Search This Blog

Saturday, May 11, 2013

HATIMAYE WAYNE ROONEY AZUNGUMZIA SUALA LA KUIFUTA MAN UNITED KWENYE UKURASA WAKE WA TWITTER

Siku chache baada ya vyomo vya habari ulimwenguni kuripoti juu ya suala la mchezaji Wayne Rooney kuifuta klabu yake ya Manchester United katika ukurasa wake rasmi wa Twitter, jana usiku mshambuliaji huyo wa England aliamua kujibu mapigo kwa kusema vyombo vya habari vimeandika upumbavu.

Katika taarifa aliyoitoa kupitia mtandao wake binafsi, Ronney alisema: "Kumekuwepo na upumbvu mwingi unaoandikwa kuhusu mimi kubadili biography yangu ya Twitter kwa kuifuta Manchester United kutoka kwenye wasifu huo.
"Sijawahi kuifuta manchester United kutoka kwenye wasifu huo kma magazeit yanavyoripoti kwa sababu sikuwahi kuandika tangu nijiunge na Twitter.
"Kilichotokea ni kwamba niliambiwa na wadhamini wangu Nike kuongeza '@nikeuk' katika wasifu huo kma ilivyo kwa wanamichezo wengine wanaowadhamini.
"Cha kufurahisha hakuna aliyeandika kuhusu hilo! Badiliko hilo lilitokea wiki tatu zilizopita na bado wanaongelea kuhusu kitu hicho kama ni kitu ambacho nimekifanya jana." alimaliza Rooney ambaye anatajwa kwamba ameomba kuondoka Manchester United mwishoni mwa msimu.

GOLI LA WIKI: THIERRY HENRY BADO ANATISHA - APIGA GOLI KALI LA TIK TAK

ABAJALO, FRIENDS RANGERS NA RED COAST WAPEWA NA DRFA KUWA KUFUZU KUCHEZA LIGI YA MABINGWA


CHAMA Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), kimezizawadia timu zake tatu za Red Coast, Abajalo na Friends Rangers zilizofanikiwa kucheza Ligi ya Mabingwa inayotarajiwa kuanza Mei 12 mwaka huu.

Makabidhiano hayo yalifanyika jana Alhmaisi (Mei 9) jioni kwenye ofisi za chama hicho, zilizopo makutano ya mtaa wa Mafia na Bonde, ambapo Red Coast waliokuwa washindi wa kwanza walikabidhiwa Sh 700, 000, huku Abajalo wao wakizawadiwa Sh 600, 000 na Friends Rangers wakijipatia Sh 500, 000.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Almas Kassongo (kushoto), akimkabidhi  Mwenyekiti wa Red Coast,  Jumanne Ayubu Sh 700, 000 ikiwa ni mchango wa chama hicho kusaidia timu hiyo katika Ligi ya Mabingwa inayotarajiwa kuanza Mei 12 mwaka huu

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa DRFA, Mohamed Mharizo, lengo la timu hizo kukabidhiwa fedha hizo ni kuzihamasisha ili ziweze kujiandaa na hatimaye kufuzu kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao.

Mwenyekiti wa DRFA, Almas Kassongo, ndiye alikabidhi fedha hizo kwa wawakilishi wa timu hizo huku akisema licha ya kiasi hicho cha fedha kuwa kidogo, lakini itakuwa chachu ya kupata mafanikio.

Viongozi waliohudhuria makabidhiano hayo kutoka DRFA  ni Mkurugenzi wa Ufundi, Joseph Kanakamfumo, Afisa Tawala, Said Pambalelo,  Mjumbe wa Kamati ya Ufundi na Mashindano, Daudi Kanuti na Mweka Hazina Ally Hassani.

Wawakilishi wa timu ni Mwenyekiti wa Red Coast, Jumanne Ayubu, Meneja wa Friends Rangers, Shaaban Marsila na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Abajalo, Abbasi Ngau.

Wakati huo huo, kamati ya ufundi ya DRFA kesho Jumamosi Harbours Club Kurasini, itakutana na Viongozi wa soka la Wanawake (TWFA), Viongozi wa soka la Vijana na Kamati ya Waamuzi ili kupanga utaratibu wa ligi na pia kuandaa kozi ya makocha.


