Search This Blog

Saturday, October 13, 2012

AZAM YAIKANDAMIZA POLISI MORO - UKUTA WAKE WAKE WAZIDI KUTISHA


Timu ya Azam FC imeendeleza ubabe kwa timu za ligi kuu baada ya kuifunga Polisi Moro 1-0 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Jamhuri, mkoani Morogoro.

Azam FC imepata ushindi huo wa ugenini na kuwa imeshinda michezo minne mfululizo ikifikisha pointi 16, kwa kushinda michezo mitano na kutoka sare mchezo mmoja.

Ushindi wa leo umeipa Azam FC rekodi ya kucheza michezo mitano ya VPL bila wavu wake kutikiswa huku golikipa Mwadini Alli akiweka kwenye vitabu vya kumbukumbu rekodi ya kusimama langoni mechi nne bila kuruhusu goli.


Katika mchezo huo timu zote zilicheza kwa hari ya kutafuta ushindi, Azam FC wakitengeneza nafasi nyingi.

Kipindi cha kwanza dk 5 mshambuliaji John Bocco alijaribu kutaka kufunga lakini akashindwa kumalizia krosi ya Salum Abubakar 'Sure Boy' na kupiga mpira uliotoka nje.

Pia kipindi hicho Kipre Tchetche alipiga mpra wa kichwa uliotoka nje dk 7, dk 16 na 28 Bocco naye alipiga mipira iliyotoka nje akiwa amebaki yeye na golikipa wa Polisi Moro..

Japokuwa uwanja haukua katika kiwango kizuri, kipindi cha pili timu zote ziliingia kwa kasi kila moja ikihitaji ushindi.

Dk 63 Kipre Tchetche aliifungia Azam FC bao la kwanza na pekee katika mchezo huo akitumia vema uzembe wa kipa wa Polisi Moro Manzi Manzi aliyepangua shuti la Bocco na kuanza kuuchezea mpira ndipo Kipre alipouchukua na kupiga shuti lililotinga moja kwa moja wavuni.

Goli hilo lilidumu hadi mpira ulipomalizika, Polisi watajutia nafasi walizopata dk 18 Faustine Lukoo na dk 72 Iman Mapunda walipiga mipira iliyookolewa na kipa Mwadini Ally wa Azam FC, huku dk 90 Malimi Basungu alianguka mwenyewe golini na kushindwa kufunga.

Mabadiliko Azam FC walitoka Himid Mao dk 78, Abdulhalim Humud dk 84 na Kipre Tchetche dk 89 baada ya kufanya kazi nzuri, nafasi zao zikachukuliwa na Michael Bolou, Abdi Kassim na Gaudence Mwaikimba.

Kocha wa Azam FC, Boris Bunjak 'Boca' amefurahishwa na ushindi huo na kuahidi kuendeleza ushindi huo katika mechi zijazo.

LIVE MATCH CENTRE: COASTAL UNION 0 - 0 SIMBA FULL TIME



DK: Mpira unamalizika hapa uwanja wa Mkwakwani kwa matokeo ya sare tasa.

DK 85: Simba  0 - 0 Coastal

DK 78: Atupele Green anakosa bao la wazi 

DK 75: Coastal wanafanya mabadiliko anaingia Danny lyanga anatoka Soud.

DK 68: Simba wanafanya mabadiliko anatoka Daniel Akuffoer anaingia Salim Kinje.

DK 65: Nsa Job anapewa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi ya pili ya njano.

DK 63: Nsa Job anapiga shuti kali linaokolewa kwa ustadi mkubwa na Juma Kaseja.

DK 60: Mwamuzi anawapa kadi za njano Nsa Job na Amir Maftah.

DK 55: Coastal wanakosa bao la wazi huku Simba wakifanya mabadiliko anatoka kinda Haruni Chanongo anaingia Uhuru Suleimani.

DK 47: Anaingia Lameck Dayton kuchukua nafasi ya Razack Khalfan aliyeumia.

DK 46: Kipindi cha pili kinaanza na ghafla Razack Khalfan anakaa chini akionekana kuwa na maumivu, machela zinambeba na kumtoa nje ya uwanja kwa jinsi inavyoonekana sidhani kama atarudi dimbani.

Mpira ni mapumziko hapa Mkwakwani Simba 0 - 0 Coastal.

DK 45: Coastal wanaendelea kuishika nafasi ya kiungo kwa sababu Selembe, Razack na Santo wanaelewana sana pia udhaifu wa Boban katika kukata unawapa wakati mgumu Kiemba na Kazimoto katika kuweza kumiliki dimba.

DK 40: Nsa Job anakosa bao la wazi bada ya kazi nzuri iliyofanywa na Selemani Kassim.

DK 35: Timu zote zinafanikiwa kufika kwenye lango la wapinzani lakini wanashindwa kuzitumia nafasi zao vizuri.

DK 30: Coastal 0 - Simba

DK 26: Simba wanapata kona yao ya kwanza lakini haizai matunda.

DK 25: Coastal wanaonekana kutawala sehemu ya kati ya kiungo inayochezwa na Jerry Santo na Razack Khalfan.

DK 20: Coastal 0 - 0 Simba

DK 15: Kichwa kizuri cha Felix Sunzu kinatoka nje.


DK 13: Haroun Chanongwa anapiga bonge la shuti linagonga mtambaa wa panya kipa wa Coastal Chove anashindwa kuzuia.


DK 10: Simba 0 - 0 Coastal


DK 9: Coastal wanafanya shambulizi la kushtukiza na mpira unatoka juu ya lango.


DK 1: Mpira unaanza hapa mkwakwani - Simba wamevaa jezi nyeupe na bukta nyekundu, Coastal wamevaa jezi nyekundu juu nyeupe chini.

KICK OFF : 10:00 - Coastal Union vs Simba SC 

Razack Yusuph Cereca, Shaffih Dauda, Shabiki na Pius Kisambale

Viongozi wa Coastal Union Mwenyekti Aurora na Nassoro Binslum

Dauda, Swedi Nkwabi na Binslum tukiwa tumepozi nje ya uwanja wa Mkwakwani Tanga tukisubiri mechi.



SIMBA NAO WATANGAZA KIKOSI KITAKACHOANZA DHIDI YA COASTAL UNION - NGASSA NA OKWI NJE

Kocha wa Simba Milovan Cirkovic ametangaza kikosi cha Simba kitakachoanza leo huku majina kama Mrisho Ngassa, Emmanue Okwi na Edo Christopher yakiwa hayamo.

Katika kikosi cha leo kinda Haruni Chanongo amepewa nafasi ya kuanza kwenye safu ya ushambuliaji sambamba na Felix Sunzu na Haruna Moshi.

Kiosi kamili

1: Juma Kaseja 

2. Said Chollo

3: Amir Maftah

4: Pascal Ochieng

5: Shomari Kapombe

6: Amri Kiemba

7: Mwinyi Kazimoto

8: Boban

9: Akuffor

10: Felix Sunzu

11: Harun Chanongo

Sub - Mweta, Paul Ngalema, Juma Nyosso, Jonas Mkude, Uhuru Suleiman, Edo Christopher.

PREVIEW: COASTAL UNION VS SIMBA - HIKI NDIO KIKOSI CHA COASTAL KILICHOTANGAZWA KWA AJILI YA KUMUUA MNYAMA

Coastal Union Fc Vs Simba Sc
Hakika ndio Habari ya iliopo Mjini kwa sasa. Mechi hii inayochezwa leo Jijini Tanga katika Uwanja wa Mkwakwani imeteka hisia kubwa za watu kwasababu Coastal union imepania mchezo huu kwa kutaka kuvunja rekodi ya Simba ambayo haijafungwa mchezo wowote mpaka sasa.


Timu zote 2 zimecheza michezo 6 huku Coastal ikiwa imejikusanyia points 9 nafasi ya 6 na Simba points 16 nafasi ya 1.
Mpaka sasa nimefanikiwa kupata kikosi cha kitachoanza cha timu ya Coastal na kipo kama ifuatavyo.

