Search This Blog

Saturday, March 31, 2012

NADIR HAROUB ALISTAHILI LEO KUCHEZA AU LA ?Kanuni  YA 25 ya udhibiti wa wachezaji :
Tff itadhibiti mienendo ya wachezaji kwa kuchukua hatua kama ifuatavyo.

A) MCHEZAJI ATAKAYETOLEWA NJE KWA KADI NYEKUNDU BAADA YA KUPATA KADI MBILI ZA NJANO, HATARUHUSIWA KUCHEZA MCHEZO MMOJA
B) MCHEZAJI ATAKAYEPEWA KADI NYEKUNDU ( STRAIGHT RED CARD ) ATAKOSA MICHEZO MIWILI. 
C) MCHEZAJI ATAKAYETOLEWA NJE KWA KADI NYEKUNDU KWA KOSA LA KUPIGA AU KUPIGANA ATASIMAMA KUSHIRIKI MICHEZO MITATU INAYOFUATA YA KLABU YAKE NA ATALIPA FAINI YA TSH 500,000
D) WACHEZAJI 5 WAKIPATA KADI KTK MCHEZO MMOJA KLABU ITALIPA FAINI  YA TSH 500,000
E) MCHEZAJI AKIPATA KADI JUMLA YA KADI TATU ZA NJANO ATASIMAMA MCHEZO MMOJA

BREAKING NEWS! PATRICK MAFISANGO IS BACK IN THE BUSINESS !

KIUNGO WA KIMATAIFA WA RWANDA MWENYE ASILI YA CONGO DRC MUTESA PATRICK MAFISANGO AMERUDISHWA KUNDINI KWA AJILI YA SAFARI YA ALGERIA,
KIUNGO HUYO ALIYEKUA AMESIMAMISHWA NA KLABU YAKE YA SIMBA AMERUDUSHWA KIKOSINI BAADA YA KUTAMBUA KOSA LAKE NA KUOMBA RADHI KWA MWALIMU,WACHEZAJI NA VIONGOZI.

BREAKING NEWS: KOCHA WA MORO UNITED AJIUZULU

Baada ya mfululizo wa matokeo mabaya katika Vodacom premier league, kocha mkuu wa Moro United Hassan Banyai ameamua kujiuzulu kuifundisha timu.

Akiongea na mtandao huu Banyai alisema ameamua kufanya hivyo baada ya kukaa chini na kuongea na viongozi wake na kuamua kukaa pembeni kumpisha mwalimu mwingine aje kuokoa jahazi linalozama la Moro United.

"Mimi nina mapenzi makubwa na Moro United, hii timu yangu na naipenda sana, hivyo siwezi kuweka maslahi yangu mbele huku kalbu yangu ikiwa inafanya vibaya. Nimeamua kukaa pembeni na kujiuzulu ili kuweza kumpisha mwalimu mwingine ambaye ataweza kushikilia pale niliposhindwa na kuweza kuikoa timu yetu isishuke daraja msimu.

"Nwashukuru viongozi wa Moro na wachezaji pia kwa yote waliyonitendea na ushirikiano walionipa tukiwa tupo pamoja katika kuhikikisha timu inafanya vizuri katika michuano mbalimbali. Naipenda sana Moro na nina imani tutapata kocha mwingine ambaye ataweza kuikoa timu yetu kutoka kushuka daraja."

LIVE MATCH CENTRE: SIMBA 2-0 A.LYON - YANGA 1-0 COASTAL UNION - FULL TIME


Hivi sasa ni kipindi cha pili na timu ya Simba inaongoza magoli 2-0 dhidi ya timu ya Africa Lyon yaliyofungwa na mchezaji Salum Machaku alliyepiga mpira wa kona uliombabatiza golikipia wa timu hiyo na kuingia moja kwa moja nyavuni, goli la pili la Simba limefungwa na Mshabuliaji Haruna Moshi Boban.


Wakati huohuo huko Tanga timu ya Yanga ya jijini Dar es salaam inamenyana na timu ya Coastal Union ya huko na sasa hivi ni kipindi cha pili, hata hivyo hakuna timu iliyokwishapata goli

LIVE UPDATES
Kutoka Uwanja wa Taifa 50'
Simba 2-0 Africa Lyon

kutoka Mkwakwani Dakika ya 60,
Coastal Union 0 - 0 Young Africans

Simba 2 Lyon 0
dak 80
 

katika uwanja wa mkwakwani dakika 76 coast 0 yanga 0 

Kutoka Uwanja wa Taifa 86'
Yanga 1-0 Coastal
 

Kutoka Uwanja wa Taifa Fulltime
Simba 2-0 Africa Lyon
 

Kutoka Uwanja wa Mkwakwani Fulltime
Yanga 1-0 Coastal Union
goli kafunga Hamis Kizza dakika 86
 

SIKU 10 MUHIMU AMBAZO ZITAAMUA HATMA YA UBINGWA WA LA LIGA KATI YA REAL MADRID NA BARCELONA.