Friday, May 10, 2013

YANGA KULAMBA MILLIONI 70 ZA UBINGWA WA VODACOM

Mdhamini  wa Ligi Kuu ya soka Tanzana Bara, Kampuni ya Vodacom imetangaza kutumia kiasi cha Shilingi Mil 200 kwa ajili ya kutoa zawadi ya fedha taslimu katika ligi inayomalizika mei 18 ambapo sasa Machampioni wa msimu huu watajinyakulia Shilingi Milioni 70.
Mbali ya bingwa, Vodacom pia itatoa fedha kwa timu inayomaliza nafasi ya pili, ya tatu na  ya nne katika msimamo wa ligi ambazo ni Sh. 35 Milioni,  huku Sh. 25 Milioni na Sh. 20 Milioni zote zikiwa na ongezeko ikilinganishwa na zawadi za fedha zilizotolewa katika msimu wa 2012 / 2013.
Zawadi hizo zimetangazwa kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kampuni hiyo kupitia Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim, ikiwa ni pamoja na kuainisha zawadi za washindi wa mchezaji mmoja mmoja pamoja na timu iliyoonyesha nidhamu kwa msimu huu.
"Mwaka huu tutatumia kiasi cha Shilingi Milioni 200 kwa ajili ya zawadi za fedha taslimu kwa  washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom huku bingwa akinyakua kitita cha Shilingi Milioni 70 ikilinganishwa na Sh 50 Milioni za msimu uliopita." Alisema Mwalim.
Mwalimu amesema lengo la kuongeza zawadi ni matokeo ya ushirikiano mzuri kati ya wadhamini wa ligi na wadau wengine wa soka na kwa pamoja kuwa na dhamira ya dhati katika kuendeleza soka nchini.
"Kila mmoja ni shahidi wa namna ambavyo soka letu limekuwa na namana ambavyo tunakabaliana hatua kwa hatua na changamoto zinazohusiana na ligi. Ni matumaini yetu kwamba tunapiga hatua na tuna matumaini ya kufikia kiwango cha juu zaidi cha maendeleo ya soka nchini yanaonekana." Aliongeza Mwalim "Kwetu sisi kama wadhamini tutajitahidi kadri inavyowezekana kuhakiksha tunaleta mabadiliko katika soka la Tanzania, tunaangalia mpira wa miguu nchini kwa upana zaidi kama mchezo unaopendwa, unaotuleta pamoja kama taifa na kuitangaza nchi yetu. Falsafa yetu hii imechangia kwa kiasi kikubwa kuwepo utulivu na ushirikiano mzuri miongoni mwa wadau na hivyo kutuletea mafanikio." Alisema Mwalim Zawadi nyingine zilizo tangazwa ni pamoja na zawadi ya mchezaji bora wa Mwaka golikipa bora, na mfugaji bora kila mmoja  anajinyakulia Shilingi Milioni 5.
Aidha, mwamumzi bora na kocha bora kila mmoja atajipatia Shilingi 7,500,000 kila huku timu iliyoongoza kwa nidhamu itapata zawadi ya fedha taslimu ya Shilingi Milioni 15.
"Tumekuwa na msimu mzuri uliojaa ushindani na hamasa, tunatarajia timu zitajipanga zaidi kwa ajili ya msimu ujao na hivyo kuendelea kuipa ubora ligi yetu."Alisema Mwalim huku akiwashukuru wadau wa mpira wa miguu nchini ikiwemo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi, Chama cha Waamuzi(FRAT), Vilabu, wachezaji na kipekee washabiki na kamati ya ligi kuu.
Amesema bila ya ushirikiano wa wadau hao na wengine ikiwemo Serikali, ligi kuu ya Vodacom isingeweza kufikia maendeleo iliyoyafikia katika msimu unaomalizika ambao kwa kiasi kikubwa ulitawaliwa na mpira wa uwanjani na si vinginevyo.

KALI YA LEO: "KAMA UNAMPENDA KOCHA WAKO USIMSAJILI CAPTAIN WA ARSENAL"


1: Viera kwenda Juventus mwaka wa pili Capelo kaondoka

2: Thierry Henry kwenda Barca msimu wa pili Frank Rijkaard kaondoka

3: William Gallas kwenda Tottenham Spurs Redknapp kaondoka

4: Cesc Fabregas kwenda Barcelona Pep Guadiola msimu wa pili akaondoka

5: Van Persie kaenda Manchester United - Sir Alex Ferguson huyoooo Je, nani atamchukua Vermerleen?

BAADA YA MTANDAO HUU KUTOA BARUA HALISI YA FIFA - TFF WATOA SIKU SABA SHAFFIH DAUDA KUTOA MAELEZO ALIPOITOA BARUA HIYO

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtaka Shaffih Dauda ambaye ni mmiliki wa tovuti ya www.shaffihdauda.com kutoa maelezo kuhusiana na barua ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) aliyoiweka kwenye mtandao wake huo.

FIFA ambayo ilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa TFF baada ya baadhi ya wagombea kuulalamikia, baadaye ilitoa maelekezo kuhusu mchakato huo kwa barua ambayo iliituma kwa Rais wa TFF, Leodegar Lenga.

Rais wa TFF katika mkutano wake na waandishi wa habari ambao Dauda alihudhuria alibainisha kuwa barua hiyo ya FIFA hawezi kupewa kila mtu, na kuruhusu waandishi kuisoma kwa Ofisa Habari wa TFF bila kuondoka nayo.

Wakati Rais Tenga anazungumza na waandishi wa habari (Mei 2 mwaka huu), nakala ya barua hiyo ya FIFA ilikuwa kwa viongozi wakuu wa TFF pekee, na viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Hivyo TFF imemtaka Dauda kutoa maelezo ya mahali alipoipata barua hiyo ndani ya siku saba.

