Search This Blog

Friday, October 12, 2012

UAMUZI WA KUMUONDOA AKRAMA KUCHEZESHA LIGI KUU UMETOKANA NA UTASHI WA KISIASA NA VIONGOZI WASIOJUA SHERIA


Siku kadhaa zilizopita shirikisho la soka nchini kupitia kamati yake ya ligi iliamua kumfungia mwamuzi mzoefu Mathew Akrama wa Mwanza aliyechezesha mechi namba 80 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Simba iliyochezwa Oktoba 3 mwaka huu kwa madai ya kushindwa kuumudu mchezo huo wa watani jadi.
Kufungiwa kwa Akrama kulikuja baada ya kelele zilizopigwa na vilabu vyote viwili pamoja wapenzi wake kwamba mwamuzi huyo hakuchezesha kwa haki mchezo huo hivyo kuuharibu kabisa kabisa mchezo wa kulwa na doto. 
Sawa kwa amono yetu wapezni wa soka tunaona Akrama weli aliboronga mchezo huo lakini kufungiwa kwake kumekufanyika kwa utashi wa kisiasa kabisa kwa sababu ya usimba na uyanga uliojaa kwenye soka letu.
Kisheria kamati ya ligi haikupaswa kukaa kujadili suala la Mathew Akram kwa sababu hata FIFA inashauri na kuagiza masula yote ya waamuzi na vyama vyao vyeme wataalam wa sheria za soka, sidhani kama kwenye kamati ya ligi yumo mtalaamu yoyote wa sheria. 

Kama hayupo hii ni hatari hatari sana. FIFA inazuia watu wenye maslahi na vilabu kushughulika na masuala yoyote yanayohusu waamuzi  kuanzia kupanga ratiba ya waamuzi mpaka kuwatolea maamuzi kama hili likiachwa likaendelea ni hatari katika maslahi ya mpira wetu kwa sababu waamuzi watachezesha kwa woga na kufikiria katika kamati kuna nani. 
Mwamuzi anafundishwa siyo kufungiwa au kuondolewa. Akikosea anaelekezwa makosa yake anapewa mchezo mwingine ili kuona maendeleo yake na kama amerekebisha aliyoelekezwa.
Ndio maana hata kwenye ligi zilizoendelea kama Uingereza marefa wakubwa kama akina Howard Webb muda mwingine wanaboronga sana lakini ni mara ngapi tumewahi kusikia wamefungiwa au wameondolewa kuchezesha ligi.
Kwanini? Kwa sababu inachukua Inachukua takribani miaka kama 6 - 10 kumpata mwamuzi kama Akrama. Sasa wapo wangapi walioandaliwa kama yeye? Hivyo badala ya kumuelekeza vizuri Akrama, refa ambaye ana uzoefu tunaanza kuchukua marefa wachanga na mwishowe suala la kufungia waamuzi halitoisha kwa sababu akikosea tu kwenye mechi ya watani atafungiwa na kuletwa mwingine.
Vilevile inashauriwa kwamba katika mechi kubwa kama ya Simba na Yanga makamisaa wanatakiwa kuwa marefa waastaafu wenye uzoefu, sasa je katika mechi ya Simba na Yanga alikuwa mtu wa aina hiyo? au alikuwepo tu mtu ambaye nae alikuwa tu ni refa wa kawaida?
Mwisho viongozi wa soka Tanzania tuache kuuongoza mchezo huu kwa utashi wa kisiasa kwani hatotufanikiwa - kila kitu kiende vile ambavyo kimepangwa na sio kufanya maamuzi kwa mazoea.

Nawasilisha

3 comments:

  1. Sidhani kama aliyeandika hii makara alifanya utafiti wa kutosha,ni kama alikurupuka,hajui alitendalo.hauwezi hukumu kamati ambayo haujui kama kuna mtaalamu pia haujui kama kamisaa alikuwa nani.tuache kulalamika kila kitu,tujipange

    ReplyDelete
  2. Ndio maana hatufiki mbali viongozi akili zao zimedumaa na mambo ya kizamani

    ReplyDelete
  3. wantanzania hakuna tunacho tenda then tukawa na iman nacho mwisho wa siku

    ReplyDelete