1.Chove (Gk)
2.Said Sued (C)
3.Juma Jabu
4.Jamali Macherenga
5.Kibacha
6.Jerry Santo
7.Soud
8.Razak Khalfan
9.Nsa job
10.Atupele Green
11.Kassim Salembe

Reserve:
1.Rajabu kaumbu (Gk)
2.Ismail suma
3.Abdul Banda
4.Lamelk
5.Mahundi
6.Aziz gilla
7.Daniel lyanga

Team coach
Hemed Morocco

WAYNE ROONEY NA WELBECK WAPIGA MBILI MBILI ENGLAND IKIICHINJA SAN MARINO 5-0


СМ - А footyroom.com by footyroom

RADAMEL FALCAO AZIDI KUTISHA - ATUPIA BAO MBILI COLOMBIA IKIIFUNGA PARAGUAY

UJERUMANI YAIPIGA 6-1 JAMHURI YA IRELAND


ger 6-1 by Futbol2101

PEDRO AIPIGA HAT TRICK SPAIN WAKIUA BELARUS 4-0 NYUMBANI KWAO


szólj hozzá: Belarus vs Spain 0:4 GOALS HIGHLIGHTS

HUNTELAAR NA VAN DER VAART WAIPA USHINDI MWEPESI UHOLANZI DHIDI YA ANDORRA


n3-0a by Futbol2101

WARUSI WAKANDAMIZA KIDUDE URENO NA RONALDO AKIWA NDANI


Russia 1-0 Portugal footyroom.com by Futbol2101

Friday, October 12, 2012

CRISTIANO RONALDO ALIKATALIWA KUSAJILIWA BURE NA OLYMPIQUE LYON

Olympique Lyon ingeweza kumsajili nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo kwa bei sawa na bure, imefahamika. 

Kocha wa wakati huo wa Sporting Lisbon, Laszlo Boloni alitaka kumsajili Tony Vairelles kutoka Lyon kwa kubadilishana na wachezaji wawili akiwamo Ronaldo. 


"Sporting de Portugal hawakuwa na pesa hivyo walipendekeza kubadilishana wachezaji na walikuwa tayari kuwatoa wachezaji wawili, mmoja wao akiwa ni Cristiano Ronaldo, lakini Lyon walikataa ...," alisema Boloni. 


Muda mfupi baadaye Ronaldo akasajiliwa na Manchester United na yaliyobaki yakawa historia.

BAJETI FINYU KATIKA USAJILI NDIO CHANZO CHA KUBORONGA LIGI KUU - JOHN SIMKOKO



Wakati akiwa kocha wa timu ya Mtibwa Sugar katika miaka ya mwishoni ya 90 na mwanzoni mwa miaka ya 2000, John Simkoko, alidhihirisha ubora wake wa ufundishaji kwa kuita mataji mawili ya ligi kuu timu ya Mtibwa katika miaka ya 1999 na 2000, akifanya kazi kama kocha mzalendo.

 Ni miaka 12 sasa tangu apate mafanikio hayo na sasa ana haha kuipatia ushindi wa kwanza katika ligi kuu timu yake ya Polisi Moro.
 Katika michezo sita waliyocheza timu hiyo imefungwa mara nne na kuambulia sare mbili. Kazi inayomkabili Simkoko ni ngumu na inayohitaji busara zaidi za kimpira kama ngazi ya kuhakikisha mambo yanaenda sawa. Lengo la kwanza kubwa ni kuhakikisha timu hiyo inafunga mabao, kwani wamefunga bao moja tu katika dakika 530 ambazo tayari wamezitumia uwanjani/ Mwandishi Baraka Mbolembole alifanya mahojiano mafupi na kocha huyo kuelekea mchezo wao dhidi ya Azam FC hapo kesho, jumamosi katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro… Shuka nayo katika www.shaffihdauda.com


SWALI. Unaizungumziaje ligi kuu ambayo inaendelea?


SIMKOKO; Ligi ina ushindani sana msimu huu, unajua kwenye mpira wa sasa namna mnavyojiandaa ndivyo mnavyoweza kupata matokeo.




SWALI. Unaikabili Azam katika mchezo wa raundi ya saba dhidi ya Azam wikiendi hii, vipi kuhusu hali ya kikosi chako?


SIMKOKO; Kuna majeraha madogo madogo lakini si yale ambayo yanaweza kusababisha wasicheze, kiujumla tunaendelea vizuri.




SWALI. Timu yako imekuwa na uwezo mdogo wa kufunga mabao, tatizo ni nini na umeshughulika nalo vipi?

 

SIMKOKO; . Ni kweli hatufungi mabao na ni kitu ambacho kinamchanganya kila mmoja kikosini. Unajua jukumu la kufunga ni la timu nzima na wakati tukitakiwa kufunga inatakiwa pia tuwe na uwezo mzuri wa kuzuia kwani ni jumuku la timu nzima kuhakikisha tunafunga mabao na kutoruhusu kufungwa pia. Kama kocha nimekuwa nikishughulika na tatizo hilo hata kabla ya ligi kuanza. Ni sehemu ya programu yangu na wachezaji nimekuwa nikiwaelekeza yale yaliyo bora.

SWALI. Unaikabili, Azam FC, jumamosi hii unauzumziaje mchezo huo?
SIMKOKO; Itakuwa mechi ngumu, lakini tutapigana kuhakikisha tunashinda. Ligi ni kama mashindano ya mita mia moja katika riadha. Kila timu inajitahidi kushinda, lakini mwisho wa siku ni timu moja tu inayotwaa ubingwa.

SWALI. Kwa hali jinsi ilivyo kwa kikosi chako katika mwenendo wa ligi, je unafikiri ipi itakuwa nafasi bora kwa kikosi chako mwishoni mwa msimu?
SIMKOKO; Lengo letu kwanza ni kukusanya pointi za kutosha, kama tukibahatika kuingia top 3 sawa, lakini muhimu kwanza ni kukusanya pointi za kutosha ili tuwe salama na tuweze kubaki ligi kuu

SWALI; Unadhani tatizo kubwa la timu yako linasababishwa na nini?
SIMKOKO; Bajeti yetu ndogo wakati wa usajili ndiyo inayotugharimu sasa, timu ilihitaji wachezaji bora zaidi kwa ajili ya ligi kuu mara baada ya kupanda, na katika soka la sasa inatakiwa kuwa nguvu katika soko la usajili ili uweze kuwapata wachezaji mahiri. Nadhani tatizo lilianzia katika bajeti yetu ya usajili.

SWALI; Unazungumziaje suala la uchezeshaji kwa waamuzi wa ligi kuu hasdi sasa?
SIMKOKO; Mimi si mtu ambaye napenda kuwazungumzia waamuzi, kuna wapenzi, mashabiki, wachambuzi na watu wengine ambao wanaweza kuwazungumzia. Mimi kazi yangu ni kufundisha tu vijana wangu na sipendi kuingia katika mijadala kuhusu uchezeshaji wao.

SWALI; Unawaambiaje sasa wapenzi wa timu yako na wamekuwa wakitoa sapoti gani kwa timu yako baada ya matokeo mabaya?
SIMKOKO; Wasikate tamaa, watambue ni sehemu ya mchezo hata sisi hatupendi kufungwa na inatuuma kuona tukipata matokeo mabaya, lakini ndiyo matokeo ya mpira yalivyo, tunajitahidi kurekebisha sehemu zenye matatizo na nadhani kutakuwa na mabadiliko katika michezo ijayo… Tuna furahi kuona wakija uwanjani kutazama vijana wao ni lazima watambue umuhimu wa wao kuja kwa wingi uwanjani na kutoa sapoti ya nguvu ili vijana watambue kuwa kuna watu wengi wanawawakilisha ndani ya mkoa wao.

