONI 2 KWA MWEZI

Hatimaye leo mchana sakata la usajili wa mchezaji wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa akiichezea klabu ya Azam msimu uliopita, kabla ya jana kuuzwa kwenda klabu ya Simba limemalizika.


Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya klabu ya Simba, leo mchana walikutana na mchezaji mwenyewe ili kuweza kukubalina juu ya mahitaji yake binafsi, baada ya jana wekundu hao wa msimbazi kumalizana na Azam.


Kwenye mkataba wake mpya na Simba, Ngassa atapewa gari aina ya Verossa, ada ya usajili millioni 30 pamoja na kupewa mshahara wa millioni 2 kwa mwezi kama alivyokuwa akilipwa kwenye klabu aliyotoka ya Azam.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari mkataba ni mwaka mmoja.




AZAM WATOA UFAFANUZI WA SAKATA LA USAJILI WA MRISHO NGASSA - YANGA ILIONYESHA KUTOMUHITAJI MCHEZAJI, AAMBIWA ABAKI AZAM NA KUKAA BENCHI MWAKA MZIMA AU AENDE SIMBA

Klabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa ya ufafanuzi juu ya sakata la mchezaji Mrisho Ngasa ambalo linaonekana kupotoshwa
1.     Azam FC ilitangaza kuwa biashara ya mchezaji Mrisho Ngasa ingefungwa siku ya Jumatano 1/08/2012 saa saba mchana na ilivitaka vilabu vyenye interest na mchezaji huyo kufika makao makuu ya Azam FC ofisi ndogo zilizopo kwenye kiwanda cha unga cha Azam-Mzizima zikiwa na pesa taslimu. Bei ya mauzo iliyopangwa ilikuwa ni Dola 50,000. Lakini katika mawasiliano ya email kwa makatibu wakuu wa Simba na Yanga, Azam FC iliweka bayana kuwa ilikuwa tayari kushusha bei ya mauzo na ingemuuza Ngasa kwa timu ambayo dau lake lingekuwa kubwa zaidi ya mwenzake.
 
Kwa maana hiyo biashara ya mchezaji mrisho ngasa ilifanyika kwa uwazi. Lengo la Azam FC lilikuwa ni kutoa haki kwa kila klabu yenye uwezo wa kifedha kuweza kupata huduma ya Ngasa.
 
Pia tunaomba ifahamike bayana kuwa mchezaji Mrisho Ngasa alipewa taarifa kuwa anauzwa na aliombwa asaidie kushawishi klabu anayoitaka ifike kwetu na ofa yake. Ngasa alitamka bayana kuwa yupo tayari kwenda klabu yoyote ambayo Azam FC itaona imekidhi mahitaji yake kwa masharti kuwa maslahi yake ya kimkataba kati yake na Azam FC yazingatiwe.
 
2.     Hadi kufikia siku ya Jumatano 01/08/2012 saa saba mchana. Ni klabu ya Simba pekee iliyojibu kwa maandishi na kuonesha nia ya kumchukua Ngasa. Yanga wao hawakuwahi kujibu email, ingawa kwa majibu ya simu Mjumbe wao wa Kamati ya usajili Bw Sefu Magari alitangaza kuwa Ngasa hana thamani ya zaidi ya milioni 20. Na Yanga haikuwa tayari kuboresha ofa yake.
 
3.     Muda wa kufungwa kwa biashara ya kumuuza Ngasa ulipofika, ni simba pekee kupitia kwa makamu Mwenyekiti wake Bw Geofrey Ngange na Mhasibu wake ndiyo waliofika wakiwa na pesa taslimu shilingi milioni 25. Yanga hawakuonekana na hawakutaka kupokea hata simu walizokuwa wakipigiwa kuulizwa kama wana interest.
 
