Search This Blog

Saturday, January 12, 2013

YANGA YAMALIZA MAZOEZI NCHINI UTURUKI LEO ASUBUHI


Wachezaji wa Young Africans, Juma Abdul, Said Bahanuzi & Didier wakifanya mazoezi ya Gym leo asubuhi katika Hotel ya Fame Residence
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 Young Africans leo asubuhi imemaliza mazoezi  yake kwa kufanya mazoezi ya kujenga mwili na uimara (Gym) iliyopo katika hoteli ya Fame Residence leo asubuhi na yakiwa ndio mazoezi ya mwisho katika kambi ya mafunzo ya wiki mbili iliyokuwa ikiendelea katika viwanja vya Fame Residence Football mijini Antlaya.

Kocha mkuu Ernest Brandts akishirikiana na Fred Felix Mizniro na Razaki Siwa leo waliongoza mazoezi ya Gym kuanzia majira ya saa tatu na nusu asubuhi mpaka majira ya saa saa tano na nusu asubuhi ambapo baada ya mazoezi hayo wachezaji wamepewa nafasi ya kupumzika kujiandaa na safari ya hapo kesho kurudi Tanzania.
 
Akiongelea michezo ya kirafiki mitatu waliocheza na timu za Armini Bielefeld, Deinizlispor na Emmen Fc kocha mkuu wa Yanga Ernest Brandts amesema michezo ilikuwa ni mizuri na wamepata nafasi ya kuona mapungufu machache yaliyojitokeza na anaamini watayafanyia kazi na kuendelea kufanya vizuri.
 
Tumecheza michezo mitatu, wa kwanza tulitoka sare na Amrinia Bielefeleld, mchezo ulikua mzuri na timu yangu ilicheza vizuri kwa dakika 90 zote za  mchezo licha ya Arminia kusawaisha bao dakika za lala salama huku mwamuzi aklishindwa kutoa maamuzi sawa na mshika kibendera wake, ambapo mfungaji alikua maeotea.
 
Mchezo wa pili dhidi ya Denizlispor nao pia timu ilicheza vizuri na kuweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini umakini wa washambuliaji ulitukosesha ushindi kwani Tegete alitumia nafasi aliyoipta kufunga bao la mapema kabla ya Waturuki hawajasawazisha kwa bao la utata  kisha kupewa penati ya utata pia.
 
Mchezo wa mwisho dhidi ya Emmen FC ulikuwa mzuri pia na kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza tuliutawala mchezo na kupata nafasi kadhaa za kufunga mabao lakini kutokua makini wa washambuliaji wetu pia kulichangia sisi kukosa ushindi, kabla ya kipindi cha pili Emmen FC kucharuka na kupata mabo mawili ya haraka haraka kutokana na uzembe wa walinzi na mlinda mlango Yusuph abDUL
 
Tunaushukuru uongozi kwa kukubali kutupa nafasi ya kuweka kambi Uturuki, tumkeaa pamoja kwa mda mrefu huku tukitoka mafunzo kwa vitendo, vifaa na mahitaji yote vikiwepo ,kukiwa na hali ya utulivu, kifupi tumejifunza mambomengi sana ya msingi ambayo yatatusaidia kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom na mashindano yatakayotukabili alisema 'Brandts'
Ally Mustafa 'Barthez, na Nizar Khalfani wakifanya mazoezi ya Gym leo asubuhi katika hoteli ya Fame Residence (SOURCE:YOUNGAFRICANS.CO.TZ

SIMBA WAENDELEA KUWASILI KWA MAKUNDI OMAN - SINGANO 'MESSI' NA ABDALLAH SESEME WAWASILI LEO


Wachezaji wawili wa Simba, Abdallah Seseme (kushoto) na Ramadhan Singano ‘Messi’, wakipokewa na Talib Hilal (kulia) na Ofisa wa Ubalozi wa Tanzania Oman, Abdallah Kilima mara baada ya kuwasili nchini Oman kujiunga na wenzao kambini, leo.
Singano na Seseme wakiwa uwanja wa ndege nchini Oman leo baada ya kutua. Wanasalimiana na waliokwenda kuwapokea. (PICHA NA SALEHE ALLY)

Friday, January 11, 2013

VITA YA MADARAKA NDANI YA REAL MADRID CHANZO KIMOJAWAPO CHA KUFANYA VIBAYA MSIMU HUU

“Kuwa na maadui ili kukupa vyote sio lazima, lakini ni vizuri. Hasa pale unapokuwa unafurahia mafanikio na unajisahau na kujiachia." Jose Mourinho

Jose Mourinho anaweza akawa amepigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza lake. Uamuzi wa kumuacha Iker Casillas, nahodha wa klabu, mchezaji ambaye ndio nembo inayowakilisha Real Madrid, uamuzi huo wa Mourinho unatafsiriwa kuwa jaribio la kujiua mwenye kwa “Special one”.

