Search This Blog

Saturday, January 18, 2014

YANGA KUIVAA KS FLAMURTARI

Young Africans kesho itashuka dimbani kucheza na timu ya KS Flamurtari Vlore inayoshika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Albania ikiwa ni sehemu ya mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu kwa timu zote, mchezo utakaofanyika katika eneo la Side Manavagat.
Huu utakua ni mchezo wa tatu wa Young Africans wa kujipima nguvu dhidi ya timu hiyo ya Ligi Kuu nchini Albani baada ya kuwa imeshacheza michezo miwili na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ankara Sekerspor na 2-0 dhidi ya timu ya Altay SK.
Kocha mkuu wa Young Africans Hans Van Der Plyum ameendelea na mazoezi leo asubuhi na jioni ataendelea na mazoezi pia kuwaandaa vijana wake kuwa tayari kwa mchezo huo, lakini pia kuwaweka tayari kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.  


Baada ya mchezo dhidi ya timu KS Flamurtari Vlore kesho, Young Africans itakamilisha ziara yake ya kambi ya mafunzo nchini Uturuki kwa kucheza na timu ya Simurq PIK inayoshikri Ligi Kuu nchini Azerbaijan katikati ya wiki ijayo kabla ya kuanza safari ya kurejea nchini Tanzania. 
Hali ya hewa jijini Manavgat ni nzuri na sio ya baridi kali kiasi kwamba haiwalazimu wachezaji kuwaa vifaa vya michezo vya baridi kwani hali inawaruhusu kuweza kufanya mazoezi na kucheza bila kuwa na mataitzo yoyote.
Mpaka sasa hakuna katika kambi ya klabu ya Young Africans nchini Uturuki hakuna mchezaji yoyote majeruhi isipokuwa kiungo Hassan Dilunga ambaye anasumbuliwa na malaria na tayari anaendelea vizuri baada ya kupatiwa tiba na daktari wa timu Dr. Suphian Juma.

Friday, January 17, 2014

KUONA SIMBA VS MTIBWA SH.5000


MABINGWA wa michuano ya mtani Jembe, timu ya Simba,
kesho inashuka katika Uwanja wa Taifa kuvaana na timu ya
Mtibwa Sugar, huku kiingilio cha chini kikiwa sh.5000.
Mchezo huo utakaoanza saa 10 jioni, ukiwa wa kirafiki,
kwa ajili ya kuziweka timu hizo sawa kabla ya kuanza kwa
Ligi Kuu tanzania Bara, inayoanza kutimua vumbi wiki
ijayo.Simba inaingia dimbani ikiwa inatoka kwenye mashindano
ya Mapinduzi, ambapo Simba ilichukua ushindi wa pili.
Katika mchezo huo Simba iliyopo chini ya kocha Zdravko
Logarusic akisaidiana na Suleiman Matola, imepanga
kutumia wachezaji wake, wote ili kiwe kipimo tosha kabla
ya Ligi Kuu.
Timu hiyo inayoshika nafasi ya nne katika msimamo wa
Ligi, imejipanga kuhakikisha inavuka mpaka nafasi ya
kwanza huku kocha wao Logarusic, akisema ana uhakika
kikosi chake kitaibuka na ushindi.Logarusic, alisema kuwa mchezo huo ni moja ya mtihani
wake wa kutambua kikosi chake, kabla ya kuanza kwa ligi
kuu.
Alisema ameambiwa kuwa Mtibwa Sugar, ni moja ya timu
nzuri hivyo anajua kwake ni kipimo kizuri.
"Nina amini mchezo wetu na Mtibwa Sugar, utakuwa mzuri
, kutokana na ubora wa timu hiyo, ninajua itasaidia timu
yangu kupata mazoezi mazuri"alisema Logarusic.
Nae kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime, alisema ana
amini mchezo huo utakuwa mzuri kwake kutokana na
wapinzani wao kutoka katika mashindano.
Mexime alisema kuwa amepata nafasi ya kucheza na timu
kubwa, ambayo itampa mazoezi mazuri.
"Nina amini mchezo huo utakuwa mzuri kwangu kwa kuwa
nacheza na timu kubwa ambayo imetoka kwenye
mashindano"alisema Mexime.
Katika mchezo huo viingilio vitakuwa shilingi 20,000 VIP A,
shilingi 10,000 katika VIP B, wakati VIP C itakuwa shilingi
7,000 na sehemu ya viti vya orange na bluu itakuwa shilingi 5000.