HIMID MAO: AZAM TUPO VIZURI KILA IDARA - SURE BOY NDIO KIUNGO BORA KABISA KWA SASA TANZANIA


Kuwasili kwa Boris Bunjuk kama kocha mkuu wa timu ya Azam FC, ni wazi kuwa wachezaji fulani watanufaika na wengine wataathiriwa na mabadiliko hayo. Azam inaonekana kucheza katika lugha moja na hata kimpira hawatofautiani sana kiuchezaji. Himid Mao Mkami kiungo chipukizi wa timu hiyo na mtoto wa mchezaji wa zamani, wa Taifa Star, Mao Mkami. Katika uchezaji wake, Himid amejitambulisha kama kiungo mwenye nguvu, wakati Baba yake alitamba zaidi akiwa na timu za Pamba ya Mwanza na Reli ya Morogoro na kujitambulisha kama 'ball dancer' mbele ya mashabiki wa soka nchi, kwa Himid ni tofauti kabisa yeye ana miaka mitano ndani ya Azam FC na anataka kuwa shujaa wa klabu yake.



SWALI; Tuzungumzie mambo ya ufundi na mbinu, unadhani nini siri ya ninyi kuwa na ukuta mgumu kwa msimu wa pili sasa, unadhani mabeki wenu ni bora zaidi nchini au kuna cha ziada ambacho kinawafanya muwe imara, kipi hicho?

HIMID; Kwanza kabisa timu yetu ni nzuri sana kuanzia mbele katikati na nyuma, pia tuna mabeki na kipa mzuri lakin siri ya kuwa na ukuta mgumu ni wachezaj wote kujitolea 100% tunapokuwa uwanjani.

 SWALI; Ninapoitazama Azam kiujumla inaonekana ni timu iliyokamilika hasa na yenye wachezaji mahiri, pamoja na ubora wenu unadhani nini ni udhaifu wenu na kipi ambacho ungependa kuwaambia wenzako kuhusu hilo la udhaifu ili mpate kuwa na matokeo bora zaidi katika ligi na michuano ya kimataifa?



HIMID; Kweli timu yetu ipo vizuri kila idara, sidhan kama kuna mapungufu sehemu yeyote kwakuwa hatujapoteza mchezo wowote hadi sasa, nafikiri tunatakiwa kupata magoli mengi zaidi ili tujiweke katika mazingira mazuri katika ligi na mashindano ya kimataifa
.

 SWALI; Unamzungumziaje kocha, Boris mbinu zake na malengo ya klabu vinaendana?

Coach ni mzuri pia Ana mbinu nzuri za ushindi ndiyo maana tuna matokeo mazuri kwa ligi

 SWALI; Ipi silaha yako uwapo uwanjani?

HIMID; Silaha yangu ni uwezo mkubwa wa kukaba.

SWALI; Kiungo gani bora ambaye umewahi kucheza naye timu moja?

HIMID; Kiungo bora kuwahi kucheza nae ni Sureboy, ana kipaji cha hali ya juu,

SWALI; Umesema silaha yako kubwa ni uwezo wa kukaba, unadhani nini unahitaji kuongeza katika mchezo wako ili uwe bora zaidi?


HIMID; Nafikiri ni mazoez ndio nahitaji kuongeza ili niwe bora zaidi

 SWALI; Sifa tano ambazo zinakufanya uwe katika kikosi cha kwanza cha Azam?

HIMID; 1. Uvumilivu,

2 kujituma,
3. Kushirikiana vizuri na wenzangu,
4. Kufuata maelekezo ya kocha,
5. Support kutoka kwa Mungu, wazazi, familia yangu na rafiki zangu

 SWALI; Polisi Moro ambayo mnacheza nayo jumamosi hii, haijashinda mchezo wowote kati ya mitano iliyocheza, unafikiria itakuwa mechi ya aina gani kwani wewe unaijua vizuri Polisi?

HIMID; Mechi itakua ngumu sana, tumejiandaa vya kutosha nafikiri tutapata matokeo mazuri


SWALI; Kwa msimu huu umeshacheza michezo mingapi na umetengeneza ama kufunga mabao mara ngapi?



HIMID; Nimecheza mechi 6, sijafunga mara nyingi nakua nyuma kwa ajili ya kuanzisha mashambulizi.
 

Swali:  Unazungumziaje mwenendo wa timu nne za juu katika ligi, ni nini taswira ya ligi uionavyo hadi kufikia raundi ya kumi?


HIMID; Ushindani ni mkubwa sana kwa timu nne za juu, lakin naweza kusema ni kwa timu zote, ligi inazidi kuwa ngumu na ikifika round ya kumi ndio itazidi kuwa ngumu na ushindani utaongezeka


 SWALI; Kipi kikosi bora ambacho umewahi kukichezea, ukiwa Azam au timu ya Taifa?

HIMID; Vikosi vyote vilikua bora........


SWALI; Nini mtazamo wako kuhusiana na soka la Tanzania?

HIMID; Soka la Tanzania liko vizuri, sema inahitajika jitihada za makusudi ili kuliinua zaidi

SIMBA DHIDI YA COASTAL KESHO MKWAKWANI - AZAM WATAKA MECHI ZAO DHIDI YA YANGA NA SIMBA ZICHEZWE CHAMAZI

Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea kesho (Oktoba 13 mwaka huu) kwa timu kumi kupambana kwenye viwanja vitano tofauti katika raundi ya saba ya ligi hiyo yenye timu 14.
 
Polisi Morogoro itaikaribisha Azam kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati mwamuzi wa FIFA, Oden Mbaga atakuwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya kuchezesha mechi kati ya wenyeji Tanzania Prisons na Oljoro JKT.
 
Jijini Tanga, Simba itakuwa mgeni wa Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Simon Mberwa kutoka Pwani akisaidiwa na Godfrey Kihwili na Abdallah Uhako wote kutoka Arusha.
 
Mechi nyingine za kesho ni Ruvu Shooting dhidi ya African Lyon kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi, na Mtibwa Sugar watacheza na Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
 
Wakati huo huo, Azam imeomba mechi zake za nyumbani dhidi ya Yanga na Simba zichezwe kwenye uwanja wake wa Azam Complex ulioko Chamazi badala ya Uwanja wa Taifa.
 
Nayo Ruvu Shooting imeomba mechi yake ya ugenini dhidi ya Yanga ya Oktoba 20 mwaka huu ichezwe Uwanja wa Taifa badala ya Uwanja wa Azam Complex.
 
Maombi hayo yatawasilishwa kwenye kikao cha Kamati ya Ligi ya TFF kinachotarajiwa kufanyika kesho (Oktoba 13 mwaka huu) kwa ajili ya kufanyiwa uamuzi.

PICHA YA LEO!

mkuu wa wilaya ya kibondo mkoani kigoma  mh.  Venance Mwamoto akionyesha vitu vyake wakati wa fainali za michuano ya polisi jamii hivi karibuni (picha na james jovin)

UAMUZI WA KUMUONDOA AKRAMA KUCHEZESHA LIGI KUU UMETOKANA NA UTASHI WA KISIASA NA VIONGOZI WASIOJUA SHERIA


Siku kadhaa zilizopita shirikisho la soka nchini kupitia kamati yake ya ligi iliamua kumfungia mwamuzi mzoefu Mathew Akrama wa Mwanza aliyechezesha mechi namba 80 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Simba iliyochezwa Oktoba 3 mwaka huu kwa madai ya kushindwa kuumudu mchezo huo wa watani jadi.
Kufungiwa kwa Akrama kulikuja baada ya kelele zilizopigwa na vilabu vyote viwili pamoja wapenzi wake kwamba mwamuzi huyo hakuchezesha kwa haki mchezo huo hivyo kuuharibu kabisa kabisa mchezo wa kulwa na doto. 
Sawa kwa amono yetu wapezni wa soka tunaona Akrama weli aliboronga mchezo huo lakini kufungiwa kwake kumekufanyika kwa utashi wa kisiasa kabisa kwa sababu ya usimba na uyanga uliojaa kwenye soka letu.
Kisheria kamati ya ligi haikupaswa kukaa kujadili suala la Mathew Akram kwa sababu hata FIFA inashauri na kuagiza masula yote ya waamuzi na vyama vyao vyeme wataalam wa sheria za soka, sidhani kama kwenye kamati ya ligi yumo mtalaamu yoyote wa sheria. 