Katika hii vita inayoendelea ya madaraka pale Bernabeau, Mourinho ameenda mbali kwenye suala hili Casillas. Raisi Florentino Perez amekuwa hafurahishwi na tabia za Mourinho na ripoti zinasema kwamba yeye yupo upande wa Casillas katika vita inayoendelea dhidi ya Mou.


MCHEZO WA MOURINHO:
Tangu alipowasili pale Madrid Mourinho ameweza kuiongoza timu yake kwa njia moja tu anayoijua yeye, utata. Imani yake ni kwamba inabidi atafute namna ya kucheza na saikolojia za wapinzani wake au 'maadui' ili kufanikiwa.

Ilikuwa ni sababu hii ambayo iliwafanya Barcelona wakatae kumpa ajira ya kuwa kocha wao mwaka 2008. Mfumo wake wa uendeshaji timu ulilpelekea watu kuchukiana na kugombana. 

Perez alimleta Madrid kuja kuondoa utawala wa Barcelona kwenye La Liga. Hasira zake dhidi ya Barcelona ambao walimchagua Guardiola badala yake ziliongoza hisia zake. Matamanio yake ya kuwatukana kisaikolojia wakatalunya na maneja wao yaliongozwa na mambo yake binafsi dhidi ya Barca. Ilionekana kuwa zaidi ya 'mind games', hii ilikuwa hatua ya utashi wake binafsi kuiharibia klabu ambayo ndio imekuwa nembo ya utamu wa soka.

Je Perez aliuza roho ya klabu kwa shetani?
Ingawa muongo uliopita umekuwa m'baya na usio na mafanikio kwa Real, lakini ufahari na asili ya Madrid siku zote umekuwa ni wa kujiona kama 'Wafalme wa Soka'. Wachezaji kama Zidane, Puskas, Di Stefano, Raul na Ronaldo De Lima wote wamewahi kuvaa uzi mweupe na kuleta mafanikio na heshima kwa klabu hiyo.

Ujio wa Cristiano Ronaldo, Benzema na Kaka ulikuwa unaaminisha ni kuundwa kwa 'Galatico' mpya. Mourinho alionekana ndio mwanaume anayefaa kuipeleka timu kwenye kilele cha mafanikio tena. Na msimu uliopita Mourinho alifanikiwa kuwa bingwa wa La Liga na jinsi mashabiki walivyoshangilia ilionyesha ni kiasi gani ubingwa huo ulikuwa na umuhimu kwa klabu, wachezaji na wapenzi wa Madrid. Madrid walikuwa hawazuiliki mwaka uliopita, wakizishinda timu kwa spidi yao kali, nguvu na viwango bora vya wachezaji. Lakini walishindwa kufanikiwa barani ulaya, wakishindwa kuleta ubingwa wa 10 wa Ulaya ambao mashabiki na Raisi wa timu hiyo wanauota kila siku. 
Ukweli ni kwamba Perez alikuwa tayari kumpa kila Mourinho kama ilikuwa ni kwa ajili ya kushinda. Huu ni mchezo hatari kuucheza na matokeo yake yanaonekana sasa. Mourinho alitaka kuwa na mamlaka ya kila kitu; usajili, soka la vijana, na mipango mengine yanayohusu kikosi chake. Kama ilivyo kwa makocha wachache kwenye ulimwengu wa soka, alitaka kupewa mamalka makubwa ndani ya klabu.
  

Ingawa Jorge Valdano aliondolewa kwa sababu hakuwa akikubaliana na Mourinho na sera zake, haikuwa rahisi kwa Mourinho. Perez anaonekana kupoteza uatayari wako wa kumkabidhi Mourinho madaraka yote na wachezaji wa muda mrefu wa kihispania wanaonekana kutokuwa na furaha na kinachoendelea. Vita kati ya kocha na wachezaji (kitu ambacho cha kawaida kwenye klabu yake ya zamani ya Chelsea) ni kitu kinachoendelea na Perez anaonekana kuwepo upande wa wachezaji dhidi ya kocha wao. 