WATANZANIA KUCHEZESHA MECHI ZA CL, CC NA WASOMALI KUCHEZESHA YANGA, WACOMORO

Watanzania wanane wameteuliwa kuchezesha mechi mbili za marudiano za raundi ya awali za Ligi ya Mabingwa Afrika (CL) na Kombe la Shirikisho (CC) zitakazochezwa wikiendi ya Februari 14 na 16 mwaka huu.

Waamuzi hao walioteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ni Israel Mujuni atakayechezesha mechi ya CL kati ya Rayon Sport ya Rwanda na AC Leopards de Dolisie ya Congo itakayofanyika jijini Kigali.

Mujuni atasaidiwa na Josephat Bulali, Samwel Mpenzu na Ramadhan Ibada, wakati Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Jean Marie Hicuburundi wa Burundi.

Naye Waziri Sheha ataongoza jopo lingine kwenye mechi ya CC kati ya FC MK ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na El Ahly Atbara ya Sudan. Mechi hiyo itachezwa jijini Kinshasa.

Sheha atasaidiwa na Ferdinand Chacha, John Kanyenye na Israel Mujuni. Kamishna wa mechi hiyo ni Chayu Kabalamula kutoka Zambia.


WASOMALI KUCHEZESHA YANGA, WACOMORO

Shrikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Somalia kuchezesha mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na Komorozine Sports ya Comoro.

Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya mchujo itafanyika jijini Dar es Salaam kati ya Februari 7 na 9 mwaka huu wakati ile ya marudiano itachezwa kisiwani Comoro kati ya Februari 14 na 16 mwaka huu.

Mwamuzi wa kati atakuwa Hassan Mohamed Hagi wakati wasaidizi wake ni Hamza Hagi Abdi, Bashir Abdi Suleiman na Bashir Olab Arab. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Eugene Musoke kutoka Uganda.

Timu ambazo zimeingia moja kwa moja katika raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa ni Coton Sport ya Cameroon, El Ahly (Misri), TP Mazembe (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), El Hilal (Sudan), Club Sportif Sfaxien (Tunisia) na Esperance (Tunisia)

Nayo mechi ya kwanza ya raundi ya mchujo kati ya Azam ya Tanzania na Ferroviario Da Beira ya Msumbiji itakayofanyika Dar es Salaam kati ya Februari 7 na 9 mwaka huu itachezeshwa na waamuzi kutoka Sudan.

Waamuzi hao ni Mutaz Abdelbasit Khairalla atakayepuliza filimbi, Waleed Ahmed Ali, Aarif Hasab Elton na El Fatih Wadeed Khaleel. Kamishna wa mechi hiyo ni Hassan Mohamed Mohamed kutoka Somalia. Mechi ya marudiano itachezwa Msumbiji kati ya Februari 14 na 16 mwaka huu.

Timu zilizotinga moja kwa moja katika raundi ya kwanza ya michuano hiyo ni Asec Mimosas ya Ivory Coast, Ismailia (Misri), Wadi Degla (Misri), Djoliba (Mali), MAS (Morocco), Bayelsa United (Nigeria), El Ahly Shandy (Sudan), E.S.S. (Tunisia), C.A.B. (Tunisia) na Zesco United (Zambia).

TFF YANOA MAKATIBU MABORESHO TAIFA STARS

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeandaa semina ya siku mbili kwa makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa kuhusu maboresho ya timu ya Taifa (Taifa Stars).

