Search This Blog

Saturday, December 7, 2013

VIDEO: MANCHESTER UNITED YAFUNGWA OLD TRAFFORD MARA MBILI MFULULIZO TANGU MWAKA 2002

VIDEO: CHELSEA CHALI - YAPIGWA NA STOKE CITY 3-2


All Goals Stoke City 3-2 Chelsea (07-12-2013... by video4all

MATOKEO EPL: MAN UNITED HALI YAZIDI MBAYA YAPIGWA NA NEWCASTLE - CHELSEA NAYO CHALI - MAN CITY YAKAZIWA


Manchester United 0-1 Newcastle
Southampton 1 – 1 Manchester City,
Liverpool 4 – 1 West Ham United,
Stoke City 3 – 2 Chelsea
West Brom 0 - 2 Norwich
Palace 2 – 0 Cardiff

KILI STARS YAIVUA UBINGWA UGANDA NA KUTINGA NUSU FAINALI - KUKIPIGA NA HARAMBEE DEC 10

Timu ya Kilimanjaro Stars leo hii imefanikiwa kufuta uteja kwa Uganda baada ya kuifunga timu hiyo katika mchezo wa robo fainali ya kombe la CECAFA Challenge Cup.

Mchezo huo wa robo wa fainali uliochezwa jioni ya leo Kili Stars imefanikiwa kuivua ubingwa The Cranes na kuingia robo nusu fainali baada ya kushinda mikwaju ya penati 3-2 huku kipa Ivo Mapunda akiibuka kuwa shujaa.


Katika dakika 90 timu hizo zilitoka sare ya bao 2-2, Stars walianza kuongoza kwa mabao mawili yaliyofungwa na Mrisho Ngassa, lakini Uganda wakasawazisha kupitia Sserunkuma Dakika ya 16 na Martin Mpuga kipind cha pili katika dakika 73.

Kwa matokeo hayo Kilimanjaro Stars itamenyana na wenyeji, Kenya, Harambee Stars katika Nusu Fainali ya Kwanza ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Desemba 10, mwaka huu Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.

WANACHAMA SIMBA KUTINGA BUNGENI JUMANNE.


WANACHAMA wa klabu ya Simba wanaompinga Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage wataelekea mjini Dodoma Jumanne kwa ajili ya kuonana na Spika wa Bunge hilo, Anna Makinda kuelezea namna Mwenyekiti huyo anavyovunja Katiba ya klabu hiyo.
Awali wanachama hao walipanga kuondoka leo kwenda Dodoma ili kesho Jumatatu waonane na spika lakini wamehairisha kutokana na kesho kuangukia siku ya Uhuru ambapo watu awaendi makazini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam kwa niaba ya  wanachama wenzake, Katibu wa tawi la mzambalauni, Daniel Kamna mwenye kadi ya uwanachama wa klabu hiyo namba 100, alisema kuwa lengo lao wanataka kufikisha matatizo ya Rage kwenye klabu hiyo kwa wabunge  hili wamshauri kuachia madaraka klabuni hapo.
"juzi tulimpa siku mbili awe amejiuzulu..., lakini ameonekana kuwa mkaidi na kiburi, sasa sisi msimamo wetu uko pale pale tumeshajipanga na tumewasiliana na wabunge wanachama wa klabu yetuambao wametualika bungeni na tutaondoka hapa Jumanne ili siku inayofuata asubuhi tuingine bungeni," alisema Kamna.
Alisema kuwa mwenyekiti wao huyo ameonyesha jeuri na kutowasikiliza wanachama waliomuweka madarakani na badala yake amekuwa na maamuzi ya peke yake yasiyokuwa na faida kwa klabu hiyo.
Kamna alisema moja ya jambo ambalo limewashangaza ni kitendo cha Mwenyekiti huyo alipokutana na mmiliki wa klabu ya Sunderland ya Uingereza mapema mwaka huu ambapo badala ya kuomba msaada kwa ajili ya klabu (Rage) aliomba msaada kwa jili ya jimbo lake la Tabora mjini.
"Sasa mtu kama huyo klabuni kwetu wa nini, ameonyesha kuweka masrai yake binafsi mbele badala ya Simba kwanza," aliongezea kusema Kamna.
Alisema kuwa Simba inawanachama na mashabiki wabunge ambao aliwataja baadhi yao kuwa ni Makongoro Mahanga, Zitto Kabwe, Iddi Azan na Mussa Azan Zungu ambao watafanikisha wao wanachama kuingia bungeni siku hiyo ya Jumatano.
"Unajua uwezi kuingia bungeni bila kuwa na mwaliko maalum kutoka kwa aidha mbunge au kiongozi mwingine pale bungeni, tayari tumepata mwaliko na tunajiandaa na safari," aliongezea kusema Kamna.
Alisema kuwa hawana ugomvi na Rage ila wanapingana naye baada ya kuonyesha vitenda vya wazi vya kuvunja katiba ya klabu hiyo hivyo wanataka ajiuzulu na kuwaachia Simba yao.
Hata hivyo alipotafutwa Rage kwa njia ya simu kuzungumzia kauri hiyo ya wanachama, simu yake ya mkononi haikuwa ikipatikana.
Klabu ya Simba ipo kwenye mvutano mkubwa wa kiuongozi katika kipindi hiki ambacho timu nyingi zipo kwenye maandalizi kwa ajili mzunguko wa pili wa ligi kuu.
Wanachama na baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji wa klabu hiyo wanamtaka Mwenyekiti wao Rage ajiuzulu kwa madai ya kushindwa kufuata katiba ya klabu hiyo.