Kama hayupo hii ni hatari hatari sana. FIFA inazuia watu wenye maslahi na vilabu kushughulika na masuala yoyote yanayohusu waamuzi  kuanzia kupanga ratiba ya waamuzi mpaka kuwatolea maamuzi kama hili likiachwa likaendelea ni hatari katika maslahi ya mpira wetu kwa sababu waamuzi watachezesha kwa woga na kufikiria katika kamati kuna nani. 
Mwamuzi anafundishwa siyo kufungiwa au kuondolewa. Akikosea anaelekezwa makosa yake anapewa mchezo mwingine ili kuona maendeleo yake na kama amerekebisha aliyoelekezwa.
Ndio maana hata kwenye ligi zilizoendelea kama Uingereza marefa wakubwa kama akina Howard Webb muda mwingine wanaboronga sana lakini ni mara ngapi tumewahi kusikia wamefungiwa au wameondolewa kuchezesha ligi.
Kwanini? Kwa sababu inachukua Inachukua takribani miaka kama 6 - 10 kumpata mwamuzi kama Akrama. Sasa wapo wangapi walioandaliwa kama yeye? Hivyo badala ya kumuelekeza vizuri Akrama, refa ambaye ana uzoefu tunaanza kuchukua marefa wachanga na mwishowe suala la kufungia waamuzi halitoisha kwa sababu akikosea tu kwenye mechi ya watani atafungiwa na kuletwa mwingine.
Vilevile inashauriwa kwamba katika mechi kubwa kama ya Simba na Yanga makamisaa wanatakiwa kuwa marefa waastaafu wenye uzoefu, sasa je katika mechi ya Simba na Yanga alikuwa mtu wa aina hiyo? au alikuwepo tu mtu ambaye nae alikuwa tu ni refa wa kawaida?
Mwisho viongozi wa soka Tanzania tuache kuuongoza mchezo huu kwa utashi wa kisiasa kwani hatotufanikiwa - kila kitu kiende vile ambavyo kimepangwa na sio kufanya maamuzi kwa mazoea.

Nawasilisha

GOLI LA SIKU : DENILSON AMUONYESHA WENGER MAMBO ANAYOYAKOSA KUTOKA KWAKE

DEL PIERO HII NDIO SABABU KWANINI NILIKATAA KUJIUNGA NA LIVERPOOL

Alessandro Del Piero amekiri kwamba alikataa nafasi ya kujiunga na Liverpool kwasababu ya kumbukumbu ya tukio la janga la Heysel.

Mashabiki wapatao 39 wa Juventus walifariki dunia katika tukio la Heysel mwaka 1985 katika mechi kati ya Juventus na Liverpol, na mshambuliaji huyo wa zamani wa Italy anaaminikuhamia kwenye timu hiyo ya EPL kusingeleta picha nzuri kwa washabiki wa timu yake pendwa Juventus.

“Mazungumzo na Sydney yalikuwa yameshaanza wakati Liverpool walipokuja kunihitaji, na hapo nikafikiria kilichotokea kule Heysel," aliliambia La Gazzetta dello Sport.

“Juventus na Liverpool wameweza kutengeneza mahusiano yao, lakini tukio lile la Heysel daima litakuwepo kwenye kumbukumbu za watu wengi."

Del Piero pia alizungumzia namna alivyosikitika kuondoka katika klabu ya Juventus, lakini akawasifu mashabiki wa timu hiyo kwa jinsi walivyomuaga .

“Sikuwahi kufikiria kama naweza kuja kuondoka Juventus namna hii. Sikufikiria hili miezi 18 iliyopita, japokuwa mambo yanabadilika.
“Naondoka huku nikiwa na fikra za kutosheka  , ingawa, nikiwa najua kwamba nilijitoa kwa kila kitu kwa ajili ya Juventus.
"Mashabiki walinifanya nisijkie fahari sana, siku zote nilikuwa najua wananipenda lakini sikuwahi kufikiria ningekuwa maarufu hivi kwao, Gig Buffon aliwahi kuniambia ananionea wivu."

Thursday, October 11, 2012

AFRICAN LYON WAUWASHA UPYA MOTO DHIDI YA TFF!



We would first like to thank the following entities for their tremendous support during these difficult times.

1.      Club Owners Association of the Premier League Clubs (All 14 Teams). The clubs have shown maturity and unity in this issue, something that has never happened before. Due to new leadership of various clubs we are very confident as we move forward, the future will be bright. Despite Vodacom’s refusal to comply with our request and TFF’s conduct, clubs have shown their willingness to fight together and put the interest of the league first.

2.      Media Outlets and Sports Analysts.  The media has done a thorough job in asking the difficult questions and more important doing their homework to clearly show that a lot of statements made by TFF are simply not true. This was not done on our behalf but on the behalf of the readers and listeners.

3.      You, the soccer fan. We thank you because your support in this shows the true passion and level of understanding Tanzanians have with regards to what is required to move this country to the next level of soccer development. You have recognized what it takes to bring about positive change in our sport and you have been heard.

4.      Our current sponsor, Zantel for showing true commitment to the development of soccer in Tanzania by maintaining their 100% sponsorship commitment to our youth development program despite the obstacles we have faced in honoring our side of the contract.

5.      African Lyon Fan, Management and Supporters. We are thankful to those very close to us who have supported us and given us the necessary courage to fight for what we still believe is right. Their wisdom and advice prevented a more tragic turn of events.

There have been efforts over the last few weeks to push under the rug the “exclusivity” debacle that erupted just prior to the start of the league.  We are here in front of you to put things straight because thus far, the method in which things have been handled has portrayed a very negative image of African Lyon’s management. The primary objective of this press conference is to clear our name. It is very worrisome when the body that has been tasked to develop this beautiful sport has placed the blame on a small club like African Lyon when in essence the problem was a direct result of their action or lack of action. If we do not resolve this issue now, it is more than likely to become a problem again in the future and may involve larger clubs who will put up an even stronger fight.

The following are FACTS and we would like TFF to dispute them otherwise
1.      The contract between TFF and Vodacom was signed on August 11th 2012, just 4 days before the start of the league.
2.      Clubs were not aware that the contract had been signed by TFF at the start of the league.
3.      Clubs had insisted that the contract should also be signed by at least three members of club owners, this did not occur.
4.      It is NOT true as stated by the President of TFF, when supporting Vodacom’s  “exclusivity” clause, that the clubs requesting an end to this clause is unprecedented. We have discovered the contrary – for example, in Ghana, the Ghana Premier League is currently sponsored by Glo Mobile Ghana with one of the teams in the league – Asante Kotoko, sponsored by MTN Ghana.  This is to name a few.
5.      Vodacom will not compensate African Lyon for denying them a potential sponsor due to her clause
6.      TFF will not compensate African Lyon for accepting the clause at the last minute prior to the league resuming.
7.      Access to the contract for clubs to understand the clauses and issues involved is limited to going to TFF office and looking at the contract there.
8.      Not one club knows the entire context of the contract, of which TFF claims has been signed and endorsed by club owners.
9.      The new contract that was recently signed still allows Vodacom until the last hour to exercise their First Right Of Refusal which clearly puts all club owners at a disadvantage with regards to getting new club sponsors.
10.  The sponsorship package being offered by Vodacom is not sufficient for any premier league club.

African Lyon cannot challenge Vodacom because the contract was between them and TFF. However, legally we have a very strong case against TFF.  We ask the following questions to TFF.

1.      Did you expect clubs to put all their efforts to secure sponsorship on hold until you signed a contract with Vodacom, which would have been just 4 days before the league starts? 