Semina hiyo inafanyika ukumbi wa Singida Motel, mjini Singida kuanzia kesho (Januari 18 mwaka huu) ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa kwa washiriki kuhusu maboresho hayo.

TFF imeandaa mpango wa maboresho kwa Taifa Stars ambapo pamoja na mambo mengine umepanga kusaka vipaji nchini nzima kwa lengo la kupanua wigo wa kupata wachezaji wanaoweza kuchezea timu hiyo.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager mwaka huu inakabiliwa na mechi za mchujo za Kombe la Afrika (AFCON) ambalo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Morocco.

Mechi hizo za mchujo zitachezwa kati ya Septemba na Novemba mwaka huu ili kupata timu 16 zitakazofuzu kucheza fainali hizo.

SHABANI KADO YUPO BIZE NA MAZOEZI NCHINI OMAN.
Golikipa wa Coastal Union,Shabani Kado akijipumzisha baada ya mazoezi makali,Kado yupo na timu yake ya Coastal Union inayojiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya VODACOM nchini Oman.

VOGTS, WOLFGANG WAIBUKIA KAMBI YA YANGA


Wachezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Ujerumani  ambao kwa sasa ni makocha wa timu ya Taifa ya Azerbeijan Berti Vogts na msaidizi wake Wolfgang leo jioni kabla ya mazoezi waliibuka katika viwanja vya hotel ya Sueno Beach na kuongea kidogo na makocha wa Young Africans Hans na Mkwasa masuala ya kiufundi kisha kuagana nao na kuwaacha waendelee na progam yao ya mazoezi.
Vogts amabaye alikuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Ujerumani kwa miaka nane (1990-1998) na kufanikiwa kushinda kombe la Ulaya mwaka 1996, na kufika hatua ya robo fainali ya kombe la Dunia mwaka 1998 alikuwa ameambatana na kocha wake msaidizi Wolfagang .
Kocha mpya wa Young Africans mholanzi Hans Van Der Plyum leo ameanza rasmi kazi ya kukinoa kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara katika viwanja vya hoteli ya Sueno Beach Side baada ya jana kuiongoza katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Altay SK.


                                                        Mkwasa na Wolfagang

Hans ambaye amejiunga na Young Africans wiki hii akichukua nafasi ya kocha mholanzi aliyeondoka Ernie Brandts amesema atajitahid kadri ya uwezo wake pamoja na wachezaji na benchi la ufundi kuona wanaisaidia timu kufika hatua nyingine mbele zaidi.
"Amesema hawezi kufanya jambo lolote peke yake bali kwa kushirikiana kwa pamoja atafanikiwa kwani katika mchezo wa jana timu yake iliweza kucheza soka la kujituma na kushirikiana mwanzo mwisho kitu ambacho ndio falsafa yake katika ufundishaji" alisema Hans.
Timu ilifanya mazoezi ya asubuhi leo saa 5 kamili kwa saa za Uturuki mpaka saa 6:30 kabla ya kupumzika na kurejea tena mazoezini jioni saa 11 kamili jioni mpaka saa 12:30 ambapo alikuwa akiwaelekeza wachezaji jinsi gani anapendelea wacheze kwa kufuata mfumo wake. Kocha Msaidizi wa Young Africans Charles Mkwasa akiwa na Kocha Berti Vogts


Akiongea na www.youngafricans.co.tz mara baada ya mazoezi ya leo kocha Hans amesema timu ya Young Africans ina wachezaji wazuri ambao wana uwezo binafsi na bado wana nafasi ya kucheza soka kwa kipindi kirefu hivyo kikubwa wanapaswa kuwa fit muda wote ili waweze kutimiza majukumu yao.
Young Africnas itaendela na mazoezi kesho na asubuhi katika viwanja vya hotel ya Sueno kujiweka sawa kwa mchezo utakaofuata wa kirafiki kabla ya kurejea nchini wik ijayo tayari kwa mikikiki ya Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa. 