4.     Kikao cha dharura cha Azam FC kilikaa na kuamua kuwa biashara ya kumuuza Ngasa ilishindikana kutokana na kutokupatikana kwa mnunuzi mwenye dola 50,000. Kwa maana hiyo Azam FC iliamua kumpeleka Ngasa kwa mkopo kwenye klabu iliyofika na kuonesha nia ya kumhitaji (Simba)
 
5.     Simba walipewa sharti la kuhakikisha wanamlipa Ngasa mshahara wake kamili (TZsh 2,000,000) pamoja na stahiki zake nyingine zote za kimkataba
 
6.     Sababu za kumpeleka Ngasa kwa mkopo ni kumuepusha na adhabu ambayo klabu ya Azam FC ingetoa kwa Ngasa kama angebaki.
7.     Azam FC inapenda kuweka wazi kuwa haijamlazimisha Ngasa kwenda Simba kama inavyopotoshwa. Kama Ngasa anataka kuvunja mkataba wake au kama Yanga bado wanamhitaji basi waje na dola 50,000 na Azam FC itawauzia kwani licha ya kwamba amepelekwa kwa mkopo simba lakini Ngasa bado ni mali ya Azam FC
 
8.     Tunaomba kuweka msimamo wetu kuwa hatupo tayari kumlipa Ngasa na kuvunja mkataba wake na hatuna sababu ya kufanya hivyo. Kama Ngasa hataki kwenda tunakompeleka Azam FC inamruhusu kubakia klabuni na kutumikia adhabu.
 
9.     Lakini Ngasa na washauri wake waelewe kuwa akiamua kubaki Azam FC atakaa nje ya uwanja kwa muda wote uliosalia kwenye mkataba wake, kwani Azam FC haipo tayari kumvisha jezi mchezaji anayefanya vitendo vya utovu wa nidhamu.
 
10. Kwa kuwa Sakata hili limeanza kuhusishwa na sakata la Mchezaji ramadhani Chombo. Naomba nitoe ufafanuzi kama ifuatavyo. Redondo alipewa option tatu za kuchagua baada ya kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu timu ilipokuwa safarini Mwanza.
a.     Kupelekwa kwa mkopo Moro United?
b.     Kupatikana kwa mnunuzi mwenye shilingi milioni 40
c.      Kukubali adhabu ya kufungiwa kwa miezi mitatu na kulipwa nusu mshahara wahati akitumikia adhabu.
Redondo alithibitisha kuipenda Azam FC kwa kukataa kuuzwa au kupelekwa kwa mkopo. Alikubali kutumikia adhabu yake na ilipoisha alirudi na kuomba msamaha na sasa ni mmoja kati ya wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juu sana. Azam FC inajivunia kuwa na mchezaji kama Redondo na bila kupepesa macho wala kung’ata maneno. Azam FC inamchukulia Redondo kama mtu spesho na mwenye mapenzi ya dhati na klabu yake na inamtaka aendelee kuwa na moyo huo.
 
Imetolewa na utawala.
Azam FC

THIERRY HENRY, ANELKA, NASRI, RIBERRY, MESUT OZIL, NA WACHEZAJI WENGINE MAARUFU WALIO NDANI YA MFUNGO WA MWEZI WA RAMADHANI


Nuri Sahin - Mchezaji wa Real Madrid na Uturuki

Bilali Ahmed maarufu kama Frank Ribery akiwa na mchezaji Hamit Altintop walipoenda Makka

Samir Nasri na utukutu wake wote mwezi huu yupo ndani ya mfungo

Karim Benzema

Hatem Ben Arfa - Kiungo wa Newcastle na Ufaransa nae nafunga mwezi mtukufu wa Ramadhani

Mesut Ozil - Raia wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki

Samir Khedira - Raia wa Ujerumani mwenye asili ya Tunisia.
Abdulsalaam Bilal maarufu kama Nicolas Anelka akiwa na mashekhe alipoenda hijja huko Makka

Bilal Abidal - maarufu kama Eric Abidal akisoma Quran akiwa kwenye ndege wakati akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa mwaka jana.

