Search This Blog

Saturday, June 22, 2013

TAKWIMU KOMBE LA MABARA: SPAIN, TORRES, NIGERIA NA TAHITI ZAWEKA REKODI MPYA

Hizi zifuatazo ni takwimu zilizojitokeza kwenye michezo ya juzi ya FIFA Confederation Cup baina ya Spain vs Tahiti na Uruguay vs Nigeria.

 - Diego Lugano alimaliza ukame wa goli ambao umedumu kwa miezi 18 - mara ya mwisho kufunga ilikuwa kwenye kombe la Ufaransa akiwa na PSG mwezi January 2012.
 
 - Diego Forlan pia nae alimaliza ukame wa mabao, juzi alifunga bao kwa upande wa Uruguay kwa mara ya kwanza tangu alipofunga dhidi ya Venezuela tarehe 2 June 2012.


 - Kipigo walichopata Nigeria kutoka kwa Uruguay kinamaanisha kwamba wamepoteza rekodi yao ya kutowahi kufungwa kwenye michuano hii. Denmark sasa ndio inabaki kuwa timu pekee kutowahi kufungwa kwenye historia ya michuano hii.  - Ushindi wa mabao 10-0 wa Spain dhidi ya Tahiti ulikuwa ndio mkubwa kuliko wowote uliowahi kutokea kwenye historia ya michuano ya mabara - ukivunja rekodi ya ushindi wa Brazil 6-0 Australia mwaka 1997 na Brazil 8-2 Saudi Arabia mwaka 1999.

 - Pia ushindi wa Spain wa 10-0 ulifikia rekodi ya uwepo wa mabao mengi katika mechi moja (Brazil 8-2 Saudi Arabia mwaka 1999)


- Fernando Torres aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat tricks mara mbili katika kombe la mabara - mara ya kwanza alifunga hat trick kwenye mchezo dhidi ya New Zealand mwaka 2009. 


 - Torres ni mchezaji wa tatu kufunga mabao manne katika mechi moja - wa kwanza Marzouk Al Otaibi na wapili ni Cuauhtemoc Blanco


 - Tahiti wamefikia rekodi ya kuruhusu mabao mengi kwenye kombe la mabara - wamefungwa jumla ya mabao 16 - rekodi hii iliwekwa na Saudi Arabia Saudi Arabia mwaka 1999

LIVERPOOL WAMSAJILI MSHAMBULIAJI LUIS ALBERTO - ANGALIA VIDEO INAYOONYESHA UJUZI WAKE WA SOKA

Liverpool wametangaza usajili wa mshambuliaji wa Sevilla Luis Alberto kwa ada ya uhamisho wa £6.8million.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 20 amesaini mkataba wa minne wa kuichezea Liverpool. 

Alberto alitumia msimu uliopita kucheza kwa mkopo kwenye timu ya Barcelona B, Alberto alifunga mabao 11 na kutengeneza mabao 17 katika mechi zote 38 alizoichezea Barca B.

ANGALIA MAUJUZI YAKE

RAFA BENITEZ ATAMBULISHWA RASMI NAPOLI LEO - ASEMA ASINGEPENDA CAVANI AONDOKE KWENDA CHELSEA, CITY WALA MADRID

Italian job: Napoli's President Aurelio De Laurentiis unviels new head coach Rafa Benitez
Raisi wa Napoli Aurelio De Laurentiis akimtambulisha kocha mpya wa timu hiyo Rafa Benitez

On the ball: Benitez shows off his skills at Napoli's training camp
Rafael Benitez ametambulishwa na kusema kwamba angependa kuendelea kubaki na mshambuliaji Edinson Cavani anyewaniwa na vilabu vya Chelsea, Man City na Real Madrid ambao Raisi wa klabu hiyo Aurelio amesema kwamba ndio klabu pekee iliyoonyesha utayari wa kulipa fedha inayotakiwa kumnunua Cavani

Friday, June 21, 2013

UWANJA WA OLD TRAFFORD ULIVYO SASA BAADA YA KUANZA KUFANYIWA MAREKEBISHO


Wiki kadhaa zilizozipita wakati nikiwa England nilitembelea jijini Manchester ambapo nilipata nafasi ya kwenda kutembelea uwanja wa Old Trafford wa Manchester United - Katika vitu kadhaa ambavyo nilipata kujua nikiwa OT, ni kwamba sehemu ya kuchezea ya uwanja huo ilikuwa inakaribia kufanyiwa marekebisho makubwa. Kwa mujibu wa msimamizi wa uwanja huo United walikuwa kwenye maandalizi ya kuondoa nyasi za zamani na kuweka mpya ambazo zingegharimu kiasi kinachozidi paundi 250,000.

Uwanja huo kwasa umeshaanza matengenezo na hivi ndivyo ulivyo sasa.

VIDEO YA SIKU: THIAGO ALCANTARA AKISAINI JEZI YA MANCHESTER UNITED

ZAHORO PAZI WA SIMBA ATEMWA - DAVID LUHENDE WA YANGA ACHUKUA NAFASI YAKE TAIFA STARS

Beki wa Yanga, David Luhende ameongezwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi ya Uganda (The Cranes) kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

Kocha Kim Poulsen amesema kutokana na uamuzi huo wa kumuongeza beki huyo wa kushoto amemuondoa mchezaji mmoja kwenye kikosi chake. Mchezaji huyo ni mshambuliaji Zahoro Pazi wa JKT Ruvu.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager sasa itaingia kambini kwenye hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam, Julai 3 mwaka huu badala ya Julai 4 mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa awali.

Mechi ya Uganda itachezwa Julai 13 mwaka huu, saa 9 kamili alasiri kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati ile ya marudiano itachezwa wiki mbili baadaye jijini Kampala, Uganda.

Wachezaji wanaotakiwa kambini ni Aggrey Morris (Azam), Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruni Chanongo (Simba), John Bocco (Azam), Juma Kaseja (Simba), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar) na Kelvin Yondani (Yanga).

Wengine ni Khamis Mcha (Azam), Mrisho Ngasa (Simba), Mudathiri Yahya (Azam), Mwadini Ali (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Nadir Haroub (Yanga), Salum Abubakar (Azam), Shomari Kapombe (Simba), Simon Msuva (Yanga) na Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar).

DIEGO FORLAN AVUNJA REKODI YA KUTOKUFUNGWA KWA NIGERIA KWENYE KOMBE LA MABARA


Nigeria 1-2 Uruguay Footyroom.com by Futbol2101

VIDEO + PHOTOS: ZIARA YA DAVID BECKHAM CHINA YALETA MAAFA - UMATI WAFURIKA KUTAKA KUMUONA - WATU 7 WAJERUHIWA


Ziara ya David Beckham huko China katika chuo Tongji University kilichopo Shngahi imeleta maafa baada wanafunzi watano na polisi wawili kujeruhiwa kutoka wingi wa watu waliokuwa wakitaka japo kumuona staa huyo wa soka duniani. 


Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United na Real Madrid alikuwa akutane na wanafunzi wa chuo hicho ambao ni wanasoka ikiwa ni moja ya kazi zake atakazofanya China katika dili lake la kuipromoti ligi kuu ya nchi hiyo.Askari akiwa amebebwa baada ya kujeruhiwa

Vurugu 


VIDEO: TORRES AWEKA REKODI YA MABAO KOMBE LA MABARA - DAVID VILLA NAE AFANYA KUFURU SPAIN WAKIICHINJA TAHITI 10 - 0Spain 10-0 Tahiti Highlights Confed Cup by coolchrisvilla

Thursday, June 20, 2013

USHAHIDI WA UWEPO WA GONZALO HIGUAIN NDANI YA JIJI LA LONDON KUJIUNGA NA ARSENAL

Higuain akisaini autograph ya shabiki wa Arsenal katika uwanja wa ndege wa Heathrow London. 
Gonzalo Higuain ameonekana akiwasili jijini London tayari kwa ajili ya vipimo vya afya ili kukamilisha uhamisho wa kujiunga na klabu ya Arsenal.

BRAZIL WATENGENEZA REKODI MBILI TOFAUTI JANA BAADA YA KUITWANGA MEXICO - DE ROSSI NAE AINGIA KWENYE VITABU VYA REKODI VYA KOMBE LA MABARA


Baada ya michezo ya jana ya kombe mabara leo tunakuletea takwimu na rekodi zilizotengenezwa jana.

 - Brazil ilitengeneza rekodi mbili jana kwenye kombe la mabara kwa ushindi wao dhidi ya Mexico. Ulikuwa ushindi wao wa tisa mfululizo na mechi yao ya 10 bila kufungwa. 

 - Mexico sasa wameruhusu nyavu zao kuguswa mara 32 kwenye kombe la mabara, mabao mengi kuliko timu yoyote.  


 
- Daniele De Rossi ndio muitaliano wa kwanza kufunga katika michuano miwili ya kombe la mabara - mara ya kwanza alifunga mwaka 2009 - dhidi ya USA.

 - Timu pekee ambayo iliwahi kutoka nyuma kwa 2-0 na kwenda kushinda katika kombe la mabara ilikuwa ni Brazil, ambao walishinda 3-2 katika fainali za mwaka 2009 - walikuwa nyuma kwa mabao mawili.

KWA TIMU HII YA VIJANA UMRI WA MIAKA 21 - SPAIN WATAENDELEA KUTAWALA SOKA LA KIMATAIFA KWA MIAKA MINGI IJAYO


Ingawa kuna mvuto mkubwa wa uimara na ubora wa kikosi cha sasa cha mabingwa wa dunia na ulaya, msingi mkuu wa mafanikio ya Spain katika miaka ya hivi karibuni yametokana na kuwa na wachezaji imara wanaounda nafasi ya kiungo ya timu hiyo Sergio Busquets, Xabi Alonso, Xavi na Andres Iniesta. 

Huku Busquets kwa utaratibu kabisa akiwa anaulinda ukuta wa nyuma, Alonso kwa pembeni akitoa msaada pamoja na kupiga pasi ndefu ndani ya dimba lote, Xavi akiwa daraja baina ya kiungo na safu ya ushambuliaji, na Iniesta akifanya maajabu yake kuelekea ndani ya eneo la penati, wachezaji hawa wanne wameshacheza jumla ya mechi 369 za kimataifa, wakijenga msingi mzuri na imara wa mafanikio ya Spain. 
Habari kwa Spain 'La Roja' (na habari nzuri kwa timu nyingine duniani) ni kwamba wachezaji watatu kwenye kundi hil- Alonso (miaka 31), Xavi (33) na Iniesta (29) - wanaweza wakawa wanaelekea ukingoni wa maisha yao ya soka la kiwango cha juu - labda kwenye Kombe la Dunia mwakani. Timu hii ya sasa inaelekea kwenye mwisho wake wa zama za mafanikio.
Ingawa, uwezo ulionyeshwa na kikosi cha timu ya taifa ya Spain chini ya umri wa miaka 21 - ambao wametwaa ubingwa wa Euro hivi karibuni kwa kuitandika Italia 4-2 - inaonekana wazi kwamba wabadala halisi wa kikosi cha sasa cha wakubwa cha Spain wapo tayari kuiteka dunia. Spain U21 nayo imeundwa juu ya msingi wa viungo watatu ambao wana sifa zenye kufanana na viungo wa kikosi cha wakubwa. 
 
Hwafanani kwa sifa zote na akina XAVI - hakuna anayeweza kuwa sawa nao - lakini wachezaji hawa watatu vijana wana nafasi ya kuja kuwa mastaa wakubwa kwa namna yao.
Wachezaji hawa ni Asier Illarramendi, Thiago Alcantara na Isco.

THE NEW XABI ALONSO: ASIER ILLARRAMENDI

Mtulivu, anayejua kuuchezea mpira - kiungo ambaye alianza maisha yake ya soka kwenye klabu ya Real Sociedad, alianza kujulikana wakati timu yake ikisaka nafasi ya kufuzu Champions League. 

Maneno haya yanaweza kutumika katika kumuelezea Xabi Alonso, ambaye soka lake liliibukia wakati Real Sociedad walipokuwa washindi wa pili wa La Liga kwenye msimu wa 2002-03 kabla ya kuondoka na kuelekea Liverpool, na Illarramendi, kiungo huyu ambaye alikuwa nyuma ya mafanikio ya Sociaedad katika kushika nafasi ya nne katika La Liga msimu uliopita.
Illarramendi ni mmoja ya mashujaa wasiotajwa sana kwenye kikosi cha U21 cha Spain kilichofanya balaa huko Israel, lakini wachambuzi wengi waliona namna alivyokuwa na umhimu ndani ya timu hiyo, na ndio maana sikushangazwa kuona klabu kama Arsenal wakihusishwa na kuiwinda saini ya mhispania.

Kama Alonso, kijana huyu ndio moyo mkuu wa timu, akicheza mbele watu wanne wa nyuma akilazimisha flow na kasi ya mchezo kwa pasi nzuri zenye maana.
Nidhamu yake ya kutokuwa mbinafsi - akijiweka nafasi ya kuulinda timu na kuwapa uhuru washambuliaji kucheza kwa uhuru, na moja ya mechi zake nyingi za kimataifa kwenye timu ya wakubwa ipo njiani. 