Kocha mkuu wa Young Africans Hans Van der Plyum akiwa na msaidizi wake Charles Mkwasa kabla ya kuanza mazoezi ya kuanza kwa mazoezi ya jioni katika viwanja vya hoteli ya Sueno Beach

ANDERSON AKWEA PIPA KUELEKEA ITALIA KUJIUNGA NA FIORENTINA

Kiungo wa Manchester United Anderson amesafiri kwenda jijini  Florence kwa ajili ya kwenda kufanya vipimo vy afya kwa ajili ya kujiunga kwa mkopo na klabu ya Serie A ya Fiorentina.

Mbrazil huyo amewaambia rafiki zake kwamba anataka uhamisho wa moja kwa moja ili kujihakikishia muda wa kucheza lakini United kwa sasa wapo tayari kutoa ruhusa ya biashara ya mkopo tu.

Anderson alitokea jijini Manchester kupitia Frankfurt leo alhamisi na anategemewa kukamilisha kila kitu kesho mchana.  


Anderson amecheza mechi 4 tu katika premier league msimu huu, na nane kwa ujumla.

Alijiunga na United mwaka 2007 akitokea Porto kwa ada ya  £20million, ameichezea timu hiyo mechi 179 na kuifungia mabao 9.  

Thursday, January 16, 2014

RAISI WA BAYERN MUNICH: RIBERY ANA THAMANI KUBWA KWETU KULIKO RONALDO - ROBBEN NA MANDUZKIC WATAENDELEA KUWEPO ALLIANZ ARENA

Pamoja na Cristiano Ronaldo kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia lakini raisi wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amesisitiza kwamba kamwe hawawezi kumbadilisha winga wao Franck Ribery na kumchukua mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo.

Winga wa Ufaransa Ribery alishika nafasi ya tatu nyuma ya mshambuliaji wa Real Madrid na Lionel Messi katika kura za Ballon d'or.

Rummenigge anasema hajasangazwa kwamba Ronaldo ameshinda tuzo hiyo lakini bado akasisitiza kwamba Ribery ana thamani kubwa kwao kuliko Ronaldo.

"Mara tu ulipoona kikundi cha watu waliomsindikiza Ronaldo kuja kwenye tuzo kutoka Madrid, haukuhitaji kuwa mtume kujua nini kinafuatia," mchezaji huyo wa zamani wa Ujerumani ya Magharibi aliiambia Bild.

"Lakini Bayern Munich hatuwezi kumbadilisha Frank na Ronaldo."

Rummenigge pia akasema kwamba Mabavaria watafanya kila waliwezalo kuhakikisha wanaendelea kuwa na Mario Mandzukic na Arjen Robben.

GUNDOGAN: NITAFANYA MAAMUZI JUU YA HATMA YANGU NDANI YA DORTMUND


Kiungo wa Borrusia Dortmund anayewindwa na klabu ya Manchester United Ilkay Gundogan ameonya kwamba hatofanya haraka katika kuamua hatima yake ndani ya klabu ya Borussia Dortmund.

Gundogan, 23, atakuwa nje ya mkataba na Dortmund mwakani na Dortmund wapo katika harakati za kumuongezea mkataba mpya baada ya kuwapoteza Mario Goetze na Robert Lewandowski 
wakienda kwa mahasimu wao Bayern Munich. United pia wanamuwinda kiungo mwenye thamani ya  £40million Marco Reus.

David Moyes anaweza kukutana na upinzani kutoka kwa  Real Madrid ambao nao wanatajwa kumtaka Gundogan, ambaye ana thamani ya £25m, lakini kiungo huyo hajacheza tangu mwaka jana mwezi wa August kwa sababu ya maumivu ya mgongo na anasisitiza kwamba atachukua muda wake katika kuamua nini kinafuata katika maisha yake ya soka.

‘Bado suala hili lipo wazi,' aliiambia gazeti la Sport Bild. ‘Dortmund ndio kipaumbele cha kwanza. Nitafanya maamuzi kamili hivi karibuni lakini mpaka sasa sijaamua chochote.

