Search This Blog

Thursday, August 2, 2012

HIVI NDIVYO ADEN RAGE ALIVYOWAPIGA BAO YANGA NA KUMSAINI MBUYI TWITE

Wakati makamu mwenyekiti wa Simba Geodfrey Nyange Kaburu na mwenyekiti wa kamati ya usajili Zakaria Hans Pope wakiwa wanamalizana na kiungo mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa na mabingwa wa Tanzania bara, upande mwingine mwenyekiti wa klabu hiyo Mheshimiwa Aden Rage nae alisafiri umbali wa kilomita zipatazo 1,459.7, kutoka Dar kwenda Kigali kukamilisha usajili wa beki wa kati wa APR Mbuyi Twite.

Wakati Rage akiwa anamsainisha Twite ambaye pia alikuwa akiwindwa na mabingwa wa Africa mashariki na kati Yanga - upande mwingine Ngassa alikuwa anatia saini kuitumikia Simba kwa miaka 2.

Kwa maana hiyo Simba wakawa wameipiga bao wapinzani wao Yanga ambao wao pia walikuwa wakiwahitaji wachezaji hao wote wawili Twite na Ngassa.

Na haya ndio matambo ya Simba kupitia msemaji wao Ezekiel Kamwaga kuhusu kuwapiga bao wapinzani wao.




Kigali, saa nne kasoro asubuhi ya leo....Mbuyi Twite anasaini mkataba wa kuitumikia Simba mbele ya Mhe; Ismail Aden Rage...Wakati akipata kahawa, jamaa mmoja anaitwa Bin Kleb akapiga simu, "Twite, siye Yanga tunakutaka sana tuambie tu tuje lini ili tumalizane....Akawekewa loud speaker; akaambiwa Mzee, hapa napata cappuccino nikiwa na Mwenyekiti wa Simba...Kleb akakata simu....2-0....1-0 ilikuwa Ngassa.......Jamani Simba ina watu kibao....Jamani Simba...Mi Casa Es Su Casa
By Aidan Charlie

21 comments:

  1. Yanga wangewataka hao wasingewakosa,waulize Nizar na kelviin yondan,yanga haikuwa serious na hao,hata shaffih unajua.tatizo lako unazi,wapi kinje na lino ambao uliwasifia sana

    ReplyDelete
  2. Sidhani kama hilo ni bao,nawapongeza simba kwa kucheza na akili za wanachama wao hasa wanapoelekea kwenye mkutano mkuu wakiwa hawajui watawaeleza nn kuhusu yondan na kutolewa mapema kagame.pili siamini kama simba ya sasa inuwezo hata wa kutoa 10M kwa anayebisha aniambie zile fedha tulichanga pale sigara kwa ajili ya familia ya mafisango ziwapi?

    ReplyDelete
  3. cshangai kwa kuchukua hao wachezaji!najua fika hii yote ni kuwafumba mdomo wanachama kuhusu okwi na yondani hasa mkijua mna uchaguz uko mbele yenu!mchezaji anaemtaka yanga cmba hawezi kutia mguu!yondani,bahanuz,nizar wote hawa mliwataka leo hii wako wp?hao wote mnaobeba walishindwa kuzisaidia timu zao ambazo zimesheheni vipaji kuliko nyinyi na yanga ikabeba ubingwa!wako wapi musa mude,lino,kinje,mbia mdundiko,sunzu mmewasifu sana shafi mchango wao uko wapi?shafi huna jipya!

    ReplyDelete
  4. huyu kamwaga ana akili za kitoto sana anaandika upuuzi badala ya kuongea mambo ya maana,yanga walikuwa hawahtaji mwalimu hana haja nao na kama wangewataka wana uwezo wa kumnunua mpaka huyo kamwaga.

    ReplyDelete
  5. Wewe Aidan acha mapenzi wa wazi, tuwekeeni habari za maana. Mie naitwa Juma, nakaa hapa Kigali, ni mtanzania nafanya kazi UN hapa. Ukweli ni kuwa Yanga hawakuwa wanamtaka Twite, mie nimempokea huyo Rage...Waandishi wa bongo tuache uongo, why cant you be professional?

    Nimempokea Rage, mie Mtanzania mwingine (Jina Kapuni)na ndugu yake Haruna wa Yanga...so unapoandika habari siyo za kweli, sidhani kama ni fair....kazi yenu ni kuripoti na siyo kushabikia...

    Juma

    ReplyDelete
  6. UMPOKEE RAGE WW KM NANI WKT RAGE KAPOKEWA NA VIONGOZI WA APR ACHENI UWONGO NYIE WABONGO WA JANGWANI.. SISI ATUSAJILI KWA SIFA BALI TUNASAJILI KWA NAFASI NA HII NDIO KANUNI YETU WANA MSIMBAZI... MNAJUA MAANA YA TAIFA KUBWA ULIZA MTAAMBIWA NA NYIE YANGA SUBILINI UCHAGUZI WA CCM WENZENU... AKA COMPANYERO FROM ILALA FC BOOM

    ReplyDelete
  7. ww acha uwongo wewe umpokee rage km nani wkt rage kapokewa na uongozi wa apr.. alafu ukisema haruna niyombovu ndugu yako tukuelewe vp.. simba sc tutabaki kuwa taifa kubwa atununui mchezaji toka shanga sc ya jangwani maji machafu tunazalisha product zetu alafu nyie shanga sc ndio mnawachukua... companyero from ilala FC BooM