MZEE AKILIMALI AIBUKA - AMUOMBA MWAMUZI WA MECHI DHIDI YA SIMBA ACHEZESHE KWA HAKI - AHAIDI KIPIGO MSIMBAZI

Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee wa klabu ya Yanga mzee Ibrahim Akilamli (katikati) akiongea na wandishi wa habari makao makuu ya klabu leo
Kuelekea mchezo dhidi ya Simba SC mei 18, Baraza wa wazee wa klabu ya Young Africans limeomba mwamuzi wa mchezo huo achezeshe kwa kufuata sheria 17 zote za mchezo na kwa kufanya hivyo mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom watoto wa Jangwani lazima wataibuka na ushindi katika mchezo huo.
Akiongea na wandishi wa habari kwa niaba ya baraza la wazee makao makuu ya klabu, katibu mkuu wa baraza la wazee Mzee Ibrahim Akilimali (Ibrahimovich) amesema wanaamini kikosi cha Yanga kitaibuka na ushindi katika mchezo huo ikiwa mwamuzi atachezesha kwa kufuata sheria zote 17 na kanuni za soka.
Akilimali amesema Yanga ni timu bora kwa sasa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kila mmoja anajua hilo, tuna wachezaji wazuri wenye kiwango cha hali ya juu ambao wamepikwa wakapikika wakaiva matunda ya mafunzo yao ndio yaliyotupatia ubingwa kabla ya ligi kumalizika.
Aidha aliongeza kuwa "Tunaahidi kwamba tutamfunga Simba SC siku ya mei 18 kutokana na umoja wetu, mshikamano na uongozi bora chini ya mwenyekiti Yusuf Manji na makamu wake Clement Sanga ambao mpaka sasa wameifnaya timu ya Yanga kuwa ya kuogopewa ukanda wote huuu".
Naye Mzee Hashim Mwika aliongeza kuwa waanahidi ushindi katika mchezo huo, idadi ya mabao haijalishi lakini kikubwa tunasema lazima tumfunge Simba mei 18 kikubwa tunaomba mwamuzi achezeshe kwa kufuata kanuni 17, na kama wakifanya hivyo basi Simba Sc wajiandae kupokea mvua ya mawe siku hiyo.
"Mwaka jana walitufunga kwa sababu hatukuwa pamoja, hatukua na maelewano lakini hivi sasa Yanga ni moja kuanzia viongozi, wachezaji, makocha na wanachama hivyo tunamini kwa kuwa pamoja na timu yetu bora lazima simba achezee kichapo "alisema mzee Mwika

ED WOODWARD MRITHI WA DAVID GILL NDANI YA MAN UNITED - ALIYE NYUMA YA MAFANIKIO YA KIBIASHARA YA MAN UNITED CHINI YA GLAZERS


Ni mtaalam wa zamani wa mambo ya uwekezaji kwenye benki na mtu muhimu nyuma ya uongozi wa familia ya Glazer, ndio yupo nyuma ya mafanikio ya kibiashara ya Manchester United.

Wakati Ed Woodward, 40, anaweza asiwe na jina kubwa, ameweza kujenga sifa wakati wa miaka yake nane ndani ya Old Trafford. 
Na kipindi kijacho cha kiangazi Woodward atachukua nafasi ya ofisa mkuu wa Manchester United David Gill mbaye atastaafu.
Akiwa amehusika kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha familia ya Glazer inainunua klabu hiyo mwaka 2005, Woodward amekuwa mtu muhimu ndani ya klabu hiyo tangu wakati huo.

Akiwa kama msaidizi wa Gill, muingereza huyo amekuwa na jukumu la kuhakikisha mbinu za biashara za United zinakuwa bora, baada ya kuondoka kwa Gill 30 June, ataingia katika majukumu ya kisoka zaidi, yakiwemo masuala ya usajili na uhamisho  pamoja majadiliano ya mishahara ya wachezaji.
Ed Woodward

Woodward anasifika sana kwa kuweza kufanikisha kupatikana kwa dili za mikataba mingi ambayo ilisababisha ongezeko kubwa la faida ndani ya miezi mitatu iliyopita - United wakitangaza faida ya £91 millioni kutoka mwezi January. 
 Kuanzia 2014, dili lingine kama la Chevrolet litaiwezesha United kulipwa na kampuni hiyo ya magari ya Marekani kiasi cha £51m kwa mwaka kutokana na udhamini wa jezi pekee yake.

Jukumu la kuiongoza United linaweza kuonekana kama kitu ambacho hakikutegemewa kwa mhitimu huyo wa fizikia wa Bristol University, japokuwa Woodward alianza kazi hiyo ya masuala ya uongozi huko PricewaterhouseCoopers akiwa kama mhasibu na mshauri wa masuala ya kodi mwaka 1993.
Mwaka 1999 alihamia JP Morgan, ambapo alifanya kazi kama ofisa mkuu wa masuala ya uwezekezaji katika masuala ya biashara za kimataifa.
Na mahala hapo ndipo alipokutana na Malcom Glazer n kumshauri ainunue Manchester United, na mwaka 2005 aliitwa kuajiriwa na United chini ya Glazers.
Mwanzoni alipewa jukumu la upangaji wa masuala ya fedha, kabla hajapewa jukumu la kuendesha biashara na masuala yote ya media ya Manchester United mwaka 2007 na baadae mwaka jana akawa mkurugenzi.

