Search This Blog

Saturday, December 7, 2013

KILI STARS YAIVUA UBINGWA UGANDA NA KUTINGA NUSU FAINALI - KUKIPIGA NA HARAMBEE DEC 10

Timu ya Kilimanjaro Stars leo hii imefanikiwa kufuta uteja kwa Uganda baada ya kuifunga timu hiyo katika mchezo wa robo fainali ya kombe la CECAFA Challenge Cup.

Mchezo huo wa robo wa fainali uliochezwa jioni ya leo Kili Stars imefanikiwa kuivua ubingwa The Cranes na kuingia robo nusu fainali baada ya kushinda mikwaju ya penati 3-2 huku kipa Ivo Mapunda akiibuka kuwa shujaa.


Katika dakika 90 timu hizo zilitoka sare ya bao 2-2, Stars walianza kuongoza kwa mabao mawili yaliyofungwa na Mrisho Ngassa, lakini Uganda wakasawazisha kupitia Sserunkuma Dakika ya 16 na Martin Mpuga kipind cha pili katika dakika 73.

Kwa matokeo hayo Kilimanjaro Stars itamenyana na wenyeji, Kenya, Harambee Stars katika Nusu Fainali ya Kwanza ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Desemba 10, mwaka huu Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.

1 comment:

  1. Hongereni nyie vijana na benchi la ufundi.Mechi dhidi ya Harambee itahitaji 'discipline' ya hali ya juu sana.wachezaji punguzeni jazba za KITOTO mnapofanyiwa faulo ili kuepukana na kadi ziszo za lazima.Mnacheza na timu mwenyeji,mwamuzi anaweza kuwa na presha,kuweni makini kwenye kuwania mipira/ukabaji ili kuepuka kufanya faulo.Mkizingatia hayo,Harambee wanafungika ndani ya dakika 90.Mungu ibariki Tanzania Bara

    David V

    ReplyDelete