Search This Blog

Saturday, December 21, 2013

SIMBA NDIYE MTANI JEMBE,YAIONESHA SOKA YANGA, YAICHAPA 3-1

 Wachezaji wa Simba na Yanga wakisalimiana.
 Kikosi cha Simba.
 Kikosi cha Yanga.
 Benchi la ufundi la timu ya Simba.
Benchi la Ufundi la Yanga.
 Henry Joseph wa Simba (kushoto) akichuana na beki wa Yanga, David Luhende.
 Henry Joseph wa Simba (kushoto) akichuana na beki wa Yanga, David Luhende.
 Mashabiki wa Simba wakishangilia bao la kwanza la timu yao.
 Raha ya ushindi.
 Furaha kwa Simba.

 Hamisi Kiiza akitafuta mbinu za kumtoka, Ramadhani singano.
 Ivo Mapunda akiruka juu kuokoa moja ya hatari langoni mwake.
 Mashabiki wa Yanga wakiwa hawaamini kilichotokea uwanjani baada ya kuchapwa 3-1 na watani zao wa jadi Simba.
 Juma Kaseja akibembelezwa na Mbuyu Twite baada ya kusababisha 
 Mmoja wa mashabiki wa Yanga akitolewa nje baada ya kuzimia uwanjani.
 Emmanuel Okwi akimtoka beki wa Simba.
 Wachezaji wa akiba wa Simba  wakishangilia baada ya filimbi ya mwisho. 
 Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic akishangilia baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa 3-1.
 Wachezaji wa Simba wakimnyanyua juu kocha wao, Zdravko Logarusic mara baada ya kumalizika kwa mchezo maalumu wa Nani Mtani Jembe uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba ilishinda 3-1.




 Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe akimkabidhi kombe nahodha wa Simba Haruna Shamte.


SIMBA NDIO MTANI JEMBE - TAMBWE APIGA 2 MNYAMA AKIWAUA YANGA 3-1


IVO MAPUNDA NA MASOTI WAANZA DHIDI YA YANGA

Simba line up: Ivo Mapunda, Haruna Shamte, Issa Rashid, Joseph Owino, Donald Musoti, Jonas Mkude, Haruna Chanongo, Henry Joseph, Amisi Tambwe, Said Hamis na Awadh Juma.

MTANI JEMBE: SIMBA VS YANGA - OKWI AANZIA BENCHI - KASEJA AANZA KIKOSI CHA KWANZA

1.Juma Kaseja - 29
2.Mbuyu Twite - 6
3.David Luhende - 3
4.Nadir Haroub "Cannavaro" - 23(C)
5.Kelvin Yondani "Cotton" - 5
6. Athuman Idd " Chuji" - 24
7.Mrisho Ngassa - 17
8.Frank Domayo - 18
9.Didier Kavumbagu - 7
10.Hamis Kiiza - 20
11.Haruna Niyonzima - 8
Subs:
1.Deogratius Munishi "Dida" -30
2.Juma Abdul - 12
3.Oscar Joshua - 4
4.Rajab Zahir - 14
5.Reliants Lusajo - 9
6.Nizar Khalfani - 16
7.Saimon Msuva
8. Hassan Dilunga - 26
9.Jerson Tegete - 10
10.Emmanuel Okwi - 25
11. Said Bahanuzi - 11
12.Hamis Thabit - 22

Friday, December 20, 2013

SIKINDE YAJICHIMBIA BAGAMOYO KUKABILI MSONDO KRISMASI




Na Mwandishi Wetu

HOMA ya pambano la watani wa jadi katika muziki wa dansi nchini kati ya Mlimani Park 'Wana Sikinde' na Msondo Ngoma 'Baba ya Muziki' litakalofanyika siku ya Krismasi imeanza kupanda kwa bendi hizo kujificha kambini na huku wakipigana vijembe.

Bendi hizo kongwe nchini zinatarajiwa kuonyeshana kazi katika onyesho litakalofanyika kwenye viwanja wa TCC Club Chang'ombe, Temeke Dar es Salaam katika kunogesha sikukuu hiyo ya Krismasi.

Katika kuonyesha wamelipania pambano hilo bendi ya Sikinde tayari imeiendea Msondo wilayani Bagamoyo kwa ajili ya kuweka kambi yao na wamewatahadharisha 'mahasimu' wao hao wasije wakatoa visingizio baada ya kugaragazwa kwenye onyesho hilo.

"Sisi tumeamua kuweka kambi yetu mjini Bagamoyo ambako tutatua viwanja vya TCC kutokea huko ili kuisambaratisha Msondo, na tunataka wajipange sawasawa ili wasije wakatoa visingizio tena kwa maana kama vyombo vipya bendi zote imepewa na Konyagi," Katibu wa Sikinde, Hamis Milambo alisema.