Woodward alikuwa hana uzoefu wowote wa kufanya kazi kwenye taasisi ya kimichezo kabla hajaja United, lakini alianza kuhudhuria vikao vya wana hisa wa premier league kwa pamoja na Gill mwaka 2012 katika jaribio la kumuongezea uelewa kuhusu siasa za soka.

Jukumu lake jipya litamfanya afanye kazi kwa karibu na Sir Alex Ferguson na mrithi wake David Moyes katika kuifanya brand ya Manchester United inafanikiwa kibiashara na kisoka kama ilivyokuwa chini ya David Gill.

Thursday, May 9, 2013

BAADA YA KUANDAMWA SANA MASHABIKI WA MAN U - MKE WA ROONEY ASEMA "MUULIZENI ROONEY MWENYEWE SIO MIMI"


Wayne Rooney kuungana na kocha wake wa kwanza wa soka la kulipwa??

Wakati Manchester United ikimtangaza David Moyes kuwa mrithi wa Sir Alex Ferguson, hatma ya mchezaji Wayne Rooney ndani ya Old Trafford imekuwa bado ya utata na kupelekea mashabiki wa klabu hiyo kuwa katika hali ya wasiwasi.

Taarifa mbalimbali zimekuwa zikisema mshambuliaji huyo amepeleka maombi ya kuondoka United kwa mara ya pili ndani ya miaka 3, akisema anahitaji changamoto mpya sehemu nyingine, huku vilabu vya Chelsea, PSG na Bayern Munich vikiwa tayari kutuma ofa kwa ajili ya kumsaini Muingereza huyo. 
 
Kutokana na sintofahamu hiyo kuhusu hatma ya Wayne Rooney ambaye sasa amebadilisha biography yake kwenye mtandao wa Twitter kutoka kuwa "mchezaji wa Manchester United mpaka kuwa NikeUK athlete" - mashabiki wa klabu wamekuwa wakimtumia tweets za vitisho na matusi kuhusu kutaka kuondoka Manchester United wakati huu timu ikiwa kwenye huzuni kubwa kwa kustaafu kwa Fergie.

Kama vile haitoshi baaada ya Wayne Rooney kukaa kimya bila kuwajibu chochote mashabiki ho kwenye Twitter wakamfuata mkewe Coleen Rooney na kuanza kumuuliza kama ni kweli wanataka kuondoka Manchester?
Mwanzoni Coleen alikaa kimya lakini baadae akashindwa kuvumilia na kuwatumia tweet moja mashabiki na kuwaambia kwamba "Mume wangu ana akaunti ya Twitter..... @WayneRooney muulizeni yeye sio mimi".

HATIMAYE DAVID MOYES ATHIBITISHWA RASMI KUMRITHI FERGUSON KWA MKATABA WA MIAKA 6


Hatimaye Manchester United imethibitisha DAVID MOYES ndio atakuwa kocha mpya wa kumrithi Sir Alex Ferguson kwa mkataba wa miaka 6.

Alex Ferguson jana alitangaza kustaafu kuifundisha timu hiyo aliyodumu nayo kwa takribani miaka 27 na akiwa anamtaja mrithi wake wake Fergie alisema: "Wakati tunajadili mtu wa kunirithi wote tulikubaliana kuhusu David Moyes.
"David ni mtu makini mwenye miiko ya kazi. Nimekuwa nikipenda ufanyaji wa kazi yake kwa muda mrefu na niliwahi kumshawishi mwaka 1998 ajiunge nami kuwa msaidizi wangu hapa. Akiwa kijana mdogo na akiwa ndio anaanza maisha yake ya ukocha na tangu wakati huo amekuwa akifanya kazi nzuri na klabu ya Everton.


"Hakuna swali kwamba ana kila ubora ambao tulikuwa tunautegemea kwa meneja mpya wa klabu hii.”- alisema Ferguson.

KALI YA LEO: MANCHESTER UNITED YAFUTA PICHA ILIYOONYESHA WANAMKARIBISHA DAVID MOYES KAMA KOCHA MPYA KWENYE FACEBOOK

Muda mfupi uliopita akaunti rasmi ya klabu ya Manchester United ilitoa pica iliyokuwa ikiwataarifu washabiki wa klabu hiyo juu ya uteuzi wa kocha wao mpya David Moyes, lakini ghafla baada ya dakika kadhaa picha ile ikaondolewa kwenye ukurasa huo wa Facebook wa United na kuzidi kuwaacha wapenzi wa soka duniani kwenye kujiuliza kwingi ni muda gani Mscotland huyo atathibitishwa na United kuwa mrithi rasmi wa Sir Alex Ferguson.