    ReplyDelete
  8. Watoa maoni hapo juu mmechangia vizuri sana, awa waandishi kanjanja ndo maana wanaandika ushabiki badala ya habari afu mkisemwa mnakuwa wakaalii.tunasubiri tarehe 23/12/2012 asign Yondani, msg sent

    ReplyDelete
  9. Kimewaoma sana wana Yebo yebo.....SIMBA OYEE

    ReplyDelete
  10. Hii blog ni bora iadiishwe jina iwe blog namba mbili ya simba...Yanga wamechukua Kagame hamkutoa analysis na coverage ya habari vya kutosha. Kuwa shabiki wa simba haina maana kila mara uandike misifa kuhusu simba tu hata pale wanapokosea.Mlishajiulza wapi mlipojikwaa hadi kuvurunda Kagame?Acha unazi kwe uandishi wa habari..ni hayo tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. unaisoma ya nini kila siku. We kama imekuuma Simba kuwachukua hao wachezaji umia kimyakimya. Hayo ni maneno ya Ezekiel Kamwaga na siyo ya mwendesha blog. PING

      Delete
  11. Akili za Wana Yanga kama za kushikiwa, nyie yanga akina nani kila mnayemtaka mna uwezo nae. Mnunueni OKWI kwa dola 100,000/= ndio tutaona kila mnayemtaka mnaweza kumnunua..Vinginevyo nyie ni kama Oljoro au Toto africa, cha kushangaza kipi hasa mnachojivunia???? Mwaka jana mlichukua Kagame mwisho wa siku mkatimua kocha na mlimuita hivyo hivyo ya kwamba alikuwa kocha bora. Huyu kocha wenu mpya nampa mechi 6 za ligi tuone kama hajafungasha virago.

    Mashabiki wa Yanga jipya hana. Jana Louis Sendeu kasema wataishtaki simba na azam kwa kumpeleka Ngassa sehemu asiyotaka. Na kasema hayo akiwa kwenye club ya yanga tena nyuma yake kukiwa na logo ya kilimanjaro. Habari hiyo imeoneka taarifa ya habari ya jana ITV usiku. Sasa aina gani ya msemaji mliyekuwa naye nyie kandambili.

    Yanga imepitwa na wakati.

    Allan Shearer..

    ReplyDelete
  12. Ushuzi mtupu,Yanga kuna mabeki wangapi wa kati leo hi iende ikaue nafasi 1 ya kusajili mchezai wa kgeni kwa kuongeza beki wa kati wa nje,hapo mnacheza na akili za Mashabiki wenu Mazuzu wa Simba,tayari kuna Vidic na Canavaro Twite aje acheze namba ngapi sasa? hapo sijakuhesabia akina Ladislas Mbogo na Chuji ambao pia hupiga hiyo namba....wote hawa wameigharimu team kiasi kidogo sana hata mishahara yao ni ya kitanzaniaX2 tofauti na hilo fuba mlilompa huyo Twite na mshahara mtakaokuwa mnampa kila mwezi

    ReplyDelete
  13. Azam wajinga sana, walikuwa na mipango mizuri sana, tatizo lao kubwa na hakika Azam itakufa siku si nyingi au itaenda Zanzibar au watapewa wana Temeke, Tatizo kubwa ni urafiki wao na Simba, hizi timu kubwa zina unafiki na ujinga mkubwa, angalia hawajawahi kufika fainali ya Kagame badala ya kujipongeza na kuangalia wapi wamekosea wanaanza kufukuzana kisa Ngasa kugoma kusaini, pili kuvaa jezi ya Yanga. Kuna mtu asiyejua Ngasa ni Yanga? Hata kama kasaini Simba yeye ni Yanga na kuna siku mtampiga Kaburu kwa kumleta Ngasa huko, Sasa rada za yanga hazitakuwa ngumu hata simba wakikaa bamba beach ni kama wapo na Yanga. Ngasa atapiga hata Hat Trick mechi za Villa squad sijui Polisi lakini ikija ile muhimu atakuwa anapangua wachezaji huku anakatisha katikati badala ya kwenda mbele, kama hamuamini mtashuhudia. Sasa Azam wanamwambia Sure boy kapokea pesa mechi na Yanga! inabidi nicheke, Ukizoae kuhonga waamuzi ndio matatizo yake hayo. Kalambo wa Azam upo hapo,

    ReplyDelete
    Replies
    1. Azam Hatufi. Azam inaingiaje kwenye hii habari. Mbona walipomnunua Ngasa kutoka Yanga hamkusema inakufa. Hahaaa, Yanga vilaza, viongozi wao vilaza. Imewauma sana Ngasa kwenda Simba. Mbona Simba hawakupiga kelele Kaseja alivyoenda Yanga????

      Delete
  14. yanga hawa na sawa na%$$&&*(&(&())*_##$#%$&^*&)++_+)_(&^% zao

    ReplyDelete
  15. yanga ni yanga tu kaka

    ReplyDelete
  16. Je ikiwa Rage ni magumashi? Atawajibika? Hatujasahau za Asamoah, Nizar, Yondani, ....

    ReplyDelete
  17. Rage hakua kwenye swaumu, saa 4 asubuhi yeye na kahawa.... Msonjo kweli jamaa!

    ReplyDelete