THE NEW XAVI: THIAGO ALCANTARA

Kiungo huyo wa Barcelona Thiago anatokea kwenye familia inayokula na kulala kupitia soka: baba yake Mazinho alikuwa mwanasoka wa kimataifa wa Brazil ambaye alikuwemo kwenye kikosi kilichoshinda World Cup 1994 wakati mdogo wake Rafael - maarufu kama Rafinha - ni zao lingine la academy ya Barcelona ambaye tayari ameshaanza kupata nafasi kwenye timu ya kwanza ya Barca.

Thiago alizaliwa nchini Italia wakati baba yake akiichezea Lecce, baadae akaenda kuishi Brazil na baadae akahamia Spain akiwa bado mtoto mdogo, akaanza kujifunza soka kwenye academy ya Barca kabla ya kuanza kupata nafasi katika kikosi cha kwanza akiwa na umri wa miaka 18. 
Akiwa nahodha aliiongoza Spain Under-21 wakati wa michuano ya Euro iliyoisha hivi karibuni, akitengeneza vichwa vya habari baada ya kuifungia timu yake hat trick kwenye fainali ya ushindi wa 4-2 dhidi ya Itali. s

Kiwango cha mechi hiyo kilileta kidogo mkanganyiko kwa sababu kufunga sio kawaida ya Thiago - amewahi kufunga mabao mawili katika mechi za timu za wakubwa - achana na hat trick. 

Lakini kijana huyu mwenye miaka 21 ni fundi haswa, akiwa na 'first touch' nzuri sana, anajua kuuchezea mpira, mpiga pasi nzuri sana kiasi kwamba watu wengi ndani ya Camp Nou wamekuwa wakimuona kama mrithi halisi wa wa Xavi. 

Ingawa, Thiago ameanza kuchoshwa na kutopata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Barca na kushindwa kwake kucheza japo asilimia 60 za mechi za msimu uliopita kunamaanisha kipengele chake cha bei ya kuuvunja mkataba wake na Barca kimeshuka kutoka 90m Euros mpaka 18m. 
Manchester United na Bayern Munichni moja kati kadhaa zinazotajwa kuwania saini yake wakati media za Catalan media zimeanza kampeni ya kumfanya ashawishike kubaki. 

Hata mtu ambaye ndio anayempigisha benchi kwenye kikosi cha kwanza, gwiji  Xavi, amemshauri kinda huyo kuendelea kubaki Camp Nou: "Thiago ni mchezaji wa aina yake. Sio tu mchezaji ambaye anasubiri aje kucheza huko mbele bali hata sasa anaweza kucheza.
"Ningependa kumshauri Thiago abaki na kuwa mvumilivu kwa sababu atapata mafanikio akiwa hapa Barca."

Kwa bahati ushauri wote huu wa Barcelona, utaangukia kwenye sikio la kiziwi, huku Thiago akitegemewa kufanya uamuzi wake wa kuondoka Barcelona hivi karibuni - Manchester United ndio anapotakiwa zaidi.

  ANDRES INIESTA MPYA: ISCO

Mshindi wa tuzo ya bora kinda barani ulaya mwaka 2012; mshindi wa Mchezaji bora chipukizi wa wa La Liga msimu wa 2011-12; mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mashindano ya Euro U21 mwaka 2013.... Francisco Roman Alarcon Suarez ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa mno.
Isco ni shabiki mkubwa wa klabu ya Barcelona na ana mbwa mdogo ambaye amempa jina la Messi, lakini wakati anakuwa amekuwa akimuhusudu sana Andres Iniesta - na hilo linaonekana. 

Kama ilivyo kwa shujaa wake, star huyu wa Malaga ni mmoja ya wachezaji wanaojua sana kukokota mpira ambaye ana balance nzuri na anaweza kupita katikati ya mabeki kwa kasi mno akitokea winga ya kushoto - pia anajua kupiga pasi za mwisho pamoja na kupiga mashuti.  
Jambo la kutisha zaidi, eneo moja ambalo ana ubora kumzidi Iniesta ni kwenye ufungaji. Alifunga mabao 17 kwa klabu yake na nchi yake msimu uliopita, yakiwemo matatu aliyoifungia Malaga na kusaidia kwenda robo fainali ya klabu bingwa ya ulaya.

Kipaji chake ni kikubwa kiasi kwamba Malaga wamemuakea kais cha 35m Euros kwa timu yoyote inayotaka kumnunua, huku  Manchester City na Real Madrid wakiwa wanaongoza mbio za kushinda saini yake. in
 
Mapema wiki hii, Isco alikiri kwamba ana ofa mbili kutoka kwenye klabu kubwa barani ulaya na hatma yake itaamuriwa mwishoni mwa mwezi huu, huku kukiwa na mategemeo ataamua kumfuata kocha wake wa zamani Manuel Pellegrini Etihad Stadium. Ikiwa hilo litatokea basi mashabiki wa City wakae tayari kwa burudani ya aina yake.

Wakati Illarramendi, Thiago na Isco wakiwa tayari kujiunga na David De Gea kwenda kwenye vilabu vikubwa na kupata nafasi - ni wazi kwamba supply ya vipaji ya Spain haionyeshi dalili zozote za kupungua.
Na haishii hapo tu: Fifa Under-20 World Cup inaanza hivi karibuni huko Uturuki na timu ya Spain inapewa nafasi kubwa ya kubeba ubingwa huo.
MANUEL PELLEGRINI KOCHA MPYA WA MAN CITY - MSOMI ALIYE TAYARI KUPANDIKIZA FALSAFA ZAKE ZA KISOMI NDANI YA MANCHESTER CITYMiaka 12 iliyopita, klabu ya Argentina San Lorenzo ilikuwa ikihitaji ushindi katika mchezo wa mwisho wa ligi ili kushinda ubingwa wa nchi hiyo. Manuel Pellegrini, kocha wa timu hiyo aliutumia usiku wa siku ya kuamkia mechi akisoma kitabu kwenye chumba kimojawapo kwenye kambi ya klabu hiyo. Umakini wake kwenye kusoma kitabu ulikatishwa, Fabricio Coloccini, wakati huo akiwa na miaka 19 akiichezea timu hiyo kwa mkopo, alikuwa akitoka chumbanikwake na kutembea kwenye korido, akionekana mwenye mawazo na hivyo kushindwa kulala, pia alikuwa na wasiwasi hata akashindwa kukaa chini akabaki anatembea tembea tu. 
Coloccini akiwa na wachezaji wa San Lorenzo wakishangilia

Pellegrini akuweza kuinuka kutoka alipokaa kwenda kumtuliza mlinzi huyo wa kiargentina bali alimwambia: "Fabricio, acha kuwa na wasiwasi kuhusu kitu chochote. Tumeshajitahidi na kufanya vizuri msimu wote, hivyo haitokuwa jambo kubwa sana kama tukichukua kombe au tusichukue."