BREAKING NEWS: EVERTON WATHIBITISHA DAVID MOYES ATAONDOKA MWISHONI MWA MSIMU - MAN UNITED BADO KIMYA

Taarifa rasmi kutoka kwa klabu ya Everton zinasema kocha David Moyes ataondoka kwenye klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Taarifa rasmi iliyotolewa na Everton ilisema "Everton inathibitisha kwamba David Moyes ataondoka kwenye klabu hii mwishoni mwa msimu.
"Kocha alikutana na mwenyekiti Bill Kenwright mapema jana jioni na kumwambia matamanio yake ya kujiunga na Manchester United.
"Mwenyekiti, kwa niaba ya klabu, angependa kutoa shukrani za dhati kwa David kwa mchango wake mkubwa alioutoa tangu alipojiunga nasi March 2002. Amekuwa meneja wa wa aina yake."


Wakati huo huo Manchester United bado haijathibitisha kwamba Moyes ndio kocha atakayemrithi Sir Alex Ferguson.

MKUTANO MKUU WA UCHAGUZI TFF SEPTEMBA 29Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) unatarajiwa kufanyika Septemba 29 mwaka huu baada ya ule wa Dharura wa marekebisho ya Katiba ulipangwa kufanyika Julai 13 mwaka huu.

Tarehe hizo zimepangwa na kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji ya TFF kilichofanyika leo (Mei 9 mwaka huu) jijini Dar es Salaam chini ya uenyekiti wa Rais wake Leodegar Tenga ambacho kupokea rasmi maagizo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na kupanga utekelezaji wake.

“Kamati ya Utendaji ya TFF imepokea rasmi barua ya FIFA na kupanga utekelezaji wake. Tumepokea maagizo ya FIFA yanayotuelekeza cha kufanya, si TFF wala mtu mwingine yeyote anayeweza kuongeza jambo lingine.

“Maagizo ni undeni Kamati ya Maadili, Kamati ya Rufani ya Maadili, fanyeni marekebisho ya Katiba, anzeni tena uchaguzi, waliokuwepo na wengine wapya waruhusiwe. Tumejitahidi kuhakikisha uchaguzi uwe kabla ya Oktoba 30 mwaka huu kama FIFA walivyotuagiza,” amesema Rais Tenga wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kazi kubwa itakuwa ni kutayarisha kanuni hizo, kwani Kamati za Maadili lazima ziwe na kanuni zake na kuhakikisha kuwa hakuna mgongano kati ya Kanuni za Nidhamu na Kanuni za Maadili.

Pia Rais Tenga amesema kuna kazi ya kuangalia jinsi zitakavyoingia katika uchaguzi ambapo maana yake muda wa mchakato wa uchaguzi utakuwa zaidi ya siku 40 za sasa, hivyo mabadiliko hayo yatagusa vilevile Kanuni za Uchaguzi.

Kwa mujibu wa ratiba ya utekelezaji, rasmu ya mwanzo ya Kanuni hizo inatakiwa iwe imetoka kufikia Mei 30 mwaka huu ambapo itapelekwa FIFA kwa ajili ya kupata mawazo yao kabla ya kuendelea na hatua inayofuata.

Juni 15 mwaka huu Kamati ya Utendaji ya TFF itakutana kupokea mapendekezo hayo ambapo baada ya kuyapitisha itayapeleka tena FIFA. Taarifa (notice) ya Mkutano Mkuu wa Dharura ambayo kikatiba ni siku 30 itatolewa Juni 12 au 13 mwaka huu.

Baada ya Mkutano Mkuu wa Dharura wa marekebisho ya Katiba, Kamati ya Utendaji itakutana kati ya Julai 14 na 15 mwaka huu kuunda Kamati ya Maadili na Kamati ya Rufani ya Maadili ili kuruhusu mchakato wa uchaguzi uanze.

MIAKA 26 YA SIR ALEX FERGUSON NDANI YA MAN UTD: Part 1&2 :

JAY Z ATAKA KUMSAINI NEYMAR ROC NATION

image


Siku chache baada ya mwanamuziki nguli wa Hip Hop Jay Z kufungua kampuni ya uwakala wa wanamichezo, taarifa kutoka kwenye kambi ya rapa huyo ni kwamba anajipanga kumsaini mshambuliaji wa Brazil Neymar kwenye kampuni yake ya Roc Nation sports agency. Hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Yahoo:
“Roc Nation” iinataka kujikita katika michezo yote hasa soka, ikijaribu kuwafanya wachezaji kuwa mastaa wa kweli duniani kwa kuwa na mikataba minono na makampuni tofauti. Ndio maana Neymar kwa sasa amepewa kipaumbele kuwa mcheza soka wa kwanza kusainiwa kwenye kampuni ya Jay Z."
Neymar ataungana na Robinson Cano wa New York Yankees na Skylar Diggins wa WNBA katika listi ya wanamichezo waliopo katika kampuni ya mume wa Beyonce inayoanza kukua kwa kasi japo imeanzishwa mapema mwaka huu.
Katika ripoti nyingine inasemekana Jay Z pia amekuwa katika mawindo ya kuwasaini wabrazil wengine Lucas Moura na Leandro DamiĆ£o, pia Jon Jones, bingwa wa sasa ndondi uzito mwepesi wa UFC.
Lakini Jay Z atakumbana na upinzani mkali kutoka kwa kampuni ya masoko ya michezo inayomilikiwa na gwiji wa Brazil Ronaldo, ambayo ilimsaini Neymar kumwakilisha katika haki zake za taswira yake mwaka 2011.