Mourinho alitaka kuibadilisha Madrid na sera yao na alitaka kupata madaraka ya kuipeleka timu mbele zaidi. Lakini anaona matamanio yake ya kuibadilisha klabu hayakubaliki na hayaaminiki. Mourinho hivyo anaamua kushindana na wanaompinga, tabia ambayo inaweza ikawa na matokeo mabaya kwa matamanio yake ya kutaka kushinda kombe la Ulaya akiwa na timu ya 3 tofauti.  

Je Mourinho  hakuielewa Madrid?

Sera yenye kuongozwa na utata inaweza kuwa ilifanikiwa katika vilabu vyake vya nyuma huko kama vile Inter na Chelsea, ilileta mafanikio na mashabiki na wachezaji walimpenda na kumtukuzakwa hilo. Ingawa, kosa lake kwa wakati huu ni kuamini Real Madrid itakuwa ni kama klabu zake alizofundisha nyuma. 

Pale Inter, Chelsea na Porto Mourinho alikuwa mshindi  na alipendwa na wachezaji na mashabiki. Alizipeleka timu zake kutawala ligi za nyumbani na ulaya akiwa na Porto na Inter. Yalikuwa ni mafanikio kwa kocha huyo mreno na hakuna la kushangaza Madrid wakaamua kumchukua. Ingawa, mafanikio katika zile klabu huko nyuma yalikuja kutokana na sera yake ya kucheza na saikolojia za wachezaji wake, vyombo vya habari na wapinzani wake ilifanya kazi.

Alivichukua vikosi ambavyo vilionekana na wengi kuwa vya kawaida na kuvifanya kuwa mabingwa. Akaja Madrid ambapo ni klabu yenye utajiri wa utamaduni na historia na yenye kujiamini yenyewe kama ndio klabu bora duniani; sio tu kwa suala la mafanikio bali pia na staili. Mashabiki walitaka mafanikio na bado wakataka kuona soka safi likitandazwa. 

Wakati staili ya Barcelona ikiwa inatajwa kuwa bora kama ilivyo kwa timu ya Spain, Madrid walikuwa wanaonekana wa kawaida. Staili ya kidachi/kikatalunya ya kucheza soka iliwavutia mashabiki na muhimu zaidi ikapelekea mafanikio makubwa katika historia ya Barcelona. 

Badala ya ya kuikumbatia staili hiyo, Mourinho akaamua kwenda kinyume chake. Alitaka timu yake icheze kama Inter zamani, ilinde, icheze kibabe ili kupunguza mashambulizi ya wachezaji hasa kwenye za El Classico. Aliwaambia wachezaji wake wafanye udanganyifu, na kuwatisha Barcelona. Ingawa, kwa sababu nyingi staili hii haikuweza kufanya kazi, Barca waliendelea kushinda na Mourinho na Madrid  walikuwa wanaonekana tu kama wagomvi, wenye wivu ya vipaji vya mahasimu wao. 

Ingawa wachezaji kama Pepe, Marcelo na Di Maria waliletwa maalum kwa sera za Mourinho ya soka, kuna wachezaji ambao hawakuwa wanakubaliana na sera zake za kucheza soka la kibabe, nje na ndani ya uwanja.  

Haikushangaza kwamba walikuwa ni Casillas, Ramos na Alonso ambao walionyesha kutokukubaliana na kuucheza mchezo wa Mourinho. Wachezaji hawa ambao walishinda kombe la dunia na Euro wakiwa na Spain hivyo walikuwa wanashea mahusiano mazuri na wachezaji wa Barca. Mourinho sasa alikuwa akitaka kuwafanya wachezaji hao wawaone Barca maadui zao na kuwaletea ubabe wenzao ambao ni marafiki zao timu ya taifa ya nchi yao. 

Akiwa na Inter na Chelsea alifanikiwa kuwaaminisha wachezaji kufuata sera yake, muda huu sera yake hiyo imekutana na upinzani mkali dhidi ya wachezaji wenye nguvu ndani ya klabu. 

Madrid msimu uliopita chini ya Mourinho walikuwa vizuri na moja ya vilabu vya kuogopwa barani ulaya. Walikuwa na safu yenye makali mno iliyokuwa na njaa ya kufanya balaa kwenye nyavu za wapinzani wao. Pointi zao na magoli yalionyesha ni kiasi gani walitisha, na hatimaye waliweza kuwafunika Barcelona.

Msimu huu mambo yamebadilika. Ule moto haupo tena, kile kilichokuwa kinawapa motisha ya kutaka kushinda zaidi kinaonekana kimepotea. Timu inaonekana kugawanyika, na klabu yote inaonekana kama jumba la sanaa za maonyesho ya nani aliyebora miongoni mwao.