Milambo alisema mashabiki wa dansi wajitokeze kwa wingi kushuhudia namna gani wanavyowachachafya wapinzani wao hao, ikizingatiwa hawajakutana kwa muda tangu mwaka jana.

Upande wa Msondo kupitia Meneja wao, Said Kibiriti, alisema hawana haja ya kutaja mahali kambi yao ilipo isipokuwa wamejiandaa kuwatoa nishai wapinzani wao siku ya onyesho hilo litakaloanza saa nane mchana.

"Sisi hatuna mchecheto wowote na mpambano huo, tunaendelea kujifua kimya kimya mahali ambapo siwezi kupataja kwa sasa," alisema Kibiriti.

Naye muimbaji anayekuja juu wa bendi hiyo ya Msondo alitokea Sikinde, Athuman Kambi, alisema amejipanga kuonyesha umahiri wake katika mpambano huo baada ya kufanya hivyo wakati akiwa Sikinde dhidi ya Msondo kwenye ukumbi wa Diamond na kuwawehusha mashabiki wa muziki wa dansi nchini.

"Najua watu watataka kuona nafanya kitu gani dhidi ya bendi yangu ya zamani iliyonitangaza vyema, wasiwe na hofu waje Desemba 25 waone nini nitakachofanya TCC Club Chang'ombe," alisema Kambi.

Mpambano huo wa Sikinde na Msondo umeandaliwa na kampuni ya Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi, gazeti la NIPASHE, Integrated Communications, CXC Africa na Salute5.

HATUMWI MTOTO DUKANI


Credit: Youngafricans.co.tz

UCHAMBUZI: YANGA Vs SIMBA

Na baraka mbolembole

Kocha mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic tayari ameonesha kufanya
mabadiliko katika upangaji wa kikosi chake, huku yule wa timu ya
Yanga, Ernie Brandts akiongeza suala la stamina kwa kikosi chake.
Logarusic alimpanga kiungo, Henry Joseph katika nafasi ya ulinzi wa
kati wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya KMKM, wikiendi iliyopita na
mchezaji huyo alionesha kiwango kizuri.

 Kwa upande wa Yanga, kuwasili nchini na kujiunga na kambi ya timu
hiyo iliyopo katika hotel ya Protea kwa mshambuliaji, Emmanuel Okwi
kunataraji kuongeza ufanisi na makali zaidi safu ya mashambulizi ambayo mara kwa mara kocha, Brandts amekuwa akisema kuwa ni ' butu' na inayopoteza nafasi nyingi za kufunga, Okwi ni silaha ya hatari, huku
ushirikiano wake na washambuliaji Hamis Kizza na Mrisho Ngassa
ukisubiriwa kwa hamu.

MARA YA MWISHO...

April 20, 2003, mabao ya harakaharaka yaliyofungwa na kiungo, Salumu
Athumani, na mshambuliaji, Herry Morris katika dakika za 30 na 32, na
lile la dakika ya pili baada ya kuanza kwa kipindi cha pili la
kiungo-mshambuliaji, Kudra Omary yaliweza kuipatia ushindi wa mabao 3-0 Yanga katika uwanja wa CCM Kirumba, awali wiki mbili nyuma timu hizo zilifungana bao 1-1 katika mchezo wa kwanza wa kirafiki katika uwanja wa Uhuru. Simba ilitangulia kufunga kupitia kwa mshambuliaji Jumanne Shengo Tondola, na Yanga wakasawazisha kupitia kwa kiungo, Mrundi, Mwinyi Rajab.
MIAKA KUMI SASA.......

Kuongezwa kwa Okwi, na Said Dilunga katika kikosi cha Yanga kunaweza
kuwa kumeipa timu hiyo uimara zaidi katikati na bunduki muhimu mbele.
Lakini hakutasahihisha udhaifu mkubwa wa safu ya ulinzi. Kwa kuwa hata mabeki chaguo la kwanza wanapokuwa fiti, safu ya ulinzi huonekana kupwaya, waliruhusu mabao matatu dhidi ya Azam FC, na baadae Simba wakachomoa mabao yao matatu. Nahodha wa kikosi hicho, Nadir Haroub
amekuwa akionesha dhahiri uwezo wake katika mchezo wa ' man to man',
ila si mzuri katika kujipanga na kuzuhia njia za hatari,

 David Luhende bado anajaribu kiwango ambacho kilimfanya kuwa mchezaji wakutumainiwa katika nafasi ya ulinzi wa kushoto, Mbuyu Twite ni namba mbilI mzuri, anashambulia na kuzuhia kwa haraka, mtaalamu wa mipira ya kurushwa na mwenye uwezo mkubwa kwa kupiga mipira iliyokufa. Kocha, Brandts mara nyingi alikuwa akipiga kelele kuwa anahitaji mshambuliaji, na golikipa, na tayari amewapata Okwi na Juma Kaseja, ila hakuonekana kudai nyongeza yoyote ya mlinzi, hasa yule wa kati. Ni Kelvin Yondan pekee anayeweza kucheza mfululizo katika kinachoweza kuitwa kiwango cha juu. Uwepo wa washambuliaji kama Betram Mombeki, Hamis Tambwe, Edward Christopher kunaweza kumkumbusha kocha huyo kosa alilolifanya.

