Search This Blog

Saturday, April 13, 2013

BAADA YA VILABU KUGOMEA MECHI ZAO KUONYESHWA BURE: TFF WATOA TAARIFA KUTOKUWEPO KWA SUPER WEEK KUTOKANA NA MATATIZO YA UFUNDI

Mechi tano kati ya sita za Super Week za Ligi Kuu ya Vodacom zilizokuwa zioneshwe moja kwa moja (live) na Kituo cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini sasa hazitaoneshwa kutokana na matatizo ya kiufundi.

Kwa mujibu wa Mtayarishaji Mtendaji (Executive Producer) wa SuperSport Kanda ya Afrika, Max Tshunungwa ambaye yuko nchini, wameshindwa kuonesha mechi hizo kutokana na matatizo ya kiufundi katika magari yao ya kurushia matangazo (OB van) yanayohudumia Afrika Mashariki- Kenya, Tanzania na Uganda.

Mechi hizo ni kati ya Azam na African Lyon, Yanga na Oljoro JKT, Azam na Simba, Coastal Union na JKT Ruvu na Mgambo Shooting na Yanga itakayochezwa Aprili 17 mwaka huu jijini Tanga.

Tatizo hilo pia limeathiri mechi za Ligi Kuu ya Kenya (KPL) ambazo hazitaonekana wikiendi hii. SuperSport ndiyo yenye haki za matangazo ya televisheni kwa ligi hiyo ya Kenya.

Tshunungwa amekutana na Sekretarieti ya TFF na Kamati ya Ligi kuelezea tatizo hilo. SuperSport kwa kushirikiana na Kamati ya Ligi na TFF watapanga mechi nyingine za Super Week kabla ya ligi kumalizika msimu huu.

Pia TFF, Kamati ya Ligi na SuperSport watakuwa na mkutano mfupi wa waandishi wa habari wakati wa mapumziko kwenye mechi ya leo kati ya Yanga na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa.

LIVE MATCH CENTRE: YANGA SC 3 - 0 JKT OLJORO


Dk 90+5 MPIRA UMEISHA! YANGA 3-0 OLJORO.

Dk 90 Mpira umeongezwa dakika 5.

Dk 90 Mpira umeongezwa dakika 5.

Dk 87 Nizar Khalfan anapiga shuti kali langoni kwa Oljoro lakini kipa Shaibu Issa anapangua na kuutoa nje mpira. YANGA 3-0 OLJORO.

Dk 82 Bahanunzi anachezewa vibaya kwa kutegwa mguu ndani ya eneo la hatari la Oljoro lakini mwamuzi anapeta.

Dk 78 Yanga inafanya mabadiliko, ametoka Msuva ameingia Nizar Khalfan. YANGA 3-0 OLJORO.

Dk 75 Mpira umechangamka kidogo timu zote zinamiliki mpira kwa zamu.

Dk 71 Frank Domayo wa Yanga anamchezea rafu Sixbert Mohamed.

Dk 67 Oljoro inafanya mabadiliko, ametoka Karage Mgunda ameingia Sixbert Mohamed. YANGA 3-0 OLJORO.

Dk 59 Majaliwa Sadik wa Oljoro ameonyeshwa kadi ya njano na mwamuzi Amon Paul wa Mara baada ya kumchezea vibaya Msuva.

Dk 58 Yanga inafanya mabadiliko, ametoka Kavumbagu ameingia Said Bahanunzi. YANGA 3-0 OLJORO.

Dk 55 Emmanuel Memba wa Oljoro anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea rafu Niyonzima.

Dk 53 Niyonzima anapiga shuti kali katika lango la Oljoro lakini kipa Shaibu Issa anapangua. Issa anaumia na kutibiwa baada ya kugongana na Kavumbagu.

Dk 50 Oljoro wanafanya mabadiliko, kipa Lucheke Musa anatoka anaingia Shaibu Issa.

Dk 46 Chuji anachezewa rafu na Paul Nonga wa Oljoro.

Dk 45 KIPINDI CHA PILI KIMEANZA
Dk 45 HALF TIME! YANGA 3-0 OLJORO.

Dk 43 GOOO....! Hamis Kiiza anaipatia Yanga bao la tatu baada ya kuiwahi pasi iliyopenyezwa kutoka katikati ya uwanja na kumchambua kipa. YANGA 3-0 OLJORO.

Dk 42 David Luhende wa Yanga anatengewa mpira mzuri na Chuji lakini shuti lake linatoka nje.

Dk 36 Msuva wa Yanga anapokea pasi safi ya Nsajigwa na kupiga krosi safi ambayo ilibaki kidogo mpira uingie wenyewe golini.

Dk 32 Yanga inafanya mabadiliko, ametoka Juma Abdul ameingia Shadrack Nsajigwa.

Dk 30 Abdul wa Yanga ametibiwa na kurudi uwanjani lakini anaanguka akiwa peke yake huku akigugumia maumivu ya kifundo cha mguu. Shadrack Nsajigwa anapasha misuli moto.

Dk 24 Didier Kavumbagu wa Yanga anashindwa kuunganisha krosi safi ya Msuva kutoka wingi ya kulia.

Dk 21 Cannavaro anaumia baada ya kugongana mchezaji wa Oljoro. Mpira unasimama kwa muda na Cannavaro anatibiwa.

Dk 19 GOOO...! Msuva anaifungia Yanga bao la pili baada ya kuipangua ngome ya Oljoro na kupiga shuti hafifu. YANGA 2-0 OLJORO

Dk 16 Oljoro wanaonekana wamezinduka nao wameanza kutawala kiungo huku wakicheza pasi fupi fupi.

Dk 13 Paul Nonga wa Oljoro anatengewa mpira vizuri na Idd Swaleh lakini shuti lake linatoka nje ya lango la Yanga.

Dk 10 Yanga imetawala mchezo hasa kiungo na imefanya mashambulizi mengi langoni kwa Oljoro.

Dk 5 GOOO....! Nadir Haroub 'Cannavaro' anaipatia Yanga bao la kwanza kwa kichwa akiunga mpira wa kona. YANGA 1-0 OLJORO

3 Simon Msuva wa Yanga anapiga shuti kali langoni kwa Oljoro kipa anaupangua na kuwa kona. Kipa anaumia baada ya kuucheza mpira huo. Mchezo unasimama ili kipa atibiwe.

Dk 1 Juma Abdul wa Yanga anapiga shuti kali langoni kwa JKT Oljoro lakini kipa Lucheke Musa anaudaka mpira. Abdul alipewa pasi na Frank Domayo.

Dk 00 MPIRA UMEANZA!