JE MOURINHO ANAMMISI MPINZANI WAKE?
Mwanzoni mwa makala haya kulikuwepo na kauli iliyosema - 
“Kuwa na maadui ili kukupa vyote sio lazima, lakini ni vizuri. Hasa pale unapokuwa unafurahia mafanikio na unajisahau na kujiachia."
 
Inaonekana sasa baada ya kufanikiwa kushinda La Liga kikosi cha Madrid msimu kilikuwa kinalenga kwenye Champions league, huku Guardiola akiwa ameondoka tayari na Madrid wakimuongeza Luka Modric kwenye kikosi chao kilichokuwa bora tayari, ilionekana hakuna kitakachowasimamisha. Lakini mambo yamegeuka sasa hivi, wanauana wenyewe kwa wenyewe sasa hivi. Suala la Guardiola kama mpinzani linaanza kuleta maana sasa. 


Mourinho alisema kwenye kauli yake hapo juu kuhusu Guardiola kwamba mpinzani wake huyo alikuwa ni mtu ambaye alimfanya awe anafanya kazi kwa juhuhdi sana. Inaonekana kwamba Mourinho alifanya kazi akimuangalia kama Guardiola kama changamoto kwake na wachezaji wake. 
Kuwashinda Barca na kocha wao ikawa ni kitu ambacho kiliingia kwenye hisia za Mourinho kuwa ni lazima hata iweje. Msimu uliopita alishinda, Guardiola alishindwa na Madrid walishangilia sana. Lakini sasa Guardiola akiwa ameondoka, Madrid wamepoteza hali ya kupigana ya msimu uliopit, Madrid wamekosa kitu cha kuwasukuma kushindana zaidi? Adui yao mkubwa aliyewasumbua vilivyo ameondoka, amewaacha Mourinho na Madrid yake wakiwa wana hisia za upweke.  

Kwa mujibu wa Mourinho alikuwa mpinzani wake aliyempa msukumo wa kushindana zaidi, hivyo inawezekana kuondoka kwake kumemfanya ali-relax kama alivyosema, kitu ambacho kinaonekana kimewaingia wachezaji na hivyo kuleta madhara kwenye matokeo.

Mourinho sasa anaonekana ameshindwa kazi, wachezaji baadhi na raisi wanaripotiwa kumchoka na kuna hisia zipo kwamba mabadiliko yanatakiwa kwenye klabu. 

Inaonekana mwisho wa Mourinho ndani ya Santiago Bernabeu umewadia. Yeye mwenyewe, wachezaji, mashabiki na raisi kuna hisia zinazojieleza wamefikia sehemu wote wanasema kauli moja 'Imetosha'. Kwa Mourinho atakuwa na machaguo mengi baada ya Madrid, sehemu ambayo atakuwa analipwa £10million kwa mwaka. Japokuwa, ikiwa ataondoka Madrid bila medali ya ushindi wa Champions league, atakuwa amefeli katika kazi yake kubwa kabisa tangu aanze kufundisha soka. 

CLOUDS MEDIA YATOKA SARE YA MABAO 3:3 NA GEBI PRESHA YA MAGOMENI JIJINI DSM.

  Hapa ilikuwa mapema kabla ya mchezo tukipeana majukumu ya kufanya uwanjani...
  Hapa mfumo ulikuwa ukitengenezwa na kupeana majukumu....
Anatory Kabezi,Benny Kinyaia,Mimi,Salum Muhando na Joram Nyaumba.
  Mashabiki wa Gebi Presha.....
    Kikosi cha Gebi Presha kabla ya kuanza mchezo...


   Kosi la Clouds Media....
   Kosi la Gebi Presha......
   Picha ya pamoja.......
    Kwenye mchezo huu nimefunga bao moja,mabao mengine yakiwekwa kimiani na Anatory Kabezi na yule kijana Juma Omary aliyetembea kwa miguu kutoka Morogoro mpaka Dar.

   


   Mchezo huu ulimalizika kwa timu hizi kufungana mabao 3:3

    Kiongozi na nahodha wa Gebi Presha Tanaluza Adam aliyenyanyua mkono ....huku mimi na Maestro tukijadiliana jambo...