SIMBA KAMA BARCELONA, YANGA KAMA REAL MADRID

Barcelona, mara zote huwa wanatoa matokeo ya kushangaza, pale wanapotabiriwa kufanya vyema huwa wanaanguka vibaya, na pele wasipotarajiwa huwa wanafanya maajabu. Wakiwa na mchezaji bora zaidi duniani, mahasimu wao wanao wachezaji wa bei mbaya ndani ya uwanja. Katika mchezo wao wa kwanza wa ' clasico', Real Madrid ilitota mbele ya Barca. Na sasa, pengine uwepo wa Haruna Niyonzima, Okwi, Hamis Kiza, Didier Kavumbagu, Twite, Kelvin, Nadir, Yanga wakawa na thamani kubwa zaidi ndani ya uwanja, kipesa. Ila Simba imekuwa timu yenye vipaji vinavyoendana na utamadunia wao wa mchezo wa pasi za chini chini.

Herry Joseph atasogea katika nafasi ya kiungo wa ulinzi ili kumpisha mlinzi, Donald Musoti kucheza na Joseph Owino. Uchezaji wa Amri Kiemba unaweza kuwa silaha, au maangamizi kwa Simba endapo atakuwa katika kiwango cha juu Simba itaendelea kuwa timu ile ile inayojiamini ikicheza na Yanga, na endapo itatokea kucheza kwa kiwango cha chini, timu itapotea uwanjani kama ilivyokuwa mwezi oktoba, wakati ule Jonas Mkude aliposhindwa kujiamini.

4-3-3

Timu ya Yanga inaweza kuwapanga kwa pamoja, Okwi, Kiza, na Ngassa katika safu ya mashambilizi jambo ambalo litawachanga walinzi wa pembeni wa Simba, ambao kwa sasa hawapo katika viwango vya juu. Simba inataraji kutumia mfumo huo pia, na uwepo wa kiungo Awadg Juma utaunganisha nguvu na viungo, Mkude na Henry, na kuwaacha Tambwe, Mombeki, na Kiemba katika safu ya mbele.

Kwa kuwa ni mechi ambayo Yanga wanaitumia kuipanga timu yao katika usawa, ni wakati mzuri wa kuwapanga pamoja, Chuji, Domayo na Niyonzima katika kiungo ili kuuchezesha mfumo huo kwa mwendo unaotakiwa, kasi na pasi za uhakika, fupi fupi au zile zenye urefu na macho ya kuangaza. Yanga wanao wachezaji hao na Simba kwa sasa ni timu inayotakiwa kujiendesha kwa mfumo wa 4-4-2 kwa kuwatumia mawinga kupiga krosi kwa washambuliaji wao ambao wanaonekana ni wazuri kwa mipira hiyo.

YANGA, JUMA KASEJA GOLINI

Ni kipa mzuri, kama ambavyo ameweza kudhihirisha hilo kwa kipindi cha miaka 11 sasa, Kaseja atasimama katika mchezo wake wa kwanza wa uhakika tangu mwezi, septemba alipoiwakilisha timu ya taifa katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za kombe la dunia dhidi ya Gambia. Aliruhusu mabao mawili wakati Yanga iliposhinda kwa mabao 3-2 dhidi ya KMKM ya Zanzibar, wiki iliyopita. Ataongeza kitu katika lango la Yanga na safu nzima ya ulinzi. Kuwakumbusha majukumu yao mara kwa mara walinzi, kucheza mipira ya kona na krosi ambayo iliwapa sare ya 3-3 katika mchezo wa mwisho wa mahasimu hao.
0714 08 43 08

IANDIKIE MAELEZO (CAPTION ) HII PICHA.


FUFA YAMUIDHINISHA RASMI OKWI KUCHEZEA YANGA



WAKATI straika mpya wa Yanga, Emmanuel Okwi akitua nchini tayari kuitumikia timu yake mpya, Shirikisho la Soka la Uganda (Fufa) limesema mchezaji huyo ni halali kuichezea Yanga na ndiyo maana walikubali kutoa hati ya uhamisho wa kimataifa (ITC).