Wiki zilizopita, watu wengi walikuwa wameshaanza kusema nani atakuwa bingwa wa La liga msimu huu huku wakihitimisha mbio za ubingwa huo, taji ya ligi likiwa limeanza kuondolewa Nou Camp kwenda Cibeles, wakati Real Madridwakiongoza kwa 10 na kuwapita kabisa Barcelona tangu mwanzoni kabisa mwa mwezi wa pili.

Lakini ndani ya siku nne za kati kati mwa mwezi wa tatu, ile advantage waliyokuwa nayo Madrid, ambayo ilionekana ni vigumu kuifikia imepunguzwa mpaka kufikia nusu.Ilikuwa haitegemewi kuwa hivi sio kwasababu Barca walikuwa hawana uwezo wa kuwafikia mahasimu wao, bali Madrid walikuwa na consistency ya kupata matokeo mazuri kila wiki, hata kufikia hatua Pep Guardiola na Johan Cruyff walishaanza kukata tamaa juu ya Barca kuwakuta Los Blancos.

Lakini bila kutegemea Madrid wameteleza mara mbili, kwanza wakiwa nyumbani walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Malaga na baadae katika dimba el madrigal dhidi ya Villareal. Katika mechi zote mbili, vijana wa Jose Mourinho walianza kufunga lakini wakaruhusu nyavu kuguswa kupitia mipira ya set pieces.

Sasa zimebakia points sita kama pengo lilopo kati yao, lakini hizi siku 10 zijazo ambazo zitahusisha mechi tatu kabla ya El Classico ndio zitaamua mbio za ubingwa. Ukiangalia kwenye karatasi unaweza ukaona kwamba Barca wana mechi nyepesi ukilinganisha na Madrid.

Usiku wa leo hii, mahasimu hawa wawili watakutana na timu mbili ngumu kuliko kutoka kaskazini mwa Spain. Real Madrdi watacheza na Osasuna huko Pamplona wakati Barca wataikaribisha Athletic Bilbao pale Nou Camp.

Los Blancos Madrid hawajawahi kushinda katika dimba la Reyno de Navarra katika mechi zao tatu zilizopita, mbili kati ya hizo waliishia kufungwa na nyingine ikiisha kwa suluhu. Pia ulikuwa uwanja huu huu ambao mwezi uliopita Barcelona waliishia kutandikwa 3-2, kipigo ambacho kilipelekea Madrid kuongoza kwa points 10. Pia itaendelea kushangaza ikiwa Osasuna hawa hawa watapunguza pengo la pointi waliloliongeza mwezi uliopita.
THE TITLE RACE: REAL MADRID & BARCELONA'S
LEAGUE FIXTURES KABLA YA THE CLASICO
  REAL MADRID H/A   BARCELONA H/A
Osasuna A Athletic Bilbao H
Valencia H Zaragoza A
Atletico Madrid A Getafe H
Sporting Gijon H Levante A
BARCELONA A REAL MADRID H


Athletic Bilbao siku zote ndio wamekuwa wapinzani ambao wanawapa shida sana The Blaugurana Barca dimbani, lakini wakatalunya kwa kiasi siku zote wamekuwa wakijitahidi mno kupata matokeo mazuri. Bilbao hawajamfunga Barca katika michezo 16 katika mechi zote za ligi za nyumbani, na mara ya mwisho wameshinda ilikuwa waliposhinda pale Nou Camp in 2001.

Kikosi cha Marcelo Biesla kinaweza kikawa katika form nzuri barani ulaya lakini kwenye La liga wamekuwa hawapo vizuri. Wamefungwa mechi tatu na kutoa suluhu katika mechi zao nne za mwisho hivyo kupelekea kushukahadi nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi japokuwa walikuwa nafasi ya tano mwanzoni mwa mwezi huu.

Baada ya mechi za weekend hii, mambo yatazidi kuwa magumu zaidi kwa Madrid. Watawakaribisha Valencia kabla ya kucheza derby na Atletico Madrid, wakati Barca watasafiri kwenda kucheza na Zaragoza na baadae watawakaribisha Getafe.

Real Madrid chini ya Mourinho wana matokeo mazuri kwa asilimia 100 dhidi ya Valencia na Atletico, lakini hilo linaweza lisiwe na maana kutokana na kila siku zinavyozidi kwenda ndivyo presha inapozidi kuongezeka kwa Los Blancos.