    Pigo hili ndo lilizaa bao la pili la Clouds Media,hili bao nilifunga mwenyewe kwa guu langu la 'dhahabu'
Kocha mchezaji Ibrahi Masoud 'Maestro' akifanya analysis ya kipindi cha kwanza na nini kikafanyike kipindi cha pili wakati wa mapumziko.
  Kiungo mkabaji Joram Nyaumba ' McBeth Sibaya ' wa Clouds Tv
    Anatory Nuno Kabezi mwenye jezi namba 11 akiwa mbioni kumuona kipa wa Gebi Presha,namimi kwa mbaaaaaliiii
    Antonio Nugaz yupo makini akisikiliza....
   Salum Muhando wa Clouds Tv akimsikiliza Kocha wakati wa mapumziko...
  Wakati wa mapumziko...tukisikiliza mawaidha toka kwa kocha mchezaji Ibrahim Masoud ' Maestro '
  Hapa nilikua na uchuuuu........
MASHABIKI WA GEBI PRESHA WAKIZUNGUKA UWANJA NA VIGOMA VYAO.

EXCLUSIVE: SIMBA WAKIWA NCHINI OMAN WAKIJIFUA

Haruna Moshi Boban akiwaongoza wachezaji wenzie wa Simba kwenye mazoezi ya leo asubuhi

Mazoezi ya viungo yakiendelea

Kocha wa Simba Patrick Leiwing akiongoza mazoezi leo asubuhi


Kiggy Makasi dimbani

PICHA ZOTE NA SALEH ALLY WA CHAMPIONI

TAIFA STARS YAPIGWA 2-1 ETHIOPIA MJINI ADDIS ABABA

Tanzania (Taifa Stars) imepoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ethiopia uliochezwa leo (Januari 11, 2013) kwenye Uwanja wa Addis Ababa hapa jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Mechi hiyo iliyochezeshwa na Bamlak Tesema wa Ethiopia ilikuwa ya kusisimua, hasa kutokana na timu zote kucheza kwa kasi kwa muda wote. Wenyeji Ethiopia ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 13 lililofungwa na Fuad Ibrahim akiwa wastani wa hatua
sita kutoka kwa mlinda mlango Juma Kaseja wa Taifa Stars.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kama kilivyokuwa cha kwanza, huku Ethiopia wakiwa wamefanya mabadiliko kwa wachezaji watano. Tanzania ilifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 50 likifungwa na Mbwana Samata baada ya kumzidi maarifa beki
mmoja wa Ethiopia.

Bao la ushindi kwa Ethiopia lilifungwa kwa kichwa dakika ya 69 na mshambuliaji Shemelis Bekele aliyeingia kipindi cha pili akiunganisha mpira wa krosi uliopigwa na winga Yossuf Sallah kutoka upande wa kushoto.


Taifa Stars inarejea nyumbani kesho (Jumamosi, Januari 12 mwaka huu) ambapo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius

Nyerere (JNIA) saa 7 kamili mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines.


Taifa Stars: Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Issa Rashid, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Amri Kiemba, Mrisho Ngasa, Salum

Abubakar, Thomas Ulimwengu/Khamis Mcha, mwinyi Kazimoto na Mbwana Samata.

YANGA YAENDELEA KULA VIPIGO UTURUKI - YAGONGWA 2-0 NA EMMEN FC



Klabu bingwa ya Afrika mashariki na kati Dar Young African wameendelea na mechi za kujifua huko nchini Uturuki kwa leo kucheza na timu ya Emmen FC ya ligi daraja la kwanza nchini Uholanzi  katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika viwanja vya Adora football - Berek pembeni kidogo ya mji wa Antlaya. Mechi hiyo imeisha hivi punde kwa Yanga kufungwa mabao 2-0.

Thursday, January 10, 2013

KIOTA CHA KUANGALIA MPAMBANO WA MAN UTD vs LIVERPOOL,ARSENAL vs MAN CITY

JE BARCELONA INAMTEGEMEA SANA LIONEL MESSI? NA JE GUARDIOLA NDIYE ANASTAHILI HIZI TUZO ZA MESSI? (PART 111)

Kwa kumtengeneza Messi kama nyota wa timu, Guardiola alitengeneza mzimu. Kwa kujaribu  kumfurahisha Messi makocha Pep na Tito waliiathiri timu. Hili linaweza kuakisiwa kwa jinsi Barcelona "Inavyomtendea" David Villa.