Friday, December 6, 2013

WILFRED ZAHA AKANUSHA KUWA NA MAHUSIANO NA MTOTO WA MOYES: ASEMA HIYO SIO SABABU YA KUKOSA NAFASI YA KUCHEZA

Untrue: Zaha never dated Lauren Moyes, daughter of United manager David, here pictured at Old Trafford
Zaha: The 21-year-old has found himself playing for the Under 21s this year instead of with the first team
Wilfried Zaha amechukua hatua ya aina yake kukanusha taarifa zilizozagaa kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na mtoto wa kike wa kocha mkuu wa Manchester United David Moyes.

Winga huyo mwenye miaka 21 alinunuliwa na Sir Alex Ferguson kwa £15milllion lakini ameshindwa kupata nafasi ya kucheza ndani ya kikosi cha kwanza chini ya David Moyes.

Kumekuwepo na taarifa kwamba amekuwa hapewi nafasi ya kucheza na Moyes kwasababu ya mahusiano yake na binti wa kocha huyo aitwaye Lauren.
Lakini Zaha - ameonekana kukerwa sana na tetesi hizo - ametumia ukurasa wake wa Twittet kuwaambia mashabiki 490,000 kwamba taarifa hizo sio za kweli.

'Sijawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi wala kukutana na binti wa David Moyes, hivyo jambo hilo haliwezi kuwa sababu ya kukosa kwangu nafasi katika kikosi cha kwanza ...,' aliandika Zaha.

'Ningependa hizi taarifa za uongo ziachwe kusambazwa….Nitaichezea Manchester United pindi kocha atakapoana nipo tayari kufanya hivyo...'

Zaha aliichezea United katika mchezo wa kombe la hisani lakini tangu wakati huo ameichezea mechi moja tu ya mashindano dhidi ya Norwich City katika League Cup.

MAKUNDI KOMBE LA DUNIA: ENGLAND, URENO ZAPANGWA MAKUNDI YA KIFO - FAINALI YA 2010 KUCHEZWA KWENYE MAKUNDI - SPAIN NA UHOLANZI KUNDI MOJA


GROUP A: Brazil, Croata, Mexico, Cameroon.
GROUP B: Spain, Holland, Chile, Australia.
GROUP C: Colombia, Greece, Ivory Coast, Japan.
GROUP D: Uruguay, Costa Rica, ENGLAND, Italy.
GROUP E: Switzerland, Ecuador, France, Honduras.
GROUP F: Argentina, Bosnia and Herzegovina, Iran, Nigeria.
GROUP G: Germany, Portugal, Ghana, USA.
GROUP H: Belgium, Algeria, Russia, South Korea.


MIMI NI BINGWA,WEWE JE ?