Young Africans line-up to face JKT Oljoro today
1.Ally Mustafa 'Barthez'
2.Juma Abdul
3.David Luhende
4.Nadir Haroub 'Cannavaro'
5.Kelvin Yondani
6.Athuman Idd 'Chuji'
7.Saimon Msuva
8.Frank Domayo 'Chumvi'
9.Didier Kavumbagu
10.Hamis Kiiza
11.Haruna Niyonzima

Subs:
1.Yusuph Abdul
2.Shadrack Nsajigwa
3.Oscar Joshua
4.Salum Telela
5.Nurdin Bakari
6.Nizar Khalfani
7.Said Bahanuzi


JKT Oljoro: Lucheke Musa, Yusuf Machogoti, Majaliwa Sadiki, Nurdin Mohamed, Shaibu Nayopa, Salim Mbonde, Karage Mgunda, Emmanuel Memba, Paul Nonga, Idd Swaleh na Hamis Salehe.

MABAO 340 YATINGA NYAVUNI LIGI KUU 2012/13 - YANGA NA AZAM VINARA WA MABA0 - AFRICAN LYON NA TOTO WAONGOZWA KWA KUFUNGWA MABAO MENGI

Mabao 340 yamefungwa kwenye mechi 307 katika Ligi Kuu Tanzania iliyoanza kutimka rasmi Septemba 20, mwaka jana na kutarajiwa kufikia tamati Mei 18, mwaja huu.
Kwa idadi ya mabao hayo ni sawa na wastani kila mechi ya ligi linafungwa goli moja.
Azam FC ni timu ambayo imethibitisha kuwa na safu kali ya ufungaji mabao huku ikifuatiwa na vinara Yanga.
Wawakilishi hao pekee wa nchi katika mashindano ya kimataifa, Azam wamezamisha mabao 39 katika mechi 22 walizocheza huku Yanga ikipachika 37 kwa michezo yake 21.
Timu tatu, African Lyon, JKT Ruvu na Toto African ambazo zipo kwenye hatari ya kushuka daraja zinaongoza kwa kufungwa mabao mengi.
Lyon imeruhusu mabao 35 kutinga kwenye nyavu zake wakati JKT Ruvu ikifungwa 34 na Toto African ikifungwa 33. 

Friday, April 12, 2013

UJIO WA MRISHO NGASSA YANGA: SHAMTE ALLY AKATA TAMAA KABISA YA KURUDI JANGWANI - ASEMA ATAACHA MPIRA KWA MUDA

WINGA Shamte Ally ni kama amekata tamaa kurudi tena Yanga kwa mara nyingine na sasa amepania kujikita kwenye shughuli zake binafsi.
 

Nyota wanne wa Yanga, Juma Seif  'Kijiko', Idrissa Rashid 'Messi', Shamte Ally 'B52' na beki Ibrahim Job wametolewa kwa mkopo na timu hiyo kwenda kuinusuru African Lyon kushuka daraja.
Shamte alisema jijini Dar es Salaam kuwa mkataba wake unamalizika Juni, mwaka huu, lakini hana tena matarajio iwapo klabu hiyo itafikiria kumrejesha kwa mara nyingine.
 

"Mkataba wangu na Yanga unamalizika mwezi Juni, mwaka huu. Lakini kwa hali inavyo kwa sasa siamini kama watanirudisha tena. Kwa sasa nimeamua kupumzika kwanza nifanye mambo yangu
mengine." alisema Shamte ambaye alijiunga na Yanga akitokea Kagera Sugar ya Bukoba.

 

Ukweli ni kwamba, ujio wa Mrisho Ngassa kwa mara nyingine kwenye kikosi cha Yanga na uwepo wa kinda Simon Msuva ni vigumu kwa benchi la ufundi kumfikiria kumrejesha Shamte.

EQUATORIAL GUINEA HATARINI KUPOTEZA USHINDI DHIDI YA CAPE VERDE KWA KUMCHEZESHA MCHEZAJI ASIE RAIA


Equatorial Guinea wapo kweye hatari ya kuvuliwa ushindi wao wa 4-3 dhidi ya Cape Verde katika michuano ya kufuzu kombe la dunia mwaka 2014 kwa kumchezesha mchezaji ambaye hakupaswa kuichezea nchi hiyo.
Fifa imesema imefungua kesi dhidi ya FA ya Equatorial Guinea baada ya nchi hiyo kupata ushindi katika mechi ya mwezi uliopita huko mjini Malabo.
Shirikisho la soka duniani mpaka sasa halijataja jina la mchezaji husika ambaye hakupaswa kuichezea nchi hiyo. 

Wakati wachezaji wote kikosi kinachoanza cha Equatorial Guinea hakuna hata mmoja aliyezaliwa ndani ya nchi hiyo - zipo sheria na kanuni zinazowaruhusu wachezaji hao kuiwakilisha nchi yao.

Kwa mujibu wa Andiko 17 la shirkisho la soka duniani, mchezaji anayepaswa kuichezea nchi fulani inabidi atimize japo moja ya masharti yafuatayo:
  • Awe amezaliwa ndani ya mipaka ya nchi iliyopo chama cha soka husika.
  • Wazazi wake wa damu, aidha mama au baba awe amezaliwa ndani ya nchi husika.
  • Babu yake au bibi yake awe amezaliwa ndani ya nchi husika. 
  • Awe ameishi mfululizo kwa miaka mitano au zaidi ndani ya nchi husika baada ya kutimiza miaka 18.

Fifa inasisitiza "nchi wanachama na vyama vya soka ndio wenye jukumu la kujiridisha kama masharti yametimizwa." 

Burkina Faso , Gabon na Sudan wote wameshapokonywa pointi kwenye michuano ya kufuzu kombe la dunia 2014 kwa kuchezesha wachezaji ambao walikuwa hawapaswi kucheza mechi kutokana na sababu mbalimbali. 

Equatorial Guinea kwa sasa wapo nafasi ya 3 kwenye kundi B la kugombea kwenda Brazil 2014 nyuma ya vinara Tunisia, ambao wameshinda mechi zote tatu mpaka sasa
 
Katika kesi inayofanana na hii ya sasa, mwaka 2011, FIFA waliizuia timu ya wanawake ya Equatorial Guinea kushiriki kwenye mashindano ya kufuzu kucheza Olimpiki na kumfungia mshambuliaji Jade Boho Sayo kwa miezi miwili kutokana na masuala ya kutokuwa na uraia halali wa kuitumikia nchi hiyo.

YANGA VS JKT OLJORO: MBUYU TWITE NJE NAFASI YAKE KUCHUKULIWA NA JUMA ABDUL

BENCHI la Ufunda la Yanga limethibitisha kuwa beki Juma Abdul ndiye atakayecheza nafasi ya Mbuyu Twite.
 

Yanga ambayo inasaka pointi 10 kutwaa taji la Ligi Kuu Bara msimu huu huku ikiwa na mechi tano mkononi, leo itacheza na Oljoro JKT ya Arusha.
 