2.      Would you actually relegate African Lyon if we fail to make it to Kagera, Mbeya due to lack of funds?

Instead of TFF making a case to the public that they unsuccessfully worked with clubs to try and remove the “exclusivity” clause, they are the ones making a case on behalf of Vodacom’s marketing department that the “exclusivity” clause should have been there. Why would you fight Vodacom’s battle with the public who clearly feel that the “clause” hurts the development of this game?



African Lyon is demanding the following from TFF;

1.      TFF should accept responsibility for this fiasco due to the ill-timed manner that the contract was signed.
2.      TFF should come forward and acknowledge to the public that they could have handled the entire contract renewal process better.
3.      TFF should contact Zantel to thank them for NOT withdrawing their commitment to sponsor African Lyon.

African Lyon’s management made contact with various government organs and respectable individuals to inform and invite them to the unveiling of our sponsorship. We owe these people a better explanation than what has been provided to them.

Our primary focus is on youth development and the success of our various programs, which will eventually benefit TFF, relies on help from potential sponsors like Zantel. Thus, it is very important we move forward from this and that the ownership of the problems does not fall on the clubs.

It is clear that Zantel’s commitment to youth development will help members beyond African Lyon. TFF will be a major beneficiary of this cause, as the kids involved will eventually play on the national team and in higher leagues, furthering the level of excellence of Tanzanian football.

FULL TIME: TOTO 1:3 YANGA



Leo kuna Mchezo mmoja wa ligi kuu ya VODACOM Tanzania Bara, mchezo huo unapigwa kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza kati ya Toto Africans na Yanga.
Blog yako inakupatia baadhi ya matukio live ya mchezo huo.

Dk 36: yanga inaongoza kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na mshambuliaji Didier Kavumbagu pamoja na beki Mbuyu Twite.

Dk : 40 Toto wanakosa bao baada ya shuti kali kupaa kidogo juu ya lango.

Dk : 42 Toto wanapata penalti

Dk : 43 Toto wanakosa penalti,Emanuel Swita amepiga nje kulia mwa golikipa Yew Berko

Dk : 45  zimeongezwa dk 2 za nyongeza.

MPIRA NI MAPUMZIKO

TOTO 0:2 YANGA.

Kipindi cha pili kimeanza.

Dk 46: yanga walipata kona iliyopigwa na Haruna Niyonzima lakini haikuzaa matunda.

Dk 50: Toto wanafanya mabadiliko anaingia Mohamed Chingo badala ya  Haruna Athumani

Dk 52: Toto wamepata kona wakaipoteza,\

Dk 54: gooooooooooooooooooooooooooooooooo! Toto Africans wanapata bao,Mussa Said ndiye aliyeifungia Toto bao baada ya mabeki wa Yanga kushindwa kuelewana.

Dk 61: Toto wamekosa bao la wazi,lilipigwa shuti na kiungo Emanuel Swita golikipa wa Yew Berko akapangua mshambuliaji Mussa akapiga nje goli likiwa wazi.

Dk 64 : Yanga wanafanya mabadiliko,viungo Athuman Idd na Frank Domayo wametoka na nafasi zao zimechuliwa na Shamte Ally na David Luhende.

Dk 68: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO! Jerry Tegete anaipatia YANGA bao la 3, pasi nzuri toka Didier Kavumbagu jerry Tegete akauwahi mpira kwenye eneo la mita 18 akampiga kipa chenga na kupasia nyavu, Hili ni bao la kwanza la msimu la Tegete.

Dk 85: Emanuel Swita wa Toto anapewa kadi ya njano, Swita pia aliwahi kuichezea Yanga kwa msimu mmoja kabla ya kurejea Toto Africans.

FT: TOTO 1:3 YANGA

MIAKA 75 BAADA YA GWIJI LA MANCHESTER UNITED BOBBY CHARLTON KUZALIWA - MFUNGAJI BORA WA MUDA WOTE WA MASHETANI WEKUNDU

Siku kama ya leo miaka 75 iliyopita alizaliwa kiungo mshambuliajimstaafu wa Manchester United na timu ya taifa ya England Sir Bobby Chalton.

Sir Bobby ambaye kwa sasa ni mwanachama wa bodi ya wakurugenzi wa Manchester United ni mmoja kati ya wachezaji wachache walioichezea United mechi nyingi na kufunga mabao mengi, anashika nafasi ya pili nyuma ya Ryan Giggs kwa kucheza mechi nyingi, akiitumikia United katika mechi 758 na kuweza kuifungia mabao 249, akiwa anaongoza katika listi ya wafungaji bora wa muda wote wa klabu ya Manchester United.





Bobby Charlton ni mmoja kati ya wachezaji wanne wa Red Devils ambao wameshawahi kushinda tuzo ya uchezaji bora wa dunia - wa kwanza alikuwa Dennis Law 1964,  akafuatia Charlton 1966, George Best mwaka 1968 na mwaka 2008 Cristiano Ronaldo.
Charlton akiwa na Fergie mwaka 2011

Charlton pia ndio mfungaji bora wa muda wote wa England akiwa ametupia mabao 49 katika mechi 106.

Charlton alikuwa mmoja wa wachezaji waliopata ajali ya ndege wakati United jijini Munich.

Pia siku kama ya leo mwaka mmoja uliopita Shaffih Dauda nilibahatika kupata mtoto wangu wa pili aitwaye Dauda Jr aka Solskjaer ambaye anashea siku moja ya kuzaliwa na mke wangu pia.


Happy Birthday Legend, Happy birthday Wife, Happy Birthday Dauda Jr Solskjaer.


  HII NDIO MAKALA YA VIDEO INAYOELEZEA MAISHA YAKE YA SOKA KIUJUMLA

GIDABUDAY: WAZIRI USIPOTEZE FEDHA ZA UMMA KUUNDA TUME KWA MADAI AMBAYO USHAHIDI WAKE UPO WAZI

Siku chache baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba waziri wa michezo na utamaduni ataunda tume ya kuchunguza TOC, mwanaharakati na mkimbiaji Willlheim Gidabudayi ameibuka na kumuomba waziri asijaribu kuunda tume hiyo kabla kupitia ripoti ya Olimiki kutoka kwa vyama vvya michezo husika kabla ya kuunda tume huru ya kuchunguza TOC kufuatia madai ya ufisadi ambao wadau kama akina Gidabudayi wumetoa sambamba na ushahidi unaoridhisha kama ambavyo ameandika hapo chini:

1). Ni kwa nini waziri asiunde tume ya kuchunguza madai ya DOLA ZA INDIA?, au wizarani pia waliitafuna dola hizo za India?. Dola 100,000 ni takriban TSH: 160,000,000/= ni ajabu sana serikali kudhani kwamba si lolote la kuchunguzwa!!.

2). Pia ni kwa nini hadi leo waziri hajawahoji TOC kuhusu matumizi ya USD 100,000 sawa na TSH: 160,000/= ambazo TOC walidai kuzitumia kwa maandalizi ya kwenda London. TOC walitoa matumizi yao kwa vyombo vya habari lakini matumizi yale yalijaa uongo ambao sisi wadau tunayo ushahidi. Je waziri anadai vipi ripoti ya Olimpiki kabla ya kuchunguza ufisadi ndani ya TOC na baadhi ya maofisa wakubwa wa wizara yake?.

3). Je ni kwa nini hadi leo waziri hajaagiza kupatiwa idadi kamili ya
  fedha zilizotolewa na Olympic Solidarity yaani "quadrennial financial aid" kuanzia 2009 hadi 2012?. Sisi wadau tumeonyesha kutoridhika na kiasi kikubwa kutumiwa na vigogo wa TOC kujinufaisha wenyewe kwa kujijengea mahekalu kana kwamba "wataishi milele".

4). Je watanzania wanafahamu kwamba (Olympic Solidarity inadai kwamba ndio wamelipia gharama za safari ya timu kwenda London!!, pia eti serikali pia ndo waliolipia safari za kwenda London!!). Je watu wenye akili timamu hawapati picha na harufu ya ufisadi?. Je hiyo siyo maana kwamba "hata waziri anapata kigugumizi kuwawajibisha TOC sababu huenda wametafuna wote"?.