PICHA ZA MAKOCHA WANAOJADILI MUSTAKABALI WA TAIFA STARS- KUTOKA ZANZIBAR

 Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe ambaye bia yake inadhamini Taifa Stars, akitoa mada wakati wa ufunguzi wa mkutano unaojumuisha wataalamu mbalimbali kutoka Tanzania bara na Zanzibar ili kuangalia namna ya kuboresha Timu ya Taifa (Taifa Stars). Waliokaa kutoka kushoto ni Rais wa ZFA Ravia Idarous Faina, Rais wa TFF Jamal Malinzi, Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar, Hamisi Said na Makamu wa Rais wa ZFA Ali Mohamed Ali. Mkutano huo wa siku tatu unaodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager unafanyika katika hoteli ya Mtoni Marine visiwani Zanzibar.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar, Hamisi Said (aliyekaa katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na jopo la makocha na wakufunzi maarufu nchini wanaokutana Visiwani Zanzibar kuangalia namna ya kuboresha Timu ya Taifa Taifa Stars. Wengine waliokaa kutoka kushoto ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager George Kavishe, Makamu wa Rais wa ZFA Ali Mohamed Ali, Rais wa TFF Jamal Malinzi, Rais wa ZFA Ravia Idarous Faina, mwenyekiti wa jopo hilo la wataalamu, Kanali mstaafu Idd Kipingu na Katibu wake Rutayuoga Pelegrinius.

KATIBU MKUU WA SIMBA ASAJILIWA RASMI KUWA WAKILI WA KUJITEGEMEA LEO HII


Katibu mkuu wa klabu ya Simba Evodius Mtawala leo hii amesajiliwa rasmi kuwa mwanasheria/WAKILI wa kujitegemea. Mtawala ambaye alisomea masuala ya sheria na katika chuo kikuu cha Mzumbe alipohitimu na kutunukiwa degree ya kwanza ya sheria, baadae akaweka gambani postgraduate ya sheria kutoka Law School of Tanzania. 

Mtawala ambaye ni mmoja ya viongozi vijana wachache katika vilabu vya soka Tanzania ambao shule imelala kichwani, pia ana masters ya business administration kutoka Esami.

*HONGERA KAMANDA*

KUNA TATIZO TIMU YA VIJANA YANGA……WACHEZAJI William Lucian ‘Gallas’, Jonas Mkude, Said Ndemla na chipukizi wengine wanaotamba katika kikosi cha Simba kwa sasa, wametokana na malezi mazuri waliyopata wakiwa katika kikosi cha vijana cha klabu hiyo.

Kikosi hicho kilichokuwa kinaundwa na wachezaji wenye umri chini ya miaka 20, kilikuwa kikipata matunzo mazuri chini ya kocha Seleman Matola na viongozi wengine waliokuwa wakiitolea macho timu hiyo.

Vijana hao walikuwa wawajibikaji wazuri ndani ya timu na taratibu mmoja mmoja wakaanza kupandishwa kikosi cha kwanza na leo hii asilimia 50 ya wachezaji wa Simba wanatokana na kikosi hicho.Tofauti na Simba, Yanga kwa upande wake haikuwa na kikosi bora kwani uongozi haukuwa karibu na timu na hata katika huduma haukuwa ukiihudumia timu ipasavyo hadi kocha Aboubakar Salum ‘Sure Boy’ akaamua kuachia ngazi.

Yanga haikuona umuhimu wa timu na badala yake ilikuwa na timu kimagumashi na ndiyo maana haikuweza kufanya vizuri katika michuano ya Kombe la Uhai mwaka jana.

Baada ya michuano ya mwaka jana, na Simba kuonekana imefanya vizuri kidogo Yanga wakashtuka na kuanza kuitazama timu kwa macho mawili lakini nguvu hiyo ya viongozi iliishia katika kuwakusanya vijana wa kuichezea timu hiyo. Unaweza kuita usajili.Ushiriki wa mwaka huu:

Katika Kombe la Uhai mwaka huu, Yanga ilishiriki na kufanikiwa kufika fainali lakini ukweli ni kwamba pongezi za kipekee zinatakiwa zifike kwa wachezaji na makocha wao Salvatory Edward na Anthony Chibasa, Salva ni kiungo mahili wa timu hiyo wa zamani.