Mtanange huo utapigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, lakini itamkosa beki wake mahiri Mnyarwandwa Mbuyu Twite ambaye anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.
 

Lakini, benchi la ufundi limesema pengo la kiraka huyo litazibwa vema na mlinzi wa kulia Juma Abdul.
 

Kocha msaidizi wa timu hiyo, Felix Minziro alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa ni pengo kumkosa Mbuyu Twite katika mechi hiyo muhimu.
 

"Ni mchezaji muhimu kwetu. Lakini  imeshatokea hawezi kucheza kwenye mchezo huo, hivyo hatuna budi kumtumia mchezaji mwingine kucheza nafasi hiyo.
 

"Nafasi yake atacheza Abdul (Juma). Ni beki mzuri ambaye anajua majukumu yake. Tunaamini atacheza vizuri na kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri." alisema Minziro.
 

Pia, beki Juma Abdul alisema anaamini atacheza vizuri kulingana na maandaliizi ambayo wamefanya na kuhakikisha wanaibuka na ushindi kuzidi kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa.
 

"Tumefanya maandalizi mazuri. Kila mchezaji morali yake ipo juu. Kwa hiyo wategemee ushindi tu," alisema Abdul aliyetua Yanga akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro pamoja na Said Bahanuzi.

YANGA KUENDELEZA UTEMI LIGI KUU KESHO - AZAM FC NA SIMBA NANI MBABE JUMAPILI?

Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea kesho (Aprili 13 mwaka huu) kwa mechi mbili zitakazochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, na Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Yanga itakuwa mwenyeji wa Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa wakati Uwanja wa Sokoine utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting.

Ligi hiyo itaendelea keshokutwa (Aprili 14 mwaka huu) kwa mechi kati ya wenyeji Azam na Simba. Mechi hiyo namba 155 itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

WASHELISHELI KUICHEZESHA AZAM CAF
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Shelisheli kuchezesha mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho kati ya Azam na AS FAR ya Morocco itakayofanyika Aprili 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Waamuzi hao ni Emile Fred atakayepuliza filimbi akisaidiwa na Steve Maire na Jean Ernesta. Mwamuzi wa mezani (fourth official) atakuwa Jean Claude Labrossa. Kamishna wa mechi hiyo ni Abbas Sendyowa kutoka Uganda.

Wakati huo huo, CAF imemteua Mtanzania Alfred Lwiza kuwa Kamishna wa mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho kati ya Liga Muculmana ya Msumbiji na Wydad Casablanca ya Morocco.

Mechi hiyo itakayochezwa kati ya Aprili 19,20 au 21 mwaka huu nchini Msumbiji itachezeshwa na waamuzi kutoka Zimbabwe wakiongozwa na Ruzive Ruzive.

FIFA KUWASILI WIKI IJAYO - KUSHUGHULIKIA MATATIZO YA UCHAGUZI WA TFF


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linapenda kuwatangazia wadau wa mpira wa miguu kuwa ujumbe wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utawasili nchini Jumatatu (Aprili 15 mwaka huu) kwa ajili ya kushughulikia mchakato wa uchaguzi mkuu wa TFF.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka FIFA, ujumbe huo utaongozwa na Mkuu wa Idara ya Uanachama ya FIFA, Primo Covarro na utafanya kazi kwa siku tatu kuanzia siku ya ujio na kuondoka Aprili 18 mwaka huu.

Ukiwa nchini, ujumbe huo utakutana na wagombea uongozi walioathiriwa na uamuzi wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF ambao waliomba mashauri yao yaangaliwe upya, wagombea ambao walikata rufani FIFA, Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Kamati ya Rufani na Sekretarieti ya TFF.

Wajumbe hao wangependa kukutana na waziri anayehusika na michezo, hivyo TFF imeiandikia Wizara ikipendekeza kuwa ujumbe huo ukutane na Waziri na wakuu wengine wa michezo Aprili 16 mwaka huu 2013 kabla ya kuanza kazi zao.

Wagombea watakaosikilizwa na ujumbe huo wa FIFA ni:
1.   Farid Salim Mbaraka Nahdi: Mgombea wa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ambaye alienguliwa na Kamati ya Uchaguzi na baadaye rufani yake kwa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF kutupwa na hali kadhalika ombi lake la kutaka shauri lake liangaliwe upya, kukataliwa.

2.   Elliud Peter Mvella: Mgombea wa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ambaye alikatwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF na kukata rufani Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF kabla ya maombi yake ya kutaka shauri lake kuangaliwa upya, kukataliwa.


3.   Mbasha Matutu: Mgombea wa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ambaye alikatwa na Kamati ya Uchaguzi na kukata rufani ambayo pia ilitupwa kabla ya kuomba shauri lake liangaliwe upya, ombi ambalo lilikataliwa.

4.   Hamad Yahya: Mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Bodi ya Ligi ambaye alipitishwa na Kamati ya Uchaguzi, lakini mwekaji pingamizi akakata rufani ambayo ilikubaliwa na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF na kuondolewa. Aliomba shauri lake liangaliwe upya, lakini Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF ikatupa ombi lake.

5.   Jamal Emily Malinzi: Mgombea wa nafasi ya urais wa TFF ambaye alipitishwa na Kamati ya Uchaguzi, lakini mwekaji pingamizi akakata rufani ambayo ilikubaliwa na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF, hivyo kuondolewa kwenye mchakato. Aliomba shauri lake liangaliwe upya, lakini likakataliwa. Hata hivyo, alikuwa ameshakata rufani FIFA.

6.   Michael Wambura: Mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa TFF ambaye alikatwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF na rufani yake kukataliwa na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF. Hakuomba shauri lake liangaliwe upya, lakini alikata rufani FIFA.

Shirikisho linawaomba wote waliotajwa hapo juu kujiandaa kwa utetezi na maelezo ya kutosha na kwamba barua za kuwaita zinafuata. (Orodha ya waathiriwa na programu ya ujumbe wa FIFA imeambatanishwa)

NI BARCELONA VS BAYERN MUNICH - REAL MADRID VS BORUSSIA DORTMUND - JE TUTASHUHUDIA EL CLASSICO WEMBLEY?

Kuna nafasi tunaweza tukashuhudia El Classico kwenye fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya kwenye dimba la Wembley baada ya Real Madrid na Barcelona kutengenishwa kwenye droo ya nusu fainali iliyofanyika muda mchache uliopita jijini Geneva Uswis. 

Kikosi cha Jose Mourinho Real Madrid kimepangwa kucheza dhidi ya Borussia Dortmund wakati Barcelona wamepangwa kucheza na Bayern Munich, hivyo kumaanisha kwamba ikiwa wapinzani wa ligi mbili tofauti - Spain na Ujerumani wanaweza kukutana kwenye fainali ya Wembley May 25.