MADUDU YA KAMATI YA MASHINDANO KWA LIGI ZA MIKOA, JINA LA TIMU BINGWA LATUMWA KABLA YA LIGI KUISHA


Ramadhani Nassib ( kushoto )- Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano

MAPEMA wiki hii Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilitoa ratiba ya mechi za mabingwa soka wa mikoa ya kisoka watakaopambana kupata timu tatu zitakazofuzu kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu huu.
Hakika hatua hii ya TFF kupitia Kamati ya Ligi imeweza kwenda na wakati kwa mujibu wa mipangilio yao, lakini nyuma ya jambo hili kuna mambo kadhaa yaliyotendeka na kulitia doa shirikisho la soka nchini.
Hadi ratiba inapangwa kuna baadhi ya mikoa ambayo haikuwa imepata mabingwa kutokana na sababu kadhaa ambazo kwa kiasi fulani ndizo zinazoendelea kuua mpira wa miguu nchini japokuwa zinaonekana ndogo ndogo.
Kwa mujibu wa TFF, uharaka wa kupangwa kwa ratiba hii umekuja baada ya Kamati ya Mashindano ya TFF chini ya Uenyekiti wa Blassy Kiondo ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, kubainia kwamba ucheleweshwaji wake unaweza kuathiri usajili wa timu zitakazopanda kucheza ligi daraja la kwanza.
Kutokana na uharaka huo, baadhi ya mikoa ilishindwa kuwasilisha majina ya mabingwa wake hadi Jumapili iliyopita ya Mei 5 nayo ni; Dodoma, Geita, iringa, Lindi, Mtwara, Manyara, Shinyanga, Simiyu, Tabora na Tanga.
Mikoa hiyo ilishindwa kupata mabingwa wake kwa wakati kutokana na mambo yafuatayo;


UCHELEWESHWAJI WA KANUNI ZA LIGI

Vyama vingi vya mikao ya soka vilichelewa kupata kanuni za ligi za mikoa hivyo kushindwa kuendesha michuano hiyo kwa wakati.

Muhusika hapa ni Kamati ya Mashindano ya TFF ambayo leo hii imelazimisha kwa mikoa kumaliza ligi zao mapema wakati yenyewe ilichelewesha kanuni za michuano hiyo. Sasa mikoa bila ya kuwa na kanuni, ingeendeshaje ligi? Hili ni tatizo.

Endapo mikoa ingepata kanuni za ligi mapema, nayo ingeanzisha ligi zao mapema na leo zingepata wawakilishi wanaofaa.

HALI YA KIJIOGRAFIA

Wilaya za Dar es Salaam za Ilala, Kinondoni na Temeke zote (hizo zina majina ya Dar es Salaam 1, Dar es Salaam 2 na Dar es Salaam 3) zinahesabika kama mikoa ya soka kama ilivyo, Tabora, Lindi, Mtwara na Simiyu; uendeshaji wa ligi za mikoa hiyo lazima uwe tofauti.

Kwa mfano timu ya mkoa wa Dar es Salaam 1, inaweza kucheza mechi yake leo kwenye Uwanja wa Mwalimu Nyerere pale Magomeni halafu keshokutwa ikacheza Uwanja wa Tandika Mabatini na isiathirike, kutokana na hali nzuri ya miundo mbinu ya kuiwezesha timu kufika uwanjani.

Ukichukulia mkoa kama Tabora, ambao una wilaya za Irambo, Igunga, Sikonge na Nzega; hali ni tofauti kwani kutoka wilaya moja hadi nyingine ni safari kubwa tena inayoweza kuchukua hata siku moja nzima.

Hii ina maana kwamba, Dar es Salaam 1 haiwezi kumaliza ligi sawa na Tabora. Hali ni hivyo hivyo hata kwa mikoa ya Lindi, Mtwara, Shinyanga na Simiyu.

Blassy Kiondo -Makamu Mwenyekiti


UKATA, UHABA WA VIWANJA
Ukitoa Dar es Salaam ambapo viwanja vingi vina uzio unaoweza kutumiwa kuingiza mashabiki kwa kulipa viingilio na kuvifanya vyama husika kuendesha ligi kikamilifu.

Katika baadhi ya mikoa ikiwemo Simiyu, viwanja vyenye hadhi ya kuchezewa ligi hiyo ni vichache ambavyo pia vingi havitoi fursa ya kuingiza kipato kutokana na ukweli kwamba hvina uzio.