"Unamaanisha nini?" Coloccini aliuliza. "Namaanisha kwamba - timu yetu ni bora kuliko zote, hilo ndio jambo muhimu, hivyo sijali kama tutashinda au kufungwa kesho."

Coloccini hakuweza kuamini maneno aliyokuwa akiyasikia kutoka kwa kocha wake. Alishangazwa sana na kauli za mwalimu wake kiasi akashindwa hata kujibu, alirudi chumbani kwake na kulala. Siku iliyofuatia wakaenda uwanjani na wakashinda mechi kisha kubeba ubingwa - na hapo ndipo Coloccini alipoona namna maneno ya Pellegrini yalivyomtuliza na kumfanya kucheza bila wasiwasi na matokeo kuisadia timu yake kubeba ubingwa. Kuna makinda wengi katika kikosi cha manchester City ambao watakuwa chini ya Pellegrini baada yaMuargentina huyo kutua Etihad - ambao watafaidi matunda ya falsafa ya saikolojia za kocha huyu.

Mapema mwezi huu, Pellegrini aliwahutubia makocha takribani  900 katika mkutano wa kimataifa wa makocha uliofanyika Malaga - Spain. Aliongolea mbinu anazotumia zilizomfanya aweze kuifikisha Malaga katika robo fainali ya Champions League msimu uliopita -- kwa bahati mbaya dakika mbili za nyongeza ziliinyima timu yake nafasi ya kwenda kucheza nusu fainali baada ya kufungwa walioinga fainali. 

KUHUSU FALSAFA ZAKE

"Kuna vitu vitatu muhimu ninavyohitaji kutoka wachezaji wangu; heshima, kujitolea/kujituma na kiwango kizuri," aliiambia Diario Sur. "Nina imani kwamba nitaweza kuingiza staili yangu ya soka katika nchi ya tano ambayo nitakuwa nafundisha soka ndani yake."

Pellegrini alianza maisha yake ya soka kwa kuichezea klabu ya Universidad de Chile, ambapo ilionekana wazi kwamba ujuzi wake wa kuwasoma na kuwaelewa watu utampeleka mbali. Alikuwa ndio mchezaji pekee aliyekuwa akisoma chuo kikuu -- alikuwa akichua engineering at Universidad Catolica -- na alikuwa mmoja kati ya wachezaji maarufu sana katika kikosi cha timu yao.

"Alikuwa mwanafunzi wa daraja la juu," anakumbuka mchezaji mwenzie Jorge Luis Ghiso, "lakini kila mtu alimheshimu na kumpenda." aliweza kuwafanya wakufunzi wake wamruhusu kuondoka darasani dakika 15 kabla ya muda ili asiwe anachelewa vipindi vya mazoezi.

Pellegrini ni mtu anayeenda na muda sana. Wakati alipotajwa kuwa kocha wa klabu ya Ecuador Liga Deportiva Universitaria de Quito, wachezaji wengi wenye makubwa walichelewa kufika mapema kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya timu moja ya mtaani - Pellegrini akawafungia mlango katika chumba cha kubadilishia nguo na kisha kukataa kuwaruhusu kucheza. Hawakuwahi kuchelewa tena sio mazoezini wala kwenye mechi. Ikiwa kocha aliyepita wa City Roberto Mancini aliiongoza timu hiyo kwa ubabe kwa wachezaji wake, Pellegrini anapendelea kuongoza kwa heshima kutoka anaowaongoza. 

"Inabidi uonyeshe kwamba una mamlaka ya kuwa kocha, lakini naweza kuwa dikteta na pia mwana demokrasia" alisema. "Dikteta kwa sababu wachezaji wanapaswa kukuheshimu, lakini kidemokrasia kwa sababu inabidi niwashawishi kama nahitaji wao wafanye hivyo."

City walisema sababu nyuma ya kufukuzwa kwa Mancini zilikuwa ni kushindwa kupata mafanikio waliojipangia (ukiachana na kufuzu kwa Champions League) na pia katika kauli hiyo hiyo walisema wanahitaji kuboresha kwa ujumla maendeleo ya klabu.

CEO wa zamani wa City Garry Cook aliiambia BBC kwamba maboresho yaliyohitajika hasa kutoka kwa mwalimu ni  - uelewa mkubwa za meneja kuifanya timu kuwa mali ya umma...kujieleza mbele ya vyombo vya habari...kuendesha biashara kwa kuwa na management nzuri katika masuala ya fedha katika kila wanachokifanya. Kwa ujumla ni kuelewa namna soka la kisasa linavyotaka kuendeshwa kibiashara, na sio timu kushinda tu mechi."

Uteuzi wa Pellegrini ni uamuzi mwingine muhimu uliofanywa na viongozi wapya wa kihispaniola - kama walivyoamua kuwekeza kwenye soka la Marekani kwa kuunda  New York City FC, klabu mpya MLS iliyoundwa kwa kushirikiana na New York Yankees, ni uamuzi unaoweza kuipeleka City hatua nyingine katika mahitaji yao ya kuteka soka la ulaya na kupata umaarufu mkubwa duniani kote.

Pellegrini, ambaye ni msomi mzuri sana hata kwenye mambo ya biashara na masoko ndio mtu sahihi wa kuitoa City ilipo kwenda hatua nyingine. Tabia yake ya kujisomea vitabu mbalimbali huwa inamsaidia katika maarifa ya ndani na nje ya uwanja. Kitabu ambacho alikuwa anasoma wakati Coloccini anahangaika na kushindwa kulala kule Argentina - kilikuwa kinahusu ni namna gani mtu au taasisi inaweza kuendelea kwenye masoko.

VIDEO: NEYMAR AENDELEZA BALAA KOMBE LA MABARA AKIIONGOZA BRAZIL KUITANDIKA MEXICO 2-0


BRA 2-0 MEX by Samusleep

TAZAMA MABAO BORA KABISA KUWAHI KUFUNGWA KWENYE HISTORIA YA KOMBE LA MABARA - RONALDINHO, KAKA, ETO'O WATISHA

ANGALIA NAMNA TEKNOLOJIA YA GOAL-LINE ILIVYOFUNGWA KWENYE VIWANJA VYA BRAZIL - MAREFA WAPEWA MAFUNZO JUU YA TEKNOLOJIA HIYO IILIYOANZA KUTUMIKA KWENYE KOMBE LA MABARA

KALI YA LEO: MCHEZAJI MPYA WA ASTON VILLA ALALA USINGIZI AKIWA ANAFANYIWA VIPIMO VYA AFYA


Mchezaji mpya wa Aston Villa aliyesajiliwa kwa ada ya £4million Jores Okore alikuwa hana wasiwasi hata kidogo juu ya uhamisho wake kwenda Aston Villa kiasi kwamba wakati akiwa anafanyiwa vipimo vya afya akapitiwa na usingizi kabisa.