Dortmund ndio timu pekee ambayo haijapoteza mechi hata moja kwenye michuano hii, na watacheza na Real kwa mara pili ndani ya msimu huu wa UCL. Dortmund waliweza kushinda na kuongoza kundi gumu lilokuwa likihusisha timu za Real, Manchester City na Ajax.

Mabingwa wa sasa wanaosubiri kuvikwa taji tu la Bundesliga  Bayern Munich wapo kwenye form ya kutisha msimu huu, wakitoka kuikanyaga Juventus nyumbani na ugenini.

Mechi za kwanza za nusu fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya zitachezwa April 23 na April 24, na marudiano zitafanyika wiki inayofuatia tarehe April 30 na May 1.

Wakati kwa upande wa UEROPA LEAGUE - Chelsea wamepangwa na FC Basel wakati  Fenerbahce watakipiga na Benfica

JOHN BOCCO: SABABU TANO ZINAZOMFANYA SHUJAA WA AZAM FC NA ADUI WA KULWA NA DOTO

MSHAMBULIAJI wa Azam FC, John Bocco 'Adebayor' anaweza kuwa ndiye mchezaji nambari moja anayechukiwa na mashabiki wa soka Tanzania hasa wa moja ya klabu hapa Tanzania.
Hata kumfanya nyota huyo kutangaza kujiondoa kwenye kikosi cha timu ya taifa, ‘Taifa Stars’ kuepuka zomea zomea za mashabiki.
Utafiti uliofanywa hivi karibuni umefichua mambo kadhaa yanayochangia Bocco kukosa sapoti ya mashabiki awapo uwanjani hasa katika kikosi cha Stars.

 
Huwezi kukataa kuwa katika soka la Tanzania, Simba na Yanga ndizo timu ambazo zinazojaza mashabiki wengi viwanjani.
Kwa hiyo, Bocco hawezi kupendwa kamwe na mashabiki wa klabu hizo kongwe nchini.

 

Unafahamu kuwa ndiye adui mkubwa wa Simba na Yanga. Azam FC imekutana mara 10 na Simba, kuanzia msimu wa 2011 - 13 katika mashindano mbalimbali.
Katika mechi hizo, Bocco amemfunga kipa Juma Kaseja wa Simba mara saba kati ya mabao 11 yaliyofungwa na Azam FC.
Mashabiki wa Simba hawawezi kumpenda hata kidogo Bocco kama ilivyo kwa watani zao Yanga.
Lakini, mashabiki wa Azam wanazo sababu tano kumsapoti Bocco akiwa Uwanjani.
 
Mpiganaji;
SAHAU kuhusu kuzifunga Simba na Yanga. Bocco ni mpiganaji. Mara zote anaipigania timu yake na yupo ‘bize’ kuhakikisha mabeki na mwamuzi hawana raha.
Anapohisi kwamba timu yake au yeye binafsi anadhulumiwa. Lazima afunge ili aweze kuwafunga midomo wanao mzomea.
Mashabiki wa Azam wanampenda kwa upiganaji wake kama ilivyo kwa ‘straika’ Kipre Tchetche aliyezamisha mabao 15 kwenye ligi na kuiweka timu hiyo nafasi ya pili.

Shabiki wa Ukweli;
NANI anabisha? Bocco amethibitisha hilo. Kuwa yeye ni shabiki wa Azam. Hata kama atakuwa na mapenzi yake binafsi kati ya klabu moja kongwe ni siri yake.
Ni suala gumu sana kwa mchezaji wa timu ambayo inajijenga kwa sasa kupata ofa yakujiunga na klabu za Simba na Yanga kisha kuikataa.
Bocco amewahi kusakwa na viongozi wa klabu hizo mbili, kongwe kwa lengo lakutaka kumsajili, lakini alizitolea nje ofa zote huku akitamka kuwa ameridhika na maisha ya Azam FC.
Hana sababu ambazo zinaweza kumshawishi kujiunga na Yanga au Simba kwa sasa wala kesho. Kila anachokihitaji anakipata akiwa na Azam FC.

Analijua Soka;
HILI ndilo jambo kubwa zaidi. Bocco analijua soka vizuri. Hata kupachikwa jina la 'Adebayor' na mashabiki wa soka. Kumfananishwa na mshambuliaji mahiri wa Tottenham Hotspur ya England na Togo, Emmanuel Adebayor.
Ni mmoja kati ya wakokotaji wazuri wa mpira ‘Tribblers’ katika Ligi Kuu Tanzania Bara ukiwaacha akina Shija Mkina wa Simba anayecheza Kagera Sugar kwa mkopo na Kipre Tchetche wa Azam FC.
Unakumbuka alivyowapiga chenga mabeki wa Simba na katika mechi ya raundi ya kwanzav ya ligi na kumchambua kipa Juma Kaseja kabla ya kufunga bao rahisi na la kuongoza dakika tisa ya mchezo huo.
Hata hivyo, dakika 29 nyota huyo aliumia na kushindwa kuendelea na mtanange huo wa ligi uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Oktoba 27, mwaka jana. Simba iliibuka na ushindi mabao 3-1.

Mabao Makali na Kuvutia;
BOCCO anapofunga mabao daima huwa yanavutia mashabiki.
Moja kati ya bao la 'TV' alilofunga ni dhidi ya Yanga msimu uliopita katika, mechi ya kwanza. Azam ilishinda mabao 3-1.
Bao hilo alifunga kwa kichwa chakuparaza akiunganisha krosi ya Mkenya Ibrahim Shikanda na kumwacha kipa Yaw Berko alisijue lakufanya.
Ana kipaji cha kipekee katika kufunga, sawa huenda hajafikia katika anga za akina Nteze John 'Lungu', Mohamed Hussein 'Mmachinga' na Edibily Lunyamila lakini ni mtu wakuogopwa anapolikaribia lango la timu pinzani.
Ndiye mfungaji bora wa ligi msimu uliopita. Alizamisha mabao 19 huku Emmaniel Okwi wa Simba aliyemfuata akifunga 12.

Amekamilika;
NI kocha yupi hataki kuwa na Bocco kwenye kikosi chake?.
Ni straika mwenye sifa zote. Ikiwa kimo na umbo, uwezo wakumiliki mpira na pia kufunga.
Bocco ana urefu wa futi 6, inchi 2.  Amekuwa akitumia vizuri kimo hicho nakuwachosha mabeki hasa kwenye mipira ya juu.
Pia, ni mtengeneza mzuri nafasi za mabao kwa wafungaji wengine inapotokea ameshikwa na mabeki wa timu pinzani.