Villa aliahidiwa kucheza nafasi ya mshambuliaji wa kati aliposajiliwa, lakini akatupwa kushoto kama ilivyokuwa kwa Henry. Alifanikiwa mwanzoni baada ya kufunga kwenye msimu wa mwaka 2010/11, kabla ya jeraha alilopata msimu uliopita kulikuwa na ripoti za kuwa kwenye hali isiyo nzuri ya kisaikolojia kwa Villa kutokana na jukumu analopewa uwanjani kwenye timu na jinsi Messi alivyokuwa anabebwa kwenye timu na Guardiola.
Zikaanza kuvuja taarifa kuwa Villa anataka kuhama huku taarifa hizo zikizidi msimu huu baada ya mchezaji huyo kupona. Hata kabla ya kuondoka kwa Vilanova kabla ya kuugua kwake alishamuondoa Villa kwenye kikosi cha wachezaji kumi na moja wanaoanza mara kwa mara. 


Nadhani ni sahihi kuitazama hali hii kama hali ambayo inajenga kitu kibaya Barcelona. Mambo mengi sana yanapitia kwa Messi hali inayofanya wenzie kukosa umuhimu na pamoja na Barca kuanza na kufikia hatua ya kati ya ligi vizuri bado kuna ukosefu mkubwa sana wa balance kwenye timu.

Msimu huu uliopita kumekuwa na hali ya 'figisu figisu' kati ya David Villa na Messi ambapo Messi alionekana kukerwa na kitendo cha Villa kutompa pasi mwenzie mapema. Isaac Tello amelazimika kubadili mchezo wake ili kukidhi haja ya yeye kucheza kikosi kimoja na Messi. Timu imekuwa sana kwa Messi kiasi kwamba mtu anajiuliza mafanikio barani ulaya yatapatikanaje. 


Ligi inaonekana kuwa ya Barca tayari na hata huko kama kambi ya Real Madrid isingekuwa na matatizo yake pengine hali isingekuwa hivi, ila mafanikio ya ukweli yanapatikana ulaya kwenye ligi ya mabingwa na kwa sasa kuna timu ambazo zinaonekana kuwa na balance kuliko Barca kama Bayern na Juventus.

Barcelona imekuwa 'MESSI SHOW' na hii imefanya aonekana kuwa mchezaji bora kuliko wengine kwenye historia ya mchezo wa soka. Hata hivyo hiyo imekuja kwa gharama kubwa ya timu ambayo inaonekana kuwa chini ya Messi na haina umuhimu zaidi yake. Wachezaji wenzie na makocha wamekuwa chini yake kwa kuwa ana nguvu sana kuwaliko wao huku wachezaji wenzie wakiwa na woga wa kutompa mipira na kumuudhi wala kutompanga kwenye kikosi cha kwanza.


Je haya ni mazingira ya kujenga mafanikio kweli au mazingira yanayojenga mwanya wa kufeli, mtu mmoja hawezi kushinda kila kitu kwa timu nzima, ni timu ndio zinazopata mafanikio. Hispania imetwaa ubingwa wa Euro mara mbili na kombe la dunia kwa kuwa wana timu iliyokamilika na yenye balance na hawakuwa na mchezaji kama Messi na kama Barcelona hawatakuwa makini watakuwa kama Argentina ambayo ina messi ambaye hana msaada mkubwa sana.


Ukweli ni kwamba Messi amekuwa jawabu jepesi kwa Barca wakati mchezo ukiwa unahitaji bao kwa upande wa timu yake. Utegemezi kwa mtu huyu utakuja kuwa na madhara, mchezaji ataona kama jukumu lake kwenye timu halipingiki na bila kujijua atatumia uwezo wake vibaya. Messi anatajwa kama kijana mpole asiye na makuu ila hakuna wa kupinga kuwa anafahamu fika kuwa ana uwezo gani na umuhimu gani kwa timu yake na hili linampa nguvu kwenye kikosi cha Barcelona.


Barcelona wanaweza kuchagua mojawapo kati ya mambo mawili. Kinachohitajika ni balance kwenye timu, na balance hii itapatikana kwa kupata mtu atakayecheza mbele na Messi kuliko inavyoonekana sasa ambapo kuna viungo wanaofanya kazi ya kumpa Messi mipira. Kama Villa sio jawabu basi atafutwe mtu wa kutimiza jukumu hili, mtu ambaye anaweza kutoka pembeni na kuingia ndani  Neymar anaonekana kuwa mtu ambaye hata Messi amemuidhinisha kufanya kazi hii.


Pili na la kushangaza kwa wengi ni hili, kama Barca wanaweza wamuuze Messi kwa fedha nyingi, ni mchezaji bora kwa sasa kuliko wote, hakuna ubishi kwenye hili na ndio anayelipwa fedha nyingi kuliko wachezaji wote pia, ila Barca watapata faida kubwa kama wakimuuza kwani mwisho wake kwenye kikosi hiki hautakuwa mzuri kwa timu yake.