Ofisa Mtendaji mkuu wa Fufa, Edgar Watson ameuambia mtandao huu kwamba, anachojua kama bosi wa Fufa ni kwamba ni kweli Okwi amesaini kuichezea Yanga na shirikisho lake limetuma ITC kwenda Tanzania kwa Yanga ili aweze kuichezea timu hiyo.
“Kwanza nataka kuweka wazi kwamba, Okwi alikuwa na kesi dhidi ya timu ya Etoile du Sahel ya Tunisia juu ya masuala ya mkataba, Fifa (Shirikisho la Soka la Kimataifa) lilimruhusu kucheza kwenye klabu ambayo anaitaka kwa muda maalum.

 


Okwi alipewa kibali maalum, hivyo si kweli kuwa alikuja kucheza SC Villa ya hapa (Uganda) kama mchezaji wa mkopo, huyu alipewa kibali maalum sasa hapo kuna tofauti ya kibali maalum na mkopo,” alisema Watson.

Alisema Okwi aliruhusiwa kucheza na Fifa na ruhusa ambayo amepewa haikuwa ikimzuia kuhamishwa au kusajili kwenda klabu nyingine, hakuna mahali anapozuiliwa kusajiliwa bali kilichofanyika ni sawa na ruhusa ya kucheza.
Watson alisema kilichotokea ni kati ya Villa, mchezaji na huko alikosajiliwa ni baina yao na hakuna kinachomzuia asisajiliwe.

“Kwa mazingira yaliyopo, hakuna kipengele chochote ambacho kinamzuia mchezaji mwenye ruhusa maalum kuhamishwa hivyo tumetoa ITC na hakuna ambacho kingemzuia Okwi kwenda kule anakotaka,” alimalizia Watson.

BONYEZA HAPA CHINI KUSIKILIZA MAHOJIANO YA EDGAR WATSON.

TULIZANA, ANGALIA KWA UMAKINI KISHA TUAMBIE KIPI KIKOSI BORA



JE HIZI TIKETI ZA MPAMBANO WA SIMBA NA YANGA ZILIZOANZA KUUZWA MITAANI JANA NI HALALI ?


Thursday, December 19, 2013

OKWI ATUA NCHINI, AHAIDI KUFANYA KAZI KUBWA AZIACHIA SAKATA LA USAJILI ETOILE DU SAHEL, VILLA NA YANGA

SAA 9:50 Alasiri ya leo, straika mpya wa Yanga, Emmanuel Okwi ametua nchini kutoka Uganda tayari kwa kuitumikia timu yake mpya ambayo imemsajili hivi karibuni kutoka SC Villa.
Mashabiki zaidi ya 600 walijitokeza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kumpokea Okwi ambaye alipokewa na viongozi wa Yanga akiwemo Ofisa Habari, Baraka Kizuguto na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Seif Ahmed ‘Seif Magari’.
Muda mfupi baada ya kutoka nje na kukutana na mashabiki hao, Okwi aliwasalimia kisha akauzngumza kidogo na waandishi wa habari ambapo alisema kwa kifupi; “Nimekuja kufanya kazi.”
Okwi alisema yeye ni mchezaji wa kulipwa na anachofahamua sasa ni kutimiza wajibu wake wa kutumikia mkataba wake aliosaini hivi karibuni kuichezea Yanga.
Muda mfupi baada ya kuzungumza na waandishi wa habari, msafara wa Okwi kuelekea makao makuu ya klabu ya Yanga ulianza huku akitumia gari aina ya Toyota Brevis Ai 300 lenye namba za usajili T 457 CRQ.
Msafara huo ulikwenda moja kwa moja mitaa ya Jangwani na Twiga yaliyo makao makuu ya Yanga na moja kwa moja alisaini kitabu cha wageni kasha akapanda juu ya jengo la ghorofa la klabu hiyo na kuwasalimia mashabiki waliojitokeza.
Baada ya kushangiliwa na mashabiki hao, Okwi aliondoshwa kutoka Jangwani na kupelekwa hotelini ambako viongozi wa Yanga wakiongozwa na mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu hiyo, Mohamed Binda.
Kesho asubuhi Okwi anatarajiwa kuanza mazoezi na kikosi cha kwanza kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama.
APEWA JEZI NAMBA 25
Okwi amezaliwa tarehe 25 Desemba, hivyo mara tu baada ya kutua nchini alivalishwa jezi namba 25 ambayo hapo kabla ilikuwa ikivaliwa na beki Ibrahim Job.
Jezi hiyo ilikuwa pia ikivaliwa na Okwi wakati anaichezea Simba ambayo aliachana nayo Januari mwaka huu.