Anaitwa Ibrahim Affelay mchezaji wa kimataifa wa Barcelona na Uholanzi


HII NI VIDEO INAYOMUONYESHA THIERRY HENRY AKITHIBITISHA KUBADILI DINI NA KUWA MUISLAM AKIFUATA MFANO WA RAFIKI ZAKE ANELKA, NA ABIDAL.

FRANK RIBERY AFUNGA GOLI LA MWAKA UJERUMANI - APIGA SHUTI KATIKATI YA UWANJA NA KUTINGA WAVUNI

ANGALIA GOLI LA SIKU - JUAN BUSTOS

EPIQ BONGO STAR SEARCH SEARCH DAR YAVUNJA REKODI - VIJANA ZAIDI YA 5000 WAJITOKEZA SIKU YA KWANZA

Mmoja wa vijana waliojitokeza kushiriki katika shindano la kusaka vipaji vya kuimba la Epiq Bongo Star Search akionyesha uwezo wake wa kupiga gita lililotengenezwa kienyeji nje ya ukumbi kabla ya kukutana na majaji kwenye fukwe ya Coco jijini Dar es Salaam leo. 
Sehemu ya vijana waliojitokeza kushiriki katika shindano la kusaka vipaji vya kuimba la Epiq Bongo Star Search wakiwa nje ya ukumbi kabla ya kukutana na majaji kwenye fukwe ya Coco jijini Dar es Salaam leo.
Majaji wa shindano la kusaka vipaji vya kuimba la Epiq Bongo Star Search (kutoka kushoto) Salama Jabir, Ritha Paulsen na Master Jay, wakiwa "mzigoni" kwenye fukwe ya Coco jijini Dar es Salaam leo. 
Mshiriki wa BSS akijaribu bahati yake mbele ya majaji

ZAIDI ya vijana 5,000 wamejitokeza katika usaili wa shindano la kusaka vipaji vya kuimba la Epiq Bongo Star Search katika fukwe za Coco leo.


Usaili huo ambao utakuwa ni wa siku tatu umeonekana kuwa ni wa aina yake hasa kutokana na idadi kubwa ya vijana waliojitokeza jana ikiwa ndio siku ya kwanza.


Katika sehemu mbalimbali za uwanja huo ilionekana kujazwa na vijana hao ambao wengi wao walikuwa wakiimba huku wengine wakiwa wanafanya mazoezi ya kutumia aina mbalimbali za vifaa vya muziki.


Akizungumzia shindano hilo, jaji mkuu wa Epiq BSS, Ritha Paulsen alisema kuwa Dar es Salaam ambao ndio mkoa wa mwisho katika usaili huo hamasa imekuwa kubwa sana kwa washiriki huku wengi wao wakiwa na matumaini makubwa ya kuchaguliwa.


"Tumeona vijana wazuri sana, na kama kawaida ya Dar tunatarajia ushindani mkali kwa mkoa huu, na ndio maana tutachukua vijana kumi na saba kutoka hapa," alisema Ritha.


Afisa Biashara wa Zantel, Sajid Khan, amepongeza umati mkubwa wa watu uliojitokeza kwa upande wa Dar es Salaam akisema kwa vipaji vilivyopatikana mwaka huu watu watarajie burudani ya kutosha vipindi vikianza kuonyeshwa kwenye luninga.


"Tunatoa zawadi kubwa kwa mwaka huu, Sh. milioni 50 pamoja na mkataba wa kurekodi, hivyo vijana wana kila sababu ya kujitokeza kwa wingi kutimiza ndoto zao," alisema Khan.


Zoezi hili litaendelea siku ya kesho (Alhamisi) na kesho (Ijumaa) ambapo washiriki 17 watakaopatikana wataungana na wengine 33 kutoka mikoani kufikisha idadi ya washiriki hamsini watakaoingia kambini.