Barca wanaweza kupata ada ya uhamisho ya rekodi ya dunia kwa Messi kama wakiamua kumuuza na pia itakuwa maamuzi mazuri, kuna wachezaji wengi na kuna mfumo ambao upo utakaoifanya Barca iendelee kuwa Juu. Klabu inaendelea kubaki na wachezaji wanapita hivyo kama Barcelona wakikubali kumuacha Messi apite watakuwa wamefanya la maana na kujinasua kwenye mtego mkubwa ambao siku si nyingi utaigharimu.

Mwisho!

MACHANGUDOA NCHINI BRAZIL WAANZA KUJIFUNZA KIINGEREZA KWA AJILI YA KOMBE LA DUNIA NA MABARA

Christ the Redeemer
 
 
Machangudoa katika moja ya miji mikubwa nchini Brazil wameanza kujiunga na madarasa yanayotoa elimu ya bure ya lugha ya kiingereza kuelekea kwenye michuano ya kombe la mabara na 2014 World Cup. 

Cida Vieira, raisi wa chama cha machangudoa katika jiji la Belo Horizonte, alisema juzi Jumanne kwamba machangudoa 20 tayari walishajiunga na kozi hiyo na anategemea wengine kama 300 katika kundi la wanachama 4,000 kuwafuata wenzao. 

Chama cha hicho kimeandaa madarasa na sasa wanatafuta waalimu. 

"Sidhani kama tutapata matatizo ya kuwapata waalim wa kiingereza kutoa elimu ya bure," alisema. "Tayari tumeshapata wanasaikolojia na madaktari watakaotoa huduma bure." 

Amesema madarasa yataanza kutoa elimu kuanzia mwezi March na yatadumu kwa muda wa miezi nane. 

"Litakuwa jambo muhimu kwa wasichana ambao wataweza kutumia lugha ya kiingereza ili kuzungumza na wateja wao na kukubaliana bei na vitu vingine." aliongea Cida kupitia simu. 

"Pia kwa sababu hiyo hiyo tutakuwa tunatoa elimu ya lugha ya kifaransa na kiitaliano." aliongeza.

Biashara ya kujiuuza ni halali huko nchini Brazil. 

Uwanja Mineiro uliopo kwenye mji wa Belo Horizonte
unachukua watazamaji 62,000, na utatumika kuchezewa mechi tatu kwenye kombe la mabara na mechi 6 kwenye kombe la dunia.

YANGA KUMALIZA NA EMMEN FC YA UHOLANZI KESHO

Na Baraka Kizuguto-Uturuki.

















Wachezaj wa Young Africans wakifanya mazoezi leo asubuhi kujiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya Emmen FC ya Uholanzi
 
Timu ya Young Africans Sports  Club kesho itashuka dimbani kucheza mchezo wake wa mwisho na watatu (3) dhidi ya  timu ya Emmen FC ya ligi daraja la kwanza nchini Uholanzi  katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika katika viwanja vya Adora football - Berek pembeni kidogo ya mji wa Antlaya.

Young Africans ambayo imeshakaa takribani siku 12 katika mji wa Antalya na kucheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya timu za Armini Bielefeld ya Ujerumani na Denizlispor ya Uturuki leo asubuhi imeendelea na mazoezi katika viwanja vya Fame Residence football mjini Antalya. 
 
Kocha Mkuu wa Young Africans Ernest Brandts amesema atatumia mchezo huo wa mwisho kama fursa pekee kwao kwani mchezo huo utakuwa kipimo kizuri kwao kwani timu ya Emmen FC ni timu nzuri na ndio maana ipo katika ligi daraja la kwanza nchini Uholanzi.
 
Akiongelea mchezo huo wa kesho  Brandts amesema timu ya Emmen FC ni timu nzuri, imekuja Antalya kuweka kambi ya mafunzo kujiandaa na mzunguko wa ligi daraja la kwanza nchini Uholanzi, hivyo ni nafasi nzuri ya kujipima uwezo na timu hiyo ya Uholanzi.
 
Aidha wachezaji Frank Domayo na Kelvin Yondani waliokuwa wameondoka jana jioni kuelekea nchini Ethiopia wameshindwa kuungana na wachezaji wenzao wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars baada ya jana jioni kufika Istambul  kukuta tiketi zao za kwenda Addis Ababa ni za tarehe 09 Februari 2013  hali iliyopelekea kukwama Istambul na kuamua kurejea mjini Antalya kuungana na wachezaji wenzao waliopo kambi.
 
