Mkurugenzi wa mashindano wa chama cha soka cha Uganda Decolas Kiiza, amethibitisha kwamba shirikisho la soka duniani
FIFA limeridhia usajili wa mshambuliaji Emmanuel Okwi kujiunga na klabu ya Yanga.
“Ndio tuliandika barua FIFA na wametujibu kwamba mchezaji yupo huru kwa kusajiliwa na timu yoyote,"Kiiza alisema.
Mapema wiki hii CEO wa FUFA, Edgar Watson, alisema kwamba waliwasiliana na FIFA ili kupata maelezo juu ya uhalali wa usajili wa Okwi.
Yanga walikamilisha usajili wa Okwi mapema wiki hii kwa mkataba wa miaka miwili na huku ikiwa bado aliruhusiwa na FIFA kujiunga na SC Villa kwa muda maalum akitokea Etoile du Sahel.
Okwi tayari amewasili nchini akitokea Uganda kuja kujiunga na klabu ya Yanga mapema leo mchana.
Allan Papaok, mkurugenzi wa kampuni ambayo inashughulikia haki za Okwi, alisema leo kwamba bado hawajakamilisha usajili wa Okwi na YANGA.
“Tutasafiri kwenda Dar es salaam wikiendi hii kwa ajili ya kukamilisha usajili huu," aliongeza bwana Allan Papaok.
Hata hivyo maofisa wengi wa chama cha soka cha Uganda wanashangaa ni namna gani FIFA inaweza kumruhusu Okwi kujiunga na Yanga, wakati akiwa ameruhusiwa kujiunga na SC Villa kwa muda maalum kutoka Etoile du Sahel, ambao walikuwa na matatizo na Okwi.
Fifa wanaendesha mpiga kimagumashi hasa nchi ambazo zinaendelea. kwa kweli wanatimiza wajibu tu. hawafanyi kazi kabisa.
ReplyDeleteFifa hawako makini kabisa
ReplyDeletefifa wako makin sana sema wabongo hawajui kutafsiri sheria kaz kuropoka ropoka tu kwenye media badala ya kutafuta facts
ReplyDelete