MAELEZO MAFUPI KUHUSU NAMBA 4: Inaaminika kwamba (unless they proof otherwise) kuna maofisa kadhaa wizarani pale wenye uwezo wa kuidhinisha fedha, hivyo wanaidhinisha kwamba timu haijalipiwa safari!!, (2004 hadi 2010) wakisha droo hizo hela wanagawana wao na TOC maana safari ilishalipiwa na OS. Pia kuna travel agent moja maarufu jijini Dar (jina nahifadhi) ndo inayotoa risiti feki ili ku - compromise serikalini!!.

5). Je watanzania hawahitaji kujua sababu za mama Pinda kupokonywa
zawadi ya Olympic Movement na badala yake kupewa mama Bayi, tena aliyempendekeza ni mumewe, je hiyo siyo matumizi mabaya ya madaraka?.
Ukizingatia hata timu ya Olimpiki kukaa kwa Bayi ilikuwa ni Voting Power ya Bayi maana yeye ni (1) Katibu Mkuu TOC, (2). Mjumbe wa RT, (3) Mmiliki wa Hostel zilizotumika kuandaa timu  ya London Games!!.
Kama serikali yetu inahubiri "utawala bora na wa kisheria" inasubiri nini kuunda tume huru kuchunguza madai hayo ili tujue Black or White!!.

MAELEZO MAFUPI KUHUSU NAMBA 5: Olympic Movement ilitaka zawadi apewe mwanamke aliyehamasisha na kuchangia michezo nchini, na jukumu hilo walipewa TOC, inashangaza sana kwamba mama Pinda aliombwa na CHANETA kuchanga fedha ili kufanikisha mashindano ya Africa, tena mama wa watu alijituma na kuonyesha unyenyekevu kwa makampuni makubwa na alifanikiwa kuchangisha mamilioni ya fedha (ambazo matumizi yake hayajawekwa wazi hadi sasa). Lakini katika kilele cha mafanikio
aliyoyasababisha mama yetu mpendwa (TUNU PINDA) zawadi ilikwenda kwa mke wa mtu ambaye (His discretion) ndo ilimuidhinisha mkewe kupata zawadi hiyo kinyemela!!. 

Kumbukeni kwamba Meja Bayi anao uhusiano wa
kimasilahi na CHANETA, pia ana masilahi na MPOKEAJI WA ZAWADI yaani mke wake; Je ni nani basi aliye - play a major roll katika kuamua nani apewe zawadi hiyo kama siyo kamanda mwenyewe!!. "Mimi naamini 100/100 kwamba mke wa waziri mkuu ametumika visivyo na hapo TOC wamedhihirisha
kutokuwa na utu!!. Ndo maana hawastahili hata kupewa haki ya kugombea tena, ndo maana tume huru ya uchunguzi itaweza kupembua UKWELI NA UWONGO.

6). Sasa imefahamika "Mystery behind Puma and Lining". Kumbe PUMA
  ilikuwa inatolewa bure na wadhamini lakini walewale WAIDHINISHAJI wa fedha wizarani (majina tunayo na muda si mrefu tutawataja moja baada ya mwingine), wakawa wana - Bill serikali "kana kwamba Puma hizi hazijalipiwa bado!!, hivyo hela zikitoka zinapigwa mifukoni!!. NDO MAANA SIKU MOJA NIKIWA KTK KIPIMA JOTO LA ITV MHESHIMIWA THADEO ALI BEHAVE KAMA NYOKA ALIYENYANGANYWA PANYA MDOMONI!!, kwani uongo?, watanzania si walishuhudia?. Sasa kama waziri anawaonea haya mafisadi hao mimi nitakwenda hadi Dodoma kuwaomba wabunge wapiganaji kusimamia swala la TUME HURU KUUNDWA DHIDI YA TOC!!, pia tukifikia hatua hiyo majina ya MAFISADI WA WIZARA HUSIKA nitazitaja mbele ya wana jangwani, Msimbazi na wadau wote wa michezo nchini bila kuogopa kuku wala jogoo.

7). Pia wizara na TOC wanatakiwa kuueleza umma iweje wanamichezo waliotuwakilisha London wapate pea moja moja tu ya viatu?. Wakati inaeleweka walistahili kupata begi kubwa lenye vifaa vyote vya michezo sambamba na "memorabilia" zilizowekwa chapa ya 2012 LONDON OLYMPIC GAMES kila mmoja wao. Inaaminika kwamba "kigogo mmoja wa wizara alikwenda London kuwapora wanamichezo mabegi hayo kwa hisani ya TOC ili vifaa hivyo vitumike katika kuwahonga wapiga kura ili BAYI na GULAM warudi madarakani sambamba na timu nzima ya sasa ya TOC ili "mchwa waendelee kutafuta for another 4 yrs".

UDHAMINI WA KAMPUNI YA MIKOPO KUWAKIMBIZA DEMBA BA, CISSE, TIOTE NA BEN ARFA NEWCASTLE??



Kumekuwepo na hisia kwamba Newcastle inaweza kuwapoteza wachezaji wake wenye imani kali ya dini ya kiislamu kama Demba Ba, Papiss Cisse, Cheik Tiote na Hatem Ben Arfa baada ya kusaini mkataba wa udhamini wa jezi ambao unaweza ukawa unakinzana na sheria za dini ya kiislam.

Newcastle wametangaza jana kwamba klabu hiyo imekamilisha dili la mamilioni ya fedha na kampuni ya mikopo ya Wonga, ingawa kumekuwepo na mawazo kwamba Ba, Cisse, Tiote na Ben Arfa wanaweza kukataa kuvaa jezi yenye logo ya kampuni hiyo inayopata faida kutokana na biashara ya kuazima fedha huku wakirudishiwa fedha hizo kwa riba - kitendo ambacho ni kinyume sheria za dini ya kiislamu, kwa maana hiyo wanaweza hata kuondoka ili kuepeukana na dhambi hiyo.

Siku za nyuma mchezaji Freddie Kanoute aligoma kuvaa jezi za Seville zilizokuwa na udhamini wa kampuni ya kamari ya 888.com kifuani. Kanoute mwishowe aliruhusiwa kuvaa jezi siyokuwa na mdhamini lakini akakubali kuvaa jezi yenye logo ya mdhamini wakati wa mazoezi akiwa na maana ya kutoitangaza kampuni hiyo kwa mashabiki wake na waklabu kiujumla.

Swali linabakia je Newcastle watakuwa tayari kuwapoteza wachezaji wao wanne muhimu au watakubalia kuwatengenezea jezi ambazo zitakuwa bila na nembo ya mdhamini mpya? Muda pekee ndio utatoa majibu.

WAYNE ROONEY KUPATA MTOTO WA PILI MWEZI MEI MWAKANI



Coleen Rooney ametangaza kwamba ni mjamzito na anategemea kupata mtoto wa pili.

Mtangazaji wa TV na mumewe, mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney walitangaza kupitia ukurasa wa Twitter kwamba wanatagemea kumuongezea ndugu mtoto wao Kai, ambaye anafikisha miaka mitatu mwezi ujao.

Coleen amasema anategemea kujifungua mwezi May 2013.

Akiandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, Coleen alisema: "Watu kadhaa waliotea, hivyo sasa habari zipo nje!! Mimi, Wayne na Kai tuna furaha kwamba tunategemea kupata member mpya katika familia yetu mnamo mwezi May.

"Ni mapema bado lakini tuna furaha kubwa, pia tungependa habari hizizitoke kutoka kwetu sisi kwanza kabla ya mtu yoyote mwingine!"

Baada ya kutangaza habari hizo kwenye Twitter wanandoa hao walipongezwa na watu maarufu mbalimbali wakiwemo marafiki kama Danielle O'Hara, Jude Cisse, Charley Webb na Piers Morgan.