Viongozi wa timu walikuwa mbali na vijana wao ambao pengine wangetiwa moyo tangu zamani kama wangeuona ujio wa viongozi katika mechi zao za awali. Ishu hapa si kufika mazoezini tu na katika mechi, lakini tutazame vijana hawa wanahamasishwa vipi kuweza kupata ushindi.

Kama nguvu ya viongozi wa Yanga ingetumika tangu mechi za kwanza, bila shaka Yanga ingekuwa bingwa na sasa tungekuwa tunazungumza mengine.Ni nani aliyekuwa akiwatembelea vijana hawa katika kambi yao pale Jangwani? Ni ahadi ipi waliyopata kama wangechukua ubingwa? Kiongozi mmoja kulundikiwa vitu vingi vya kufanya kwa vijana hawa, inasababisha wachezaji kumzoea mtu mmoja tu na kujiona si sehemu ya Yanga.

Ikumbukwe ya kwamba, kikosi hichi ndiyo kioo cha timu ijayo ya Yanga ambayo sasa inaelekea ukingoni. Hivi mkataba ya kina Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima, Hamisi Kiiza na wengine ikiisha huku fedha ya ziada ya usajili ikikosekana Yanga itapata wapi wachezaji kama si kuwatumia vijana hawa?

Nadhani bado kuna tatizo la kiungozi katika timu ya vijana ya Yanga, kwani kocha anaonekana kama ndiye meneja anayejua matatizo yote ya kila mchezaji na kutatua au kuweka daraja la wachezaji na uongozi.

Kuna kitu Yanga inapaswa kukifanya ili iweze kufanikiwa katika soka la vijana na iweze kufanikiwa kwani kwa kuendelea kufanya mambo ya sasa hali itaendelea kuwa ya kawaida na mafanikio hayataonekana.

Viongozi wasiibuke kutoka walipojichimbia na kujisogeza kwa timu baada ya kuona inaelekea kupata mafanikio, huu ni utamaduni ambao haufai kama kweli tunataka mafanikio katika soka.

CRISTIANO RONALDO, ASHLEY COLE, PIQUE, LEBRON JAMES WAWAONGOZA WANAMICHEZO KUMKUMBUKA HAYATI NELSON MANDELA


'MATOKEO MABAYA HAYATOTUATHIRI KIBIASHARA - TUNA UWEZO WA KUSAJILI WACHEZAJI WATANO' - ASEMA BOSS WA MANCHESTER UNITED

CEO wa klabu ya Manchester United Ed Woodward amesisitiza kwamba klabu yao haihitaji kuendelea kushinda mataji ili kuweza kuendela kuvutia wadhamini. 

United imeweza kupunguza kwa kiasi kikubwa deni lao kutoka na kuongezeka kwa wadhamini wengi kwenye klabu hiyo. 

Matokeo ya robo ya kwanza ya mwaka wa kifedha umeonyesha ongezeko la mapato katika udhamini, ambayo yameendelea kuongezeka, huku madili kibao ya udhamini yakiendelea kusainiwa. 

Na Woodward ana uhakika kwamba jambo litaendelea haijalishi hali ngumu ya matokeo wanayopitia United katika kipindi hiki. 
Akiongea na jarida la fanzine ‘United We Stand’, katika mahojiano yaliyofanyika mwezi wa 10 lakini yamechapishwa leo baada ya mchezo wa jana dhidi ya Everton, Woodward anaelezea sababu zake juu ya mtazamo wake.

'Ukweli halisia ni kwamba huwezi kushinda kila siku. 

'Angalia mfano mzuri Liverpool. Bado wanauza namba kubwa ya jezi na dili zuri na la pili kwa ukubwa katika Premier League.
'Wana moja ya mkataba mzuri wa kiufundi - na hawajashinda ubingwa wa ligi tangu 1990. 
'Ikiwa tuna mwaka mmoja m'baya then tunao msuli mkubwa wa kiuchumi wa kubadilisha timu. Tuna uwezo mkubwa wa kiuchumi ambao badala ya kuuza wachezaji watatu na kununua watatu, sie tunaweza kununua watano.'