‘Nitarudi katika ubora wangu. Naamini kipindi nilichokaa nje kimenifanya kuwa bora na imara zaidi. Lakini ni vigumu kutabiri lini hasa nitacheza tena.'

MATIC AREJEA CHELSEA KWA ADA YA PAUNDI MILIONI 21Chelsea imekamilisha uhamisho wa kiungo raia wa Serbia Nemanja Matic has kutoka klabu ya Benfica ya Ureno.
Matic ambaye anarejea Chelsea baada ya kuihama akiwa ni sehemu ya uhamisho wa beki David Luiz,amesajiliwa tena kwa mkataba wa miaka 5 na nusu kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 21.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 tayari amekabidhiwa jezi namba 21.


Wednesday, January 15, 2014

HATIMAE KELVIN GARNETT ATIMIZA NDOTO YAKE YA KUKUTANA NA WACHEZAJI WA CHELSEA,SCHURRLE NA BA WAMTEMBEZA STAMFORD BRIDGE.


TWEETS ZA MASTAA BAADA YA TUZO ZA FIFA BALLON D'OR 2013.


AKIFANIKIWA KUJIUNGA NA WEST HAM UT, LACINA TRAORE ATAINGIA KWENYE ORODHA YA WACHEZAJI WAREFU KWENYE LIGI KUU YA ENGLAND

                                                                    WAREFU.                                     VIJEBA.


MANCHESTER UTD BADO YAONGOZA LIGI YA MAUZO YA JEZI...


SIMBA KUPIMANA NGUVU NA MTIBWA SUGAR

MABINGWA wa Mtani Jembe na washindi wa pili wa michuano ya
Mapinduzi, Jumamosi watajitupa katika Uwanja wa Taifa, kuvaana
na timu ya Mtibwa Sugar.
Mchezo huo wa kirafiki utakuwa wa mwisho kwa klabu ya Simba,
kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, inayoanza kutimua
vumbi Januari 25 mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam jana Kocha msaidizi wa Simba,
Suleiman Matola, alisema wameamua kupata mechi moja katika
uwanja wa taifa kabla ya kuanza kwa ligi.
Matola alisema sababu kuu ya kuamua kucheza mchezo huo ni
moja ya sehemu yao ya kuipa timu yao mazoezi katika uwanja wa
Taifa, ambao itachezea mechi zake za nyumbani.
Alisema wameamua kucheza mechi na timu ya Mtibwa, kwa
sababu wanaitambua bora wake, hivyo wakicheza nayo inawapa
maandalizi mazuri.
Matola alisema kuwa mchezo huo utafanyika majira ya saa 10.jioni,
ikiwa ni moja ya sehemu ya kocha wao Zdravko Lugarusic, kutaka
timu ngumu, ya kucheza na timu ya Simba.
"Haya ni maamuzi ya kocha mkuu Logarusic, anataka kuichezesha
timu yake na timu ngumu, ambayo itaipa mazoezi mazuri timu
yake, kabla ya kuanza kwaa ligi kuu"alisema Matola.
Simba iliyorejea juzi jijini Dar es Salaam, ikirtokea Zanzibar katika
michuano ya Mapinduzi, ambapo ilifika hatua ya fainali na kupata
ushindi wa pili wa michuano hiyo.

MOYES ATEMBELEA NCHI SITA ZA ULAYA NDANI YA SIKU NNE , SASA MASHABIKI WANASUBIRIA ALICHOKIVUNA...


UMEGUNDUA KITU GANI KUTOKANA NA NAMNA KURA ZILIVYOPIGWA ?

Waandishi wa Habari
1. Ribery 524
2. Ronaldo 399
3. Messi 365
  Makocha:   
1. Ronaldo 456 2. Messi 402 3. Ribery 314
Manahodha :   
1. Ronaldo 510 2. Messi 438 3. Ribery 289