Matokeo yake, mechi nyingi zinachezwa katika kiwanja kimoja na mzunguko wa ligi kuwa mkubwa ukichangiwa na umbali kutoka ilipo timu moja na nyingine.

Ukitoa mipira 20 kutoka TFF, vyama vingi vya soka vya mikoa vinajiendesha ‘kimaghumashi’ kutokana na kutokuwa na chanzo cha maana cha mapato.

Tunapozungumzia ukata tunaweza kutumia mfano wa timu ya Small Kids ya Rukwa iliyoshushwa daraja kutoka daraja la kwanza baada ya kushindwa kutokea uwanjani kutokana na ukata. Iwapo timu ya daraja la kwanza inakabiriwa na ukata, hali itakuwaje kwa timu ya daraja la nne?Matokeo yake;

MECHI ZACHEZWA ASUBUHI NA JIONIKuna taarifa kwamba, baadhi ya mikoa mabingwa wake walipangwa kutokana na maelekezo ya baadhi ya viongozi wa kamati ya mashindano na TFF kwa ujumla huku ligi zikiwa zinaendelea.

Baadhi ya mikoa ililazimika kucheza mechi asubuhi na jioni ili tu kupata bingwa, tena kwa njia zisizo halali lengo likiwa kuwafurahisha viongozi wa kamati waliotaka majina ya timu katika tarehe waliyotaka wao.

MAJINA YA MABINGWA YALITUMWA KABLA YA TIMU KUTWAA UBINGWA
Mbaya zaidi viongozi wa mikoa walilazimishwa kutuma jina la bingwa huku mechi zikiendelea hivyo kulazimika kupanga matokeo ili wasije kuumbuka mwisho wa siku.

Hakika viongozi wengi wa vyama vya soka vya mikoa walikuwa katika hali ngumu kwani wapo ambao usalama wao waliuweka shakani hasa kutokana na kulazimisha timu ambayo jina lake limetumwa Dar es Salaam kama bingwa, kuhakikisha inashinda.

Wapo baadhi ya viongozi ambao tayari wameshajiwekea doa katika utawala wao kwa kujikuta wakishiriki mchezo huu wa kutuma majina kabla ya bingwa kupatikana.

Mbaya zaidi hata waamuzi wa baadhi ya mechi walikuwa wanakwenda katika vituo vya mechi hizo za ligi za mikoa kwa maelekezo ya kamati ya mashindano bila ya kamati hiyo kuwasiliana na vyama vya mikoa.KITAKACHOENDELEA….Timu za mikoa ya Dar es Salaam zitaendelea kufanya vizuri na hata mikoa mingine inaona kilichopo ni kampeni ya wazi kwa TFF na Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kuhakikisha mkoa huo unapata tmu nyingi za ligi kuu, ili kujiingizia kipato kwa njia ya fedha za milangoni.

TFF inatambua fika kwamba timu za Dar es Salaam ndizo zinazoiingizia kiasi kikubwa cha fedha za milangoni katika mechi zake, lakini kuna jambo ambalo wanalifanya kimakosa lakini hawajui.

Mechi za timu ya taifa, Taifa Stars nazo zikichezwa bado DRFA inanufaika peke yake kama chama cha mkoa. Hii si halali. Taifa Stars ni timu ya taifa, hivyo pato linalokwenda DRFA lilipaswa kupelekwa kwa mgawanyo kwa mikoa yote.

Kwa mfumo wa sasa, DRFA itakuwa na uwezo wa kuingiza timu nyingi katika Ligi Daraja la Kwanza kila mara kwani hata kama zikikwama kama chama kinaweza kuokoa jahazi tofauti na mikoa mingine.

MSIMAMO WETU;
Kamati ya Mashindano inaweza kuchukua jambo hili kama changamoto na kulifanyia kazi. Nia yetu ni kuona soka la Tanzania linapiga hatua.

Wednesday, May 8, 2013

KIBONZO CHA LEO !
CHEMSHA BONGO! HUYU NI MCHEZAJI MPYA WA TIMU GANI PIA TAJA JINA LAKE!