Na msuli huo wa kiuchumi unamaanisha kwamba haki za kubadilisha jina la uwanja wa Old Trafford hazitouzwa kamwe.

'Ni muhimu kwa  Old Trafford kubaki Old Trafford,' alisema.
'Akina Glazers ni watu ambao wana misingi ya kufuata sana utamaduni.
'Watu wametuuliza kama tunafikiria kuuza haki za jina la uwanja, hatuwezi kufanya hivyo.'

BAADA YA KUFUNGIWA MWAKA MMOJA KWA KUTUMIA MADAWA - DECO AKATA RUFAA MAHAKAMANI


Kiungo wa zamani wa klabu ya Chelsea na Barcelona Deco amekata rufaa katika mahakama ya kimataifa ya michezo CAS kupinga adhabu ya kufungiwa mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kutumia madawa yasiyoruhusiwa michezoni.

Deco, 36, ambaye alitangaza kustaafu soka mwezi August mwaka huu, alipimwa na kukutwa na madawa aina ya furosemide mwilini mwake wakati huo akiwa anaichezea klabu ya Brazil - Fluminense mnamo mwezi March.

Kiungo huyo alijitetea kwamba madawa yaliyokutwa mwilini mwake yalitokana na kunywa vinywaji wa vitamin.

Thursday, December 5, 2013

GATTUSO: HAKUNA NAFASI YA MWANAMKE KATIKA SOKA, APONDA BINTI WA BERLUSCONI KUPEWA UONGOZI MILAN


KIUNGO wa zamani wa klabu ya AC Milan na timu ya taifa ya Italia, Gennaro Gattuso ameponda nafasi ya mwanamke kuwajibika katika majukumu ya kiuongozi katika soka akionyesha wazi kupinga kuteuliwa kwa Barbara Berlusconi kuwa kiongozi wa Milan.

Barbara, ambaye ni binti wa rais wa Milan, waziri mkuu wa zamani wa Italia, Silvio Berlusconi, atafanya kazi sambamba na Adriano Galliani kwa muda wa miaka miwili kitendo ambacho kinaweza kusababisha mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Ariedo Braida kujiuzulu.

Gattuso haamini kwamba uamuzi huo ni sahihi kwa klabu hiyo na amezidi kuiponda Milan kwa kumpa mwanamke majukumu makubwa ndani ya timu yenye nguvu Italia

"Samahani, lakini siamini kama mwanamke ana nguvu katika utawala wa soka," alisema Gattuso alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja cha redio. "Hivyo ndivyo ninavyoona. Nafikiri ilitakiwa heshima zaidi kwa mtu kama Galliani."

Kutokana na uteuzi huo wa Barbara, wiki iliyopita Galliani aliandika barua ya kujiuzulu kwa kile kilichoelezwa kwamba binti huyo atakuwa na nguvu zaidi ya uamuzi kuliko yeye kitu alichodhani ni dharau kwake. Hata hivyo, rais Berlusconi alimwomba Galliani kutengua uamuzi huo.

Katika kuweka mambo sawa, Galliani amepewa jukumu la kusimamia miradi yote ya michezo wakati Barbara atashughulikia mambo ya masoko na mengine ya kijamii.

Gattuso mwenye umri wa miaka 35, kwa sasa hana kazi baada ya kutimuliwa kuinoa klabu ya daraja la pili ya Palermo baada ya kutofanya vizuri ndani ya mwezi mmoja. Gattuso pia amewahi kuinoa klabu ya Sion ya Uswisi lakini nako alitimuliwa Mei mwaka huu.

KOCHA WA SIMBA MIEZI SITA ATAFANYA KITU GANI?


SARAKASI za uongozi ndani ya klabu ya Simba bado zinaendelea huku pande mbili zinazolumbana kushika hatamu ya uongozi, kila upande ukimtangaza kocha wake.

Upande wa kwanza unaongozwa na Kaimu Mwenyekiti, Joseph Itang’are ‘Mzee Kinesi’ umempa kazi Kocha raia wa Croatia, Zdravko Logarusic wakati upande wa pili unaoongozwa na Mwenyekiti Ismail Aden Rage, ukisema bado Abdallah Kibadeni ndiye kocha.