Mchezaji huyo mwenye miaka 20 anayetokea FC Nordsjaelland aliweza baadae kuamka na kwenda kusaini mkataba wa miaka minne na Villa. 

Mdenmark huyo, ambaye ameshaichezea timu yake ya taifa mechi 7, alikaririwa akisema: “Nikiwa nafanyiwa vipimo vya MRI scan nilikuwa natakiwa nikae kimya - mawazoni nikawa nafikiria namna maisha ndani ya jiji la Birmingham yatakavyokuwa. Namna nitakavyokuwa naongea kiingereza, lakini hatimaye nikalala baada ya lisaa limoja na nusu kwenye vipimo na nikaamka saa moja baadae."

KLABU ANAYOCHEZEA SAMUEL ETO'O YAFUNGIWA KUCHEZA KWENYE UWANJA WAKE WA NYUMBANI


Klabu ya Russia Anzhi Makhachkala kwa mara nyingine tena itabidi wacheze mechi zao nyumbani za ulaya nje ya uwanja wao kwa msimu ujao kutokana masuala ya ulinzi, shirikisho la soka UEFA limesema leo Jumatano. 

 "Jopo la dharura la UEFA lilikutana na kuamua kwamba kutokana usalama mdogo huko Dagestan na Caucasus Kaskazini, hakuna mashindano yoyote ya UEFA yatakayoruhusiwa  kuchezwa katika eneo hilowakati wa msimu wa 2013/14 season," UEFA ilisema kupitia taarifa yake.
 "Kwa maana hiyo, Anzhi Makhachkala wameombwa kuchagua uwanja mwingine wa kuchezea mechi zao za nyumbani kwa msimu wa 2013/14 kwa ajili ya UEFA Europa League."
 Anzhi wametumia fedha nyingi kusajili wachezaji kama mcameroon Samuel Eto'o na kumuajiri kocha mdachi Guus Hiddink pia kumsajili mbrazili Willian kwa 35 million euros ($47 million).
 Walimaliza kwenye nafasi ya 3 kwenye ligi ya Russia msimu uliopita, wakikosa nafasi ya kwenda kwenye Champions League.
 Anzhi walicheza mechi zao za Europa League huko Moscow msimu uliopita kufuatia kifungo kama hichi kutokana kwa UEFA. 

Wednesday, June 19, 2013

DAVID DE GEA AMKARIBISHA THIAGO ALCANTARA MANCHESTER - HUU NDIO UJUMBE ALIOMUANDIKIAPichani chini ni Thiago Alcântara akiwa na mpira uliotumika kwenye fainali ya EURO U21 jana kati ya Hispania na Italy. Thiago aliondoka na mpira huo baada ya kufunga mabao matatu (hat-trick). 


Wachunguzi wa mambo wameuchunguza mpira huo na kugundua kuwa mpira unaonekana ukiwa na maandishi ya kispanish yanayosema ''NOS VEMOS EN MANCHESTER" maana yake kwa kiingereza ni "SEE YOU IN MANCHESTER". Inasemekana maneno hayo yaliandikwa na Golikipa David de Gea. Maandishi mengine yanayoonekana kwenye mpira huo ni ya wachezaji wengine wa timu ya taifa ya Hispania Under 21.

GENNARO GATTUSO ATEULIWA KUWA KOCHA MPYA WA KLABU YA PALERMO

Klabu ya Palermo inayoshiriki ligi ya daraja la kwanza Serie B nchini Italia imetangaza kwamba mchezaji wa zamani wa kimataifa wa nchi hiyo na klabu ya AC Milan Gennaro Gattuso ndio kocha mpya wa klabu hiyo.

Gattuso anakuwa kocha wa 11 kuliongoza benchi la ufundi la klabu hiyo katika kipindi cha miaka miwili na nusu.

Palermo wamemthibitisha leo Gennaro Gattuso kuwa kocha wao mpya na kumpa mkataba wa mwaka mmoja.

Rosaneri walishuka kutoka Serie A kwenye msimu wa 2012-13 kufuatia kumaliza kwenye nafasi ya 18th kwenye msimamo wa ligi na sasa wamemua kumpa mkataba Gattuso ambaye alikuwa mmoja wa wachezaji wa kikosi cha Azzurri waliobeba ubingwa dunia mwaka 2006.

Gattuso ana uzoefu mdogo kwenye masuala ya ukocha - hivi karibuni alipandishwa kutoka kuwa mchezaji mpaka kocha kwenye klabu ya Sion - akiwa kocha wa tano kuiongoza klabu hiyo ya Uswiss katika msimu wa 2012-13.

KOMBE LA MABARA: MEXICO NDIO TIMU YA MWISHO KUIFUNGA BRAZIL KWENYE KOMBE HILI - MIAKA 8 ILIYOPITA

Jared Borgetti executes an overhead-kick as Didi, Emerson and Ze Roberto watch on 
SIKU KAMA YA LEO 2005
Mara ya mwisho kwa Brazil kupoteza mchezo kwenye michuano ya kombe la mabara ilikuwa miaka nane iliyopita siku kama ya leo walipofungwa na Mexico. Jared Borgetti ndio alikuwa mfungaji wa bao pekee kwenye mchezo huo.

MIAKA 125 TANGU KUANZISHWA KWA MFUMO WA LIGI KWENYE SOKA KUHADHIMISHWA KWA MECHI 6 ZA KIHISTORIA

Mfumo wa soka kuchezwa kwa ligi utatimiza misimu 125 tangu kuanza kwake kwa kuchezwa kwenye mechi 6 mwanzoni mwa ufunguzi wa ligi. 

Mechi mbili zimechaguliwa kutoka kwenye kila daraja - mechi ambazo zitahusisha baadhi ya timu ambazo zilikuwa za kwanza kuunda mfumo wa ligi msimu wa 1888-89, michezo hiyo itaanza kuchezwa kwenye wikiendi ya August 3.

Timu hizo ni Derby County ambayo itaikaribisha Blackburn Rovers wakati mahasimu Burnley na Bolton Wanderers watakutana pale Turf Moor - moja ya viwanja vitatu vya kihistoria bado kinatumika kwenye ligi ya daraja la kwanza.