BAKARI MALIMA JEMBE ULAYA: MSUVA USIOGOPE UJIO WA MRISHO NGASSA YANGA - KAZANA UPIGANIE NAMBA YAKO

BEKI wa zamani wa Yanga, Bakari Malima 'Jembe Ulaya' amemtaka winga Simon Msuva kutotikisika iwapo Mrisho Ngassa atajiunga na timu hiyo.
Malima alisema jijini Dar es Salaam kuwa Simon Msuva ambaye kwa sasa ni winga wa kulia wa kutegemewa katika kikosi cha Yanga asiogope kusikia ujio wa Ngassa isipokuwa cha zaidi azingatie mazoezi na kujituma pindi anapokuwa uwanjani.
“Msuva usiogope wala usipate papara unaposkia kuwa Ngassa anarudi Yanga, Njie wote wakali na nakushauri wewe kama mdogo wangu kuwa ujio wa Ngassa usikupe hofu kwani kwenye soka lazima uwe na mgongano wa wachezaji kwenye namba ili kuleta ushindani."
"Kwa hiyo, cha kuzingatia ni kufanya mazoezi zaidi na kujituma pindi unapopata nafasi,” alisema Malima.
Pia, amesifu uwezo wa Msuva akiwa dimbani na kudai kuwa kasi yake inamsaidia kuwachosha mabeki."
"Ukitazama kwa sasa Yanga inafanya mashambulizi yake kupitia winga ya kulia ambapo anacheza Msuva. Nikutokana na kocha kumwamini na kasi yake."
"Lakini amekuwa akishindwa kufanya yale ambayo mwalimu ana mwelekeza. Nadhani ana muda bado wakujifunza na kuwa mchezaji mzuri hata kushinda Ngassa kama atazingatia yote ambayo anaelekezwa na kujitunza."
Pia, Malima alisema iwapo Ngassa atatua katika klabu hiyo msimu ujao Yanga itakuwa imemaliza kazi kwani nafasi ya kushinda taji la ligi itakuwepo na hata kushinda mataji mengine makubwa kama Kombe la Kagame na hata kucheza kwa mafanikio Ligi ya Mabingwa Afrika.

KIPRE TCHETCHE AZIDI KUNG'ARA KWA UFUNGAJI WA MABAO LIGI KUU - AZAM WAKIZIDI KUICHIMBI KABURI AFRICAN LYONWawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, klabu ya Azam fc wana lambalamba leo hii wamewabamiza bila huruma Africa Lyon mabao 3-1, katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara uliopigwa leo hii dimba la Chamazi Complex maeneo ya Mbande nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Mabao ya Azam fc yametiwa kambani na wachezaji Khamis Mcha “Vialli” dakika ya 12, huku nyota wa klabu hiyo kutoka Pwani ya magharibi mwa Afrika, nchi ya Ivory coast, Kipre Herman Tchetche akikwamisha kimiani mabao mawili katika dakika ya 31 na 61 ya mchezo huo.
Bao pekee la kufutia machozi kwa upande wa Africa Lyon wanaohitaji kukwepa mkasi wa kushuka daraja limewekwa kimiani na Adam Kingwande dakika ya 37 kipindi cha kwanza.
Akizungumza muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Afisa habari wa Azam fc, Jafar Idd Maganga amesema wamefurahi kupata ushindi mnono mbele ya wapinzani wao ambao wanajitahidi kufanya vizuri ngwe hii ya lala salama ili wasalie ligi kuu msimu ujao.
“Kipindi cha kwanza kiukweli Lyon walitulia na kucheza vizuri, lakini kipindi cha pili tuliwazidi sana na tumewashinda kwa halali, sasa hesabu zetu ni mnyama Simba ambaye tunakumbana naye mwishoni mwa wiki hii”. Alisema Idd.
Idd alisema baada ya kuibuka na ushindi leo hii wamefikisha pointi 46 wakizidiwa na Yanga pointi 3 walioko kileleni kwa kujikusanyia pointi 49 ingawa Azam wao wamecheza mechi moja zaidi, wao wanajipanga kushinda kila mchezo uliosalia wakianza na wekundu wa msimbazi Simba walioweka rehani ubingwa wao msimu huu.
“Si kazi nyepesi, kila mtu amejipanga barabara dakika hizi za lala salama, lakini tuna timu nzuri inayoweza kushindana, sasa kocha wetu anajipanga upya kwa ajili ya Simba ambayo imejaza vijana waliotufunga siku za nyuma”. Aliongeza Idd.
Wakati hayo yakijili kwa Azam fc, wapinzani wao Africa Lyon wamekiri kupoteza kihalali mchezo huo kwani walizidiwa umakini na wenyeji wao.
Katibu mkuu wa klabu hiyo Ernest Brown amesema walipata nafasi za kufunga, lakini safu yao ya ushambuliaji ni butu sana na ndio maana walishindwa kutumia mtaji huo.
“Nafikiri walichotuzidi wapinzani wetu ni kucheza na nafasi, walitumia vyema makosa yetu na kuvuna mabao matatu yaliyowapa pointi tatu muhimu, lakini tunajipanga kwa michezo ijayo, hakika hatuna cha kujutia, ni kusonga mbele. Aliongeza Brown.
Akizungumzia kitendo cha kocha wao mkuu Mkenya Charles Otieno kutolewa kwa kadi nyekundu na mwamuzi wa mchezo huo, Brown alisema kitebdo hicho kimetokea kutokana na wawili hao kutoelewana.
“Otieno alitaka kuzungumza na mwamzi, kilichotakiwa ni busara za mwamzi, soka sio vita hata siku moja, angemsikiliza wangeelewana, lakini kumtoa benchi yalikuwa maamzi ya haraka sana”. Alisema Brown.
Katibu huyo alisisitiza kuwa kutolewa kwa kocha wao hakukuathiri mchezo huo kwani wachezaji wao waliendelea kupambana japokuwa walizidiwa na wapinzania wao ambao kwa sasa wako vizuri zaidi ya Lyon.
Baada ya michezo hiyo, mwishoni mwa wiki yaani Jumamosi, Vinara wa ligi hiyo Yanga ya Dar es Salaam wataumana na JKT Oljoro, wakati jumapili mabingwa wa zamani wa Tanzania, Coastal unioni ya Tanga watakuwa na kibarua kizito mbele ya wekundu wa msimbazi simba uwanja wa taifa.
VIKOSI:
Azam: Aishi Salum, Himidi Mao, Waziri Salum, Jockins Atudo, Luckson Kakolaki, Jabir Aziz, Kipre Tchetche, Ibrahim Mwaipopo, Abdi Kassim, Salum Abubakar, Mcha Khamisi
African Lyon: Noel Lucas, Ibrahim Isaac, Sunday Bakari, Yussuf Mlipili, Obinna Salamusasa, Juma Seif, Jackob Massawe, Mohamed Samatta, Adam Kingwande, Freddy Lewis, Ndela Kashakala