Lakini wakati hali ikiwa hivyo, upande wa Mzee Kinesi ndiyo unaoonekana umeshinda kwani tayari Logarusic ameshatua nchini na ameshaanza kazi ya kuifundisha Simba kwenye mazoezi yake yanayoendelea kwenye Uwanja wa Kinesi, Shekilango jijini Dar es Salaam.

Ina maana kwamba kambi ya Mzee Kinesi ndiyo inayomilikia timu kwa sasa na timu ndiyo Simba yenyewe. Upande mwingine unaweza kuwa unamiliki majengo ya kufanyia mikutano lakini hatamu ya timu ipo mikononi mwa kundi linalompinga Rage
Simba imeingia mkataba wa miezi sita na Logarusic ili ainoe klabu hiyo inayoshika nafasi ya nne katika Ligi Kuu Bara lakini nyuma ya pazia kuna mambo mengi nyuma yake.

Kwanza Logarusic anakutana na kikosi ambacho hamfahamu mchezaji hata mmoja wa Simba, kidogo ingekuwa rahisi kwake kama angalau angekuwa na ufahamu hata mdogo wa kikosi cha timu hiyo.

Hii inamaanisha kwamba, Logarusic sasa anaenda kukibomoa kikosi cha kwanza cha Simba ambacho kwa kiasi fulani kilikuwa kimeshaanza kuaminiwa na Kibadeni.

Sasa Logarusic anawasubiri wachezaji wa Simba waliopo katika kikosi cha Kilimanjaro Stars na Zanzibar Herose ambao wapo Nairobi Kenya wakishiriki fainali za Kombe la Chalenji zinazofikia tamati Desemba 13 mwaka huu.

Kwa kuwa Logarusic hana cha kupoteza ndani ya miezi sita yake ya mkataba moja kwa moja hawezi kuwa na mawazo ya mbali zaidi katika kuifundisha klabu hiyo kwani, anafahamu fika hata afanyeje hali inaweza kuwa tofauti kwake baada ya muda huo.

Tazama hata usajili uliofanywa na Simba haujulikani kama umefuata ripoti ya nani kati ya kamati ya utendaji na ile ya Kibadeni ambayo inaelezwa haina mambo mengi ya kiufundi.Nipo na George Masatu...

Masatu aeleza kifundi,

Beki wa zamani wa Simba, George Masatu ameonyesha wazi kwamba haungi mkono ujio wa kocha mpya katika kikosi cha Simba tena mwenye mkataba mfupi na anasema hilo ni jambo hatari kwa maendeleo ya klabu kubwa kama Simba.

Masatu anasema ingekuwa jambo jema kama Simba ingempa mkataba Logarusic baada ya kuisha kwa msimu huu kwani angepata muda mzuri wa maandalizi pia angejua nafasi ipi yenye matatizo katika kikosi chake.

“Muda ni mdogo katika maandalizi na moja kwa moja kocha mpya anaweza kufanikiwa endapo tu wachezaji watajituma kupita kiasi kwani ni ngumu kubadili mfumo kwa mazoezi ndani ya muda mfupi,” alisema Masatu.


Haitakuwa haki kumlaumu Logarusic akishindwa,

Kwa kawaida Logarusic akifungwa mechi mbili mfululizo katika mzunguko wa pili wa ligi, lazima mashabiki wa Simba watamlaumu na mbaya zaidi wanaweza hata kumuanzishia maneno ya kumtimua.

Mbaya zaidi hata viongozi wake waliompa kazi wanaweza wakashindwa kuvumulia hali hiyo na moja kwa moja wataanza kutazama namna ya kumtoa huku wakijaribu kumpangia kikosi ili kupata ushindi kama wanavyodhani.

Tunachokiomba wote ni kuona Logarusic anafanikiwa katika kazi yake na kuiweka Simba katika ramani mpya ya soka nchini na Afrika kwa ujumla kwani ikifanikiwa kutwaa ubingwa wa bara itapata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika au ikishika nafasi ya pili itacheza Kombe la Shirikisho Afrika.

Simba ambayo sasa ipo katika mapambano makali ndani na nje ya uwanja, mashabiki wake wanapaswa kuungana na kuwa kitu kimoja kuweka macho yao yote katika timu uwanjani na si katika kambi za uongozi ambazo zote hazipo kwa manufaa ya klabu.