Deepdale, uwanja wa nyumbani wa Preston North End, ni uwanja mwingine wa kihistoria na wataikaribisha Wolverhampton Wanderers. Utakuwa mchezo wa 2,343 wa soka la ligi kuchezwa kwenye uwanja huo - ukiwa ndio uwanja uliochezewa mechi nyingi zaidi za ligi kuliko vingine. 
Mchezo mwingine wa pili wa League One utahusisha klabu kongwe kabisa ya proffessional, Notts County, kwenda kucheza kwenye uwanja mkongwe kabisa wa kisasa, wa Sheffield United uitwao Bramall Lane.

Kwenye League Two, Newport County - timu ambayo imepanda daraja hivi karibuni kupitia Conference play-offs - watacheza na Accrington Stanley. Na mechi iliyochezwa zaidi katika historia ya mfumo wa ligi kati ya Rochdale na Hartlepool United - itachezwa kwa mara 137.


KUELEKEA MECHI YA BRAZIL VS MEXICO USIKU WA LEO: HIZI NDIO TAKWIMU MUHIMU KUHUSU MCHEZO HUO - MEXICO HAIJASHINDA MECHI YOYOTE KOMBE LA MABARAA KWA MIAKA 8 SASA

Tuna masaa kadhaa ya kusubiri mechi ya pili wa kombe la mabara. Mchezo huo utakuwa dhidi ya Mexico na hizi ndio takwimu zinazohusisha mechi walizokutana magwiji hawa wa soka la bara la Amerika. 

 - Huu utakuwa mchezo wa nne kati ya Brazil-Mexico katika kombe la mabara, hivyo kuifanya mechi hii ndio ndio iliyochezwa mara nyingi zaidi katika historia ya michuano hii - mechi nyingine iliyochezwa mara nyingi ni Brazil-USA

 - Mchezo huu utakuwa wa 30 kwa Brazil katika michuano hii, ikiwa ndio timu iliyocheza mechi nyingi zaidi. 


 - Mexico wanawafuatia Brazil kwa kucheza mechi nyingi, mchezo wao wa leo utakuwa wa 21. 


 - Timu hizi mbili zimekutana mara 37, huku Seleção wakiongoza kwa ushindi wa mechi 21, wakati Mexico wameshinda mara 10.


 - Ushindi wa muhimu zaidi kwa Mexico katika hizo mara 10 ulikuwa mwaka 1999 katika kombe la mabara, ulikuwa mbele ya mashabiki wao 110,000 kwenye uwanja wa Azteca stadium


-  Mechi hii inazikutanisha timu pekee kwenye kombe la mabara 2013 ambazo zimeshashinda ubingwa wa kombe la mabara. 


 - Ushindi wa mwisho wa Mexico kwenye kombe la mabara ulikuwa siku kama ya leo - tarehe 19 June, 2005. Ni miaka 8 kamili. 

NIGERIA YABAKI KUWA TIMU PEKEE KUTOFUNGWA KWENYE KOMBE LA MABARA TANGU KUANZISHWA KWAKE BAADA YA KUIPA KIPIGO CHA 6-1 TAHITI

 Timu ya taifa ya Nigeria jana usiku iliitandika TAHITI mabao 6-1 kwenye michuano ya kombe la mabara inayoendelea huko nchini Brazil. Mchezo huo umetengeneza takwimu nyingi sana - zipo kama ifuatavyo:

- Nnamdi Oduamadi ndi mwanasoka wa kwanza wa kiafrika kufunga mabao 3 kwenye mechi moja katika michuano ya Mabara 

 - Jonathan Tehau ndio mchezaji wa kwanza wa Tahiti kwenye michuano ya FIFA 


 - Nigeria wanabaki kuwa ndio timu pekee ambayo haijawahi kupoteza mchezo katika historia michuano hii kwa timu ambazo zimewahi kushiriki. Wakishinda mara mbili na kutoa suluhu mara mbili. 


 - Jonathan Tehau ndio mchezaji wa kwanza kufunga kwa pande zote kwenye mechi ya michuano ya FIFA - na bado timuyake ikafungwa. Wachezaji sita wengine waliowahi kufanya hivyo wote timu zao walizokuwa wakizichezea zilishinda mechi zao. 


 - Matokeo ya Tahiti 1-6 Nigeria ni matokeo ya moja kati ya mechi 8 za kombe la mabara zilizozaa magoli mengi - 7.  Ni mechi moja tu ya Brazil 8-2 Saudi Arabia ndio imezidi idadi hiyo ya mabao kwa mechi. 

HUYU NDIO MCHEZAJI MWENYE UMRI MKUBWA ZAIDI KUWAHI KUCHEZA KWENYE KOMBE LA MABARA - ANATOKA AFRIKA

Siku kama ya leo 2005
Golikipa wa Tunisia Ali Boumnijel alicheza kwenye mechi dhidi ya Ujerumani kwenye mashindano ya kombe la mabara akiwa na miaka 39 na miezi miwili, na akaweka rekodi ya mchezaji mwenye umri mkubwa kabisa kushiriki kwenye michuano hiyo.

SIKU KAMA YA LEO MWAKA 2009: EGYPT YAWEKA REKODI YA KUWA TIMU YA KWANZA KUIFUNGA ITALIA

Siku kama ya leo mwaka 2009
Mechi kati ya Italy na Egypt ilikuwa ni ya 100 kuchezwa kwenye historia ya kombe la mabara. Egypt waliifunga Italia kwa 1-0, na hivyo kuwa timu ya kwanza kutoka Africa kuifunga Azzurri.

Tuesday, June 18, 2013

THIAGO ALCANTARA APIGA HAT TRICK NA KUIPA SPAIN UBINGWA WA EURO (U21) KWA USHINDI WA MABAO 4-2 DHIDI YA ITALIA


Spain vs Italy 4:2 GOALS HIGHLIGHTS (U21 EURO... by footballdaily1

SAKATA LA USAJILI WA CRISTIANO RONALDO - REAL MADRID WAPO TAYARI KUMLIPA FEDHA ANAYOTAKA - TATIZO LABAKI KWENYE HAKI ZA TASWIRA YAKE.

Cristiano Ronaldo anakaribia kukubaliana na Real Madrid juu ya mkataba mpya wa kuendelea kubaki Santiago Bernabeu - kwa klabu hiyo ya jiji la Madrid kumfanya Ronaldo kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi kuliko wote kwenye ulimwengu wa soka duniani.

