Search This Blog

Thursday, August 2, 2012

EXCLUSIVE: MRISHO NGASSA AMALIZANA NA SIMBA - ALIPWA MILLIONI 30, GARI NA MSHAHARA WA MILLIONI 2 KWA MWEZI

Hatimaye leo mchana sakata la usajili wa mchezaji wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa akiichezea klabu ya Azam msimu uliopita, kabla ya jana kuuzwa kwenda klabu ya Simba limemalizika.


Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya klabu ya Simba, leo mchana walikutana na mchezaji mwenyewe ili kuweza kukubalina juu ya mahitaji yake binafsi, baada ya jana wekundu hao wa msimbazi kumalizana na Azam.


Kwenye mkataba wake mpya na Simba, Ngassa atapewa gari aina ya Verossa, ada ya usajili millioni 30 pamoja na kupewa mshahara wa millioni 2 kwa mwezi kama alivyokuwa akilipwa kwenye klabu aliyotoka ya Azam.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari mkataba ni mwaka mmoja.




16 comments:

  1. simba wanatapatapa baada ya kuvurunda kagame.tusubiri tuone kama ngassa ataweza kuwavusha kwenye mawimbi yanayowakabili hivi sasa.thamani ya ngassa na mchango wake uwanjani itabidi viende sambamba,vinginevyo muda mfupi tu ataanza kuzushiwa kwamba anahujumu timu kwani tunawafahamu mashabiki wa simba na viongozi wao walivyo vigeugeu.hayo yaliwakuta akina,Banka,Mukenya,Barasa,Lunyamila,Mmmachinga,Malima,Omari Hussein,Athumani China,Mtwa kiwelo,Tigana,Mulumba,Silvatus Ibrahim,Rajabu Mwinyi ambao walisajiliwa kwa mbwembwe na baadaye kutoswa kwa aibu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nini maana ya kutapatapa?kusajiri mchezaji haimaanishi kuwa timu inatapatapa simba wamegundua udhaifu kwenye kikosi ndio maana wanajipanga upya acheni kelele kama 'Inzi'Yanga haina pesa mwenye pesa Manji sasa mwenyewe kagoma kwakuwa dau lake dogo m20 sasa simba wameingia kwa dau kubwa sasa hivi tusubiri tuone simba wamelamba dume ama garasa?.

      Delete
  2. Hatumtaki Simba huyo! Ina maana mechi zote tukicheza na Yanga hatacheza huyo maana yeye ni Yanga damu!

    ReplyDelete
  3. Kamanda wa ukweli,kambi popote,kila la heri uendako"simba" ,lakini wakikuzingua tu,you must back home.

    ReplyDelete
  4. hahahah mbona hawajasema ni mkataba wa muda gani

    ReplyDelete
  5. Haya ni Maisha tuu,Mwachen Ngassa aende popote ilimradi Maslahi yawe Mazuri...!

    ReplyDelete
  6. kama kweliNgassa ana nia na mpira na mpira ni kazi yake basi aheshimu maamuzi aliyoyafanya kuchezea simba aachane na upenzi wakizamani tutaendelea kuwa wapinzani ila inapofikia swala la maendeleo basi afanye kweli aaachane na ushabiki namtakia maisha mema na yafuraha msimbazi acheze vizur simba haina tatizo na m2 baaaaaaaaaaaaaaaaaaac

    ReplyDelete
  7. Ngasa aina ya uchezaji wake utamcost,labda acheze kama forward no 10 pale simba ajifue kweli kweli.karibu simba ngasa!!!!

    ReplyDelete
  8. Ngasa aina ya uchezaji wake utamcost,labda acheze kama forward no 10 pale simba ajifue kweli kweli.karibu simba ngasa!!!!

    ReplyDelete
  9. Cha mgema huliwa na mlevi..!

    ReplyDelete
  10. Ngasa awache ushabiki wake wa Yanga. Proffessional footballers huweka ushabiki pembeni na kutumikia kwa moyo wote club zao. Nadhani amepata funzo baada ya Azam kumtupia virago.

    ReplyDelete
  11. wana yanga mnafurahisha sana, eti watamgeuzia kibao! hilo mnaliona kwa simba tu? mlishatimua timu nzima akabaki kimanda tu baada ya kupigwa nne kwa moja na mnyama, au mmesahau? na baada zile tano za juzi mtuhumiwa namba moja alikua nurdin bakari.ama hakika nyani haoni kundule! ngasa acheze mpira na aache unazi kwani ndio uliomuondoa azam. wapo watu kama kina beckham alishasema yeye ni mchezaji wa madrid lakini mshabiki wa man u. walcot mchezaji wa arsenal mshabiki wa liverpool, kwa hiyo kupenda timu nyengine na kucheza timu nyengine sio hatari ila kinachotakiwa ni uwajibikaji.

    ReplyDelete
  12. kwa upande wangu sioni kama atakuwa msaada msimbazi hicho kitakuwa kirusi tu kwenye mechi angeenda zke jangwani huyo hata kama mpira kwake ni kazi bado mapenzi yake ni yanga ko mezi za simba na yanga atakuwa hachezi sababu anajua msimu ujao atakuwa yanga tu.

    ReplyDelete
  13. Haina shida hata kama Ngasa ni mnazi wa Yanga. Mbona Kaseja ni mnazi wa Simba lakini alienda Yanga na alicheza bila shida then akarudi zake Simba. Hawa wachezaji ni professionals bwana na mpira ndo maisha na kazi yao.

    ReplyDelete
  14. kwa jinsi swala la Ngassa lilivyoanza hadi kumalizika kwa Ngassa kukubali kucheza simba,2013-2014 Ngassa atacheza yanga.

    ReplyDelete
  15. nadhani simba watakua wameshatambua nini maana ya maneno "MJINI SHULE" mnamchukua mchezaji kwa mkopo, mnawapa azam pesa mingi, mnamlipa mchezaji mshahara mkubwa, mnampa booonge la mkoko alafu mwisho wa siku haki zote za kummiliki mchezaji bado ziko azam..............dah poleni sana bandugu ila hata hivyo kawasaidia kushika nafasi ya tatu kwenye ligi, nafasi ambayo hamkustahili kushika kwa mwaka huu.

    ReplyDelete