Kumekuwepo na matatizo ya kisaikolojia kwa Madrid chini mreno huyu, kwa ushahidi ulionekana mwsihoni mwa msimu uliopita presha ilipokuwa kubwa Madrid wakapoteza mechi 2 muhimu dhidi ya Sporting Gijon na Zaragoza.
THE TITLE RACE: REAL MADRID & BARCELONA'S
LEAGUE FIXTURES BAADA YA THE CLASICO
  REAL MADRID H/A   BARCELONA H/A
Sevilla H Rayo Vallecano A
Athletic Bilbao A Malaga H
Granada A Espanyol H
Mallorca H Real Betis A


Kwa Barca, Getafe inaweza ikawa chungu kwa Catalan giant, ikiwa wao ndio moja ya timu pekee zilizoifunga Barca msimu . Lakini Nou Camp uwanja ambao klabu hiyo inayotoka mji wa Madrid hawajawahi kuibuka na ushindi na ni mara mbili tu wameweza kuondoka na droo,hivyo kuifunga Barca sio rahisi kihivyo.

Ikiwa Madrid watapoteza mjini Pamplona weekend  na wakafungwa pia mjini Catalunya tarehe 22 ya mwezi wa nne, na vijana wa Guardiola wakashinda mechi zao zote kuelekea El Classico, mapambano ya kugombea siku hiyo yatakuwa makubwa mno. Barcelona watakuwa wamekata pengo lote la pointi sita na watakuwa wao watakaokuwa juu ya msimamo kuelekea katika michezo minne ya mwisho wa La Liga.

Japokuwa, ikiwa Los Blancos watawanyoosha Osasuna na kuongeza wigo wa pointi kwa kuwafunga Vancia na Atletico, basi kutokea hapo Madrid watakuwa wana nafasi kubwa ya kubeba ndoo hata ya El Classico. Nani angeweza kufikiri Osasuna atacheza part  kubwa katika kuamua ubingwa uende wapi msimu huu.

MAFISANGO: SIMBA WAMEMWAGA UGALI NAMWAGA MBOGA

KUFUATIA kusimamishwa na uongozi wa Simba, Patrick Mafisango, sasa anataka alipwe fedha zake ili arudi kwao Rwanda.
Kiungo huyo Mnyarwanda mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, alisimamishwa kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu.
Inadaiwa aliripoti kambini Jumatano iliyopita akiwa amelewa chakari na alinaswa na Meneja, Nico Nyagawa. Kambi ya timu hiyo iko Bamba Beach, Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Inasemekana badala ya kujieleza kwa uungwana, Mafisango alianza kumrushia matusi Nyagawa.
Alipokuwa akielekea chumbani, alikutana na kocha Milovan Cirkovic, ambaye naye alimhoji.
Imeelezwa kuwa Mafisango pia alimtukana na Mserbia huyo, ambaye aliutaarifu uongozi uliofikia uamuzi huo wa kumwondoa kambini.
Akizungumza na Mwanaspoti, Mafisango alisema: "Nimechoka na majungu, kuna watu wachache wanataka kuniharibia jina langu.
"Ninachotaka sasa, Simba inilipe haki zangu zilizobaki kabla ya mkataba wangu kuisha, nauli ya mtoto (Crespo), mke wangu na mimi, nirudi nyumbani nikafanye mambo mengine.
"Nimevumilia sana, naambiwa ni mlevi na mambo kibao ambayo kwa kipindi kirefu navumilia. Majungu haya ndiyo nasikia hapa Tanzania, mbona nimecheza timu mbalimbali, Rwanda na Congo hakukuwa na matatizo?"
Mafisango pia alitemwa na Azam kutokana na matatizo hayo ya utovu wa nidhamu.
Hata hivyo, Milovan alitetea msimamo wa kumtimua Mafisango akisema hawezi kuvumilia mchezaji asiyekuwa na nidhamu.

