Search This Blog

Friday, June 21, 2013

ZAHORO PAZI WA SIMBA ATEMWA - DAVID LUHENDE WA YANGA ACHUKUA NAFASI YAKE TAIFA STARS

Beki wa Yanga, David Luhende ameongezwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi ya Uganda (The Cranes) kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

Kocha Kim Poulsen amesema kutokana na uamuzi huo wa kumuongeza beki huyo wa kushoto amemuondoa mchezaji mmoja kwenye kikosi chake. Mchezaji huyo ni mshambuliaji Zahoro Pazi wa JKT Ruvu.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager sasa itaingia kambini kwenye hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam, Julai 3 mwaka huu badala ya Julai 4 mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa awali.

Mechi ya Uganda itachezwa Julai 13 mwaka huu, saa 9 kamili alasiri kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati ile ya marudiano itachezwa wiki mbili baadaye jijini Kampala, Uganda.

Wachezaji wanaotakiwa kambini ni Aggrey Morris (Azam), Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruni Chanongo (Simba), John Bocco (Azam), Juma Kaseja (Simba), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar) na Kelvin Yondani (Yanga).

Wengine ni Khamis Mcha (Azam), Mrisho Ngasa (Simba), Mudathiri Yahya (Azam), Mwadini Ali (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Nadir Haroub (Yanga), Salum Abubakar (Azam), Shomari Kapombe (Simba), Simon Msuva (Yanga) na Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar).

2 comments:

  1. Hatimaye sasa Kim Poulsen ameacha ubishi na kuanza kusikiliza ushauri na kuufanyia kazi..Angalia alipoteua Young Taifa Stars alimuacha Luhende na badala yake katika nafasi hiyo aliwaita Miraji Adam,Emily Mgeta,Waziri Salum na Samih Haji ambaye kwa muda mrefu hajacheza Azam.Vicent Barnabas hajawahi kucheza nafasi ya beki kwa muda wote aliocheza ligi kuu kuanzia 2005,na si aina ya wachezaji wanaoweza kubadilishwa kutoka ushambuliaji kwenda kwenye ulinzi kama ilivyokuwa akina Nsajigwa,Twaha Hamidu n.k.sidhani kama anao ubora wa kuwazidi mabeki wa asili wa pembeni kama Cholo na Juma Abdul.Pamoja na kasi yake lakini Kwa sasa umri wake ni mkubwa,kimo chake ni kifupi na ana tatizo la kuangalia zaidi chini wakati akiwa na mpira.

    ReplyDelete
  2. Mrisho ngasa ni yanga sio simba.

    ReplyDelete