Madrid wapo kwenye mazungumzo ya mwisho mwisho na wawakilishi wa Ronaldo kwa dili lenye thamani ya €155 million kwa mkataba wa miaka mitano - mkataba ambalo utamfanya Ronaldo aweke kibindoni €15m kwa mwaka baada ya kukatwa kodi - dili ambalo linatajwa kuwa la thamani zaidi katika historia ya soka duniani.

Ronaldo, ambaye amefunga mabao 201 katika 199 ndani ya misimu minne aliyokaa Santiago Bernabeu, aliwapa tumbo joto viongozi wa Madrid baada ya alhamisi ya wiki iliyopita kuandika kwenye mtandao wa Twitter kwamba: "All the news about my renewal with Real Madrid are false."


Ronaldo ambaye miezi kadhaa huko nyuma aliwahi kukaririwa akisema hana furaha ndani ya Madrid katika kile alichosema kwamba ni sababu zinazomfanya asiwe na furaha ndani ya klabu hiyo viongozi wa Madrid wanazifahamu- sababu ambazo inasemekana zimetokana na sapoti ndogo anayopata kutoka kwa klabu yake hasa katika mbio za kugombea Ballon d'Or, pia kitu kingine ni ugomvi wake na mchezaji mwenzie  Marcelo.

Madrid walimsajili Ronaldo kutoka Manchester United kwa rekodi ya uhamisho ya €94 million wakati wa kiangazi mnamo mwaka 2009, mara tu baada ya kurudi kwenye uongozi kwa Raisi  Florentino Perez. Kwa sasa Ronaldo analipwa kiasi cha €10m baada ya kodi.

Wakati Ronaldo aalipowasili Spain, kulikuwa na kitu kinachoitwa 'Beckham Law', ambayo iliwaruhusu wageni ambao wameishi nchini humo kwa miaka chini ya 10 na ambao wanavuna zaidi ya kiasi cha €120,000  kwa mwaka kulipa kodi ya chini kiasi cha asilimia 23 na sio ile ya kawaida ya asilimia 45, bado ilikuwepo. David Beckham alikuwa mmoja wa watu wa kwanza  kupata faida ya sheria hiyo baada ya kuhamia Madrid akitokea kupata  Manchester United mnamo mwaka 2003.

Japokuwa baadae serikali ya Spain ikaifuta sheria hiyo na sasa mkataba mpya wa Ronaldo utakuwa unakatwa kiasi cha 52% kama kodi. Hivyo, Madrid itabidi watoe package ya €31m ili baada ya makato Ronaldo abaki na kiasi cha €15m ambacho anakitaka.

Madrid, wanatambua umuhimu wa kuendelea kuwa na Ronaldo. Klabu hiyo hivi karibuni imemkosa Neymar, wakati wakionekana kukata tamaa ya uwapata wachezaji wa Dortmund Ilkay Gundogan na Robert Lewandowski. Wachezaji wengine ambao walikuwa kwenye hesabu zao kama vile Sergio Aguero na Radamel Falcao, hawatoenda Madrid pia, wakati Gareth Bale ni gharama zaidi kumpata na hataki kuomba uhamisho kutoka Tottenham na huku Edinson Cavani anaonekana kuwa hana thamani ya fedha ambayo Napoli wanaitaka kutokana mauzo ya Cavani. Hivyo kubaki na Ronaldo ni jambo muhimu.

Raisi wa klabu hiyo alikaririwa hivi karibuni akisema kwamba atafanya chochote kuhakikisha Mreno huyo anabakia ndani ya jiji la Madrid hata kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi kwenye ulimwengu wa soka.

Madrid sasa wapo tayari kumpa Ronaldo anachokitaka na kumfanya apate fedha nyingi kuliko Lionel Messi, ambaye analipwa kiasi cha €13m kwa mwaka kabla ya bonasi ndani ya Barcelona, na Falcao, ambaye anapata kiasi cha €14m kwa mwaka ndani ya Monaco. Samuel Eto'o analipwa kiasi cha €20m kwa mwaka na Anzhi Makhachkala, ingawa dili hilo la mcameroon huyo lina muda wa miaka mitatu tu na kwa ujumla dili la Ronaldo litampita Eto'o.

Tatizo kubwa na kizingiti kikubwa katika makubaliano ya mkataba mpya wa Ronaldo na Madrid ni suala la haki za taswira yake. Cristiano kwa sasa anamiliki asilimia 60 wakati klabu inachukua 40 zinazobakia. Ronaldo anahitaji maboresho makubwa kwenye suala hili - inaaminika anataka haki zake zote za taswira yake kwa maana ya asilimia 100 - kitu ambacho Madrid hawakubaliani nacho. Hapo ndipo makubaliano juu ya mkataba mpya yanapochelewa.

TIMU YA THAILAND YASAKA WACHEZAJI TANZANIA - GOSAGE MTUMWA APEWA ITC KWENDA KUCHEZA YEMENI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa mchezaji Mtanzania Gossage Mtumwa ili aweze kucheza mpira nchini Yemen.

Mtumwa ambaye anatoka katika kituo cha kukuza na kuendeleza vipaji cha Rollingstone cha Arusha aliombewa hati hiyo na Chama cha Mpira wa Miguu cha Yemen (YFA) kwa ajili ya kucheza nchini humo.

TFF inamtakia kila la kheri Mtumwa katika safari yake ya Yemen, na ni matarajio yetu kuwa atakuwa balozi mzuri wa Tanzania nchini humo ili wachezaji wengine wa Tanzania nao wapate fursa ya kucheza mpira wa miguu nchini Yemen.

KLABU THAILAND YASAKA WACHEZAJI TANZANIA
Klabu ya Thai Port Football ya Thailand inatafuta wachezaji nchini Tanzania kwa ajili ya kucheza mpira wa miguu nchini humo na katika nchi nyingine barani Ulaya.

Kupitia kwa wakala wake, klabu hiyo imetuma taarifa kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikitaka wachezaji wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 28 kwa ajili ya kuwafanyia majaribio ambapo watakaofuzu watacheza nchini humo na katika klabu nyingine za Ulaya ambazo wana ushirikiano nazo.

Wachezaji wenye nia ya kufanya majaribio wanatakiwa kutuma taarifa za wasifu wao (CV) kwa klabu hiyo kwa njia ya emaili, wawe na pasi ya kusafiria pamoja na pasi ya mchezaji (player passport).

Wakala atapitia vitu hivyo, na kwa wachezaji atakaowahitaji atawatumia tiketi za ndege na viza kwa ajili ya kwenda kufanya majaribio nchini humo, na watakaofanikiwa kabla ya kusaini nao mikataba watawasiliana na klabu zao nchini (kwa wale wenye klabu).