Thursday, April 11, 2013

HAWA NDIO WACHEZAJI 10 AMBAO KILA WALIPOFUNGA TIMU ZAO HAZIKUPOTEZA MECHI KWENYE LIGI KUU YA ENGLAND

Sergio Aguero's goal in Man City's 2-1 win at Man United was the 25th Premier League game in which the Argentine has scored and in every one of those games his team has emerged without defeat. That puts him among the top 10 Premier League goal scoring good luck charms; players who never suffered defeat in a game when they found the back of the net. At number 10 are former Forest star Bryan Roy and ex-Man United fill-back Denis Irwin, who both netted in 18 Premier League games, without defeat…

Goli la Sergio Aguero kuiwezesha Man City kushinda 2-1 dhidi ya United, ulikuwa ni mchezo wa 25 ambao muargentina huyo alifunga bao katika kila mechi na timu yake ikaibuka na matokeo chanya. Hilo linamuweka kwenye listi ya wachezaji 10 wa Premier League ambao pindi wanapofunga timu zao huwa hazipotezi mchezo - yaani ni wachezaji ambao hawakuwahi kuonja machungu ya kufungwa pindi wanapozifungia timu zao. Kwenye nafasi ya 10 yupo mchezaji wa zamani wa Nottigham Forest Bryan Roy na beki wa kushoto wa zamani wa Man United Denis Irwin, ambao wote walifunga kwenye mechi 18 za premier league, bila kupoteza mchezo...


NO. 9
Norwegian Riise is famous for his thunderbolt shot and has yet to taste defeat in the 19 Premier League games he has scored in for Liverpool and Fulham

John Arne Riise, alifunga kwenye mechi 19 za Premier League, alishinda 13, suluhu 6 - Mnorway huyu alikuwa ni mchezaji maarufu kwa kupiga magoli ya mashuti ya mbali - aliweza kufunga katika mechi 19 za ligi akiwa na jezi ya Liverpool na Fulham na katika michezo hiyo hakuonja kipigo hata kidogo.

 NO. 8

Former Man United favourite Lee Sharpe also scored in 19 Premier League games, but won 17 of those compared to Riise's 13, drawing the other two.

Lee Sharpe, alifunga kwenye mechi 19 za Premier League, akashinda 17, na suluhu 2 - Mchezaji huyu wa zamani wa Man United Lee Sharpe alifunga kwenye michezo 19 ya ligi kuu ya Engand, lakini akashinda michezo 17 ukilinganisha na 13 ya Riise - huku akitoa suluhu michezo miwili tu.

NO. 7Tottenham have yet to lose a Premier League match in which Aaron Lennon has scored

Tottenham Hotspur hawajawahi kufungwa pindi Aaron Lennon anapofunga, kijana amefunga kwenye mechi 24 za Premier League, Spurs ikishinda mechi 22, suluhu 2.

 NO. 6Argentine Aguero extended the record of Man City avoiding defeat whenever he scores in the Premier League with his winner at Old Trafford

 Sergio Aguero, amefunga kwenye mechi 25 za Premier League, ushindi kwenye mechi 23, suluhu 2.

NO. 5
Norwegian Leonhardsen experienced his most successful spell at Wimbledon, but also scored goals for Liverpool and Tottenham, without suffering Premier League defeat in any of those games

5. Oyvind Leonhardsen, alicheza na kufunga kwenye mechi 28 za Premier League games, ushindi kwenye mechi 21, suluhu kwenye 7 - Mnorway Leonhardsen alikuwa na wakati mzuri sana akiwa na Wimbledon, lakini alifunga mabao akiwa na Liverpool na Tottenham, bila kuonja uchungu wa kufungwa kwenye mechi hizo.

NO. 4 Milner scored his first Premier League goal aged just 16 and has yet to suffer defeat when finding the back of the net for Leeds, Newcastle United, Aston Villa and Man City.

James Milner, amecheza na kufunga 30 za Premier League, ushindi mechi 24, suluhu mechi 6 - Milner alifunga goli lake la kwanza la Premier League akiwa na umri wa miaka 16 na tangu wakati huo hajawahi kupoteza mechi pindi anapoifungia timu yake goli  tangu akiwa Leeds, Newcastle United, Aston Villa na Man City.

NO. 3
Arsenal were invincible whenever Fabregas found the back of the net for them in the Premier League

 Cesc Fabregas, alifunga kwenye mechi 32 Premier League, alishinda mechi 27, na suluhu 5 - Arsenal walikuwa hawafungiki wakati nahodha wao Fabregas alipokuwa kwenye orodha ya wafungaji wa mchezo husika wa premier league.

NO. 2The former Chelsea forward never lost a match when he score for the Blues in England's top flight.

 Salomon Kalou, aliifunga Chelsea katika mechi 32 za Premier League, walishinda mechi 29, na kutoa suluhu 3.

NO. 1

 Head and shoulders above the rest, Vassell had an incredible record of never losing when scoring for Aston Villa and Man City in the top flight. shame he couldn't tuck it away from 12 yards for England at Euro 2004!

Namba moja inakamatwa na mshambuliaji Darius Vassell, ambaye alifunga kwenye mechi 46 za Premier League, na kuziwezesha timu zake za Aston Villa na Man City kushinda kwenye mechi 36, na kutoa suluhu 10.

HII NDIO SIRI YA UTAJIRI WA MANCHESTER UNITED - INA WADHAMINI 33 DUNIANI WANAYOIFANYA UNITED KUWA THAMANI($3BILLION) KULIKO VILABU VYOTE VYA MICHEZO DUNIANIMshahara wa Wayne Rooney £250,000 kwa wiki pekee unamaanisha kwamba Manchester United wana listi ya bili ndefu za kulipa, lakini kwa bahati nzuri kwa Fergie kuna makampuni kibao yaliyopo duniani kote yanayoingizia fedha za kumwaga kwenye akaunti ya klabu hiyo ya Uingereza.  

Man United mpaka sasa inawezekana ikawa ndio timu yenye wadhamini wengi kuliko timu nyingine yoyte ya soka duniani, ikiwa na wadhamini wapatao 33. Kupitia picha hapo chini utaona mahala makampuni hayo yalipo na maelezo kuhusu nini wanachojishughulisha nacho kama biashara zao ambazo zinawawezesha kujihusisha kibiashara na klabu inayotajwa kuwa na thamani kubwa zaidi ulimwenguni.
Ramani inayoonyesha namna Manchester United inavyoitawala dunia kwa kuwa wadhamini kwenye takribani kila bara - hapa unaona mahala wadhamini hao wanapopatikana.

WADHAMINI WA UNITED KWA MUJIBU WA MTANDAO WA KLABU HIYO NA THAMANI YA KILA MKATABA KWA MWAKA.