Kikosi cha wachezaji 27 waliopo kambi mjini Antalya kimeendelea na mazoezi ya asubuhi kujiandaa na mchezo huo wa kesho amabao utakua ni mchezo wa mwisho kabla ya timu ya Young Africans kuanza safari ya kurejea nchini Tanzania siku ya jumapili.
 
Young Africans inatarajia kuondoka mjini Antalya siku ya jumapili mchana kupitia Istambul ambapo itaondoka majira ya saa 1 usiku, saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki na inatarajiwa kufika Dar es salaam Tanzania majira ya saa 10 usiku kasoro.



















Jerson Tegete, Omega Seme & Ladislaus Mobgo wakiwa mazoezini leo asubuhi
 

AZAM YAIKUNG'UTA SIMBA KWA PENATI NA KUTINGA FAINALI YA MAPINDUZI CUP TENA


G

RONALDO APIGIGA HAT TRICK HUKU MADRID IKIIFUNGA CELTA VIGO 4-0

GAPCO yadhamini tena Nusu Marathon ya Walemavu



Kwa mara nyingine tena kampuni ya mafuta ya GAPCO Tanzania imetambua umuhimu wa wanariadha wenye ulemavu kwa kuwapa fursa ya kushiriki kwenye mbio za Kilimanjaro Marathon 2013 kwa kudhamini mbio ya nusu marathon kwa ajili ya walemavu itakayojulikana kama GAPCO GAPCO 21km Disabled Half Marathon.
Mkuu wa Mauzo na Maskoko wa GAPCO, Ben Temu amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa “Ushiriki wa wanariadha wenye ulemavu unaleta msisimko mpya kwenye Kilimanjaro Marathon kwa mara nyingine tena. Kukimbia marathon kunaendana na mambo ambayo GAPCO inayaamini katika shughuli zake za kila siku – mtazamo chanya, kipaumbele katika kujiamini na azma ya kusonga mbele”.
“Ushiriki wa walemavu ni ushaidi kwamba watu wenye ulemavu sio tu kwamba wanaweza kufanya mambo makubwa bali pia inadhiirisha kuwa wana uwezo wa kutimiza jukumu lolote kwa ufanisi wa hali ya juu. Kama wadhamini tunahimiza jamii nzima pamoja na makampuni mengine yajitolee kudhamini walemavu waweze kushiriki Kilimanjaro Marathon katika siku zijazo,” alisema.
Mbio za hizo zitakuwa na sehemu tatu ambazo ni kiti cha magurumu (wheelchair), baiskeli ya miguu mitatu, na walemavu wanaokimbia. Washindi watajipatia zawadi nono ambazo jumla yake ni zaidi ya shilingi milioni 3.
GAPCO ina nia thabiti ya kuwasaidia wanariadha walemavu ili waweze kutimiza ndoto zao na kuthibitisha kwamba wanaweza.
Kwa mujibu wa John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waadaaji wa mbio hizo, Kilimanjaro Marathon ni kati yam bio zenye mvuto zaidi duniani kutokana na kwamba zinafanyika chini ya Mlima Kilimanjaro na ndio maana huvutia washiriki kutoka nchi zaidi ya 40 kila mwaka. Mbio hazivutii wanariadha peke yao bali pia watalii ambao huchangia pato la taifa”, alisema.

GARETH BALE AMTAJA RONALDO KUWA MCHEZAJI BORA WA DUNIA ALIYEKAMILIKA - HUKU AKITUPIA HAT TRICK SIKU MOJA BAADA YA KUKOSA BALLON D'OR


sSiku moja baada ya kupotezwa vibaya na Lionel Messi katika tuzo za mchezaji bora wa dunia, Cristiano Ronaldo anaonekana amerudi kiwanjani kuja kuthibitisha uwezo wake kwa vitendo baada ya jana usiku kurudi dimbani na kutupia hat trick katika mechi ya pili ya kombe la mfalme dhidi ya Celta Vigo.

Katika mchezo huo wa jana Madrid walishinda kwa jumla 4-0, Khedira akifunga 1 na Cristiano akitupia matatu, hivyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5-2.

Wakati Ronaldo akitupia hat trick hiyo, mchezaji wa Tottenham Hotspur Gareth Bale aliandika kwenye mtandao wa Twitter kwamba anaamini Cristiano Ronaldo ndio mchezaji bora wa dunia aliyekamilika huku akisema Ronaldinho na Cristiano Ronaldo ndio wachezaji bora kabisa aliowahi kucheza dhidi yao.