Search This Blog

Thursday, December 19, 2013

OKWI ATUA NCHINI, AHAIDI KUFANYA KAZI KUBWA AZIACHIA SAKATA LA USAJILI ETOILE DU SAHEL, VILLA NA YANGA

SAA 9:50 Alasiri ya leo, straika mpya wa Yanga, Emmanuel Okwi ametua nchini kutoka Uganda tayari kwa kuitumikia timu yake mpya ambayo imemsajili hivi karibuni kutoka SC Villa.
Mashabiki zaidi ya 600 walijitokeza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kumpokea Okwi ambaye alipokewa na viongozi wa Yanga akiwemo Ofisa Habari, Baraka Kizuguto na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Seif Ahmed ‘Seif Magari’.
Muda mfupi baada ya kutoka nje na kukutana na mashabiki hao, Okwi aliwasalimia kisha akauzngumza kidogo na waandishi wa habari ambapo alisema kwa kifupi; “Nimekuja kufanya kazi.”
Okwi alisema yeye ni mchezaji wa kulipwa na anachofahamua sasa ni kutimiza wajibu wake wa kutumikia mkataba wake aliosaini hivi karibuni kuichezea Yanga.
Muda mfupi baada ya kuzungumza na waandishi wa habari, msafara wa Okwi kuelekea makao makuu ya klabu ya Yanga ulianza huku akitumia gari aina ya Toyota Brevis Ai 300 lenye namba za usajili T 457 CRQ.
Msafara huo ulikwenda moja kwa moja mitaa ya Jangwani na Twiga yaliyo makao makuu ya Yanga na moja kwa moja alisaini kitabu cha wageni kasha akapanda juu ya jengo la ghorofa la klabu hiyo na kuwasalimia mashabiki waliojitokeza.
Baada ya kushangiliwa na mashabiki hao, Okwi aliondoshwa kutoka Jangwani na kupelekwa hotelini ambako viongozi wa Yanga wakiongozwa na mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu hiyo, Mohamed Binda.
Kesho asubuhi Okwi anatarajiwa kuanza mazoezi na kikosi cha kwanza kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama.
APEWA JEZI NAMBA 25
Okwi amezaliwa tarehe 25 Desemba, hivyo mara tu baada ya kutua nchini alivalishwa jezi namba 25 ambayo hapo kabla ilikuwa ikivaliwa na beki Ibrahim Job.
Jezi hiyo ilikuwa pia ikivaliwa na Okwi wakati anaichezea Simba ambayo aliachana nayo Januari mwaka huu.

No comments:

Post a Comment