Search This Blog

Friday, April 12, 2013

JOHN BOCCO: SABABU TANO ZINAZOMFANYA SHUJAA WA AZAM FC NA ADUI WA KULWA NA DOTO

MSHAMBULIAJI wa Azam FC, John Bocco 'Adebayor' anaweza kuwa ndiye mchezaji nambari moja anayechukiwa na mashabiki wa soka Tanzania hasa wa moja ya klabu hapa Tanzania.
Hata kumfanya nyota huyo kutangaza kujiondoa kwenye kikosi cha timu ya taifa, ‘Taifa Stars’ kuepuka zomea zomea za mashabiki.
Utafiti uliofanywa hivi karibuni umefichua mambo kadhaa yanayochangia Bocco kukosa sapoti ya mashabiki awapo uwanjani hasa katika kikosi cha Stars.

 
Huwezi kukataa kuwa katika soka la Tanzania, Simba na Yanga ndizo timu ambazo zinazojaza mashabiki wengi viwanjani.
Kwa hiyo, Bocco hawezi kupendwa kamwe na mashabiki wa klabu hizo kongwe nchini.

 

Unafahamu kuwa ndiye adui mkubwa wa Simba na Yanga. Azam FC imekutana mara 10 na Simba, kuanzia msimu wa 2011 - 13 katika mashindano mbalimbali.
Katika mechi hizo, Bocco amemfunga kipa Juma Kaseja wa Simba mara saba kati ya mabao 11 yaliyofungwa na Azam FC.
Mashabiki wa Simba hawawezi kumpenda hata kidogo Bocco kama ilivyo kwa watani zao Yanga.
Lakini, mashabiki wa Azam wanazo sababu tano kumsapoti Bocco akiwa Uwanjani.
 
Mpiganaji;
SAHAU kuhusu kuzifunga Simba na Yanga. Bocco ni mpiganaji. Mara zote anaipigania timu yake na yupo ‘bize’ kuhakikisha mabeki na mwamuzi hawana raha.
Anapohisi kwamba timu yake au yeye binafsi anadhulumiwa. Lazima afunge ili aweze kuwafunga midomo wanao mzomea.
Mashabiki wa Azam wanampenda kwa upiganaji wake kama ilivyo kwa ‘straika’ Kipre Tchetche aliyezamisha mabao 15 kwenye ligi na kuiweka timu hiyo nafasi ya pili.

Shabiki wa Ukweli;
NANI anabisha? Bocco amethibitisha hilo. Kuwa yeye ni shabiki wa Azam. Hata kama atakuwa na mapenzi yake binafsi kati ya klabu moja kongwe ni siri yake.
Ni suala gumu sana kwa mchezaji wa timu ambayo inajijenga kwa sasa kupata ofa yakujiunga na klabu za Simba na Yanga kisha kuikataa.
Bocco amewahi kusakwa na viongozi wa klabu hizo mbili, kongwe kwa lengo lakutaka kumsajili, lakini alizitolea nje ofa zote huku akitamka kuwa ameridhika na maisha ya Azam FC.
Hana sababu ambazo zinaweza kumshawishi kujiunga na Yanga au Simba kwa sasa wala kesho. Kila anachokihitaji anakipata akiwa na Azam FC.

Analijua Soka;
HILI ndilo jambo kubwa zaidi. Bocco analijua soka vizuri. Hata kupachikwa jina la 'Adebayor' na mashabiki wa soka. Kumfananishwa na mshambuliaji mahiri wa Tottenham Hotspur ya England na Togo, Emmanuel Adebayor.
Ni mmoja kati ya wakokotaji wazuri wa mpira ‘Tribblers’ katika Ligi Kuu Tanzania Bara ukiwaacha akina Shija Mkina wa Simba anayecheza Kagera Sugar kwa mkopo na Kipre Tchetche wa Azam FC.
Unakumbuka alivyowapiga chenga mabeki wa Simba na katika mechi ya raundi ya kwanzav ya ligi na kumchambua kipa Juma Kaseja kabla ya kufunga bao rahisi na la kuongoza dakika tisa ya mchezo huo.
Hata hivyo, dakika 29 nyota huyo aliumia na kushindwa kuendelea na mtanange huo wa ligi uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Oktoba 27, mwaka jana. Simba iliibuka na ushindi mabao 3-1.

Mabao Makali na Kuvutia;
BOCCO anapofunga mabao daima huwa yanavutia mashabiki.
Moja kati ya bao la 'TV' alilofunga ni dhidi ya Yanga msimu uliopita katika, mechi ya kwanza. Azam ilishinda mabao 3-1.
Bao hilo alifunga kwa kichwa chakuparaza akiunganisha krosi ya Mkenya Ibrahim Shikanda na kumwacha kipa Yaw Berko alisijue lakufanya.
Ana kipaji cha kipekee katika kufunga, sawa huenda hajafikia katika anga za akina Nteze John 'Lungu', Mohamed Hussein 'Mmachinga' na Edibily Lunyamila lakini ni mtu wakuogopwa anapolikaribia lango la timu pinzani.
Ndiye mfungaji bora wa ligi msimu uliopita. Alizamisha mabao 19 huku Emmaniel Okwi wa Simba aliyemfuata akifunga 12.

Amekamilika;
NI kocha yupi hataki kuwa na Bocco kwenye kikosi chake?.
Ni straika mwenye sifa zote. Ikiwa kimo na umbo, uwezo wakumiliki mpira na pia kufunga.
Bocco ana urefu wa futi 6, inchi 2.  Amekuwa akitumia vizuri kimo hicho nakuwachosha mabeki hasa kwenye mipira ya juu.
Pia, ni mtengeneza mzuri nafasi za mabao kwa wafungaji wengine inapotokea ameshikwa na mabeki wa timu pinzani.

No comments:

Post a Comment