AON
Principal sponsor of Manchester United - £20m a year 


DHL
Official logistics partner of Manchester United - £10m 


NIKE
Official kit supplier of Manchester United - £25.4m 


CHEVROLET
Official automotive partner of Manchester United - £12m 

SINGHA
Official beer of Manchester United - £2m 


THOMAS COOK
Official travel partner of Manchester United - £1.3m 


BWIN
Official online gaming and betting partner of Manchester United - £2.4m 


CASILLERO DEL DIABLO
Official wine partner of Manchester United - £2m 

HUBLOT
Official timekeeper of Manchester United - £4m 

 
Mikataba ya hapo chini yote inakadiriwa kuwa na thamani kati ya £1m - £2m...
 
SMIRNOFF
Official responsible drinking partner of Manchester United 


TOSHIBA MEDICAL SYSTEMS
Official medical systems partner of Manchester United 


STC
Official integrated telecommunications partner of Manchester United for Saudi Arabia 


PCCW
Official integrated telecommunications partner of Manchester United in Hong Kong 


TURKISH AIRLINES
Official airline partner 


EPSON
Official office equipment partner of Manchester United 


 
MISTER POTATO
Official savoury snack partner of Manchester United 


YANMAR
Official global partner 

TM
Official integrated telecommunications partner of Manchester United in Malaysia 

GLOBACOM
Official integrated telecommunications partner of Manchester United for Nigeria, Ghana, Republic of Benin 

VIVA KUWAIT
Official integrated telecommunications partner of Manchester United in Kuwait 

MTN
Official integrated telecoms partner of Manchester United for South Africa / Zambia / Rwanda / Uganda / Swaziland / Botswana.

AIRTEL
Official telecommunications partner of Manchester United in India/Sri Lanka/Seychelles/Bangladesh.

ZONG
Official telecommunications partner of Manchester United in Pakistan 

GLOBUL
Official telecommunications partner of Manchester United in Bulgaria 

MAMEE
Official noodles partner of Manchester United for Asia, Oceania and Middle East 

VIVA
Official integrated telecommunications partner of Manchester United in Bahrain 

TURK TELEKOM
Official integrated telecommunications partner of Manchester United in Turkey 

A.P. HONDA
Official motorcycle partner of Manchester United in Thailand

AIRTEL AFRICA
Official telecoms partner in Burkina Faso, Chad, DR Congo, Gabon, Kenya, Madagascar, Malawi, Niger, Sierra Leone, Tanzania, Congo Brazzaville 

BEELINE
Official telecommunications partner of Manchester United in Vietnam, Cambodia and Laos

BAKCELL
Official telecommunications and broadcast partner of Manchester United for Azerbaijan 

KAGOME
Official soft drink partner of Manchester United for Japan 

WAHAHA
Official soft drink partner of Manchester United for China 

PT MULTISTRADA
Official tyre partner of Manchester United 

KANSAI
Official paint partner of Manchester United

JE WEWE UNA KIPI CHA KUCHANGIA KWENYE HUU MJADALA !


JAY Z KUUZA HISA ZAKE BROOKLYN NETS ILI KUWA WAKALA WA WACHEZAJI WA NBA - NETS KUPOTEZA JINA KUBWA KWENYE BIASHARA


Mwanamuziki nguli na tajiri yupo katika hatua za mwisho za kuuza hisa zake kwenye timu ya mpira wa kikapu ya Brooklyn Nets ili aweze kuwa wakala wa wachezaji wa NBA, ikiwezekana kabla ya mwisho wa msimu. Mpango huo kwa sasa upo katika kuufanikisha, mtu mmoja mwenye ukaribu wa kambi ya Jay Z alisema jana Jumatano.
Sheria za NBA zinakataza mtu yoyote mwenye miliki kwenye timu kufanya kazi ya uwakala kwa wachezaji.
Hivi karibuni Jay Z kupitia kampuni take ya Roc Nation aliingia mkataba wa ushirikiano na Creative Artists Agency (CAA) na matumaini yao ni kuanza kushindani dili za kuwakilisha wachezaji wa NBA kuanzia mwezi June mwaka huu.   
Jay-Z anamiliki asilimia chache sans kwenye timu ya Nets, lakini amesaidia sans katika kuitangaza timu hiyo na kuihamisha kutoka New Jersey kwenda Brooklyn. Alikuwa mstari wa mbele katika kukamilisha makao makuu ya timu hiyo yenye thamani ya $1 billion ya Barclays Center, pia akisaidia katika ubunifu wa jezi mpya za timu hiyo. Kisha akaizindua Barclays Center kwa shows nane mfululizo kwa mafanikio kwa kuuza tiketi zote. 
Jay Z ambaye ni mume wa mwanamuziki Beyonce ana urafiki na wachezaji wengi wakubwa wa NBA, Lebron James na winging kibao, kwa haraka Jay Z anaweza kufanikiwa sans kwenye biashara hiyo ya uwakala. 
Jay Z na kampuni yake mpya ya uwakala hivi karibuni alimsaini  star wa New York Yankees All-Star Robinson Cano. 

LIG KUU BARA, WANA TAMTAM WAKABWA, PRISONS WANG`ARA, POLISI WAJIHATARISHA ZAIDI!