Piers Morgan ambaye ni shabiki mkubwa Arsenal aliandika: "Hongera kwa habari hii nzuri @WayneRooney & @ColeenRoo - na tuombe mtoto apate muonekano wako...."

Rooney na Coleen ambao ni marafiki tangu utotoni walioana nchini Italy mwakak 2008 baada ya kuwa wamechumbiana kwa miaka 5. Walianza mapenzi tangu walipokuwa na miaka 16, wakati Coleen akiwa bado yupo shule.

Wednesday, October 10, 2012

HAPPY BIRTHDAY: TONY ADAMS

MGOMBEA AGOMA KUHOJIWA NA BABA MKWE WA MPINZANI WAKE.


 



USAILI WA WAGOMBEA MKOA WA MBEYA WATAWALIWA NA VITUKO.

 Na Moses Ng'wat,Mbeya.
 USAILI wa wagombea wanaowania nafasi  mbalimbali  za uongozi  katika chama cha soka  mkoa wa Mbeya, (MREFA), jana uligubikwa na vituko vya aina yake,  baada ya mmoja wa wagombea wa nafasi ya Uenyekiti,  kumkataa mjumbe wa kamati ya uchaguzi kwa madai kuwa ana mgongano wa kimasilahi na mpinzani wake.
 Mjumbe wa Kamati ya uchaguzi aliyekataliwa na kulazimika kutolewa ndani ya chumba cha usaili ili haki itendeke kwa mgombea ni Katibu, Prince Mwaihojo, ambaye anadaiwa kuwa ni Mkwe wa mgombea mmoja wa nafasi ya Uenyekiti John Mwamwaja.
 Gazeti hili lilishuhudia katibu huyo wa Kamati ya uchaguzi, akitoka nje muda mfupi tu baada ya mmoja wa wagombea ya nafasi ya uenyekiti Elias Mwanjala, alipoitwa ndani ya chumba cha usaili.
 “Mimi nafikiri lazima nitendewe haki haiwezekani mimi nihojiwe na mtu ambaye anamafungamano ya kidamu na mpinzani wangu, ndio maana nilipofika ndani ya chumba cha usaili nilitoa angalizo na nashukuru Mwenyekiti alielewa na kukubali kumtoa nje ” alisema Mwanjala alipoulizwa.
 Kwa upande wake, Mwaihojo alipoulizwa juu ya sakata hilo la kukataliwa,  alikiri kuwa lilitokea na si la ajabu katika mahala popote ambapo haki inaafutwa, hivyo kitendo hicho hakizuii mchakato wa kuwapata viongozi wa chama hicho.
 Akitoa taarifa ya mchakato wa zoezi hilo baada ya kumalizika, Mwaihojo alisema zoezi hilo la usaili kwa limefanikiwa kwa asilimia 90 kwa kuwa wagombea 14 walifanyiwa usaili na kubakiza wagombea wanne tu ambao watamalizia hawakufanyiwa.
 Kwa mujibu wa Mwaihojo, wagombea wanne ambao hawajafanyiwa usali ni Katibu anayemaliza muda wake Lawrence Mwakitalu, Andongwisye Panja, Thomas Kasombwe Sinkwembe ambao wote walitoa udhulu kutokana na kukabiliwa na shughuli mbalimbali ikiwemo kusimamia mitihani ya kidato cha nne inayoendelea hivi sasa.
 Uchaguzi wa MREFA unatarajia kufanyika oktoba 27, jambo litakalowezesha kupatikana kwa uongozi mpya utakaohudumu kwa miaka mine kama katiba ya chama hicho inavyoeleza.
 Aliwataja watu waliojitokeza kuomba nafasi za uongozi  kwa nafasi ya Mwenyekiti kuwa ni John Mwamwaja ambaye ni makamu Mwenyekiti wa uongozi unaomaliza muda wake, wakati wengine ni Majuto Mbuguyo aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji katika Halmashauri ya
Wilaya ya Tanga, pamoja na Elias Mwanjala ambaye katika uchaguzi Mkuu uliopita aligombea ubunge katika jimbo la Kyela na kuangushwa vibaya na mbunge wa sasa Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye pia ni Waziri wa Uchukuzi.
Makamu Mwenyekiti ni  Omary Mahinya, wakati nafasi ya Katibu Mkuu, Lawrence Mwakitalu, anayemaliza muda wake,Suleiman Haroub na Redson Kaisi, ambapo Katibu Msaidizi ni William Mwamlima na nafasi ya Mkutano Mkuu wa Taifa Tahdeo Kalua na Danny Korosso.
Kwa upande mweka Hazina ni Asajile Kavenga, Uswege Luhanga, wakati wajumbe wa kamati ya utendaji ni Lwitiko Mwamndela, Thomas Kasombwe, Boniface Sinkwembe.

STARS INGEKUWAJE ENDAPO VIJANA HAWA WA MAXIMO WANGEKUWEPO HADI SASA?


 Wakati aliyekuwa kocha wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania kwa kipindi cha miaka mine (2006 - 2010), Marcio Maximo alipokuja nchini aliingia na mtazamo tofauti kuhusiana na soka la Tanzania, Maximo aliamini kuwa nchi yoyote amnbayo inahitaji mafanikio ya kweli ya soka ni lazima ijizatiti zaidi katika soka la vijana.

 Hata nchini kwao, Brazil soka la vijana ndiyo msingi wao mkubwa wa mafanikio waliyonao, lakini alitambua kwa nchi changa kama Tanzania si rahisi kuingia haraka katika soka la vijana na kupata mafanikio. Aliamini uchumi na aina yetu ya utekelezaji mambo huwa ni ya taratibu sana, lakini hiyo haikuwa sababu ya yeye kushindwa kuingiza vijana wadogo kutoka katika baadhi ya shule za secondary nchini katika timu ya Taifa kwa nia ya kujifunza kwa manufaa ya siku za usoni ya kikosi hicho.

Wakati wachezaji waliokuwa wakitegemewa na Watanzania kuingia katika matatizo ya kinidhamu, Maximo aliona ni vyema kutembea kila nchi na vijana wadogo kama Jerry Tegete, Kiggy Makassy, Himid Mao Makami, Tumba Sued na wengineo na si wachezaji nyota kama kina Juma Kaseja, Haruna Moshi, Mussa Mgosi, Athuman Idd “Chuji”, Amir Maftah na wengineo ambao kwa mujibu wake walikuwa wavurugaji wakubwa wa program zake za ufundi katika timu hiyo.

Ni miaka takribani sita sasa na ni Himid Mao na Salum Abubakary "Sure Boy" ambao bado wanacheza soka la kiwango cha juu, kuanzia kwa wachezaji vijana walioaminiwa na kupewa thamani kubwa na kocha huyo kama Abdulhalim Humud, Jabir Aziz, Ramadhani Chombo, Salum Telela walioingia katika matatizo ya mara kwa mara ya kinidhamu katika klabu zao, Taifa Stars imeshindwa kusonga zaidi japo vijana hao tayari wameshacheza zaidi ya misimu mitano katika ligi kuu ya Tanzania. Wengi wameshuka viwango na wengine hawapo kabisa katika soka la ushindani.

Wakati Tanzania ikipiga hesabu za kufuzu kwa michuano mikubwa kuanzia mwaka 2006 wengi walitarajia jambo hilo kutokea walau kwa miujiza kutokana na aina ya wachezaji vijana ambao walionesha mwanga wakiwa tayari na uzoefu wa mashindano makubwa ya kiafrika.