Kila la kheri Logarusic na harakati zake za kuinoa Simba, daima Simba itafanikiwa endapo wanachama na mashabiki wataungana na kukubaliana kwa kila jambo linalotokea ndani ya Simba.

BAADA YA KIPIGO CHA JANA KUTOKA KWA EVERTON - SOMA BARUA HII YA WAZI YA SHABIKI WA MAN U KWENDA KWA DAVID MOYESMpendwa Moyes,Kwa heshima na taadhima juu ya ukweli kwamba uliteuliwa na Sir Alex Ferguson, ningependa kutoa maoni namna nisivyoridhishwa na unavyoendelea kuiharibu ngome ambayo ilituchukua miaka mingi kuijenga.


Kwanza, kuhusu mchezo dhidi ya Everton, haikuwa siri kwamba  Fellaini, Giggs na Wellbeck hawakuwa na msaada kwa timu… huzuni ni kwamba Kagawa na Rafael wakawa wahanga wa ile  'small team mentality' ambayo inaonyesha wazi ni vigumu kuiondoa kichwani mwako!! Ukamuingiza Chicharito dakika za mwisho ili nae akumbane na aibu uliyotuletea.


Ikiwa bado hujajua, wewe sasa ni kocha Manchehester United na utamaduni wa Manchester united hatuchezi ili kushinda tu mechi kadhaa bali ni kushinda ubingwa wa ligi. KUTOKA KWENYE MTAZAMO WA KIJAMII 

Je una ufahamu wowote namna ulivyotutengenezea mazingira magumu sisi mashabiki wa (MAN UTD) kuvaa jezi zetu za MAN UTD?? Unajua namna ambavyo tunaepukana na mitandao ya kijamii kwa kuogopa madongo na maneno ya kejeli ya wapinzani wetu? Nina uhakika ulisikia, wakati ukiwa Everton kwamba sisi tuna kelele na tunaongea sana kuhusu ubora wa yetu lakini mpaka sasa hautupi msingi wa kuweza kuizungumzia timu yetu kwa mazuri, unatupa unyonge ambao hatujauzoea. MTAZAMO WA KIUCHUMI 

Jaribu kufikiria kuhusu wale wenzetu ambao huwekeza fedha zao katika michezo ya kubet ambao sasa wengine wanafilisika kutokana na timu kufanya vibaya.


Angalia namna mapato ya baa na migahawa yanavyoathirika kwa sababu wengi wetu mashabiki wa United tunaangalia mpira tumejifungia majumbani mwetu. Nafahamu unajua wengi wetu tunakunywa sana. MTAZAMO WA KIIMANI. 

Vitabu vya dhambi zetu hivi sasa vimezidi kuisha kurasa kwa sababu umetufanya tumekuwa tunatukana sana siku hizi, kutabasamu kwetu imekuwa tatizo na badala yake presha zetu zinaishia kwa wake zetu, watoto wetu na watu wetu wa karibu wasio na hatia.MTAZAMO WA KIAFYA 

Maisha yetu ya siku hizi yamekuwa kama wagonjwa wa "Insomnia" (Ugonjwa wa ukosefu wa usingizi) wiki mpaka wiki, wengi wetu mashabiki wa Man UTD sasa tumekuwa katika hatari ya kupata magonjwa ya presha kwa msongo wa mawazo unaotupa, pia unajua madaktari wengi ni mashabiki wa Man UTD hivyo unaweza ku-imagine namna wagonjwa ambao ni mashabiki wa  Arsenal, Chelsea na Liverpool wanavyokuwa katika wakati mgumu kutibiwa vizuri (especially in the theatre)Nakataa kuamini kwamba sisi ni timu ndogo kwa sababu tumekuwa tukitafuna bubble gum na kubeba tu makombe. Tumegoma kutumia mikono yetu yote miwili kuhesabu tofauti ya pointi zilizopo baina yetu na viongozi wa msimamo wa ligi. Tumegoma kuona ukiwaacha wachezaji wa maana kwenye benchi na kufanya majaribio yako na Fellaini(Nyoshi), Giggs na Welbeck.  Nakutakia kheri ukiwa unaanza vita ya kupigania ajira yako ndani ya old Trafford na ningependa kukushauri kwamba jaribu kutafuna bubble gum, utaonekana vizuri kiasi. P.S: Hongera kwa kutimiza lengo lako; Kuifunga Man UTD ndani ya old Trafford na kutibua rekodi yetu. Kwa huzuni kubwa na masikito,