Na Baraka Mpenja
Ligi kuu soka Tanzania bara imeendelea kushika kasi kwa mechi tatu kushuhudiwa katika miji ya Mbeya na Morogoro.
Maafande wa jeshi la magereza, Tanzania Prisons wameshuka dimbani kuwakaribisha Mgambo JKT  katika uwanja wa Sokonne. Dakika tisini za mchezo huo zimemalizika kwa Prisons kuwabamiza wageni wao  bao  1-0.
Akizungumza kwa furaha nyingi kutoka jijini humo, katibu mkuu wa Prisons, Sadick Jumbe, amesema bao pekee la ushindi limefungwa na nyota wao Nurdin Issa Chona.
Jumbe alisema ushindi wa leo ni faraja kubwa kwa mashabiki wa soka mkoani humo, na sasa wanapanga upya majeshi yao kuwakaribisha Ruvu Shooting ya mkaoni Pwani, mchezo utakaopigwa jumamosi ya wiki hii jijini humo.
Pia aliongeza kuwa leo hii uwanja ulifurika mashabiki wengi sana ambao wameishangilia timu hiyo kwa muda wote wa mchezo, na kama itakuwa hivyo mechi zilizosalia lazima wapate ushindi.
Kwa upande wa Mgambo JKT kupitia kwa katibu mkuu wake, Antony Mgaya, wamesema matokeo ya leo ni mabaya sana kwao na yameathiri hesabu zao za kupambana kushuka daraja.
Mgaya alisema soka ni matokeo matatu, kufunga, kufungwa na kutoa sare, leo wamefungwa, basi wanapiga hesabu za michezo inayofuata.
Mkoani Morogoro katika dimba la Jamhuri, Polisi Moro wameshindwa kutumia vyema uwanja wao wa nyumbani baada ya kulazimisha suluhu pacha ya bila kufungana na maafande wa jesi la kujenga taifa, Ruvu Shooting kutoka mkaoni Pwani.
Afisa habari wa klabu hiyo, Clemence Banzo amesema wameyapokea matokeo ya leo kwa shingo upande kwani mechi inayofuata wanakutana na mabingwa watetezi, wekundu wa Msimbazi ambao kwa sasa wanahitaji kupata ushindi.
Banzo alisema kushindwa kuibuka na ushinid katika mchezo wa leo, kumewafanya wazidi kujihatarisha zaidi na mstari wa kushuka daraja.
Kwa upande wa Ruvu Shooting kupitia kwa afisa habari wake Masau Bwire, wamesema wamepokea matokeo hayo kwani pointi moja ugenini si haba.
Masau alisema ingawa wameshindwa kufanya vizuri leo, lakini maamuzi ya waamuzi wa leo yamechangia kuwanyima ushindi.
Mbali na mchezo huo, huko mashamba ya miwa ya Manungu, wana tamtam Mtibwa sugar wameshindwa kupata ushindi baada ya kukabwa koo na kutoka sare ya 2-2 dhidi ya vijana wa mitaa ya kishamapanda Mwanza, Toto Africa.
Afisa habari wa Mtibwa, Tobias Kifaru Lugalambwike, amesema mabao ya Mtibwa yamefungwa dakika ya tatu na John Ndanda, na dakika ya 17 Hassan Banda alipachika bao la pili kwa mkwaju wa penati.
Kifaru alisema kipindi cha pili kilianza kwa kasi zaidi huku vijana wa Toto wakicheza soka safi na katika dakika 74 Mohamed Hussein aliandika kimiani bao la kwanza la kusawazisha, na dakika ya 87 nyota huyo aliisawazishia klabu yake bao la pili.
Afisa habari huyo alisema mchezo wa leo umeharibiwa na hali ya mvua iliyonyesha  asubuhi na kuharibu hali ya uwanja Manungu Complex uliokumbwa na utelezi.
Baada ya mitanange ya jana, ligi hiyo itaandelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa dimba la Chamazi, Azam fc watakuwa na kibarua kigumu mbele ya Africa Lyon.


WAKAZI WA JIJI LA MBEYA WAPATA MATUMAINI MAPYA MARA BAADA YA TIMU YAO YA PRISSON KUIBUKA NA USHINDI WA GOLI MOJA DHIDI YA JKT MGAMBO

KATIKA DAKIKA YA 18 KIPINDI CHA KWANZA NURDIN ISSA ALIPACHIKA GOLI LANGONI MWA JKT MGAMBO MARA BAADA YA KUPIGWA KONA NA KUMKUTA NURDIN AMBAPO  MOJA KWA MOJA ALIPACHIKA GOLI LA KWANZA NA LA USHINDI
NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI PHILIPO MULUGO NDIYE ALIEKUWA MGENI RASMI KATIKA MECHI HIYO AMEIPATIA TIMU YA PRISSON SHILINGI LAKI TANO KWA USHINDI WA LEO NA AMESEMA KILA ITAKAPO SHINDA ATAENDELEA KUTOA KIASI HICHO CHA PESA.

Kwa hisani ya : http://mbeyayetu.blogspot.com/

HII NDIYO CHELSEA BWANA !

MARKET FC YAFUFUKA, YAIFUNGA KILWA FC 6 - 0

023

Bechi la ufundi la Timu ya Market Fc leo dhidi ya Kilwa Fc likionekana lenye faraja kubwa, (Market Fc 6-Kilwa Fc 0)003Bechi la Ufundi la Timu ya Kilwa Fc wakifuatilia mchezo kwa makini, (Market Fc 6 – Kilwa Fc 0)004

Wachezaji wa Market Fc wakishangilia moja ya magoli yao leo hii dhidi ya Kilwa Fc (Market Fc 6 – Kilwa Fc 0)

Na: Fungwa K, Lindi

Leo Ligi daraja la Tatu Mjini Lindi iliendelea ikiwa ni Mechi ya Tatu ikiwakutanisha Market Fc ya mjini lindi na Kilwa Fc ya wilayani Kilwa Mkoani Lindi, Hapo jana Mechi zilizochezwa ilikuwa ni Beach Boys ikiikaribisha Kusini Soccer zote zikiwa ni za mjini Lindi na hadi mwisho wa Mchezo Kusini Soccer ilitoka Kifua mbele kwa magoli 2 – 1.

Market Fc leo ikionesha Kandanda Safi imejikusanyia Point tatu muhimu mara baada ya kupoteza mchezo wake wa awali baada ya kukubali kichapo cha magoli 4 – 1 dhidi ya Kariakoo Fc, Leo hii imeitundika Kilwa Fc Magoli 6 – 0. Kipindi cha kwanza cha mchezo huo kiliisha kwa Market Fc kutoka kifuambele kwa goli 3-0, wafungaji wakiwa ni Mustafa Makacha 18dk, Yahaya Mkweche 36dk, Mohamedi Salumu 43.
Kilwa Fc walianza kipindi cha pili kwa kufanyamabadiliko kidogo sehemu ya kiungo lakini mabadiliko hayo hayakuzaa matunda kwani Mlinda mlango wao alionyesha udhaifu mkubwa na kuruhusu Magoli ya Kizembe.
Ni Idrisa Benedict alieendeleza wimbi la magoli kwa timu yake kwa kufunga goli la nne mnamo dakika ya 56, dakika 65 Yahaya Mkweche Kwa maraya pili alimchungulia golikipa huyo na kuandika goli la nne kwa timu yake ya Market, huku yeye akiweza kuonngeza idadi ya magoli mnamo dakika ya 73 kwa kufunga harttrick yake ya kwanza katika mashindano haya. Hadi mwisho wa mchezo matokeo yalikuwa Market Fc 6 - Kilwa Fc 0. Ligi hiyo itaendelea tena hapo kesho kwa kuzikutanisha Kariakoo Fc Vs Kusini Soccer katika uwanja wa Ilulu, mchezo huo unatarajia Kuanza mnamo saa 10:00 jioni.

KATIKA PICHA UWANJA WA ILULU: MPIRA HAKUKOSI VIOJA HEBU ANGALIA....

018Waamuzi wa mchezo wa leo kati ya Market Fc Vs Kilwa Fc, katika Uwanja wa Ilulu.005006010Washabiki nao hawakuwanyuma kuwashangilia wachezaji wao pale walipoona wanapiga pasi za uhakika na magoli mazuri katika mchezo huo.007Shabiki la marketi Hiloooooooooooo019