MASAA MACHACHE BAADA YA FERGUSON KUSTAAFU HISA ZA MANCHESTER UNITED ZASHUKA KWA 4.5%

Manchester United imekuwa na siku mbaya sana leo hii, muda mchache wa baada ya Sir Alex Ferguson kutangaza kustaafu.
Habari za kustaafu kwa Ferguson zilitangazwa wakati soko la hisa la Marekani likiwa bado limefungwa. Wakati lilipofunguliwa hisa za klabu hiyo zikashuka thamani kwa asilimia  4.5%.
Klabu ilisema wakati ikielekea kwenye biashara ya kuuza hisa mwaka jana kwamba biashara hiyo itategemea na uwezo wa kuvutia na kuwapata wachezaji wakubwa.
"Mrithi yoyote wa meneja wa sasa anaweza kutokuwa na mafanikio kama aliyonayo Fergie," ilionya.
Mpaka kufikia mchana jijini New York, hisa zilishashuka kwa 1.5%.
Tetesi zimeshaanza kusambaa nani atakuwa mrithi wa Sir Alex, ambaye ameshinda makombe 38 wakati wa utawala wake wa miaka 26 ndani ya Old Trafford, huku meneja wa Everton David Moyes na kocha wa Real Madrid Jose Mourinho wote wanapewa nafasi.
Yoyote atakayepata kazi hiyo atajiunga na klabu yenye deni linalofikia £370m, na ikiwa inaongozwa na familia ya Glazer.
 Glazer alinunua Manchester United kwa £790m mwaka 2005 katika dili lililofanyika kwa utata mkubwa na kuifanya klabu kuwa na madeni.
Tangu Manchester United waingie kwenye biashara ya kuuza hisa, hisa hizo zimepanda thamani kwa asilimia 34.

TWEETS ZA CRISTIANO RONALDO, BECKHAM, PIQUE, RAMOS, ALVES, ESSIEN, OWEN, NISTELROOY NAO WAZUNGUMZIA KUSTAAFU KWA SIR ALEX FERGUSONLIVE MATCH CENTRE: SIMBA SC VS MGAMBO

Full time Simba 1 - 0 Mgambo

Dk 90 Zimeongezwa dakika tatu za nyongeza.

Dk 88 Simba inaendelea kumiliki mpira na hakuna dalili ya kusawazisha bao.

Dk 81 Simba imefanya mabadiliko ametoka Messi ameingia Salim Kinje. Simba 1-0 Mgambo.

Dk 75 Haruna Shamte wa Simba anamchezea rafu Fully Maganga wa Mgambo.

Dk 73 Kandulu wa Mgambo anachezewa faulo nje kidogo ya lango la Simba.

Dk 65 Messi wa Simba anaichambua ngome ya Mgambo lakini anashindwa kupiga shuti langoni. Simba 1-0 Mgambo

Dk 59 Mgambo wanafanya mabadiliko ametoka Chande Magoja ameingia Musa Ng'unda.

Dk 56 Issa Kandulu wa Mgambo anakosa bao la wazi akishindwa kuunga mpira kwa kichwa. Simba 1-0 Mgambo.

Dk 45 za kipindi cha zinaanza Simba inafanya mabadiliko anatoka Chollo ameingia Omar Salum.

Dk 45 HALF TIME! Simba 1-0 Mgambo.

Dk 45 zimeongezwa dakika mbili. Simba 1-0 Mgambo.

Dk 40 YELLOW CARD..! Chollo anaonyeshwa kadi ya njano kwa mchezo mbaya.

Dk 30 Simba inafanya mabadiliko anatoka William Lucian ameingia Rashid Mkoko.

Dk 25 YELLOW CARD....! William Lucian wa Simba anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya beki wa Mgambo!

Dk 20 Amri Kiemba anashindwa kuunganisha krosi safi ya Chollo akiwa peke yake na kipa wa Mgambo, Mmassa.

Dk 19 Peter Mwalyanzi wa Mgambo anapiga shuti kali langoni kwa Simba lakini kipa Juma Kaseja anaudaka mpira.

Dk 15 Kipa wa Mgambo, Godson Mmassa anagongana na Chollo mpira unasimama kwa muda ili kipa atibiwe.

Dk 14. Simba inapata kona lakini wanashindwa kuitumia vyema.

DK 8 Haruna Chanongo anaipatia Simba bao la kuongoza.

Mpira umeanza hapa uwanja wa Taifa.

Simba line up: Juma Kaseja, Nassor Masoud 'Chollo', Haruna Shamte, Miraji Adam, Hassan Khatib, Jonas Mkude, Edward Christopher, William Lucian, Amri Kiemba, Ramadhan Chanongo 'Messi' na Haruna Chanongo.

Mgambo JKT; Godson Mmassa, Salum Mlima, Ramadhan Kambwili, Bashiru Chanacha, Bakari Mtama, Salum Kipanga, Chande Magoja, Peter Mwalyanzi, Issa Kandulu, Fully Maganga na Nassor Gumbo.

TWEETS ZA WAZIRI MKUU WA UK, SEPP BLATTER, PETER SCHMEICHEL, SAHA, VIEIRA, KOMPANY, ARSENAL NA WEST HAM KUHUSU KUSTAAFU KWA SIR ALEX FERGUSONMJADALA: NANI KUWA MRITIHI WA FERGUSON MANCHESTER UNITED - MOURINHO, KLOPP, MOYES, ANCELOTTI AU HEYNCKES???

NANI KUMRITHI SIR ALEX FERGUSON MANCHESTER UNITED???

HAWA NDIO BAADHI YA MAKOCHA AMBAO MAJINA YAO YANATAJWA
Ole Gunnar Solkjear

David Moyes


Mourinho au Jurgen Klopp


Carlo Ancelotti

Jupp Heynckes