Ni mie mshabiki mkubwa  Man UTD 

HATUMTAKI RAGE AJIONDOE MWENYEWE IFIKAPO JUMAMOSI DEC 7 
Wanachama wa Simba wamemtaka Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage kujiudhuru ifikapo jumamosi baada ya hapo wao wanakwenda mjini Dodoma ili kumshinikiza ajihudhuru.
 
Wakizungumza katika ukumbi wa idara ya Habari Maelezo mchana wa leo, Alhamis Desemba 5, 2013 walisema wamechoka na vituko vya mwenyekiti wao maana kila wakimtaka aitishe mkutano mkuu amekuwa akikiuka.
 
"Tunasema hatumtaki Rage na Wambura wake maana kila siku yeye anavunja katiba sasa asubiri maamuzi ya wanachama kama tutamfutia uanachama au tutamuondoa kabisa madarakani
 
Kwa Hisani ya : HABARI NA MATUKIO

KAMA YAYA TOURE KAMA ABDI KASSIM....MECHI YA NANI MTANI JEMBE KUCHEZWA DESEMBA 21Mechi ya Nani Mtani Jembe kati ya Simba na Yanga zinazodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itachezwa Jumamosi, Desemba 21, 2013 saa kumi kamili jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Meneja wa Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe amesema “Tayari Simba na Yanga zimesaini makubaliano ya kucheza MECHI YA NANI MTANI JEMBE (NANI MTANI JEMBE MATCH). Pambano hili  ni zawadi ya kufungia mwaka kwa mashabiki na kila timu imetia sahihi makubaliano kwamba itachezesha kikosi cha kwanza ili kuwapa mashabiki burudani ya uhakika.”
Kavishe aliongeza kuwa mechi hii ni maalum kwa ajili ya kuhitimisha kampeni ya Nani Mtani Jembe ambayo imeendeshwa kwa zaidi ya miezi miwili ikiwapa fursa mashabiki wa timu hizi kuchangia timu zao kila wanapoburudika na bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Kilimanjaro Premium Lager   ilitenga kiasi cha shilingi milioni 100 zinazoshindaniwa na Simba na Yanga kupitia mashabiki wake na tarehe 21 Desemba ndio utakuwa mwisho wa kampeni ya Nani Mtani Jembe ambapo baada ya mechi  fedha hizo zitagawanywa kwa kila timu kulingana na matokeo ya kura za mashabiki na klabu zitajiamulia namna ya kutumia fedha hizo.
Kampeni hii imeleta msisimko mkubwa sana kati ya mashabiki na hadi sasa matokeo ya kampeni hii yanaonyesha kwamba Yanga wanaongoza wakiwa na kiasi cha shilingi milioni 76 huku Simba wakiwa na kiasi cha shilingi milioni 24
Mashabiki wa Simba na Yanga wanaoshiriki katika kampeni ya Nani Mtani Jembe wanaendelea kunufaika zaidi na zawadi kabambe zilizoandaliwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager ili kuongeza msisimko na ushiriki katika kampeni hiyo ambapo mashabiki watatu wa Simba na mashabiki watatu wa Yanga wanajishindia kiasi cha shilingi 300,000/= kila mmoja katika droo zinazofanyika mara moja kila wiki. Droo kubwa itafanyika tarehe 21 Desemba.  Ambapo katika droo hiyo kubwa shilingi milioni 6 zitatolewa kama zawadi kwa washindi wawili -  mmoja shabiki wa Yanga na mwingine shabiki wa Simba ambapo kila mmoja atajishindia shilingi milioni tatu. 

 Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Mussa Katabaro, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala na Mkurugezi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba wakioshela alama ya dole baada ya kutangaza Simba na Yanga kucheza mechi ya Nani Mtani Jembe itakayochezwa Desemba 21 jijini Dar es salaam (Executive Solutions)