NSAJIGWA, BEN MWALALA NA WACHEZAJI WENGINE KUMALIZA KOZI YA UKOCHA JUMANNE

Nahodha wa zamani wa Yanga Shedrack Nsajigwa akiwa na Baadhi ya makocha wakiwemo wachezaji wa zamani wakifuatilia mafunzo ya ukocha ngazi ya pili.

Kocha mkuu wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage akitoa somo kwa makocha wanashiriki kozi ya ukocha ngazi ya pili ndani ya darasa kwenye Ukumbi wa Harbours Club, Kurasini.

Kocha mkuu wa Twiga Stars akitoa somo kwa makocha wa kozi ya ngazi ya pili kwa vitendo
KOZI ya makocha wa ngazi ya pili (Intermediate) inayosimamiwa na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), inatarajiwa kufungwa Jumanne ijayo baada ya kudumu kwa wiki nne.
Kozi hiyo ilianza Juni 3 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Harbours Club, uliopo Kurasini chini ya Mkufunzi Rogasin Kaijage, ambaye ni Kocha wa timu ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ ambapo makocha mbalimbali pamoja na wachezaji wa zamani wamejitokeza kushiriki.
Ofisa Habari wa DRFA, Mohamed Mharizo alisema kozi hiyo imekuwa na mafanikio na wanatarajia makocha walioshiriki katika kozi hiyo watakuwa na mchango mkubwa katika kuendeleza mpira wa miguu katika mkoa wa Dar es Salaan na Taifa kwa ujumla.
“Hadi sasa tunashukuru kuona tunafanikisha kozi hii ambayo wengi wameitikia wito, mwisho wa kozi hii ndio mwanzo wa kozi nyingine.
“Lakini haya ya kozi ya makocha ni moja ya majukumu ya Kamati ya Ufundi ya DRFA yaliyoainishwa katika Katiba, hivyo hili ni moja ya shabaha yetu na mengine mengi mazuri yanafuata,” alisema Mharizo.
 Kozi hiyo ni ya kwanza kuendeshwa na DRFA tangu kuingia madarakani kwa uongozi mpya wa chama hicho Desemba 12, chini ya Mwenyekiti wake Almas Kassongo.

SUNDERLAND NA SYMBION KUJENGA ACADEMY MBILI ZA SOKA DAR ES SALAAM


CEO wa klabu ya Sunderland, Margaret Byrne, ameusifia ushirikiano na Tanzania kwamba ni hatua kubwa kuendelea mbele.
The Black Cats wameingia mkataba na kampuni ya nishati ya Power kujenga cademy kubwa ya soka nchini, ndani ya jiji la Dar es Salaam.
Raisi Jakaya Kikwete alitembelea makao makuu ya klabu ya Sunderland huko Wearside siku ya jumapili katika kukata rasmi utepe wa kuanza kwa project hiyo.
“Ni siku muhimu kwa klabu na klabu na mji wetu,” Byrne alisema.
“Kutembelewa na mheshimiwa Raisi hapa wakati akiwa UK kuhudhuria mkutano wa viongozi wa G8 ni jambo kubwa kutoka kwake na mawaziri wake. Ni zuri sana kwetu.
Hatua za mwanzo kwa ajili ya Academy zilizinduliwa siku hiyo ya jumapili, kwenye tukio ambalo lilihudhuriwa na mwenyekiti wa Sunderland Ellis Short.
Project hiyo itaisaidia Tanzania katika kukuza soka lake pia kuwapa nafasi kubwa vijana wadogo kabisa kuweza kuendeleza vipaji vyao kwenye academy hiyo. 
Sunderland watajenga majengo pamoja na kutoa makocha wa kufundisha.
“Hatua ya kwanza itatuhusisha sisi kufanya kazi na Symbion Power kujenga academy ya kijamii, tukiruhusu watoto wengi kuja na kufurahia kucheza mchezo wa soka,” Byrne alielezea.
“Hatua ya pili itatuhusisha sisi kufanya kazi na Symbion labda ikiwezekana na taasisi nyingine kujenga kituo cha kisasa cha kufundishia soka.
“Tutoa usaidizi mkubwa wa vifaa vingi tunavyotumia kwenye academy yetu ya Academy of Light na pia na maarifa tuliyoyapata na tunayoyapata kutoka kwenye project ya EPPP (Elite Player Performance Plan).


NIGERIA YAANZA NA BALAA KOMBE LA MABARA - WAIKANDAMIZA 6-1 TAHITI


Nigeria vs TahitI 6:1 GOALS HIGHLIGHTS by footballdaily1

Monday, June 17, 2013

MAGOLI YA SIKU: JUMA KASEJA NA CASILLAS NA MIKWAJU YA FAULO YA YAYA TOURE NA LUIS SUAREZ

IKER CASILLAS VS LUIS SUAREZ JUMA KASEJA VS YAYA TOURE

TAIFA STARS NA IVORY COAST WAINGIZA MILLIONI 500

Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, Kundi C, Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Ivory Coast (The Elephants) iliyochezwa jana (Juni 16 mwaka huu) imeingiza sh. 502,131,000 kutokana na watazamaji 57,203.

Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.

Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 76,596,254.24 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 7,809,104.

Asilimia 15 ya uwanja sh. 62,658,846.26, asilimia 20 ya gharama za mechi sh. 83,545,128.35 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 20,886,282.09.

Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 250,635,385.06 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,531,769.25 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.

Mechi iliyopita ya Stars dhidi ya Morocco (Lions of the Atlas) kwenye uwanja huo iliingiza sh. 226,546,000.

BAADA YA KUIKOSA SAFARI YA BRAZIL 2014 - TAIFA STARS SASA KUINGIA KAMBINI JULAI 4 - SAMATTA NA ULIMWENGU WATEMWA

Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameiita tena kambini timu hiyo Julai 4 mwaka huu kujiandaa kwa mechi ya kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inavunja kambi leo (Juni 17 mwaka huu) baada ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, kundi C Kanda ya Africa dhidi ya Ivory Coast iliyochezwa jana (Juni 16 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kim amesema wachezaji watakaoitwa kambin ni wote walioko kwenye timu hivi sasa isipokuwa Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaocheza mpira nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) katika klabu ya TP Mazembe Englebert.

Wachezaji hao ni Juma Kaseja, Aishi Manula, Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi.

Mechi hiyo namba 37 dhidi ya Uganda (The Cranes) itachezwa jijini Dar es Salaa kati ya Julai 12 na 14 mwaka huu wakati ile ya marudiano itafanyika wiki mbili baadaye katika Uwanja wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Jiji la Kampala.

RAISI JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA KLABU YA SUNDERLAND YA UINGEREZA