Search This Blog

Saturday, May 11, 2013

ABAJALO, FRIENDS RANGERS NA RED COAST WAPEWA NA DRFA KUWA KUFUZU KUCHEZA LIGI YA MABINGWA


CHAMA Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), kimezizawadia timu zake tatu za Red Coast, Abajalo na Friends Rangers zilizofanikiwa kucheza Ligi ya Mabingwa inayotarajiwa kuanza Mei 12 mwaka huu.

Makabidhiano hayo yalifanyika jana Alhmaisi (Mei 9) jioni kwenye ofisi za chama hicho, zilizopo makutano ya mtaa wa Mafia na Bonde, ambapo Red Coast waliokuwa washindi wa kwanza walikabidhiwa Sh 700, 000, huku Abajalo wao wakizawadiwa Sh 600, 000 na Friends Rangers wakijipatia Sh 500, 000.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Almas Kassongo (kushoto), akimkabidhi  Mwenyekiti wa Red Coast,  Jumanne Ayubu Sh 700, 000 ikiwa ni mchango wa chama hicho kusaidia timu hiyo katika Ligi ya Mabingwa inayotarajiwa kuanza Mei 12 mwaka huu

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa DRFA, Mohamed Mharizo, lengo la timu hizo kukabidhiwa fedha hizo ni kuzihamasisha ili ziweze kujiandaa na hatimaye kufuzu kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao.

Mwenyekiti wa DRFA, Almas Kassongo, ndiye alikabidhi fedha hizo kwa wawakilishi wa timu hizo huku akisema licha ya kiasi hicho cha fedha kuwa kidogo, lakini itakuwa chachu ya kupata mafanikio.

Viongozi waliohudhuria makabidhiano hayo kutoka DRFA  ni Mkurugenzi wa Ufundi, Joseph Kanakamfumo, Afisa Tawala, Said Pambalelo,  Mjumbe wa Kamati ya Ufundi na Mashindano, Daudi Kanuti na Mweka Hazina Ally Hassani.

Wawakilishi wa timu ni Mwenyekiti wa Red Coast, Jumanne Ayubu, Meneja wa Friends Rangers, Shaaban Marsila na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Abajalo, Abbasi Ngau.

Wakati huo huo, kamati ya ufundi ya DRFA kesho Jumamosi Harbours Club Kurasini, itakutana na Viongozi wa soka la Wanawake (TWFA), Viongozi wa soka la Vijana na Kamati ya Waamuzi ili kupanga utaratibu wa ligi na pia kuandaa kozi ya makocha.


No comments:

Post a Comment