source: www.mwanaspoti.co.tz

DIAMONDS ARE FOREVER @MLIMANI CITY YAFANA

 Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Diamond Platinum akiwarusha mashabiki waliohudhuria katika tamasha lake la Diamond Are Forever lililofanyika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
 Diamond akionyesha umahili wake wa kuimba.
 ...Kumbe jini kisilani kaingia katika utamu wa penzi langu, alikuwa akiimba
 ...hapa alikuwa akimwaga mauno mbele ya mashabiki waliohudhuria.
 Janeth Sostenes akifanya mahojiano na Godwin Gondwe.
 ...Aha! madansa wa Diamond wakiwajibika nae
 Mashabiki wa kutosha wakifuatilia show.
 ...Diambond akiwajibika vilivyo
 ...Madansa wakiwajibika
 ...Safi sana 
 ...Utata ulianzia hapa pale Dimond alishuka stejini na kwenda kwenye meza waliokuwa wamekaa akina Steve Nyerere na Mboni Masimba na ndipo alipopewa t-shirt ambayo kwa mujibu wa udadisi na uchunguzi wa udadavuzi wa mambo wa Kajuna Blog, ilisemekana kuwa t-shirt hiyo ilikuwa inapicha ya mwanadada ambaye alikuwa akitoa na Diamond kwa sasa. Na ilikuwa ni maalum kwa ajili ya kumrusha roho Wema Sepetu.
 ...Mwanadada Mboni Masimba akimkabidhi Diamond t-shirt huku Steve Nyerere akimtunza, vile vile alichukua t-shirt aliyopewa na kuipeleka kwa mwanadada Jokate Mwegelo.
 ...Hapa akikabidhiwa t-shirt na kupewa maelekezo mahali pa kuipeleka.
 ...Baada ya hapo kumaliza lile movie la kwanza aliendelea na kupita katika meza mbali mbali huku akiwasalimia wageni waalikwa.
 ...Akiimba na bendi ya Odama ambayo alimpa ushirikia mkubwa.
 ...Mauno yamekolea
 ...Akiendelea kutoa shukrani kwa wageni waliofika kumsapoti. Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Q-chief  akimpa sapoti mdogo wake Diamond
 ...Ehe! utata mkubwa ambao ulizuka ni hapa ambapo mwanadada huyu alimtuza dola za Kimarekani, Diamond
 ...Diamond aliendelea kuimba huku mwanadada huyo akimtunza huku akitoa tabasamu na kicheko
 Mwadada huyo hapa alikuwa amemaliza na kuondoka kwa mikogo..
Baada ya Diamond kurudi stejini ndipo mwanadada Wema Sepetu alienda kumtuza na pesa zake kukataliwa. Wema alikaa akimbembeleza kwa muda wa dakika 10 japo zoezi lake halikufanikiwa.
 ...Diamond aliendelea kuwajibika huku Wema akijaribu kumbembeleza
 ...Bembeleza, bembeleza na wewe jamaa ndiyo aliendelea kuwajibika
 ...Ndipo alipochukia na kuzitupia hizo hela stejini huku akiondoka huku akiwa amenuna
 ...Shamim Mwasha akilaumu kitendo alichokifanya Diamond cha kukataa hela alizoenda kutuzwa na Wema... 'Haiwezekani hii ni aibu sana'
Pesa alizokataa kuzichukua zikiwa zimetupwa 
 ...Hapa alipiga kitu cha 'Nimpende Nani'
 ...Jokate na marafiki zake wakishangilia
 ...Baada ya tuio hilo kutokea Mange Kimambi alimuita mshereheshaji wa tamasha hilo, Taji Liundi na kumuomba amuite Diamond aje amuombe msamaha na ndipo Diamond akakataa.
 ...Diamond alishuka na kuelekea kwa mwanadada Jokate Mwegelo na kuanza kukata mauno.
 ...mwanadada Mboni Masimba akiwa amevaa t-shirt alizokuwa amevaa.
 ...Aha! nimependeza sana
Taji Liundi akimbembeleza Diamond ili aende nae kwa Wema ndipo Diamond akakataa. 


 ...Mwanadada Mariam (Miss Popular) akimfuta jasho Diamond wakati Taji Liundi akimbembeleza ili aende kwa Wema.
 ...Diamond akiserebuka na warembo
 Marafiki wa Wema Sepetu wakijaribu kumbembeleza wakati akimwaga chozi... huku watu wengine wakishangilia na kuimba aibu yetu au aibu yao???
 ...hapa mwanadada akijaribu kubembeleza bila matumaini.
 Msanii wa kizazi kipya, Ommy Dimpozzz akimpa sapoti Diamond...huku akitoa ushuhuda wa maisha yake na    ya Diamond walipotoka.
 ...baada ya ujumbe wa Ommy Dimpozz, Diamond alimwaga chozi na hapa alikuwa akijifuta.
 Amini nae hakuwa nyuma kumpa sapoti
 ...Barnaba, Amini na Diamond wakiwajibia
Baada ya Barnaba kuimba wimbo wa 'Napembelezwa' ndipo mwanadada Wema alienda kumtuza na kutoa machungu yake.

Picha zote kwa hisani ya http://kajunason.blogspot.com/