JERRY TEGETE; Yeye amekwama kabisa ndani ya timu yake ya Yanga. Kosa kubwa kwake ni pale alipoamua kurudi Tanzania kucheza mechi ‘isiyo na maana’ ya Simba na Yanga, April mwaka 2010, japo alifunga mabapo mawili katika mchezo huo, Jerry aliishia hapo na wala mabao yake hayakuisaidia timu yake kwani walilala 4-3. Amekuwa na miaka miwili migumu katika maisha yake ya soka na kuna wakati alifikiria kuachana na soka, aliingia timu ya Taifa akitokea shule ya Makongo Sekondary mwaka 2006 na mwaka mmoja baadaye akasajiliwa na Yanga ambako yupo hadi sasa. Aliweza kujitambulisha kama mfungaji mahiri zaidi katika soka la Tanzania, kwa kutumia kichwa, kuvizia na daima ni mchezaji ambaye hujipanga vizuri katika nafasi yake, mfungaji wa wafungaji anaendea mwishoni akiwa bado kijana mdogo huku akipigwa benchi mara kadhaa ndani ya Yanga baada ya kukimbia na ofa ya kucheza soka la kulipwa barani ulaya Sweden.
KIGGY MAKASSY KIGGY; Sulley Ally Muntari wa Bongo, alifunga bao kali pale, Cairo miaka mitatu iliyopita huku golini akiwepo kipa bora barani Afrika, Essam El Haidary, Kiggy alifunga bao la umbali wa zaidi ya mita 25 tena akiwa chini ya miaka 22, lilikuwa bao ambalo pengine bado halijafungwa tena katika uwanja wa kimataifa wa Cairo na liliwaaacha watangazaji wa mechi hiyo wakisema ni bao bora kati ya mabao sita ambayo yalifungwa katika mchezo baina ya Misri na Tanzania siku hiyo. Stars ilifungwa mabao 5-1 lakini kuna kitu ambacho kilionesha tulichonacho, vipaji. Mara kadhaa alifunga hivyo katika ardhi ya Tanzania, lakini baada ya misimu miwili ya taabu ndani ya Yanga amekimbilia Simba msimu huu lakini hana makali aliyokuwa nayo kipindi kile.
JUMA JABU; Alipoitwa kwa mara ya kwanza katika timu ya Taifa alikuwa mchezaji wa Ashanti United, alisajiliwa na Simba mwaka 2008 na kudumu hapo kwa miaka minne. Kwa mujibu wa pasipoti yake yupo chini ya miaka 26 lakini Jabu hakuwa na makali kwa kipindi cha miaka miwili ya mwisho akiwa Simba, mara kadhaa alijaribu kuibuka lakini majeraha yakawa yanamrudisha chini. Nahodha wa timu ya Taifa ya vijana ambayo ilifuzu na kuondolewa katika michuano ya Afrika mwaka 2005 kwa kudanganya umri kwa kiungo Nurdin Bakary, amekimbilia timu ya Coastal Union ya Tanga na anafanya vizuri kiasi tofati na alipokuwa Simba, akicheza namba sita Jabu alijitambulisha kama mpigaji mzuri wa mipira ya ‘free kick’ na mipira ya penati na kona. Alikutana na kipindi kigumu cha maumivu akiwa Simba na inawezekana ikiwa sababu kubwa ya yeye kuanguka kisoka akiwa bado kijana.

TUMBA SUED; Kuna wakati, Azam FC ilikuwa na wachezaji watu ndugu katika kikosi chao cha kwanza, Tumba Sued alikuwa ni beki mzuri wa kati ambaye alikuwa anaitwa mara kwa mara katika timu ya Taifa kwa nia ya kuendelezwa alikuwa akitokea timu ya vijana ya Azam na haraka akawa ‘patna’ mzuri na kaka yake Salum Sued katika ngome ya kati ya Azam, wakati Said Sued akifanya vizuri katika nafasi ya kiungo, Tumba akatokea kuwa beki bora kijana nchini mbele ya majeruhi Dickson Daudi, haraka alipopata mafanikio katika msimu wake wa kwanza akiicheza timu kubwa ya Azam, Tumba akiingia katika maisha ya ndoa na mara kadhaa akaingia katika matatizo ya kinidhamu na klabu yake na hata alipoenda timu ya Moro United hakuwa yule ambaye alitajwa mara kwa mara na kocha, Maximo katika kikosi chake kwa nia ya kuja kuisadia timu hiyo katika siku za usoni, amepotea na wala hasikiki tena.

DICKSON DAUD; Rafu mbaya ambayo alichezewa na mmoja wa wachezaji wa timu ya JKT Ruvu katika mchezo wa ligi kuu ndogo kituo cha Dodoma mwaka 2007, inawezekana kabisa ndiyo iliyommaliza, wakati Maximo akitamba na ukuta wa nidhamu wa Victor Costa, Salum Sued, Hamis Yusuph na Nadir Haroub hakuwa na mashaka na warithi wa nafasi zao hata kama kungetokea majeraha yoyote, Dickson Daud alikuwa beki bora zaidi wa kati U23 katika miaka ya mwanzo ya kocha maximo alikuwa mlinzi shupavu na aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kuruka juu na kufunga mabao ya vichwa, anahitaji kujiamini tena kama anataka kuwa mchezaji mzuri tena, ameanza vizuri msimu huu na tayari ameonesha mwanga mkubwa kuwa ataibuka tena, alifunga bao zuri katika mechi ambayo timu yake ya Mtibwa iliifunga Yanga mabao 3-0.

SALUM KANONI; Huyu alichukuliwa kama mbadala wa muda mrefu wa beki namba mbili wa Stars, Shadrack Nsajigwa, lakini mara baada ya kujiunga na Simba mwaka 2005 akitokea Bandari ya Mtwara, Kanoni akawa namba mbili mbadala wa walinzi Said Sued na Nurdin Bakary walipokuwa na majeraha, lakini hata pale nyota hao walipokuwa wazima ilibidi wapambane kugombea nafasi ya kucheza mbele ya kinda huyu, taratibu akachukua nafasi ya kudumu ndani ya Simba na kuitwa Stars na kucheza baadhi ya michezo chini ya makocha, Maximo na hata wakati wa Jan Poulsen, Tatizo lake kubwa ni kuridhika na kujiona tayari amefika safari yake ya soka ndani ya Simba, na baada ya miaka saba, akiwa ndani ya klabu hiy, Kanoni ameondolewa na sasa yupo Kagera Sugar akijaribu kupigania kurudisha makali yake, ameshafunga mabao mawili katika ligi kuu hadi sasa, so far anaendelea vizuri.

ABDULHALIM HUMUD; Gaucho wa Tanzania, alikuwa ni kiungo ‘maestro’ ambaye aliweza vyema jukumu la kushambulia na kuzuia ‘box to box’ aliyekuwa na uwezo na mapafu yasiyochoka, tabia mbaya na kujiona ni mkali zaidi ya hata, Mohammed Aboutrika, Ricardo Kaka’, Alex Song na hata Yaya Toure vimemmaliza alitua Simba na kushindwa kuchomoza mbele ya wachapa kazi kama Jery Santo na Hillary Echessa na kukimbia benchi, akaenda Azam lakini tayari ameonekana kuzidiwa nguvu na Ibrahimu mwaipopo katika kiungo wa ulinzi ndani ya Azam na wakati vijana Himid Mao na Salum Abubakary wakihitaji mafanikio ya mchezo wao Humud anapigana kurudisha makali yake chini ya kocha Boris Bunjuk ambaye ameonekana kumuamini kiungo huyu.

KOCHA WA YANGA TOM SAINTFIET APATA KAZI YA UKOCHA NCHINI YEMEN


Siku chache baada ya kufutwa kazi ya kuiongoza timu ya Young Africans ya nchini Tanzania, Kocha Tom Saintfiet raia wa Ubelgiji amepata ajira mpya ya kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Yemen.

Tom alifutwa kazi na timu ya Yanga baada ya timu hiyo kuanza vibaya katika michuano ya ligi kuu ya Vodacom licha ya kuisaidia kutwaa taji la mashindano ya kanda ya Afrika Mashariki na Kati.

Saintfiet, ambaye aliwahi kuwa kocha wa Ethiopia ameanza kazi siku ya Jumamosi na ataiongoza timu yake mpya dhidi ya Lebanon katika mechi ya kirafiki iliyopangwa kufanyika Oktoba 16.